Jumatano, 2 Machi 2016

Jinsi ya Kuhudumia watu wenye Uhitaji



Leo tutachukua Muda kutafakari namna na jinsi ya kumuhudumia mtu mwenye matatizo, watu wenye matatizo ni kama ile wagonjwa waliolazwa mahospitalini, au waloko majumani, watu waliorudi nyuma na kukata tamaa kwaajili ya wokovu, watu wanaopitia mateso kwaajili ya wokovu watu waliofiwa na kadhalika lengo la kujifnza jinsi ya kuwahudumia ni kwa makusudi ya kuwachukulia mizigo yao ili wote tufike mbinguni Wagalatia 6;2 ,1wakoritho 12;25-27. Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia yafuatayo;-

      Huduma ya Masaidiano katika kanisa ni ya muhimu hasa nyakayti hizi za mwisho                 


  •  Jinsi ya kuwafikia watu wenye Matatizo
  • Namna ya kuwahudumia wenye matatizo ya aina mbalimbali.


Jinsi ya kuwahudumia watu wenye Matatizo.
Endapo tunagundua kuwa mwenzetu katika imani anaanza kulegea au amepatwa na tatizo tunapaswa kumsaidia kwa kumpa msaada wa kiroho kwanza  kwa kumlisha neon la Mungu na hatimaye  tutaangalia msaada wowote wa kimwil kulingana natatizo alilonalo  kutokana na neema tuliyonayo 2wakoritho 8;11-12 tutamfuatilia mwenzetu huku tukizingatia mahusiano ya kijinsia  ili injili yetu isitukanwe na kuwa kwazo la kuwafungia wau Ufalme wa Mungu, Tunawaendea watu wenye matatizo kwa upole huku tukiwa kwanza tumewaombea kwa uzito mkubwa Wakolosai 1;9,4;2-3 tutamomba Mungu ili kwamba atupe hekima ya kuwaendea na kuzungumza nao na kasha ndipo tutaanza kutoa msaada wa kiroho na kimwili kama Mungu atakavyotuongoza.

Namna ya kuwahudumia wenye matatizo ya aina mbalimbali.
1.       Jinsi ya kuwahudumia wagonjwa wa aina mbalimbali
Tuwajulishe kuwa Mungu hajawaacha kwa sababu wanafanya mapenzi ya Mungu Zaburi 37;25 Ayubu alipokuwa katika hali mbaya ya kutisha aliyacheka maangamizo na njaa kwa sababu alijua  kuwa hii ilikuwa njia ya Mungu kumpa daraja la juu  na ndivyo ilivyokuwa Ayubu 42;10-17 Tuwatie Moyo na kuwaambia Bwana aliyachukua magonjwa yetu na udhaifu wa kila namna  kwa hiyo wajipe moyo kwa kuwa Mungu anakwenda kuwafungua Isaya 53;4-5, Mathayo 8;17 Mungu alipomuinua mkwewe Petro alipokuwa amelala hoi kitandani atakuinua na wewe katika jina la Yesu Luka 4;38-39 Baada ya kumtia moyo inatupasa kumuombea na kumsaidia shughuli za kimwili.

2.       Jinsi ya kuwahudumia wanaopitia mateso kwaajili ya Wokovu
Kanisa ni lazima litafute kila namna ya kuwatia moyo kwa neno la Mungu wale wanaopitia mateso ni muhimu kwao kufahamu kuwa tukiteswa kwaajili ya Kristo tuna heri maana tutapokea taji ya Uzima tukivumilia mpaka mwisho 1Petro 4; 12-16 Yakobo 1; 12 Ni muhimu kufahamu kuwa tukimfuata Yesu Kristo ambaye ndiye kielelzo chetu tutachukiwa, kuudhiwa na kudharauliwa pia tutaeswa na kuonewa na kunenwa mabaya  hii sio ajabu hiki ni kipimo tu kinachoashiria kuwa sasa tuko na Mungu na kuwa shetani ameudhiwa na uamuzi wetu hasa  kwa msingi huio tusizimie roho  na kumpa tena shetani ushindi kwa kukata tamaa kwa sababu ya mateso haya ya muda mfupi lakini tuitegemee neema na kumshinda shetani kwa kuitegemea neema na kuendelea katika imani  1Petro2;19-25 waebrania 2;18,Warumi 8;35-39 wafilipi 1;29-30

3.       Jinsi ya kuwahudumia watu waliofwa kwa ujumla
Tuwatie moyo na kuwafariji kwa maandiko kama haya 1Wathesalonike 4; 13-17 Kutoka katika uso wa dunia sio kitu cha ajabu ni njia ya Mungu ya kumpeleka mtu pazuri zaidi akiwa amejiandaa  hapa hapa duniani Mwanzo 3;19 Duniani sisi wote ni wapitaji tu Ndio maana tunapaswa kujiandaa kwa makao ya milele na Mungu Amosi 4;12 1Petro 2;11.

4.       Jinsi ya kuwatia moyo waliokata tamaa kimaisha.
Ni muhimu kuwatia moyo wapendwa wa aina hiyo kwamba wasibabaike wala kufadhaika  na wala wasiogope  maana bwana anasema ujapopita katika  maji mengi hayata kugharikisha  kwa kuwa Bwana atakuwa pamoja nawe Isaya 43;1-5,41;10 Mungu hawezi kukusahau Isaya 49;14-16 kinachotakiwa ni kutokujisumbukia  nafsi zetu maana Bwana anajua kuwa tuna haja  na yote hayo ila anatpa msingi wa kutafuta kwanza ufalme wa ungu na kisha haja zetu zijulikane na Mungu  na tumuombe Mungu bila kukata tama Bwana ataushindia  Luka 12; 21-31 Wafilipi 4;4-7

5.       Jinai ya kuwahudumia waliorudi nyuma.
Mtu anaporudi nyuma anapaswa kuendewa kwa upole na Upendo na kumwambia kuwa bado Mungu anakupenda na anahitaji ukawe naye baadaye Mbingun kwenye raha ya milele na milele, Petro aliporudi nyuma kwa kumkana mara tatu alitubu kwa majonzi na kutambua kuwa shetani alimdanganya, Bwana alipomtokea tena na kumtumia sana kwaajili ya ufalme wake, wewe nawe kumbuka wapi ulikoanguka ukatubu na kuurudia upendo wako wa kwanza Ezekiel 3;19-20,21;18;20-22 tunapochukua mzigo mkubwa  kuwafuatilia wale waliorudi nyuma sisi tunajiwekea Baraka  na kufutiwa wingi wa dhambi Yakobo 5; 19-20 Lakini tuwe macho ili kwamba adui naye asije akatutupata kwa kutumia huyu aliyerudi nyuma na kututeka Wagalatia 6;1-2. 

6.       Jinsi ya kuwatia moyo walio wavivu wa Ibada
Ni muhimu kutumuia maandiko kama Luka 12;16-21,Yakobo 4;13-16 na Mathayo 16;26-27 kwa kusudi la kuwakumbusha umuhimu wa kuhudhuria Ibada hili ni jambo la msingi linalodhihirisha uhai wa kiroho wa kila Mwamini.

Hakuna maoni: