Maana nawaambia Haki yenu isipozidi Hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo Hamtaingia kamwe katika Ufalme wa Mbinguni.
Moja ya maandiko ambayo hutumiwa
vibaya na wahubiri wengi wa injili ni Mathayo 5;20 kimsingi kutokana na
maandiko haya wakristo waliookoka wametengenezewa makongwa mengi sana kwa kawaida mstari huo inasomeka hivi “Maana nawaambia haki yenu isipozidi Hiyo haki ya waandishi na
mafarisayo hamtaingia kamwe katika ufalme wa Mbinguni” ndugu msomaji
wakristo wengi wamefanywa kuwa watumwa na kubeba mizigo isiyowahusu kupiia
andiko hili jinsi andiko hili lilivyo na kile kinachotafasiriwa au kukaziwa na
wahuiri ni tofauti sana na hata na jinsi Kristo alivyokusudia andiko hili kutumika kwa ujmla kile ambacho
wahubiri wengi wanakimaanisha katika maandiko haya ni kama maandiko haya
yanasomeka hivi “Maana nawaambia Matendo yenu
yasipozidi Hayo Matendo ya waandishi na mafarisayo hamtaingia kamwe
katika ufalme wa Mbinguni” nimewahi kuwasikia wahubiri wakikazia wakristo kuwa
na matendo yanayowazidi mafarisayo na waandishi yaani waalimu wa sheria
tunapounganisha na swala zima la wokovu mafundisho ya aina hiyo sio injili
tuliyoipokea oka kwa Bwana, wakati Fulani kwa sababu ya mafundisho ya aina hiyo
nilikuwa nimejipangia kuwa ni lazima niamke kuomba Alfajiri kama vile waislam
wafanyavyo na kwakuwa niliamini kuwa wao hawana Mungu wa kweli kama niliye naye
kwa msisitizo wa mahubiri ya wachungaji wengi nilijifunza kuwa ninalazimika
kuamka kabla ya Waislamu na kumuomba Mungu ili matendo yangu yazidi hayo
matendo ya mafarisayao na kwakuwa maisha yangu ya mwanzo kabla ya kumjua Mungu
nilikuwa nikilala na kuamka kwa saa nilizotaka uamkaji wa Alfajiri lilikuwa
jambo jipya katika maisha yangu niliambiwa kuwa huko Korea Ya kusini wakristo
huamka alifajiri na kumuomba Mungu na wamepata mafaniko makubwa sana lakini
sisi Afrika Mashariki wamishionari wetu hawakuwa wametufunza hivyo kwa hiyo
nilichapa usingizi lakini nilipomjua Mungu na kujifunza kuhusu kuamka alifajiri
nligunduia kuwa ninapaswa kuwawahi waislamu na siku kama ikitokea nimechelewa
kuamka na wakanitangulia nilijihisi vibaya na kuona kuwa siku hiyo ni chungu na
sio siku nzuri io niliiishi kwa maumivu ambayo sikuwa nayo kabla ya kuokoka kwa
nini nilijifunza kuwa matendo yangu lazima yazidi yale ya Mafarisayo. Kumbe
nilikuja kugundua siri kutoka kwa roho wa Mung kuwa Mungu hakumaanisha kile
nilichokianya kimsingi Yesu alikuwa akizungumzia “HAKI” na sio “MATENDO”
nililazimika kujifunza kuhusu haki kamamstari halisi unavyosema na niligundua
kuwa kwanza hakuna mwanadamu mwenye haki hata mmoja Warumi 3;10-12,Biblia
inasema hivi “Kama ilivoandikwa ya kwamba hakuna mwenye
haki hata mmoja hakuna afahamuye, Hakuna amtafutaye Mungu Wote wamepotoka
wameoza wote pia hakuna mtenda mema la! Hata mmoja” nilijiuliza kama
hakuna mwenye haki hata mmoja inakuwaje Yesu aseme haki yet isipozidi haki ya
mafarisayo hatutauona ufalme wa Mbinguni? Nikagundua kuwa kumbe Mafarisayo
hawakuwa na haki hawakuwa na haki ya kweli haki waliyokuwa nayo ilikuwa haki ya
nje tu Mathayo 23;25-28 Yesu anawaonya mafarisayo “Ole
wenu waandishi na Mafarisao wanafiki …..” kumbe mafarisayo walikuwa wanafiki
hawakuwa na haki ya kweli haki yao ilikuwa haki ya nje walifanya mambo ili
waonekane na watu Mathayo 23;5a “Tena matendo
yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu;” kumbe mafarisayo haki yao ilikuwa ni haki ya nje haki
ya kujionyesha tu walionekana na watu kuwa ni wenye haki lakini kwa kweli
hawakuwa na haki ya kweli na ndio maana Yesu alisisitiza kuwa ni lazima iwepo
haki mbadala ,haki ambayo ni tofauti na haki na ile ya mafarisayo haki ya
nje sasa ili mtu aweze kuingia katika
ufalme wa mbinguni hawezi kuingia kwa haki kama ile ya mafarisayo ambayo
ilikuwa ya nje ni kweli walionekana wanshika sheria walionekana wanaomba,
walisifu na kufunga walisoma neno la Mungu
na hata kuhudhuria ibada hata
hivyo walifanya hayo ili waonekane na watu wasifiwe waonekane kuwa wao ni wa
kiroho na washika dini wakubwa huu haukuwa mtazamo sahii haki mbadala ni haki
ambayo haitokani na matendo ya sheria ni
haki kutoka moyoni ni haki itokanayo na imani
ni neema ya kukubali kazi aliyoifanya kristo kwaajili yetu Msalabani ni
haki itokanayo na Kristo Warumi 3;21-26 Waefeso 2;1-9 hii ndio haki mbadala
aliyoizungumzia Bwana Yesu kwa hiyo Kristo hajatuita katika mashindano ya
kuwazidi wale tunaowaita mafarisayo kwa matendo kama ukifanya hivyo
wakikushinda unakuwa chni ya kongwa ambalo hata kabla ya kuokoka hukuwa nalo na
unaweza kujikuta ukichomwa moyo kama mimi nilipokuwa nikikosa maombo ya
alfajiri kumbe lilikuwa kongwa!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni