Utangulizi:
Mafundisho kuhusu Roho Mtakatifu yamekuwa
hayapewi kipaumbele kinachostahili Katika makanisa mengi,wengi hawampi utukufu
wowote na wakati mwingine imekuwa ngumu hata kumtaja tu, Ni kama vile Roho Mtakatifu
hayuko au amesahaulika kabisa.
Katika karne ya 18 kulikuwa na makundi
makubwa ya watu waliopinga waziwazi kama Roho Mtakatifu ni halisi, ni nafisi au
kama ni Mungu,Thomas Goodwin alithibitisha kuwa katika nyakati zao 1660 Roho
hakupewa kipaumbele, na George Smeaton katika nyakati zao 1880 alisema
mafundisho kuhusu Roho Mtakatifu yalizaraulika kabisa siku zote za maisha yao.
Hata katika kizazi hiki cha karne ya 20
ambapo kuna uamsho mkubwa ulioenea pande zote Duniani bado kuna watu wanapuuzia
utendaji na vipawa vya Roho Mtakatifu na wengine huona kama
havina sehemu katika kanisa.
Hata hivyo katika siku zetu kuna ufahamu
mkubwa na halisi wa uelewa wa uhalisi wa
Roho Mtakatifu na utendaji wake, Roho anafanya kazi katika maisha ndani ya mioyo
yetu anatenda kazi ndani ya wanaume na wanawake katika sehemu zote za ulimwengu
Tuna poendelea kujifunza na kuangalia kwa upana kuhusu Roho Mtakatifu katika
somo hili kutatupa nafasi ya kutoa kipaumbele
kwa kazi zake utendaji wake, asili yake na umuhimu wake na itatuleta katika uwazi wa kuelewa namna
tunavyoweza kushirikiana naye katika utendaji wa kazi ya Mungu ambayo bila yeye
inakuwa ngumu.
Neema anayotoa yeye katika utendaji wa kazi
yake utatusaidia kutembea katika nguvu zake na kushangilia urahisi unaopatikana
katika kazi ya ukombozi tukifanya kazi na Roho Mtakatifu, Lakini kama anapuuziwa
tusishangae kujiona kuwa kwa haraka na kwa Muda mfupi tunabaki kuwa vikundi vya
kihuni visivyo na mwelekeo na vyenye kujawa na kila aina ya majungu, yaliyojaa
fitina na faraka zisizo na ufumbuzi kwa kumdharau Roho Mtakatifu. Mchungaji Innocent
Kamote yuko pamoja nawe katika somo hili Muhimu ili tujikumbushe umuhimu wa
Roho mtakatifu katika maisha yetu na Huduma kisha tuweze kumtafuta kwa bidii na
kurudisha nguvu uwepo na utendaji wa Mungu katika siku zetu Mungu na akubariki
Ni maombi yangu kuwa somo hili litakuwa
Baraka kwako na kwa kanisa lako na huduma najua kadiri tutakavyojifunza kuhusu
Roho Mtakatifu ndivyo tutakavyo ruhusu kiu na mtiririko wa Roho katika maisha
yetu na huduma na hivyo tutajaa furaha kubwa kuona Mungu akifanya kazi pamoja
nasi. Tunashuhudia kupoa kwa kasi sana kwa makanisa mengi ya kipentekoste leo
kuliko wakati wa miaka ya themanini katika taifa letu tunaweka kuokoa kupotea
kukubwa kwa kasi ya kipentekoste kama tu tutajiachia kwake atuhudumie katika
somo hili na kutujaza na kuturudisha
katika viwangio vya nyakati za kanisa la kwanza.
Sura ya Kwanza; ROHO MTAKATIFU NI NANI?
Pneumatology - Ni somo linalohusu nafsi, Kazi,
Karama, utendaji na huduma za Roho Mtakatifu Kama inavyofundishwa katika Agano
la kale na Agano Jipya, Mkazo ukiwa katika kubatizwa na kujaa nguvu za Roho Mtakatifu na kutembea nazo.
Neno
Pneomatology - Ni muunganiko wa
maneno mawili ya kiyunani Pneuma-ambalo maana yake ni Roho, au pumzi au upepo na
neno (Logos) ology-ambalo maana yake ni Elimu kuhusu kwa hivyo neno Pneumatology ni
Elimu kuhusu Roho mtakatifu.Kwa kiebrania
ni Ruah hivyo Pneumatology pia inaweza kuwa Ruachology.
Kwa
nini Tunasoma Pneumatology.
Ziko
sababu nyingi sana zinazotufanya tujifunze kuhusu Roho Mtakatifu zifuatazo ni
baadhi tu ya sababu hizo.
- Kwa sababu Biblia inazungumza au inafundisha kuhusu Roho Mtakatifu.
- Maandiko yanamfunua kuwa ni nafsi, ni Mungu na anaweza kutambulika ni Halisi na anaeleweka
- Biblia inaeleza kuwa ndiye aliyevuvia watu kuandika Neno la Mungu
- Kazi zake zinaonekana katika Agano la kale na katika agano jipya.
- Biblia inaonyesha kuwa ana uhusiano na kuzaliwa maisha na huduma ya Kristo (Masihi)
- Inasaidia katika kutetea imani kuhusu ujazo wqa Roho Mtakatifu na utendaji wake na kuwa ni halisi hata katika siku zetu leo
- Inatusaidia kufahamu kuhusu utendaji, vipawa na Karama mbalimbali na umuhimu wa matunda ya Roho mtakatifu.
- Inatusaidia kujifunza, kutumia kuhubiri na kufundisha kuhusu Roho Mtakatifu kwa maisha yetu na ya wengine katika mwili wa Kristo yaani kanisa.
Umuhimu wa Roho mtakatifu.
Roho
Mtakatifu ana umuhimu gani na kwa nini tujifunze kuhusu Roho Mtakatifu?
Tukifahamu uhalisi utendaji uweza na nguvu zake na jinsi anavyohusika katika
kazi nzima ya ukombozi wa mwanadamu na umuhimu wake kwetu kamwe hatuwezi kuacha
kujifunza au kutaka kufahamu Kuhusu Roho Mtakatifu.
1.
Roho mtakatifu ana sifa zote
zinazoihusu nafsi
§
Ana
akili na ufahamu
§
Ana
maamuzi
§
Ana
maarifa.
§
Ana
upendo na hisia
2.
Roho Mtakatifu hufanya kazi zote
zinazoweza kufanywa na nafsi.
§
Anakaa
ndani ya Mwamini
§
Anafundisha
na anakumbusha
§
Anashuhudia
§
Anashawishi
kwa habari ya dhambi (kuonyesha jinsi dhambi isivyofaa)
§
Anaongoza
katika kweli,anasikia
§
Anazungumza
alizungumza na filipo
§
Anaita
watu katika huduma
§
Anatuma
watumishi katika huduma
§
Anakataza
baashi ya matendo
§
Anatuombea
§
Anaamuru
3.
Roho Mtakatifu anaweza
kufanyiwa kile ambacho nafsi yoyote inaweza kufanyiwa
§
Anaweza kudanganywa
§
Kujaribiwa
§
Kuhuzunishwa
§
Kuzimishwa
§
Kukufuriwa
§
Kumuitia,
kuumizwa n.k.
Kama
basi Roho Mtakatifu Ingekuwa ni nguvu tu kama nguvu ya umeme isingeweza
kuhuzunishwa na kufanyiwa mabo kama hayo tuliyoyaona hapo juu
Aidha angekuwa si nafsi katika maandiko
asingeandikwa kwa kutumia neno linalo husisha nafsi mfano katika Yohana 16;7
“…Huyo Msaidizi hatakuja..”,mst 13 “…Lakini Yeye atakapokuja..”mst 14;”Yeye
atanitukuza” “Atatwaa” namna anavyotajwa Roho mtakatifu hapo kwakweli
haimaanishi kuwa Yeye ni nguvu bali ni Nafsi Person. Na sio kitu Thing
4.
Roho
Mtakatifu ni halisi katika Biblia
§ Nyakati
za Biblia watu walifahamu wazi kabisa pale roho mtakatifu alipotenda kazi
§ Ilikuwa
ni hakika na halisi kabisa na hawakuwa na haja ya kuhisi
§ Woote
katika Agano la kale na jipya walifahamu pale Roho mtakatifu alipofanya kazi na
walijua kuwa ni
Ø Halisi
Ø Inayoelezeka
Ø Na
yenye matokeo maalumu.
- Ni wazi kuwa Mika kwa uweza wa Roho mtakatifu alihubiri kinyume na dhambi (Mika 3;8)
o
Amosi kwa msukumo wa ndani aliwasilisha maono na
kutangaza hukumu ya mungu (Amosi 3;8)
o
Kunena kwa Lugha kulivyo leo na kulivyokua wakati wa
Agano jipya sawa na Matendo 2;4 ni
halisi kama ilivyo leo
o
Roho mtakatifu alihitajika sana wakati ule na
anahitajika sana leo,dini yoyote ile
haitakuwa na maana kama haina Roho mtakatifu kama tunataka kujua kuwa Roho
mtakatifu anapewa kipaumbele gani angalia ni vitabu vingapi vimeandikwa kuhusu
Roho mtakatifu leo,Ni masaa mangapi yamechukuliwa na watu katika kuomba kuhusu
Roho mtakatifu,ni jumbe ngapi zinazohubiriwa kuhusu roho mtakatifu ni wangapi
wamechukua muda kusoma ili wafahamu vizuri kuhusu Roho mtakatifu unapofanya
tathimini hii utapata picha kuwa anapewa kipaumbele kiasi gani ? hebu jumlisha
jumbe za utoaji na za Roho mtakatifu zipi ni Nyingi makanisani Unapaswa
kufikiri mara mbili!
5.
Roho mtakatifu ana sifa za
Mungu.
Wakati mwingine moja kwa moja au pasipo moja
kwa moja sifa zinazomuhusu Mungu zimepelekwa moja kwa moja Kwa roho Mtakatifu
na hizi ni sifa zinazomuhusu Mungu peke yake mfano;-
- Ni mwenye nguvu zote- Omnipotence Zaburi 104;30 Zekaria 4;6.
- Anajua yoote- Omniscience Isaya 40;13;1Koritho 2;10-11.
- Yuko mahali kote-Omnipresence Zaburi 139;1-8,Yohana 14;17.
- Ni wa milele Eternality –hana mwanzo wala mwisho Waebrania 9;14
6.
Anafanya kazi ambazo hufanywa
na Mungu peke yake
Roho
Mtakatifu anahusika katika kazi ambazo kwa kawaida ni kazi za Mungu pekee hii
ikijumuisha na sifa alizo nazo haziwezi kuhusu nafsi za kawaida isipokuwa Mungu
tu Kwa mfano kazi zifuatazo
- Amehusika katika kazi ya Uumbaji hivyo ni Muumba Mwanzo 1;2. Ayubu 33;4.
- Anafufua wafu alihusika katika kumfufua Kristo Warumi 8;11
- Anabadilisha maisha ya watu kwa kuwazaa mara ya pili Yohana 3;5-6.
- Anashawishi watu kwa habari ya haki dhambi na hukumu Yohana 16;8.
- Anahusika katika swala la kutoa pepo ndiye anayetoa pepo Mathayo 12;28.
- Sifa yake Mtakatifu ni sifa ya Mungu tu maana hakuna mwanadamu au kiumbe kitakatifu yeye ametajwa mara 95 katika maandiko ni yeye ndiye anayehusika katika kazi ya utakaso
- Anahusishwa katika kanuni ya ubatizo Math 28;19
- Alihusika katika ubatizo wa Yesu Kristo Luka 3;21-22.
- Anahusihwa katika salam za Neema 2Koritho 13;14
- Wokovu wa mwanadamu hauwezi kuwa kamili bila kuhusisha ushirika huu wa utatu
7.
Roho
Mtakatifu ni tofauti na Baba na Mwana.
- Roho Mtakatifu hushirikiana na baba na mwana katika utatu katika njia inayoonyesha kuwa ni Mungu huku ikiwa wazi kuwa ni nafsi tofauti
- Yesu Kristo mwenyewe alimuita Roho Mtakatifu Mfariji mwingine Yohana 14;15-18,26 kwa kiyunani ni Parakletos ambalo maana yake ni Mfariji, mwalimu, Mwenyekutia nguvu, muombezi, wakili, Yeye aliyetayari au karibu kusaidia neno Another hutumika katika maneno mawili Heteros ambalo maana yake ni mwingine tofauti na Allos ambalo maana yake ni mwingine wa aina ileile.
- Hivyo wa aina nyingine humaanisha tofauti na Kristo lakini wa aina kama ya Kristo hivyo Roho Mtakatifu ni nafsi nyingine ya aina moja na Yesu aina yao ni asili ya uungu.
8.
Tatizo
la uungu wakati wa kanisa la karne ya kwanza.
Nyakati za kanisa la kwanza
ni wachache walikataa mafundisho kuhusu utatu,Baadhi ya maandiko ya mababa wa
kanisa kama Irenaeus na Tertulian walionekana kuelemea katika upande huo wa
Mungu mmoja lakini hii ilikuwa ni kwa sababu katika ulimwengu wa miungu mingi
inayoabudiwa ilikuwa ni sawa kuwa na wakristo wenye msimamo wa kuamini kuwa
Mungu ni mmoja na ana nafsi tatu.
Tatizo lilianza kujitokeza pale watu
walipoanza kutofautisha Baba,Mwana na Roho Mtakatifu na mgogoro mkubwa ulikuwa
ukimhusu Yesu Kristo ambapo jamii ya watu kama Gnostics walimtofautisha Yesu na Kristo, walimaanisha
Kristo ni kiumbe kutoka kwa Mungu na ni mtakatifu sana lakini Yesu ni mwili na hivyo Yohana mtume
aliyaita mafundisho hayo kuwa ni ya mpinga Kristo (1Yohana 4;2,2Yohana 7).Pia
walifundisha kuwa Roho Mtakatifu ni kiumbe vilevile kutoka kwa Mungu na si
Mungu,Baadhi ya wasomi wengine walifundisha mambo yafuatayo;
§ Origen
msomi kutoka Alexandria Misri katika karne ya tatu alimfanya Mungu baba kuwa Mungu
kamili na Yesu kuwa chini ya Baba na sio mungu na Roho Mtakatifu akiwa chini
zaidi kosa hili lilipelekea kukosesha wengi kwa mfano watu wa Makedonia
hawakumuita Roho Mungu kabisa ingawaje pia hawakumuita kiumbe.
§ Arius
katika karne ya nne alisema kuwa Yesu ni kiumbe tu na ameitwa Mungu kwa sababu tu anafurahia
upendeleo wa Mungu na pia hakumpa Roho nafasi ya uungu ni kwa sababu hizi mpaka
leo wako watu ambao hudhani kuwa Roho Mtakatifu ni nguvu tu ya kawaida
§ Callistus
wa Rumi moja ya waandishi wa zamani
alifundisha kuwa Baba na Mwana ni nafsi ileile tu moja na Roho Mtakatifu
alijibadili kuwa mwana na ni sawa na
Baba
§ Sabellius
katika mwaka wa 250 Baada ya Kristo alisema Baba, Mwana na Roho ni yuleyule
mmoja tu isipokuwa hujifunua katika namna mbalimbali kama muumba alijifunua kama Baba, duniani
katika kazi ya ukombozi alijifunua kama mwana na anapofanya kazi na kanisa
amejifunua kama Roho
§ Tatizo
lilisuluhishwa kwa kikao cha Nikea mwaka 325 B.K. ambapo walitambua kuwa Kristo
ni nafsi na kukubali kuwa wanamwamini Roho Mtakatifu bila kutoa ufafanuzi zaidi
Hata hivyo mtu mashuhuri mwenye mvuto Athanasius aliyefariki 373 Alisimama
kuweka sawa akitambua kuwa Baba si Mwana wala Mwana si Roho na kuweka wazi kuwa
Tunamwamini Mungu mmoja katika nasfi
tatu na hizi nafsi tatu ni Mungu mmoja
§ Kanisa
la uingereza pamoja na kanisa la Methodist wao waliweka msimsitizo katika
Biblia na kutoa ukiri wa kimethodisti
mwaka 1789 wao waliamini katika umoja wa Mungu kuna nafsi tatu katika umoja
wakiwa na nguvu na umilele sawa na hao ni Baba,Mwana na Roho wao ni kama
walibadili maneno lakini hawakuwa mbali na Athanasius hata hivyo swala hili
lilifungua mlango wa kujifunza zaidi kuhusu kazi za Roho Mtakatifu hata leo
§ Mwaka
wa 156 B.K.kulitokea uamsho wa kundi lililoitwa Montanism na sababu kubwa ya
kutokea kwa uamsho wao ilikuwa ni kupambana na desturi zilizoibuka katika
kanisa,kulitegemea kanisa badala ya Roho Mtakatifu na uongozi wake,walipinga
swala la kuweko kwa maaskofu na maongozi ya kibinadamu na kuacha kumtegemea
Roho wa Mungu,Mafundisho yao yalikazia kurudi kwa Yesu Kristo na kuwa angekuja
na kustawisha ufalme wake,walikuwa na msimamo mkali kwa ajili ya mafundisho
kuhusu Roho Mtakatifu na uvuvio,walisisitiza maadili na kupinga maswala ya
kupata elimu ya theolojia,Hawakuruhusu mtu kuoa kama mkeo angefariki au
mumeo,walifunga sana,na walikula vyakula vikavu wasomi wengi wanaamini huu
ulikuwa ni sawa na upentekoste uliokuja
baadae hata hivyo wanakosoa ile hali ya kukosa kiasi,kukataa elimu ya
theolojia,na kutojali mfumo wa uongozi na kuwa elimu ni muhimu kwani hulifanya
kanisa kuwa na nguvu montaniats waliteswa sana kwa sababu ya watu wasiotaka
mabadiliko.Tertulian alikuwa moja wa watu wasomi aliyejiunga na montanism mwaka wa 200 B.K. na uamsho huu ukatiwa nguvu
sana
ASILI YA ROHO MTAKATIFU
Kwa kawaida ni vigumu kujua kwa haraka
asili ya mtu bila kujua majina yake kamili kwetu waafrika ni rahisi kujua asili
ya mtu akitumia jina lake la asili Mfano Peter Mmari au Anna Shayo mara
yanapotajwa majina haya utajua kuwa watu hao wana asili ya kichaga na majina
kama Ngonyani,Mapunda,Nakatembo,Mbawala,Komba na ndunguru yanapotajwa
yatakujulisha kwa haraka kuwa watu wa jinsi hii ni watu wa Songea kwa nini kwa
sababu majina yanatusaidia kujua asili,Ili tuweze kujua asili ya Roho Mtakatifu
ni muhimu kujua majina yake
A: Huitwa Roho wa
Mungu.
Roho Mtakatifu anaitwa Roho wa Mungu kwa
sababu kwanza ana asili ya uungu,ana sifa zote zinazomfanya Mungu awe
Mungu,Hawgawanyiki(Ebrania 9;14) ni wa milele,ni mwenye nguvu zote (Luka 1;35)
Yuko mahali kote kwa wakati mmoja,
Zaburi 139;7-10,Anajua yote hata mafumbo katika moyo wa mwanadamu 1Koritho
2;10,Yeye hufanya kazi zote ambazo Mungu anafanya kama uumbaji Mwanzo
1;2,anabadilisha na kufufua Ayubu 33;4;Yohana 3;5-8 na Rumi 8;11 Roho mtakatifu
yuko katika cheo kimoja na Baba na Mwana 1Koritho 12;4-6 Yeye ni nafsi na sio
nguvu fulani kama watu wengine wanavyofikiri sio msukumo ana akili,hisia
anafundisha ana amua, anaamuru,hutuombea(Rumi 8;27Efeso 4;30,Yohana
14;26,Galatia 4;6 Rumi 8;26) ana uamuzi ?utashi na anafunua.
B: Huitwa
Roho wa Kristo.
Anaitwa Roho wa kristo katika maandiko
Rumi 8;9 hii ni kwa sababu amatumwa kwa jina la Kristo na huombwa kwa jina la
Kristo na humtukuza Kristo (Yohana 14;26,16;14).Kama alivyo Roho wa Mungu pia
ni Roho wa Kristo,Tangu mwanzo alikuwa akisema na manabii kuhusu kuja kwa Yesu
Kristo 1Petro 1;10-11.na kwakuwa tumekuwa wana Mungu alimtuma Roho wa mwana
wake katika mioyo Yetu aliaye Abba yaani baba Wagalatia 4;6
C: Huitwa Mfariji.
Jina hili amepewa kati ya Yohana 14-17
neno mfariji kwa kiyunani ni ”Paracletos”
ambalo maana yake ni aliyeitwa kwa niaba ya mwingine apate kusaidia ni
msahuri na wakili Yohana 14;16 hata hivyo hii haimaanishi kuwa Kristo ameacha
kuwa karibu na sisi 1Yohana 2;1 Roho mtakatifu ni msaada wa kiungu ni msaada wa
kimbingu ambaye anatoa msaada unaohitajika katika maisha yetu na huduma Nami
nitamwomba baba naye atawapatia msaidizi mwingine akae naye hata milele Roho wa
kweli Yohana 14;16,26,Yohana 15;26 Yohana 16;7.
D: Huitwa Roho Mtakatifu
Tabia
ya Mungu siku zote yeye ni Mtakatifu Roho wa Mungu ni Mungu hivyo naye ni Mtakatifu na ndiye anayefanya kazi ya utakaso ndani ya
muamini tunapomuhitaji, kwakweli hakuna toba ya kweli inayoweza kupatikana
katika moyo wa mwanadamu bila msaada wa Roho Mtakatifu Yeye ndiye sababu ya
kusamehewa dhambi zetu Kutoka 23;20-22 kumtii yeye siku zote kutaleata matokeo
ya moyo safi na tabia njema Rumi 1;4, Nifundishe kutenda mapenzi yako kwa kuwa
wewe ndiwe Mungu wangu na Roho wako mwema aniongoze katika njia iliyo nyooka Zaburi 143;10.
E: Huitwa Roho wa Ahadi.
Pamoja
na kuwa alikuwa akihusika katika shughuli mbalimbali tangu katika agano la kale
Roho mtakatifu alihaidiwa kuwa angekuja Rasmi na kumwagwa kwa watu woote Ezekiel 36;27,Yoel 2;28 na pia Kristo
mwenyewe alihaidi ujio wa Roho Mtakatifu baada yake hivyo huitwa roho wa ahadi
Luka 24;49,Galatia 3;14
F: Huitwa Roho wa kweli.
Ni
Roho wa kweli na hakuna uwongo wowote ndani ya roho mtakatifu wala hawezi
kutuongoza kinyume na maandiko au kweli ya Mungu,kamwe haiwezekani kutokea
mgongano kati ya Roho Mtakatifu na Neno hata siku moja kwa ujumla neno la Mungu
ni neno la Roho Mtakatifu Efeso 6;17 na
kama mwandishi wa Biblia 2 Petro 1;21, hivyo hawezi kuwa kinyume na neno lake
mwenyewe. Muongozo wa Biblia siku zote
ni muongozo wa Roho Mtakatifu hivyo atatuongoza sawa na neno Yohana
14;16-17.15;26 1Yohana 4;2,6 Na hivi ndivyo tuwezavyo kumjua Roho wa Mungu kila roho isiyo mkiri Kristo kwamba yu aja
katika mwili haitokani na Mungu
G: Huitwa Roho wa Neema.
Roho
Mtakatifu ni Roho wa neema pia Yeye Hubeba ujumbe kuelekea katika nafsi ya
mwanadamu na kutoa mwaliko wa toba na kusababisha mwenye dhambi kukubali
utendaji wa Mungu katika maisha yake ,roho wa neema pia husaidia katika kutoa
neema ya kutuwezesha kuomba kwa kuugua kwa uchungu Zekaria 12;10 na kwa sababu
Roho wa Mungu hutoa neema ni vibaya kukosana na Roho huyu kwani kukosana na
Roho wa neema kutakufanya ukose namna ya kuwa na toba ya kumfikia Mungu
Waebrania 10;29 kwa sababu Roho ndiye anayetoa neema ya mtu kutubu dhambi zake
na uovu wake na kuuacha pia ndie anayesaidia na kutoa nguvu ya kututakasa na
kutusafisha hivyo ukimpinga unapingana na yeye anayetoa neema ya mtu kutubu na
kutakasika
H.Huitwa pia Roho wa Uzima.
Sheria
yake Roho wa uzima ni sheria ya imani na upendo na ndiyo inayotuweka huru
kutoka katika sheria ya dhambi na mauti na hivyo mtu akiishi kwa Roho anaishi
kwa ushindi dhidi ya dhambi na mauti
Warumi 8;2,Ufunuo 11;11 Hali kadhalika Yeye hutia uzima katika kila kiumbe ”Namwamini Roho Mtakatifu ,Bwana mtoa
Uzima”...Hivi ndivyo usemavyo sehemu ya ukiri wa imani hii inamaana ya kuwa
licha ya kuwa yeye ni muumba ndiye anayesababisha uhai wa asili na wa kiroho na
kuwa uwezo wa kukufufuliwa uko katika uwezo wake
I: Huitwa Roho wa Upitisho (Adoption).au uana
Roho Mtakatifu sio tu wa uzima lakini ndiye
anayehusika na kutuzaa mara ya pili na kuwa na uhusiano na Mungu hivyo pia
huitwa roho wa uana kwa sababu anatupa uwezo wa kufanyika kuwa wana wa Mungu au
anatupitisha kutoka kuwa wana wa giza na kutufanya kuwa wana wa nuru au wana wa
Mungu Warumi 8;15 kwa hivyo katika mioyo yetu tunapewa ujasiri wa kumuita Mungu
Baba au kulia abba wala hatuwi watumwa tena bali wana Galatia 4;6.
J: Huitwa Roho wa Hukumu
Roho
mtakatifu pia huitwa roho wa hukumu katika KJV Spirit of Burning hii ina maana anasima mia hukumu haki na
sheria na utaratibu ni mtakatifu na hatavumilia dhambi ni polisi wa maadili ni
hakimu wa haki ya Mungu anapinga dhambi,anaiweka wazi anaithibitisha na anawabadilisha
watu kutoka katika dhambi Isaya 4;4 kusudi la kuiweka dhambi kwetu ni ili
tuitubu na sio kutuaibisha na hufanya
kazi ya kututenga na dhambi Isaya 25:5-6.
K. Huitwa Roho wa Hekima na ufunuo
Kwa
kweli yeye ni Roho wa ufahamu,ushauri,maarifa,ufunuo na uchaji wa Mungu Isaya
11;2 analeta ufunuo ana angazia anatoa ujuzi wa kiroho na anaongoza na anaamsha
hari katika mioyo yetuMaandiko yenyewe ni matokeo ya kazi yake alitoa hekima na ujuzi kwa mafundi Kutoka
28;3 anatoa hekima ya maongozi Kumbukumbu la Torati 34;9 Roho wa Mungu, maarifa,
ufahamu, mashauri na nguvu, hekimana uchaji wa Mungu ulitabiriwa kukaa juu ya
Kristo Isaya 11;2 Efeso 1;17 3;4-5 Mathayo 10;20 Roho atatupa kipi cha
kuzungumza wakati wa matatizo
L: Huitwa Roho wa kinywa chake
Roho wa Mungu hunena kwa niaba ya Mungu na
Kristo wake na pia hutangaza hukumu za Mungu kwa hivyo hata mpinga Kristo
atashindwa kupitia Roho wa Kinywa chake kristo 1Thesalonike 2;8
M: Huitwa Roho wa Imani
Roho
Mtakatifu huitwa pia Roho wa imani yeye
ndiye anayetoa neema ya kuamini katika Yesu Kristo na kutupa uhakika na ujasiri
hata kuweza kukiri kwa ujasiri 2Koritho 4;13,Hutusaidia kumuamini Yesu na
kupata wokovu,Hutusaidia kumuamini Yesu na kupokea miujiza yetu na mahitaji
yetu,Pale Yesu asemapo imani yako imekuponya imani hiyo si yetu kwa hakika ila
ni zawadi ipatikanayo kupitia Roho mtakatifu kutusaidia kupokea kutoka kwa
Bwana
N: Huitwa Roho wa utukufu.
Kama roho wa Utukufu wa Mungu hukaa juu yetu na kutunza furaha ya
wokovu ndani yetu hata wakati wa mateso kwa ajili ya jina la Yesu hivyo
maandiko yasema Kama mkiteswa kwa ajili ya jina la Yesu mna heri kwakuwa Roho
wa utukufu na wa Mungu anakaa juu Yenu.1Petro 4;14
O; Huitwa Chanda cha Mungu.
Kwa kuhitimisha Roho Mtakatifu pia huitwa
chanda cha Mungu Luka 11;26 Yeye ni nguvu zake aliyejuu luka 1;26-35 na ni roho
wa milele Ebrania 9;14,Wachawi wa Misri walikiri kuwa utendaji uliokuwa
ukifanywa na Musa na Haruni kule Misri ulikuwa ni utendaji unaotokana na Uweza
wa Roho Mtakatifu au utendaji wa Mungu hiki ni chanda cha Mungu
ALAMA ZA ROHO MTAKATIFU
Mifano
ni mojawapo ya njia rahisi na kuu ya mawasiliano na ambayo mungu aliitumia
kuzungumza na watu ili waweze kuelewa kwa urahisi,Tangu zamani Mungu ametumia
njia hii .Kristo pia alitumia mifano,Hapa ziko alama ambazo zinaweza au
zimetumika kibiblia ili kutusaidia kuelewa mabo kwa upana na urahisi,hapa ziko
alama zinazotusaidia kuelezea utendaji wa Roho Mtakatifu katika njia iliyo
rahisi kila mtu kuelewa
A: Alama ya Moto
Alama ya moto inatumika kutufundisha kazi
za utakaso ,utisho,na ujasiri ,moto kama msukumo au wivu unaozalishwa na Roho
mtakatifu unatusukuma katika kuifanya
kazi yake yeye ni Roho wa kazi (Yeremia 20;9),Moto unapowashwa unazagaa au
unaenea kwa kasi na kuruka na kuyeyusha,pia unaangamiza na kusafisha moto ni
alama ya uwepo wa Mungu (Isaya
66;7,4;4,Mathayo 3;11,Luka 3;16,Matendo 2;3).
B;Alama ya maji
Woote tunajua umuhimu wa maji katika maisha
ya mwanadamu kwa kifupi maji na uhai vina uhusiano mkubwa sana ni uzima,yanasafisha,yanaondoa kiu yana
burudisha yanatuliza yanazalisha na kusababisha uhai wa mimea na yanakuza
lakini pia maji yana nguvu kubwa sana kama ya natembea au ukipingana na mkondo
wake maji hutumika kuelezea kazi za Roho
Mtakatifu Kutoka 17;6,Ezekiel 36;25-27,47;1,Yohana 3:5,4;14,7;38-39
C: Alama ya upepo
Upepo unawakilisha utendaji unaoonekana wa
nguvu isiyoonekana,Roho Mtakatifu anapokuwa kazini kazi zake huonekana lakini
yeye mwenyewe haonekani kwa macho ya kibinadamu kama jinsi isivyowezekana
kupingana na nguvu za upepo halikadhalika huwezi kupingana na kazi za utendaji
wa Mungu Roho Mtakatifu Yeremia 4;12, Isaya 66;15, 2Falme 2;11 Upepo wa nguvu
za mungu uliwaletea wana wa Israel kware kule jangwani na wakajazana ka umbali
wa kilomita za mraba kumi na ujazo wa futi tatu sawa na ridhaa mbili Hesabu
11;31
D; Alama ya Muhuri
Kwa
kawaida muhuri unawakilisha umiliki na uhalali,pia unawakilisha mamlaka na
usalama au uthibitisho Kwa msingi huo Roho Mtakatifu anapokuwa ndani yetu
anawakilisha kuwa sisi tu mali ya Mungu Efeso 1;13 2Timotheo 2;19,Yohana
6;27,2Koritho 1;22,Ufunuo 5;1 kwa akawaida kama mtu ataandika barua kisha asiweke
sahihi au muhuri kunakuwa na wasiwasi kuwa huenda ikawa barua hiyo si yake
Hivyo Roho mtakatifu ni uhakiki ya kuwa sisi ni mali ya Kristo Warumi 8;14-16
E: Alama ya mafuta.
Moja ya alama inayotumika sana kama alama
ya Roho mtakatifu Huenda ni mafuta
lakini kwa kawaida mafuta yaliyotumika ni mafuta ya mizeituni ambayo
yalielekezwa kutumiwa wakati wa agano la kale na kutumika kama alama ya Roho
Mtakatifu, Mafuta haya yalitumika wakati wa kuwaweka wakfu makuhani ambapo
walimwagiwa mafuta hayo vichwani mwao Kutoka 29;7,30;30 Walawi
8;12;21;10-12.Zaburi 133;2 mafuta pia yalipomwagwa juu ya kiongozi mfalme ajaye
yalimaanisha kuwa taji ya kifalme iko juu ya mtu huyo lakini pia ilikuwa
ikiwakumbusha kuwa utawala ni kazi ya Mungu na humpa yeyote amtakaye1Samuel
10;1,16;13,Psalm 89;20 1 Wafalme 1;39 2Falme 9;6.Mafuta pia yalitumika kumpaka
mgonjwa aliyepona ukoma Walawi 14;17-18 mafuta yalitumika pia wakati wa sadaka
ya unga iliyoletwa kwa Bwana Lawi 22na
sio katika sadaka ya dhambi Lawi 5;11,Mafuta hayo pia yalitumika kama mafuta ya
taa ya vinara saba iliyokuwa patakatifu Kutoka 27:20 Kwa mujibu wa Yakobo
alitaka pia yaambatane na maombezi ya wagonjwa kwa kuwapaka Yakobo 5;14,Roho
Mtakatifu huyaangazia maisha yetu ya kiroho na neno la mungu ili kusudi
tulielewe vema, hutufariji na kutuponya, mafuta yanapenya, yanalainisha,
yanaponya,yanalinda, yanaondoa ugumu au ukakasi na yananenepesha mwili.
F: Alama ya mvinyo .
Ni
jambo geni labda wakati mwingine kuitumia alama ya mvinyo kuihusisha na Roho Mtakatifu
lakini ukweli unabaki kuwa Roho huleta msisimko mkubwa kwa waamini wa
kipentekoste na karismatiki siku ya Pentekoste mitume walifikiriwa kuwa
wamelewa kwa mvinyo Matendo 2;13 huenda watu hawa walidhihaki hivyo kutokana na
muonekano wa Mitume katika siku ile, Mvinyo huleta uchangamfu hasa inapotokea
kuwa mtu ana huzuni Muhubiri 10;19 hata hivyo hii haimaanishi kuwa tunapaswa
kunywa mvinyo lakini badala yake waamini wanapaswa kuishi maisha yenye viwango
zaidi ya wanywa mvinyo Efeso 5;18
G: Alama ya Njiwa
Alama ya njiwa hutumiwa na wapentekoste
wengi kumuelezea Roho Mtakatifu huenda hii ni kwa sababu Roho Mtakatifu
alishuka juu ya Yesu akiwa na umbo kama njiwa Luka 3;22, Njiwa ni alama ya
amani busara na utulivu hizi ni tabia alizo nazo Roho wa Mungu, kwakuwa Roho
huzungumza kwa upole ni muhimu kuwa makini kumsikiliza, tunapokataa mashauri
yake na kuipinga sauti yake ya upole inayotushauri mambo bora ndani ya mioyo
yetu tunamzimisha na wakati mwingine tunamuhuzunisha kiasi cha kuugua na anapotuacha
amani ya kweli hutoweka lakini akiwepo amani huwepo Hata hivyo Roho wa Mungu ni
mwaminifu sana kwa waamini na kwa kusudi la Mungu lilioko ndani mwetu.
ROHO MTAKATIFU NDIYE ALIYEVUVIA MAANDIKO
Maandiko
yaani Biblia ni kazi ya Mungu na Roho Mtakatifu ndiye muhusika mkuu wa
usimamizi wa kazi ya maandiko
Umuhimu wa maandiko
Neno la Mungu lililoandikwa
lilihitajika kwa ajili ya wokovu kwa sababu tunahitaji ujuzi na kweli za wokovu
wetu ambao msingi wake ni katika kufa na kufufuka kwake Yesu Kristo kwani
hatuwezi kujiokoa wenyewe kupitia matendo yetu mema na mawazo yetu mazuri
Mungu ni Mungu aliyetamani kujifunua kwa
wanandamu yeye mwenyewe na ili kazi yake anayoifanya iweze kujulikana kwa miaka
na miaka mpaka wakati huu tulionao leo watu
wanahitaji nakala ya yale Mungu aliyokuwa anasema na ambayo anatenda.
Kwa hivyo neno la Mungu ndio
njia pekee ambayo kwa hiyo tunaweza kujua na kuelewa na kuamini kweli kuhusu
Mungu na mpango wake kwa wanadamu na hivyo neno lazima lienezwe Warumi 10;13-17.
Matendo ya Roho Mtakatifu na Neno lililovuviwa
2Petro 1;20-21, Manabii ambao waliandika
neno la Mungu waliongozwa na Roho Mtakatifu walitii na kukubali kuubeba mpango
wake kwa wanadamu wengi walijitambulisha kwa jumbe zao kuwa zinatoka kwa Mungu.
Neno Neno la Bwana likanijia limetajwa mara 3,800 katika Biblia hii ikijumuisha
neno asema Bwana wa majeshi Roho aliwaongoza katika njia ya moja kwa moja
akiwapa wao neno la Mungu
Matendo mengine yalifanywa na
watu katika agano la kale kwa uongozi wa Roho Mtakatifu mfano
·
Gideoni alipiga tarumbeta baada ya kujiwa na Roho wa
Mungu Waamuzi 6;34
·
Samsoni alimchana mwana simba vipande baada ya kujiwa na
Roho Mtakatifu Waamuzi 14;4
·
Sauli aligeuzwa kuwa mtu mwingine na aliweza kutabiri
baada ya kujiwa na Roho wa Mungu 1Samuel 10;6
·
Wanafunzi walinena kwa lugha baada ya Roho Mtakatifu kuja
juu yao Matendo 24;10;46 19;6.
·
Roho Mtakatifu alivuvia watu kuandika Neno la Mungu-
wengi walioandika neno la Mungu hawakufanya hivyo kwa mapenzi yao walifanya
hivyo kwa kuwa Mungu Roho Mtakatifu aliwataka kufanya hivyo 2Petro 1;20-21,
·
Roho Mtakatifu hufanya kazi ya kutuangazia au kutufunulia
neno la Mungu kusudi tulielewe vema, Roho Mtakatifu ambaye aliwaongoza
waandishi kuandika neno la Mungu hufanya
kazi ya kumuangazia au kumpa ufunuo mtu anayelisoma neno la Mungu akiwa na Moyo
uliovunjika na kutaka kujua humpa ufahamu.tafasiri na namna ya kulitumia neno
hilo kwa usahii kusoma pekee hakuwezi kusaidia kupata ufahamu kuhusu kweli za
kimaandiko 1 Koritho 2;14 Mungu hakumtoa Roho Mtakatifu kwa kusudi tu la
kuongoza waandishi bali pia kwa kusudi la kuangazia neno la Mungu kwetu ili
kutimiza kusudi ambalo Mungu amelikusudia liweze kutimizwa hivyo kuangaziwa au
ufunuo hutusaidia katika kuyaelewa maandiko, kutafasiri na kuyatumia.
Asili ya uvuvio
Ni
nini maana ya neno uvuvio? Kwa bahati mbaya si makanisa yote yanakubaliana na
wazo la uvuvio. Kwa miaka mingi sana kumekuweko na hoja mbalimbali na mawazo mbalimbali
yatolewayo kuhusu uvuvio wakati mwingine yana ukweli lakini yanakuwa magumu
kuelezeka
A:Mawazo mablimbali yasiyo sahii sana kuhusu uvuvio
Uvuvio Asili
au Ufahamu wa kupita kawaida intuition theory
Wao
huamini kuwa uvuvio ni tendo la kawaida la uwezo wa kufahamu ulio juu ya
viwango vya kawaida wao huamini ni uwezo wa kawaida wa binadamu kuwa kwa uwezo
wa asili anakuwa na viwango vya juu vya ufahamu ambapo huweza kupata kweli za
rohoni.
Udhaifu
wa wazo hili
Hufanya
uvuvio wa kibiblia uwe hauna tofauti na maandiko yoyote ya kawaida
yaliyoandikwa kwa viwango vya juu kama yale ya akina Willium Shakespeare na
nyimbo kuu za kanisa, Hii inachanganya kati ya kazi za Roho Mtakatifu aktika
kuvuvia na kuangazia au kufunulia, Kuangazia hakuhusiani na kuleta kweli mpya
bali kuielewa kweli ambayo tayari imekwisha funuliwa katika neno.
Uvuvio
wa baadhi ya maandiko tu Partial inspirations theory
Wao
huamini kuwa Mungu alitoa uwezo uliohitajika na wa kuaminika katika kulileta
neno la Kweli la Mungu kwa waandishi walioamriwa kuandika kwa hivyo iliwafanya
wasikosee katika baadhi ya mambo ya imani lakini si katika mambo mengine mfano
waliweza kukosea katika maswala ya kihistoria na kisayansi
Uvuvio
wa mawazo na sio maneno
Wao
huamini kuwa Mungu alivuvia wazo la ufunuo fulani lakini aliwaachia wanadamu
hao kuamua kuwa watayaandika vipi. Dhana ya wazo hili si sahii ni vigumu
kufikiri wazo kisha ukaandika tofauti,wazo linaweza kutafasiriwa vizuri kwa
maneno hivyo tunaamini kuwa maneno yalivuviwa na sio swala la mawazo.
Uvuvio Huria
Hawa
huamini kuwa Biblia ina maneno ya Mungu hii ina maana kwamba pia yako maneno ya
kawaida ya watu ambayo yamechanganyika, wanaamini kuwa ni kitabu hasa cha
kidini lakini kuna Historia, Habari, vizazi, mashairi ya kimapenzi, mipangilio
na mambo yasiyopangiliwa wala kujali mtiririko maalumu au kamili. Dhana
hii inataka kuhatarisha kwani ina maana
kuwa waandishi walijiamulia tu wapi waandike wapi ni uvuvio wapi hawakuvuviwa
wapi Mungu anazungumza na wapi mwanadamu anaweka mkono wake
Uvuvio wa Imla
Hawa
huamini kuwa manabii walipopokea uvuvio
wa kuandika waliandika moja kwa moja kile ambacho Mungu alikuwa akikisema hii
inamaanisha wao walikuwa kama kalamu tu, Roho aliwavaa kiasi ambacho hawakuwa
na uhuru wao wenyewe isipokuwa kuandika kile Mungu anachokusudia kwa hivyo huamini kuwa kila neno lilitoka
moja kwa moja kwa Mungu na hivyo wao walifanya kazi kama mashine tu Dhana hii
siyo sahii kwani Mungu alitumia watu na sio mashine au vifaa, Mungu hakuwafanya
wasiwe na ubinadamu wao hivyo si kila kitu waliandika si kama bomba la
kupitishia moja kwa moja kile Mungu alichokisema lakini waliandika kile ambacho
Mungu alikuwa akikiweka katika mioyo yao
B: Mawazo Mbalimabli sahii kuhusu uvuvio
·
Uvuvio shirikishi - Uvuvio lilikuwa tendo la Roho
Mtakatifu kwa waandishi akifanya kazi pamoja nao na kazi yao ilikuwa ni
kusikiliza na kutii na kuandika
·
Uvuvio ulikuwa ni muongozo wa Roho Mtakatifu kwa
waandishi akiwaongoza katika kuchagua nini cha kuandika na maneno ya kuandika
·
Roho Mtakatifu aliwalinda waandishi kutoka katika kukosea
na kuruka uvuvio huu ulihusu kile kilichoandikwa na haikuwa lazima yawe mawazo
au fikra
·
Mungu aliwafanya waandishi kuwa wafanya kazi pamoja naye akitumia
misamiati yao, mitindo yao ya uandishi na uzoefu wao katika kuzipeleka kweli
·
Maandiko yamevuviwa kwa sababu ni matokeo ya kazi ya Roho
Mtakatifu kupitia waandishi yeye aliwaongoza katika kazi nzima ya uandishi ili
kwamba kweli ya Mungu iweze kunukuliwa katika Biblia kama neno kamili la Mungu.
C:
Kweli halisi
·
Uvuvio ni msingi wa kuaminika kwa Biblia na hapa
tunaizungumzia Biblia yoote
·
Biblia nzima kwani imevuviwa ni sahihi haina makosa na ni
halisi haijatiwa mkono
·
Ni sahii katika maswala yoote ya kihistoria au kisayansi
na maadili na maswala ya mafundisho kwa wanadamu
·
Ukweli huu ni kwa maandiko yoote katika Biblia bila
kuwekea mipaka kwamba ni baadhi ya mafundisho yake tu ndio yamevuviwa
D: Tafasiri sahii
·
Neno lina mawazo mbalimbali kuhusu Mungu, Kristo, Msalaba,
Ufufuo na ubatizo wa Roho Mtakatifu
·
Ina nukuu halisi na tafasiri sahii kuhusu kweli nyingi
·
Ndiyo inayotupa ukweli na muongozo sahii kwa ajili yetu
E: Roho
Mtakatifu ni Roho wa kweli na nguvu.
·
Mungu ni Mungu mkamilifu na mnyoofu katika njia zake
·
Yesu ni Kweli
·
Roho Mtakatifu ni Roho wa kweli
·
Kila kinachozungumzwa katika maandiko kuhusu Mungu,Yesu
na Roho Mtakatifu ni cha kweli Biblia inatuambia kweli zote zinazomuhusu Kristo
na Mungu na kile ambacho Yesu alisema kuhusu Roho Mtakatifu ni halisi Roho
anabeba ushahidi huo
Mamlaka Ya Roho Mtakatifu
Uvuvio unaifanya Biblia kuwa kitabu pekee
ambacho ni muongozo wa kweli wa imani na maisha
Mamlaka ya Biblia.
Imefungwa pamoja na mwanadamu inajua mawazo
yake, dhamiri yake moyo wake na matakwa yake na inamuongoza katika imani
sahihi,Waebrania 4;12-13 aidha Biblia ina njia sahii na muongozo sahii Roho
aliivuvia na analitumia neno kuwa muongozo wa maisha yetu, Jukumu letu ni
kulisoma, kulitafakari na kulitendea kazi Roho pekee anajua mapenzi kamili ya
Mungu na kwa msingi huo anajua ni namna gani atuongoze na amechagua maandiko
yawe Muongozo wetu kwa kuyavuvia
Andiko huua
Ukitumia akili zako tu kutaka kuyafahamu
maandiko utaharibikiwa wengi wanaofuata yaliyoandikwa tu bila msaada wa Roho
Mtakatifu wameishia katika ufarisayo uliokithiri au uhuru usio na mipaka
Msingi wa Kumtegemea Roho katika Kuyafahamu maandiko
Yesu
aliyajua maandiko na alifahamu kuwa yanaongoza lakini alitaka watu wayafahamu
kwa usahii kwa hivyo alileta tafasiri sahihi kwa matumizi ya neno, Roho Mtakatifu
anayajua maandiko na hutusaidia kuichunguza Biblia kupata muongozo unaohitajika,
Hivyo basi tunahitaji msaada wa Roho Mtakatifu katika kuielewa Biblia vema na
kuitii,Tunahitaji kufikiri zaidi ya andiko moja kuelewa lipi jema na lipi baya
Roho mtakatifu hutupa ufunuo wa neno kupitia ufunuo wake wa kiungu ufahamu huo
unaitwa Dechomai kwa kiyunani.
·
Ufahamu wa kawaida wa kiakili “Oida” Oida
·
Ufahamu wa kawaida wa kisomi au kisayansi
“Ginosko” Ginosko
·
Ufahamu wa kawaida mwepesi
“lambano” Lambano
·
Ufahamu unaotokana na Ufunuo wa Roho wa Mungu na
shuku ya kiungu “Dechomai”Dechomai
Roho Mtakatifu hutumia neno
Baadhi
ya watu hujaribu kumfuata Roho Mtakatifu bila kukubaliana na neno au mamlaka ya
Biblia.Kifaa kikuu Roho mMakatifu anachokitumia katika kutuongoza ni maandiko
yaani Biblia Neno la Mungu pia huitwa upanga wa Roho kwa hivyo basi Neno ni
silaha ya pekee ya Roho Mtakatifu ni kupitia neno na Roho Mtakatifu sisi nasi
tunaweza kuwa nyenzo yake Roho husimama na neno na hajipingi mwenyewe
ROHO MTAKATIFU NI MUUMBA NA MTIA UZIMA
Mshirika katika uumbaji Mwanzo 1;2 Kuna
uhusiano wa Roho Mtakatifu na Mungu Baba na Mwana katika uumbaji.
·
Uumbaji ni jambo lililohusisha utatu woote wa Mungu
katika hali ilyo sawa Baba ni muumba ndiye aliyeumba mbingu na inchi na bahari
na vyoote viujazavyo na ni chanzo cha uhai Matendo 4;24
·
Mwana pia ni mtoa uzima
jukumu lake ni la pili katika uumbaji Yohana 1;3 kwa maana kupitia yeye
umbaji wote ulifanyika, Mungu alisema naye kama alivyosema na manabii Yeye
alikuwa ni neno halisi la Mungu na kupitia yeye ulimwengu ulifanyika na kuweko
·
Roho Mtakatifu ni mtoa uzima pia na ndiye anayehakikisha
vitu vyote vinahaishwa pasipo Roho hakuna uzima
ni nguvu ya uumbaji wa Mungu na ndiye aliyefanya mambo yatokee au ndiye
aliyetenda neno lilipotoka Zaburi 104;30.katika Agano la kale Roho
Mtakatifu alipewa upekee kama nafsi yeye
alikuwa neno lililohai na njia ya uumbaji wa vitu vyote
Roho wa Bwana akatulia juu ya uso wa maji
Kazi
za Roho Mtakatifu zinaonekana katika uumbaji kwa kuanzia na Mwanzo 1;2 Biblia mojawapo ya kiingereza cha kisasa inasomeka
hivi.- ”A mighty wind that swept over the surfece of water” kwa hivyo wao
hupotosha maana halisi kwa kumchukulia Roho Mtakatifu kama upepo wa mvumo wa machafuko Tornado hii si dhana sahii kwani
hakukuhitajika upepo wa jinsi hii wakati Mungu akiwa kazini Biblia inasema Roho wa Mungu na sio upepo wa
mvumo Roho wa Mungu hutumika kuelezea sikuzote Nguvu za utendaji wa Mungu au
uwepo halisi wa Mungu kivitendo na kutulia juu ya uso wa maji ni kinyume na
upepo wa mvumo je upepo wa mvumo unawezaje kutulia? Tafasiri kama hizi
zinapingana pia na kile tunachosoma katika maandiko mengine ya Biblia kumhusu
Roho Mtakatifu na matendo yake katika uumbaji
Roho Mtakatifu na uumbaji wa Mwanadamu
Roho Mtakatifu pia amehusika katika
uumbaji wa mwanadamu, Mungu alipomuumba mwanadamu alijumuisha wingi alionao kwa
kusema na tumuumbe mwanandamu kwa sura na mfano wetu (Utatu) sura na mfano hapa
ilimaanisha hali ya kiroho na kimaadili kwa asili ndani ya mwanadamu ni ya
Mungu katika uumbaji huu kazi ya Roho Mtakatifu inaonekana katika kumfanya
mwanadamu awe na asili halisi ya Kiroho, haki, utakatifu na maarifa
Pumzi ya Mungu
Roho
Mtakatifu huitwa pia Pumzi ya Mungu katika uumbaji anagalia Ayubu 33;4 kwa
hivyo pumzi ya Mungu ni sawasawa na Roho wa Mungu kwa hivyo katika uumbaji Roho
wa Mungu hufanya yoote huuisha kimwili na kiroho, Pumzi hii ya Mungu pia
ilifanya kazi ya kumtofautisha mwanadamu na mnyama wa kawaida hivyo ni
mwanadamu pekee anyebeba sura na mfano wa Mungu na hivyo kumfanya mwanadamu
pekee kuwa na uwezo wa kuwasiliana na Mungu na kumuabudu, Roho wa Mungu
alifanya kazi katika maisha ya mwanadamu wakati wa uumbaji akijihusisha na maandalizi
ya uumbaji huo na pia kuweka uzima wa kimwili na kiroho na hivyo mwanadamu
akawa kiumbe hai neno nafsi linamaanisha mtu kamili, mwenye pumzi ya uhai na
mavumbi ya nchi mwenye uwezo wa kujitegemea na kuwa na maamuzi yake mwenyewe na
kuweza kufanya kile anachoamua kufanya
Roho ya mwanadamu Mwenyewe.
Hapa
tunahitaji kujifunza tofauti ya roho ya mwanadamu mwenyewe na Roho Mtakatifu na
pia kuangalia anguko la mwanadamu baadhi ya watu wamekosea na kuwafundisha watu
kuwa wao ni miungu au hata wao ni Yesu hawa ni watu wanaoamini kuwa mungu ni
kila kitu na kila kitu ni mungu wanamfanya Mungu kuwa anafanana na uumbaji wake
woote lakini kwa hakika sisi sio Mungu
Wengine huamini kuwa maisha ya mwanadamu
na roho ya mwanadamu ni Mungu mkubwa ndani yake, Ni kweli kuwa roho zetu hutoka
kwa Mungu na kwake hurejea lakini hii haimaanishi kuwa mwanadamu ni mungu kwa
kiasi ndani mwake na ndani yake tena Roho Mtakatifu kwa ujumla hii inamaana ya
kuwa mwanadamu hawezi kwa namna yoyote ile kuwepo katika mwili bila uhai ambao
Mungu anatoa hivyo roho ya kibinadamu sio Mungu ndani ya mwanadamu Kumbukumbu
la Torati 2;80
Kama ni hivyo inawezekanaje Roho
nzuri ikapingana na Mungu, Mungu hawezi kijipinga mwenyewe au asili yake
Wengine wanaamini kwa sababu ya anguko
roho ya mwanadamu imekufa na haziko mpaka zinapoitwa tena wakati wa kuzaliwa
mara ya pili Torati 2;30 inaonyesha kuwa ingekuwa vigumu roho hiyo kufanya
ugumu kama imekufa au haiko, Mwanzo 9;6 inaheshimu sura na mfano wa Mungu ndani
ya mwanadamu kwa kukataza mauaji,Kwa matokeo ya dhambi sura na mfano wa Mungu
ndani ya mwanadamu imeathiriwa imekuwa katika hali mbaya lakini iko palepale na
hii ndio maana mtu muovu mtu wa dhambi bado pia hutenda mema na mambo ya
kuvutia mazuri kama miziki, mashairi, uvumbuzi wa vitu mbalimbali katika
teknolojia sayansi na madawa n.k.
Uhusiano wa Roho Mtakatifu na roho ya mwanadamu na asili
ya anguko la mwanadamu
Roho ya mwanadamu kwa asili iliumbwa na
Mungu kupitia Roho Mtakatifu, Hivyo Roho Mtakatifu ni asili ya mambo yoote
mazuri aliyonayo mwanadamu.
Anguko la mwanadamu.
Tunataka
kujifunza kwanini mwanadamu anahitaji kuzaliwa upya kupitia Roho Mtakatifu, Hii
ni kwa sababu kupitia anguko la mwanadamu athari iliyojitokeza ni ya kimwili na
kiroho na imeathiri maisha yote ya mwanadamu na utendaji wake, Dhambi
imeharibu mambo mazuri ya mwanadamu na
wakati woote anakusudia maovu, mwanadamu amekufa kiroho kwa hivyo hawezi
kumpendeza Mungu wala kutimiza kusudi la Mungu, jambo la msingi kwa mwanadamu
ni kuzaliwa mara ya pili na kuupokea wokovu kwa imani na kupitia neema
inayotolewa na Mungu kupitia Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu hutufanya upya na
kutuwezesha na hii ndiyo kazi ya Roho wa Mungu hata baada ya anguko la
mwanadamu, Roho huendelea kufanya kazi ya kutuumba kwa upya na kututia nguvu
katika hali zote ya kimwili na kiroho Mwanzo 3;15 tunahaidiwa wokovu
Utendaji wa Roho Mtakatifu baada ya Anguko la mwanadamu.
Ayubu
34;14-15 na Zaburi 104;30 zinaonyesha kazi endelevu ya Roho Mtakatifu kwa
ujumla wake baada ya uumbaji
·
Hutia nguvu na uzima kwa ulimwengu na kwamba bila Roho wa
Mungu hakuna uhai unaoweza kuendelea
·
Hufanya kazi kwa ulimwengu kuwaonyesha njia, akihukumu
matendo yetu kuturekebisha na kututia nguvu kuendelea kiroho kama tunakubali
msaada wake.
·
Mungu ameweka kanuni fulani za kawaida na za kimaadili na
ni Roho wa Mungu anayesukuma sisi kuzifuata kanuni hizo na hizi hufanya kazi
kwa wasiookolewa kwa ufunuo wa ujumla na kwa waliookolewa kwa ufunuo maalum
·
Yeye kazi yake si kuhukumu ulimwengu tu wakati woote
lakini hufundisha hushauri na kututhibitishia lililo jema au lililobaya kwa
kusudi la kutufanya tuachane na uovu Roho alifanya hivyo kwa watu wa Efeso Matendo
19;1,23-27 ambapo watu waliokuwa wakijishughulisha na uchawi na uganga waliacha
uovu huo kwa wingi wao, Popote pale ulimwenguni inapotokea ukristo unashuka
katika viwango inatokea kumomonyoka kwa maadili kwa kiasi kikubwa, maovu na mauaji na mengineyo
yakishamiri,Mungu alitembea kabla ya gharika na wanadamu waliokubali kutembea
nae, alitembea na Enoko na alimchukua juu, alitembea na Nuhu na alimwokoa na
gharika na alitembea na Seth na kuuchagua uzao wake kuwa baraka duniani, Mungu
amekuwa mwaminifu kutembea na wengi walioongozwa na Roho wake na ambao walikuwa
kama chombo cha Roho Mtakatifu cha kuionyesha njia ulimwenguni Seth ulikuwa
ukoo uliohaidiwa kumleta masihi mkombozi wa ulimwengu Mwanzo 3;15, Enoko
aliyetwaliwa kama ishara ya wokovu kwa wale watakaomcha Mungu, Mahalalel mtu
aliyemsifu Mungu na kuliitia jina la bwana ishara ya wito wa Mungu kuabudiwa na
wengine wengi
·
Biblia inaonyesha kuwa Mungu hajawai kukiacha kizazi
chochote bila watu walioishi kwa ushuhuda wake na hataacha kufanya hivyo hata
milele.
Roho Mtakatifu anataka watu wazaliwe kwa upya
Katika
kitabu cha mwanzo Mungu anaonyesha dalili za kinabii za Roho Mtakatifu kuhitaji
watu wazaliwe mara ya pili hili linathibitika kwa maswala muhimu yafuatayo
Mwanzo 6;5-8
·
Wakati wa Nuhu aliangamiza wenye dhambi woote na kuanza
kizazi kipya cha mwanadamu wale waliomcha yeye
·
Kuzaliwa kwa upya kunakohitajika leo ni kuzaliwa kiroho
kwa watu kufanya maamuzi ya kumgeukia Mungu na kupewa neema ya kuushinda uovu
wakisaidiwa na Roho wa Mungu
·
Kuzaliwa huku kwa upya kunaweza kupatikana si kwa nguvu na jitihada zetu bali kwa
kuzaliwa kwa upya kunakotokana na Roho wa Mungu na njia ya kutunza maisha hayo
mapya katika Kristo ni kwa kuendelea kuwa na ushirikiano na Roho Mtakatifu
tukitazamia kuishi maisha makamilifu kama ya Mungu hebu hiki kiwe kilio cha
maisha Yetu siku zote kutamani kuishi maisha kama yale aliyoishi Kristo
Sura
ya Pili; ROHO MTAKATIFU WAKATI WA AGANO LA KALE
Roho Mtakatifu na Mwanzo wa Israel
Abrahamu
na mababa wa Israel
Ni wazi kuwa Abrahamu na mababa wengine wa
imani walikuwa ni watu walioongozwa na Roho Mtakatifu ,Abrahamu alikuwa mtu wa
imani na kwa kweli historia yake ni wazi
kuwa ni historia ya Mtu aliyetembea na roho Mtakatifu na itakuwa ni jambo la kushangaza sana Kama
Abrahamu Mtu ambaye Paulo anamtumia kama Mtu wa Imani katika Warumi 9;1-22, Wagalatia
3;6-18 kisha akawa mtu amabye hakujazwa kwa Roho mtakatifu
Abrahamu alikuwa Nabii Mwanzo
20;7
Nabii ni mzungumzaji kwa niaba ya
Mungu,mungu alizungumza naye na alimpa maelekezo ya kufanya kama alivyofanya
kwa wengine,aliwafundisha wengine kumuabudu Mungu wa kweli madhabahu alizozijenga ilikuwa ni ibada za
wazi zenye kumshuhudia Mungu wa kweli,na Kama ilivyo kwa manabii wengi
aliwaombea wakosaji aliomba kwa ajili ya Sodoma jambo lililofanywa na manabii
wengine kama Musa Hesabu 14;13-20,Kmbukumbu 9;20 1Samuel 7;5,12;19,23 yeremia
7;16 na Amosi 7;2,5 mungu aliwaita wasiofaa ili awafanye wakamilifu Mwazno 20;7
Ibrahimu akisema uongo, Manabii waliongozwa na Roho Mtakatifu
Wapakwa mafuta Zaburi 105;8-22
Abrahamu, Isaka, Yakobo na Yusufu walikuwa
wateule wa Mungu na walipakwa mafuta kama manabii wa Mungu.Mungu aliwatumia
hawa woote kama wanenaji kwa niaba ya Mungu kwa sababu karibu wote walikuwa
sehemu ya kutimiza agano la Mungu alilolifanya na Ibrahimu Mwanzo 12;1-3 unabii
huu ulihusu
·
Baraka binafsi za Ibrahimu
·
Baraka kwa taifa la Israel
·
Na Baraka kwa ulimwengu mzima mwanzo 12;1-3
Kupakwa mafuta katika Biblia ilikuwa ni
ishara ya kujazwa kwa Roho mtakatifu Zaburi 105;15 ingawa hatuoni hawa
wakipakwa mafuta kwa ishara lakini Roho alikuwa juu yao aliwatetea na walikuwa masihi zake kwelikweli
Mwanzo 12;3,Zaburi 105;15 au 105;8-14 Mungu hapa aliwalinda masihi zake hao
kutoka kwa Wafalme kama Farao na Abimeleki ambao waliwasumbua Ibrahimu na Isaka,yakobo
na hata Yusufu,ulinzi wa Mungu kwa masihi wake ni wa uhakika Yeremia
1;7,9,17-19, ili tuweze kuendelea kuufurahia ulinzi huu kuendelea katika imani
ni muhimu pamoja na kuendelea kutii 1Falme 13;1-32
Baada ya Yusufu kufasiri ndoto ya Farao yeye mwenyewe alikiri kuwa Roho wa Mungu
alikuwa juu ya Yusufu Mwanzo 41;38.
Roho Mtakatifu na Ujenzi wa Hema ya kukutania
Kutoka 31;2-3,35;30-31 ujenzi wa hema ya
kukutania ulifanyika kwa ajili ya Mungu na kwa utukufu wake,Hema hii ilijengwa
kwa kusudi la kuwafundisha Israel kufanya kazi pamoja na kuwa hema ilikuwa ni
mahali ambapo mungu angeendelea kufunua uwepo wake,Ujenzi wake ulikuwa wa ajabu
hii inatufundisha kuwa kazi ya Mungu inahitaji zaidi ya juhudi za kibinadamu
tunahitaji mguso wa upako wa Roho Mtakatifu
ili Mungu atukuzwe katika lolote tulifanyalo,ujuzi wetu na elimu yetu na
ufundi tulionao unaweza kunolewa kitaalamu zaidi kwa upako wa Roho Mtakatifu
Mungu alimjaza Bezaleli na Aholiabu kwa
Roho wake mtakatifu kwa ajili ya ujenzi wa hema ya kukutania na kuwafundisha
wengine hivyo Bezaleli na Aholiabu walikuwa ni wajenzi pakee wa Hema waliojazwa
kwa Roho Mtakatifu Roho ndani yao alikuwa ndiye chanzo cha hekima ,ufahamu
ubunifu na maarifa na utendaji mzima uliohitajika Kutoka 31;2-3,35;30-31 kwa
msingi huu basi mungu alifanya hivyo ili kwamba Bezalel na Aholiab
wasizitegemee akili zao za kawaida na
ujuzi wao pekee bali wa Bwana, Hekima iliwasaidia kuwapa ubunifu na nini cha
kufanya ili kufikia lengo lililokusudiwa, Maarifa yaliwasaidia kujua nini
kinahitajika na ni njia gani itumike kukamilisha lengo ufahamu uliwapa mwanga
na ujuzi wa kufanya maamuzi Hili linatufundisha kuwa wahubiri, wanamuziki,
waimbaji na watendaji mbalimbali wa kanisa tunamuhitaji sana Roho mtakatifu
katika kazi zake.
Roho Mtakatifu juu ya Musa na wazee sabini wa Israel
Hesabu 11;10-30
Roho mtakatifu alihisika kipekee juu ya
uongozi wa Musa na wana wa Israel,Musa aliitwa nabii ni Mungu mwenyewe
aliyemuita kuwa nabii katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto Hesabu 12;6-8,kutoka
3;6-15,4;14-16 na 7;1-2 hata ingawa Mungu alimtumia Haruni kuzungumza kwa niaba
ya Musa bado mungu alizungumza na Musa kwanza hivyo musa alikuwa nabii,mungu
aliweka Roho wake ndani ya musa Hesabu 11;17 kwa kweli Roho anatosha kwa
mahitaji yetu.
Mzigo wa uongozi kwa Musa ulikuwa ni
mkubwa sana na alimwambia mungu kuwa huu ni mzigo usiobebeka na ambao ni kama
baba aliyeachiwa mtoto mchanga jibu la Mungu kwa Musa lilikuwa ni kama makemeo
kwa sehemu hata hivyo alimshauri Musa kuchagua wazee sabibi kwa sifa za
kumsaidia Kutoka 18;18-26, Mungu alishuka na kutwaa sehemu ya Roho juu ya Musa
na kuwajaza wale wazee ili wamsaidie kwa huduma na kuubeba mzigo pamoja nae na
kuamua kesi mbalimbali na kuwatia moyo watu wa Mungu. Mungu ni kama alikuwa
akimfundisha Musa kuwa angeweza na kuwa alipaswa kumtegemea Roho Mtakatifu kwa
kazi hiyo Roho Mtakatifu ni mkuu mno kiasi cha kutuwezesha kubeba Mzigo wowote
na changamoto zozote tunazoweza kukutana nazo
Kuishi chini ya Viwango alivyokusudia Roho Mtakatifu
Hesabu 11;26-29
Baadhi ya wazee wale waliopokea Roho
mtakatifu walifurahia swala hilo kwa muda mfupi na baadae nguvu ile
ilikoma,Baadhi ya wazee wawili Eldadi na Medadi waliokuwa wameitwa na Musa
miongoni mwa wale sabini lakini hawakwenda katika hema lakini nao walijazwa
Roho hukohuko walikokuweko wao kwa bahati nzuri Roho alidumu ndani yao na
waliendelea kutabiri kambini Yoshua alitamani Musa awazuie hata hivyo Musa
alimkemea kuwa asiwe na wivu kwa ajili yake kwani angetamani kama wote
wangejazwa kwa Roho Mtakatifu.
Mwanatheolojia Origen aliifananisha Roho
iliyokuwa juu ya Musa kama taa ya vinara sabini iziyozimika. Musa alijua kuwa
kutenda kazi kwa Roho mtakatifu hakuko juu ya uwezo wake wala sehemu au mahali
maalumu wala muda,Mungu hutoa viongozi wa kibinadamu lakini mamlaka yao haiwezi
kuzidi Mamlaka ya Roho Mtakatifu na Neno lake,Viongozi wa kiroho ni lazima
wawaongoze watu katika utendaji wa karama za Roho Mtakatifu sawasawa na neno bila wivu wowote Musa
aligundua kuwa watu wenye kunung’unika,wenye kuasi,wasioamini wanaishi chini ya
kiwango alichokusudia Roho Mtakatifu,Kwa kawaida watu woote walitakiwa kuwa
kama Eldadi na Medadi ambao Roho aliendelea kuwa wakudumu katika maisha yao
Tamaa ya Musa ya kutamani watu woote wawe Manabii ilitabiriwa na nabii Yoel
katika Yoel 2;29-29 na kutimizwa siku ya Pentekoste katika Matendo 2;4,16
Roho Mtakatifu na ulinzi dhidi ya Israel Hesabu 22
Wakati wa agano la kale sio tu Roho
Mtakatifu alishughulika na Muwsa tu bali pia aliwashughulikia maadui wa Israel,
Mfalme balaki wa Moabu ni moja ya watu
waliopambana na utendaji wa Roho Mtakatifu Israela walikuwa wanakuja kwa
ushindi na tayari walikuwa wameshaishinda miji ya Gilead na bashani ng’ambo ya
mashariki ya mto Yordani mfalme alipoona aina ya ushindi aliogopa akitambua ya kuwa alikuwa akifuata
katika kupoteza ufalme wake na alifahamu
kuwa Nguvu ya Israel ni ya Rohoni na si vinginevyo (Bwana alikuwa pamoja nao)
na kwa jinsi hiyo basi alihitaji Bwana ageuke dhidi yao kama njia ya kuwapata
israel na kuwashinda alimtafuta mtu
aliyeitwa Balaam ili awalaani na sio kuwabariki balaam alitoa sadaka nyingi
kila kilima alipopokea baraka badala ya laana kwa Israel alihamia kilima
kingine ili apate kibali kwa Bwana awalaani Israel Roho wa Mungu alimtumia
Balaam kuwabariki Israel,Kwakweli balaam
alikuwa ni mpiga ramli tu na alikuwa nabii wa uongo au mchawi kwa lugha rahisi
wachawi hao wa zamani waliamini kuwa wangeweza kumshawishi Mungu yoyote yule
akubaliane na matakwa yao lakini badala
yake Mungu alimwamuru Balaamu awabariki Israel na kutoa unabii wa kweli Hesabu
22;21-35 Mungu alimshinda Balaam mchawi mashuhuri kwa Roho Makatifu
Balaam alitabiri na unabii wake ulitoka kwa
Roho Mtakatifu,Yeye alitabiri ushindi kwa Israel na alirudia kile alichotamkiwa
Ibrahimu katika Mwanzo 12;3 na sehemu ya unabii wa balaamu ulimuhusu masihi
Yesu Hesabu 24;17 kumbe Mungu aweza kutumia uovu katika kutimiza makusudi yake
alimtumia Balaam mbabiloni Roho alimkalia kwa muda kwakuwa hakudumu ndani ya
Balaam na kwa uroho na uchu wa mali alikufa kwa kuipinga kweli na kuwa kinyume
na Israel.
Roho mtakatifu Juu ya Yoshua Hesabu 27;18;Kumbukumbu 34;9
Yoshua huenda ndiye yule kijana nayetajwa
kuwa alikuwa mtumishi wa Musa Hesabu 11;28 lakini inaonekana kuwa mahali fulani
wakati wa mahangaiko ya jangwani yaliyochukua muda wa miaka 40 hivi alijazwa na
Roho wa Mungu na hekima Kumbukumbu 34;9 Yeye alikuwa mtu ambaye Roho aliendelea
kudumu ndani yake Hesabu 27;18 la muhimu zaidi inaonekana kuwa aliendelea kuwa
mwenye kujaa Roho na aliyejifunza kumtegemea na hii ilipelekea kuchaguliwa kuwa
kiongozi baadae, Roho wa Mungu alikuwajuu ya Yoshua mapema zaidi hata kabla ya
Musa kumwekea mikono Hapa tunajifunza kuwa Roho wa Mungu hufanya kazi ya
kuwaandaa watu kwa kzi za uongozi wa watu wake, Roho alikuwa ameanza kumuongoza
Yoshua na kumfundisha mapema kabla mtu
yeyote hajajua kuwa Yoshua angekuja kuwa nani Mungu ni mwaminifu na si kusudio
lake kuwaacha watu bila ya kuwa na uongozi
ROHO MTAKATIFU KATIKA HISTORIA YA
ISRAEL.
Kuporomoka kwa Kiroho baada ya Yoshua
Ziko sababu kadhaa
zilizopelekea kuporomoka kwa kiroho kwa taifa la Israel baada ya Yoshua
·
Woote tunajua kuwa Mungu aliwapigania Israel na kuwapa
ushindi mkubwa kabla ya kifo cha Yoshua, Pia watu walikuwa wamemuahidi Yoshua
kuwa wangemtumikia Mungu.
·
Mungu alikuwa amewaamuru Israel kuwaondoa wakanaani woote
baada ya kuwa wamegawana inchi yote ya kanaani
·
Kabila ya Yuda waliwaondoa wakanaani woote walioishi
katika inchi ya milimamilima lakini walishindwa kuwaondoa wote waliokuwa katika
ukanda wa tambarale kwa sababu ya kutokuamini ,makabila mengine pia
yalishindwa kuwaondoa wenyeji wote wa kanaani nje ya mipaka yao kwa sababu ya kutokutii
,
·
Israel walipopata nguvu eti waliamua kuwatoza kodi
wakanaani badala ya kuwafukuzilia mbali hii ni kwa sababu ya Kupenda fedha
na starehe, Baadhi ya makabila pia walishindwa kuwaondoa wakanaani woote
nje ya mipaka yao Kushindwa kuwaondoa wakanaani
·
Waisrael wlishindwa pia kuzibomoa madhabahu za wakanaani
waliokuwa na ibada mbaya sana za mabaali na maashera hii ni kwa sababu ya kupenda
umaarufu wa kidunia.
·
Mafanikio yaliwaongoza katika kupenda starehe na ibada
zikawa za kawaida, Kizazi kilichofuata kilipuuziwa hakikupata kabisa mafundisho
ya kiroho wala hawakumjua Mungu kwa ajili yao wenyewe makuhani na viongozi
walikuwa wamebebwa na desturi za kikanaani zaidi hawakuwa na ujuzi binafsi
kuhusu Mungu wala hawakujua nguvu zake Kutokumjua Mungu, Walisikia
miujiza aliyokuwa ameifanya zamani lakini hawakuona lolote kwa ajili yao
wenyewe
·
Hatari hii ndiyo inayolikumba kanisa la leo kizazi
kilichopita kinaweza kukaa chini na
kusimulia tu yale waliyoyaona wao katika utendaji wa Roho Mtakatifu na karama
zake lakini hawawezi kuonyesha kivitendo ni namna gani kizazi kipya kinaweza
kutembea na Mungu Kizazi kipya kinakuwa makanisani wakisikia tu jinsi watu
walivyokuwa wakijazwa Roho Mtakatifu na miujiza iliyokuwa ikitendeka lakini
hawavioni kivitendo katika maisha yao mapya Leo hii hata watoto wa maaskofu na
wachungaji hawawajui Mungu wa Baba zao lakini Baba hao ni viongozi wa kiroho
makanisani wakiwa ni viongozi wenye kuiba sadaka za watu na wenye mahubiri
mengi kuhusu utoaji wakijilimbikizia posho kubwa wakiua wale wanaoonekana kuwa
na vipawa na kuwa rohoni kuliko wao wamepoa na imebaki historia tu katika
maisha yao na huduma zao huku wakiwa wamedumaa kiroho , hawakui wala hawaruhusu
mafunuo ya kimungu katika mioyo yao, hivyo wamebaki na mapokeo na misimamo ya
hovyo na isiyo ya kibiblia, Lazima tuamke na kuamua kuanza kufundisha kwa nguvu
na kwa upya kumhusu Roho Mtakatifu na kufanya maombi na maombezi
yatakayodhihirisha utendaji wake,
Roho Mtakatifu Juu ya Waamuzi katika Israel
Mungu alichagua waamuzi kwa njia
mbalimbali huku akiwajaza kwa roho wake Mtakatifu ili wafanye kazi za
kutawala,kuhukumu na kuwaokoa wanapoonewa,Waamuzi walikuwa pia viongozi wa
kimaadili,kisiasa na kiroho,Maisha ya kiroho wakati wa waamuzi yalikuwa kama
jinsi tulivyoona hapo juu kulikuwa na mzunguko wa aina hii
Mara nyingi walikuwa wakifanya dhambi na
dhambi hizo zilisababisha Mungu kuruhusu mateso kutoka kwa maadui zao
wakanaani, walipoteseka walikuwa wakihuzunika na kumlilia Mungu kwa toba huku
wakihitaji msaada wake Yeye alituma waamuzi akiwajza kwa Roho mtaklatifu na
waliwaokoa kisha walilala tena na kuanza kufanya dhambi, Ingawaje kitabu cha
waamizi kinawaita waamuzi hao Mwokozi lakini mwokozi halisi alikuwa ni mungu
mwenyewe Yeye aliwajaza waamuzi kwa Roho wake Mtakatifu na wakifanya kazi hiyo
ya wokovu wote walichaguliwa na Mungu na walitumiwa katika njia za tofauti
·
Othiniel alileta ushindi kabla hajaitwa kuwa mwamuzi kama
mtu alifanya jambo kwa imani na utii kwa Mungu alihesabika kuwa mtu waimani
kabla ya ujazo wa Roho mtakatifu Kwa uwezo wa Roho mtakatifu alitumiwa kuwaokoa kutoka kwa maadui zao wa
mesopotamia au waaramu na kuwashinda Waamuzi 3;10
·
Debora alikuwa nabii mke na inasadikiwa ndiye aliyekuwa
wakiroho zaidi ya waamuzi wote na aliitwa mwamuzi hata kabla hajaleta ushindi
wowote wa kijeshi watu waliamini kuwa ana uhusiano na Mungu alijulikana kwa
hekima ambayo mungu alikuwa amempa alipewa hekima hii na Roho Mtakatifu ili
kuwasaidia watu kuwaongoza na kuwafariji na kuwapa changamoto kuacha tofauti
zao
·
Gideoni Waamuzi
3;10,6;34 alitokea kabila ya manase na alitokea katika familia Muhimu
sana Roho wa Mungu alimvaa au alimjaa Gideon na hivyo alizivunja madhabahu za
baali na maashera na alipiga tarumbeta, alifuata maelekezo ya Mungu kuandaa
jeshi kwa ajili ya vita hatua ambazo zilihitaji utii na alileta ushindi
·
Yephta alitumiwa pamoja na kuwa na makosa Waamuzi
3;10,11;29,32 Yeye hakuwa muhimu katika macho ya watu alidharauliwa na
ulimwengu Mungu huweza kumtumia mtu bila kujali historia yake Roho alipomjia
alimuongoza kwenda vitani kuwashughulikia maadui walikuwa ni wana waamoni
waliokuwa wakiwatesa Israel Hata hivyo alishindwa kumtegemea Roho Mtakatifu
akidhani kuwa ushindi wake ungekuja kutokana na nadhiri ya kijinga
aliyoifanya hata hivyo roho hakupuuzia
nadhiri yake na ushindi ulipatikana Roho
wa mungu anapokuwa juu yetu huwa haingilii mapenzi yatu au matakwa yetu
·
Samsoni aliongozwa na Roho kufanya mambo ya ajabu Waamuzi
13-14,14;19,6 wazazi wake Samsono walikuwa wacha Mungu Mungu alimuandaa Samsoni
kabla hajazaliwa ,Alizaliwa akiwa Mnadhiri wa mungu yaani mtu aliyeywekwa wakfu
kwa ajili ya Mungu,Roho wa Mungu alianza kumtumia mapema katika maisha yake
,Ukweli kuwa mtu aliyekulia katika histiria ya uchaji wa Mungu sio uhakika wa
kuwa hataweza kufanya mambo maovu au ya kibinafsi,Roho alikuwa alimtumia Samson
kwa nguvu akimpa nguvu za kupambana na maadui,Kinyume cha hapo Samson huwa
mwanadamu wa kawaida kabisa.Jambo la msingi tunaloweza kujifunza kwa Samsoni ni
kuwa wanadhiri kwa ndani kujitoa kwa Mungu,kujiweka wakfu,na kuendelea kuwa na
ushirika wa kudumu na Mungu Roho Mtakatifu
Roho Mtakatifu Juu ya Manabii na Wafalme
Manabii kama Samuel na wafalme kama Saul
na Daudi nao walipakwa mafuta kwa uwezo wa Roho Mtakatifu wakati wao au wakati
wa Samuel Hekalu huko shilo lilikuwa limebomolewa na wafilisti walikuwa ndio
watawala wa wakuu katika inchi ,na sanduku la agano lilikuwa limetwaliwa,
Samuel aliinuka kuwa nabii,Mwalimu,kuhani na muombezi,Manabii wakati mwingine
walikuwa wanapakwa mafuta 1Wafalme
19;6,makuhani pia walikuwa wakipakwa mafuta suku zote kwa kazi hii Kutoka 30;30,40;13-15 na Wafalme
30;23-34,Wafalme pia walikuwa wakipakwa mafuta kwa ajili ya shughuli za ufalme
1samuel 10;1,16;3,12, 1Falme 34,30;23-34 mafuta hayo yalikuwa ni mafuta
maalumu ya mizeituni yaliyotengenezwa
kwa mchanganyiko maalumu Kutoka 30-23-34 na haikuruhusiwa kuyaigiza yalitumika
pia kupaka vitu vilivyowekwa wakfu au vilivyotumika katika hema ya
kukutania yakiashiria kuweka wakfu kwa
Bwana na yaliwakilisha uwepo wa Roho
Mtakatifu
·
Eli alimpaka mafuta Samuel mafuta haya yalikuwa na
mchanganyiko maalumu nna ilikuwa ni Ishara ya uwepo wa Roho Mtakatifu mwenyewe
na ni manabii,makuhani na wafalme waliopakwa mafuta hayo Mafuta ya kweli na
halisi alikuwa ni Roho Mtakatifu na sio yale mafuta yaliyokuwa ni alama tu ya
uwakilishi kwa Roho wa Mungu
·
Sauli na Daudi pia walipakwa mafuta,Daudi alipopakwa
mafuta Roho wa Mungu alikuja juu yake mara moja kwa nguvu na kukaa ndani yake
siku zote 1Samuel 16;13-14 lakini kwa Saul ilikuwa inakuja kwa muda tu Samuel
10;6
Roho Mbaya kutoka kwa Bwana ikaja juu ya sauli
1Samuel 16;14 Biblia inasema, ..”Basi Roho
ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua.”
.hapa kuna mijadala ya kitheolojia kuhusu roho mbaya kutoka wa Bwana
·
Wengine wanaamini ni ugonjwa wa kuweweseka ambao
uliruhusiwa na Mungu
·
Wengine wanaamini ni Pepo kutoka kwa shetani ambaye
alikuwa akimshambulia Sauli na kule kusema kutoka kwa Bwana maana yake ni kuwa
Mungu aliruhusu hii ni kama ile shida iliyompata Ayubu ambayo Mungu alikuwa
ameruhusu shetani kumshambulia Ayubu
· Wengine
huamini kuwa neno uovu hapa lilitumika kama hukumu yaani Mungu alituma Roho ya
hukumu juu ya Sauli kwa ajili ya dhambi zake
ROHO MTAKATIFU; KATIKA MAANDIKO YA
MANABII.
Roho Mtakatifu na Waandishi wa zaburi
Tangu
wakati wa Samuel na Daudi Muziki umeendelea kuwa sehemu muhimu katika ibada kwa
watu wa Mungu roho Mtakatifu alikuwa muhimu kwa waimbaji pia zaburi 51;11
Mwimbaji huyu bila shaka ni daudi anaomba asiondolewe Roho Mtakatifu Huyu
alielewa kuwa uwepo wa Mungu huendana na kuwepo kwa Roho Mtakatifu na namuomba
Roho amlinde asikosee tena,Zaburi pia zinaonyesha kuwa Roho Mtakatifu yuko kila
mahali anahitaji kutuongoza na kuhakikisha tunakua kiroho
Roho Mtakatifu na maandiko ya Ayubu na Sulemani
Ayubu
anamuhesabu Roho Mtakatifu kama muumbaji wa Mbingu Ayubu 26;13, na anaamini
kuwa uzima wake unatokana na kuwepo kwa Roho wa Mungu Ayubu 27;3 Elihum katika
Ayubu aliamini kuwa Roho wa Mungu huwapa akili wanadamu Ayubu 32;8
Suleimani pia anazungumzia habari ya
kumwagwa kwa roho wa Mungu ili kuwajulisha watu maneno ya mungu Mithali 1;23
Roho wa Mungu katika kitabu cha Wafalme na Nyakati
A.
Manabii Karibu
manabii wote waliongozwa na roho na walivuviwa na Roho Mtakatifu 1Petro 1;1-21,
kulikuwa na uamsho wakati wa baadhi ya wafalme,manabii walikuwa wanenaji kwa
niaba ya Mungu na waliweka msingi kwa ajili ya mambo yajayo manabii waliwatia
moyo wafalme na kukemea ibada za sanamu
wao wanacghukua nafasi muhimu katika kitabu cha wafalme Mungu aliwaongoza
kuzungumza kwa Roho wake
B.
Eliya na
Elisha, wakati wa Ahabu na Yezebel mungu alimuinua Eliya na Ghafala alianza
kufanya miujiza,Ahabu alikuwa mfale mwenye nguvu za kisiasa lakini alikuwa
dhaifu kiroho, Yezebel bint wa kifalme alichochea na kuingiza ibada za Baal na
kushawishi watyu kumuacha Mungu Kusudi la mungu kumuinua Eliya ilikuwa ili
aweze kuwaleta watu katika uamuzi wa kumuabudu yeye na kumkataa baal Roho
alimuongoza licha ya kuwa kulikuwa na hali za kukatishwa tamaa kwa muda.
Elisha aliomba
upako maradufu wa Roho mtakatifu yaani Roho yuleyule na nguvu zilezile 2Wafalme
2;9,utii wa Elisha na huduma yake kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ilisababisha
kuitwa Mtu mtakatifu wa Mungu 2Wafalme
4;9 kazi kubwa ya Roho Mtakatifu kupitia manabii katika wafalme na nyakati
ilikuwa ni kuleta uamsho mkubwa na ibada ya kweli ya Mungu
Roho Mtakatifu na maandiko ya manabii
Yoel 2;28-32
Alitabiriwa kuwa angemwagwa kwa wanadamu woote
au kwa woote wenye mwili Mwanzo 6;12,13 Kumbukumbu 5;26 na Ayubu 12;10 Petro
alionyesha wazi kutimia kwa andiko hilo siku ya Pentekoste matendo 2;16, ahadi
hii inavunja mipaka ya ukabila na utaifa
inaondoa tofauti za miaka umri au jinsia ”wana wenu na binti zenu” inavunja tamaduni
utumwa na ubwana na hivi ndivyo ilivyo
leo si myahudi tu au myunani si weupe au weusi watu wote waweza kupokea Roho
mtakatifu Roho mtakatifu pia huitwa mvua ya baadaye Yoel 2;23
Mika 3;8
Mika alijazwa kwa nguvu za
Roho mtakatifu na haki na ujasiri Mika 3;8 na hii ni moja ya maneno yaliyo wazi
katika agano la kale yalioonyesha nini maana ya mtu kujazwa Roho Mtakatifu
Roho Mtakatifu juu ya Nabii Isaya
Isaya aliishi kipindi kimoja sawa na Mika,
wakati huu watu waliishi katika dhambi na kustarehe wito wa Isaya ulikuwa ni
kuwaleta katika kustarehe na kumfurahia Roho Mtakatifu,Roho Mtakatifu alileta
Moto sio kwa ajili ya uovu tu bali pia kuutangaza wakati wa kuja kwa masihi Isaya
4;3-5 Mungu aliwatumia waashuru kuwafundisha Israel kwamba alichokisema Isaya
kilikuwa sahii
Roho Mtakatifu ni Roho wa Masihi
Kazi za Roho Mtakatifu kumhusu Masihi
zinaonekana ndani ya nabii Isaya,Yeye alitabiri kuwa Roho wa Mungu atakuwa juu
ya Masihi Isaya 11;1-5,Ishara ya kuzaliwa kwa Immanuel kupitia Bikira Isaya
7;14,majina yote aliyoyataja Isaya
kumhusu masihi yalikuwa dhahiri katika maisha ya masihi Isaya
9;6-7,Isaya alitabiri kuwa Roho mtakatifu angetenda kazi kwa viwango vya juu
ndani ya masihi Roho ya hekima namna ya kuitumia kweli katika maisha na kwa
usahii,Roho ya ufahamu ujuzi katika mema na mabaya na kupambanua, Roho ya
Ushauri yaani muongozo wa kimungu na hitimisho sahii,Roho ya nguvu yaani
ujasiri na nguvu ya kutenda mapenzi ya Mungu,Roho ya maarifa ujuzi binafsi wa
kujua mafunuo ya kiungu na kweli yake, Roho ya kumcha Mungu yaani kumuhofu
kumuheshimu na kujitiisha katika ubwana wake, Roho ya Bwana kwa kzi ya ukombozi
mamlaka kwa kusudi la kuishi na ya kuwa masihi hataweza kukosea katika utendaji
wake.
Isaya pia alimtabiri Masihi kama mtumishi
wa mungu atakayeifanya kazi yake ,hii ni kwa sababu taif la Israel kama
watumishi wake walishindwa kufanya kazi yake ingawaje wale wateule mabaki
wachache walifanya kwa uaminifu na walitumika kuandaa njia kwa ajili ya masihi
kama akina Simon Luka 2;28 Masihi mwenyewe alifanya kazi kwa ukamilifu
wote kwani kwa hakika amefanya kazi ya
wokovu na ukombozi wa mwanadamu
Isaya anamtaja Masihi kama Mpakwa mafuta
Isaya 61;1-11,kuwa masihi angeleta dini ya kweli si kwa wayahudi tu bali kwa
watu woote ulimwenguni,kama mtumishi wa Mungu Masihi angekuwa daraja kati ya
Mungu bna wanadamu na mwenye kuleta agano jipya
Masihi angepakwa mafuta ili kuhubiri habari njema kwa masikini na
kuwafungua wanaoteswa na kuwa masihi angekuja katika ukamilifu woote
Isaya anamuona Roho Mtakatifu kama Roho wa
Nguvu na maongozi Isaya 40;7-8 yeye ameweza kuifanya kazi hii huko nyuma sasa
na wakati ujao alikaa juu ya msihi alipokuja kwa mara ya kwanza Roho anauwezo
wa kuhukumu alimwezesha masihi kukabili kazi ya ukombozi kwa kustahimili mateso
Roho huyu angetuongoza sisi katika kazi ya kuiponya mioyo iliyovunjika na kutoa
ushindi dhidi ya dhambi na shetani,angeleta uponyaji, angetumwa kwetu na
angemwagwa kwetu kama maji ya kuondoa kiu au mafuriko katika inchi liyo kavu au
iliyokauka hizi ni kazi za Roho mtakatifu alizozitabiri Isaya
Roho Mtakatifu kama mkono wa Bwana wa nguvu katika
Ezekiel
Baadhi ya manabii walishindwa kumuelezea
vizuri Roho Mtakatifu na wengine walishindwa kabisa lakini hii haimaanishi kuwa hawakuwa chini ya
uvuvio wake Yeremia na Ezekiel
wanafanana katika kumuelezea Roho mtakatifu wao walitumia majina kama kidole au chanda cha
Mungu,Mkono wa Bwana ,Roho wa Bwana ambavyo vyote vilimaanisha nguvu za
utendaji wake
Ezekiel kwa mtazamo wake Roho Mtakatifu ni
wa Kujenga nasi wa machafuko Yeye kwanza anamuona Roho akiwa pamoja na kerubi aliowaona katika maono
Ezekiel 1;12,20,10;17 Ezekiel alipewa uelewa kuhusu utendaji wa Roho Mtakatifu
katika uzoefu wake,Kusudi la Roho wa Mungu kuwa juu ya Ezekiel ilkuwa ni
kumwezesha yeye awe na uwezo wa kuelewa jumbe atakazokuwa akisikia kwa mungu kupitia Roho hii
inatufundisha kuwa nabii anahitaji ujazo wa Roho mtakatifu kusudi aweze kupokea
ujumbe kutoka kwa mungu na anamuhitaji zaidi katika kujua namna ya kuupeleka
ujumbe huo.Aidha ezekiel ana muona Roho wa Mungu akihusika katika kuifanya upya
Israel Ezekiel 36-37 hii inauhusiano wa kuirejeza Israel kiroho na hata kimwili
pia,hagai na Zekaria pia waliziona kazi za mbele za Roho wa Mungu
Roho wa nguvu na uweza na Roho wa Neema
Roho wa Mungu kwa kweli ni Roho
asiyebadilika ndani ya kitabu cha Hagai
anaonekana kuwa wa milele ni Mungu na habadiliki na kuwa anaendelea kufanya
kazi na watu wake, Zekaria yeye anamuona kamaRoho wa nguvu na uweza na mwenye
kutoa neema yaani upendeleo usiokoma Zekaria 4;6. Zerubabel alikuwa gavana wa
Yuda na mjenzi wa hekalu wakati huu hakukuwa na vifaa wala uwezo wa kutosha
wala watu wakutosha kufanikisha kazi hiyo Hakukuwa na pesa, watu na vitu vya
ujenzi wala misaada lakini nabii aliwaambia si kwa nguvu wala si kwa uweza bali
kwa Roho wangu mimi asema Bwana, Hii inatukumbusha kuwa mungu siku zote hufanya
kazi Kwa Roho wake na kuwa kuwepo kwake ni zaidi ya fedha ,nguvu za watu na
vifaa yeye ni zaidi ya yote
Roho Mtakatifu ni Mvua zile za vuli zijazo Hosea 6;3.
Mvua
za vuli zijazo ilikuwa ni ujio wa Roho kuanzia wakati wa Pentekoste ,Hosea 6;3
ni unabii kuwa Mungu angewajilia watu wake kama mvua hii ni mvua inayokuja
kuandaa mavuno ya nafsi za wanadamu kupitia
kuhubiriwa kwa injili kupitia nguvu za Roho Mtakatifu kwa kawaida huko
Israel wana majira katika maeneo manne kama ilivyo hapa Tanzania au Tanga wao
wana Baridi-Kipupwe,Vuli-Mvua zijazo,kiangazi,Mvua kuu zile za zamani.
Uhusiano wa Roho Mtakatifu na Neno la Mungu
Kama tulivyoona tangu awali kuwa
kunauhusiano mkubwa wa Roho Mtakatifu na maandiko Agano la kale limetufundisha
kuwa kuna uhusiano wa karibu sana kati ya neno la mungu na Roho wa
Mungu,Manabii walitumika kama njia ya Roho wa mungu kutuletea neno lake,mafundisho
ilikuwa ni huduma muhimu ya manabii na walikuwa wakitimiza njia ya Roho
Mtakatifu kwani yeye ni mwalimu kila nafsi inayo mkaribia Roho wa mungu
huonekana kulipenda neno la Mungu.
Somo la tatu. ROHO MTAKATIFU
KATIKA MAISHA NA HUDUMA YA MASIHI
Roho Mtakatifu katika maisha ya Kristo
Utangulizi
Kati ya miaka 400 hivi ya ukimya mpaka
kuzaliwa kwa Kristo walikuiwepo masalia ya watu ambao walikuwa wakitembea au
walikuwa wamejazwa kwa Roho Mtakatifu,alipozaliwa Yesu Kristo waliongozwa na
Roho wa Mungu aliyekuwa juu yao kumtambua yeye kama aliyetumwa na Mungu kwa
ajili ya ukombozi wa ulimwengu katika eneo hili tutakuwa tunaangalia kazi ya
utendaji wa Roho mtakatifu katika kuzaliwa kwa Yesu na Kubatizwa kwake na
huduma yake na pia tutajadili kuhusu dhambi ya kumkufuru Roho mtakatifu
Roho Mtakatifu na matarajio ya kuzaliwa kwa Masihi
A; Kuhusu Masalia
1.
Luka 1-2 zinaonyesha kuwa bado kulikuwa na masalia au
watu waaminifu ambao walikuwa wakiendelea kuyashika mafundisho ya manabii.
2. Miongoni
mwao alikuweko Zekaria kuhani pamoja na mkewe Elizabeth wazazi wa Yohana
mbatizaji wao ni mfano wa wacha Mungu Masalia
3. Miongoni
mwa watu wa kawaida sio kuhani alikuwako Simeon na Anna Bint fanuel
wakiwakilisha wengi waliokuwa wakiutazamia ukombozi Luka 2;25 ukombozi huu pia
uliitwa majina kama Faraja,Luka 2;25
4.
Makundi yoote haya yalikuwa yakiutazamia wokovu na kuhusishwa
kwa unabii juu ya kuja kwa masihi hii ina maana ya kuwa Roho Mtakatifu alikuwa
akifanya kazi katika Israel ya kuandaa
kuja kwa masihi na huduma yake
B; Wajibu wa Yohana mbatizaji.
1.
Yohana mbatizaji alikuwa ni kiungo muhimu kwa watakatifu
wa agano la kale na agano jipya ingawaje alibaki kuwa mtu wa agano la kale na hakuingizwa
katika mahusiano tuliyo nayo ya agano jipya
2. Aliishi
kama mnadhiri kuonyesha kuwa ni mtu aliyejitoa moja kwa moja kwa Mungu maisha
yake yoote
3. Aliongozwa
na kufundishwa na kuandaliwa na Roho Mtakatifu katika maisha yake binafsi na ya
huduma alijazwa kwa Roho Mtakatifu na alijazwa tangu tumboni, aliandaliwa kama
atakayetangulia mbele za Bwana na
alikuja katika Roho na nguvu za Eliya alikuwa ni mrithi wa Eliya na manabii
wote na inasemekana yeye ni zaidi ya nabii Mathayo 11;9-11 Yesu alimtambua kama
Eliya ajaye Mathayo 17;10-13 na hii ilikuwa ni kutimizwa kwa unabii wa Malaki,
Malaki 4;5-6
4.
Ingawa Yohana mwenyewe alisema yeye siye Eliya Yohana
1;21 alichomaanisha hapa kuwa siye Eliya yule mwenyewe ingawaje alikuja katika
huduma ya Eliya Hivyo kile alichomaanisha Yesu kumhusu Yohana ni kuja katika
Roho Nguvu na huduma ya Eliya na kutimiza unabii ule wa Malaki
C; Kuzaliwa na Bikira Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu Luka
1;26-38.
1.
Ni Mathayo na Luka tu ndio wanaoelezea muujiza huu wa
kuzaliwa Kwa Yesu Kristo kupitia Bikira
2. Hii
inathibitika pale Malaika Gabriel alipomwambia Mariam kuwa utazaa mwana naye
ataitwa mwana wa aliye juu (Yaani mwana wa Mungu) na kuwa kwa yeye atakaa
katika kiti cha enzi cha Daudi baba yake
alijiuliza swali kuwa ingewezekanaje huku yeye hajui mume
3.
Malaika alimwambia kuwa Roho Mtakatifu atakujilia juu
yako kwa nguvu na nguvu zake aliyejuu zitakufunika kama kivuli kwa hivyo
kitakachozaliwa kitaitwa Mwana wa Mungu Luka 1;35 Mathayo 1;21 pia
inathibitisha kuwa malaika alimwambia Yusufu
kuwa mimba ya Mariam ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu
D: Fundisho kuhusu kufunikwa kama kivuli
a.
Historia inaonyesha kuwa uwepo wa Mungu kama wingu ulimfunika Musa katika mlima wa sinai na pia ulikuwa
ukionekana katika hema Kutoka 24;18,40;34-35
b.
Pia inakumbusha wakati wa uumbaji Roho alivyokuwa ametulia
juu ya uso wa maji Mwanzo 1;2 ingawa hapa haimaanishi kuwa Yesu alikuwa
anaumbwa pia haimaanishi kuwa Roho alifanya tendo la ndoa na Mariam Roho
alikuwa akifanya muujiza wa uwezekano wa Bikira kushika mimba bila mbegu ya
kibinadamu ya kiume kuhusika Hivyo Yesu kuzaliwa na bikira ni Muujiza kabisa.
E: Roho Mtakatifu ndani ya Masihi
Kwa ujumla tunaweza kusema
kuwa Roho Mtakatifu ameunganishwa na huduma na ujio wa Yesu Kristo, Hivyo kuna
uhusiano mkubwa sana kati ya maisha yake yoote na matukio yake yoote katika
kila sehemu ya huduma na maisha yake
·
Alihaidiwa
kwa Masihi
Agano la kale na manabii wote walitabiri
kuhusu ujio wa masihi na pia kuhusu Roho Mtakatifu kuwa juu ya masihi Isaya
11;1-2,42;1 na 61;1 na unabii huu wa Isaya ulitimizwa kwa maneno tunayoyasoma
katika Luka 4;18 na Yohana 7;37-39
·
Alihudumu
pamoja na Masihi
Baada
ya Yesu kupakwa mafuta na Roho wa Mungu kuwa juu yake aliongozwa katika huduma
na Roho akiwa na umri wa miaka kama 30 Isaya 61;1,Luka 4;18-19 Matendo 10;38
Roho alihusika katika huduma na utendaji mzima wa Kristo ikiwemo miujiza ambayo
yoote aliifanya kwa uwezo wa Roho Mathayo 12;28 Matendo 10;38
·
Roho
Mtakatifu wakati wa Mateso
Kama
jnisi alivyomuongoza kuelekea jangwani ili ajaribiwe Roho wa Mungu alimtia
Nguvu Yesu kukubali kukabiliana na
kukubali kujitoa katika maisha ya Mateso na aibu ya msalabani Waebrania
9;14
·
Roho
Mtakatifu wakati wa Kufufuka kwa Masihi
Yesu alifufuliwa kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu Waefeso 1;19-24,1Petro 3;18 Hata pale msalabani Yesu alitiwa nguvu
kuvumilia mateso yale lakini sio kuwa asisikie maumivu bali aweze kukubali
kuyatimiza mapenzi ya Mungu katika hali ya maumivu Warumi 1;4,8;11
·
Uhusiano
wa kupaa na kushuka kwa Roho Mtakatifu
Kristo
alipopaa ndipo aliporuhusu kushuka kwa Roho Mtakatifu kwa watu woote hivyo
ilikuwa ni lazima Yesu aende ili Roho aje na ujio wa Roho Mtakatifu ni
uthibitisho wazi wa kuwa Yesu alipaa mbinguni Yohana 1;32-33.
F: Fundisho la Roho na Moto
1)
Maoni
tofauti kuhusu Kubatizwa kwa Moto.
Yohana Mbatizaji
alitabiri kuwa Yesu angebatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto Mathayo 3;11, Luka
3;16 na ni Mathayo na Luka tu walioandika kuhusu swala hili
Wahubiri wa ki Holiness waluiohubiri katika karne ya 19;
walipanua ahadi hii kwa kufundisha kuwa ni swala linalohusiana na Moto wa
kiroho utakao teketeza dhambi kabisa hivyo waamini walitakiwa kuomba ubatizo wa
moto kwa ajili ya utakaso au ubatizo wa pendo liwakalo au ubatizo wa moto
(a)
Baadhi ya wanatheolojia hutofautisha kati ya Ubatizo wa
moto na ule wa Roho
(b)
Wengine huona ni ubatizo wa eneo fulani wa Roho Mtakatifu.
(c)
Wengine hawaoni kuwa kuna tofauti wanaamini kuwa maneno ya Yohana ilikuwa ni
kutangaza tu kama atawabatiza kwa moto
wa Roho Mtakatifu
(d)
Je wasomi wa leo wanasemaje?;-
§ Ni
ndimi za moto kama zile za siku ya Pentekoste ikimaanisha ni wivu mtakatifu
uliowahakikishia kuwa mitume wana moto kwa ajili ya Mungu
§ Kwakuwa
kuna maandiko mengine katika Mathayo 3;11,12 moto huu humaanisha moto wa hukumu
yaani huduma ya Roho Mtakatifu ya kuhukumu na kuzichoma dhambi
§ Dr.
Henry H. Ness alichangia kuwa kile ambacho moto hufanya katika hali ya asili
ndicho Roho Mtakatifu hukifanya katika
ulimwengu wa roho anaangaza,anasafisha na ana nguvu kila tukio la asili moto
ufanyacho ndicho Roho hukifanya
§ Elder
Cumming alisema ubatizo kwa moto ni aina za majaribu tunayopitia ambayo Mungu
huyaruhusu kwa watu wake.
§ Frank
M. Boyd alisema kuwa ubatizo wa Roho na
wa moto sio vitu viwili tofauti lakini ule wa Roho ni halisi na ule wa
moto ni ishara.
§ Dr.
Walbod yeye alisema maandiko yaliunganisha kile angefanya Yesu wakati wa kuanza
kwa kanisa na huduma yake wakati wa
utawala wa miaka 1000 kwamba kuanza kwa kanisa kulitokea kwa ujio wa Roho
Mtakatifu na kuanza kwa utawala wa miaka 1000 kutatanguliwa na umwagiko wa moto
wa hukumu juu ya mpinga kristo na majeshi yake wakati wa vita vya Harmaggedon
1Thesalonike 1;7-8 Yohana kama nabii aliviona kwa pamoja ubatizo wa Roho na wa
moto
§ Dr,
Stanley M. Horton yeye alisema Yohana alishindwa kutofautisha kati ya ubatizo wa Roho Mtakatifu na ule wa
Moto lakini Bwana Yesu alivibainisha wazi aliwaambia wanafunzi wake katika
Matendo 1;3-5 mtabatizwa katika Roho baada ya siku hizi chache hakutaja
moto,hii ilimaanisha ubatizo ule wa Roho uliotokea kuanzia siku ya Pentekoste
lakini kwa habari ya ule wa moto utakuwa mwishoni kama Paulo alivyoeleza katika
2Thesalonike 1;7-8 ambapo inazungumzia hukumu
§ Kwa
msingi huo basi kuna ukweli katika maelezo ya Dr Walbod na Dr.Horton kwamba
ubatizo wa Roho na wa Moto ni nyanja mbili tofauti,Yohana hakutofautisha kati
ya ujio wa Yesu mara ya kwanza na ujio wa Yesu mara ya pili,Ingawaje Yesu
mwenyewe alitofautisha kati ya ujio wa Roho mara ya kwanza na ule wa mara ya
pili wa hukumu na hivyo aliusema wazi hakuja kuleta moto wa hukumu katika ujio
wake wa kwanza Yohana 3;17
Kielelezo kinaonyesha Yohana aliona nyakati hizi mbili
kama wakati mmoja tu
Kusudi la Ubatizo wa moto
Ø
Kuonyesha hukumu ya Moto usiozimika
Ø Yesu
mwenyewe aliuzungumzia ubatizo wa Roho Mtakatifu kama Nguvu kwa ajili ya
utumishi na si sana kuhusu utakaso na
usafishaji Matendo 1;8
Ø Utakaso
unahusu kujiweka wakfu na kujitoa kwa Mungu na mapenzi yake kwa hivyo kupitia kujitoa na kuishi kwa
nidhamu na kuendelea kuwa na ushirika na Roho Mtakatifu na kulitumia neno la
Mungu.
Roho Mtakatifu akiwa na Umbo kama njiwa
Ni muhimu kujadili pia kuhusu kushuka
kwa Roho Mtakatifu wakati wa ubatizo wa Bwana Yesu na utambulisho wa Mungu Baba
kuwa huyu ni mwanangu Mpendwa nimependezwa naye na jinsi Kristo alivyojifanya
mwanadamu hili Tendo lilikuwa na maana
gani?
A; Kumtambulisha Mbatizaji
1.
Roho Mtakatifu kushuka akiwa na umbo kama la njiwa ilikuwa
ni Ishara kwa Yohana Mbatizaji kwamba Yesu atakuwa ndiye yule anayebatiza Kwa Roho Mtakatifu na
hii ilikuwa ni kutimia kwa unabii katika Isaya 11;2,42;1 na 61;1.
2.
Roho Mtakatifu alishuka wakati Yesu alipokuwa anaomba
alipokuwa amepanda kutoka majini hii inatufundisha kuwa Maombi na sifa humfanya
Roho wa Mungu kushuka juu ya waamini Luka 24;53,Matendo 1;14
3.
Ubatizo wa maji hapa ulitofautiana na ule wa kuja kwa
Roho Mtakatifu hii inamaanisha kuwa ubatizo wa maji hauna muungano wa moja kwa
moja na ubatizo wa Roho Mtakatifu
ingawaje huwa inatokea watu kujazwa Roho wakiwa wanabatizwa ubatizo wa
maji.
4.
Yohana Mbatizaji hakuhitaji ubatizo wa Roho mbele ya
Yesu alihitaji kubatizwa kwa maji kwani
alikuwa ametembea na Roho Mtakatifu na amekuwa akiongozwa naye tangu utoto
hivyo kupitia Roho wa Mungu pia alihubiri akiwataka watu watubu Tendo la Roho
kushuka akiwa na umbo kama njiwa huenda liliruhusiwa kwa Yohana mbatizaji pekee
na sauti ile kutoka Mbinguni ilikuwa ni tangazo la kuonyesha kuanza kwa huduma
ya Masihi
5.
Mungu alikuwa analiona Tendo hilo kuwa ni kutii kwake
Yesu Kristo kujitambulisha kama mwanadamu na pia kuwa tayari kwa huduma ya
ukombozi na kuukabili msalaba
B; Kujitambulisha na wanadamu
1.
Tendo la kubatizwa kwa maji kwa Yesu Kristo lilikuwa kama
la kujifananisha na wanadamu
2.
Shetani alipomjaribu ili ageuze mawe kuwa mkate Yesu
alikataa kwani angekubali tendo hilo lingekuwa kama amekataa kujifananisha nasi
§
Angefanya mawe kuwa mkate ingekuwa rahisi kwake kuendelea
kutumia asili yake ya kiungu kutoka katika asili ya kibinadamu ya kusikia njaa,
maumivu, n.k.na hivyo hata maumivu ya msalaba hayangeweza kuwa halisi.
§
Aliamua kabisa kuchukua nafasi yake kama mwanadamu ili
kwamba aweze kuteseka na njaa na hisia nyingine za kiibinadamu ili aweze
kuchukuliana nasi Waebrania 4;15.
§ Yesu
kama Mungu mwanadamu alihitaji Roho Mtakatifu amuongoze katika huduma kwa
wanadamu na kujitambulisha kama anayebatiza kwa Roho Mtakatifu.
C; Kuongozwa na Roho Mtakatifu Mathayo 4;1,Luka 4;1
1.
Kwa kukubali kuwa mwanadamu Yesu alijiweka katika utii
kwa uongozi wa Roho Mtakatifu na hivyo alijaa Roho Mtakatifu kuandaliwa kwa
ajili ya huduma na kumuwezesha kuifanya kazi ya Mungu.
2.
Hivyo aliongozwa kwanza Nyikani apate kujaribiwa na
Ibilisi, alikuwa amejaa Roho na hivyo
alifunga siku arobaini 40, hakutumia nguvu yake ya kiungu kushinda majaribu
alitumia kile ambacho sisi tunacho silaha zilezile Neno la Mungu, Upako wa Roho Mtakatifu, ni
silaha ambazo ziko na kuwa hata sisi tunaweza kuzitumia.
3.
Yesu alimshinda Shetani kwa ujumla katika maeneo yaleyale
ambayo Eva alijaribiwa katika Bustani ya Eden
|
Aina ya
Jaribu
|
|
Muhusika
|
Adamu na
Eva
|
Yesu
|
Mahali
pa jaribu
|
Bustani ya Edeni
|
Jangwani
|
Alikuwa
na nani ?
|
Walikuwa
na Mungu
|
Pekee
akiongozwa na Roho
|
Aina ya
jaribu
|
Tamaa ya mwili
|
Tamaa ya mwili
|
|
Tamaa ya
macho
|
Tamaa ya
macho
|
|
Kiburi cha uzima
|
Kiburi cha uzima
|
Matokeo
|
Anguko
|
Aliushinda
ulimwengu
|
|
|
|
4.
Ushindi wa Yesu unatuonyesha njia ya sisi kuwa na ushindi
dhidi ya ulimwengu na dhambi
5.
Yesu aliendelea kuongozwa na Roho Mtakatifu na alikwenda
Galilaya Luka 4;14
6.
Majaribu makuu ya watumishi wa Mungu ni pamoja na Zinaa, Kupenda
pesa, Kiburi na vyeo au umaarufu, kukatishwa tamaa, kujihurumia na kutokuamini
pamoja na ubinafsi.
D; Kuhudumu katika nguvu za Roho Mtakatifu
Karibu katika maeneo yote Yesu alihudumu
katika nguvu za Roho Mtakatifu katika eneo hili tutakuwa tukiangalia maeneo
mbalimbali ya maisha ya utumishi wa Yesu Kristo katika uweza wa Roho Mtakatifu.
1.
Roho
Mtakatifu na huduma ya Kufundisha na uponyaji.
§
Huduma yote ya Yesu Kristo ilimtegemea Roho Mtakatifu na
inaonyesha ukamilifu wa ushirikiano kati ya Baba mwana na Roho.
§
Nguvu hii ilijidhihirisha kwanza katika mafundisho yake
huko Galilaya watu walihisi mamlaka ya
kupita kawaida na lilikuwa na uwezo Luka
4;31
§
Yeye mwenyewe alitangaza wazi kuwa Roho wa Bwana alikuwa
juu yake hii ilikuwa ni kutimiza unabii katika Isaya 61;1-2,angalia Luka
4;18-21.
§
Injili ya Mathayo inaonyesha kuwa huduma ya uponyaji pia
ndani ya Yesu Kristo ilikuwa ni kutimiza unabii ya kuwa Roho wa Mungu alikuwa
juu ya mtumishi wake Yesu Kristo Mathayo 12;15
hii ni kutimiza unabii katika Isaya 42;4
2.
Kufurahi
katika Roho Mtakatifu Luka 10;20
§
Furaha iliyokuwa juu ya Yesu Kristo ilikuwa furaha ya
Roho Mtakatifu aliyekuwa naye siku zote, alifurahi katika Roho pia pale
alipoona kazi ya Mungu ndani ya wanafunzi wake 70 aliowatuma kuhubiri na
kuponya wagonjwa, walikuwa watu wa kawaida lakini walifanya miujiza mikubwa na jinsi Mungu alivyowapa nguvu ya kutoa pepo
§
Siri ya furaha aliyokuwa nayo Yesu ni matarajio yake ya
baadaye ya ushindi mkubwa utakaopatikana dhidi ya shetani kupitia kazi za Roho
Mtakatifu juu ya waamini
§ Hii
ina maana ya kuwa Roho Mtakatifu ni furaha yetu kuu na chanzo kikuu cha furaha
ya wanaoamini.
E; DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU
Chanzo kikubwa cha kuweko kwa mjadala
kuhusu dhambi ya kukumkufuru Roho Mtakatifu kilichangiwa na changamoto kuhusu
Nguvu inayofanya kazi ndani ya Yesu Kristo Mathayo12;21;32, Marko 3;22-30, Luka
11;15-20;12;30 tangu wakati huu kumekuweko na maoni mbalimbali kuhusu dhambi ya
kumkufuru Roho Mtakatifu
A; Maoni mbalimbali kuhusu dhambi ya kumkufuru Roho
Mtakatifu
·
Bieder Wolf – aliamini kuwa hii ni dhambi ya kudhalilisha
inayoweza kufanywa na wale ambao wamemjua na wamewahi kujazwa kwa Roho Mtakatifu
hawa ni wale ambao wamekionja kipawa cha mbinguni, karama neno na nguvu za
zamani zijazo kisha wakarudi nyuma kwa kukengeuka Waebrania 6;4-6,10;29.
·
Wanaoamini katika dhana hii wanaamini kuwa dhambi ya
kumkufuru Roho inaweza kufanywa na watu wale walio na ujuzi kuhusu Mungu kwani
hao ndio wanaoweza kukengeuka
·
Jerome na Chrysostom (mtafasiri wa Biblia iitwayo Vulgate
na muhubiri mashuhuri) waliamini kuwa watu wasiomjua Mungu pia au ambao
hawajaokolewa na wakafanya sawa na mafarisayo walivyofanya hapa wanaweza pia
kufanya dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ambayo haisameheki, wengine
wanaamini kuwa iliwezekana kuifanya dhambi hii pale tu Yesu alipokuwa duniani
basi, yaani kwamba njia ya kumkufuru Roho ilikuwa ni lazima umkabili Yesu tu na
kumkashifu kuwa miujiza anayoifanya ni kwa uwezo wa ibilisi
·
John Weslay Mwanzilishi wa Kanisa la Methodist alisema
njia pekee ya kumkufuru Roho Mtakatifu au dhambi isiyosameheka ni kuisingizia
miujiza ya Kristo kuwa ni ya shetani
·
John Broadus (Professor wa Southern Baptist seminary)
alikuwa na maoni haya kwamba dhambi ya kumkufuru Roho inaweza kufanywa na wale
wanaosema miujiza inayofanywa kwa nguvu za Roho Mtakatifu inafanywa na shetani
na aliamini pia kwa kuwa maswala ya miujiza yalikwishapita yaani ni ya wakati
wa Yesu na Mitume tu dhambi hiyo haiwezi kufanyika tena
·
Msomi wa Kijerumani aitwae Frant Delitzsch alikuwa na
maoni yafuatayo kuhusu Kumkufuru Roho
Mtakatifu haikuhusiana na neno la kumkufuru pekee au tendo la mtu kukufuru na
kupinga lakini linachukuliwa pamoja na mkao wa fikra wenye ugumu unaojifunua
ndani ya mtu ambao uanjenga dhambi isiyosameheka`
·
Maoni yangu Kama Mchungaji Innocent Kamote mwandishi
na mwalimu wa somo hili ni kuwa Roho Mtakatifu ni njia inayompelekea mtu
kuzaliwa mara ya pili na kuokolewa lakini si hivyo tu yeye humshawishi hata mtu
aliyeokoka kama amefanya dhambi afikie toba na katika majukumu ya kimungu ya Utatu
hii ni kazi ya Roho Mtakatifu hivyo basi tukio lolote lile liwe la kukashifu
miujiza yake ama vinginevyo lakini likafikia kwenye kiwango cha kumfanya aache
kazi ya kukufanya utubu hautakuwa na jinsi nyingine yoyote inayoweza kukufanya
upate neema ya kutubu na kwa jinsi hiyo umemkufuru Roho Mtakatifu au umefikia
katika mstari ambao anaujua yeye Roho kuwa haustahili tena kupata Msamaha na ni
vigumu kujua mtu aliyekataliwa ila Mungu tu hujua lakini dalili ni kuendelea
kuwa na ukaidi dhidi ya wito wa toba na kazi zote za Roho Mtakatifu kwani
hufanya miujiza kusudi tumwamini tuokolewe au tuimarishwe,au tuendelee katika
neema yake.
Tafasiri Nyingine kuhusu dhambi ya kumkufuru Roho
Mtakatifu
·
Kumkufuru Roho hujumuisha swala zima la kumkataa kwa kwa
hiyari kabisa
·
Wale ambao Yesu aliwaonya walikuwa katika hali ya
kujaribu kuwazuia watu wasimuamini Yesu na kuwa waachane nae
·
Hii ni jamii ya watu wanaotukuza matendo ya kishirikina
kuliko ya Mungu akili zao ziko katika muelekeo wa kuona kuwa kila kitu ni cha
kishetani tu
·
Ni hali ya kukataa kabisa kwa kukengeuka na kumkataa Yesu
na kanisa
·
Kama mtu anajisikia kushawishika, kuvutiwa kijhusisha, hamu,
kuchangamkia, kukubaliana na kufurahia
jambo lolote la kiroho basi kwake huyo kuna matumaini hajamkufuru Roho.
·
Hukumu kamili kama mtu amemkufuru Roho au la ukweli
unabaki kuwa Mungu pekee ndiye ajuaye jambo hilo na sio mwanadamu wa aina
yeyote
Onyo lililo kali
·
Sababu ya kutolewa kwa maonyo makali sana kuhusu
kumkufuru Roho Mtakatifu ni pamoja na
mzingira yafuatayo;-
Ø
Maadui wa Yesu Kristo walisema Yesu ana Pepo mchafu hawa
walikuwa ni mafarisayo na walisema kuwa Yesu anatoa pepo kwa Mkuu wa Pepo yaani
kwa nguvu za shetani
Ø
Kwa ujumla hawa walikuja Yerusalem wakiwa na lengo na
makusudi ya kumdhalilisha Yesu kwa hivyo kwa makusudi kabisa walikuwa
wakiupindisha ukweli na kudanganya kuhusu kile ambacho Yesu alichokuwa akifanya
kwa wivu
Ø
Yesu alionya kuwa kufuru dhidi yake au Baba yake
ingesamehewa lakini sivyo ilivyo kwa Roho Mtakatifu Yesu alikuwa akifundisha
kuhusu chanzo cha nguvu za utendaji wa
Mungu
§
Yesu alikuwa akionyesha kuwa ni kitu kisichoweza
kufikirika kuwa Shatani anawafukuza mashetani wenzake Shetani akimtoa shetani?
§
Yesu alikuwa akiweka bayana kwamba alikuwa akitoa pepo
kwa Roho Mtakatifu
§
Yesu kwa mujibu wa injili ya Luka
alikuwa akitumia chanda cha Mungu
kuwasilisha nguvu za Mungu ambazo kwa hizo alikuwa akitoa Pepo
§ Na
kuwa kwa nguvu hizo alikuwa akifunua kuwa ufalme wa Mungu umekwisha
kuwajilia na uponyaji ni moja ya manufaa
ya ufalme huo.
Maoni ya mwalimu wa somo;
§ Roho
Mtakatifu ni mjumbe wa Mungu kwa wanadamu
kuwashawishi kwa habari ya dhambi haki na hukumu ili waikubali kweli ya
Mungu Yohana 16;8-11 Hivyo mwanadamu anapoendelea kumpinga Roho mtakatifu
kuanzia na jumbe zake, muijiza yake, neno la Mungu na hata vitabu vya kiroho na
kwa hivyo anafunga mlango unaoweza kumuongoza yeye katika toba na hivyo kukosa
msamaa wa Mungu.
ROHO
MTAKATIFU NA HUDUMA YA MAFUNDISHO YA YESU KRISTO
Kwa jumla
katika eneo hili tunaangalia kile ambacho Yesu Kristo mwenyewe alikifundisha
kumhusu Roho Mtakatifu mengi ya mafundisho hayo yamo katika injili ya Yohana na
mengi yalielekezwa kwa wanafunzi wake
A; Mtoaji wa karama ya Roho.Luka 11;13 kwa nini tuombe
kwa akjili ya karama ya Roho Mtakatifu
§ Kiini kikuuu mafundisho ya Yesu
Ø
Yesu alitambua kazi za uvuvio wa Roho Mtakatifu katika
agano la kale Marko 12;36 Mathayo 13;Luka 20; 42 pamoja na kusudio zima la
utendaji wa Roho Mtakatifu kuhusiana na masihi
Ø
Alitambua kuwa Roho Mtakatifu ni zawadi ya Mungu na kuwa
ni ufunguo wa yote aliyo nayo Mungu kwa
ajili yetu Mathayo 7;7-11, Luka 11;9-13.
Ø
Kwamba Roho angekuwa pamoja nao akiwasaidia katika huduma
kwa kuwapaka mafuta hata katikati ya mateso Mathayo 10;16-20; Marko
13;9-11,Luka 12;11,12;12-15.
Ø
Aliwaamuru kuwabatiza waamini kwa jina la Baba na mwana
na Roho Mtakatifu Mathayo 28;19
Ø
Aliwaamuru kusubiri Yerusalem mpaka wamevikwa uwezo
utokao juu Luka 24;49 nguvu za Roho
zingekuwa juu yao kuwafanya mashahidi
Matendo 1;8.
Ø
Aliwapa mfano wa wanawali kumi Mathayo 25;3-4,8 ambao
huchukuliwa kuwa ni mfano wa kuwepo kwa utendaji wa Roho Mtakatifu katika moyo
wa mwamini
Ø
Yesu alifundisha kuwa waamini wanapaswa kumuomba Mungu
kwa imani kuhitaji Roho Mtakatifu alisema kama baba wa duniani wanaweza kuwapa
watoto wao vitu vyema ingawa wao ni waovu je Baba wa mbinguni hatatupa Roho
Mtakatifu sisi tumuombae Roho Mtakatifu ni zawadi nzuri hivyo hata kama
tumejazwa tunapaswa kuendelea kuomba ujazo wa Roho Mtakatifu
Ø Kwa
kufanya hivyo tunainyesha kiu na shauku tuliyonayo kumhusu Roho mfano mzuri ni
jinsi wale 120 walivyoomba hata wakapewa Roho Mtakatifu siku ya pentekoste
Chanzo cha
mto wa Jordani kilichopo huko kaisaria filipi mahali ambapo Petro alikiri kuwa
Yesu ni Mwana wa Mungu Mathayo16;13 na Kristo kuhaidi kuwa juu ya ukiri huo
atalijenga kanisa lake chanzo hiki kichokauka ni mfano tosha wa kuendelea
kutiririka kwa Roho wa Mungu kwa wote wamtakao katika Picha na maelezo kwa
hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote
WANAFUNZI WATUMWA KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU
§ Kuwa
pamoja nao katika huduma Mathayo 10;19-20
Yesu aliwaonya wanafunzi kuwa wasifikiri kuwa kila mtu atawapokea
tu na kuikubali injili hata pamoja na nguvu kubwa ambayo kwayo injili
inahubiriwa ni lazima watarajie vikwazo, kufungwa magerezani, kupigwa, kudhrauliwa
na kupelekwa mahakamani na mbele ya wafalme na maliwali lakini pamoja na hayo Yesu aliwaahidia
ushindi
Kama wakristo ni lazima tumtegemee Roho Mtakatifu hata
tuakapopelekwa mabarazani kwa ajili ya imani yetu Yeye atatupa hekima na maneno
ya kusema kufanya kila jambo kwa ushuhuda wake na si kwa ajili ya kujitetea
Kitabu cha matendo ya mitume kimejaa mifano inayoonyesha
mitume walivyoweza katika Matendo 3
Ø
Walitoa ushuhuda wa kuuawa kwake Yesu Kristo na kufufuka
wala hawakuwa wamejiandaa
Ø
Roho aliwapa lile lililokuwa muhimu kwao kulizungumza
maneno na hekima wapinzani na washitaki hawakuweza kupata cha kuwapinga
Ø
Bwana wakati mwingine aliwaokoa na wakati mwingine
aliwaacha waifie imani Bwana alikuwa pamoja nao katika huduma na mateso
waliyokutana nayo
§ Wanafunzi walitumwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu
Agizo kuu liliambatana na kujazwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu
Mathayo 28;18-20, Matendo 1;8
Kusudi la msingi la nguvu hizi ni kufundisha na kufanya
wanafunzi ambao wangependa kujifunza zaidi kumhusu Yesu na neno la Mungu
Ili ishara na miujiza ifuatane nao na injili hii ilipaswa
kuhubiriwa kwa kila kiumbe na hususani jamii za watu ulimwenguni zilizo
kataliwa Marko 16;20
Uamsho mkubwa wa kipentekoste unasambaa duniani pale watu
wa kawaida wanapokubali kuchukua jukumu la kuihubiri injili kwa wengine.
Mchanganuo kuhusu kuzaliwa kwa maji na kwa Roho Yohana 3;5
·
Kuzaliwa
kwa maji
Kuna
maana karibu nne zinazozungumzia kuhusu kuzaliwa kwa maji
1.
Ubatizo wa maji
a.
Wako baadhi ya wana theolojia wa kisakrament wanaoamini
kuwa ubatizo wa maji ni wa muhimu sana kwa wokovu na kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu
b.
Mafundisho ya kibiblia
Ubatizo wa maji ni ishara ya
ya ushuhuda wa nje wa maisha mapya ambayo tayari mtu ameshayapokea na hii ni
sawa na ubatizo wa Yohana haukuwa unaleta toba bali ulikuwa unathibitisha toba.
c.
Chanzo halisi cha maisha ya kiroho ni Roho Mtakatifu
2.
Maoni ya kuzaliwa kwa asili (maji ya wakati wa kuzaliwa).
a.
Wanaounga mkono maoni haya wanadai kuwa maji
yanawakilisha kule kuzaliwa kwa kwanza kwa kawaida au kwa asili natural birth
ambako kwa kawaida hutanguliwa na kumwagika kwa maji wakati wa uchungu
b.
Mtazamo sahii
Mawazo ya watu hawa yana
pingana na mtazamo wa injili ya Yohana kwa kuunganisha kuzaliwa kiroho na
kuzaliwa kwa asili maandiko kwa asili yake yanaonyesha kutokuunganisha kuzaliwa
kwa pili na kuzaliwa kwa asili kuzaliwa mara ya pili ni kazi kamili ya
Mungu kwa hivyo kuzaliwa kwa maji na kwa
Roho vyote vinahusisha kile kinachotoka kwa Mungu
3.
Maoni kuhusu kuzaliwa kwa Neno
a.
Katika maoni haya inachukuliwa kuwa kuzaliwa kwa maji ni
kuzaliwa kwa neno Efeso 5;26 hii inawezekana kwa sababu biblia inazungumzia uwezekano
wa kuzaliwa kwa neno 1Petro 1;23,25, Yoha 1;18,15;13 Biblia inaushahidi kuwa
maeneo mengi Roho ametumia neno kuwaleta watu katika wokovu.Rumi 10;8,14.
·
Kuzaliwa
kwa Roho
Hii
ni kazi ya Roho mtakatifu pekee yeye ndiye anayesababisha watu kuzaliwa mara ya
pili Yohana 6;63 yeye pia ni mtoa uzima 2 Koritho 3;6 .Kuzaliwa mara ya pili
ni kazi ya Roho mtakatifu katika kutufanya
upya ni yeye anayepanda mbegu isiyoharibika
katika mioyo ya wanadamu 1Petro 1;23 anapolitumia neno kama mbegu katika
moyo husababisha toba inayoleta wokovu
kwa imani na ni yeye anayewaandika watu kwa Kristo 1 Korotho 12;13.
·
Kuishi
kwa Roho Yohana 7;37-39,4;10,14.
Maji
ya uzima Yohana 4;10-14 Maji ya asili.
1.
Yesu alitoa maji ya uzima kwa mwanamke msamaria badala ya
maji ya asili kutoka katika kisima kirefu pale kijijini
2.
Maji hayo anayotoa Yesu mtu Yeyote anywae maji hayo
hataona kiu tena maji hayao ni wokovu Yesu hutoa na huweza kukupa uzima wa
milele
3.
Katika mistari hii maji huwakilisha wokovu na uzima wa
milele ambayo ndiyo pekee yanaweza kuleta pumziko na amani na usalama wa maisha
haya na maisha yajayo
Mito
ya maji ya uzima Yohana 37-39
1.
Sikukuu ya vibanda ilikuwa ni kwa ajili ya ukumbusho wa
miaka 40 ya masumbufu ya jangwani kwa wana wa Israel,ilikuwa ikiwakumbusha kuwa
wanapaswa kumtegemea Mungu kama baba zao
katika siku ambazo Mungu aliwalisha kwa manna kutoka mbinguni na
kuwapa maji kutoka katika mwamba
2.
Kwa mujibu wa tamaduni za siku zao inasemekana kuwa siku ya mwisho ya sikuu ya
majuma wakati wa sikukuu ya vibanda kuhani wa zamu huruhusu maji kutoka katika
kisima cha siloamu na kuyamwagia ndani ya ua wa
hekalu
3.
Miezi sita kabla ya kifo chake Yesu alitangaza kuwa kila
mwenye kiu na aje kwake anywe maji ya uzima ambayo kwayo hataona kiu tena na
kuwa ndani yake mito ya maji ya uzima itatiririka hii inafafanua kitu ziadi ya wokovu hapa
waamini wanakua chanzo cha mito ya maji ya uzima kusambaza kwa wengine hii
ilikuwa ni ahadi ya Roho Mtakatifu ambayo ilianza kutimia siku ya pentekoste.
Maji pia ni ishara ya nguvu, uamsho, utoshelevu na kuburudisho.
4.
Wanafunzi kabla ya siku ya pentekoste walikuwa na Roho Mtakatifu
lakini hakuwa ndani yao ”With them” not
”In them” lakini ahadi ya kufurika na kujaa ilitimia siku ya Pentekoste.
Kuabudu
katika Roho na kweli Yohana 4;23-24.
1.
Chini ya agano jipya Mungu haitaji watu wake kwenda
Yerusalem kwa kusudi la kuabudu kila mtu aweza kumfikia Mungu kupitia Kristo
ambaye ni kuhani mkuu lakini ni lazima wale wamuabuduo wawe katika Roho kwa
kuwa Mungu ni Roho
Kisima cha siloamu kama kinavyoonekana leo
katika Yerusalemu hapa ndipo Kuhani alipofungulia maji ili kutiririka katika ua
wa hekalu kwa kusudi la kuburudisha watu watalii wanaonekana kuyafurahia maji
ya kisima cha siloamu Picha na maelezo maktaba ya Rev.Kamote
Mfariji
mwingine
5.
Maana ya msingi ya
neno Mfariji inatumika kumuelezea Roho Mtakatifu
6.
Neno hili pia lilitumika kumuelezea msemaji kwa niaba
ya au mtafasiri
7.
Wasomi wengi wa kikatoliki hulitumia neno hili kumaanisha
Mwanasheria Advocate au lowyer
8.
Lakini maana ya asili ya neno hili mfariji pia humaanisha
mwanasheria mtaalamu au kitaaluma
9.
Kama mfariji Roho hutufundisha kweli yote na kusha wishi
wenye dhambi kutubu na kuifuata kweli, Neno Mfariji mwingine maana yake wa aina kama yake atakayefundisha
na kufanya kama Yesu alivyofanya
Kazi
za Roho Mtakatifu Yohana 16;8-11
1.
Kuushawishi ulimwengu kwa habari ya dhambi
¨
Dhambi inayowatenga watu na Mungu ni kutokuamini hii ni hali ya kumkataa Yesu kama Bwana na
mwokozi wa maisha Yetu, Tunapotambua yale tuliyomfanyia Yesu ndipo tunapoweza
kujua ubaya wa dhambi
¨
Roho anaposhawishi watu kwa habari ya dhambi huwashawishi
ili waweze kuamini na kuifikia toba
2.
Kuushawishi ulimwengu kwa habari ya haki
¨
Haki kamili ilidhihirishwa katika maisha ya Kristo, Roho
huwashawishi watu kutamani kuishi katika viwango ambavyo Yesu aliishi kama
mfano wa kuigwa kwa wanadamu na watu wanaomcha Mungu
3.
Kuushawishi ulimwengu kwa habari ya hukumu
¨ Ulimwengu
huu na mpangilio wake utahukumiwa Matendo 17;30-31 Roho Mtakatifu huwakumbusha
wanadamu kuwa wale woote wanaomfuata Shetani watahukumiwa na pia wale wasio
mwamini mwokozi
Akawapulizia
pumzi yake akawavuvia Yohana 20;21-23.
Moja
ya maswala yanayoleta utata wa kitheolojia ni pamoja na swala la Kristo
kuwapulizia pumzi na kuwavuvia akiwaambia pokeeni Roho Mtakatifu wanafunzi wake
je swala hili humaanisha nini?
Ø
Maoni
Mabalimbali
§
Humaanisha kuwa walipuliziwa pumzi ya nguvu na walipokea
nguvu
§
Pumzi ilikuwa ni ishara ya unabii wa kile kitakachotokea
katika siku ya Pentekoste kwa hivyo kwa wakati ule hawakupokea chochote
§
Wengine waliamini kuwa walipokea sehemu ya ubatizo wa Roho Mtakatifu
§
Walipokea maisha mapya ya ufufuo wa Yesu Kristo ambaye
wakati huu alikuwa amefufuka na hivyo walifanyika viumbe vipya Luka 24;49.
Ø
Utata wa andiko hili
§
Yohana 16;7 Ilionyesha kuwa Yesu angepaa kwanza kisha
ndipo Roho aje
§
Yohana 20;22 kupulizia pumzi kusingekuwa tena ni ishara
kama wangepokea Roho kwa wakati uleule
§
Yohana 16;16-22,20;22 inaonyesha kuwa ilikuwa lazima Yesu
aende kwa baba kabla ya kuja kwa Roho Mtakatifu
Kipimo
kamili kuhusu uvuvio wa Roho Mtakatifu
§
Kutimia kwa unabii wa Yoeli kunaonyesha kuwa Roho
alimwagwa na kuwa hakutolewa kwa kipimo.Hivyo tukio kamili la ujazo wa Roho
lilitimia siku ya Pentekoste
§
Mkazo wa Roho mtakatifu ni katika nguvu na katika Yohana
20;22 ni mamlaka
§
Walichopokea wanafunzi katika Yohana 20;22 kilitamkwa
katika agano jipya aidha ikumbukwe kuwa Yohana aliandika akiwa na athari za
kitabu cha mwanzo katika fahamu zake
§
Kwa kupokea Roho wanafunzi walikuwa wakithibitishwa kuwa
wao ni wanafunzi wa Yesu hivyo baada ya kuwavuvia wanafunzi walipokea Roho kama
anavyopiokea Mtu wakati wa kuzaliwa mara ya pili na sio ule ujazo wa Roho
Mtakatifu
SOMO LA NNE: ROHO MTAKATIFU NA KANISA.
Huduma ya Roho Mtakatifu katika Matendo ya Mitume.
Agizo la mwisho la Bwana Yesu
·
Kitabu cha matendo ya mitume ni kitabu cha matendo ya
Roho Mtakatifu kwani yoote yaliyotendeka yalitendeka kwa uwezo wa Roho Mtakatifu,
Hata hivyo maisha na mafundisho ya mitume yalimuhusu Yesu Kristo zaidi kuliko
Roho Mtakatifu wao ndio walikuwa mashuhuda wa mafundisho na mateso na ufufuo wa
Yesu Kristo Roho Mtakatifu mara moja aliwaongoza katika kazi ya kuhihubiri
injili na kustawisha kanisa hivyo mitume
walikuwa vyombo vya Roho wa Mungu .
·
Kuisubiri
ahadi ya Baba. Luka 24;49;Matendo ya mitume 1;4-8 Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni zawadi
iliyohaidiwa na Baba,Wanafunzi iliwapasa kuisuburi Yerusalem kwa sababu
walihitaji nguvu za Roho Mtakatifu ndipo waanze kuifanya kazi ya Mungu,walihitajika
kuwa pamoja kwa nia moja ili Roho ashuke na kutimiza kile Mungu alichokuwa
anataka ubatizo wa Roho Mtakatifu ulikuwa ni uzamisho wa uhusiano ambao
ulitakiwa kuendelea na kuwa mkubwa sana kwa ujumla ubatizo wa Roho Mtakatifu
unapewa majina mengi sana katika kitabu cha matendo mfano;-
a.
Wakajaa
b.
Kumwagiwa Roho
c.
Kupokea Roho
d.
Kushuka juu yao
e.
Kuja juu yao
·
Muda
wa kusubiri. Pale Yerusalemu wanafunzi walisubiri kwa Muda upatao
siku kumi huu ulikuwa ni wakati kati ya Kupaa kwa Yesu na siku ya Pentekoste
Matendo 1;14 wakati huu walikuwa wakikutana kwa pamoja na kufanya maombi
hekaluni pia walifanya uchaguzi wa Matiya kuchukua nafasi ya Yuda.
·
Kushuka
kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste.
A.
Maana
ya sikukuu ya Pentekoste
1.
Ilikuwa ni sikukuu ya kusheherekea Mavuno ya ngano
2.
Baada ya wayahudi kutawanyika na kuishi sehemu mbalimbali
ulimwenguni mavuno ya ngano ambayo hufanyika mwishoni mwa mwezi mei walianza
kuweka mkazo siku ya pentekoste kuwa sikukuu ya kusheherekea kushuka kwa sheria katika mlima wa Sinai
katika sherehe hizi wayahudi wapatao 180,000 walikuja kuabudu wengi walikuwa
wakitoka katika inchi mbalimbali ambazo
zilizungumza lugha nyingine na hivyo walioishi huko hizo zilikuwa ni lugha zao
sasa Pentekoste iliadhimishwa siku ya hamsini baada ya pasaka
3.
Katika Agano jipya siku ya pentekoste inachukuliwa kama
ishara ya kuanza kwa mavuno ya roho za watu kwa sababu ya kazi ya ukombozi
iliyofanywa na Yesu pale msalabani
B.
Upepo
na Ndimi za moto.Matendo 2;1-4.
1.
Ishara ya upepo
a.
”Uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi’ baadhi
huamini hii kuwa ni nguvu kwa ajili ya utumishi na baadhi huamini kuwa hii
Pumzi ya Roho Mtakatifu yenye kubadilisha au kuzaa upya ambayo huleta maisha
mapya.
b.
Ndimi zilizogawanyikana
kama ndimi za moto baadhi huamini kwamba hii ni ishara ya kukubaliwa kwa
kanisa kama mwili wa Kristo na pamoja na kukuibaliwa kwa kila muamini kama
hekalu la Roho Mtakatifu
c.
Ishara ya moto haikuweza kujitokeza tena katika maeneo
mengine popote watu walipojazwa Roho Mtakatifu
mfano Samaria au Kaisaria hii huenda ni kwa sababu
-Ishara ya
moto ilitokea mara moja tu hususani siku ya kuliweka wakfu Hema ya kukutania
katika agano la kale na huenda ilitokea mara moja tu siku ya pentekoste kama ishara ya kukubaliwa kwa kanisa au kila
muamini ambao ni hema mpya
C.
Kukua kwa kanisa kwa kasi Matendo 2;42.
1. Kushuka kwa Roho Mtakatifu
haukuwa tu mwanzo wa kanisa bali pia ulikuwa mwanzo wa kanisa kukua kwa kasi ya
ajabu sana Ghafla tunaona watu 3000
wakimwamini Mungu ghafla wakijifunza kutoka kwa mitume na kutii kila
walichokisema au kukiagiza haraka sana ushirika kati ya Mungu na wanadamu
ulikuwa na ushirika kati ya watu wao kwa wao walikuwa na umoja na walifurahi
kushirikiana na kuumega mkate, bila shaka ni kwa sababu ya Roho Mtakatifu
waliabudu pamoja na kuishi kivitendo katika yale waliyofundishwa huku Ishara na
miujiza ikiwa inatembea kila mahali miujiza hii iliwatia nguvu imani zao,
miujiza ilikuwa sehemu ya maisha yao
2. Kujazwa Tena . Hili ni jambo
ambalo wapentekoste wengi wanalipuuzia wanafikiri ujazo wa Roho mara moja tu
imetosha lakini wachunguzi wa Biblia wanasema unaweza kujazwa tena na tena hiki kinaonekana mwandishi Luka akikirudia na
kila kinapojitokeza kunakuwa na matukio mengine ya kutiwa nguvu katika
huduma Matendo 4;13,31,13;9-12 hivyo hii
inamaanisha watu walibatizwa kwa Roho siku baada ya Siku lakini walijazwa Roho
tena na tena Efeso 5;18 kila kujazwa tena kunapotokea kutiwa nguvu kwa upya
hutokea
3; Shughuli nyingine za Roho wa Mungu katika
Matendo ya Mitume
Alitatua matatizo katika kanisa Matendo 5;3-4
Alihusishwa na uchaguzi wa mashemasi Matendo 6;1-6
Alihusika katika utendaji wa miujiza Matendo 6;8,8;1
Aliwajaa watu kama Paulo Matendo 9;17-18 Paulo
aliwafundisha wengine wajae Roho Efeso
5;17-18 na pia aliwaambia wakoritho kuwa ananena kwa lugha kuliko wao
wote 1koritho 14;18
Watu wa mataifa walijazwa Roho pale Kaisaria Matedno 10;44-46 hili ni tukio lenye kuvutia
sana kwani halikuwa tofauti na siku ya Pentekoste mitume walipojawa na Roho hii
ilikuwa ishara ya kuwa Mungu amewakubali mataifa kama anavyo weza kuwakubali
wayahudi
Watu wa Efeso pia walijazwa kwa Roho Mtakatifu Matendo
19;1-7 hawa mwanzoni walikuwa hawajasikia habari za Roho Mtakatifu ingawa
walikuwa wanafunzi wa Yesu Baada ya Paulo kufika aliwaombea ujazo wa Roho na
wakampokea wakanena kwa Lugha
Mitume waliongozwa na Roho wa Mungu hata katika kazi zao
za injili au huduma ya kimisheni kwa mfano Matendo 13, kuwahitaji kwa huduma, na
pia alitoa mwelekeo wa wapi kwa kwenda mfano kuhusu kwenda Antiokia n.k.
Nguvu katika maisha
Msimzimishe Roho 1Thesalonike 5;19.
Kwa
ni nini Paulo aliwaambia wathesalonike wasimzimishe Roho? Roho Mtakatifu ni
kama moto, injili ilipohubiriwa Thesalonike ilikuja kwa nguvu na kwa uwezo wa
Roho Mtakatifu 1Thesalonike 1;5,
Wathesalonike walijazwa Roho Mtakatifu
na hivyo walikuwa na furaha licha ya kuweko kwa mateso namna
walivyohubiriwa na namna walivyopokea injili vina uhusiano mkubwa na Roho
mtakatifu wayahudi walimpinga Paulo wakidhani kuwa Kazi ya Roho Mtakatifu ndani
yake na wenzake ilikuwa ikiupindua ulimwengu Matendo 17;6.
Msimzimishe
Roho ni neno lenye uhusiano na kuzima moto au kuuua Waebrania 11;34,Daniel
3;25-28 Hii ilikuwa na maana kuwa Roho Mtakatifu anawezakuzimishwa hii ni
kutokana na mambo mabalimbali ambayo wakristo wanaweza kuyafanya hii
ikijumuisha maswala kadhaa kama ;-1Thesalonike 5;20
Kupinga unabii na kuuchukulia kama kitu kisicho na maana
Kupinga kwa ukali au kukataa au kukosoa kile
kinachofanywa na Roho
Kuzimisha au kuua kipawa chochote kinacho husiana na kazi
au karama za Roho Mtakatifu
Badala ya kukataa unabii kinachotakiwa ni kuupima kwa
maandiko na mbaya ukataliwe na mzuri utunzwe Torati 13;1-4,18;21-22 1koritho
14;29
Kumzimisha Roho pia kunaweza kukawa na maana ya
kutokuishi maisha ya usafi
Kuwa na tabia mbaya kinyume na mapenzi ya Mungu
Na upinzani dhidi ya Kazi za Mungu kwaajili ya kuhofia
nguvu za giza au wanadamu kuigiza
Roho Mtakatifu na Sheria Galatia 3;1-14
Roho
Mtakatifu anapatikana kwa imani, Baadhi ya wakristo mataifa wa Galatia
walijaribu kuishika sheria ya Musa na desturi wakidhani vinasaidia katika kuwa
sawa na Mungu waalimu wa kiyahudi waliwafundisha na kuwashurutisha
kutahiriwa,kujiepusha na vyakula fualani,na kushika sabato
Wagalatia walisahau kuwa walimpokea Roho
kwa imani katika Yesu Kristo kabla hawajadanganyika kuishika Sheria ya Musa hii
ilikuwa ni ushahidi tosha ya kuwa wokovu sio jitihada za mwanadamu na kuwa kazi
njema haziwezi kumfanya mwanadamu apokee wokovu Paulo aliona ni ujinga kwani
walikuwa wakiuacha uhuru wao katika Kristo na kujiingiza katika utumwa wa mwili,
Imani na utii kwa neno ndio funguo pekee ya kumshiriki Roho Mtakatifu.Tunaweza
kufurahia baraka za Ibrahimu sasa kwa njia ya imani kwa kuwa baraka kwa
Ibrahimu ilikuja kwa njia ya imani na sio matendo hivyo hata mataifa waishio
kwa imani ni wana wa Ibrahimu Sheria badala ya kuleta uzima na baraka ilileta hukumu na kifo kwa sababu hakuna
mwanadamu anaweza kuishika kwani hakuna mwanadamu aliye mkamilifu
Roho aliaye Abba (Baba).Wagalatia 4;16,Rumi 8;15.
Nyakati za Biblia mwana hangeweza kuwa
Mrithi na angefananishwa na mtumwa tu mpaka wakati wa umri wake mtimilifu
ulipokuwa umewadia ndipo angeweza kufanywa mwana na kuwa na haki na majukumu kama mwanafamilia
halali, mataifa kupitia imani ya Ibrahimu tumekuwa wana wa halali wa Mungu Yesu alikufa ili kutufanya kuwa wana wa
halali wa familia ya Mungu Efeso 2;19 ni kwa sababu hii Roho wa Mungu hulia
baba ndani yetu Abba ni neno la kiaramu lenye maana sawa na Baba Roho ndani
yetu hutufanya au hutupa haki ya kumuita Mungu kama baba yetu, hivyo kuanza
kuweka imani katika kutahiriwa na matendo mengine ya sheria kunamtoa mtu nje ya neema ya mungu Imani
huzaa matendo mazuri na sio matendo mazuri kuzaa imani au wokovu
Matendo ya mwili na Matunda ya Roho
1.
Ushindi
dhidi ya Matendo ya mwili
·
Paulo anatumia neno matendo ya mwili kumaanisha tabia ya
uovu inayokaa ndani yetu inayotuongoza katika dhambi na tamaa zake, tamaa hizi
pia huitwa utu wa kale ambayo kwa ujumla
hupingana na tabia ya utu mpya unaotokana na Roho Mtakatifu dawa yake ni kuishi
kwa Roho siku hadi siku
·
Matendo haya ya kale yanapojitokeza ndani yetu hii maana
yake tumeacha kuishi kwa Roho ushahidi unaoonyesha kuwa tunaishi kwa Roho au
tunaongozwa na Roho ni pale inapotokea matendo yetu ya mwili yanaonekana kuwa
yamesulibiwa kabisa msalabani na kuwa tunakusudia kuwa na matunda ya Roho
mtakatifu katika maisha yetu
·
Yanapodhihirika matendo ya mwili katika maisha yetu hii
maana yake ni kuwa tumeacha kuongozwa na Roho na kuwa mwili ndio kiongozi kwa
wakati huo hiii pia inadhihirisha jinsi tulivyodumaa kiroho na kuwa katika
hatari au mwelekeo wa Kwenda motoni
·
Makundi ya matendo ya mwili yamegawanyika katika maeneo
makuu manne
a.
Uasherati, Uchafu na ufisadi hii ni ile tabia ya kale ya
zinaa na kupenda kuangalia mambo ya uchiuchi n.k.
b.
Ibada ya sanamu na uchawi au ashirikina
c.
Uadui, ugomvi, wivu, hasira, Fitina, Faraka, uzushi, husuda,
ulafi.
d.
Ulevi.
·
Biblia inawahakikishia watu wanaoendelea kuishi kwa
matendo ya mwili kuwa hawataweza kuurithi kabisa uzima wa milele Wagalatia
5;21.
·
Mungu anaweza kumtumia hata muhubiri mwenye matendo ya
mwili lakini hii haimaanishi kuwa Mungu anataka mtu huyo aendelee kuwa hivyo
linapotokea jambo kama hili inawezekana kuwa Rehema za Mungu zinamvuta mtu huyo
kutubu na kuacha au Mungu ameliheshimu neno lake au Imani ya mtu yule
anayeombewa imefanya kazi na kumgusa
Mungu, Mungu aliendelea kumvumilia Samson kwa muda mrefu lakini mwishowe
kushindwa kwake kuishi katika Roho kulipelekea kumalizika kwake.
·
Mungu anaendelea kuwavumilia watumishi wengi wa mungu ambao
wamejaa matendo ya mwili hata leo wanaupendeleo, wana wivu, wana ugomvi waizi
wa sadaka au wana matumizi mabaya ya sadaka za waumini hawajali maisha ya
kiroho ya waumini wao, wanatengeneza hata skendo ili kuua wengine kihuduma tusipoangalia
tutakosa mbingu ambazo tumewahubiria wengine kwa muda wa kutosha.Kutumiwa na
Mungu sio kibali cha kukubaliwa .
Matunda ya Roho Wagalatia 5;22-23
1.
Matunda ya Roho Mtakatifu yamegawanyika katika makundi
makuu matatu
·
Katika uhusiano na Mungu tunapata Furaha, Amani na Upendo
·
Katika uhusiano na wengine tunapata Uvumilivu, Fadhili, Utu wema na
Uaminifu
·
Katika uhusiano wetu na Imani yetu tunapata Upole,kiasi,
·
Hata hivyo Biblia inatumia neno Tunda la Roho na sio
matunda ya Roho hii inamaanisha msisitizo wenye maana ya kuwa na msisi tizo
mmoja kwa mtu anayetembea katika Roho
yaani kama Roho anakuongoza inaaminika kuwa matunda yoote yatadhihirika
ndani yako kwani Roho atatawala maisha yako yoote na sio nusunusu neno tunda
kwa kiyunani ni kerpos ni umoja kama
wa chungwa ambalo ndani lina vijisehemu vidogovidogo lakini likikamuluiwa lote
hutoa juisi ya chungwa.
Uchambuzi kuhusu matunda ya Roho kwa ufupi.
Kwa
ujumla mtu anayetembea na Roho au mwenye kuongozwa na Roho na kuzaa matunda ya
Roho anatarajiwa kuwa mwenye kuchukua nafasi ya chini hatakuwa mtu wa kujisifu
Wagalatia 5;26,atahakikisha kuwa anawasaidia hata wale waliorudi nyuma Galatia
6;1-2,atakuwa na upendo akifanya kila kitu kutoka moyoni akiwatumikia wengine Galatia
5;13 hii inatokana na chanzo cha upendo kuungwa nasi kupitia Roho Mtakatifu 1Yohana 4;7-8 na atakuwa mwenye furaha na hii ni matokeo ya
upendo alionao Warumi 14;17 Furaha hii haitokani na mazingira halikadhalika
Amani ambayo ni matokeo ya kuishi vizuri na wenzetu, Uvumilivu uwezo wa
kusamehe na kutochukua hatua kwa haraka ili usikwaze au kumfanyia mwengine
yasiyofaa utuwema hii inahusiana na
ukomavu katika swala la ukarimu, Uaminifu kuwa mkweli na mtii na kutumia vizuri
kila tunachokuwa tumekabidhiwa kama mawakili wema upole Mathayo 11;29 hali ya
uvumilivu na kutokusukuma watu au kuwalazimisha na kiasi hali ya kuweza
kujizuia au kustahimili au kujistahimili ni kujizuia hata katika jambo ambalo
ungeweza kulifanya katika mazingira huria uliyo nayo bila kujali hatari yake.
Jinsi ya kuwa na matunda ya Roho
Kadiri
mkristo anavyoendelea kuwa mtii kwa Roho wa Mungu na neno lake ndivyo na
matunda ya Roho yanavyoweza kuendelea kuzaliwa ndani yake hii itajumuisha pia
swala zima la kuishi kwa kukataa mambo ya mwili na hivyo matunda yatakuwa ndani
yake, Endelea kumuhubiri Kristo tukiusubiri ukombozi kamili wa mwili huu
1Koritho 15;15-52
Huduma
katika Roho
Hekima ya mwanadamu na hekima itokanayo na Roho wa Mungu
Wakoritho walijisifia sana hekima ambayo
ilitokana na ujuzi wa kibinadamu Ginosko
na waliitukuza sana lakini kuna tofauti ya hekima ya kibinadamu na ile
itolewayo na Roho wa Mungu ni rahisi kuona wakati mwingine mambo yakikubalika
kabisa katika hali ya kibinadamu na fikira zake lakini yakawa kinyume na
mafundisho na mfano wa Yesu Kristo wayunani walishindwa kabisa kuona mantiki ya
kifo cha Yesu msalabani kwa sababu walitumia akili za kibinadamu na falsafa na
hoja za kawaida na hata hekima ya
kibinadamu na kwa sababu hiyo waliona ni ujinga wala haiingii akilini kukombolewa
kwa mwanadamu eti kwa mtu kufa juu ya msalaba haingii akilini hata kidogo.
Paulo anasema alikataa kutumia njia ya
kibinadamu katika kuihubiri injili Yeye alitumia nguvu za Roho Mtakatifu katika
kuipeleka injili. Kuijua siri ya nguvu za Mungu kungeweza kumfanya mwanadamu
kukaa katika imani wakoritho walihitaji nguvu za Mungu na Kristo aliyesulibiwa
kama hekima itokayo kwa Mungu 1 koritho 1;24.
Kufunuliwa kwa Roho.
Ni Roho wa Mungu pekee awezaye kufunua
siri ya kufa kwa Yesu msalabani, hata kama injili zote nne zimeelezea kwa
ufasaha sababu ya kufa kwa Yesu msalabani bado inamuhitaji Roho wa Mungu
kufanya kazi ya kumfanya mtu alielewe hilo. Ni kupitia Roho wa Mungu tunaweza
kujua mambo hata yaliyomo katika moyo wa Mungu 1 Koritho 2;10. Hili ni vigumu
kwa mwanadamu wa kawaida kujua nini kinaendelea katika moyo wa Mungu, Ni Roho
pekee awezaye kuyafanya hayo
Usiishi kama mtu wa Kawaida.
Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu 1
Koritho 3;16 Ninyi ni Hekalu la Roho wa Mungu hii inamaana ya kuwa kila muumini
ni patakatifu pa patakatifu pa Roho wa Mungu maana ninyi inatuhusu kanisa woote
hivyo miili yetu ni mali yake hii inamaana tunapaswa kutoa kipaumbele katika
kumuabudu na kumtumikia miili yetu ni lazima itumike kwa utukufu wake, Mungu
hapendezwi na tabia ya kuitumia miili yetu kwa ajili ya dhambi au iharibikiwe
kwa ajili ya dhambi 1 Koritho 6;14. kama alimfufua Kristo aweza kuifufua na
miili yetu itoke katika hali ya kuharibiwa na dhambi mwili wetu haujatenganishwa
na roho zetu hivyo tukifanya dhambi tunafanya juu ya miili yetu wenyewe 1
koritho 6;13-20 hivyo ni muhimu kwetu kuishi kama watu wa Rohoni.
Elimu na kiroho.
Wengine wanaamini kuwa hatihitaji Elimu
kama Roho wa Mungu akiwa ndani yetu lakini kwa kweli Elimu ni moja ya nyenzo
ambazo Roho Mtakatifu huzitumia kama tu
tutakuwa wanyenyekevu na kujidhabihu kwake, Haijalishi una elimu kiasi gani
bado tunamuhitaji Roho Mtakatifu sana kwa habari ya kufahamu mambo ya Rohoni
kwa mfano tunahitaji kunena kwa lugha wakati mwingine ili kujijenga kiroho
kutafuta kwetu elimu ni lazima kuendane na kumpa Mungu utukufu inamuhitaji Roho
wa Mungu kumfunua Kristo kwetu na kutupa neema na kuifanya halisi katika maisha
yetu
Roho
– Elimu = Uzushi
Elimu
– Roho = Ufarisayo au ukatoliki
Elimu
+ Roho – Unyenyekevu = Anguko la Lusifer/Kiburi.
Roho
+ Elimu + Unyenyekevu = Huduma kama ya Paulo mtume
Huduma
katika kanisa.
Swala la
kutoa unabii 1Koritho 13-14.
Kuna
tofauti kati ya kunena kwa lugha na kutoa unabii katika asili yake na matumizi
yake
a.
Kwa
ajili ya kulijenga Kanisa.
·
Kwa upendo kabisa washirika wanapaswa kuelekezwa namna ya
kuzitumia karama hizi ya kunena kwa lugha na karama ya unabii ndani ya kanisa.
·
Kusudi kuu ni kulijenga kanisa au kuwatia moyo waumini
ndani ya kanisa,kuwatia nguvu ya kiroho na kulijenga kanisa kiroho na kiidadi
·
Mtu anaponena kwa lugha anajijenga yeye Binafsi lakini
anapotoa unabii ni kwa kusudi la kulijenga kanisa hivyo kunena kwa lugha maana
yake ni kuzungumza na Mungu kwa roho ambapo mnenaji na Mungu pekee ndio wenye
kuelewa
·
Lakini Roho wa Mungu anapoleta ujumbe kwa unabii lengo ni
kulijenga kanisa kulitia moyo na kulifariji hivyo ni muhimu kwake watu woote
wakaelewa unabii kwa msingi huo unabii unahitajika zaidi katika kanisa kwa
sababu unalijenga kanisa
·
Kunena kwa Lugha bila kupata tafasiri kunakuwa hakuna
maana sana lakini kama mtu akinena kwa lugha kama njia ya kuleta ujumbe na
ukatafasiriwa basi utakuwa na maana kwani utafanya kazi ileile ya kulijenga
kanisa
b.
Kunena
kwa lugha kunahitaji Tafasiri.
·
Kama kunena kwa lugha + kutafasiri = unabii basi kunena
kwa lugha na unabii vyote vinahitajika katika kanisa kwa kulijenga kanisa
katika namna tofauti tofauti kwani kunena kwa lugha ni ishara ya kuingilia kati
kwa Mungu Roho mtakatifu
·
Kuna mambo ya msingi manne yanayo wakilishwa kama kunena
kwa lugha kutaambatana na kutafasiriwa
Ø
Ufunuo huu sio ufunuo wa kweli mpya bali ufunuo wa maana
ya kweli fulani ya kiroho au maandiko
Ø
Maarifa huu ni ufahamu wa kiroho kuhusiana na jambo
fulani
Ø
Unabii na mafundisho yaani ujumbe ambao Mungu ameukusudia
kwa kanisa na mafundisho ambayo Mungu ameyakusudia kwa kanisa
·
Hivyo kama kunena kwa lugha hakutakuwa na Tafasiri basi
hii ina maana muhusika anawasiliana na Mungu na kujijenga mwenyewe na
unapotafasiriwa basi unalijenga kanisa 1 Koritho 14;2 bila tafasiri hakuna
mawasiliano Mstari wa 13-15
·
Kunena kwa lugha kunahitaji tunda la kiasi kwani kunena
pekee kunaweza kusilete matunda yaani kufahamu hivyo unahitaji mlingano kati ya
kunena katika roho na kunena katika akili au ufahamu wa kawaida na kuimba
katika Roho na kuimba katika ufahamu wa kawaida 1Koritho 14;15
c.
Sababu
za kunena kwa Lugha
·
Ni kwa ajili ya mtu binafsi na kwaajili ya kujijenga
nafsi yako 1 Koritho 14;2-4 ni kutimia kwa unabii wa Isaya kumuhusu Yesu Isaya
28;11,1Koritho 14;21,Marko 16;17 Matendo 2;4.10;46;19;6,1Koritho 14;5,14-18,39.
·
Kunena kwa Lugha pia ni uthibitisho wa kuwa Yesu
amefufuka na ametukuzwa Yohana 16;7,Matedno 2;26.
·
Ni ishara ya ujazo wa Roho Mtakatifu 1 koritho 14;4 na
waamuzi 20
·
Ni ishara ya kuwa Roho Mtakatifu anatuombea Warumi 8;26 1
Koritho 14;4,Efeso 6;2 ni njia ya kufurahi kiroho 1Koritho 14;12,15, Isaya
28;12.
·
Ni Ishara ya kutimizwa kwa neno la Mungu linapokuwa
limehubiriwa Marko 16;1,20.1Koritho 14;22.
d.
Kunena
kwa Lugha Kama ishara.
·
Kunena kwa lugha pia ni Ishara kwa wasioamini watu
walioamini wote wanajua kuwa kunena kwa lugha au unabii ni ishara ya kuingilia
kati kwa Mungu kwa kuwa wote tumeungwa katika roho
·
Kunena kwa lugha bila ya tafasiri kwa wasioamini kunaweza
kuonekana kama kitu kisicho na maana na hii inaweza kuwapelekea kudhihaki kama
ilivyokuwa siku ya Pentekoste
·
Hivyo kunena kwa lugha kunakoambatana na tafasiri kwa
wasioamini kunaweza kuleta maana nzuri na ya kujenga kwao na hiki ndicho Paulo
alichokuwa anakikazia
e.
Sheria
za kunena kwa Lugha na Unabii.
·
Kulingana na melekezo katika Wakoritho 14;27-28 tunaweza
kujenga hoja za sheria za matumizi ya kunena kwa lugha pamoja na unabii kama
ifuatavyo
1.
Matumizi ya kunena kwa lugha
Ø
Lazima idadi idhibitiwe wanene wawili au watatu katika
kanisa
Ø
Lazima kuweko kupokezana na kutafasiri yaani kunena mmoja
mmoja na mwingine atafasiri
Ø
Kama hakuna wa kutafasiri basi mmnenaji asinene kwa nguvu
kubwa kama mwenye ujumbe lengo la jambo hili sio kumzimisha Roho bali kuweko
utaratibu badala ya machafuko au vurugu ”God is The God of oder ”
2.
Matumizi ya Unabii
Ø
Unapotolewa unabii ni lazima ukubali upimwe na wengine
Ø
Tukio la kuupima linahusiana na kuangalia kama uko sawa
na maandiko na kuangalia ni nini Mungu amekusudia tukifanye
Ø
Mungu anataka kuwatumia watu mbalimbali na vipawa
mbalimbali katika kanisa hivyo mtu anayehudumu katika Roho anapaswa kuwafikiri
wengine katika upendo
f.
Mungu
ni Mungu wa amani na sio machafuko.
·
Kama karama zitatenda kazi katika msingi wa upendo
kutakuweko amani na wala si machafuko
·
Mkristo aliyekomaa atakuwa tayari kukubali maelekezo
yoyote ya matumizi ya karama kutoka katika maandiko na atakubali tofauti
zilizoko kwa amani
·
Karama ni msaada wa kutusaidia kusaidia wengine kwa lengo
la kutukomaza katika kumuelekea Kristo, kuwa na karama sio dalili ya kukomaa
kiroho na hivyo bado tunahitaji kujinyenyekeza katika huduma ya kichungaji ili
tuweze kuwa salama, misingi ya fundisho la kweli haujengwi katika unabii pekee
bali na neno la Mungu hivyo ni muhimu kwetu kukubali maelekezo ya kichungaji.
SURA
YA TANO: ROHO MTAKATIFU NA HUDUMA ZAKE.
Kutakaswa na Roho Mtakatifu
Waebrania 12;14.
1) Maana ya Utakaso.
Utakaso
ni kazi ya Roho Mtakatifu kwa mtu aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kuwa mbali na
dhambi na kumuweka wakfu kwa ajili ya Mungu.
a.
Kuweka wakfu, Kutakasa, kutoa
kwa ajili ya, kutengwa kwa ajili ya.
i.
Vyote vina maana moja ni
kutenga na uovu au na yule muovu na kumuweka Kristo ndani ya maisha ya Mtu.
ii.
Neno watakatifu katika
maandiko lina maana ya waliotengwa 1 koritho 1;2,6;1 Philip 1;1.
iii.
Kazi ya utakaso hufanywa na
Baba, Mwana na Roho mtakatifu kwa ujumla wanashirikiana
iv.
Kazi kwa ujumla ni jukumu la
Roho mtakatifu katika maisha yetu yote
v.
Tunahitaji hata hivyo kufanya
sehemu yetu katika swala la utakaso kwa kukaa katika neno, kuendelea kuamini,
maisha ya maombi na kujitoa kunasaidia katika kukamilisha kazi ya utakaso
b.
Kutengwa mbali na dhambi kuna
maana tatu zifuatazo
i.
Kutengwa mara moja Instant
sanctification huku ni kutakaswa kutoka katika matendo ya dhambi kimaadili na
kuhesabiwa haki na kuzaliwa upya hili hufanyika mara tu mtu anapookolewa na
kutolewa katika giza kuletwa katika nuru 2Koritho 5;17
ii.
Kutengwa kwa ajili ya
huduma na kwa ajili ya Mungu Progressive
sanctification mtu anapotengwa kwa ajili ya huduma hilo pekee lina muweka wakfu
lakini anapaswa kuendelea katika kuishi maisha matakatifu aidha kadiri kila
muamini kwa jitihdada zake binafsi na ushirikiano wake anaoutoa kwa neno na
Roho wa Mungu hukamilika siku hadi siku hivyo huendelea kutakaswa huu ni utakaso
endelevu.
iii.
Kutengwa kamilifu Perfect sanctification
utakaso wa jinsi hii mtu anapokuwa
amefariki dunia huku akiendelea kumuanmini Mungu na kuishi katika Mungu mtu
hawezi kukamilika kabisa akiwa angalipo duniani hili tutalijadili baadae hapo
chini
2) Kwanini
Biblia imetoa amri ya kuwa wakamilifu?
Mathayo 5;48, 1Petro 1;15-16, Lawi 19;2,11;44.
Biblia imeamuru tuwe wakamilifu au watakatifu kama Baba yetu wa Mbinguni hii ni
amri je amri hii ina maana gani? Na Kristo ametuahidi basi ninyi mtakuwa
wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu haya yana maana
zifuatazo
1.
Kiwango cha kipimo cha maisha
tunayopaswa kuyaishi ni Mungu mwenyewe.
2.
Neno kuwa mkamilifu lina
maana ya kukomaa, kuwa kamili
3.
Hatuwezi kuchukua tamaduni za
kibinadamu,au vyuo vya kibinadamu na mafundisho yao kama kipimo cha kuwa
wakamilifu lazima tuangalie Mungu mwenyewe anataka nini. Mungu ni mkamilifu na
mwenye upendo.
4.
Mapenzi yake kwetu ni sisi
kuwa kama yeye alivyo 1Thesalonike 5;23 yeye anataka kutuona tukiwa mbali na
dhambi au huru kutoka dhambini na haitaji kutuona tukifanya dhambi kwa kusudi
au kwa kutokukusudia bali kusikia furaha ya watoto wake Yeye aweza kabisa
kutulinda na dhambi tukimruhusu afanye hivyo kwa hiyari yetu kwani tunapofanya
dhambi twafanya kwa hiyari yetu
3) Maono
mbalimbali kuhusu ukamilifu
·
Wako wanaoamini kuwa
mwanadamu hawezi kuwa kamili katika maisha haya
ingawaje tunapaswa kuendelea kutamani na kuishi kwa utakatifu
·
Wengine wanaamini kuwa
ukamilifu ni kuwa huru mbali na kutenda dhambi ya aina yoyote ile na kuwa na
upendo uliokamilika na kuwa chini ya neema nyingi inayotusaidia kukamilika huu
ni ukamilifu wa kuendelea kujitahidi Wafilipi 3;12-15. Huu ni ukamilifu usiokata
tamaa katika kuendelea kumwangalia Yesu kama lengo letu kumuelekea Mungu.
·
Wako wanaoamini kuwa utakaso
ni tendo endelevu 1 Yohana 1;7-10 hivyo tunapaswa kuendelea katika kuikulia
neema, kuendelea kutakaswa kwa damu ya Yesu na kuendelea kuishi maisha yanayohusiana
na ukristo mpaka kifo.
4) Namna
ya kujiendeleza katika Utakaso.
Ufahamu wa
Kiroho
Tunapaswa kujihakikishia kuwa tunakuwa na
maarifa ya kiroho na ujuzi kuhusu Mungu Mithali 2;2-5,Yohana 17;3.Kolosai
1;9-10.Efeso 1;17-18 tunapoendelea kumjua Mungu na kuwa na maarifa ya kiroho
tutaweza kugundua maisha yetu ya dhambi na mahitaji yetu sisi wenyewe Mwalimu
mkuu hapa ni Roho Mtakatifu ambaye atatumia neno la Mungu na uzoefu wa kutembea
nasi na kwa jinsi hiyo atatusaidia kujifunza kumhusu Mungu kiu ya Paulo ilikuwa
hii nasi lazima tutake kumjua sana Filipi 3;10
Kujitoa
katika maombi na kutafakari.
Mwanzo 21;21-26,1koritho 1;2; Roho Mtakatifu
ni msaada wetu mkuu tumtegemee yeye katiika maombi yetu atusaidie na maombi
yetu yaambatane na kumsifu yeye
Kuendelea
kuwa na imani.
2Thesalonike 5;1-3 waebrania 10;22 Habakuki
2;4 Mathayo 25;21-23.ni muhimu kukua katika imani kamwe tusikubali
kudumaa,tujifunze kuwa na ujasiri kwa Mungu tukiendela kumuamini kuwa anaweza
kufanya kile ambacho alikwisha kukifanya anaweza kukifanya naam na atakifanya,
Msamaha ni swaola linalopatikana kwaimani kama Mungu alikusamehe kabla
hujaokoka atashindwaje kukusamehe leo ukiwa tayari amesha kuokoa na
atashindwaje kuendelea kukusamehe pokea msamaha wa Mungu kwa imani na songa
mbele
Kuendelea
katika kuyatii mapenzi ya Mungu.
Yohana 6;38,mathayo 26;42 na Waebrania 5;8
Yesu alipokuwa duniani akiwa na mwili kama wa kwetu alichokifanya ni kuyatii
mapenzi ya baba yake wa Mbuinguni hivyo
mapenzi yetu lazima yawe kamili katika mapenzi ya baba yetu wa Mbinguni
Sulubisha
utu wa kale.
Hii maana yake inakupasa kuendelea
kuyakataa matendo ya mwili na ubinafsi na kuishi kwa roho yaani kukubali Mungu
ayafishe kabisa matendo ya mwili tamaa na matakwa ya mwili endelea kutamani kuzaa
matunda ya Roho na ukubali kukua na kukua na kukua kila wakati
Kubali
Kumtumikia Mungu
Tunapokubali kupakwa mafuta na roho wa
Mungu basi tukubali kutumiwa na yeye Matendo 10;38,Isaya 26;12,Filipi 2;3
Wakati mwingine mungu ataruhusu mateso ambayo yatatuweka karibu na yeye
tukubali kufundishwa na Mungu.
Tazamia
kurudi kwa Yesu
Warumi 5;2,15;13 1Petro 1;2-8,1Timotheo
4;7-8 ni muhimu kutazamia kurudi kwa Yesu haraka tumaini hili linapokuwa kubwa
ndani yetu husaidia kuishi maisha matakatifu kurudi kwa Bwana kunaweza
kukutokea wewe mwenyewe binafsi au kwa kanisa zima kwa jumla hivyo jiandae kwa
kujiweka tayari tukijua kuwa wakati wowote Yeyeyajae atakuja wala hatakawia
KUBATIZWA KATIKA ROHO
MTAKATIFU
Ubatizo
wa Roho Mtakatifu.
Kusudi
kubwa la ujazo wa Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya nguvu za utumishi lakini hata
hivyo kuna maoni mbalimbali ya wanatheolojia kuhusu ujazo wa Roho Mtakatifu
ambayo ni muhimu kwetu kama tutayatafakari
1. Nguvu kwa ajili ya utumishi.
a. Maoni ya wa Wesleyani (The Wesleyani
view)
·
Wao
wanaamini makusudi makuu ya ubatizo wa Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya utakaso
na kutuweka mbali na dhambi ili tuwe wakamilifu
·
Waalimu
wa maoni haya wanatokea katika jamii ya wa holiness ambao walikazia mafundisho
ya utakaso au ukamilifu
·
Waasisi
wa mafundisho haya ni kama John Wesley 1703-1791 na Charles Finney 1792-1875.
b. Maoni ya Kesdwick wa 1870
·
Aliamini
kuwa kusudi kuu la kujazwa Roho Mtakatifu ni Kwa ajili ya nguvu na sio
kusafishwa kutoka dhambini
·
Mwinjilisti
maarufu Dwight L. Moody, R.A.Torey, A.J. Godon na A.B.S. waanzilishi wa ukristo
huko Chicago walichangia na kuendeleza maoni hayo kwa kuchangia kuwa pia ujazo
unasaidia katika utakaso endelevu Progressive sanctification.
c. Kweli ya Neno la Mungu
·
Woote
waliojazwa kwa Roho Mtakatifu walikuwa tayari wamesafishwa au wamezaliwa mara ya pili na tayari walikuwa
ni waamini katika Kristo
·
Kusudi
la msingi la kujazwa kwa Roho Mtakatifu sio kutufanya kuwa watakatifu au
kutufanya tuwe na furaha bali kutupa
nguvu za kazi au za utumishi
·
Hivyo
ni wazi kuwa nguvu za Roho Mtakatifu kwa kanisa kwa nyakati hizi zote ni kwa
ajili ya kukamilisha mpango wa Mungu na kazi zake.
2.
Ishara ya ya nje ujazo wa Roho
Mtakatifu.
Ni muhimu kuelewa kuwa kuna tofauti
kati ya Ishara ya nje ya ujazo wa Roho Mtakatifu na karama ya kunena kwa Lugha
kama huduma kwa ajili ya kulijenga kanisa hapa pia kuna maoni mbalimbali kuhusu
swala hili.
1. Maoni ya R.A.Torrrey
-
Aliamini
kuwa nguvu ndio ushahidi pekee unaotakiwa kuonyesha kuwa mtu huyo amejazwa kwa
Roho mtakatifu
2. Maoni ya Donald Gee 1969 katika
kitabu chake cha Pentecost
-
Aliamini
kuwa njia pekee ya Mungu kuonyesha
ishara kuwa Roho ameshuka na kulijaza hekalu lake ilikuwa ni ishara iliyotokea kwa wakatu ule
kama ilivy kwa habari ya kunena kwa Lugha
kama ilivyotokea pale nyumbani kwa Kornelio
3. Maoni ya kibiblia
-
Mara
nyingi ni ishara ya kunena kwa lugha ambayo hutokea mara moja baada ya kujazwa
-
Pili
ni ishara ya kukua kiroho hata kufikia kuzaa matunda ya Roho hii ni ishara
endelevu kuwa anaendelea kuweko.
-
Biblia
inaonyesha hata hivyo kuwa si wakristo wote walinena kwa lugha 1Koritho 12;30
hii ilimaanisha kuwa si wakoritho woote walionena kwa lugha au kuna baadhi ya
wakoritho hawakuwahi kunena kwa lugha
hata hivyo katika lugha ya sili ya kigiriki yaani kiyunani maana halisi
ni kuwa sio woote waliendelea kunena kwa lugha na sio kuwa hawajawahi kunena
kabisa andiko hili pia linaweza kuwa na maana ya kuwa si wakoritho wote wana
karama ya kunena kwa Lugha kwa kusudi la kulijenga kanisa
-
Wengi
wanaopinga kuhusu kunena kwa lugha wanasema ni vigumu kupata uthibitisho kamili
kutoka katika kitabu cha Matendo ya mitume
3;
Jinsi ya kupokea ujazo wa Roho Mtakatifu.
A.
Kumtafuta
mbatizaji kuliko kubatizwa.
Ili kumsaidia mtu kupokea ujazo
wa Roho Mtakatifu ni muhimukutoa maelekezo au msisitizo wa kumtafuta mtoaji
zaidi ya zawadi, Abrahamu alimuamini Mungu na ahadi zake Mwanzo 15; 6, Yohana
mbatizaji alikazia watu kuzaa matunda kama matokea ya toba zao kabla hata
hajawabatiza na aliwaelekeza watu kumpokea yeye anayebatiza kabla hata ya
kupokea ubatizo ni lazima tuweke imani yetu kwa Yesu anayebatiza Yohana 14;
16,16;7
B.
Imani
ndio ufunguo.
Ili mtu apokee ujazo wa Roho
anapaswa kupokea kwa imani huu ndio ufunguo pekee wa kupokea Wagalatia 3;2,14
Matendo 15;8-9 Roho Mtakatifu anapatikana kwa imani mwamini ni lazima aendelee kuamini katika
ahadi za Mungu na kuamini kuwa mungu ataitimiza ahadi yake
C.
Lazima
ujue kuwa Roho Mtakatifu amekwisha kutumwa duniani rasmi kuanzia siku ya
Pentekoste kwa ajili ya woote watakaomwamini hivyo lazima utarajie
D.
Fundisha
kuhusu RohoMtakatifu mara nyingi kile tunachokihubiri ndicho kinachotokea toa
maelekezo yatakayopandisha imani kama Yesu alivyofanya Luka 24;48-49 matendo
1;40-5.
E.
Omba
na mara nyingi maombi kuhusu Roho Mtakatifu na ujazo wake yanapaswa kuombwa kwa
kupaza sauti Luka 11;13, aidha inaonekana kutamani kujaa Roho kunapaswa kuwa
kama kiu mtu anapokuwa na kiu na kuhitaji maji ya kunywa huomba au hunywa Yesu
amekwisha kutoa mwaliko wa kunywa kama una kiu Yohana 7;37
4;
Maswala ya Kupokea ujazo wa Roho
Mtakatifu kwa kuwekewa mikono.
·
Kuna
mijadala mingi siku hizi kuhusu swala la kuwekewa mkono kwa ajili ya kupokea
Roho Mtakatifu au hata miujiza Mingine ni muhimu basi kujadili swala hili kwa
kina ili kuondoa mashaka yaliyopo kuhusu uwekaji mikono.
·
Tendo
la uwekaji mikono hufanywa na watumishi wa Mungu ili kuruhusu kupitisha Baraka
anayoikusudia Mungu kwa mtu husika, hivyo muwekaji mikono ni bomba tu la
kupitisha maji lakini sio chanzo cha hayo maji chanzo ni Mungu hii maana yake
ni kuwa mtu anayehitaji ujazo wa Roho Mtakatifu bado anapaswa kuiweka imani
yake kwa Mungu na sio katika mikono ya watumishi Matendo 8; 14-17, 19; 1-7.
·
Tendo
la kuwekewa mikono pia lilitumika kama kichocheo kwa karama za Roho kujitokeza
ndani ya mtu ili apate kutimiza jukumu alilokusudiwa au huduma iliyokusudiwa
hii ilikuwa ni ishara ya kuwatakia neema za Mungu wale ambao Mungu amewaita
katika huduma Fulani ili awatumie 1Timotheo 4;14,Matendo 13;1-3,
·
Tendo
la uwekaji mikono halikuwa la hovyohovyo lilikuwa linachukuliwa kwa tahadhari
sana ili kujilinda na madhara 1Timotheo 5; 22. Hii ni kwa sababu tendo la
uwekaji mikono pia lilihusiana na kurithiana kitu kati ya mwekaji na mwekewa
kwa mfano Mwanzo 48;8-20 Yakobo alipoweka mikono juu ya Efraimu na Manase
aliwarithi kuwa wanawe nao walimrithi kuwa watoto wake badala ya wajukuu,Hivyo
tendo la uwekaji mikono pia hufanya kazi ya kurithishana kitu kati ya wawekewa
na muwekewa
·
Uwekaji
mikono pia ulizingatia aina ya mkono anayowekewa mtu kwa mfano kama mtu
aliwekewa mkono wa kuume au kulia hii ilimaanisha kuwa huyo atakuwa mkubwa na
aliyewekewa wa kushoto huyo atakuwa mdogo hata kama ana umri mkubwa
·
Baadhi
ya watu huofia swala la kuwekewa mikono kwa kuogopa kurithishwa mambo yasiyofaa
lakini baadhi hupinga kwa kusema Mungu si dhalimu kile ambacho mtu anakiomba
ndicho hupewa huwezi kuomba mkate ukapewa jiwe kwa baba yetu wa Mbinguni lakini
ushahidi wakibiblia umeonyesha watu kuponywa kuombewa neema au kujazwa Roho
kupitia uwekaji mikono jambo la kukumbuka ni kuwa bado imani ndio ufunguo mkuu
kwani muwekaji hana kitu cha ziada anachoweka yeye ila Mungu
·
Swala
zima la uwekaji mikono tunaweza kusema ni la kibiblia na msingi wake ni
kuwatakia neeema wale ambao aidha wanahitaji uponyaji au ujazo au kuwekwa wakfu
katika huduma na kadhalika hatuwezi kulipinga kinachotahadharishwa ni kuwa
muwekaji mikono hapaswi kuwa na kiburi na kujifikiri ni yeye awezaye kufanya
jambo hili kitu kama hiki Petro alimuonya Simeon mchawi ambaye alitaka
kulitumia tendo la uwekaji mikono kama njia ya kujipatia heshima Matendo
8;18-24.
5;
Matokeo ya ujazo wa Roho Mtakatifu.
1. Utajaa na kufurika Roho
maishani mwako
2. Utahisi uwepo wa Mungu kwa
ndani zaidi na kuufurahia
3. Utahisi kujitoa kwa Mungu kwa
hiyari zaidi bila kusukumwa
4. Utahisi kumpenda Yesu zaidi na
kuwapenda wengine
5. Utakuwa na ufahamu mzuri zaidi
wa neno la Mungu
6. Utajihisi huru zaidi na
utajisikia kumshuhudia Kristo kwa ujasiri
7. Utakuwa na nguvu za kumtumikia
Mungu na shauku ya kumtumikia itajengeka ndani yako
8. Utakuwa na furaha na amani na
mahusiano mazuri na wengine
6;
Kujazwa kwa Roho Mtakatifu sio mwisho wa
kutafuta ujazo huo.
1. Wapentekoste wengi hapa ndipo
walipokosea ni muhimu kufahamu kuwa kujazwa Roho Mtakatifu mara ya kwanza sio
ndo mwisho wa kutafuta ujazo zaidi wa Roho Mtakatifu
2. Kwa asili siku ya pentekoste
uilikuwa ni mwanzo tu wa kazi ya mavuno kwa ajili ya ufalme wa Mungu lakini
waliookolewa pia walipaswa kukaa katika ibada,mafundisho na kumtumikia Mungu na
maombi ujazo wa Roho utupelekee katika
kumtumikia Mungu ndipo sa tutaona utendaji wake vipawa na Karama za Roho
mtakatifu zikijitokeza na kufanya kazi kwa viwango vikubwa.
Karama za Roho Mtakatifu
Kuna
karama nyingi sana na za aina mbalimbali na watu huzigawanya katika makundi
mbalimbali kama wapendavyo karama hizi zote kwa ujumla zimegawanyika katika,
makundi makuu matatu ambayo kwa ujumla wake yanagusa utatu wa Mungu yaani
karama zitokazo kwa Mungu Baba na karama zitokazo kwa Mungu mwana na zile
zitokazo kwa Mungu Roho ambazo ni maarufu zaidi kama karama za Roho na ambazo
wengi huzifahamu 1Koritho 12; 4-6 hapo tunaona utatu woote ukihusika katika
utoaji wa Karama
1. Karama za kutenda kazi 1koritho
12;6 hizi hutoka kwa Baba
2. Karama za huduma 1koritho 12;5
hizi hutoka kwa Bwana yaani mwana au Yesu
3. Karama za Neema au karama za
Roho 1 Koritho 12;4 hizi hutoka kwa Roho.
Nyingi ya makundi ya karama hizo hapo juu
zimegusiwa katika kitabu cha Warumi, Waefeso na kitabu cha Wakoritho kwa
mantiki ya kimakundi niliyoiorodhesha hapo juu kwa mfano
·
Karama
za kutenda kazi au za masaidiano ziko katika Warumi 12;6-8 “Energemata”
·
Karama
za huduma au maongozi ziko katika Waefeso 4;11 “Diakonai”
·
Karama
za neema au za Roho ziko katika 1Koritho 12;7-11 “Charismata”
Ziko
njia mbalimbali za namna na jinsi watu au waalimu huzigawanya karama hizi
katika kusudi la kuzifundisha kwa wepesi kulingana na mwalimu anavyopendelea
kwa mfano wako ambao huzigawa hivi
1. Wako wanaozigawa sawa na mtiririko
wa kibiblia
2. Wako wanaozigawa kulingana na
jinsi zinavyofanana kwa asili
3. Wako wanaozigawa katika mfumo
wa kimatukio kwa mfano mitume,waalimu,na wainjilisti wanawaweka katika kundi la
Karama zinazosafiri wakati Mchungaji huwekwa katika kundi la karama inayotulia
sehemu moja au ya maongozi na kusaidia
4. Wengine huzugawa kulingana na
jinsi zinavyofanya kazi au za sirini na
za wazi za kawaida na za kupita kawaida vyovyote vile mtu atakavyozigawa jambo
la msingi ni namna tunavyoweza kuwasaidia wakristo kuzielewa na kutambua karama
walizo nazo na kuzitumia hilo ndilo jambo la msingi
Kwa
uchambuzi yakinifu niliouchagua ningependa kurudi katika makundi yale matatu ya
karama ili tufanye uchambuzi utakaokidhi matakwa ya jamii yetu haya ni makundi
yale makuu ya Karama za kutenda kazi, karama za huduma na karama za Roho na
ingawa msisistizo wetu ni katika karama za Roho tutazigusia zile nyingine japo
kwa mukhutasari
1. Karama za kutenda kazi 1koritho
12;6 hizi hutoka kwa Baba
Karama hizi ziko kwa wingi katika Warumi
12; 6-8 hizi ni karama za kutenda kazi ambazo pia huitwa karama za masaidiano
hizi ni maalumu kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la mahali pamoja na zinapaswa
kuwako kwa kila muamini ziko pia kwa ajili ya kusaidia utawala wa kichungaji
katika kanisa la mahali pamoja labda ndio maana huitwa pia karama za masaidiano
1Koritho 12; 28
2. Karama za huduma au maongozi katika
Waefeso 4;11-16
Hizi
ni karama zinazoshughulika na ustawishaji wa kanisa karama hizi Mungu huzitoa
kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa kuwajenga kiroho hata wafike kwenye
cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo au wafikie kukua kiroho au kukomaa
Kiroho.
3. Karama za Roho hizi ni karama za madhihirisho
ya Roho Mtakatifu ndani ya mtu aliyeokoka kumwezesha mtu huyo kufanya mambo
mbalimbali kwa kusudi la kulijenga kanisa, kulitia moyo na kudhihirisha kazi za
utendaji wa Mungu katika meneo mbalimbali ya maisha na kusababisha watu kuamini
au kutiwa moyo na kujengwa.
Uchambuzi wa karama za aina Mbalimbali.
Karama za Huduma
Ni
karama kwa mtu aliyeokoka kumwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kuhudumu katika
neema aliyopewa na Mungu na kutimiza jukumu lake kama Mtume, Nabii,
Mwinjilisti, Mchungaji au Mwalimu.
Mtume.
Neno mtume limetokana na neon la asili la
kiyunani “apostolic” ambapo tunapata neon apostle la kiingereza maana ya neno
hili ni mjumbe au aliyetumwa au yeye aliyetumwa amwakilishe mwingine au yeye
anayewakilisha mamlaka kutoka kwa yeye aliyemtuma. Yesu kristo ndiye mtume mkuu.Mitume
wale 12 walikuwa tofauti na mitume wengine ukiondoa Yuda wao watahukumu kabila kumi na mbili za wana
wa Israel wakati wa ufalme wa Mungu au utawala wa masihi, neon mitume pia
lilitumiwa kwa watu wengine walioitwa na Kristo baadaye katika huduma kama
Epefrodito, Barnaba, Paulo, Andronibas na Yunisi
Sifa za Mtume
·
Walitakiwa
kuwa mashahidi wa huduma mafundisho na ufufuo wa Yesu yaani walioamini kabla ya
siku ya Pentekoste Matendo 1;21-22
·
Paulo
Mtume anaingia katika sifa hii kwa sababu alifundishwa injili yake na Yesu
Kristo mwenyewe hivyo kwa namna moja au nyingine alimuona Yesu na hivyo alikuwa
na uhakika kuwa yu hai Wagalatia 1; 11-122;6-9.
·
Ofisi
ya Mtume ilipewa watu maalumu tu na
ilikuwa ni kwa kusudi maalumu hivyo si kila mtu angeweza kuwa Mtume na hizi ni
sababu za kibiblia
i.
Mitume
walikuwa 12 tu na walifundishwa na Yesu mwenyewe
ii. Walikuwa na kazi maalumu ya
kuweka msingi wa kanisa na kuandika neon la Mungu yaani agano jipya na
kustawisha viwango vya ukristo vilivyohitajika kwa mafundishao na maisha ya
ukristo.
iii. Majina yao yameandikwa katika
misingi ya mawe 12 ya Yerusalem mpya
iv. Watahukumu kabila 12 za wana wa
Israel wakati wa millennium au utawala wa Masihi wa miaka 1000.
v. Walimuona Yesu baada ya ufufuo
na walikuwa ni mashahidi waliojionea kwa macho kuwa Yesu amefufuka
Huduma ya kitume.
Wengi wanaojiita mitume leo sio mitume
isipokuwa huenda labda wana huduma ya kitume na huduma ya kitume inaweza
kuonekana katika maeneo makuu manne ambayo yanathibitisha kuwa hii ni huduma ya
kitume
1. Kunakuwa na Ishara na maajabu
katika huduma zao Matendo 2;43;512.
2.
Ni
waalimu wa neno la Mungu Matendo 2;42 na wenye mzigo wa huduma ya Neno la Mungu
na msingi wa mafundisho ya kweli katika ukristo Matendo 4;33,5;32.
3.
Wana
mzigo wa kustawisha makanisa au kanisa na likasambaa au kukua kwa haraka au
kuwa na mzigo wa kukamilisha agizo kuu katika nguvu za Roho Mtakatifu na
kulieneza katika kila sehemu ulimwenguni na kuweka watumishi kulisimamia.
4.
Wana
ujasiri wa ajabu wa kumtii Mungu kuliko wanadamu na kuwa tayari hata kupoteza
maisha yao kwa ajili ya injili wakiwa na uwezo mkubwa wa kujikana nafsi zao kwa
ajili ya injili ni wa kwanza katika kanisa 1Koritho 12;28.
5.
Watu
wootwe wanaojiita mitume leo ni lazima wahakikishe kuwa wanapimwa sawa na
vigezo vya neno la Mungu Mathayo 24; 24 Ufunuo 2; 2.
Nabii
Nabii
kwa kiyunani ni apothengomai yaani muonaji au msemaji kwa kiebrania Navi au
Nabi katika agano jipya kazi kubwa ya Manabii kama inavyoainishwa na agano
jipya ni wasemaji kwa niaba ya Mungu na wenye kutia moyo watu wa Mungu au
kanisa la Mungu
Manabii
agano la kale
-
Walizungumza
kwa niaba ya Mungu
-
Walifundishwa
na Mungu na kuelekezwa ni ni cha kusema
-
Wengi
wa Mnabii wa agano la kale walikuwa wasemaji kuliko waandishi
-
Kutabiri
ilikuwa ni sehemu ndogo sana ya huduma ya Manabii mengi waliyoyasema yalihusu wakati
uliokuweko na mambo yaliyokuweko
Manabii
agano jipya.
-
Yesu
ni nabii mkuu zaidi ya wote na alikuja kutimiza kile kilichosemwa na Manabii
katika agano la kale
-
Manabii
wengi wa agano jipya hawaleti neno jipya bali ufunuo Fulani kuhusu neno na
kweli Fulani zinazopaswa kufanyiwa kazi Yohana 13;2-3
-
Yuda
na Sila walikuwa Manabii Matendo 15;32 walitia moyo na kuwajenga waamini
waliwatia nguvu 1Koritho 14;3, wao walitia moyo na kuonya lakini
hawakumshambulia mtu moja kwa moja, Agabo alitumiwa kutabiri Matendo 11;28,21;11
-
Wale
ambao walitumiwa pia kwa karama ya unabii mara kwa mara waliitwa Manabii
1Koritho 14;29,32,37,Biblia pia imeonya kuweko kwa Manabii wa uongo hivyo ni
muhimu wakajharibiwa au kupimwa sawa na neno la Mungu 1Yohana 4;1 kazi kubwa ya
ujumbe wa nabii ni kujenga
Kazi
kubwa za nabii kama zinavyoonekana katika mchoro huo hapo juu, kutabiri ilikuwa
ni sehemu ndogo tu ya kazi za Manabii
Mwinjilisti
Jina linatokana na neno la kiyunani
Evangelists ambalo maana yake yeye anayetangaza habari njema kimsingi hawa ni
watu wenye karama ya kushuhudia watu wasioamini na kufanikiwa kuwaleta kwa Yesu
na kumuamini na kupokea wokovu Yesu alikuwa ni mwinjilisti mkuu sana wainjilisti kwa kawaida hueneza habari
njema mzigo wao mkuu ni kuwaona au
kuuuona ulimwengu ukimjia Mungu kwa kuokolewa lengo lake kuu ni kuwapata wenye
dhambi, timotheo inaonekana kuwa huduma yake ya msingi ilikuwanui kufundisha
ndipo Paulo Mtume alipomtia moyo kuhubiri injili pia 2Timotheo 4;2,5, 1Timotheo
1;18,4;14 Bila kujali kuwa wanatumia sauti kubwa au ndogo wanarukaruka au la
wainjilisti wamejaliwa ushawishi wa watu wengi kukubali injili inapohubiriwa na
wao
-
Mfano
mzuri wa mwinjilisti halisi katika Biblia ni Filipo alihubiri huko Samaria na
Samaria ikalikubali neon la Mungu na kumuamini Kristo 8;4,5,35 wengi waliamini
na kubatizwa Matendo 8;6,12
-
Miujiza
mingi mikubwa iliambatana na huduma ya uinjilisti pamoja na kufunguliwa kwa
watu waliokuwa na mapepo Matendo 8;6,7
-
Wainjlilisti
walihubiri watu wengi na wakati mwingine watu wachache au hata mtu mmoja filipo
aliongozwa kumuhubiri towashi wa Ethiopia Matendo 8;26 huduma ya uinjilisti
ilimfanya aende mji kwa mji Matendo 8;40
wanachotakiwa wainjlisti ni kuihubiri injili ya kweli Wagalatia 1;8-9
Mchungaji na
Mwalimu
Kuna
uhusiano wa karibu kati ya mwalimu na Mchungaji hii inaonekana katika Maandiko
kuunganishwa Efeso 4;11 ni nini maana ya Mchungaji?
Pastor
kiingereza kwa kiyunani linatumika neon poimane yaani kiongozi wa kanisa la
mahali pamoja kwa asili neon hilo lilitumika kama Poimaimo yaani Mchungaji wa
kondoo kazi ya Mchungaji ni kuwalinda au kuwalea kondoo wa Mungu Kristo yesu
alikuwa Mchungaji mwema Mchungaji anatarajiwa pia kuwa mwalimu huduma ya ualimu
ndiyo inayolifanya kanisa kukua zadi kuliko nyingine Mchungaji lazima awe
mwalimu pia watu wa Mungu wameletwa kwako ili uwaelekeze, kupoteza kondoo ni
dhambi Mchungaji anayeshindwa kuwaongoza kondoo na kuwafukuza ameshindwa kazi
ya kichungaji Mungu hatupi watu wakamilifu anatupa ili wakamilike kama
umeshindwa kuwasaidia wakamilike unataka nani awakamilishe? Galatia 6;1-6
Yakobo 5;19-20. Mchungaji kama mwalimu lazima akumbuke kuwa tumepewa Roho
Mtakatifu yeye ni mwalimu mkuu hivyo ni lazima tukubali kufundishika Appolo
alikuwa mwalimu mzuri lakini pia alikuwa akifundishika matendo 18;26 hakuna
mwalimu mzuri ambaye hajapata kuwa chini ya waalimu wengine hata Yesu alikaa
chini ya waalimu Luka 2;46. Jukumu kubwa zaidi la mwalimu ni kuwapa watu
maarifa na kuwafunulia neon la Mungu wapate kulifahamu kwa kusudi la
kuliiimarisha kanisa.
Uchambuzi wa karama za Roho.
Karama
za Roho Mtakatifu ziko nyingi sana kwa ujumla karama haziesabiki laki ni
tutachambua baadhi hususani zile ambazo zinzjulikana sana kwa sababu Paulo
aliziorodhesha katika 1koritho 12;4-8 na zaidi Orodha hii haimaanishi kuwa ndio
zimeisha lakini Paulo alikuwa anatoa mwanga tu kuhusu utendaji wa karama ili
tuzifahamu kwa urahisi tutazigawa katika makundi makuu matatu yafuatayo;-
Karama
za uweza au madhihirisho
-
Imani
au neno la mamlaka
-
Uponyaji
-
Miujiza
Karama
za mafunuo
-
Neno
la Hekima
-
Neno
la Maarifa
-
Kupambanua
roho
Karama
za Usemi
-
Aina
za Lugha
-
Tafasiri
za lugha
-
Unabii
Uchambuzi karama za uweza.
Imani au neno la
mamlaka.
Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka inayowekwa
na Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kuamini au kutamka neno katika Mungu na kusababisha
Muujiza mfano ni 1Koritho12;9,13;12,
Mathayo 21;21-22, Marko 9;23-24,11;22-24, Luka 17;6, Matendo 3;1-8,6;5-8, Yakobo 5;14-15.
Uponyaji
Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka inayowekwa
na Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kufanya maombezi
yanayosababisha kuukarabati mwili au kuurejesha katika hali yake ya kawaida
bila kutumia akili za kibinadamu mfano Mathayo 4;23-24,8;16,9;35,10;1,8 Marko
1;32-34 Yohana 6;2,14;12 matendo 4;30, 5;15-16.19;11-12 n.k
Miujiza
Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka inayowekwa
na Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kufanya maombezi
yanayosababisha miujiza kutokea ikiwemo kutoa pepo mfano ni Mathayo
4;23,8;16,10;1,8,13;54,Marko 1;32-33,3;15, 6;13,16;17,Luka
4;40-41,9;1,10;17,Yohana 7;3,10;25 Matendo 2;22,4;30,Galatia 3;5,n.k
Neno miujiza katika Lugha ya
kiyunani Greec linagawanywa katika makundi makuu manne
1. Semeion –
ambalo maana yake ni Ishara Luka
23;8, Matendo 4;16.
2. Teras –
ambalo maana yake ni Maajabu,Mambo ya kushangaza Matendo 6;8
3. Dunamis -
ambalo maana yake ni miujiza ya kupita
kawaida Matendo 19;11,Matendo 2;22
4. Paradoxon –
ambalo maana yake ni Mambo mageni au ya
ajabu Luka 5;26
Uchambuzi wa karama za
mafunuo.
Neno la hekima
Hii ni Karama kwa mtu aliyeokoka inayowekwa
na Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kulitumia neno la Mungu
au ujumbe wa hekima kwa ajili ya kutatua tatizo Fulani lenye utata mfano
matendo 6;3,1koritho 12;8 13;2,9,12 au Marko 12;13-17.
Neno la Maarifa.
Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka kumuwezesha
mtu huyo kwa Roho Mtakatifu kuwa na uwezo wa kufahamu jambo lililofichika
katikamaisha ya binadamu na kuleta ufumbizi katika mazingira ya kweli ya
kibiblia Matendo 10;47-48,13;2,15;7-11 Matendo 5;9-10 n.k
Kupambanua roho.
Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka kumuwezesha
mtu huyo kuwa na uwezo kupitia Roho Mtakatifu kutambua kuwa ni roho gani
inatenda kazi kati ya roho ya mwanadamu, ya Shetani na Roho wa Mungu ili
kuhakiki kama kinachotenda kazi ni cha kimungu? 1koritho 12;10,14;29 Matendo
2;4-11, Matendo 13;8-12; 16;16-18.
Uchambuzi wa karama za usemi.
Aina za lugha
Hii
ni karama kwa mtu aliyeokoka chini ya uweza wa Roho Mtakatifu kumwezesha mtu
huyo kuongea au kusikia Lugha mpya ya wanadamu au ya malaika ambayo hajawahi
kujifunza 1koritho 12;10,28,30,13;1Matendo 2;4-11
Tafasiri za Lugha.
Hii
ni karama kwa mtu aliyeokoka inayowekwa na Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo
kuwa na uwezo wa kufasiri lugha au kinachoongelewa ambacho watu na yeye
hawakijui bila kutumia akili 1Koritho 12;10,30,14;5,13,26-28 mfano Daniel
aliweza kusoma maneno mene mene …………
Unabii
Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka
kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kupokea na kutoa ujumbe kwa kanisa
kupitia Roho Mtakatifu kwa kusudi la kujenga au kutia moyo au kuonya bila
kutumia akili Luka 1;40-45,Luka 1;46-55.luka 1;67-79 Matendo 2;14 21;9,10-11
MUHKTASARI KUHUSU ROHO MTAKATIFU
Kwa
muhktasari tunaweza kusema kuwa Roho Mtakatifu ni Suluhisho la matatizo yoote katika
kanisa au kiboko cha matatizo yoote na hii ndio maana nyakati za kanisa la
kwanza alipewa kipaumbele kinachostahiki Luka 24;49 Matendo1;8 nyakati za
kanisa la kwanza swala la Roho Mtakatifu lilipewa kipaumbele kama swala la sala
ya toba Matendo 8;14 na 19;1-7 kama kuna upungufu wa aina yoyote leo katika
kanisa basi tunapaswa kurudi kwenye msingi na kujiuliza kwa ni nini wenzetu
walimpa kipaumbele hii ni kwa sababu walijua kuwa;-
Ni suluhisho kwa
tatizo la Kimaongozi
Kama kuna jambo lina shida kubwa hapa
duniani basi swala la maongozi linashida kubwa na ndio maana tunashuhudia leo
migogoro mikubwa ya kimaongozi dunia haitaweza kusahau viongozi waovu waliopata
kuweko kama Mao, Hittler Idd amin Nimrodi sadaamu na Osama n.k ambao
wameiongoza dunia au mataifa yao katika maumivu na kuuwa wengi suluhishi ni
kuwa na viongozi waliojaa Roho Mtakatifu “Spirit
Filled Leaders” hili Farao
aliliona Mwanzo 41;38, Daniel 5;5-12,Hesabu 11;10-17 Isaya 63;10-14. Makuhani
Manabii na wafalme katika Israel ilibidi wapakwe mafuta ili wapokee Roho ndipo
waongoze.
Ni suluhisho la
uadui
Roho Mtakatifu pia ana uwezo mkubwa wa
kuwadhibiti maadui na kuhakikisha usalama wetu hasa pale wanapotuandama na
kutusakama 2 Falme 6;8-12,1Samuel 19;18-24 hivyo mahali alipo Roho wa Mungu
pana usalama
Ni suluhisho la
uonevu
Nyakati za agano la kale wana waisrael
walipoonewa na maadui walio wazunguka Mungu aliwainulia waamuzi na kuwajaza kwa
Roho ili kukomesha uonevu Waamuzi 14;5,6,15;3,14-16. Watu wanapoonewa na
shetani msaada wa pekee utaupata kwa mtu mwenye Roho wa Mungu
Ni suluhisho la
upinzani wa kidini
Tunaishi katika wakati mgumu ambapo kuna
changamoto za aina nyingi zikiwemo za kidini uislamu unakua kwa kasi na huku
wanawashambulia wakristo kwa namna nyingi sana huko ulaya uislamu unakua kwa
kasi hakuna namna yoyote ile tunaweza kukabiliana na changamoto hizi isipokuwa
kwa Roho Mtakatifu Matendo 6;8-10,7;55 mitume walipokutana na upinzani wowote
wa kidini hawakuogopa kwani walikuwa wakijaa Roho Matendo 5;17;-29,4;5-14
Ni suluhisho
dhidi ya nguvu za giza uchawi.
Nyakati
hizi tulizo nazo ni nyakati ambazo pamoja na maendeleo yoote yaliyoko bado
uchawi unakua kwa kasi sana huko ujerumani watu wanakusanyika katika misitu
mmoja ili kujifunza uchawi pia ziko website ambazo zinafundisha uchawi katika
mitandao ya intrenet
Biblia inaamini kuwa uchawi upo na namna ya kukabiliana nao lazima ujae Roho Mtakatifu
kutoka 7;10-13,Daniel 5;7.Hesabu 23;7-8,22-23 matendo 8;4-21,13;6-12 tusipokuwa
makini tunaweza kuabudu na wachawi hata katika makanisa ya kiroho
Ni suluhisho
dhiidi ya mateso na uonevu wa ibilisi
Roho Mtakatifui anapokuwa juu ya mtu hushughulika pia na maonevu yawapatayo
watu Yesu alifanya kazi duniani kama mwanadamu akimtegemea Roho Mtakatifu watu
wa Mungu wanateseka huduma mahospitalini haziridhishi inahitajika kanisa liwe
na majibu ya matatizo na shida za watu Ni kwa Roho wa Mungu tu tunaweza kufanya
hivyo Luka 4;18-19,Matendo 10;38.
Ni suluhisho kwa
woga kukata tamaa na kukabiliana na changamoto za ulimwengu huu
Matendo
2;1 Petro aliyekuwa muoga sasa anaonekana kusimamia kwa ujasiri kwa sababu
amejazwa Roho,anatusaidia katika kuishi maisha matakatifu na kuwa mbali na
sheria ya dhambi na mauti warumi 8;2
Nisuluhisho la
hekima tunapokuwa katika hali ya kutokujua nini cha kufanya
Mara
nyingi katika ulimwengu huu tumekutana na changamoto nyingi kiasi cha kuchanganyikiwa
na hata kufikia hatua ya kutokujua nini cha kufanya tunamuhitaji roho
mtajkatifu katika kutusaidia kutatua matatizo 1 falme 3;16-27 matendo
15,Kufanya uamuzi 1falme 12;4-11 kuhimili migandamizo kama ya Ayubu Ayubu 1.
Hitimisho
Nina mshukuru Mungu aliyenisaidia kuandaa
mafundisho haya kuhusu Roho Mtakatifu ni imani yangu kuwa yatakuwa msaada
mkubwa kwa kanisa la Mungu Hapa nchini na nje ya nchi Yatendee kazi yaliyomo
humu na hii itatufanya sisi waalimu kufurahia Baraka za Mungu pale tunapoona
kile tunachokifundisha kikifanyiwa kazi na kuzaa matunda yanayo kusudiwa Mungu
na akubariki Endelea kuniombea kwa habari ya huduma hii ili niweze kuwa Baraka
kubwa zaidi kwako na kwa kanisa la Mungu Ubarikiwe sana Wako katika utumishi
Mchungaji Innocent Mkombozi Kamote
Maoni 1 :
Unavitabu ulivyochapisha Mason haya
Chapisha Maoni