Toba hupokelewa wakati gani?
Ndugu msomaji wangu nataka kuzungumzia kwa
masikitiko kuhusu kongwa lingine ambalo wahubiri wengi sana wanawafungia watu
mizigo na kuwatishwa kupitia kutokuelewa au kiburi cha uzima au kuchukua nafasi
ya Mungu hii itafahamika zaidi kwa kujiuliza swali kuwa Toba hupokelewa na
Mungu wakati gani? Bila shaka umepata kusikia au kuona au kushuhudia watu
waliookoka wakitangazwa na wachungaji mimbarini kuwa wametengwa kwa miezi sita
au mitatu au mwaka au penginepo yamekukuta wewe mwenyewe hata kama moyo wako
umepondeka na umemaliza na Mungu lakini unalazimika kutengwa kwa muda anaotaka
mchungaji au askofu je swala hili ni sawa na injili au ni mapokeo? Na kwa
makanisa yenye misimamo mikali zaidi watu hufukuzwa au kuondolewa ushirika pia
unaweza kuwa umesikia hili je ni sawa na injili je kama watu hawa wametubu kwa
Mungu toba yao imepokelewa anayewafunga ni nani Munu au Mwanadamu? Nataka kabla
sijajibu maswali haya nikurudishe nyuma kidogo katika somo la wokovu nilipokuwa
nikizungumzia kuhusu toba ni nini Bila shaka nilieleweka vema lakini nataka
kufafanua tena kidogo kisha kujibu swali hili muhimu.
Ni muhimu kufahamu kuwa Toba ya kweli haipaswi kupitia kwa wanadamu!
Neno
Toba repent ni kuhuzunika moyo kwa
mujibu wa Biblia ya Kiebrania neno Sigh hutumika
ambalo maana yake ni kuhuzunika moyo, kujuta, kughairi, kuomboleza au kuwa na
mpango mpya Tunaweza kuona asili ya neno hili katika Mwanzo 6;6-7 Biblia inasema
hivi “Bwana akaghairi kwa kuwa
amemfanya mwanadamu duniani akahuzunika
moyo Bwana akasema nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba usoni pa nchi
mwanadamu na mnyama na kitambaacho na ndege wa angani kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya” kwa
msingi huo basi neno kutubu kwa kiibrania ni kuhuzunika na kughairi mpango fulani
uliokuwa nao. kwa hiyo kimsingi toba ni lazima iwe na mfuatano wa kuhuzunika
moyo na kuchukua hatua mdhubuti. Kuhuzunika bila kuchukua hatua sio toba kamili.
Kama ulikuwa unafanya jambo fulani lazima ughairi Kutoka 32; 14, 1Samuel 15;11
Neno
toba Katika Biblia ya kiyunani linatumika neno Metanoeo au metanoia au metamelomai ambalo maana yake ni kuwa
na hisia nyingine, au kuhuzunika na kuchukua hatua ni kubadilika hivyo toba ni
kuhuzunika na kubadilika au kuhuzunika na kuchukua hatua mfano Mathayo 21:
28-31 Biblia inasema hivi “Lakini mwaonaje mtu mmoja
alikuwa na wana wawili, akamwendea yule wa kwanza akasema mwanangu nenda kafanye kazi katika
shamba la mizabibu, Akajibu akasema naenda Bwana asiende, Akamwendea Yule wa pili akasema
vilevile, Naye akajibu akasema Sitaki baadaye akatubu akaenda , Je katika hao
wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia ni Yule wa pili…”Bila
shaka ni wazi kabisa kuwa katika mfano huu wa Bwana Yesu alikuwa akionyesha ni
nani ametubu toba ya kweli, kuhuzunika bila kuchukua hatua sio toba kamili Yuda
alihuzunika alipokuwa amemsaliti bwana Yesu alifanya vema kuhuzunika lakini hakufanya mapinduzi dhidi ya huzuni
yake bali aliamua kwenda kujiua hii haikuwa toba kamili, Toba ya kweli
hujumuisha kuhuzunika na kubadilika kimtazamo na toba hii ya kweli itapelekea
maisha yako kuwa yenye furaha hutakuwa mtumwa wa huzuni tena utawekwa huru
kutoka kongwa la huzuni.
Mafundisho kuhusu toba leo
yamefanywa kuwa magumu na wahubiri na wamewafunga watu katika makongwa yasiyokuwa
na Dawa kwa nini kwa sababu kama umefahamu vema maana ya toba utaweza kuona
kuwa toba hutokea wakati mkosaji amedhamiria kwa dhati kutambua na kurekebisha makosa
yake kwa wakati uleule na anapokea msamaha wakati uleule anapokuwa amelazimika
au ameamua kutubu, kumbuka kuwa hata kuokolewa kwetu kulitegemeana na toba
tuliyotubu kwa kumuamini Kristo na ingawa tulikuwa wabaya na tusiofaa kwa Mungu
saa ileile tulipotubu tuliweza kupokea wokovu na Mungu akatukubali kana kwamba
tumezaliwa tena na ndivyo ilivyo, hebu tuangalie kibiblia kwa maneno ya Mungu
zaidi kuona kuwa toba hutokea wakati gani? Nitatoa mifano michache ya kibiblia
ili tuweze kujifunza kimsingi toba hutokea wakati gani?






“Naitwa Sulemani Mdeni , sipendi kuzungumza mengi sana kwa
sababu habari yenyewe imejaa vitu vingi vidogovidogo, nitasema yale ya muhimu
tu ambayo ndiyo hasa yamenifanya niandike
habari hii, Nilizaliwa Tanga mjini mwaka 1954, nilikulia na kusomea Tanga
ambapo nilipofika darasa la nne pale Chumbageni , nilianguka mtihani ambapo
nilichukuliwa na mjomba kwenda Hedaru huko upareni, mjomba wangu alikuwa ni
fundi cherehani, nilipofika Hedaru mwaka 1966 nilianza kujifunza kushona wakati huo Hedaru kalikuwa ni kamji kadogo
sana, nilijifunza uufundi hapo na kuwa fundi mzuri sana, Mwaka 1975 nilikwenda
Korogwe ambapo nilipata kazi dukani kwa mzee mmoja pale Manundu. Siku moja
mwaka 1977 niliamua kwenda Tanga kumsalimu mzazi wangu mama.
Nikiwa
hapo nyumbani siku moja mama aliniambia kwamba kuna mtoto anateswa sana nyumba
ya jirani, Nilimuuliza sababu ya kuteswa, mama akaniambia ni mtoto wa kaka wa
huyo jirani ambapo mtoto wa huyo alikuweko, Niliambiawa alifika hapo baada ya wazazi wake kufa na huyo ndugu ndiyo
akamchukua, niliuliza mateso yake nikaambiwa kwamba alikuwa anafanyishwa kazi
kama punda, anapigwa sana na kusimangwa
na kuna wakati watoto wa huyo jirani yetu wanataka kumlawiti, mama
aliniambia kuwa kwa wakati ule Yule mtoto alikuwa anaumwa sana , niliambiwa
kwamaba alikuwa na kidonda kikubwa sana ambacho alikipata kwa kujikata na ndoo
iliyomwangukia wakati akichota maji, nilisimuliwa mengi sana kuhusu maswala ya
mtoto Yule na roho ikaniuma sana , hasa baada ya kuambiwa pamoja na hali
aliyonayo bado anafanyishwa kazi sana , hata watoto wa kike wa ile nyumba ya
jirani walikuwa hawafanyi kazi isipokuwa mtoto tule ambaye niliambiwa alikuwa
na umri wa miaka kumi na mbili tu. Nilipiga akili hatimaye niliipata, (nilikuwa
na rafiki yangu polisi naomba nisitaje kituo) pale Tanga niliamua nikamwambie
aje awatishe wale majirani zetu na kumchukua mtoto kwa lengo la kumpeleka
Hospitali, haja yangu ilikuwa ni kumchukua mtoto Yule na kwenda naye Korogwe.
Ni
kweli mpango wangu ulifanikiwa bila wale majirani kujua kuwa kwamba nilikuwa
nimeusuka mimi, mtoto Yule alichukuliwa na polisi na kupelekwa kweli Bombo
Hospitali kuu mkoani hapa , baada ya siku nne ambapo muda wangu wa kuondoka
ulikuwa umefika niliondoka na Yule
mtoto, alikuwa ni mtoto mwenye mwili mkubwa licha ya kuonewa na alionyesha pia
kuwa na akili, nilimuuliza kama mangependa kusoma na alikubali, nilimtafutia shule ambapo
alianza darasa la nne kama nilivyokuwa
nimefikiria mtoto alikuwa na akili sana
kwani alianza kuongoza , alimaliza la saba mwaka 1980 na kufaulu kwenda shule
ya sekondari Magamba Lushotoalisoma hapo hadi mwaka 1985 ambapo alimaliza
kidato cha nne, hakufaulu vizuri sana , lakini ilikuwa inaeleweka , alipokuwa
kidato cha pili alianza uhuni wa mambo ya kutafuta wasichana na kuvuta sigara.
Niliitwa mara mbili shuleni na alisimamishwa shule mara moja ,hata mimi alianza
kunidharau sasa, lakini jinsi maisha yake yalivyokuwa niliona sina budi kuendelea kumsaidia ,
alipomaliza shule alikuwa ni mtu wa vijiwe tu na ukimsemesha anasema hawezi
kuzungumza na watu wasiosoma , yaani alibadilika sana.
Niliamua
kumsaidia apate kazi , nilipata bahati siku moja ya kukutana na mzee mmoja
amabaye nilimshonea suti ya sherehe ya miaka 20 ya ndoa yake, pamoja na familia
yake , amabaye aliafurahishwa sana na kazi yangu, mzee huyu zamania alikuwa
serikalini, nilimuombea kazi huyu kijana , ambaye kwangu alikuwa kama mdogo
wangu hasa kwa kuzingatia kuwa sikuwa na mdogo wa kiume , huyu mzee
alinisaidia nikapata kazi kwaajili ya
huyu ndugu yangu kwenye kampuni moja pale (Tanga naomba nisiitaje)ilikuwa kama
bahati kwani alipata kazi mahali pazuri sana , nikisema pazuri kwa mazingira ya
kijinga ni mahali ambapo aliweza
kuiba hii ilikuwa ni mwaka 1990. Baada
ya kuanza kazi sikumuona tena hadi mwaka 1993 nilipoenda Tanga nilimpitia kazini kwake kumjulia hali, ambapo
hakuchangamka kabisa, ilikuwa kama vile hakuwa akinifahamu, Sikujali kwani hata
mama aliniambia kwamba kuna siku alipatwa na dharula akaenda kumuomba msaada,
akamwambia mama kwamba hana kitu, ikiwa ni uongo mkubwa, wakati huu huyu bwana
mdogo alishajenga nyumba Muheza na alishanunua kiwanja pale Korogwe na alikuwa
na teksi Dar hiyo ni kwa miaka mitatu tu, sikujali niliumia lakini nilijiambia
lengo langu la kumsaidia lilikuwa limetimia Nilisema hayo kutoka moyoni kabisa.
Mwaka
1996 nilikuwa ndio kwanza nimeoa mke wa pili baada ya Yule wa kwanza
kunishinda, siku moja jioni wakati mimi na mke wangu tunatembea pale Tanga
nilikutana na Yule bwana mdogo , Nilishangaa kwamba alinichangamkia sana,
Aliniomba radhi kuwa hanitembelei kule Korogwe
kwa sababau yuko bize, sana amepandishwa cheo kazini , Nilimtambulisha
kwa mke wangu mpya na aliuliza kwa
mshangao kama nimemuacha Yule shemeji yake (mke wangu wa kwanza)niliomwambia
ndio hakusema neno lakini nadhaniu alifurahi, kwani walikuwa
hawaelewani kabisa, alinipa hela nakumbuka kwa mara ya kwanza kabisa tangu kuanza kazi, nilitaka kuzikataa lakini
niliona haitakuwa vizuri zilikuwa ni 12,000 kwa wakati ule zilikuwa nyingi
kidogo, halafu alihaidi kwamba angenitembelea Korogwe.
Alinitembelea
kweli siku nne tu baadaye, alifika nyumbani kwanza mimi nikiwa kazini, Kuanzia
hapo akawa anakuja nyumbani kwangu haipiti wiki amekuja kusalimu, Akawa analeta
vyakula, samaki na hata nguo anatununulia, hatimaye akanisaidia nikapata zabuni
ya kushona nguo za kazini kwao. Niliweza kumalizia nyumba yangu pale Pongwe kwa
fedha hizo, lakini siku moja mwaka 1997
jirani yangu mmoja tena mtu mzima aliniomba
tuzungumze nikamkubalia, aliniambia jioni nikifunga kazi tukae mahali
tuzungumze. Huyu mzee alianza kwanza kwa maneno ya hekima na busara, halafu
alisema alichoniitia, Sikuwa nategemea alichiniambia kwamba mke wangu alikuwa
ananiendea kinyume, alisema wazi kwamba alikuwa akitembea na Yule kijana ambaye
huyu mzee alikuwa anamjua tangu namleta pale akiwa ananuka kidonda, sikuamini
kwani kwa jinsi nilivyokuwa namjua Yule mzee niliamini kuwa kuna ukweli.
Niliporudi nyumbani sikumuuliza mke wangu ingawa nilikuwa na maumivu ambayo
nina sitakuja kuyahisi tena maishani mwangu, Yule mzee alinishauri nisiseme
chochote nyumbani kwani kumfumania mke wangu kwenye tendo ingekuwa rahisi sana.
Siku
mbili tu baada ya taarifa ile Yule mzee alinifuata kazini kwangu na kuniambia
kwamba mke wangu yuko na Yule bwana mdogo nyumba ya wageni, Alinitajia nyumba
yenyewe na tuliondoka naye kwenda huko, Ni kweli alikuwa hapo na Yule kijana,
sikuumia palepale sijui kwanini, nilipohakikisha nilifunga mlango na kuondoka.
Yule mzee alinisaidia kufanya utaratibu wa talaka, nilitoa talaka siku ileile
na baada ya kutoa talaka ndipo hasa nilipohisi maumivu ya kweli, niliumia kiasi
kwamba niliona ni lazima ningekufa, hguwa sinywi pombe lakini nilitaka kwenda kunywa,
ilipofika saa nne usiku niliingia chumbani kwangu na kuzima taa halafu
nilichukua mswala na kukaa chini
nilianza kumshitakia Mungu nilianza kunuia mabaya kwayule kijana nilipotea kabisa kwenye sala ile ya kunuia ubaya hadi majogoo yanawika.
Nilisali hadi nikaona mwanga nisioujua, nililenga ubaya tu.
Najua
hutaamini, siku ya nne tangu tukio lile nikiwa nyumbani kwa mama yangu ambapo
nilienda kupumzika nililetewa taarifa kwamba Yule kijana alikuwa ameshakamatawa
na yuko Polisi, niliambia alikuwa amekamatwa kwa tuhuma za wizi,wiki moja
baadaye kilakitu alichokuwa anakimiliki kilikamatwa na alikuwa rumande, lakini wiki mbili baadaye
aliachiwa huru baada ya mwenye
kampuni kumuomba polisi wamwachie maana
amepata mali zake, aliachiwa akiwa hana hata senti tano, alihamia mji wa Tanga
. Mwaka huohuo nilihama kutoka Korogwe kuja Tanga na kuanzisha shughuli pale
Pongwe, Lakini nilipofikiria kuwa nyumba ile nimeijenga kwa zabuni ya dhambi
niliiuza, mwaka 2002 nikiwa nyumbani pamoja na mama na ndugu zangu wawili wa
kike tuliona mtu akija. alikuwa ni
mwanaume ambaye wazi alikuwa anaumwa , alikuwa mchafu, kupindukia na
alikuwa na kidonda mguuni, baada ya kutusalimia ndipo polepole tulipobaini kwamba alikuwa ni Yule kijana,
Mahali alipokuwa na kidonda mguuni ni palepale ambapo alikuwa na kile kidonda wakati namchukua, alipokwisha kusalimu
alipiga magoti na kusema kaka najua ni
vigumu kunisamehe, lakini naomba uendelee kufikiria kunisamehe siku moja hata nikiwa nimeshakufa, nilikuwa
mjinga, kichaa, mnyama asiyefaa hata kuliwa…” alianza kulia , mimi nilinyamaza
kimya nikimtazama sikuwa na hasira naye kabisa,
dada zangu na mama ndio walikuwa wakimzonga huku wakimcheka kwa kebehi, Naomba
kaka uniombee heri niwe binadamu tena , ni wewe ulinifanya nikawa binadamu
nikakosa shukuraninaomba uniombee niwe mwenye hekima tu nipate hekima tu si utajiri..’
Akina
dada na mama walimcheka na kuanza
kumtukana Mimi sikufanya hivyo nilimsjhika mkono Yule kijana na kumuinua Ni kweli
umekosa na umejua kosa lako, mimi na
wewe tutaomba pamoja kwa Mungu urejewe
Ufahamu, Dada zangu walipiga kelele za
mshangao na kupinga jambo lile
nilimsaidia Yule kijana kuoga na
alipewa chakula ingawa kwa masimango, usiku nilimwomba aingie chumbani kwake
aombe anachokitaka kimtokee, nami nliingia chumbani mwangu na kuanza
kusali nikimwombea mabadiliko, Najua
wakati mwingine ni vigumu kuamini mambo haya lakini nasema hivi yapo, huyu
kijana alikaa pele nyumbani na kidonda chake kilikauka baada ya wiki tatu tu, wakati alikuwa
amehangaika nacho kwa mwaka mzima, unajua huyu kijana siku hizi yuko wapi?
Ukiona watu wanaokuja Dar wakitokea Mombasa kama wafanya biashara ulizia Bwana
Abuubakar au jitu kubwa, Amerudi kwenye hali yake ya kawaida ya zamani bwana
mafedha lakini hivi sasa anajua kuheshimu nwatu hata watoto wadogo, na mimi
nimepata ndugu hivi sasa. Je nguvu ya maombi iko wapi? Je kumtendea mtu uovu ni
swala unalolichukuaje na unalielezea vipi? Je huoni kwamba Kusamehe ni jambo la
muhimu sana? Najua kuwa unakodoma mimacho kwa mshangao lakini Kristo alisema
waombeeni wanaowaudhi watendeeni mema adui zenu.
Bila
shaka utakuwa umejifunza maswala muhimu sana kutoka katika kisa hiki cha Sulemani
mdeni ingawa yeye sio mkristo lakini anaona umuhimu wa kusamehe sisi nasi inatupasa
kuwa watu wa kusamehe, tusifurahi watu wanapofanya makosa na kukimbilia
kuhukumu huku tunafahamu wazi kuwa na sisi ni binadamu wala tusifanye msamaha
kuwa kitu kinachopatikana kwa shida sana hali wokovu unapatikana kwa urahisi
sana Bwana alipe neema kanisa na kuliponya kutoka katika kongwa la kuwatenga
watu kwa muda ssio wa kibiblia bali kama tu mchungaji anavyojisikia hayo sio
mafundisho ya injili wala wokovu tulionao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni