Alhamisi, 3 Machi 2016

Mafundisho Kuhusu Roho Mtakatifu ! "Pneumatology"


Utangulizi:
     Mafundisho kuhusu Roho Mtakatifu yamekuwa hayapewi kipaumbele kinachostahili Katika makanisa mengi,wengi hawampi utukufu wowote na wakati mwingine imekuwa ngumu hata kumtaja tu, Ni kama vile Roho Mtakatifu hayuko au amesahaulika kabisa.


     Katika karne ya 18 kulikuwa na makundi makubwa ya watu waliopinga waziwazi kama Roho Mtakatifu ni halisi, ni nafisi au kama ni Mungu,Thomas Goodwin alithibitisha kuwa katika nyakati zao 1660 Roho hakupewa kipaumbele, na George Smeaton katika nyakati zao 1880 alisema mafundisho kuhusu Roho Mtakatifu yalizaraulika kabisa siku zote za maisha yao.

     Hata katika kizazi hiki cha karne ya 20 ambapo kuna uamsho mkubwa ulioenea pande zote Duniani bado kuna watu wanapuuzia utendaji na vipawa vya Roho Mtakatifu na wengine huona kama havina sehemu katika kanisa.

     Hata hivyo katika siku zetu kuna ufahamu mkubwa na halisi wa uelewa  wa uhalisi wa Roho Mtakatifu na utendaji wake, Roho anafanya kazi katika maisha ndani ya mioyo yetu anatenda kazi ndani ya wanaume na wanawake katika sehemu zote za ulimwengu Tuna poendelea kujifunza na kuangalia kwa upana kuhusu Roho Mtakatifu katika somo hili kutatupa nafasi ya kutoa kipaumbele  kwa kazi zake utendaji wake, asili yake na umuhimu wake  na itatuleta katika uwazi wa kuelewa namna tunavyoweza kushirikiana naye katika utendaji wa kazi ya Mungu ambayo bila yeye inakuwa ngumu.

    Neema anayotoa yeye katika utendaji wa kazi yake utatusaidia kutembea katika nguvu zake na kushangilia urahisi unaopatikana katika kazi ya ukombozi tukifanya kazi na Roho Mtakatifu, Lakini kama anapuuziwa tusishangae kujiona kuwa kwa haraka na kwa Muda mfupi tunabaki kuwa vikundi vya kihuni visivyo na mwelekeo na vyenye kujawa na kila aina ya majungu, yaliyojaa fitina na faraka zisizo na ufumbuzi kwa kumdharau Roho Mtakatifu. Mchungaji Innocent Kamote yuko pamoja nawe katika somo hili Muhimu ili tujikumbushe umuhimu wa Roho mtakatifu katika maisha yetu na Huduma kisha tuweze kumtafuta kwa bidii na kurudisha nguvu uwepo na utendaji wa Mungu katika siku zetu Mungu na akubariki

     Ni maombi yangu kuwa somo hili litakuwa Baraka kwako na kwa kanisa lako na huduma najua kadiri tutakavyojifunza kuhusu Roho Mtakatifu ndivyo tutakavyo ruhusu kiu na mtiririko wa Roho katika maisha yetu na huduma na hivyo tutajaa furaha kubwa kuona Mungu akifanya kazi pamoja nasi. Tunashuhudia kupoa kwa kasi sana kwa makanisa mengi ya kipentekoste leo kuliko wakati wa miaka ya themanini katika taifa letu tunaweka kuokoa kupotea kukubwa kwa kasi ya kipentekoste kama tu tutajiachia kwake atuhudumie katika somo hili na kutujaza  na kuturudisha katika viwangio vya nyakati za kanisa la kwanza.

Sura ya Kwanza;           ROHO MTAKATIFU NI NANI?

     Pneumatology - Ni somo linalohusu nafsi, Kazi, Karama, utendaji na huduma za Roho Mtakatifu Kama inavyofundishwa katika Agano la kale na Agano Jipya, Mkazo ukiwa katika kubatizwa na kujaa nguvu za Roho Mtakatifu na kutembea nazo.
     Neno Pneomatology -  Ni muunganiko wa maneno mawili ya kiyunani Pneuma-ambalo maana yake ni Roho, au pumzi au upepo na neno (Logos) ology-ambalo maana yake ni Elimu kuhusu kwa hivyo neno Pneumatology ni Elimu kuhusu Roho mtakatifu.Kwa kiebrania  ni Ruah hivyo Pneumatology pia inaweza kuwa Ruachology.
     Kwa nini Tunasoma Pneumatology.
Ziko sababu nyingi sana zinazotufanya tujifunze kuhusu Roho Mtakatifu zifuatazo ni baadhi tu ya sababu hizo.
  • Kwa sababu Biblia inazungumza au inafundisha kuhusu Roho Mtakatifu.
  • Maandiko yanamfunua kuwa ni nafsi, ni Mungu na anaweza kutambulika ni Halisi na anaeleweka
  • Biblia inaeleza kuwa ndiye aliyevuvia watu kuandika Neno la Mungu
  • Kazi zake zinaonekana katika Agano la kale na katika agano jipya.
  • Biblia inaonyesha kuwa ana uhusiano na kuzaliwa maisha na huduma ya Kristo (Masihi)
  • Inasaidia katika kutetea imani kuhusu ujazo wqa Roho Mtakatifu na utendaji wake na kuwa ni halisi hata katika siku zetu leo
  • Inatusaidia kufahamu kuhusu utendaji, vipawa na Karama mbalimbali na umuhimu wa matunda ya Roho mtakatifu.
  • Inatusaidia kujifunza, kutumia kuhubiri na kufundisha kuhusu Roho Mtakatifu kwa maisha yetu na ya wengine katika mwili wa Kristo yaani kanisa.
     Umuhimu wa Roho mtakatifu.
Roho Mtakatifu ana umuhimu gani na kwa nini tujifunze kuhusu Roho Mtakatifu? Tukifahamu uhalisi utendaji uweza na nguvu zake na jinsi anavyohusika katika kazi nzima ya ukombozi wa mwanadamu na umuhimu wake kwetu kamwe hatuwezi kuacha kujifunza au kutaka kufahamu Kuhusu Roho Mtakatifu.
1.       Roho mtakatifu ana sifa zote zinazoihusu nafsi
§  Ana akili na ufahamu
§  Ana maamuzi
§  Ana maarifa.
§  Ana upendo na hisia
2.       Roho Mtakatifu hufanya kazi zote zinazoweza kufanywa na nafsi.
§  Anakaa ndani ya Mwamini
§  Anafundisha na anakumbusha
§  Anashuhudia
§  Anashawishi kwa habari ya dhambi (kuonyesha jinsi dhambi isivyofaa)
§  Anaongoza katika kweli,anasikia
§  Anazungumza alizungumza na filipo
§  Anaita watu katika huduma
§  Anatuma watumishi katika huduma
§  Anakataza baashi ya matendo
§  Anatuombea
§  Anaamuru
3.       Roho Mtakatifu anaweza kufanyiwa kile ambacho nafsi yoyote inaweza kufanyiwa
§  Anaweza  kudanganywa
§  Kujaribiwa
§  Kuhuzunishwa
§  Kuzimishwa
§  Kukufuriwa
§  Kumuitia, kuumizwa n.k.
Kama basi Roho Mtakatifu Ingekuwa ni nguvu tu kama nguvu ya umeme isingeweza kuhuzunishwa na kufanyiwa mabo kama hayo tuliyoyaona hapo juu
    Aidha angekuwa si nafsi katika maandiko asingeandikwa kwa kutumia neno linalo husisha nafsi mfano katika Yohana 16;7 “…Huyo Msaidizi hatakuja..”,mst 13 “…Lakini Yeye atakapokuja..”mst 14;”Yeye atanitukuza” “Atatwaa” namna anavyotajwa Roho mtakatifu hapo kwakweli haimaanishi kuwa Yeye ni nguvu bali ni Nafsi Person. Na sio kitu Thing
4.       Roho Mtakatifu ni halisi katika Biblia
§  Nyakati za Biblia watu walifahamu wazi kabisa pale roho mtakatifu alipotenda kazi
§  Ilikuwa ni hakika na halisi kabisa na hawakuwa na haja ya kuhisi
§  Woote katika Agano la kale na jipya walifahamu pale Roho mtakatifu alipofanya kazi na walijua kuwa ni
Ø  Halisi
Ø  Inayoelezeka
Ø  Na yenye matokeo maalumu.
  • Ni wazi kuwa Mika kwa uweza wa Roho mtakatifu alihubiri kinyume na dhambi (Mika 3;8)
o   Amosi kwa msukumo wa ndani aliwasilisha maono na kutangaza hukumu ya mungu (Amosi 3;8)
o   Kunena kwa Lugha kulivyo leo na kulivyokua wakati wa Agano jipya  sawa na Matendo 2;4 ni halisi kama ilivyo leo
o   Roho mtakatifu alihitajika sana wakati ule na anahitajika  sana leo,dini yoyote ile haitakuwa na maana kama haina Roho mtakatifu kama tunataka kujua kuwa Roho mtakatifu anapewa kipaumbele gani angalia ni vitabu vingapi vimeandikwa kuhusu Roho mtakatifu leo,Ni masaa mangapi yamechukuliwa na watu katika kuomba kuhusu Roho mtakatifu,ni jumbe ngapi zinazohubiriwa kuhusu roho mtakatifu ni wangapi wamechukua muda kusoma ili wafahamu vizuri kuhusu Roho mtakatifu unapofanya tathimini hii utapata picha kuwa anapewa kipaumbele kiasi gani ? hebu jumlisha jumbe za utoaji na za Roho mtakatifu zipi ni Nyingi makanisani Unapaswa kufikiri mara mbili!
5.       Roho mtakatifu ana sifa za Mungu.
 Wakati mwingine moja kwa moja au pasipo moja kwa moja sifa zinazomuhusu Mungu zimepelekwa moja kwa moja Kwa roho Mtakatifu na hizi ni sifa zinazomuhusu Mungu peke yake mfano;-
  1. Ni mwenye nguvu zote- Omnipotence Zaburi 104;30 Zekaria 4;6.
  2. Anajua yoote- Omniscience Isaya 40;13;1Koritho 2;10-11.
  3. Yuko mahali kote-Omnipresence Zaburi 139;1-8,Yohana 14;17.
  4. Ni wa milele  Eternality –hana mwanzo wala mwisho Waebrania 9;14
6.       Anafanya kazi ambazo hufanywa na Mungu peke yake
Roho Mtakatifu anahusika katika kazi ambazo kwa kawaida ni kazi za Mungu pekee hii ikijumuisha na sifa alizo nazo haziwezi kuhusu nafsi za kawaida isipokuwa Mungu tu Kwa mfano kazi zifuatazo
  • Amehusika katika kazi ya Uumbaji hivyo ni Muumba Mwanzo 1;2. Ayubu 33;4.
  • Anafufua wafu alihusika katika kumfufua Kristo Warumi 8;11
  • Anabadilisha maisha ya watu  kwa kuwazaa mara ya pili Yohana 3;5-6.
  • Anashawishi watu kwa habari ya haki dhambi na hukumu Yohana 16;8.
  • Anahusika katika swala la kutoa pepo ndiye anayetoa pepo Mathayo 12;28.
  • Sifa yake Mtakatifu ni sifa ya Mungu tu maana hakuna mwanadamu au kiumbe kitakatifu yeye ametajwa mara 95 katika maandiko ni yeye ndiye anayehusika katika kazi ya utakaso
  • Anahusishwa katika kanuni ya ubatizo Math 28;19
  • Alihusika katika ubatizo wa Yesu Kristo Luka 3;21-22.
  • Anahusihwa katika salam za Neema 2Koritho 13;14
  • Wokovu wa mwanadamu hauwezi kuwa kamili bila kuhusisha ushirika huu wa utatu
7.       Roho Mtakatifu ni tofauti na Baba  na Mwana.
  • Roho Mtakatifu hushirikiana na baba na mwana  katika utatu katika njia inayoonyesha kuwa ni Mungu huku ikiwa wazi kuwa ni nafsi tofauti
  • Yesu Kristo mwenyewe alimuita Roho Mtakatifu Mfariji mwingine Yohana 14;15-18,26 kwa kiyunani ni Parakletos ambalo maana yake ni Mfariji, mwalimu, Mwenyekutia nguvu, muombezi, wakili, Yeye aliyetayari au karibu kusaidia neno Another hutumika katika maneno mawili Heteros ambalo maana yake ni mwingine tofauti na Allos  ambalo maana yake ni mwingine wa aina ileile.
  • Hivyo wa aina nyingine humaanisha tofauti na Kristo lakini wa aina kama ya Kristo hivyo Roho Mtakatifu ni nafsi nyingine  ya aina moja na Yesu aina yao ni asili ya uungu.
8.       Tatizo la uungu wakati wa kanisa la karne ya kwanza.
Nyakati za kanisa la kwanza ni wachache walikataa mafundisho kuhusu utatu,Baadhi ya maandiko ya mababa wa kanisa kama Irenaeus na Tertulian walionekana kuelemea katika upande huo wa Mungu mmoja lakini hii ilikuwa ni kwa sababu katika ulimwengu wa miungu mingi inayoabudiwa ilikuwa ni sawa kuwa na wakristo wenye msimamo wa kuamini kuwa Mungu ni mmoja na ana nafsi tatu.
   Tatizo lilianza kujitokeza pale watu walipoanza kutofautisha Baba,Mwana na Roho Mtakatifu na mgogoro mkubwa ulikuwa ukimhusu Yesu Kristo ambapo jamii ya watu kama Gnostics  walimtofautisha Yesu na Kristo, walimaanisha Kristo ni kiumbe kutoka kwa Mungu na ni mtakatifu sana  lakini Yesu ni mwili na hivyo Yohana mtume aliyaita mafundisho hayo kuwa ni ya mpinga Kristo (1Yohana 4;2,2Yohana 7).Pia walifundisha kuwa Roho Mtakatifu ni kiumbe vilevile kutoka kwa Mungu na si Mungu,Baadhi ya wasomi wengine walifundisha mambo yafuatayo;
§  Origen msomi kutoka Alexandria Misri katika karne ya tatu alimfanya Mungu baba kuwa Mungu kamili na Yesu kuwa chini ya Baba na sio mungu na Roho Mtakatifu akiwa chini zaidi kosa hili lilipelekea kukosesha wengi kwa mfano watu wa Makedonia hawakumuita Roho Mungu kabisa ingawaje pia hawakumuita kiumbe.
§  Arius katika karne ya nne alisema kuwa Yesu ni kiumbe tu  na ameitwa Mungu kwa sababu tu anafurahia upendeleo wa Mungu na pia hakumpa Roho nafasi ya uungu ni kwa sababu hizi mpaka leo wako watu ambao hudhani kuwa Roho Mtakatifu ni nguvu tu ya kawaida
§  Callistus wa Rumi moja ya waandishi wa zamani  alifundisha kuwa Baba na Mwana ni nafsi ileile tu moja na Roho Mtakatifu alijibadili kuwa mwana  na ni sawa na Baba
§  Sabellius katika mwaka wa 250 Baada ya Kristo alisema Baba, Mwana na Roho ni yuleyule mmoja tu isipokuwa hujifunua katika namna mbalimbali  kama muumba alijifunua kama Baba, duniani katika kazi ya ukombozi alijifunua kama mwana na anapofanya kazi na kanisa amejifunua kama Roho
§  Tatizo lilisuluhishwa kwa kikao cha Nikea mwaka 325 B.K. ambapo walitambua kuwa Kristo ni nafsi na kukubali kuwa wanamwamini Roho Mtakatifu bila kutoa ufafanuzi zaidi Hata hivyo mtu mashuhuri mwenye mvuto Athanasius aliyefariki 373 Alisimama kuweka sawa akitambua kuwa Baba si Mwana wala Mwana si Roho na kuweka wazi kuwa Tunamwamini Mungu mmoja  katika nasfi tatu  na hizi nafsi tatu ni Mungu mmoja
§  Kanisa la uingereza pamoja na kanisa la Methodist wao waliweka msimsitizo katika Biblia  na kutoa ukiri wa kimethodisti mwaka 1789 wao waliamini katika umoja wa Mungu kuna nafsi tatu katika umoja wakiwa na nguvu na umilele sawa na hao ni Baba,Mwana na Roho wao ni kama walibadili maneno lakini hawakuwa mbali na Athanasius hata hivyo swala hili lilifungua mlango wa kujifunza zaidi kuhusu kazi za Roho Mtakatifu hata leo
§  Mwaka wa 156 B.K.kulitokea uamsho wa kundi lililoitwa Montanism na sababu kubwa ya kutokea kwa uamsho wao ilikuwa ni kupambana na desturi zilizoibuka katika kanisa,kulitegemea kanisa badala ya Roho Mtakatifu na uongozi wake,walipinga swala la kuweko kwa maaskofu na maongozi ya kibinadamu na kuacha kumtegemea Roho wa Mungu,Mafundisho yao yalikazia kurudi kwa Yesu Kristo na kuwa angekuja na kustawisha ufalme wake,walikuwa na msimamo mkali kwa ajili ya mafundisho kuhusu Roho Mtakatifu na uvuvio,walisisitiza maadili na kupinga maswala ya kupata elimu ya theolojia,Hawakuruhusu mtu kuoa kama mkeo angefariki au mumeo,walifunga sana,na walikula vyakula vikavu wasomi wengi wanaamini huu ulikuwa ni sawa na upentekoste  uliokuja baadae hata hivyo wanakosoa ile hali ya kukosa kiasi,kukataa elimu ya theolojia,na kutojali mfumo wa uongozi na kuwa elimu ni muhimu kwani hulifanya kanisa kuwa na nguvu montaniats waliteswa sana kwa sababu ya watu wasiotaka mabadiliko.Tertulian alikuwa moja wa watu wasomi aliyejiunga na montanism  mwaka wa 200 B.K. na uamsho huu ukatiwa nguvu sana

ASILI YA ROHO MTAKATIFU
     Kwa kawaida ni vigumu kujua kwa haraka asili ya mtu bila kujua majina yake kamili kwetu waafrika ni rahisi kujua asili ya mtu akitumia jina lake la asili Mfano Peter Mmari au Anna Shayo mara yanapotajwa majina haya utajua kuwa watu hao wana asili ya kichaga na majina kama Ngonyani,Mapunda,Nakatembo,Mbawala,Komba na ndunguru yanapotajwa yatakujulisha kwa haraka kuwa watu wa jinsi hii ni watu wa Songea kwa nini kwa sababu majina yanatusaidia kujua asili,Ili tuweze kujua asili ya Roho Mtakatifu ni muhimu kujua majina yake

 A: Huitwa Roho wa Mungu.

     Roho Mtakatifu anaitwa Roho wa Mungu kwa sababu kwanza ana asili ya uungu,ana sifa zote zinazomfanya Mungu awe Mungu,Hawgawanyiki(Ebrania 9;14) ni wa milele,ni mwenye nguvu zote (Luka 1;35) Yuko mahali kote kwa wakati  mmoja, Zaburi 139;7-10,Anajua yote hata mafumbo katika moyo wa mwanadamu 1Koritho 2;10,Yeye hufanya kazi zote ambazo Mungu anafanya kama uumbaji Mwanzo 1;2,anabadilisha na kufufua Ayubu 33;4;Yohana 3;5-8 na Rumi 8;11 Roho mtakatifu yuko katika cheo kimoja na Baba na Mwana 1Koritho 12;4-6 Yeye ni nafsi na sio nguvu fulani kama watu wengine wanavyofikiri sio msukumo ana akili,hisia anafundisha ana amua, anaamuru,hutuombea(Rumi 8;27Efeso 4;30,Yohana 14;26,Galatia 4;6 Rumi 8;26) ana uamuzi ?utashi na anafunua.

 B: Huitwa Roho wa Kristo.

     Anaitwa Roho wa kristo katika maandiko Rumi 8;9 hii ni kwa sababu amatumwa kwa jina la Kristo na huombwa kwa jina la Kristo na humtukuza Kristo (Yohana 14;26,16;14).Kama alivyo Roho wa Mungu pia ni Roho wa Kristo,Tangu mwanzo alikuwa akisema na manabii kuhusu kuja kwa Yesu Kristo 1Petro 1;10-11.na kwakuwa tumekuwa wana Mungu alimtuma Roho wa mwana wake katika mioyo Yetu aliaye Abba yaani baba Wagalatia 4;6

C: Huitwa Mfariji. 

     Jina hili amepewa kati ya Yohana 14-17 neno mfariji kwa kiyunani ni ”Paracletos” ambalo maana yake ni aliyeitwa kwa niaba ya mwingine apate kusaidia ni msahuri na wakili Yohana 14;16 hata hivyo hii haimaanishi kuwa Kristo ameacha kuwa karibu na sisi 1Yohana 2;1 Roho mtakatifu ni msaada wa kiungu ni msaada wa kimbingu ambaye anatoa msaada unaohitajika katika maisha yetu na huduma Nami nitamwomba baba naye atawapatia msaidizi mwingine akae naye hata milele Roho wa kweli Yohana 14;16,26,Yohana 15;26 Yohana 16;7.

D: Huitwa Roho Mtakatifu

     Tabia ya Mungu siku zote yeye ni Mtakatifu Roho wa Mungu ni Mungu hivyo naye ni Mtakatifu  na ndiye anayefanya kazi ya utakaso ndani ya muamini tunapomuhitaji, kwakweli hakuna toba ya kweli inayoweza kupatikana katika moyo wa mwanadamu bila msaada wa Roho Mtakatifu Yeye ndiye sababu ya kusamehewa dhambi zetu Kutoka 23;20-22 kumtii yeye siku zote kutaleata matokeo ya moyo safi na tabia njema Rumi 1;4, Nifundishe kutenda mapenzi yako kwa kuwa wewe ndiwe Mungu wangu na Roho wako mwema aniongoze katika njia iliyo nyooka Zaburi 143;10.

E: Huitwa Roho wa Ahadi.

     Pamoja na kuwa alikuwa akihusika katika shughuli mbalimbali tangu katika agano la kale Roho mtakatifu alihaidiwa kuwa angekuja Rasmi na kumwagwa kwa watu woote  Ezekiel 36;27,Yoel 2;28 na pia Kristo mwenyewe alihaidi ujio wa Roho Mtakatifu baada yake hivyo huitwa roho wa ahadi Luka 24;49,Galatia 3;14

F: Huitwa Roho wa kweli.

    Ni Roho wa kweli na hakuna uwongo wowote ndani ya roho mtakatifu wala hawezi kutuongoza kinyume na maandiko au kweli ya Mungu,kamwe haiwezekani kutokea mgongano kati ya Roho Mtakatifu na Neno hata siku moja kwa ujumla neno la Mungu ni neno la Roho Mtakatifu  Efeso 6;17 na kama mwandishi wa Biblia 2 Petro 1;21, hivyo hawezi kuwa kinyume na neno lake mwenyewe.  Muongozo wa Biblia siku zote ni muongozo wa Roho Mtakatifu hivyo atatuongoza sawa na neno Yohana 14;16-17.15;26 1Yohana 4;2,6 Na hivi ndivyo tuwezavyo kumjua Roho wa Mungu  kila roho isiyo mkiri Kristo kwamba yu aja katika mwili haitokani na Mungu

G: Huitwa Roho wa Neema.

     Roho Mtakatifu ni Roho wa neema pia Yeye Hubeba ujumbe kuelekea katika nafsi ya mwanadamu na kutoa mwaliko wa toba na kusababisha mwenye dhambi kukubali utendaji wa Mungu katika maisha yake ,roho wa neema pia husaidia katika kutoa neema ya kutuwezesha kuomba kwa kuugua kwa uchungu Zekaria 12;10 na kwa sababu Roho wa Mungu hutoa neema ni vibaya kukosana na Roho huyu kwani kukosana na Roho wa neema kutakufanya ukose namna ya kuwa na toba ya kumfikia Mungu Waebrania 10;29 kwa sababu Roho ndiye anayetoa neema ya mtu kutubu dhambi zake na uovu wake na kuuacha pia ndie anayesaidia na kutoa nguvu ya kututakasa na kutusafisha hivyo ukimpinga unapingana na yeye anayetoa neema ya mtu kutubu na kutakasika

H.Huitwa pia Roho wa Uzima.

     Sheria yake Roho wa uzima ni sheria ya imani na upendo na ndiyo inayotuweka huru kutoka katika sheria ya dhambi na mauti na hivyo mtu akiishi kwa Roho anaishi kwa ushindi  dhidi ya dhambi na mauti Warumi 8;2,Ufunuo 11;11 Hali kadhalika Yeye hutia uzima katika kila kiumbe  ”Namwamini Roho Mtakatifu ,Bwana mtoa Uzima”...Hivi ndivyo usemavyo sehemu ya ukiri wa imani hii inamaana ya kuwa licha ya kuwa yeye ni muumba ndiye anayesababisha uhai wa asili na wa kiroho na kuwa uwezo wa kukufufuliwa uko katika uwezo wake

I: Huitwa Roho wa Upitisho (Adoption).au uana

      Roho Mtakatifu sio tu wa uzima lakini ndiye anayehusika na kutuzaa mara ya pili na kuwa na uhusiano na Mungu hivyo pia huitwa roho wa uana kwa sababu anatupa uwezo wa kufanyika kuwa wana wa Mungu au anatupitisha kutoka kuwa wana wa giza na kutufanya kuwa wana wa nuru au wana wa Mungu Warumi 8;15 kwa hivyo katika mioyo yetu tunapewa ujasiri wa kumuita Mungu Baba au kulia abba wala hatuwi watumwa tena bali wana Galatia 4;6.

J: Huitwa Roho wa Hukumu

     Roho mtakatifu pia huitwa roho wa hukumu katika KJV Spirit of Burning  hii ina maana anasima mia hukumu haki na sheria na utaratibu ni mtakatifu na hatavumilia dhambi ni polisi wa maadili ni hakimu wa haki ya Mungu anapinga dhambi,anaiweka wazi anaithibitisha na anawabadilisha watu kutoka katika dhambi Isaya 4;4 kusudi la kuiweka dhambi kwetu ni ili tuitubu na sio kutuaibisha  na hufanya kazi ya kututenga na dhambi Isaya 25:5-6.

K. Huitwa Roho wa Hekima na ufunuo

     Kwa kweli yeye ni Roho wa ufahamu,ushauri,maarifa,ufunuo na uchaji wa Mungu Isaya 11;2 analeta ufunuo ana angazia anatoa ujuzi wa kiroho na anaongoza na anaamsha hari katika mioyo yetuMaandiko yenyewe ni matokeo ya kazi yake  alitoa hekima na ujuzi kwa mafundi Kutoka 28;3 anatoa hekima ya maongozi Kumbukumbu la Torati 34;9 Roho wa Mungu, maarifa, ufahamu, mashauri na nguvu, hekimana uchaji wa Mungu ulitabiriwa kukaa juu ya Kristo Isaya 11;2 Efeso 1;17 3;4-5 Mathayo 10;20 Roho atatupa kipi cha kuzungumza wakati wa matatizo

L: Huitwa Roho wa kinywa chake 

     Roho wa Mungu hunena kwa niaba ya Mungu na Kristo wake na pia hutangaza hukumu za Mungu kwa hivyo hata mpinga Kristo atashindwa kupitia Roho wa Kinywa chake kristo 1Thesalonike 2;8

M: Huitwa Roho wa Imani

     Roho Mtakatifu huitwa pia Roho wa imani  yeye ndiye anayetoa neema ya kuamini katika Yesu Kristo na kutupa uhakika na ujasiri hata kuweza kukiri kwa ujasiri 2Koritho 4;13,Hutusaidia kumuamini Yesu na kupata wokovu,Hutusaidia kumuamini Yesu na kupokea miujiza yetu na mahitaji yetu,Pale Yesu asemapo imani yako imekuponya imani hiyo si yetu kwa hakika ila ni zawadi ipatikanayo kupitia Roho mtakatifu kutusaidia kupokea kutoka kwa Bwana

N: Huitwa Roho wa utukufu.

     Kama roho wa Utukufu  wa Mungu hukaa juu yetu na kutunza furaha ya wokovu ndani yetu hata wakati wa mateso kwa ajili ya jina la Yesu hivyo maandiko yasema Kama mkiteswa kwa ajili ya jina la Yesu mna heri kwakuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anakaa juu Yenu.1Petro 4;14

O; Huitwa Chanda cha Mungu.
     Kwa kuhitimisha Roho Mtakatifu pia huitwa chanda cha Mungu Luka 11;26 Yeye ni nguvu zake aliyejuu luka 1;26-35 na ni roho wa milele Ebrania 9;14,Wachawi wa Misri walikiri kuwa utendaji uliokuwa ukifanywa na Musa na Haruni kule Misri ulikuwa ni utendaji unaotokana na Uweza wa Roho Mtakatifu au utendaji wa Mungu hiki ni chanda cha Mungu

ALAMA ZA ROHO MTAKATIFU

    Mifano ni mojawapo ya njia rahisi na kuu ya mawasiliano na ambayo mungu aliitumia kuzungumza na watu ili waweze kuelewa kwa urahisi,Tangu zamani Mungu ametumia njia hii .Kristo pia alitumia mifano,Hapa ziko alama ambazo zinaweza au zimetumika kibiblia ili kutusaidia kuelewa mabo kwa upana na urahisi,hapa ziko alama zinazotusaidia kuelezea utendaji wa Roho Mtakatifu katika njia iliyo rahisi kila mtu kuelewa

A: Alama ya Moto
     Alama ya moto inatumika kutufundisha kazi za utakaso ,utisho,na ujasiri ,moto kama msukumo au wivu unaozalishwa na Roho mtakatifu  unatusukuma katika kuifanya kazi yake yeye ni Roho wa kazi (Yeremia 20;9),Moto unapowashwa unazagaa au unaenea kwa kasi na kuruka na kuyeyusha,pia unaangamiza na kusafisha moto ni alama ya uwepo wa Mungu  (Isaya 66;7,4;4,Mathayo 3;11,Luka 3;16,Matendo 2;3).

B;Alama ya maji
    Woote tunajua umuhimu wa maji katika maisha ya mwanadamu kwa kifupi maji na uhai vina uhusiano mkubwa sana  ni uzima,yanasafisha,yanaondoa kiu yana burudisha yanatuliza yanazalisha na kusababisha uhai wa mimea na yanakuza lakini pia maji yana nguvu kubwa sana kama ya natembea au ukipingana na mkondo wake  maji hutumika kuelezea kazi za Roho Mtakatifu Kutoka 17;6,Ezekiel 36;25-27,47;1,Yohana 3:5,4;14,7;38-39

C: Alama ya upepo
     Upepo unawakilisha utendaji unaoonekana wa nguvu isiyoonekana,Roho Mtakatifu anapokuwa kazini kazi zake huonekana lakini yeye mwenyewe haonekani kwa macho ya kibinadamu kama jinsi isivyowezekana kupingana na nguvu za upepo halikadhalika huwezi kupingana na kazi za utendaji wa Mungu Roho Mtakatifu Yeremia 4;12, Isaya 66;15, 2Falme 2;11 Upepo wa nguvu za mungu uliwaletea wana wa Israel kware kule jangwani na wakajazana ka umbali wa kilomita za mraba kumi na ujazo wa futi tatu sawa na ridhaa mbili Hesabu 11;31

D; Alama ya Muhuri
      Kwa kawaida muhuri unawakilisha umiliki na uhalali,pia unawakilisha mamlaka na usalama au uthibitisho Kwa msingi huo Roho Mtakatifu anapokuwa ndani yetu anawakilisha kuwa sisi tu mali ya Mungu Efeso 1;13 2Timotheo 2;19,Yohana 6;27,2Koritho 1;22,Ufunuo 5;1 kwa akawaida kama mtu ataandika barua kisha asiweke sahihi au muhuri kunakuwa na wasiwasi kuwa huenda ikawa barua hiyo si yake Hivyo Roho mtakatifu ni uhakiki ya kuwa sisi ni mali ya Kristo Warumi 8;14-16

E: Alama ya mafuta.
      Moja ya alama inayotumika sana kama alama ya Roho mtakatifu Huenda ni mafuta  lakini kwa kawaida mafuta yaliyotumika ni mafuta ya mizeituni ambayo yalielekezwa kutumiwa wakati wa agano la kale na kutumika kama alama ya Roho Mtakatifu, Mafuta haya yalitumika wakati wa kuwaweka wakfu makuhani ambapo walimwagiwa mafuta hayo vichwani mwao Kutoka 29;7,30;30 Walawi 8;12;21;10-12.Zaburi 133;2 mafuta pia yalipomwagwa juu ya kiongozi mfalme ajaye yalimaanisha kuwa taji ya kifalme iko juu ya mtu huyo lakini pia ilikuwa ikiwakumbusha kuwa utawala ni kazi ya Mungu na humpa yeyote amtakaye1Samuel 10;1,16;13,Psalm 89;20 1 Wafalme 1;39 2Falme 9;6.Mafuta pia yalitumika kumpaka mgonjwa aliyepona ukoma Walawi 14;17-18 mafuta yalitumika pia wakati wa sadaka ya unga iliyoletwa kwa Bwana  Lawi 22na sio katika sadaka ya dhambi Lawi 5;11,Mafuta hayo pia yalitumika kama mafuta ya taa ya vinara saba iliyokuwa patakatifu Kutoka 27:20 Kwa mujibu wa Yakobo alitaka pia yaambatane na maombezi ya wagonjwa kwa kuwapaka Yakobo 5;14,Roho Mtakatifu huyaangazia maisha yetu ya kiroho na neno la mungu ili kusudi tulielewe vema, hutufariji na kutuponya, mafuta yanapenya, yanalainisha, yanaponya,yanalinda, yanaondoa ugumu au ukakasi na yananenepesha mwili.

F: Alama ya mvinyo .
     Ni jambo geni labda wakati mwingine kuitumia alama ya mvinyo kuihusisha na Roho Mtakatifu lakini ukweli unabaki kuwa Roho huleta msisimko mkubwa kwa waamini wa kipentekoste na karismatiki siku ya Pentekoste mitume walifikiriwa kuwa wamelewa kwa mvinyo Matendo 2;13 huenda watu hawa walidhihaki hivyo kutokana na muonekano wa Mitume katika siku ile, Mvinyo huleta uchangamfu hasa inapotokea kuwa mtu ana huzuni Muhubiri 10;19 hata hivyo hii haimaanishi kuwa tunapaswa kunywa mvinyo lakini badala yake waamini wanapaswa kuishi maisha yenye viwango zaidi ya wanywa mvinyo Efeso 5;18

G: Alama ya Njiwa
     Alama ya njiwa hutumiwa na wapentekoste wengi kumuelezea Roho Mtakatifu huenda hii ni kwa sababu Roho Mtakatifu alishuka juu ya Yesu akiwa na umbo kama njiwa Luka 3;22, Njiwa ni alama ya amani busara na utulivu hizi ni tabia alizo nazo Roho wa Mungu, kwakuwa Roho huzungumza kwa upole ni muhimu kuwa makini kumsikiliza, tunapokataa mashauri yake na kuipinga sauti yake ya upole inayotushauri mambo bora ndani ya mioyo yetu tunamzimisha na wakati mwingine tunamuhuzunisha kiasi cha kuugua na anapotuacha amani ya kweli hutoweka lakini akiwepo amani huwepo Hata hivyo Roho wa Mungu ni mwaminifu sana kwa waamini na kwa kusudi la Mungu lilioko ndani mwetu.

ROHO MTAKATIFU NDIYE ALIYEVUVIA MAANDIKO
     Maandiko yaani Biblia ni kazi ya Mungu na Roho Mtakatifu ndiye muhusika mkuu wa usimamizi wa kazi ya maandiko

Umuhimu wa maandiko
     Neno la Mungu lililoandikwa lilihitajika kwa ajili ya wokovu kwa sababu tunahitaji ujuzi na kweli za wokovu wetu ambao msingi wake ni katika kufa na kufufuka kwake Yesu Kristo kwani hatuwezi kujiokoa wenyewe kupitia matendo yetu mema na mawazo yetu mazuri
     Mungu ni Mungu aliyetamani kujifunua kwa wanandamu yeye mwenyewe na ili kazi yake anayoifanya iweze kujulikana kwa miaka na miaka mpaka wakati huu tulionao leo  watu wanahitaji nakala ya yale Mungu aliyokuwa anasema na ambayo anatenda.
Kwa hivyo neno la Mungu ndio njia pekee ambayo kwa hiyo tunaweza kujua na kuelewa na kuamini kweli kuhusu Mungu na mpango wake kwa wanadamu na hivyo neno lazima lienezwe Warumi 10;13-17.

Matendo ya Roho Mtakatifu na Neno lililovuviwa
     2Petro 1;20-21, Manabii ambao waliandika neno la Mungu waliongozwa na Roho Mtakatifu walitii na kukubali kuubeba mpango wake kwa wanadamu wengi walijitambulisha kwa jumbe zao kuwa zinatoka kwa Mungu. Neno Neno la Bwana likanijia limetajwa mara 3,800 katika Biblia hii ikijumuisha neno asema Bwana wa majeshi Roho aliwaongoza katika njia ya moja kwa moja akiwapa wao neno la Mungu
Matendo mengine yalifanywa na watu katika agano la kale kwa uongozi wa Roho Mtakatifu mfano
·         Gideoni alipiga tarumbeta baada ya kujiwa na Roho wa Mungu Waamuzi 6;34
·         Samsoni alimchana mwana simba vipande baada ya kujiwa na Roho Mtakatifu Waamuzi 14;4
·         Sauli aligeuzwa kuwa mtu mwingine na aliweza kutabiri baada ya kujiwa na Roho wa Mungu 1Samuel 10;6
·         Wanafunzi walinena kwa lugha baada ya Roho Mtakatifu kuja juu yao Matendo 24;10;46 19;6.
·         Roho Mtakatifu alivuvia watu kuandika Neno la Mungu- wengi walioandika neno la Mungu hawakufanya hivyo kwa mapenzi yao walifanya hivyo kwa kuwa Mungu Roho Mtakatifu aliwataka kufanya hivyo 2Petro 1;20-21,
·         Roho Mtakatifu hufanya kazi ya kutuangazia au kutufunulia neno la Mungu kusudi tulielewe vema, Roho Mtakatifu ambaye aliwaongoza waandishi kuandika neno la Mungu  hufanya kazi ya kumuangazia au kumpa ufunuo mtu anayelisoma neno la Mungu akiwa na Moyo uliovunjika na kutaka kujua humpa ufahamu.tafasiri na namna ya kulitumia neno hilo kwa usahii kusoma pekee hakuwezi kusaidia kupata ufahamu kuhusu kweli za kimaandiko 1 Koritho 2;14 Mungu hakumtoa Roho Mtakatifu kwa kusudi tu la kuongoza waandishi bali pia kwa kusudi la kuangazia neno la Mungu kwetu ili kutimiza kusudi ambalo Mungu amelikusudia liweze kutimizwa hivyo kuangaziwa au ufunuo hutusaidia katika kuyaelewa maandiko, kutafasiri na kuyatumia.

Asili ya uvuvio
     Ni nini maana ya neno uvuvio? Kwa bahati mbaya si makanisa yote yanakubaliana na wazo la uvuvio. Kwa miaka mingi sana kumekuweko na hoja mbalimbali na mawazo mbalimbali yatolewayo kuhusu uvuvio wakati mwingine yana ukweli lakini yanakuwa magumu kuelezeka

A:Mawazo mablimbali yasiyo sahii sana kuhusu uvuvio

     Uvuvio Asili au Ufahamu wa kupita kawaida intuition theory
Wao huamini kuwa uvuvio ni tendo la kawaida la uwezo wa kufahamu ulio juu ya viwango vya kawaida wao huamini ni uwezo wa kawaida wa binadamu kuwa kwa uwezo wa asili anakuwa na viwango vya juu vya ufahamu ambapo huweza kupata kweli za rohoni.

     Udhaifu wa wazo hili
     Hufanya uvuvio wa kibiblia uwe hauna tofauti na maandiko yoyote ya kawaida yaliyoandikwa kwa viwango vya juu kama yale ya akina Willium Shakespeare na nyimbo kuu za kanisa, Hii inachanganya kati ya kazi za Roho Mtakatifu aktika kuvuvia na kuangazia au kufunulia, Kuangazia hakuhusiani na kuleta kweli mpya bali kuielewa kweli ambayo tayari imekwisha funuliwa katika neno.

     Uvuvio wa baadhi ya maandiko tu Partial inspirations theory
Wao huamini kuwa Mungu alitoa uwezo uliohitajika na wa kuaminika katika kulileta neno la Kweli la Mungu kwa waandishi walioamriwa kuandika kwa hivyo iliwafanya wasikosee katika baadhi ya mambo ya imani lakini si katika mambo mengine mfano waliweza kukosea katika maswala ya kihistoria na kisayansi

     Uvuvio wa mawazo na sio maneno
 Wao huamini kuwa Mungu alivuvia wazo la ufunuo fulani lakini aliwaachia wanadamu hao kuamua kuwa watayaandika vipi. Dhana ya wazo hili si sahii ni vigumu kufikiri wazo kisha ukaandika tofauti,wazo linaweza kutafasiriwa vizuri kwa maneno hivyo tunaamini kuwa maneno yalivuviwa na sio swala la mawazo.

     Uvuvio  Huria
Hawa huamini kuwa Biblia ina maneno ya Mungu hii ina maana kwamba pia yako maneno ya kawaida ya watu ambayo yamechanganyika, wanaamini kuwa ni kitabu hasa cha kidini lakini kuna Historia, Habari, vizazi, mashairi ya kimapenzi, mipangilio na mambo yasiyopangiliwa wala kujali mtiririko maalumu au kamili. Dhana hii  inataka kuhatarisha kwani ina maana kuwa waandishi walijiamulia tu wapi waandike wapi ni uvuvio wapi hawakuvuviwa wapi Mungu anazungumza na wapi mwanadamu anaweka mkono wake
    
     Uvuvio wa Imla
Hawa huamini  kuwa manabii walipopokea uvuvio wa kuandika waliandika moja kwa moja kile ambacho Mungu alikuwa akikisema hii inamaanisha wao walikuwa kama kalamu tu, Roho aliwavaa kiasi ambacho hawakuwa na uhuru wao wenyewe isipokuwa kuandika kile Mungu anachokusudia  kwa hivyo huamini kuwa kila neno lilitoka moja kwa moja kwa Mungu na hivyo wao walifanya kazi kama mashine tu Dhana hii siyo sahii kwani Mungu alitumia watu na sio mashine au vifaa, Mungu hakuwafanya wasiwe na ubinadamu wao hivyo si kila kitu waliandika si kama bomba la kupitishia moja kwa moja kile Mungu alichokisema lakini waliandika kile ambacho Mungu alikuwa akikiweka katika mioyo yao

B: Mawazo Mbalimabli sahii kuhusu uvuvio
·         Uvuvio shirikishi - Uvuvio lilikuwa tendo la Roho Mtakatifu kwa waandishi akifanya kazi pamoja nao na kazi yao ilikuwa ni kusikiliza na kutii na kuandika
·         Uvuvio ulikuwa ni muongozo wa Roho Mtakatifu kwa waandishi akiwaongoza katika kuchagua nini cha kuandika na maneno ya kuandika
·         Roho Mtakatifu aliwalinda waandishi kutoka katika kukosea na kuruka uvuvio huu ulihusu kile kilichoandikwa na haikuwa lazima yawe mawazo au fikra
·         Mungu aliwafanya waandishi kuwa wafanya kazi pamoja naye akitumia misamiati yao, mitindo yao ya uandishi na uzoefu wao katika kuzipeleka kweli
·         Maandiko yamevuviwa kwa sababu ni matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu kupitia waandishi yeye aliwaongoza katika kazi nzima ya uandishi ili kwamba kweli ya Mungu iweze kunukuliwa katika Biblia kama neno kamili la Mungu.

      C: Kweli halisi
·         Uvuvio ni msingi wa kuaminika kwa Biblia na hapa tunaizungumzia Biblia yoote
·         Biblia nzima kwani imevuviwa ni sahihi haina makosa na ni halisi haijatiwa mkono
·         Ni sahii katika maswala yoote ya kihistoria au kisayansi na maadili na maswala ya mafundisho kwa wanadamu
·         Ukweli huu ni kwa maandiko yoote katika Biblia bila kuwekea mipaka kwamba ni baadhi ya mafundisho yake tu ndio yamevuviwa

D: Tafasiri sahii
·         Neno lina mawazo mbalimbali kuhusu Mungu, Kristo, Msalaba, Ufufuo na ubatizo wa Roho Mtakatifu
·         Ina nukuu halisi na tafasiri sahii kuhusu kweli nyingi
·         Ndiyo inayotupa ukweli na muongozo sahii kwa ajili yetu

       E: Roho Mtakatifu ni Roho wa kweli na nguvu.
·         Mungu ni Mungu mkamilifu na mnyoofu katika njia zake
·         Yesu ni Kweli
·         Roho Mtakatifu ni Roho wa kweli
·         Kila kinachozungumzwa katika maandiko kuhusu Mungu,Yesu na Roho Mtakatifu ni cha kweli Biblia inatuambia kweli zote zinazomuhusu Kristo na Mungu na kile ambacho Yesu alisema kuhusu Roho Mtakatifu ni halisi Roho anabeba ushahidi huo

Mamlaka Ya Roho Mtakatifu
     Uvuvio unaifanya Biblia kuwa kitabu pekee ambacho ni muongozo wa kweli wa imani na maisha

Mamlaka ya Biblia.
     Imefungwa pamoja na mwanadamu inajua mawazo yake, dhamiri yake moyo wake na matakwa yake na inamuongoza katika imani sahihi,Waebrania 4;12-13 aidha Biblia ina njia sahii na muongozo sahii Roho aliivuvia na analitumia neno kuwa muongozo wa maisha yetu, Jukumu letu ni kulisoma, kulitafakari na kulitendea kazi Roho pekee anajua mapenzi kamili ya Mungu na kwa msingi huo anajua ni namna gani atuongoze na amechagua maandiko yawe Muongozo wetu kwa kuyavuvia

Andiko huua
     Ukitumia akili zako tu kutaka kuyafahamu maandiko utaharibikiwa wengi wanaofuata yaliyoandikwa tu bila msaada wa Roho Mtakatifu wameishia katika ufarisayo uliokithiri au uhuru usio na mipaka

Msingi wa Kumtegemea Roho katika Kuyafahamu maandiko
     Yesu aliyajua maandiko na alifahamu kuwa yanaongoza lakini alitaka watu wayafahamu kwa usahii kwa hivyo alileta tafasiri sahihi kwa matumizi ya neno, Roho Mtakatifu anayajua maandiko na hutusaidia kuichunguza Biblia kupata muongozo unaohitajika, Hivyo basi tunahitaji msaada wa Roho Mtakatifu katika kuielewa Biblia vema na kuitii,Tunahitaji kufikiri zaidi ya andiko moja kuelewa lipi jema na lipi baya Roho mtakatifu hutupa ufunuo wa neno kupitia ufunuo wake wa kiungu ufahamu huo unaitwa Dechomai kwa kiyunani.

·         Ufahamu wa kawaida wa kiakili “Oida” Oida
·         Ufahamu wa kawaida wa kisomi au kisayansi “Ginosko” Ginosko
·         Ufahamu wa kawaida  mwepesi  “lambano” Lambano
·         Ufahamu unaotokana na Ufunuo wa Roho wa Mungu na shuku ya kiungu “Dechomai”Dechomai

Roho Mtakatifu hutumia neno
     Baadhi ya watu hujaribu kumfuata Roho Mtakatifu bila kukubaliana na neno au mamlaka ya Biblia.Kifaa kikuu Roho mMakatifu anachokitumia katika kutuongoza ni maandiko yaani Biblia Neno la Mungu pia huitwa upanga wa Roho kwa hivyo basi Neno ni silaha ya pekee ya Roho Mtakatifu ni kupitia neno na Roho Mtakatifu sisi nasi tunaweza kuwa nyenzo yake Roho husimama na neno na hajipingi mwenyewe

ROHO MTAKATIFU NI MUUMBA NA MTIA UZIMA
     Mshirika katika uumbaji Mwanzo 1;2 Kuna uhusiano wa Roho Mtakatifu na Mungu Baba na Mwana katika uumbaji.
·         Uumbaji ni jambo lililohusisha utatu woote wa Mungu katika hali ilyo sawa Baba ni muumba ndiye aliyeumba mbingu na inchi na bahari na vyoote viujazavyo na ni chanzo cha uhai Matendo 4;24
·         Mwana pia ni mtoa uzima  jukumu lake ni la pili katika uumbaji Yohana 1;3 kwa maana kupitia yeye umbaji wote ulifanyika, Mungu alisema naye kama alivyosema na manabii Yeye alikuwa ni neno halisi la Mungu na kupitia yeye ulimwengu ulifanyika na kuweko
·         Roho Mtakatifu ni mtoa uzima pia na ndiye anayehakikisha vitu vyote vinahaishwa pasipo Roho hakuna uzima  ni nguvu ya uumbaji wa Mungu na ndiye aliyefanya mambo yatokee au ndiye aliyetenda neno lilipotoka Zaburi 104;30.katika Agano la kale Roho Mtakatifu  alipewa upekee kama nafsi yeye alikuwa neno lililohai na njia ya uumbaji wa vitu vyote

Roho wa Bwana akatulia juu ya uso wa maji
      Kazi za Roho Mtakatifu zinaonekana katika uumbaji kwa kuanzia na Mwanzo 1;2 Biblia  mojawapo ya kiingereza cha kisasa inasomeka hivi.- ”A mighty wind that swept over the surfece of water” kwa hivyo wao hupotosha maana halisi kwa kumchukulia Roho Mtakatifu kama upepo wa mvumo  wa machafuko Tornado hii si dhana sahii kwani hakukuhitajika upepo wa jinsi hii wakati Mungu akiwa kazini  Biblia inasema Roho wa Mungu na sio upepo wa mvumo Roho wa Mungu hutumika kuelezea sikuzote Nguvu za utendaji wa Mungu au uwepo halisi wa Mungu kivitendo na kutulia juu ya uso wa maji ni kinyume na upepo wa mvumo je upepo wa mvumo unawezaje kutulia? Tafasiri kama hizi zinapingana pia na kile tunachosoma katika maandiko mengine ya Biblia kumhusu Roho Mtakatifu na matendo yake katika uumbaji

Roho Mtakatifu na uumbaji wa Mwanadamu
     Roho Mtakatifu pia amehusika katika uumbaji wa mwanadamu, Mungu alipomuumba mwanadamu alijumuisha wingi alionao kwa kusema na tumuumbe mwanandamu kwa sura na mfano wetu (Utatu) sura na mfano hapa ilimaanisha hali ya kiroho na kimaadili kwa asili ndani ya mwanadamu ni ya Mungu katika uumbaji huu kazi ya Roho Mtakatifu inaonekana katika kumfanya mwanadamu awe na asili halisi ya Kiroho, haki, utakatifu na maarifa

Pumzi ya Mungu
     Roho Mtakatifu huitwa pia Pumzi ya Mungu katika uumbaji anagalia Ayubu 33;4 kwa hivyo pumzi ya Mungu ni sawasawa na Roho wa Mungu kwa hivyo katika uumbaji Roho wa Mungu hufanya yoote huuisha kimwili na kiroho, Pumzi hii ya Mungu pia ilifanya kazi ya kumtofautisha mwanadamu na mnyama wa kawaida hivyo ni mwanadamu pekee anyebeba sura na mfano wa Mungu na hivyo kumfanya mwanadamu pekee kuwa na uwezo wa kuwasiliana na Mungu na kumuabudu, Roho wa Mungu alifanya kazi katika maisha ya mwanadamu wakati wa uumbaji akijihusisha na maandalizi ya uumbaji huo na pia kuweka uzima wa kimwili na kiroho na hivyo mwanadamu akawa kiumbe hai neno nafsi linamaanisha mtu kamili, mwenye pumzi ya uhai na mavumbi ya nchi mwenye uwezo wa kujitegemea na kuwa na maamuzi yake mwenyewe na kuweza kufanya kile anachoamua kufanya

Roho ya mwanadamu Mwenyewe.
     Hapa tunahitaji kujifunza tofauti ya roho ya mwanadamu mwenyewe na Roho Mtakatifu na pia kuangalia anguko la mwanadamu baadhi ya watu wamekosea na kuwafundisha watu kuwa wao ni miungu au hata wao ni Yesu hawa ni watu wanaoamini kuwa mungu ni kila kitu na kila kitu ni mungu wanamfanya Mungu kuwa anafanana na uumbaji wake woote lakini kwa hakika sisi sio Mungu
     Wengine huamini kuwa maisha ya mwanadamu na roho ya mwanadamu ni Mungu mkubwa ndani yake, Ni kweli kuwa roho zetu hutoka kwa Mungu na kwake hurejea lakini hii haimaanishi kuwa mwanadamu ni mungu kwa kiasi ndani mwake na ndani yake tena Roho Mtakatifu kwa ujumla hii inamaana ya kuwa mwanadamu hawezi kwa namna yoyote ile kuwepo katika mwili bila uhai ambao Mungu anatoa hivyo roho ya kibinadamu sio Mungu ndani ya mwanadamu Kumbukumbu la Torati 2;80
Kama ni hivyo inawezekanaje Roho nzuri ikapingana na Mungu, Mungu hawezi kijipinga mwenyewe au asili yake
     Wengine wanaamini kwa sababu ya anguko roho ya mwanadamu imekufa na haziko mpaka zinapoitwa tena wakati wa kuzaliwa mara ya pili Torati 2;30 inaonyesha kuwa ingekuwa vigumu roho hiyo kufanya ugumu kama imekufa au haiko, Mwanzo 9;6 inaheshimu sura na mfano wa Mungu ndani ya mwanadamu kwa kukataza mauaji,Kwa matokeo ya dhambi sura na mfano wa Mungu ndani ya mwanadamu imeathiriwa imekuwa katika hali mbaya lakini iko palepale na hii ndio maana mtu muovu mtu wa dhambi bado pia hutenda mema na mambo ya kuvutia mazuri kama miziki, mashairi, uvumbuzi wa vitu mbalimbali katika teknolojia sayansi na madawa n.k.

Uhusiano wa Roho Mtakatifu na roho ya mwanadamu na asili ya anguko la mwanadamu
     Roho ya mwanadamu kwa asili iliumbwa na Mungu kupitia Roho Mtakatifu, Hivyo Roho Mtakatifu ni asili ya mambo yoote mazuri aliyonayo mwanadamu.

Anguko la mwanadamu.
     Tunataka kujifunza kwanini mwanadamu anahitaji kuzaliwa upya kupitia Roho Mtakatifu, Hii ni kwa sababu kupitia anguko la mwanadamu athari iliyojitokeza ni ya kimwili na kiroho na imeathiri maisha yote ya mwanadamu na utendaji wake, Dhambi imeharibu  mambo mazuri ya mwanadamu na wakati woote anakusudia maovu, mwanadamu amekufa kiroho kwa hivyo hawezi kumpendeza Mungu wala kutimiza kusudi la Mungu, jambo la msingi kwa mwanadamu ni kuzaliwa mara ya pili na kuupokea wokovu kwa imani na kupitia neema inayotolewa na Mungu kupitia Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu hutufanya upya na kutuwezesha na hii ndiyo kazi ya Roho wa Mungu hata baada ya anguko la mwanadamu, Roho huendelea kufanya kazi ya kutuumba kwa upya na kututia nguvu katika hali zote ya kimwili na kiroho Mwanzo 3;15 tunahaidiwa wokovu

Utendaji wa Roho Mtakatifu baada ya Anguko la mwanadamu.
    Ayubu 34;14-15 na Zaburi 104;30 zinaonyesha kazi endelevu ya Roho Mtakatifu kwa ujumla wake baada ya uumbaji
·         Hutia nguvu na uzima kwa ulimwengu na kwamba bila Roho wa Mungu hakuna uhai unaoweza kuendelea
·         Hufanya kazi kwa ulimwengu kuwaonyesha njia, akihukumu matendo yetu kuturekebisha na kututia nguvu kuendelea kiroho kama tunakubali msaada wake.
·         Mungu ameweka kanuni fulani za kawaida na za kimaadili na ni Roho wa Mungu anayesukuma sisi kuzifuata kanuni hizo na hizi hufanya kazi kwa wasiookolewa kwa ufunuo wa ujumla na kwa waliookolewa kwa ufunuo maalum
·         Yeye kazi yake si kuhukumu ulimwengu tu wakati woote lakini hufundisha hushauri na kututhibitishia lililo jema au lililobaya kwa kusudi la kutufanya tuachane na uovu Roho alifanya hivyo kwa watu wa Efeso Matendo 19;1,23-27 ambapo watu waliokuwa wakijishughulisha na uchawi na uganga waliacha uovu huo kwa wingi wao, Popote pale ulimwenguni inapotokea ukristo unashuka katika viwango inatokea kumomonyoka kwa maadili kwa kiasi  kikubwa, maovu na mauaji na mengineyo yakishamiri,Mungu alitembea kabla ya gharika na wanadamu waliokubali kutembea nae, alitembea na Enoko na alimchukua juu, alitembea na Nuhu na alimwokoa na gharika na alitembea na Seth na kuuchagua uzao wake kuwa baraka duniani, Mungu amekuwa mwaminifu kutembea na wengi walioongozwa na Roho wake na ambao walikuwa kama chombo cha Roho Mtakatifu cha kuionyesha njia ulimwenguni Seth ulikuwa ukoo uliohaidiwa kumleta masihi mkombozi wa ulimwengu Mwanzo 3;15, Enoko aliyetwaliwa kama ishara ya wokovu kwa wale watakaomcha Mungu, Mahalalel mtu aliyemsifu Mungu na kuliitia jina la bwana ishara ya wito wa Mungu kuabudiwa na wengine wengi
·         Biblia inaonyesha kuwa Mungu hajawai kukiacha kizazi chochote bila watu walioishi kwa ushuhuda wake na hataacha kufanya hivyo hata milele.

Roho Mtakatifu anataka watu wazaliwe kwa upya
     Katika kitabu cha mwanzo Mungu anaonyesha dalili za kinabii za Roho Mtakatifu kuhitaji watu wazaliwe mara ya pili hili linathibitika kwa maswala muhimu yafuatayo Mwanzo 6;5-8
·         Wakati wa Nuhu aliangamiza wenye dhambi woote na kuanza kizazi kipya cha mwanadamu wale waliomcha yeye
·         Kuzaliwa kwa upya kunakohitajika leo ni kuzaliwa kiroho kwa watu kufanya maamuzi ya kumgeukia Mungu na kupewa neema ya kuushinda uovu wakisaidiwa na Roho wa Mungu
·         Kuzaliwa huku kwa upya kunaweza kupatikana  si kwa nguvu na jitihada zetu bali kwa kuzaliwa kwa upya kunakotokana na Roho wa Mungu na njia ya kutunza maisha hayo mapya katika Kristo ni kwa kuendelea kuwa na ushirikiano na Roho Mtakatifu tukitazamia kuishi maisha makamilifu kama ya Mungu hebu hiki kiwe kilio cha maisha Yetu siku zote kutamani kuishi maisha kama yale aliyoishi Kristo

Sura ya Pili; ROHO MTAKATIFU WAKATI WA AGANO LA KALE

Roho Mtakatifu na Mwanzo wa Israel

Abrahamu na mababa wa Israel
     Ni wazi kuwa Abrahamu na mababa wengine wa imani walikuwa ni watu walioongozwa na Roho Mtakatifu ,Abrahamu alikuwa mtu wa imani  na kwa kweli historia yake ni wazi kuwa ni historia ya Mtu aliyetembea na roho Mtakatifu  na itakuwa ni jambo la kushangaza sana Kama Abrahamu Mtu ambaye Paulo anamtumia kama Mtu wa Imani katika Warumi 9;1-22, Wagalatia 3;6-18 kisha akawa mtu amabye hakujazwa kwa Roho mtakatifu
Abrahamu alikuwa Nabii Mwanzo 20;7
     Nabii ni mzungumzaji kwa niaba ya Mungu,mungu alizungumza naye na alimpa maelekezo ya kufanya kama alivyofanya kwa wengine,aliwafundisha wengine kumuabudu Mungu wa kweli  madhabahu alizozijenga ilikuwa ni ibada za wazi zenye kumshuhudia Mungu wa kweli,na Kama ilivyo kwa manabii wengi aliwaombea wakosaji aliomba kwa ajili ya Sodoma jambo lililofanywa na manabii wengine kama Musa Hesabu 14;13-20,Kmbukumbu 9;20 1Samuel 7;5,12;19,23 yeremia 7;16 na Amosi 7;2,5 mungu aliwaita wasiofaa ili awafanye wakamilifu Mwazno 20;7 Ibrahimu akisema uongo, Manabii waliongozwa na Roho Mtakatifu

Wapakwa mafuta Zaburi 105;8-22
     Abrahamu, Isaka, Yakobo na Yusufu walikuwa wateule wa Mungu na walipakwa mafuta kama manabii wa Mungu.Mungu aliwatumia hawa woote kama wanenaji kwa niaba ya Mungu kwa sababu karibu wote walikuwa sehemu ya kutimiza agano la Mungu alilolifanya na Ibrahimu Mwanzo 12;1-3 unabii huu ulihusu
·         Baraka binafsi za Ibrahimu
·         Baraka kwa taifa la Israel
·         Na Baraka kwa ulimwengu mzima mwanzo 12;1-3
     Kupakwa mafuta katika Biblia ilikuwa ni ishara ya kujazwa kwa Roho mtakatifu Zaburi 105;15 ingawa hatuoni hawa wakipakwa mafuta kwa ishara lakini Roho alikuwa juu yao  aliwatetea na walikuwa masihi zake kwelikweli Mwanzo 12;3,Zaburi 105;15 au 105;8-14 Mungu hapa aliwalinda masihi zake hao kutoka kwa Wafalme kama Farao na Abimeleki ambao waliwasumbua Ibrahimu na Isaka,yakobo na hata Yusufu,ulinzi wa Mungu kwa masihi wake ni wa uhakika Yeremia 1;7,9,17-19, ili tuweze kuendelea kuufurahia ulinzi huu kuendelea katika imani ni muhimu pamoja na kuendelea kutii 1Falme 13;1-32
      Baada ya Yusufu  kufasiri ndoto ya Farao  yeye mwenyewe alikiri kuwa Roho wa Mungu alikuwa juu ya Yusufu Mwanzo 41;38.

Roho Mtakatifu na Ujenzi wa Hema ya kukutania
     Kutoka 31;2-3,35;30-31 ujenzi wa hema ya kukutania ulifanyika kwa ajili ya Mungu na kwa utukufu wake,Hema hii ilijengwa kwa kusudi la kuwafundisha Israel kufanya kazi pamoja na kuwa hema ilikuwa ni mahali ambapo mungu angeendelea kufunua uwepo wake,Ujenzi wake ulikuwa wa ajabu hii inatufundisha kuwa kazi ya Mungu inahitaji zaidi ya juhudi za kibinadamu tunahitaji mguso wa upako wa Roho Mtakatifu  ili Mungu atukuzwe katika lolote tulifanyalo,ujuzi wetu na elimu yetu na ufundi tulionao unaweza kunolewa kitaalamu zaidi kwa upako wa Roho Mtakatifu
     Mungu alimjaza Bezaleli na Aholiabu kwa Roho wake mtakatifu kwa ajili ya ujenzi wa hema ya kukutania na kuwafundisha wengine hivyo Bezaleli na Aholiabu walikuwa ni wajenzi pakee wa Hema waliojazwa kwa Roho Mtakatifu Roho ndani yao alikuwa ndiye chanzo cha hekima ,ufahamu ubunifu na maarifa na utendaji mzima uliohitajika Kutoka 31;2-3,35;30-31 kwa msingi huu basi mungu alifanya hivyo ili kwamba Bezalel na Aholiab wasizitegemee akili zao za kawaida  na ujuzi wao pekee bali wa Bwana, Hekima iliwasaidia kuwapa ubunifu na nini cha kufanya ili kufikia lengo lililokusudiwa, Maarifa yaliwasaidia kujua nini kinahitajika na ni njia gani itumike kukamilisha lengo ufahamu uliwapa mwanga na ujuzi wa kufanya maamuzi Hili linatufundisha kuwa wahubiri, wanamuziki, waimbaji na watendaji mbalimbali wa kanisa tunamuhitaji sana Roho mtakatifu katika kazi zake.

Roho Mtakatifu juu ya Musa na wazee sabini wa Israel Hesabu 11;10-30
     Roho mtakatifu alihisika kipekee juu ya uongozi wa Musa na wana wa Israel,Musa aliitwa nabii ni Mungu mwenyewe aliyemuita kuwa nabii katika kichaka kilichokuwa kinawaka moto Hesabu 12;6-8,kutoka 3;6-15,4;14-16 na 7;1-2 hata ingawa Mungu alimtumia Haruni kuzungumza kwa niaba ya Musa bado mungu alizungumza na Musa kwanza hivyo musa alikuwa nabii,mungu aliweka Roho wake ndani ya musa Hesabu 11;17 kwa kweli Roho anatosha kwa mahitaji yetu.
      Mzigo wa uongozi kwa Musa ulikuwa ni mkubwa sana na alimwambia mungu kuwa huu ni mzigo usiobebeka na ambao ni kama baba aliyeachiwa mtoto mchanga jibu la Mungu kwa Musa lilikuwa ni kama makemeo kwa sehemu hata hivyo alimshauri Musa kuchagua wazee sabibi kwa sifa za kumsaidia Kutoka 18;18-26, Mungu alishuka na kutwaa sehemu ya Roho juu ya Musa na kuwajaza wale wazee ili wamsaidie kwa huduma na kuubeba mzigo pamoja nae na kuamua kesi mbalimbali na kuwatia moyo watu wa Mungu. Mungu ni kama alikuwa akimfundisha Musa kuwa angeweza na kuwa alipaswa kumtegemea Roho Mtakatifu kwa kazi hiyo Roho Mtakatifu ni mkuu mno kiasi cha kutuwezesha kubeba Mzigo wowote na changamoto zozote tunazoweza kukutana nazo

Kuishi chini ya Viwango alivyokusudia Roho Mtakatifu Hesabu 11;26-29
    Baadhi ya wazee wale waliopokea Roho mtakatifu walifurahia swala hilo kwa muda mfupi na baadae nguvu ile ilikoma,Baadhi ya wazee wawili Eldadi na Medadi waliokuwa wameitwa na Musa miongoni mwa wale sabini lakini hawakwenda katika hema lakini nao walijazwa Roho hukohuko walikokuweko wao kwa bahati nzuri Roho alidumu ndani yao na waliendelea kutabiri kambini Yoshua alitamani Musa awazuie hata hivyo Musa alimkemea kuwa asiwe na wivu kwa ajili yake kwani angetamani kama wote wangejazwa kwa Roho Mtakatifu.
    Mwanatheolojia Origen aliifananisha Roho iliyokuwa juu ya Musa kama taa ya vinara sabini iziyozimika. Musa alijua kuwa kutenda kazi kwa Roho mtakatifu hakuko juu ya uwezo wake wala sehemu au mahali maalumu wala muda,Mungu hutoa viongozi wa kibinadamu lakini mamlaka yao haiwezi kuzidi Mamlaka ya Roho Mtakatifu na Neno lake,Viongozi wa kiroho ni lazima wawaongoze watu katika utendaji wa karama za Roho Mtakatifu  sawasawa na neno bila wivu wowote Musa aligundua kuwa watu wenye kunung’unika,wenye kuasi,wasioamini wanaishi chini ya kiwango alichokusudia Roho Mtakatifu,Kwa kawaida watu woote walitakiwa kuwa kama Eldadi na Medadi ambao Roho aliendelea kuwa wakudumu katika maisha yao Tamaa ya Musa ya kutamani watu woote wawe Manabii ilitabiriwa na nabii Yoel katika Yoel 2;29-29 na kutimizwa siku ya Pentekoste katika Matendo 2;4,16

Roho Mtakatifu na ulinzi dhidi ya Israel Hesabu 22
     Wakati wa agano la kale sio tu Roho Mtakatifu alishughulika na Muwsa tu bali pia aliwashughulikia maadui wa Israel, Mfalme balaki wa Moabu  ni moja ya watu waliopambana na utendaji wa Roho Mtakatifu Israela walikuwa wanakuja kwa ushindi na tayari walikuwa wameshaishinda miji ya Gilead na bashani ng’ambo ya mashariki ya mto Yordani mfalme alipoona aina ya ushindi  aliogopa akitambua ya kuwa alikuwa akifuata katika kupoteza ufalme wake  na alifahamu kuwa Nguvu ya Israel ni ya Rohoni na si vinginevyo (Bwana alikuwa pamoja nao) na kwa jinsi hiyo basi alihitaji Bwana ageuke dhidi yao kama njia ya kuwapata israel na kuwashinda  alimtafuta mtu aliyeitwa Balaam ili awalaani na sio kuwabariki balaam alitoa sadaka nyingi kila kilima alipopokea baraka badala ya laana kwa Israel alihamia kilima kingine ili apate kibali kwa Bwana awalaani Israel Roho wa Mungu alimtumia Balaam kuwabariki Israel,Kwakweli  balaam alikuwa ni mpiga ramli tu na alikuwa nabii wa uongo au mchawi kwa lugha rahisi wachawi hao wa zamani waliamini kuwa wangeweza kumshawishi Mungu yoyote yule akubaliane  na matakwa yao lakini badala yake Mungu alimwamuru Balaamu awabariki Israel na kutoa unabii wa kweli Hesabu 22;21-35 Mungu alimshinda Balaam mchawi mashuhuri kwa Roho Makatifu
    Balaam alitabiri na unabii wake ulitoka kwa Roho Mtakatifu,Yeye alitabiri ushindi kwa Israel na alirudia kile alichotamkiwa Ibrahimu katika Mwanzo 12;3 na sehemu ya unabii wa balaamu ulimuhusu masihi Yesu Hesabu 24;17 kumbe Mungu aweza kutumia uovu katika kutimiza makusudi yake alimtumia Balaam mbabiloni Roho alimkalia kwa muda kwakuwa hakudumu ndani ya Balaam na kwa uroho na uchu wa mali alikufa kwa kuipinga kweli na kuwa kinyume na Israel.

Roho mtakatifu Juu ya Yoshua Hesabu 27;18;Kumbukumbu 34;9
     Yoshua huenda ndiye yule kijana nayetajwa kuwa alikuwa mtumishi wa Musa Hesabu 11;28 lakini inaonekana kuwa mahali fulani wakati wa mahangaiko ya jangwani yaliyochukua muda wa miaka 40 hivi alijazwa na Roho wa Mungu na hekima Kumbukumbu 34;9 Yeye alikuwa mtu ambaye Roho aliendelea kudumu ndani yake Hesabu 27;18 la muhimu zaidi inaonekana kuwa aliendelea kuwa mwenye kujaa Roho na aliyejifunza kumtegemea na hii ilipelekea kuchaguliwa kuwa kiongozi baadae, Roho wa Mungu alikuwajuu ya Yoshua mapema zaidi hata kabla ya Musa kumwekea mikono Hapa tunajifunza kuwa Roho wa Mungu hufanya kazi ya kuwaandaa watu kwa kzi za uongozi wa watu wake, Roho alikuwa ameanza kumuongoza Yoshua na kumfundisha  mapema kabla mtu yeyote hajajua kuwa Yoshua angekuja kuwa nani Mungu ni mwaminifu na si kusudio lake kuwaacha watu bila ya kuwa na uongozi

ROHO MTAKATIFU KATIKA HISTORIA YA ISRAEL.

Kuporomoka kwa Kiroho baada ya Yoshua

Ziko sababu kadhaa zilizopelekea kuporomoka kwa kiroho kwa taifa la Israel baada ya Yoshua
·         Woote tunajua kuwa Mungu aliwapigania Israel na kuwapa ushindi mkubwa kabla ya kifo cha Yoshua, Pia watu walikuwa wamemuahidi Yoshua kuwa wangemtumikia Mungu.
·         Mungu alikuwa amewaamuru Israel kuwaondoa wakanaani woote baada ya kuwa wamegawana inchi yote ya kanaani
·         Kabila ya Yuda waliwaondoa wakanaani woote walioishi katika inchi ya milimamilima lakini walishindwa kuwaondoa wote waliokuwa katika ukanda wa tambarale kwa sababu ya kutokuamini ,makabila mengine pia yalishindwa kuwaondoa wenyeji wote wa kanaani nje ya mipaka yao kwa sababu ya kutokutii ,
·         Israel walipopata nguvu eti waliamua kuwatoza kodi wakanaani badala ya kuwafukuzilia mbali hii ni kwa sababu ya Kupenda fedha na starehe, Baadhi ya makabila pia walishindwa kuwaondoa wakanaani woote nje ya mipaka yao Kushindwa kuwaondoa wakanaani
·         Waisrael wlishindwa pia kuzibomoa madhabahu za wakanaani waliokuwa na ibada mbaya sana za mabaali na maashera hii ni kwa sababu ya kupenda umaarufu wa kidunia.
·         Mafanikio yaliwaongoza katika kupenda starehe na ibada zikawa za kawaida, Kizazi kilichofuata kilipuuziwa hakikupata kabisa mafundisho ya kiroho wala hawakumjua Mungu kwa ajili yao wenyewe makuhani na viongozi walikuwa wamebebwa na desturi za kikanaani zaidi hawakuwa na ujuzi binafsi kuhusu Mungu wala hawakujua nguvu zake Kutokumjua Mungu, Walisikia miujiza aliyokuwa ameifanya zamani lakini hawakuona lolote kwa ajili yao wenyewe
·         Hatari hii ndiyo inayolikumba kanisa la leo kizazi kilichopita  kinaweza kukaa chini na kusimulia tu yale waliyoyaona wao katika utendaji wa Roho Mtakatifu na karama zake lakini hawawezi kuonyesha kivitendo ni namna gani kizazi kipya kinaweza kutembea na Mungu Kizazi kipya kinakuwa makanisani wakisikia tu jinsi watu walivyokuwa wakijazwa Roho Mtakatifu na miujiza iliyokuwa ikitendeka lakini hawavioni kivitendo katika maisha yao mapya Leo hii hata watoto wa maaskofu na wachungaji hawawajui Mungu wa Baba zao lakini Baba hao ni viongozi wa kiroho makanisani wakiwa ni viongozi wenye kuiba sadaka za watu na wenye mahubiri mengi kuhusu utoaji wakijilimbikizia posho kubwa wakiua wale wanaoonekana kuwa na vipawa na kuwa rohoni kuliko wao wamepoa na imebaki historia tu katika maisha yao na huduma zao huku wakiwa wamedumaa kiroho , hawakui wala hawaruhusu mafunuo ya kimungu katika mioyo yao, hivyo wamebaki na mapokeo na misimamo ya hovyo na isiyo ya kibiblia, Lazima tuamke na kuamua kuanza kufundisha kwa nguvu na kwa upya kumhusu Roho Mtakatifu na kufanya maombi na maombezi yatakayodhihirisha utendaji wake,

Roho Mtakatifu Juu ya Waamuzi katika Israel
     Mungu alichagua waamuzi kwa njia mbalimbali huku akiwajaza kwa roho wake Mtakatifu ili wafanye kazi za kutawala,kuhukumu na kuwaokoa wanapoonewa,Waamuzi walikuwa pia viongozi wa kimaadili,kisiasa na kiroho,Maisha ya kiroho wakati wa waamuzi yalikuwa kama jinsi tulivyoona hapo juu kulikuwa na mzunguko wa aina hii

     Mara nyingi walikuwa wakifanya dhambi na dhambi hizo zilisababisha Mungu kuruhusu mateso kutoka kwa maadui zao wakanaani, walipoteseka walikuwa wakihuzunika na kumlilia Mungu kwa toba huku wakihitaji msaada wake Yeye alituma waamuzi akiwajza kwa Roho mtaklatifu na waliwaokoa kisha walilala tena na kuanza kufanya dhambi, Ingawaje kitabu cha waamizi kinawaita waamuzi hao Mwokozi lakini mwokozi halisi alikuwa ni mungu mwenyewe Yeye aliwajaza waamuzi kwa Roho wake Mtakatifu na wakifanya kazi hiyo ya wokovu wote walichaguliwa na Mungu na walitumiwa katika njia za tofauti
·         Othiniel alileta ushindi kabla hajaitwa kuwa mwamuzi kama mtu alifanya jambo kwa imani na utii kwa Mungu alihesabika kuwa mtu waimani kabla ya ujazo wa Roho mtakatifu Kwa uwezo wa Roho mtakatifu  alitumiwa kuwaokoa kutoka kwa maadui zao wa mesopotamia au waaramu na kuwashinda Waamuzi 3;10
·         Debora alikuwa nabii mke na inasadikiwa ndiye aliyekuwa wakiroho zaidi ya waamuzi wote na aliitwa mwamuzi hata kabla hajaleta ushindi wowote wa kijeshi watu waliamini kuwa ana uhusiano na Mungu alijulikana kwa hekima ambayo mungu alikuwa amempa alipewa hekima hii na Roho Mtakatifu ili kuwasaidia watu kuwaongoza na kuwafariji na kuwapa changamoto kuacha tofauti zao
·         Gideoni Waamuzi  3;10,6;34 alitokea kabila ya manase na alitokea katika familia Muhimu sana Roho wa Mungu alimvaa au alimjaa Gideon na hivyo alizivunja madhabahu za baali na maashera na alipiga tarumbeta, alifuata maelekezo ya Mungu kuandaa jeshi kwa ajili ya vita hatua ambazo zilihitaji utii na alileta ushindi
·         Yephta alitumiwa pamoja na kuwa na makosa Waamuzi 3;10,11;29,32 Yeye hakuwa muhimu katika macho ya watu alidharauliwa na ulimwengu Mungu huweza kumtumia mtu bila kujali historia yake Roho alipomjia alimuongoza kwenda vitani kuwashughulikia maadui walikuwa ni wana waamoni waliokuwa wakiwatesa Israel Hata hivyo alishindwa kumtegemea Roho Mtakatifu akidhani kuwa ushindi wake ungekuja kutokana na nadhiri ya kijinga aliyoifanya  hata hivyo roho hakupuuzia nadhiri yake na ushindi ulipatikana  Roho wa mungu anapokuwa juu yetu huwa haingilii mapenzi yatu au matakwa yetu
·         Samsoni aliongozwa na Roho kufanya mambo ya ajabu Waamuzi 13-14,14;19,6 wazazi wake Samsono walikuwa wacha Mungu Mungu alimuandaa Samsoni kabla hajazaliwa ,Alizaliwa akiwa Mnadhiri wa mungu yaani mtu aliyeywekwa wakfu kwa ajili ya Mungu,Roho wa Mungu alianza kumtumia mapema katika maisha yake ,Ukweli kuwa mtu aliyekulia katika histiria ya uchaji wa Mungu sio uhakika wa kuwa hataweza kufanya mambo maovu au ya kibinafsi,Roho alikuwa alimtumia Samson kwa nguvu akimpa nguvu za kupambana na maadui,Kinyume cha hapo Samson huwa mwanadamu wa kawaida kabisa.Jambo la msingi tunaloweza kujifunza kwa Samsoni ni kuwa wanadhiri kwa ndani kujitoa kwa Mungu,kujiweka wakfu,na kuendelea kuwa na ushirika wa kudumu na Mungu Roho Mtakatifu 

Roho Mtakatifu Juu ya Manabii na Wafalme
     Manabii kama Samuel na wafalme kama Saul na Daudi nao walipakwa mafuta kwa uwezo wa Roho Mtakatifu wakati wao au wakati wa Samuel Hekalu huko shilo lilikuwa limebomolewa na wafilisti walikuwa ndio watawala wa wakuu katika inchi ,na sanduku la agano lilikuwa limetwaliwa, Samuel aliinuka kuwa nabii,Mwalimu,kuhani na muombezi,Manabii wakati mwingine walikuwa wanapakwa mafuta  1Wafalme 19;6,makuhani pia walikuwa wakipakwa mafuta suku zote kwa kazi hii  Kutoka 30;30,40;13-15 na Wafalme 30;23-34,Wafalme pia walikuwa wakipakwa mafuta kwa ajili ya shughuli za ufalme 1samuel 10;1,16;3,12, 1Falme 34,30;23-34 mafuta hayo yalikuwa ni mafuta maalumu  ya mizeituni yaliyotengenezwa kwa mchanganyiko maalumu Kutoka 30-23-34 na haikuruhusiwa kuyaigiza yalitumika pia kupaka vitu vilivyowekwa wakfu au vilivyotumika katika hema ya kukutania  yakiashiria kuweka wakfu kwa Bwana  na yaliwakilisha uwepo wa Roho Mtakatifu
·         Eli alimpaka mafuta Samuel mafuta haya yalikuwa na mchanganyiko maalumu nna ilikuwa ni Ishara ya uwepo wa Roho Mtakatifu mwenyewe na ni manabii,makuhani na wafalme waliopakwa mafuta hayo Mafuta ya kweli na halisi alikuwa ni Roho Mtakatifu na sio yale mafuta yaliyokuwa ni alama tu ya uwakilishi kwa Roho wa Mungu
·         Sauli na Daudi pia walipakwa mafuta,Daudi alipopakwa mafuta Roho wa Mungu alikuja juu yake mara moja kwa nguvu na kukaa ndani yake siku zote 1Samuel 16;13-14 lakini kwa Saul ilikuwa inakuja kwa muda tu Samuel 10;6

Roho Mbaya kutoka kwa Bwana ikaja juu ya sauli
     1Samuel 16;14 Biblia inasema, ..”Basi Roho ya Bwana ilikuwa imemwacha Sauli na roho mbaya kutoka kwa Bwana ikamsumbua.” .hapa kuna mijadala ya kitheolojia kuhusu roho mbaya kutoka wa Bwana
·         Wengine wanaamini ni ugonjwa wa kuweweseka ambao uliruhusiwa na Mungu
·         Wengine wanaamini ni Pepo kutoka kwa shetani ambaye alikuwa akimshambulia Sauli na kule kusema kutoka kwa Bwana maana yake ni kuwa Mungu aliruhusu hii ni kama ile shida iliyompata Ayubu ambayo Mungu alikuwa ameruhusu shetani kumshambulia Ayubu
·       Wengine huamini kuwa neno uovu hapa lilitumika kama hukumu yaani Mungu alituma Roho ya hukumu juu ya Sauli kwa ajili ya dhambi zake

ROHO MTAKATIFU; KATIKA MAANDIKO YA MANABII.

Roho Mtakatifu na Waandishi wa zaburi
     Tangu wakati wa Samuel na Daudi Muziki umeendelea kuwa sehemu muhimu katika ibada kwa watu wa Mungu roho Mtakatifu alikuwa muhimu kwa waimbaji pia zaburi 51;11 Mwimbaji huyu bila shaka ni daudi anaomba asiondolewe Roho Mtakatifu Huyu alielewa kuwa uwepo wa Mungu huendana na kuwepo kwa Roho Mtakatifu na namuomba Roho amlinde asikosee tena,Zaburi pia zinaonyesha kuwa Roho Mtakatifu yuko kila mahali anahitaji kutuongoza na kuhakikisha tunakua kiroho 

Roho Mtakatifu na maandiko ya Ayubu na Sulemani
     Ayubu anamuhesabu Roho Mtakatifu kama muumbaji wa Mbingu Ayubu 26;13, na anaamini kuwa uzima wake unatokana na kuwepo kwa Roho wa Mungu Ayubu 27;3 Elihum katika Ayubu aliamini kuwa Roho wa Mungu huwapa akili wanadamu Ayubu 32;8
    Suleimani pia anazungumzia habari ya kumwagwa kwa roho wa Mungu ili kuwajulisha watu maneno ya mungu Mithali 1;23

Roho wa Mungu katika kitabu cha Wafalme na Nyakati
A.           Manabii Karibu manabii wote waliongozwa na roho na walivuviwa na Roho Mtakatifu 1Petro 1;1-21, kulikuwa na uamsho wakati wa baadhi ya wafalme,manabii walikuwa wanenaji kwa niaba ya Mungu na waliweka msingi kwa ajili ya mambo yajayo manabii waliwatia moyo wafalme na kukemea ibada za sanamu  wao wanacghukua nafasi muhimu katika kitabu cha wafalme Mungu aliwaongoza kuzungumza kwa Roho wake
B.           Eliya na Elisha, wakati wa Ahabu na Yezebel mungu alimuinua Eliya na Ghafala alianza kufanya miujiza,Ahabu alikuwa mfale mwenye nguvu za kisiasa lakini alikuwa dhaifu kiroho, Yezebel bint wa kifalme alichochea na kuingiza ibada za Baal na kushawishi watyu kumuacha Mungu Kusudi la mungu kumuinua Eliya ilikuwa ili aweze kuwaleta watu katika uamuzi wa kumuabudu yeye na kumkataa baal Roho alimuongoza licha ya kuwa kulikuwa na hali za kukatishwa tamaa kwa muda.
     Elisha aliomba upako maradufu wa Roho mtakatifu yaani Roho yuleyule na nguvu zilezile 2Wafalme 2;9,utii wa Elisha na huduma yake kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ilisababisha kuitwa Mtu mtakatifu wa Mungu   2Wafalme 4;9 kazi kubwa ya Roho Mtakatifu kupitia manabii katika wafalme na nyakati ilikuwa ni kuleta uamsho mkubwa na ibada ya kweli ya Mungu

Roho Mtakatifu na maandiko ya manabii
     Yoel 2;28-32
 Alitabiriwa kuwa angemwagwa kwa wanadamu woote au kwa woote wenye mwili Mwanzo 6;12,13 Kumbukumbu 5;26 na Ayubu 12;10 Petro alionyesha wazi kutimia kwa andiko hilo siku ya Pentekoste matendo 2;16, ahadi hii inavunja mipaka ya ukabila na utaifa  inaondoa tofauti za miaka umri au jinsia  ”wana wenu na binti zenu” inavunja tamaduni utumwa na ubwana  na hivi ndivyo ilivyo leo si myahudi tu au myunani si weupe au weusi watu wote waweza kupokea Roho mtakatifu Roho mtakatifu pia huitwa mvua ya baadaye Yoel 2;23
   Mika 3;8
Mika alijazwa kwa nguvu za Roho mtakatifu na haki na ujasiri Mika 3;8 na hii ni moja ya maneno yaliyo wazi katika agano la kale yalioonyesha nini maana ya mtu kujazwa Roho Mtakatifu

Roho Mtakatifu juu ya Nabii Isaya
     Isaya aliishi kipindi kimoja sawa na Mika, wakati huu watu waliishi katika dhambi na kustarehe wito wa Isaya ulikuwa ni kuwaleta katika kustarehe na kumfurahia Roho Mtakatifu,Roho Mtakatifu alileta Moto sio kwa ajili ya uovu tu bali pia kuutangaza wakati wa kuja kwa masihi Isaya 4;3-5 Mungu aliwatumia waashuru kuwafundisha Israel kwamba alichokisema Isaya kilikuwa sahii

Roho Mtakatifu ni Roho wa Masihi
     Kazi za Roho Mtakatifu kumhusu Masihi zinaonekana ndani ya nabii Isaya,Yeye alitabiri kuwa Roho wa Mungu atakuwa juu ya Masihi Isaya 11;1-5,Ishara ya kuzaliwa kwa Immanuel kupitia Bikira Isaya 7;14,majina yote aliyoyataja Isaya  kumhusu masihi yalikuwa dhahiri katika maisha ya masihi Isaya 9;6-7,Isaya alitabiri kuwa Roho mtakatifu angetenda kazi kwa viwango vya juu ndani ya masihi Roho ya hekima namna ya kuitumia kweli katika maisha na kwa usahii,Roho ya ufahamu ujuzi katika mema na mabaya na kupambanua, Roho ya Ushauri yaani muongozo wa kimungu na hitimisho sahii,Roho ya nguvu yaani ujasiri na nguvu ya kutenda mapenzi ya Mungu,Roho ya maarifa ujuzi binafsi wa kujua mafunuo ya kiungu na kweli yake, Roho ya kumcha Mungu yaani kumuhofu kumuheshimu na kujitiisha katika ubwana wake, Roho ya Bwana kwa kzi ya ukombozi mamlaka kwa kusudi la kuishi na ya kuwa masihi hataweza kukosea katika utendaji wake.
     Isaya pia alimtabiri Masihi kama mtumishi wa mungu atakayeifanya kazi yake ,hii ni kwa sababu taif la Israel kama watumishi wake walishindwa kufanya kazi yake ingawaje wale wateule mabaki wachache walifanya kwa uaminifu na walitumika kuandaa njia kwa ajili ya masihi kama akina Simon Luka 2;28 Masihi mwenyewe alifanya kazi kwa ukamilifu wote  kwani kwa hakika amefanya kazi ya wokovu na ukombozi wa mwanadamu
     Isaya anamtaja Masihi kama Mpakwa mafuta Isaya 61;1-11,kuwa masihi angeleta dini ya kweli si kwa wayahudi tu bali kwa watu woote ulimwenguni,kama mtumishi wa Mungu Masihi angekuwa daraja kati ya Mungu bna wanadamu na mwenye kuleta agano jipya  Masihi angepakwa mafuta ili kuhubiri habari njema kwa masikini na kuwafungua wanaoteswa na kuwa masihi angekuja katika ukamilifu woote
     Isaya anamuona Roho Mtakatifu kama Roho wa Nguvu na maongozi Isaya 40;7-8 yeye ameweza kuifanya kazi hii huko nyuma sasa na wakati ujao alikaa juu ya msihi alipokuja kwa mara ya kwanza Roho anauwezo wa kuhukumu alimwezesha masihi kukabili kazi ya ukombozi kwa kustahimili mateso Roho huyu angetuongoza sisi katika kazi ya kuiponya mioyo iliyovunjika na kutoa ushindi dhidi ya dhambi na shetani,angeleta uponyaji, angetumwa kwetu na angemwagwa kwetu kama maji ya kuondoa kiu au mafuriko katika inchi liyo kavu au iliyokauka hizi ni kazi za Roho mtakatifu alizozitabiri Isaya



Roho Mtakatifu kama mkono wa Bwana wa nguvu katika Ezekiel
     Baadhi ya manabii walishindwa kumuelezea vizuri Roho Mtakatifu na wengine walishindwa kabisa  lakini hii haimaanishi kuwa hawakuwa chini ya uvuvio wake  Yeremia na Ezekiel wanafanana katika kumuelezea Roho mtakatifu  wao walitumia majina kama kidole au chanda cha Mungu,Mkono wa Bwana ,Roho wa Bwana ambavyo vyote vilimaanisha nguvu za utendaji wake
     Ezekiel kwa mtazamo wake Roho Mtakatifu ni wa Kujenga nasi wa machafuko Yeye kwanza anamuona Roho akiwa  pamoja na kerubi aliowaona katika maono Ezekiel 1;12,20,10;17 Ezekiel alipewa uelewa kuhusu utendaji wa Roho Mtakatifu katika uzoefu wake,Kusudi la Roho wa Mungu kuwa juu ya Ezekiel ilkuwa ni kumwezesha yeye awe na uwezo wa kuelewa jumbe atakazokuwa  akisikia kwa mungu kupitia Roho hii inatufundisha kuwa nabii anahitaji ujazo wa Roho mtakatifu kusudi aweze kupokea ujumbe kutoka kwa mungu na anamuhitaji zaidi katika kujua namna ya kuupeleka ujumbe huo.Aidha ezekiel ana muona Roho wa Mungu akihusika katika kuifanya upya Israel Ezekiel 36-37 hii inauhusiano wa kuirejeza Israel kiroho na hata kimwili pia,hagai na Zekaria pia waliziona kazi za mbele za Roho wa Mungu 

Roho wa nguvu na uweza na Roho wa Neema
     Roho wa Mungu kwa kweli ni Roho asiyebadilika  ndani ya kitabu cha Hagai anaonekana kuwa wa milele ni Mungu na habadiliki na kuwa anaendelea kufanya kazi na watu wake, Zekaria yeye anamuona kamaRoho wa nguvu na uweza na mwenye kutoa neema yaani upendeleo usiokoma Zekaria 4;6. Zerubabel alikuwa gavana wa Yuda na mjenzi wa hekalu wakati huu hakukuwa na vifaa wala uwezo wa kutosha wala watu wakutosha kufanikisha kazi hiyo Hakukuwa na pesa, watu na vitu vya ujenzi wala misaada lakini nabii aliwaambia si kwa nguvu wala si kwa uweza bali kwa Roho wangu mimi asema Bwana, Hii inatukumbusha kuwa mungu siku zote hufanya kazi Kwa Roho wake na kuwa kuwepo kwake ni zaidi ya fedha ,nguvu za watu na vifaa yeye ni zaidi ya yote

Roho Mtakatifu ni Mvua zile za vuli zijazo Hosea 6;3.
     Mvua za vuli zijazo ilikuwa ni ujio wa Roho kuanzia wakati wa Pentekoste ,Hosea 6;3 ni unabii kuwa Mungu angewajilia watu wake kama mvua hii ni mvua inayokuja kuandaa mavuno ya nafsi za wanadamu kupitia  kuhubiriwa kwa injili kupitia nguvu za Roho Mtakatifu kwa kawaida huko Israel wana majira katika maeneo manne kama ilivyo hapa Tanzania au Tanga wao wana Baridi-Kipupwe,Vuli-Mvua zijazo,kiangazi,Mvua kuu zile za zamani.

Uhusiano wa Roho Mtakatifu na Neno la Mungu
     Kama tulivyoona tangu awali kuwa kunauhusiano mkubwa wa Roho Mtakatifu na maandiko Agano la kale limetufundisha kuwa kuna uhusiano wa karibu sana kati ya neno la mungu na Roho wa Mungu,Manabii walitumika kama njia ya Roho wa mungu kutuletea neno lake,mafundisho ilikuwa ni huduma muhimu ya manabii na walikuwa wakitimiza njia ya Roho Mtakatifu kwani yeye ni mwalimu kila nafsi inayo mkaribia Roho wa mungu huonekana kulipenda neno la Mungu.

Somo la tatu.  ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA NA HUDUMA YA MASIHI

Roho Mtakatifu katika maisha ya Kristo

Utangulizi
      Kati ya miaka 400 hivi ya ukimya mpaka kuzaliwa kwa Kristo walikuiwepo masalia ya watu ambao walikuwa wakitembea au walikuwa wamejazwa kwa Roho Mtakatifu,alipozaliwa Yesu Kristo waliongozwa na Roho wa Mungu aliyekuwa juu yao kumtambua yeye kama aliyetumwa na Mungu kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu katika eneo hili tutakuwa tunaangalia kazi ya utendaji wa Roho mtakatifu katika kuzaliwa kwa Yesu na Kubatizwa kwake na huduma yake na pia tutajadili kuhusu dhambi ya kumkufuru Roho mtakatifu

Roho Mtakatifu na matarajio ya kuzaliwa kwa Masihi

A; Kuhusu Masalia
1.       Luka 1-2 zinaonyesha kuwa bado kulikuwa na masalia au watu waaminifu ambao walikuwa wakiendelea kuyashika mafundisho ya manabii.
2.       Miongoni mwao alikuweko Zekaria kuhani pamoja na mkewe Elizabeth wazazi wa Yohana mbatizaji wao ni mfano wa wacha Mungu Masalia
3.       Miongoni mwa watu wa kawaida sio kuhani alikuwako Simeon na Anna Bint fanuel wakiwakilisha wengi waliokuwa wakiutazamia ukombozi Luka 2;25 ukombozi huu pia uliitwa majina kama Faraja,Luka 2;25
4.       Makundi yoote haya yalikuwa yakiutazamia wokovu na kuhusishwa kwa unabii juu ya kuja kwa masihi hii ina maana ya kuwa Roho Mtakatifu alikuwa akifanya kazi  katika Israel ya kuandaa kuja kwa masihi na huduma yake

B; Wajibu wa Yohana mbatizaji.
1.       Yohana mbatizaji alikuwa ni kiungo muhimu kwa watakatifu wa agano la kale na agano jipya ingawaje alibaki kuwa mtu wa agano la kale na hakuingizwa katika mahusiano tuliyo nayo ya agano jipya
2.       Aliishi kama mnadhiri kuonyesha kuwa ni mtu aliyejitoa moja kwa moja kwa Mungu maisha yake yoote
3.       Aliongozwa na kufundishwa na kuandaliwa na Roho Mtakatifu katika maisha yake binafsi na ya huduma alijazwa kwa Roho Mtakatifu na alijazwa tangu tumboni, aliandaliwa kama atakayetangulia mbele za Bwana  na alikuja katika Roho na nguvu za Eliya alikuwa ni mrithi wa Eliya na manabii wote na inasemekana yeye ni zaidi ya nabii Mathayo 11;9-11 Yesu alimtambua kama Eliya ajaye Mathayo 17;10-13 na hii ilikuwa ni kutimizwa kwa unabii wa Malaki, Malaki 4;5-6
4.       Ingawa Yohana mwenyewe alisema yeye siye Eliya Yohana 1;21 alichomaanisha hapa kuwa siye Eliya yule mwenyewe ingawaje alikuja katika huduma ya Eliya Hivyo kile alichomaanisha Yesu kumhusu Yohana ni kuja katika Roho Nguvu na huduma ya Eliya na kutimiza unabii ule wa Malaki

C; Kuzaliwa na Bikira Kwa uwezo wa Roho Mtakatifu Luka 1;26-38.
1.       Ni Mathayo na Luka tu ndio wanaoelezea muujiza huu wa kuzaliwa Kwa Yesu Kristo kupitia Bikira
2.       Hii inathibitika pale Malaika Gabriel alipomwambia Mariam kuwa utazaa mwana naye ataitwa mwana wa aliye juu (Yaani mwana wa Mungu) na kuwa kwa yeye atakaa katika kiti cha enzi cha Daudi baba yake  alijiuliza swali kuwa ingewezekanaje huku yeye hajui mume
3.       Malaika alimwambia kuwa Roho Mtakatifu atakujilia juu yako kwa nguvu na nguvu zake aliyejuu zitakufunika kama kivuli kwa hivyo kitakachozaliwa kitaitwa Mwana wa Mungu Luka 1;35 Mathayo 1;21 pia inathibitisha kuwa malaika alimwambia Yusufu  kuwa mimba ya Mariam ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu

D: Fundisho kuhusu kufunikwa kama kivuli
a.       Historia inaonyesha kuwa uwepo wa Mungu  kama wingu ulimfunika Musa  katika mlima wa sinai na pia ulikuwa ukionekana katika hema Kutoka 24;18,40;34-35
b.       Pia inakumbusha wakati wa uumbaji Roho alivyokuwa ametulia juu ya uso wa maji Mwanzo 1;2 ingawa hapa haimaanishi kuwa Yesu alikuwa anaumbwa pia haimaanishi kuwa Roho alifanya tendo la ndoa na Mariam Roho alikuwa akifanya muujiza wa uwezekano wa Bikira kushika mimba bila mbegu ya kibinadamu ya kiume kuhusika Hivyo Yesu kuzaliwa na bikira ni Muujiza kabisa.

E: Roho Mtakatifu ndani ya Masihi
Kwa ujumla tunaweza kusema kuwa Roho Mtakatifu ameunganishwa na huduma na ujio wa Yesu Kristo, Hivyo kuna uhusiano mkubwa sana kati ya maisha yake yoote na matukio yake yoote katika kila sehemu ya huduma na maisha yake
·        
            Alihaidiwa kwa Masihi
     Agano la kale na manabii wote walitabiri kuhusu ujio wa masihi na pia kuhusu Roho Mtakatifu kuwa juu ya masihi Isaya 11;1-2,42;1 na 61;1 na unabii huu wa Isaya ulitimizwa kwa maneno tunayoyasoma katika Luka 4;18 na Yohana 7;37-39

·         Alihudumu pamoja na Masihi
     Baada ya Yesu kupakwa mafuta na Roho wa Mungu kuwa juu yake aliongozwa katika huduma na Roho akiwa na umri wa miaka kama 30 Isaya 61;1,Luka 4;18-19 Matendo 10;38 Roho alihusika katika huduma na utendaji mzima wa Kristo ikiwemo miujiza ambayo yoote aliifanya kwa uwezo wa Roho Mathayo 12;28 Matendo 10;38

·         Roho Mtakatifu wakati wa Mateso
     Kama jnisi alivyomuongoza kuelekea jangwani ili ajaribiwe Roho wa Mungu alimtia Nguvu Yesu kukubali kukabiliana na  kukubali kujitoa katika maisha ya Mateso na aibu ya msalabani Waebrania 9;14
·         Roho Mtakatifu wakati wa Kufufuka kwa Masihi
     Yesu alifufuliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu Waefeso 1;19-24,1Petro 3;18 Hata pale msalabani Yesu alitiwa nguvu kuvumilia mateso yale lakini sio kuwa asisikie maumivu bali aweze kukubali kuyatimiza mapenzi ya Mungu katika hali ya maumivu Warumi 1;4,8;11

·         Uhusiano wa kupaa na kushuka kwa Roho Mtakatifu
    Kristo alipopaa ndipo aliporuhusu kushuka kwa Roho Mtakatifu kwa watu woote hivyo ilikuwa ni lazima Yesu aende ili Roho aje na ujio wa Roho Mtakatifu ni uthibitisho wazi wa kuwa Yesu alipaa mbinguni Yohana 1;32-33.

F: Fundisho la Roho na Moto

1)       Maoni tofauti kuhusu Kubatizwa kwa Moto.

     Yohana Mbatizaji alitabiri kuwa Yesu angebatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto Mathayo 3;11, Luka 3;16 na ni Mathayo na Luka tu walioandika kuhusu swala hili
Wahubiri wa ki Holiness waluiohubiri katika karne ya 19; walipanua ahadi hii kwa kufundisha kuwa ni swala linalohusiana na Moto wa kiroho utakao teketeza dhambi kabisa hivyo waamini walitakiwa kuomba ubatizo wa moto kwa ajili ya utakaso au ubatizo wa pendo liwakalo au ubatizo wa moto
(a)     Baadhi ya wanatheolojia hutofautisha kati ya Ubatizo wa moto na ule wa Roho
(b)     Wengine huona ni ubatizo wa  eneo fulani wa Roho Mtakatifu.
(c)     Wengine hawaoni kuwa kuna tofauti  wanaamini kuwa maneno ya Yohana ilikuwa ni kutangaza tu  kama atawabatiza kwa moto wa Roho Mtakatifu
(d)     Je wasomi wa leo wanasemaje?;-
§  Ni ndimi za moto kama zile za siku ya Pentekoste ikimaanisha ni wivu mtakatifu uliowahakikishia kuwa mitume wana moto kwa ajili ya Mungu
§  Kwakuwa kuna maandiko mengine katika Mathayo 3;11,12 moto huu humaanisha moto wa hukumu yaani huduma ya Roho Mtakatifu ya kuhukumu na kuzichoma dhambi
§  Dr. Henry H. Ness alichangia kuwa kile ambacho moto hufanya katika hali ya asili ndicho  Roho Mtakatifu hukifanya katika ulimwengu wa roho anaangaza,anasafisha na ana nguvu kila tukio la asili moto ufanyacho ndicho Roho hukifanya
§  Elder Cumming alisema ubatizo kwa moto ni aina za majaribu tunayopitia ambayo Mungu huyaruhusu kwa watu wake.
§  Frank M. Boyd alisema kuwa ubatizo wa Roho na  wa moto sio vitu viwili tofauti lakini ule wa Roho ni halisi na ule wa moto ni ishara.
§  Dr. Walbod yeye alisema maandiko yaliunganisha kile angefanya Yesu wakati wa kuanza kwa kanisa na huduma yake  wakati wa utawala wa miaka 1000 kwamba kuanza kwa kanisa kulitokea kwa ujio wa Roho Mtakatifu na kuanza kwa utawala wa miaka 1000 kutatanguliwa na umwagiko wa moto wa hukumu juu ya mpinga kristo na majeshi yake wakati wa vita vya Harmaggedon 1Thesalonike 1;7-8 Yohana kama nabii aliviona kwa pamoja ubatizo wa Roho na wa moto
§  Dr, Stanley M. Horton yeye alisema Yohana alishindwa kutofautisha  kati ya ubatizo wa Roho Mtakatifu na ule wa Moto lakini Bwana Yesu alivibainisha wazi aliwaambia wanafunzi wake katika Matendo 1;3-5 mtabatizwa katika Roho baada ya siku hizi chache hakutaja moto,hii ilimaanisha ubatizo ule wa Roho uliotokea kuanzia siku ya Pentekoste lakini kwa habari ya ule wa moto utakuwa mwishoni kama Paulo alivyoeleza katika 2Thesalonike 1;7-8 ambapo inazungumzia hukumu
§  Kwa msingi huo basi kuna ukweli katika maelezo ya Dr Walbod na Dr.Horton kwamba ubatizo wa Roho na wa Moto ni nyanja mbili tofauti,Yohana hakutofautisha kati ya ujio wa Yesu mara ya kwanza na ujio wa Yesu mara ya pili,Ingawaje Yesu mwenyewe alitofautisha kati ya ujio wa Roho mara ya kwanza na ule wa mara ya pili wa hukumu na hivyo aliusema wazi hakuja kuleta moto wa hukumu katika ujio wake wa kwanza Yohana 3;17



                   Kielelezo  kinaonyesha Yohana aliona nyakati hizi mbili kama wakati mmoja tu

Kusudi la Ubatizo wa moto
Ø  Kuonyesha hukumu ya Moto usiozimika
Ø  Yesu mwenyewe aliuzungumzia ubatizo wa Roho Mtakatifu kama Nguvu kwa ajili ya utumishi na si sana  kuhusu utakaso na usafishaji Matendo 1;8
Ø  Utakaso unahusu kujiweka wakfu na kujitoa kwa Mungu na mapenzi yake  kwa hivyo kupitia kujitoa na kuishi kwa nidhamu na kuendelea kuwa na ushirika na Roho Mtakatifu na kulitumia neno la Mungu.

Roho Mtakatifu akiwa na Umbo kama njiwa
          Ni muhimu kujadili pia kuhusu kushuka kwa Roho Mtakatifu wakati wa ubatizo wa Bwana Yesu na utambulisho wa Mungu Baba kuwa huyu ni mwanangu Mpendwa nimependezwa naye na jinsi Kristo alivyojifanya mwanadamu  hili Tendo lilikuwa na maana gani?

A; Kumtambulisha Mbatizaji
1.       Roho Mtakatifu kushuka akiwa na umbo kama la njiwa ilikuwa ni Ishara kwa Yohana Mbatizaji kwamba Yesu atakuwa  ndiye yule anayebatiza Kwa Roho Mtakatifu na hii ilikuwa ni kutimia kwa unabii katika Isaya 11;2,42;1 na 61;1.
2.       Roho Mtakatifu alishuka wakati Yesu alipokuwa anaomba alipokuwa amepanda kutoka majini hii inatufundisha kuwa Maombi na sifa humfanya Roho wa Mungu kushuka juu ya waamini Luka 24;53,Matendo 1;14

3.       Ubatizo wa maji hapa ulitofautiana na ule wa kuja kwa Roho Mtakatifu hii inamaanisha kuwa ubatizo wa maji hauna muungano wa moja kwa moja na ubatizo wa Roho Mtakatifu  ingawaje huwa inatokea watu kujazwa Roho wakiwa wanabatizwa ubatizo wa maji.
4.       Yohana Mbatizaji hakuhitaji ubatizo wa Roho mbele ya Yesu  alihitaji kubatizwa kwa maji kwani alikuwa ametembea na Roho Mtakatifu na amekuwa akiongozwa naye tangu utoto hivyo kupitia Roho wa Mungu pia alihubiri akiwataka watu watubu Tendo la Roho kushuka akiwa na umbo kama njiwa huenda liliruhusiwa kwa Yohana mbatizaji pekee na sauti ile kutoka Mbinguni ilikuwa ni tangazo la kuonyesha kuanza kwa huduma ya Masihi
5.       Mungu alikuwa analiona Tendo hilo kuwa ni kutii kwake Yesu Kristo kujitambulisha kama mwanadamu na pia kuwa tayari kwa huduma ya ukombozi na kuukabili msalaba

B; Kujitambulisha na wanadamu
1.       Tendo la kubatizwa kwa maji kwa Yesu Kristo lilikuwa kama la kujifananisha na wanadamu
2.       Shetani alipomjaribu ili ageuze mawe kuwa mkate Yesu alikataa kwani angekubali tendo hilo lingekuwa kama amekataa kujifananisha nasi
§  Angefanya mawe kuwa mkate ingekuwa rahisi kwake kuendelea kutumia asili yake ya kiungu kutoka katika asili ya kibinadamu ya kusikia njaa, maumivu, n.k.na hivyo hata maumivu ya msalaba hayangeweza kuwa halisi.
§  Aliamua kabisa kuchukua nafasi yake kama mwanadamu ili kwamba aweze kuteseka na njaa na hisia nyingine za kiibinadamu ili aweze kuchukuliana nasi Waebrania 4;15.
§  Yesu kama Mungu mwanadamu alihitaji Roho Mtakatifu amuongoze katika huduma kwa wanadamu na kujitambulisha kama anayebatiza kwa Roho Mtakatifu.

C; Kuongozwa na Roho Mtakatifu Mathayo 4;1,Luka 4;1
1.       Kwa kukubali kuwa mwanadamu Yesu alijiweka katika utii kwa uongozi wa Roho Mtakatifu na hivyo alijaa Roho Mtakatifu kuandaliwa kwa ajili ya huduma na kumuwezesha kuifanya kazi ya Mungu.
2.       Hivyo aliongozwa kwanza Nyikani apate kujaribiwa na Ibilisi, alikuwa amejaa Roho  na hivyo alifunga siku arobaini 40, hakutumia nguvu yake ya kiungu kushinda majaribu alitumia kile ambacho sisi tunacho silaha zilezile  Neno la Mungu, Upako wa Roho Mtakatifu, ni silaha ambazo ziko na kuwa hata sisi tunaweza kuzitumia.
3.       Yesu alimshinda Shetani kwa ujumla katika maeneo yaleyale ambayo Eva alijaribiwa katika Bustani ya Eden


Aina ya Jaribu

Muhusika
Adamu na Eva
Yesu
Mahali pa jaribu
Bustani ya Edeni
Jangwani
Alikuwa na nani ?
Walikuwa na Mungu
Pekee akiongozwa na Roho
Aina ya jaribu
Tamaa ya mwili
Tamaa ya mwili

Tamaa ya macho
Tamaa ya macho

Kiburi cha uzima
Kiburi cha uzima
Matokeo
Anguko
Aliushinda ulimwengu




4.       Ushindi wa Yesu unatuonyesha njia ya sisi kuwa na ushindi dhidi ya ulimwengu na dhambi
5.       Yesu aliendelea kuongozwa na Roho Mtakatifu na alikwenda Galilaya  Luka 4;14
6.       Majaribu makuu ya watumishi wa Mungu ni pamoja na Zinaa, Kupenda pesa, Kiburi na vyeo au umaarufu, kukatishwa tamaa, kujihurumia na kutokuamini pamoja na ubinafsi.

D; Kuhudumu katika nguvu za Roho Mtakatifu
     Karibu katika maeneo yote Yesu alihudumu katika nguvu za Roho Mtakatifu katika eneo hili tutakuwa tukiangalia maeneo mbalimbali ya maisha ya utumishi wa Yesu Kristo katika uweza wa Roho Mtakatifu.

1.       Roho Mtakatifu na huduma ya Kufundisha na uponyaji.
§  Huduma yote ya Yesu Kristo ilimtegemea Roho Mtakatifu na inaonyesha ukamilifu wa ushirikiano kati ya Baba mwana na Roho.
§  Nguvu hii ilijidhihirisha kwanza katika mafundisho yake huko Galilaya  watu walihisi mamlaka ya kupita kawaida  na lilikuwa na uwezo Luka 4;31
§  Yeye mwenyewe alitangaza wazi kuwa Roho wa Bwana alikuwa juu yake hii ilikuwa ni kutimiza unabii katika Isaya 61;1-2,angalia Luka 4;18-21.
§  Injili ya Mathayo inaonyesha kuwa huduma ya uponyaji pia ndani ya Yesu Kristo ilikuwa ni kutimiza unabii ya kuwa Roho wa Mungu alikuwa juu ya mtumishi wake Yesu Kristo Mathayo 12;15  hii ni kutimiza unabii katika Isaya 42;4

2.       Kufurahi katika Roho Mtakatifu Luka 10;20
§  Furaha iliyokuwa juu ya Yesu Kristo ilikuwa furaha ya Roho Mtakatifu aliyekuwa naye siku zote, alifurahi katika Roho pia pale alipoona kazi ya Mungu ndani ya wanafunzi wake 70 aliowatuma kuhubiri na kuponya wagonjwa, walikuwa watu wa kawaida lakini walifanya miujiza mikubwa  na jinsi Mungu alivyowapa nguvu ya kutoa pepo
§  Siri ya furaha aliyokuwa nayo Yesu ni matarajio yake ya baadaye ya ushindi mkubwa utakaopatikana dhidi ya shetani kupitia kazi za Roho Mtakatifu juu ya waamini
§  Hii ina maana ya kuwa Roho Mtakatifu ni furaha yetu kuu na chanzo kikuu cha furaha ya wanaoamini.

E; DHAMBI YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU
       Chanzo kikubwa cha kuweko kwa mjadala kuhusu dhambi ya kukumkufuru Roho Mtakatifu kilichangiwa na changamoto kuhusu Nguvu inayofanya kazi ndani ya Yesu Kristo Mathayo12;21;32, Marko 3;22-30, Luka 11;15-20;12;30 tangu wakati huu kumekuweko na maoni mbalimbali kuhusu dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu

A; Maoni mbalimbali kuhusu dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu
·         Bieder Wolf – aliamini kuwa hii ni dhambi ya kudhalilisha inayoweza kufanywa na wale ambao wamemjua na wamewahi kujazwa kwa Roho Mtakatifu hawa ni wale ambao wamekionja kipawa cha mbinguni, karama neno na nguvu za zamani zijazo kisha wakarudi nyuma kwa kukengeuka Waebrania 6;4-6,10;29.
·         Wanaoamini katika dhana hii wanaamini kuwa dhambi ya kumkufuru Roho inaweza kufanywa na watu wale walio na ujuzi kuhusu Mungu kwani hao ndio wanaoweza kukengeuka
·         Jerome na Chrysostom (mtafasiri wa Biblia iitwayo Vulgate na muhubiri mashuhuri) waliamini kuwa watu wasiomjua Mungu pia au ambao hawajaokolewa na wakafanya sawa na mafarisayo walivyofanya hapa wanaweza pia kufanya dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu ambayo haisameheki, wengine wanaamini kuwa iliwezekana kuifanya dhambi hii pale tu Yesu alipokuwa duniani basi, yaani kwamba njia ya kumkufuru Roho ilikuwa ni lazima umkabili Yesu tu na kumkashifu kuwa miujiza anayoifanya ni kwa uwezo wa ibilisi
·         John Weslay Mwanzilishi wa Kanisa la Methodist alisema njia pekee ya kumkufuru Roho Mtakatifu au dhambi isiyosameheka ni kuisingizia miujiza ya Kristo kuwa ni ya shetani
·         John Broadus (Professor wa Southern Baptist seminary) alikuwa na maoni haya kwamba dhambi ya kumkufuru Roho inaweza kufanywa na wale wanaosema miujiza inayofanywa kwa nguvu za Roho Mtakatifu inafanywa na shetani na aliamini pia kwa kuwa maswala ya miujiza yalikwishapita yaani ni ya wakati wa Yesu na Mitume tu dhambi hiyo haiwezi kufanyika tena
·         Msomi wa Kijerumani aitwae Frant Delitzsch alikuwa na maoni yafuatayo kuhusu  Kumkufuru Roho Mtakatifu haikuhusiana na neno la kumkufuru pekee au tendo la mtu kukufuru na kupinga lakini linachukuliwa pamoja na mkao wa fikra wenye ugumu unaojifunua ndani ya mtu ambao uanjenga dhambi isiyosameheka`
·         Maoni yangu Kama Mchungaji Innocent Kamote  mwandishi  na mwalimu wa somo hili ni kuwa Roho Mtakatifu ni njia inayompelekea mtu kuzaliwa mara ya pili na kuokolewa lakini si hivyo tu yeye humshawishi hata mtu aliyeokoka kama amefanya dhambi afikie toba na katika majukumu ya kimungu ya Utatu hii ni kazi ya Roho Mtakatifu hivyo basi tukio lolote lile liwe la kukashifu miujiza yake ama vinginevyo lakini likafikia kwenye kiwango cha kumfanya aache kazi ya kukufanya utubu hautakuwa na jinsi nyingine yoyote inayoweza kukufanya upate neema ya kutubu na kwa jinsi hiyo umemkufuru Roho Mtakatifu au umefikia katika mstari ambao anaujua yeye Roho kuwa haustahili tena kupata Msamaha na ni vigumu kujua mtu aliyekataliwa ila Mungu tu hujua lakini dalili ni kuendelea kuwa na ukaidi dhidi ya wito wa toba na kazi zote za Roho Mtakatifu kwani hufanya miujiza kusudi tumwamini tuokolewe au tuimarishwe,au tuendelee katika neema yake. 

Tafasiri Nyingine kuhusu dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu
·         Kumkufuru Roho hujumuisha swala zima la kumkataa kwa kwa hiyari kabisa
·         Wale ambao Yesu aliwaonya walikuwa katika hali ya kujaribu kuwazuia watu wasimuamini Yesu na kuwa waachane nae
·         Hii ni jamii ya watu wanaotukuza matendo ya kishirikina kuliko ya Mungu akili zao ziko katika muelekeo wa kuona kuwa kila kitu ni cha kishetani tu
·         Ni hali ya kukataa kabisa kwa kukengeuka na kumkataa Yesu na kanisa
·         Kama mtu anajisikia kushawishika, kuvutiwa kijhusisha, hamu, kuchangamkia, kukubaliana  na kufurahia jambo lolote la kiroho basi kwake huyo kuna matumaini hajamkufuru Roho.
·         Hukumu kamili kama mtu amemkufuru Roho au la ukweli unabaki kuwa Mungu pekee ndiye ajuaye jambo hilo na sio mwanadamu wa aina yeyote

Onyo lililo kali
·         Sababu ya kutolewa kwa maonyo makali sana kuhusu kumkufuru Roho Mtakatifu  ni pamoja na mzingira yafuatayo;-
Ø  Maadui wa Yesu Kristo walisema Yesu ana Pepo mchafu hawa walikuwa ni mafarisayo na walisema kuwa Yesu anatoa pepo kwa Mkuu wa Pepo yaani kwa nguvu za shetani
Ø  Kwa ujumla hawa walikuja Yerusalem wakiwa na lengo na makusudi ya kumdhalilisha Yesu kwa hivyo kwa makusudi kabisa walikuwa wakiupindisha ukweli na kudanganya kuhusu kile ambacho Yesu alichokuwa akifanya kwa wivu
Ø  Yesu alionya kuwa kufuru dhidi yake au Baba yake ingesamehewa lakini sivyo ilivyo kwa Roho Mtakatifu Yesu alikuwa akifundisha kuhusu  chanzo cha nguvu za utendaji wa Mungu
§  Yesu alikuwa akionyesha kuwa ni kitu kisichoweza kufikirika kuwa Shatani anawafukuza mashetani wenzake Shetani akimtoa shetani?
§  Yesu alikuwa akiweka bayana kwamba alikuwa akitoa pepo kwa Roho Mtakatifu
§  Yesu kwa mujibu wa injili ya  Luka  alikuwa akitumia chanda cha Mungu  kuwasilisha nguvu za Mungu ambazo kwa hizo alikuwa akitoa Pepo
§  Na kuwa kwa nguvu hizo alikuwa akifunua kuwa ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia  na uponyaji ni moja ya manufaa ya ufalme huo.

Maoni ya mwalimu wa somo;
§  Roho Mtakatifu ni mjumbe wa Mungu kwa wanadamu  kuwashawishi kwa habari ya dhambi haki na hukumu ili waikubali kweli ya Mungu Yohana 16;8-11 Hivyo mwanadamu anapoendelea kumpinga Roho mtakatifu kuanzia na jumbe zake, muijiza yake, neno la Mungu na hata vitabu vya kiroho na kwa hivyo anafunga mlango unaoweza kumuongoza yeye katika toba na hivyo kukosa msamaa wa Mungu.

          ROHO MTAKATIFU NA HUDUMA YA MAFUNDISHO YA YESU KRISTO
Kwa jumla katika eneo hili tunaangalia kile ambacho Yesu Kristo mwenyewe alikifundisha kumhusu Roho Mtakatifu mengi ya mafundisho hayo yamo katika injili ya Yohana na mengi yalielekezwa kwa wanafunzi wake
A; Mtoaji wa karama ya Roho.Luka 11;13 kwa nini tuombe kwa akjili ya karama ya Roho Mtakatifu
§  Kiini kikuuu mafundisho ya Yesu
Ø  Yesu alitambua kazi za uvuvio wa Roho Mtakatifu katika agano la kale Marko 12;36 Mathayo 13;Luka 20; 42 pamoja na kusudio zima la utendaji wa Roho Mtakatifu kuhusiana na masihi
Ø  Alitambua kuwa Roho Mtakatifu ni zawadi ya Mungu na kuwa ni ufunguo wa yote aliyo nayo Mungu  kwa ajili yetu Mathayo 7;7-11, Luka 11;9-13.
Ø  Kwamba Roho angekuwa pamoja nao akiwasaidia katika huduma kwa kuwapaka mafuta hata katikati ya mateso Mathayo 10;16-20; Marko 13;9-11,Luka 12;11,12;12-15.
Ø  Aliwaamuru kuwabatiza waamini kwa jina la Baba na mwana na Roho Mtakatifu Mathayo 28;19
Ø  Aliwaamuru kusubiri Yerusalem mpaka wamevikwa uwezo utokao juu  Luka 24;49 nguvu za Roho zingekuwa juu yao  kuwafanya mashahidi Matendo 1;8.
Ø  Aliwapa mfano wa wanawali kumi Mathayo 25;3-4,8 ambao huchukuliwa kuwa ni mfano wa kuwepo kwa utendaji wa Roho Mtakatifu katika moyo wa mwamini
Ø  Yesu alifundisha kuwa waamini wanapaswa kumuomba Mungu kwa imani kuhitaji Roho Mtakatifu alisema kama baba wa duniani wanaweza kuwapa watoto wao vitu vyema ingawa wao ni waovu je Baba wa mbinguni hatatupa Roho Mtakatifu sisi tumuombae Roho Mtakatifu ni zawadi nzuri hivyo hata kama tumejazwa tunapaswa kuendelea kuomba ujazo wa Roho Mtakatifu
Ø  Kwa kufanya hivyo tunainyesha kiu na shauku tuliyonayo kumhusu Roho mfano mzuri ni jinsi wale 120 walivyoomba hata wakapewa Roho Mtakatifu siku ya pentekoste



Chanzo cha mto wa Jordani kilichopo huko kaisaria filipi mahali ambapo Petro alikiri kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu Mathayo16;13 na Kristo kuhaidi kuwa juu ya ukiri huo atalijenga kanisa lake chanzo hiki kichokauka ni mfano tosha wa kuendelea kutiririka kwa Roho wa Mungu kwa wote wamtakao katika Picha na maelezo kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote

WANAFUNZI WATUMWA KWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU

§  Kuwa pamoja nao katika huduma Mathayo 10;19-20
*      Yesu aliwaonya wanafunzi kuwa wasifikiri kuwa kila mtu atawapokea tu na kuikubali injili hata pamoja na nguvu kubwa ambayo kwayo injili inahubiriwa ni lazima watarajie vikwazo, kufungwa magerezani, kupigwa, kudhrauliwa na kupelekwa mahakamani na mbele ya wafalme na maliwali  lakini pamoja na hayo Yesu aliwaahidia ushindi
*      Kama wakristo ni lazima tumtegemee Roho Mtakatifu hata tuakapopelekwa mabarazani kwa ajili ya imani yetu Yeye atatupa hekima na maneno ya kusema kufanya kila jambo kwa ushuhuda wake na si kwa ajili ya kujitetea
*      Kitabu cha matendo ya mitume kimejaa mifano inayoonyesha mitume walivyoweza katika Matendo 3
Ø  Walitoa ushuhuda wa kuuawa kwake Yesu Kristo na kufufuka wala hawakuwa wamejiandaa
Ø  Roho aliwapa lile lililokuwa muhimu kwao kulizungumza maneno na hekima wapinzani na washitaki hawakuweza kupata cha kuwapinga
Ø  Bwana wakati mwingine aliwaokoa na wakati mwingine aliwaacha waifie imani Bwana alikuwa pamoja nao katika huduma na mateso waliyokutana nayo

§  Wanafunzi walitumwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu
*      Agizo kuu liliambatana na kujazwa kwa nguvu za Roho Mtakatifu Mathayo 28;18-20, Matendo 1;8
*      Kusudi la msingi la nguvu hizi ni kufundisha na kufanya wanafunzi ambao wangependa kujifunza zaidi kumhusu Yesu na neno la Mungu
*      Ili ishara na miujiza ifuatane nao na injili hii ilipaswa kuhubiriwa kwa kila kiumbe na hususani jamii za watu ulimwenguni zilizo kataliwa Marko 16;20
*      Uamsho mkubwa wa kipentekoste unasambaa duniani pale watu wa kawaida wanapokubali kuchukua jukumu la kuihubiri injili kwa wengine.

Mchanganuo kuhusu kuzaliwa kwa maji na kwa Roho Yohana 3;5
·         Kuzaliwa kwa maji
Kuna maana karibu nne zinazozungumzia kuhusu kuzaliwa kwa maji
1.       Ubatizo wa maji
a.       Wako baadhi ya wana theolojia wa kisakrament wanaoamini kuwa ubatizo wa maji ni wa muhimu sana kwa wokovu na  kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu
b.       Mafundisho ya kibiblia
Ubatizo wa maji ni ishara ya ya ushuhuda wa nje wa maisha mapya ambayo tayari mtu ameshayapokea na hii ni sawa na ubatizo wa Yohana haukuwa unaleta toba bali ulikuwa unathibitisha toba.
c.       Chanzo halisi cha maisha ya kiroho ni Roho Mtakatifu
2.       Maoni ya kuzaliwa kwa asili (maji ya wakati wa kuzaliwa).
a.       Wanaounga mkono maoni haya wanadai kuwa maji yanawakilisha kule kuzaliwa kwa kwanza kwa kawaida au kwa asili natural birth ambako kwa kawaida hutanguliwa na kumwagika kwa maji wakati wa uchungu
b.       Mtazamo sahii
Mawazo ya watu hawa yana pingana na mtazamo wa injili ya Yohana kwa kuunganisha kuzaliwa kiroho na kuzaliwa kwa asili maandiko kwa asili yake yanaonyesha kutokuunganisha kuzaliwa kwa pili na kuzaliwa kwa asili kuzaliwa mara ya pili ni kazi kamili ya Mungu  kwa hivyo kuzaliwa kwa maji na kwa Roho vyote vinahusisha kile kinachotoka kwa Mungu
3.       Maoni kuhusu kuzaliwa kwa Neno
a.       Katika maoni haya inachukuliwa kuwa kuzaliwa kwa maji ni kuzaliwa kwa neno Efeso 5;26 hii inawezekana kwa sababu biblia inazungumzia uwezekano wa kuzaliwa kwa neno 1Petro 1;23,25, Yoha 1;18,15;13 Biblia inaushahidi kuwa maeneo mengi Roho ametumia neno kuwaleta watu katika wokovu.Rumi 10;8,14.
·         Kuzaliwa kwa Roho
Hii ni kazi ya Roho mtakatifu pekee yeye ndiye anayesababisha watu kuzaliwa mara ya pili Yohana 6;63 yeye pia ni mtoa uzima 2 Koritho 3;6 .Kuzaliwa mara ya pili ni  kazi ya Roho mtakatifu katika kutufanya upya ni yeye anayepanda mbegu isiyoharibika  katika mioyo ya wanadamu 1Petro 1;23 anapolitumia neno kama mbegu katika moyo  husababisha toba inayoleta wokovu kwa imani na ni yeye anayewaandika watu kwa Kristo 1 Korotho 12;13.

·         Kuishi kwa Roho Yohana 7;37-39,4;10,14.
*      Maji ya uzima Yohana 4;10-14 Maji ya asili.
1.       Yesu alitoa maji ya uzima kwa mwanamke msamaria badala ya maji ya asili kutoka katika kisima kirefu pale kijijini
2.       Maji hayo anayotoa Yesu mtu Yeyote anywae maji hayo hataona kiu tena maji hayao ni wokovu Yesu hutoa na huweza kukupa uzima wa milele
3.       Katika mistari hii maji huwakilisha wokovu na uzima wa milele ambayo ndiyo pekee yanaweza kuleta pumziko na amani na usalama wa maisha haya na maisha yajayo
*      Mito ya maji ya uzima Yohana 37-39
1.       Sikukuu ya vibanda ilikuwa ni kwa ajili ya ukumbusho wa miaka 40 ya masumbufu ya jangwani kwa wana wa Israel,ilikuwa ikiwakumbusha kuwa wanapaswa kumtegemea Mungu kama baba zao  katika siku ambazo Mungu aliwalisha kwa manna kutoka mbinguni na kuwapa  maji kutoka katika mwamba
2.       Kwa mujibu wa tamaduni za siku zao  inasemekana kuwa siku ya mwisho ya sikuu ya majuma wakati wa sikukuu ya vibanda kuhani wa zamu huruhusu maji kutoka katika kisima cha siloamu na kuyamwagia ndani ya ua wa  hekalu
3.       Miezi sita kabla ya kifo chake Yesu alitangaza kuwa kila mwenye kiu na aje kwake anywe maji ya uzima ambayo kwayo hataona kiu tena na kuwa ndani yake mito ya maji ya uzima itatiririka  hii inafafanua kitu ziadi ya wokovu hapa waamini wanakua chanzo cha mito ya maji ya uzima kusambaza kwa wengine hii ilikuwa ni ahadi ya Roho Mtakatifu ambayo ilianza kutimia siku ya pentekoste. Maji pia ni ishara ya nguvu, uamsho, utoshelevu na kuburudisho.
4.       Wanafunzi kabla ya siku ya pentekoste walikuwa na Roho Mtakatifu lakini hakuwa ndani yao  ”With them” not ”In them” lakini ahadi ya kufurika na kujaa ilitimia siku ya Pentekoste.
*      Kuabudu katika Roho na kweli Yohana 4;23-24.
1.       Chini ya agano jipya Mungu haitaji watu wake kwenda Yerusalem kwa kusudi la kuabudu kila mtu aweza kumfikia Mungu kupitia Kristo ambaye ni kuhani mkuu lakini ni lazima wale wamuabuduo wawe katika Roho kwa kuwa Mungu ni Roho 

     Kisima cha siloamu kama kinavyoonekana leo katika Yerusalemu hapa ndipo Kuhani alipofungulia maji ili kutiririka katika ua wa hekalu kwa kusudi la kuburudisha watu watalii wanaonekana kuyafurahia maji ya kisima cha siloamu Picha na maelezo maktaba ya Rev.Kamote

*      Mfariji mwingine
5.       Maana  ya msingi ya neno Mfariji inatumika kumuelezea Roho Mtakatifu
6.       Neno hili pia lilitumika kumuelezea msemaji kwa niaba ya  au mtafasiri
7.       Wasomi wengi wa kikatoliki hulitumia neno hili kumaanisha Mwanasheria Advocate au lowyer
8.       Lakini maana ya asili ya neno hili mfariji pia humaanisha mwanasheria mtaalamu au kitaaluma
9.       Kama mfariji Roho hutufundisha kweli yote na kusha wishi wenye dhambi kutubu na kuifuata kweli, Neno Mfariji mwingine  maana yake wa aina kama yake atakayefundisha na kufanya kama Yesu alivyofanya 

*      Kazi za Roho Mtakatifu  Yohana 16;8-11
1.       Kuushawishi ulimwengu kwa habari ya dhambi
¨      Dhambi inayowatenga watu na Mungu ni kutokuamini  hii ni hali ya kumkataa Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha Yetu, Tunapotambua yale tuliyomfanyia Yesu ndipo tunapoweza kujua ubaya wa dhambi
¨      Roho anaposhawishi watu kwa habari ya dhambi huwashawishi ili waweze kuamini na kuifikia toba
2.       Kuushawishi ulimwengu kwa habari ya haki
¨      Haki kamili ilidhihirishwa katika maisha ya Kristo, Roho huwashawishi watu kutamani kuishi katika viwango ambavyo Yesu aliishi kama mfano wa kuigwa kwa wanadamu na watu wanaomcha Mungu
3.       Kuushawishi ulimwengu kwa habari ya hukumu
¨      Ulimwengu huu na mpangilio wake utahukumiwa Matendo 17;30-31 Roho Mtakatifu huwakumbusha wanadamu kuwa wale woote wanaomfuata Shetani watahukumiwa na pia wale wasio mwamini mwokozi

*      Akawapulizia pumzi yake akawavuvia Yohana 20;21-23.
Moja ya maswala yanayoleta utata wa kitheolojia ni pamoja na swala la Kristo kuwapulizia pumzi na kuwavuvia akiwaambia pokeeni Roho Mtakatifu wanafunzi wake je swala hili humaanisha nini?
Ø  Maoni Mabalimbali
§  Humaanisha kuwa walipuliziwa pumzi ya nguvu na walipokea nguvu
§  Pumzi ilikuwa ni ishara ya unabii wa kile kitakachotokea katika siku ya Pentekoste kwa hivyo kwa wakati ule hawakupokea chochote
§  Wengine waliamini kuwa walipokea  sehemu ya ubatizo wa Roho Mtakatifu
§  Walipokea maisha mapya ya ufufuo wa Yesu Kristo ambaye wakati huu alikuwa amefufuka na hivyo walifanyika viumbe vipya Luka 24;49.
Ø  Utata  wa andiko hili
§  Yohana 16;7 Ilionyesha kuwa Yesu angepaa kwanza kisha ndipo Roho aje
§  Yohana 20;22 kupulizia pumzi kusingekuwa tena ni ishara kama wangepokea Roho kwa wakati uleule
§  Yohana 16;16-22,20;22 inaonyesha kuwa ilikuwa lazima Yesu aende kwa baba kabla ya kuja kwa Roho Mtakatifu
*      Kipimo kamili kuhusu  uvuvio wa Roho Mtakatifu
§  Kutimia kwa unabii wa Yoeli kunaonyesha kuwa Roho alimwagwa na kuwa hakutolewa kwa kipimo.Hivyo tukio kamili la ujazo wa Roho lilitimia siku ya Pentekoste
§  Mkazo wa Roho mtakatifu ni katika nguvu na katika Yohana 20;22 ni mamlaka
§  Walichopokea wanafunzi katika Yohana 20;22 kilitamkwa katika agano jipya aidha ikumbukwe kuwa Yohana aliandika akiwa na athari za kitabu cha mwanzo katika fahamu zake
§  Kwa kupokea Roho wanafunzi walikuwa wakithibitishwa kuwa wao ni wanafunzi wa Yesu hivyo baada ya kuwavuvia wanafunzi walipokea Roho kama anavyopiokea Mtu wakati wa kuzaliwa mara ya pili na sio ule ujazo wa Roho Mtakatifu

        SOMO LA NNE: ROHO MTAKATIFU NA KANISA.
Huduma ya Roho Mtakatifu katika Matendo ya Mitume.

Agizo la mwisho la Bwana Yesu
·         Kitabu cha matendo ya mitume ni kitabu cha matendo ya Roho Mtakatifu kwani yoote yaliyotendeka yalitendeka kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Hata hivyo maisha na mafundisho ya mitume yalimuhusu Yesu Kristo zaidi kuliko Roho Mtakatifu wao ndio walikuwa mashuhuda wa mafundisho na mateso na ufufuo wa Yesu Kristo Roho Mtakatifu mara moja aliwaongoza katika kazi ya kuhihubiri injili na kustawisha kanisa  hivyo mitume walikuwa vyombo vya Roho wa Mungu .
·        
        Kuisubiri ahadi ya Baba. Luka 24;49;Matendo ya mitume 1;4-8  Ubatizo wa Roho Mtakatifu ni zawadi iliyohaidiwa na Baba,Wanafunzi iliwapasa kuisuburi Yerusalem kwa sababu walihitaji nguvu za Roho Mtakatifu ndipo waanze kuifanya kazi ya Mungu,walihitajika kuwa pamoja kwa nia moja ili Roho ashuke na kutimiza kile Mungu alichokuwa anataka ubatizo wa Roho Mtakatifu ulikuwa ni uzamisho wa uhusiano ambao ulitakiwa kuendelea na kuwa mkubwa sana kwa ujumla ubatizo wa Roho Mtakatifu unapewa majina mengi sana katika kitabu cha matendo mfano;-
a.       Wakajaa
b.       Kumwagiwa Roho
c.       Kupokea Roho
d.       Kushuka juu yao
e.       Kuja juu yao
·         Muda wa kusubiri. Pale Yerusalemu wanafunzi walisubiri kwa Muda upatao siku kumi huu ulikuwa ni wakati kati ya Kupaa kwa Yesu na siku ya Pentekoste Matendo 1;14 wakati huu walikuwa wakikutana kwa pamoja na kufanya maombi hekaluni pia walifanya uchaguzi wa Matiya kuchukua nafasi ya Yuda.
·         Kushuka kwa Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste.
A.     Maana ya sikukuu ya Pentekoste
1.       Ilikuwa ni sikukuu ya kusheherekea Mavuno ya ngano
2.       Baada ya wayahudi kutawanyika na kuishi sehemu mbalimbali ulimwenguni mavuno ya ngano ambayo hufanyika mwishoni mwa mwezi mei walianza kuweka mkazo siku ya pentekoste kuwa sikukuu ya kusheherekea  kushuka kwa sheria katika mlima wa Sinai katika sherehe hizi wayahudi wapatao 180,000 walikuja kuabudu wengi walikuwa wakitoka katika inchi mbalimbali  ambazo zilizungumza lugha nyingine na hivyo walioishi huko hizo zilikuwa ni lugha zao sasa Pentekoste iliadhimishwa siku ya hamsini baada ya pasaka
3.       Katika Agano jipya siku ya pentekoste inachukuliwa kama ishara ya kuanza kwa mavuno ya roho za watu kwa sababu ya kazi ya ukombozi iliyofanywa na Yesu pale msalabani
B.     Upepo na Ndimi za moto.Matendo 2;1-4.
1.       Ishara ya upepo
a.       ”Uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi’ baadhi huamini hii kuwa ni nguvu kwa ajili ya utumishi na baadhi huamini kuwa hii Pumzi ya Roho Mtakatifu yenye kubadilisha au kuzaa upya ambayo huleta maisha mapya.
b.       Ndimi zilizogawanyikana  kama ndimi za moto baadhi huamini kwamba hii ni ishara ya kukubaliwa kwa kanisa kama mwili wa Kristo na pamoja na kukuibaliwa kwa kila muamini kama hekalu la Roho Mtakatifu
c.       Ishara ya moto haikuweza kujitokeza tena katika maeneo mengine popote watu walipojazwa Roho Mtakatifu  mfano Samaria au Kaisaria hii huenda ni kwa sababu
       -Ishara ya moto ilitokea mara moja tu hususani siku ya kuliweka wakfu Hema ya kukutania katika agano la kale na huenda ilitokea mara moja tu siku ya pentekoste  kama ishara ya kukubaliwa kwa kanisa au kila muamini ambao ni hema mpya
       C. Kukua kwa kanisa kwa kasi Matendo 2;42.
           1. Kushuka kwa Roho Mtakatifu haukuwa tu mwanzo wa kanisa bali pia ulikuwa mwanzo wa kanisa kukua kwa kasi ya ajabu sana  Ghafla tunaona watu 3000 wakimwamini Mungu ghafla wakijifunza kutoka kwa mitume na kutii kila walichokisema au kukiagiza haraka sana ushirika kati ya Mungu na wanadamu ulikuwa na ushirika kati ya watu wao kwa wao walikuwa na umoja na walifurahi kushirikiana na kuumega mkate, bila shaka ni kwa sababu ya Roho Mtakatifu waliabudu pamoja na kuishi kivitendo katika yale waliyofundishwa huku Ishara na miujiza ikiwa inatembea kila mahali miujiza hii iliwatia nguvu imani zao, miujiza ilikuwa sehemu ya maisha yao
          2. Kujazwa Tena . Hili ni jambo ambalo wapentekoste wengi wanalipuuzia wanafikiri ujazo wa Roho mara moja tu imetosha lakini wachunguzi wa Biblia wanasema unaweza kujazwa tena na tena  hiki kinaonekana mwandishi Luka akikirudia na kila kinapojitokeza kunakuwa na matukio mengine ya kutiwa nguvu katika huduma  Matendo 4;13,31,13;9-12 hivyo hii inamaanisha watu walibatizwa kwa Roho siku baada ya Siku lakini walijazwa Roho tena na tena Efeso 5;18 kila kujazwa tena kunapotokea kutiwa nguvu kwa upya hutokea
        3; Shughuli nyingine za Roho wa Mungu katika Matendo ya Mitume
*      Alitatua matatizo katika kanisa Matendo 5;3-4
*      Alihusishwa na uchaguzi wa mashemasi Matendo 6;1-6
*      Alihusika katika utendaji wa miujiza Matendo 6;8,8;1
*      Aliwajaa watu kama Paulo Matendo 9;17-18 Paulo aliwafundisha wengine wajae Roho Efeso  5;17-18 na pia aliwaambia wakoritho kuwa ananena kwa lugha kuliko wao wote  1koritho 14;18
*      Watu wa mataifa walijazwa Roho pale Kaisaria  Matedno 10;44-46 hili ni tukio lenye kuvutia sana kwani halikuwa tofauti na siku ya Pentekoste mitume walipojawa na Roho hii ilikuwa ishara ya kuwa Mungu amewakubali mataifa kama anavyo weza kuwakubali wayahudi
*      Watu wa Efeso pia walijazwa kwa Roho Mtakatifu Matendo 19;1-7 hawa mwanzoni walikuwa hawajasikia habari za Roho Mtakatifu ingawa walikuwa wanafunzi wa Yesu Baada ya Paulo kufika aliwaombea ujazo wa Roho na wakampokea wakanena kwa Lugha
*      Mitume waliongozwa na Roho wa Mungu hata katika kazi zao za injili au huduma ya kimisheni kwa mfano Matendo 13, kuwahitaji kwa huduma, na pia alitoa mwelekeo wa wapi kwa kwenda mfano kuhusu kwenda Antiokia n.k.

Nguvu katika maisha
Msimzimishe Roho 1Thesalonike 5;19.
      Kwa ni nini Paulo aliwaambia wathesalonike wasimzimishe Roho? Roho Mtakatifu ni kama moto, injili ilipohubiriwa Thesalonike ilikuja kwa nguvu na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu  1Thesalonike 1;5, Wathesalonike walijazwa Roho Mtakatifu  na hivyo walikuwa na furaha licha ya kuweko kwa mateso namna walivyohubiriwa na namna walivyopokea injili vina uhusiano mkubwa na Roho mtakatifu wayahudi walimpinga Paulo wakidhani kuwa Kazi ya Roho Mtakatifu ndani yake na wenzake ilikuwa ikiupindua ulimwengu Matendo 17;6.
      Msimzimishe Roho ni neno lenye uhusiano na kuzima moto au kuuua Waebrania 11;34,Daniel 3;25-28 Hii ilikuwa na maana kuwa Roho Mtakatifu anawezakuzimishwa hii ni kutokana na mambo mabalimbali ambayo wakristo wanaweza kuyafanya hii ikijumuisha maswala kadhaa kama ;-1Thesalonike 5;20
*      Kupinga unabii na kuuchukulia kama kitu kisicho na maana
*      Kupinga kwa ukali au kukataa au kukosoa kile kinachofanywa na Roho
*      Kuzimisha au kuua kipawa chochote kinacho husiana na kazi au karama za Roho Mtakatifu
*      Badala ya kukataa unabii kinachotakiwa ni kuupima kwa maandiko na mbaya ukataliwe na mzuri utunzwe Torati 13;1-4,18;21-22 1koritho 14;29
*      Kumzimisha Roho pia kunaweza kukawa na maana ya kutokuishi maisha ya usafi
*      Kuwa na tabia mbaya kinyume na mapenzi ya Mungu
*      Na upinzani dhidi ya Kazi za Mungu kwaajili ya kuhofia nguvu za giza au wanadamu kuigiza
Roho Mtakatifu na Sheria Galatia 3;1-14
       Roho Mtakatifu anapatikana kwa imani, Baadhi ya wakristo mataifa wa Galatia walijaribu kuishika sheria ya Musa na desturi wakidhani vinasaidia katika kuwa sawa na Mungu waalimu wa kiyahudi waliwafundisha na kuwashurutisha kutahiriwa,kujiepusha na vyakula fualani,na kushika sabato
      Wagalatia walisahau kuwa walimpokea Roho kwa imani katika Yesu Kristo kabla hawajadanganyika kuishika Sheria ya Musa hii ilikuwa ni ushahidi tosha ya kuwa wokovu sio jitihada za mwanadamu na kuwa kazi njema haziwezi kumfanya mwanadamu apokee wokovu Paulo aliona ni ujinga kwani walikuwa wakiuacha uhuru wao katika Kristo na kujiingiza katika utumwa wa mwili, Imani na utii kwa neno ndio funguo pekee ya kumshiriki Roho Mtakatifu.Tunaweza kufurahia baraka za Ibrahimu sasa kwa njia ya imani kwa kuwa baraka kwa Ibrahimu ilikuja kwa njia ya imani na sio matendo hivyo hata mataifa waishio kwa imani ni wana wa Ibrahimu Sheria badala ya kuleta uzima na baraka  ilileta hukumu na kifo kwa sababu hakuna mwanadamu anaweza kuishika kwani hakuna mwanadamu aliye mkamilifu
Roho aliaye Abba (Baba).Wagalatia 4;16,Rumi 8;15.
      Nyakati za Biblia mwana hangeweza kuwa Mrithi na angefananishwa na mtumwa tu mpaka wakati wa umri wake mtimilifu ulipokuwa umewadia ndipo angeweza kufanywa mwana  na kuwa na haki na majukumu kama mwanafamilia halali, mataifa kupitia imani ya Ibrahimu tumekuwa wana wa halali wa Mungu  Yesu alikufa ili kutufanya kuwa wana wa halali wa familia ya Mungu Efeso 2;19 ni kwa sababu hii Roho wa Mungu hulia baba ndani yetu Abba ni neno la kiaramu lenye maana sawa na Baba Roho ndani yetu hutufanya au hutupa haki ya kumuita Mungu kama baba yetu, hivyo kuanza kuweka imani katika kutahiriwa na matendo mengine ya sheria  kunamtoa mtu nje ya neema ya mungu Imani huzaa matendo mazuri na sio matendo mazuri kuzaa imani au wokovu
Matendo ya mwili na Matunda ya Roho
1.       Ushindi dhidi ya  Matendo ya mwili
·         Paulo anatumia neno matendo ya mwili kumaanisha tabia ya uovu inayokaa ndani yetu inayotuongoza katika dhambi na tamaa zake, tamaa hizi pia huitwa  utu wa kale ambayo kwa ujumla hupingana na tabia ya utu mpya unaotokana na Roho Mtakatifu dawa yake ni kuishi kwa Roho siku hadi siku
·         Matendo haya ya kale yanapojitokeza ndani yetu hii maana yake tumeacha kuishi kwa Roho ushahidi unaoonyesha kuwa tunaishi kwa Roho au tunaongozwa na Roho ni pale inapotokea matendo yetu ya mwili yanaonekana kuwa yamesulibiwa kabisa msalabani na kuwa tunakusudia kuwa na matunda ya Roho mtakatifu katika maisha yetu
·         Yanapodhihirika matendo ya mwili katika maisha yetu hii maana yake ni kuwa tumeacha kuongozwa na Roho na kuwa mwili ndio kiongozi kwa wakati huo hiii pia inadhihirisha jinsi tulivyodumaa kiroho na kuwa katika hatari au mwelekeo wa Kwenda motoni
·         Makundi ya matendo ya mwili yamegawanyika katika maeneo makuu manne
a.       Uasherati, Uchafu na ufisadi hii ni ile tabia ya kale ya zinaa na kupenda kuangalia mambo ya uchiuchi n.k.
b.       Ibada ya sanamu na uchawi au ashirikina
c.       Uadui, ugomvi, wivu, hasira, Fitina, Faraka, uzushi, husuda, ulafi.
d.       Ulevi.
·         Biblia inawahakikishia watu wanaoendelea kuishi kwa matendo ya mwili kuwa hawataweza kuurithi kabisa uzima wa milele Wagalatia 5;21.
·         Mungu anaweza kumtumia hata muhubiri mwenye matendo ya mwili lakini hii haimaanishi kuwa Mungu anataka mtu huyo aendelee kuwa hivyo linapotokea jambo kama hili inawezekana kuwa Rehema za Mungu zinamvuta mtu huyo kutubu na kuacha au Mungu ameliheshimu neno lake au Imani ya mtu yule anayeombewa  imefanya kazi na kumgusa Mungu, Mungu aliendelea kumvumilia Samson kwa muda mrefu lakini mwishowe kushindwa kwake kuishi katika Roho kulipelekea kumalizika kwake.
·         Mungu anaendelea kuwavumilia watumishi wengi wa mungu ambao wamejaa matendo ya mwili hata leo wanaupendeleo, wana wivu, wana ugomvi waizi wa sadaka au wana matumizi mabaya ya sadaka za waumini hawajali maisha ya kiroho ya waumini wao, wanatengeneza hata skendo ili kuua wengine kihuduma tusipoangalia tutakosa mbingu ambazo tumewahubiria wengine kwa muda wa kutosha.Kutumiwa na Mungu sio kibali cha kukubaliwa .
Matunda ya Roho Wagalatia 5;22-23
1.       Matunda ya Roho Mtakatifu yamegawanyika katika makundi makuu matatu
·         Katika uhusiano na Mungu tunapata Furaha, Amani na Upendo
·         Katika uhusiano na wengine  tunapata Uvumilivu, Fadhili, Utu wema na Uaminifu
·         Katika uhusiano wetu na Imani yetu tunapata Upole,kiasi,
·         Hata hivyo Biblia inatumia neno Tunda la Roho na sio matunda ya Roho hii inamaanisha msisitizo wenye maana ya kuwa na msisi tizo mmoja kwa mtu anayetembea katika Roho  yaani kama Roho anakuongoza inaaminika kuwa matunda yoote yatadhihirika ndani yako kwani Roho atatawala maisha yako yoote na sio nusunusu neno tunda kwa kiyunani ni kerpos ni umoja kama wa chungwa ambalo ndani lina vijisehemu vidogovidogo lakini likikamuluiwa lote hutoa juisi ya chungwa.
Uchambuzi kuhusu matunda ya Roho kwa ufupi.
 Kwa ujumla mtu anayetembea na Roho au mwenye kuongozwa na Roho na kuzaa matunda ya Roho anatarajiwa kuwa mwenye kuchukua nafasi ya chini hatakuwa mtu wa kujisifu Wagalatia 5;26,atahakikisha kuwa anawasaidia hata wale waliorudi nyuma Galatia 6;1-2,atakuwa na upendo akifanya kila kitu kutoka moyoni akiwatumikia wengine Galatia 5;13 hii inatokana na chanzo cha upendo kuungwa nasi  kupitia Roho Mtakatifu 1Yohana 4;7-8  na atakuwa mwenye furaha na hii ni matokeo ya upendo alionao Warumi 14;17 Furaha hii haitokani na mazingira halikadhalika Amani ambayo ni matokeo ya kuishi vizuri na wenzetu, Uvumilivu uwezo wa kusamehe na kutochukua hatua kwa haraka ili usikwaze au kumfanyia mwengine yasiyofaa  utuwema hii inahusiana na ukomavu katika swala la ukarimu, Uaminifu kuwa mkweli na mtii na kutumia vizuri kila tunachokuwa tumekabidhiwa kama mawakili wema upole Mathayo 11;29 hali ya uvumilivu na kutokusukuma watu au kuwalazimisha na kiasi hali ya kuweza kujizuia au kustahimili au kujistahimili ni kujizuia hata katika jambo ambalo ungeweza kulifanya katika mazingira huria uliyo nayo bila kujali hatari yake.
Jinsi ya kuwa na matunda ya Roho
     Kadiri mkristo anavyoendelea kuwa mtii kwa Roho wa Mungu na neno lake ndivyo na matunda ya Roho yanavyoweza kuendelea kuzaliwa ndani yake hii itajumuisha pia swala zima la kuishi kwa kukataa mambo ya mwili na hivyo matunda yatakuwa ndani yake, Endelea kumuhubiri Kristo tukiusubiri ukombozi kamili wa mwili huu 1Koritho 15;15-52
     
Huduma katika Roho

Hekima ya mwanadamu na hekima itokanayo na Roho wa Mungu
     Wakoritho walijisifia sana hekima ambayo ilitokana na ujuzi wa kibinadamu Ginosko na waliitukuza sana lakini kuna tofauti ya hekima ya kibinadamu na ile itolewayo na Roho wa Mungu ni rahisi kuona wakati mwingine mambo yakikubalika kabisa katika hali ya kibinadamu na fikira zake lakini yakawa kinyume na mafundisho na mfano wa Yesu Kristo wayunani walishindwa kabisa kuona mantiki ya kifo cha Yesu msalabani kwa sababu walitumia akili za kibinadamu na falsafa na hoja za kawaida  na hata hekima ya kibinadamu na kwa sababu hiyo waliona ni ujinga wala haiingii akilini kukombolewa kwa mwanadamu eti kwa mtu kufa juu ya msalaba haingii akilini hata kidogo.
     Paulo anasema alikataa kutumia njia ya kibinadamu katika kuihubiri injili Yeye alitumia nguvu za Roho Mtakatifu katika kuipeleka injili. Kuijua siri ya nguvu za Mungu kungeweza kumfanya mwanadamu kukaa katika imani wakoritho walihitaji nguvu za Mungu na Kristo aliyesulibiwa kama hekima itokayo kwa Mungu 1 koritho 1;24.

Kufunuliwa kwa Roho.
     Ni Roho wa Mungu pekee awezaye kufunua siri ya kufa kwa Yesu msalabani, hata kama injili zote nne zimeelezea kwa ufasaha sababu ya kufa kwa Yesu msalabani bado inamuhitaji Roho wa Mungu kufanya kazi ya kumfanya mtu alielewe hilo. Ni kupitia Roho wa Mungu tunaweza kujua mambo hata yaliyomo katika moyo wa Mungu 1 Koritho 2;10. Hili ni vigumu kwa mwanadamu wa kawaida kujua nini kinaendelea katika moyo wa Mungu, Ni Roho pekee awezaye kuyafanya hayo

Usiishi kama mtu wa Kawaida.
     Miili yetu ni hekalu la Roho Mtakatifu 1 Koritho 3;16 Ninyi ni Hekalu la Roho wa Mungu hii inamaana ya kuwa kila muumini ni patakatifu pa patakatifu pa Roho wa Mungu maana ninyi inatuhusu kanisa woote hivyo miili yetu ni mali yake hii inamaana tunapaswa kutoa kipaumbele katika kumuabudu na kumtumikia miili yetu ni lazima itumike kwa utukufu wake, Mungu hapendezwi na tabia ya kuitumia miili yetu kwa ajili ya dhambi au iharibikiwe kwa ajili ya dhambi 1 Koritho 6;14. kama alimfufua Kristo aweza kuifufua na miili yetu itoke katika hali ya kuharibiwa na dhambi mwili wetu haujatenganishwa na roho zetu hivyo tukifanya dhambi tunafanya juu ya miili yetu wenyewe 1 koritho 6;13-20 hivyo ni muhimu kwetu kuishi kama watu wa Rohoni.

Elimu na kiroho.
     Wengine wanaamini kuwa hatihitaji Elimu kama Roho wa Mungu akiwa ndani yetu lakini kwa kweli Elimu ni moja ya nyenzo ambazo  Roho Mtakatifu huzitumia kama tu tutakuwa wanyenyekevu na kujidhabihu kwake, Haijalishi una elimu kiasi gani bado tunamuhitaji Roho Mtakatifu sana kwa habari ya kufahamu mambo ya Rohoni kwa mfano tunahitaji kunena kwa lugha wakati mwingine ili kujijenga kiroho kutafuta kwetu elimu ni lazima kuendane na kumpa Mungu utukufu inamuhitaji Roho wa Mungu kumfunua Kristo kwetu na kutupa neema na kuifanya halisi katika maisha yetu
Roho – Elimu = Uzushi
Elimu – Roho = Ufarisayo au ukatoliki
Elimu + Roho – Unyenyekevu = Anguko la Lusifer/Kiburi.
Roho + Elimu + Unyenyekevu = Huduma kama ya Paulo mtume

Huduma katika kanisa.
Swala la kutoa unabii 1Koritho 13-14.
Kuna tofauti kati ya kunena kwa lugha na kutoa unabii katika asili yake na matumizi yake
a.       Kwa ajili ya kulijenga Kanisa.
·         Kwa upendo kabisa washirika wanapaswa kuelekezwa namna ya kuzitumia karama hizi ya kunena kwa lugha na karama ya unabii ndani ya kanisa.
·         Kusudi kuu ni kulijenga kanisa au kuwatia moyo waumini ndani ya kanisa,kuwatia nguvu ya kiroho na kulijenga kanisa kiroho na kiidadi
·         Mtu anaponena kwa lugha anajijenga yeye Binafsi lakini anapotoa unabii ni kwa kusudi la kulijenga kanisa hivyo kunena kwa lugha maana yake ni kuzungumza na Mungu kwa roho ambapo mnenaji na Mungu pekee ndio wenye kuelewa
·         Lakini Roho wa Mungu anapoleta ujumbe kwa unabii lengo ni kulijenga kanisa kulitia moyo na kulifariji hivyo ni muhimu kwake watu woote wakaelewa unabii kwa msingi huo unabii unahitajika zaidi katika kanisa kwa sababu unalijenga kanisa
·         Kunena kwa Lugha bila kupata tafasiri kunakuwa hakuna maana sana lakini kama mtu akinena kwa lugha kama njia ya kuleta ujumbe na ukatafasiriwa basi utakuwa na maana kwani utafanya kazi ileile ya kulijenga kanisa
b.      Kunena kwa lugha kunahitaji Tafasiri.
·         Kama kunena kwa lugha + kutafasiri = unabii basi kunena kwa lugha na unabii vyote vinahitajika katika kanisa kwa kulijenga kanisa katika namna tofauti tofauti kwani kunena kwa lugha ni ishara ya kuingilia kati kwa Mungu Roho mtakatifu
·         Kuna mambo ya msingi manne yanayo wakilishwa kama kunena kwa lugha kutaambatana na kutafasiriwa
Ø  Ufunuo huu sio ufunuo wa kweli mpya bali ufunuo wa maana ya kweli fulani ya kiroho au maandiko
Ø  Maarifa huu ni ufahamu wa kiroho kuhusiana na jambo fulani
Ø  Unabii na mafundisho yaani ujumbe ambao Mungu ameukusudia kwa kanisa na mafundisho ambayo Mungu ameyakusudia kwa kanisa
·         Hivyo kama kunena kwa lugha hakutakuwa na Tafasiri basi hii ina maana muhusika anawasiliana na Mungu na kujijenga mwenyewe na unapotafasiriwa basi unalijenga kanisa 1 Koritho 14;2 bila tafasiri hakuna mawasiliano Mstari wa 13-15
·         Kunena kwa lugha kunahitaji tunda la kiasi kwani kunena pekee kunaweza kusilete matunda yaani kufahamu hivyo unahitaji mlingano kati ya kunena katika roho na kunena katika akili au ufahamu wa kawaida na kuimba katika Roho na kuimba katika ufahamu wa kawaida 1Koritho 14;15
c.       Sababu za kunena kwa Lugha
·         Ni kwa ajili ya mtu binafsi na kwaajili ya kujijenga nafsi yako 1 Koritho 14;2-4 ni kutimia kwa unabii wa Isaya kumuhusu Yesu Isaya 28;11,1Koritho 14;21,Marko 16;17 Matendo 2;4.10;46;19;6,1Koritho 14;5,14-18,39.
·         Kunena kwa Lugha pia ni uthibitisho wa kuwa Yesu amefufuka na ametukuzwa Yohana 16;7,Matedno 2;26.
·         Ni ishara ya ujazo wa Roho Mtakatifu 1 koritho 14;4 na waamuzi 20
·         Ni ishara ya kuwa Roho Mtakatifu anatuombea Warumi 8;26 1 Koritho 14;4,Efeso 6;2 ni njia ya kufurahi kiroho 1Koritho 14;12,15, Isaya 28;12.
·         Ni Ishara ya kutimizwa kwa neno la Mungu linapokuwa limehubiriwa Marko 16;1,20.1Koritho 14;22.
d.      Kunena kwa Lugha Kama ishara.
·         Kunena kwa lugha pia ni Ishara kwa wasioamini watu walioamini wote wanajua kuwa kunena kwa lugha au unabii ni ishara ya kuingilia kati kwa Mungu kwa kuwa wote tumeungwa katika roho
·         Kunena kwa lugha bila ya tafasiri kwa wasioamini kunaweza kuonekana kama kitu kisicho na maana na hii inaweza kuwapelekea kudhihaki kama ilivyokuwa siku ya Pentekoste
·         Hivyo kunena kwa lugha kunakoambatana na tafasiri kwa wasioamini kunaweza kuleta maana nzuri na ya kujenga kwao na hiki ndicho Paulo alichokuwa anakikazia
e.       Sheria za kunena kwa Lugha na Unabii.
·         Kulingana na melekezo katika Wakoritho 14;27-28 tunaweza kujenga hoja za sheria za matumizi ya kunena kwa lugha pamoja na unabii kama ifuatavyo
1.       Matumizi ya kunena kwa lugha
Ø  Lazima idadi idhibitiwe wanene wawili au watatu katika kanisa
Ø  Lazima kuweko kupokezana na kutafasiri yaani kunena mmoja mmoja na mwingine atafasiri
Ø  Kama hakuna wa kutafasiri basi mmnenaji asinene kwa nguvu kubwa kama mwenye ujumbe lengo la jambo hili sio kumzimisha Roho bali kuweko utaratibu badala ya machafuko au vurugu ”God is The God of oder ”
2.       Matumizi ya Unabii
Ø  Unapotolewa unabii ni lazima ukubali upimwe na wengine
Ø  Tukio la kuupima linahusiana na kuangalia kama uko sawa na maandiko na kuangalia ni nini Mungu amekusudia tukifanye
Ø  Mungu anataka kuwatumia watu mbalimbali na vipawa mbalimbali katika kanisa hivyo mtu anayehudumu katika Roho anapaswa kuwafikiri wengine katika upendo
f.        Mungu ni Mungu wa amani na sio machafuko.
·         Kama karama zitatenda kazi katika msingi wa upendo kutakuweko amani na wala si machafuko
·         Mkristo aliyekomaa atakuwa tayari kukubali maelekezo yoyote ya matumizi ya karama kutoka katika maandiko na atakubali tofauti zilizoko kwa amani
·         Karama ni msaada wa kutusaidia kusaidia wengine kwa lengo la kutukomaza katika kumuelekea Kristo, kuwa na karama sio dalili ya kukomaa kiroho na hivyo bado tunahitaji kujinyenyekeza katika huduma ya kichungaji ili tuweze kuwa salama, misingi ya fundisho la kweli haujengwi katika unabii pekee bali na neno la Mungu hivyo ni muhimu kwetu kukubali maelekezo ya kichungaji.

SURA YA TANO: ROHO MTAKATIFU NA HUDUMA ZAKE.
Kutakaswa na Roho Mtakatifu Waebrania 12;14.
1)       Maana ya Utakaso.
     Utakaso ni kazi ya Roho Mtakatifu kwa mtu aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kuwa mbali na dhambi na kumuweka wakfu kwa ajili ya Mungu.
a.       Kuweka wakfu, Kutakasa, kutoa kwa ajili ya, kutengwa kwa ajili ya.
i.         Vyote vina maana moja ni kutenga na uovu au na yule muovu na kumuweka Kristo ndani ya maisha ya Mtu.
ii.       Neno watakatifu katika maandiko lina maana ya waliotengwa 1 koritho 1;2,6;1 Philip 1;1.
iii.      Kazi ya utakaso hufanywa na Baba, Mwana na Roho mtakatifu kwa ujumla wanashirikiana
iv.     Kazi kwa ujumla ni jukumu la Roho mtakatifu katika maisha yetu yote
v.       Tunahitaji hata hivyo kufanya sehemu yetu katika swala la utakaso kwa kukaa katika neno, kuendelea kuamini, maisha ya maombi na kujitoa kunasaidia katika kukamilisha kazi ya utakaso
b.       Kutengwa mbali na dhambi kuna maana tatu zifuatazo
i.         Kutengwa mara moja Instant sanctification huku ni kutakaswa kutoka katika matendo ya dhambi kimaadili na kuhesabiwa haki na kuzaliwa upya hili hufanyika mara tu mtu anapookolewa na kutolewa katika giza kuletwa katika nuru 2Koritho 5;17
ii.       Kutengwa kwa ajili ya huduma  na kwa ajili ya Mungu Progressive sanctification mtu anapotengwa kwa ajili ya huduma hilo pekee lina muweka wakfu lakini anapaswa kuendelea katika kuishi maisha matakatifu aidha kadiri kila muamini kwa jitihdada zake binafsi na ushirikiano wake anaoutoa kwa neno na Roho wa Mungu hukamilika siku hadi siku hivyo huendelea kutakaswa huu ni utakaso endelevu.
iii.      Kutengwa kamilifu Perfect sanctification utakaso wa jinsi hii  mtu anapokuwa amefariki dunia huku akiendelea kumuanmini Mungu na kuishi katika Mungu mtu hawezi kukamilika kabisa akiwa angalipo duniani hili tutalijadili baadae hapo chini
2)       Kwanini Biblia imetoa amri ya kuwa wakamilifu?
       Mathayo 5;48, 1Petro 1;15-16, Lawi 19;2,11;44. Biblia imeamuru tuwe wakamilifu au watakatifu kama Baba yetu wa Mbinguni hii ni amri je amri hii ina maana gani? Na Kristo ametuahidi basi ninyi mtakuwa wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu haya yana maana zifuatazo
1.       Kiwango cha kipimo cha maisha tunayopaswa kuyaishi ni Mungu mwenyewe.
2.       Neno kuwa mkamilifu lina maana ya kukomaa, kuwa kamili
3.       Hatuwezi kuchukua tamaduni za kibinadamu,au vyuo vya kibinadamu na mafundisho yao kama kipimo cha kuwa wakamilifu lazima tuangalie Mungu mwenyewe anataka nini. Mungu ni mkamilifu na mwenye upendo.
4.       Mapenzi yake kwetu ni sisi kuwa kama yeye alivyo 1Thesalonike 5;23 yeye anataka kutuona tukiwa mbali na dhambi au huru kutoka dhambini na haitaji kutuona tukifanya dhambi kwa kusudi au kwa kutokukusudia bali kusikia furaha ya watoto wake Yeye aweza kabisa kutulinda na dhambi tukimruhusu afanye hivyo kwa hiyari yetu kwani tunapofanya dhambi twafanya kwa hiyari yetu
3)       Maono mbalimbali kuhusu ukamilifu
·         Wako wanaoamini kuwa mwanadamu hawezi kuwa kamili katika maisha haya  ingawaje tunapaswa kuendelea kutamani na kuishi kwa utakatifu
·         Wengine wanaamini kuwa ukamilifu ni kuwa huru mbali na kutenda dhambi ya aina yoyote ile na kuwa na upendo uliokamilika na kuwa chini ya neema nyingi inayotusaidia kukamilika huu ni ukamilifu wa kuendelea kujitahidi Wafilipi 3;12-15. Huu ni ukamilifu usiokata tamaa katika kuendelea kumwangalia Yesu kama lengo letu kumuelekea Mungu.
·         Wako wanaoamini kuwa utakaso ni tendo endelevu 1 Yohana 1;7-10 hivyo tunapaswa kuendelea katika kuikulia neema, kuendelea kutakaswa kwa damu ya Yesu na kuendelea kuishi maisha yanayohusiana na ukristo mpaka kifo.
4)       Namna ya kujiendeleza katika Utakaso.
Ufahamu wa Kiroho
     Tunapaswa kujihakikishia kuwa tunakuwa na maarifa ya kiroho na ujuzi kuhusu Mungu Mithali 2;2-5,Yohana 17;3.Kolosai 1;9-10.Efeso 1;17-18 tunapoendelea kumjua Mungu na kuwa na maarifa ya kiroho tutaweza kugundua maisha yetu ya dhambi na mahitaji yetu sisi wenyewe Mwalimu mkuu hapa ni Roho Mtakatifu ambaye atatumia neno la Mungu na uzoefu wa kutembea nasi na kwa jinsi hiyo atatusaidia kujifunza kumhusu Mungu kiu ya Paulo ilikuwa hii nasi lazima tutake kumjua sana Filipi 3;10
Kujitoa katika maombi na kutafakari.
     Mwanzo 21;21-26,1koritho 1;2; Roho Mtakatifu ni msaada wetu mkuu tumtegemee yeye katiika maombi yetu atusaidie na maombi yetu yaambatane na kumsifu yeye
Kuendelea kuwa na imani.
      2Thesalonike 5;1-3 waebrania 10;22 Habakuki 2;4 Mathayo 25;21-23.ni muhimu kukua katika imani kamwe tusikubali kudumaa,tujifunze kuwa na ujasiri kwa Mungu tukiendela kumuamini kuwa anaweza kufanya kile ambacho alikwisha kukifanya anaweza kukifanya naam na atakifanya, Msamaha ni swaola linalopatikana kwaimani kama Mungu alikusamehe kabla hujaokoka atashindwaje kukusamehe leo ukiwa tayari amesha kuokoa na atashindwaje kuendelea kukusamehe pokea msamaha wa Mungu kwa imani na songa mbele
Kuendelea katika kuyatii mapenzi ya Mungu.
     Yohana 6;38,mathayo 26;42 na Waebrania 5;8 Yesu alipokuwa duniani akiwa na mwili kama wa kwetu alichokifanya ni kuyatii mapenzi ya baba yake wa Mbuinguni  hivyo mapenzi yetu lazima yawe kamili katika mapenzi ya baba yetu wa Mbinguni
Sulubisha utu wa kale.
     Hii maana yake inakupasa kuendelea kuyakataa matendo ya mwili na ubinafsi na kuishi kwa roho yaani kukubali Mungu ayafishe kabisa matendo ya mwili tamaa na matakwa ya mwili endelea kutamani kuzaa matunda ya Roho na ukubali kukua na kukua na kukua kila wakati
Kubali Kumtumikia Mungu
     Tunapokubali kupakwa mafuta na roho wa Mungu basi tukubali kutumiwa na yeye Matendo 10;38,Isaya 26;12,Filipi 2;3 Wakati mwingine mungu ataruhusu mateso ambayo yatatuweka karibu na yeye tukubali kufundishwa na Mungu.
Tazamia kurudi kwa Yesu
     Warumi 5;2,15;13 1Petro 1;2-8,1Timotheo 4;7-8 ni muhimu kutazamia kurudi kwa Yesu haraka tumaini hili linapokuwa kubwa ndani yetu husaidia kuishi maisha matakatifu kurudi kwa Bwana kunaweza kukutokea wewe mwenyewe binafsi au kwa kanisa zima kwa jumla hivyo jiandae kwa kujiweka tayari tukijua kuwa wakati wowote Yeyeyajae atakuja wala hatakawia

KUBATIZWA KATIKA ROHO MTAKATIFU
Ubatizo wa Roho Mtakatifu.        
Kusudi kubwa la ujazo wa Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya nguvu za utumishi lakini hata hivyo kuna maoni mbalimbali ya wanatheolojia kuhusu ujazo wa Roho Mtakatifu ambayo ni muhimu kwetu kama tutayatafakari
1. Nguvu kwa ajili ya utumishi.
      a. Maoni ya wa Wesleyani (The Wesleyani view)
·         Wao wanaamini makusudi makuu ya ubatizo wa Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya utakaso na kutuweka mbali na dhambi ili tuwe wakamilifu
·         Waalimu wa maoni haya wanatokea katika jamii ya wa holiness ambao walikazia mafundisho ya utakaso au ukamilifu
·         Waasisi wa mafundisho haya ni kama John Wesley 1703-1791 na Charles Finney 1792-1875.
     b. Maoni ya Kesdwick wa 1870
·         Aliamini kuwa kusudi kuu la kujazwa Roho Mtakatifu ni Kwa ajili ya nguvu na sio kusafishwa kutoka dhambini
·         Mwinjilisti maarufu Dwight L. Moody, R.A.Torey, A.J. Godon na A.B.S. waanzilishi wa ukristo huko Chicago walichangia na kuendeleza maoni hayo kwa kuchangia kuwa pia ujazo unasaidia katika utakaso endelevu Progressive sanctification.
    c. Kweli ya Neno la Mungu
·         Woote waliojazwa kwa Roho Mtakatifu walikuwa tayari wamesafishwa  au wamezaliwa mara ya pili na tayari walikuwa ni waamini katika Kristo
·         Kusudi la msingi la kujazwa kwa Roho Mtakatifu sio kutufanya kuwa watakatifu au kutufanya tuwe na furaha  bali kutupa nguvu za kazi au za utumishi
·         Hivyo ni wazi kuwa nguvu za Roho Mtakatifu kwa kanisa kwa nyakati hizi zote ni kwa ajili ya kukamilisha mpango wa Mungu na kazi zake.
2. Ishara ya ya nje ujazo wa Roho Mtakatifu.
            Ni muhimu kuelewa kuwa kuna tofauti kati ya Ishara ya nje ya ujazo wa Roho Mtakatifu na karama ya kunena kwa Lugha kama huduma kwa ajili ya kulijenga kanisa hapa pia kuna maoni mbalimbali kuhusu swala hili.
1.        Maoni ya R.A.Torrrey
-          Aliamini kuwa nguvu ndio ushahidi pekee unaotakiwa kuonyesha kuwa mtu huyo amejazwa kwa Roho mtakatifu
2.       Maoni ya Donald Gee 1969 katika kitabu chake cha Pentecost
-          Aliamini kuwa njia pekee ya Mungu  kuonyesha ishara kuwa Roho ameshuka na kulijaza hekalu lake  ilikuwa ni ishara iliyotokea kwa wakatu ule kama ilivy kwa habari ya kunena kwa Lugha  kama ilivyotokea pale nyumbani kwa Kornelio
3.       Maoni ya kibiblia
-          Mara nyingi ni ishara ya kunena kwa lugha ambayo hutokea mara moja baada ya kujazwa
-          Pili ni ishara ya kukua kiroho hata kufikia kuzaa matunda ya Roho hii ni ishara endelevu kuwa anaendelea kuweko.
-          Biblia inaonyesha hata hivyo kuwa si wakristo wote walinena kwa lugha 1Koritho 12;30 hii ilimaanisha kuwa si wakoritho woote walionena kwa lugha au kuna baadhi ya wakoritho hawakuwahi kunena kwa lugha  hata hivyo katika lugha ya sili ya kigiriki yaani kiyunani maana halisi ni kuwa sio woote waliendelea kunena kwa lugha na sio kuwa hawajawahi kunena kabisa andiko hili pia linaweza kuwa na maana ya kuwa si wakoritho wote wana karama ya kunena kwa Lugha kwa kusudi la kulijenga kanisa
-          Wengi wanaopinga kuhusu kunena kwa lugha wanasema ni vigumu kupata uthibitisho kamili kutoka katika kitabu cha Matendo ya mitume 
3; Jinsi ya kupokea ujazo wa Roho Mtakatifu.
A.      Kumtafuta mbatizaji kuliko kubatizwa.
Ili kumsaidia mtu kupokea ujazo wa Roho Mtakatifu ni muhimukutoa maelekezo au msisitizo wa kumtafuta mtoaji zaidi ya zawadi, Abrahamu alimuamini Mungu na ahadi zake Mwanzo 15; 6, Yohana mbatizaji alikazia watu kuzaa matunda kama matokea ya toba zao kabla hata hajawabatiza na aliwaelekeza watu kumpokea yeye anayebatiza kabla hata ya kupokea ubatizo ni lazima tuweke imani yetu kwa Yesu anayebatiza Yohana 14; 16,16;7
B.      Imani ndio ufunguo.
Ili mtu apokee ujazo wa Roho anapaswa kupokea kwa imani huu ndio ufunguo pekee wa kupokea Wagalatia 3;2,14 Matendo 15;8-9 Roho Mtakatifu anapatikana kwa imani  mwamini ni lazima aendelee kuamini katika ahadi za Mungu na kuamini kuwa mungu ataitimiza ahadi yake
C.     Lazima ujue kuwa Roho Mtakatifu amekwisha kutumwa duniani rasmi kuanzia siku ya Pentekoste kwa ajili ya woote watakaomwamini hivyo lazima utarajie
D.     Fundisha kuhusu RohoMtakatifu mara nyingi kile tunachokihubiri ndicho kinachotokea toa maelekezo yatakayopandisha imani kama Yesu alivyofanya Luka 24;48-49 matendo 1;40-5.
E.      Omba na mara nyingi maombi kuhusu Roho Mtakatifu na ujazo wake yanapaswa kuombwa kwa kupaza sauti Luka 11;13, aidha inaonekana kutamani kujaa Roho kunapaswa kuwa kama kiu mtu anapokuwa na kiu na kuhitaji maji ya kunywa huomba au hunywa Yesu amekwisha kutoa mwaliko wa kunywa kama una kiu Yohana 7;37
4; Maswala ya Kupokea ujazo wa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono.
·         Kuna mijadala mingi siku hizi kuhusu swala la kuwekewa mkono kwa ajili ya kupokea Roho Mtakatifu au hata miujiza Mingine ni muhimu basi kujadili swala hili kwa kina ili kuondoa mashaka yaliyopo kuhusu uwekaji mikono.
·         Tendo la uwekaji mikono hufanywa na watumishi wa Mungu ili kuruhusu kupitisha Baraka anayoikusudia Mungu kwa mtu husika, hivyo muwekaji mikono ni bomba tu la kupitisha maji lakini sio chanzo cha hayo maji chanzo ni Mungu hii maana yake ni kuwa mtu anayehitaji ujazo wa Roho Mtakatifu bado anapaswa kuiweka imani yake kwa Mungu na sio katika mikono ya watumishi Matendo 8; 14-17, 19; 1-7.
·         Tendo la kuwekewa mikono pia lilitumika kama kichocheo kwa karama za Roho kujitokeza ndani ya mtu ili apate kutimiza jukumu alilokusudiwa au huduma iliyokusudiwa hii ilikuwa ni ishara ya kuwatakia neema za Mungu wale ambao Mungu amewaita katika huduma Fulani ili awatumie 1Timotheo 4;14,Matendo 13;1-3,
·         Tendo la uwekaji mikono halikuwa la hovyohovyo lilikuwa linachukuliwa kwa tahadhari sana ili kujilinda na madhara 1Timotheo 5; 22. Hii ni kwa sababu tendo la uwekaji mikono pia lilihusiana na kurithiana kitu kati ya mwekaji na mwekewa kwa mfano Mwanzo 48;8-20 Yakobo alipoweka mikono juu ya Efraimu na Manase aliwarithi kuwa wanawe nao walimrithi kuwa watoto wake badala ya wajukuu,Hivyo tendo la uwekaji mikono pia hufanya kazi ya kurithishana kitu kati ya wawekewa na muwekewa
·         Uwekaji mikono pia ulizingatia aina ya mkono anayowekewa mtu kwa mfano kama mtu aliwekewa mkono wa kuume au kulia hii ilimaanisha kuwa huyo atakuwa mkubwa na aliyewekewa wa kushoto huyo atakuwa mdogo hata kama ana umri mkubwa
·         Baadhi ya watu huofia swala la kuwekewa mikono kwa kuogopa kurithishwa mambo yasiyofaa lakini baadhi hupinga kwa kusema Mungu si dhalimu kile ambacho mtu anakiomba ndicho hupewa huwezi kuomba mkate ukapewa jiwe kwa baba yetu wa Mbinguni lakini ushahidi wakibiblia umeonyesha watu kuponywa kuombewa neema au kujazwa Roho kupitia uwekaji mikono jambo la kukumbuka ni kuwa bado imani ndio ufunguo mkuu kwani muwekaji hana kitu cha ziada anachoweka yeye ila Mungu
·         Swala zima la uwekaji mikono tunaweza kusema ni la kibiblia na msingi wake ni kuwatakia neeema wale ambao aidha wanahitaji uponyaji au ujazo au kuwekwa wakfu katika huduma na kadhalika hatuwezi kulipinga kinachotahadharishwa ni kuwa muwekaji mikono hapaswi kuwa na kiburi na kujifikiri ni yeye awezaye kufanya jambo hili kitu kama hiki Petro alimuonya Simeon mchawi ambaye alitaka kulitumia tendo la uwekaji mikono kama njia ya kujipatia heshima Matendo 8;18-24.
5; Matokeo ya ujazo wa Roho Mtakatifu.
1.       Utajaa na kufurika Roho maishani mwako
2.       Utahisi uwepo wa Mungu kwa ndani zaidi na kuufurahia
3.       Utahisi kujitoa kwa Mungu kwa hiyari zaidi bila kusukumwa
4.       Utahisi kumpenda Yesu zaidi na kuwapenda wengine
5.       Utakuwa na ufahamu mzuri zaidi wa neno la Mungu
6.       Utajihisi huru zaidi na utajisikia kumshuhudia Kristo kwa ujasiri
7.       Utakuwa na nguvu za kumtumikia Mungu na shauku ya kumtumikia itajengeka ndani yako
8.       Utakuwa na furaha na amani na mahusiano mazuri na wengine
6; Kujazwa kwa Roho Mtakatifu sio mwisho wa kutafuta ujazo huo.
1.       Wapentekoste wengi hapa ndipo walipokosea ni muhimu kufahamu kuwa kujazwa Roho Mtakatifu mara ya kwanza sio ndo mwisho wa kutafuta ujazo zaidi wa Roho Mtakatifu
2.       Kwa asili siku ya pentekoste uilikuwa ni mwanzo tu wa kazi ya mavuno kwa ajili ya ufalme wa Mungu lakini waliookolewa pia walipaswa kukaa katika ibada,mafundisho na kumtumikia Mungu na maombi  ujazo wa Roho utupelekee katika kumtumikia Mungu ndipo sa tutaona utendaji wake vipawa na Karama za Roho mtakatifu zikijitokeza na kufanya kazi kwa viwango vikubwa.

Karama za Roho Mtakatifu
Kuna karama nyingi sana na za aina mbalimbali na watu huzigawanya katika makundi mbalimbali kama wapendavyo karama hizi zote kwa ujumla zimegawanyika katika, makundi makuu matatu ambayo kwa ujumla wake yanagusa utatu wa Mungu yaani karama zitokazo kwa Mungu Baba na karama zitokazo kwa Mungu mwana na zile zitokazo kwa Mungu Roho ambazo ni maarufu zaidi kama karama za Roho na ambazo wengi huzifahamu 1Koritho 12; 4-6 hapo tunaona utatu woote ukihusika katika utoaji wa Karama
1.       Karama za kutenda kazi 1koritho 12;6 hizi hutoka kwa Baba
2.       Karama za huduma 1koritho 12;5 hizi hutoka kwa Bwana yaani mwana au Yesu
3.       Karama za Neema au karama za Roho 1 Koritho 12;4 hizi hutoka kwa Roho.
     Nyingi ya makundi ya karama hizo hapo juu zimegusiwa katika kitabu cha Warumi, Waefeso na kitabu cha Wakoritho kwa mantiki ya kimakundi niliyoiorodhesha hapo juu kwa mfano
·         Karama za kutenda kazi au za masaidiano ziko katika Warumi 12;6-8 “Energemata”
·         Karama za huduma au maongozi ziko katika Waefeso 4;11 “Diakonai”
·         Karama za neema au za Roho ziko katika 1Koritho 12;7-11 “Charismata”
Ziko njia mbalimbali za namna na jinsi watu au waalimu huzigawanya karama hizi katika kusudi la kuzifundisha kwa wepesi kulingana na mwalimu anavyopendelea kwa mfano wako ambao huzigawa hivi
1.       Wako wanaozigawa sawa na mtiririko wa kibiblia
2.       Wako wanaozigawa kulingana na jinsi zinavyofanana kwa asili
3.       Wako wanaozigawa katika mfumo wa kimatukio kwa mfano mitume,waalimu,na wainjilisti wanawaweka katika kundi la Karama zinazosafiri wakati Mchungaji huwekwa katika kundi la karama inayotulia sehemu moja au ya maongozi na kusaidia
4.       Wengine huzugawa kulingana na jinsi  zinavyofanya kazi au za sirini na za wazi za kawaida na za kupita kawaida vyovyote vile mtu atakavyozigawa jambo la msingi ni namna tunavyoweza kuwasaidia wakristo kuzielewa na kutambua karama walizo nazo na kuzitumia hilo ndilo jambo la msingi
Kwa uchambuzi yakinifu niliouchagua ningependa kurudi katika makundi yale matatu ya karama ili tufanye uchambuzi utakaokidhi matakwa ya jamii yetu haya ni makundi yale makuu ya Karama za kutenda kazi, karama za huduma na karama za Roho na ingawa msisistizo wetu ni katika karama za Roho tutazigusia zile nyingine japo kwa mukhutasari
1.       Karama za kutenda kazi 1koritho 12;6 hizi hutoka kwa Baba
     Karama hizi ziko kwa wingi katika Warumi 12; 6-8 hizi ni karama za kutenda kazi ambazo pia huitwa karama za masaidiano hizi ni maalumu kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la mahali pamoja na zinapaswa kuwako kwa kila muamini ziko pia kwa ajili ya kusaidia utawala wa kichungaji katika kanisa la mahali pamoja labda ndio maana huitwa pia karama za masaidiano 1Koritho 12; 28
2.       Karama za huduma au maongozi katika Waefeso 4;11-16
Hizi ni karama zinazoshughulika na ustawishaji wa kanisa karama hizi Mungu huzitoa kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu kwa kuwajenga kiroho hata wafike kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo au wafikie kukua kiroho au kukomaa Kiroho.
       3.  Karama za Roho hizi ni karama za madhihirisho ya Roho Mtakatifu ndani ya mtu aliyeokoka kumwezesha mtu huyo kufanya mambo mbalimbali kwa kusudi la kulijenga kanisa, kulitia moyo na kudhihirisha kazi za utendaji wa Mungu katika meneo mbalimbali ya maisha na kusababisha watu kuamini au kutiwa moyo na kujengwa.

 Uchambuzi wa karama za aina Mbalimbali.
Karama za Huduma
Ni karama kwa mtu aliyeokoka kumwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kuhudumu katika neema aliyopewa na Mungu na kutimiza jukumu lake kama Mtume, Nabii, Mwinjilisti, Mchungaji au Mwalimu.
Mtume.
      Neno mtume limetokana na neon la asili la kiyunani “apostolic” ambapo tunapata neon apostle la kiingereza maana ya neno hili ni mjumbe au aliyetumwa au yeye aliyetumwa amwakilishe mwingine au yeye anayewakilisha mamlaka kutoka kwa yeye aliyemtuma. Yesu kristo ndiye mtume mkuu.Mitume wale 12 walikuwa tofauti na mitume wengine ukiondoa Yuda  wao watahukumu kabila kumi na mbili za wana wa Israel wakati wa ufalme wa Mungu au utawala wa masihi, neon mitume pia lilitumiwa kwa watu wengine walioitwa na Kristo baadaye katika huduma kama Epefrodito, Barnaba, Paulo, Andronibas na Yunisi
Sifa za Mtume
·         Walitakiwa kuwa mashahidi wa huduma mafundisho na ufufuo wa Yesu yaani walioamini kabla ya siku ya Pentekoste Matendo 1;21-22
·         Paulo Mtume anaingia katika sifa hii kwa sababu alifundishwa injili yake na Yesu Kristo mwenyewe hivyo kwa namna moja au nyingine alimuona Yesu na hivyo alikuwa na uhakika kuwa yu hai Wagalatia 1; 11-122;6-9.
·         Ofisi ya Mtume ilipewa watu maalumu tu  na ilikuwa ni kwa kusudi maalumu hivyo si kila mtu angeweza kuwa Mtume na hizi ni sababu za kibiblia
i.         Mitume walikuwa 12 tu na walifundishwa na Yesu mwenyewe
ii.       Walikuwa na kazi maalumu ya kuweka msingi wa kanisa na kuandika neon la Mungu yaani agano jipya na kustawisha viwango vya ukristo vilivyohitajika kwa mafundishao na maisha ya ukristo.
iii.      Majina yao yameandikwa katika misingi ya mawe 12 ya Yerusalem mpya
iv.     Watahukumu kabila 12 za wana wa Israel wakati wa millennium au utawala wa Masihi wa miaka 1000.
v.       Walimuona Yesu baada ya ufufuo na walikuwa ni mashahidi waliojionea kwa macho kuwa Yesu amefufuka
Huduma ya kitume.
       Wengi wanaojiita mitume leo sio mitume isipokuwa huenda labda wana huduma ya kitume na huduma ya kitume inaweza kuonekana katika maeneo makuu manne ambayo yanathibitisha kuwa hii ni huduma ya kitume
1.       Kunakuwa na Ishara na maajabu katika huduma zao Matendo 2;43;512.
2.       Ni waalimu wa neno la Mungu Matendo 2;42 na wenye mzigo wa huduma ya Neno la Mungu na msingi wa mafundisho ya kweli katika ukristo Matendo 4;33,5;32.
3.       Wana mzigo wa kustawisha makanisa au kanisa na likasambaa au kukua kwa haraka au kuwa na mzigo wa kukamilisha agizo kuu katika nguvu za Roho Mtakatifu na kulieneza katika kila sehemu ulimwenguni na kuweka watumishi kulisimamia.
4.       Wana ujasiri wa ajabu wa kumtii Mungu kuliko wanadamu na kuwa tayari hata kupoteza maisha yao kwa ajili ya injili wakiwa na uwezo mkubwa wa kujikana nafsi zao kwa ajili ya injili ni wa kwanza katika kanisa 1Koritho 12;28.
5.       Watu wootwe wanaojiita mitume leo ni lazima wahakikishe kuwa wanapimwa sawa na vigezo vya neno la Mungu Mathayo 24; 24 Ufunuo 2; 2.
Nabii
Nabii kwa kiyunani ni apothengomai yaani muonaji au msemaji kwa kiebrania Navi au Nabi katika agano jipya kazi kubwa ya Manabii kama inavyoainishwa na agano jipya ni wasemaji kwa niaba ya Mungu na wenye kutia moyo watu wa Mungu au kanisa la Mungu
Manabii agano la kale
-          Walizungumza kwa niaba ya Mungu
-          Walifundishwa na Mungu na kuelekezwa ni ni cha kusema
-          Wengi wa Mnabii wa agano la kale walikuwa wasemaji kuliko waandishi
-          Kutabiri ilikuwa ni sehemu ndogo sana ya huduma ya Manabii mengi waliyoyasema yalihusu wakati uliokuweko na mambo yaliyokuweko
Manabii agano jipya.
-          Yesu ni nabii mkuu zaidi ya wote na alikuja kutimiza kile kilichosemwa na Manabii katika agano la kale
-          Manabii wengi wa agano jipya hawaleti neno jipya bali ufunuo Fulani kuhusu neno na kweli Fulani zinazopaswa kufanyiwa kazi Yohana 13;2-3
-          Yuda na Sila walikuwa Manabii Matendo 15;32 walitia moyo na kuwajenga waamini waliwatia nguvu 1Koritho 14;3, wao walitia moyo na kuonya lakini hawakumshambulia mtu moja kwa moja, Agabo alitumiwa kutabiri Matendo 11;28,21;11
-          Wale ambao walitumiwa pia kwa karama ya unabii mara kwa mara waliitwa Manabii 1Koritho 14;29,32,37,Biblia pia imeonya kuweko kwa Manabii wa uongo hivyo ni muhimu wakajharibiwa au kupimwa sawa na neno la Mungu 1Yohana 4;1 kazi kubwa ya ujumbe wa nabii ni kujenga
                  
Kazi kubwa za nabii kama zinavyoonekana katika mchoro huo hapo juu, kutabiri ilikuwa ni sehemu ndogo tu ya kazi za Manabii
Mwinjilisti
     Jina linatokana na neno la kiyunani Evangelists ambalo maana yake yeye anayetangaza habari njema kimsingi hawa ni watu wenye karama ya kushuhudia watu wasioamini na kufanikiwa kuwaleta kwa Yesu na kumuamini na kupokea wokovu Yesu alikuwa ni mwinjilisti mkuu sana  wainjilisti kwa kawaida hueneza habari njema  mzigo wao mkuu ni kuwaona au kuuuona ulimwengu ukimjia Mungu kwa kuokolewa lengo lake kuu ni kuwapata wenye dhambi, timotheo inaonekana kuwa huduma yake ya msingi ilikuwanui kufundisha ndipo Paulo Mtume alipomtia moyo kuhubiri injili pia 2Timotheo 4;2,5, 1Timotheo 1;18,4;14 Bila kujali kuwa wanatumia sauti kubwa au ndogo wanarukaruka au la wainjilisti wamejaliwa ushawishi wa watu wengi kukubali injili inapohubiriwa na wao
-          Mfano mzuri wa mwinjilisti halisi katika Biblia ni Filipo alihubiri huko Samaria na Samaria ikalikubali neon la Mungu na kumuamini Kristo 8;4,5,35 wengi waliamini na kubatizwa Matendo 8;6,12
-          Miujiza mingi mikubwa iliambatana na huduma ya uinjilisti pamoja na kufunguliwa kwa watu waliokuwa na mapepo Matendo 8;6,7
-          Wainjlilisti walihubiri watu wengi na wakati mwingine watu wachache au hata mtu mmoja filipo aliongozwa kumuhubiri towashi wa Ethiopia Matendo 8;26 huduma ya uinjilisti ilimfanya aende mji kwa mji Matendo 8;40  wanachotakiwa wainjlisti ni kuihubiri injili ya kweli Wagalatia 1;8-9
Mchungaji na Mwalimu
      Kuna uhusiano wa karibu kati ya mwalimu na Mchungaji hii inaonekana katika Maandiko kuunganishwa Efeso 4;11 ni nini maana ya Mchungaji?
Pastor kiingereza kwa kiyunani linatumika neon poimane yaani kiongozi wa kanisa la mahali pamoja kwa asili neon hilo lilitumika kama Poimaimo yaani Mchungaji wa kondoo kazi ya Mchungaji ni kuwalinda au kuwalea kondoo wa Mungu Kristo yesu alikuwa Mchungaji mwema Mchungaji anatarajiwa pia kuwa mwalimu huduma ya ualimu ndiyo inayolifanya kanisa kukua zadi kuliko nyingine Mchungaji lazima awe mwalimu pia watu wa Mungu wameletwa kwako ili uwaelekeze, kupoteza kondoo ni dhambi Mchungaji anayeshindwa kuwaongoza kondoo na kuwafukuza ameshindwa kazi ya kichungaji Mungu hatupi watu wakamilifu anatupa ili wakamilike kama umeshindwa kuwasaidia wakamilike unataka nani awakamilishe? Galatia 6;1-6 Yakobo 5;19-20. Mchungaji kama mwalimu lazima akumbuke kuwa tumepewa Roho Mtakatifu yeye ni mwalimu mkuu hivyo ni lazima tukubali kufundishika Appolo alikuwa mwalimu mzuri lakini pia alikuwa akifundishika matendo 18;26 hakuna mwalimu mzuri ambaye hajapata kuwa chini ya waalimu wengine hata Yesu alikaa chini ya waalimu Luka 2;46. Jukumu kubwa zaidi la mwalimu ni kuwapa watu maarifa na kuwafunulia neon la Mungu wapate kulifahamu kwa kusudi la kuliiimarisha kanisa.

Uchambuzi wa karama za Roho.
Karama za Roho Mtakatifu ziko nyingi sana kwa ujumla karama haziesabiki laki ni tutachambua baadhi hususani zile ambazo zinzjulikana sana kwa sababu Paulo aliziorodhesha katika 1koritho 12;4-8 na zaidi Orodha hii haimaanishi kuwa ndio zimeisha lakini Paulo alikuwa anatoa mwanga tu kuhusu utendaji wa karama ili tuzifahamu kwa urahisi tutazigawa katika makundi makuu matatu yafuatayo;-
*      Karama za  uweza au madhihirisho
-          Imani au neno la mamlaka
-          Uponyaji
-          Miujiza
*      Karama za mafunuo
-          Neno la Hekima
-          Neno la Maarifa
-          Kupambanua roho
*      Karama za Usemi
-          Aina za Lugha
-          Tafasiri za lugha
-          Unabii

Uchambuzi karama za uweza.

Imani au neno la mamlaka.
    Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka inayowekwa na Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kuamini  au kutamka neno katika Mungu na kusababisha Muujiza mfano ni  1Koritho12;9,13;12, Mathayo 21;21-22, Marko 9;23-24,11;22-24, Luka 17;6, Matendo 3;1-8,6;5-8,  Yakobo 5;14-15.

Uponyaji
    Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka inayowekwa na Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kufanya maombezi yanayosababisha kuukarabati mwili au kuurejesha katika hali yake ya kawaida bila kutumia akili za kibinadamu mfano Mathayo 4;23-24,8;16,9;35,10;1,8 Marko 1;32-34 Yohana 6;2,14;12 matendo 4;30, 5;15-16.19;11-12 n.k

Miujiza
    Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka inayowekwa na Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kufanya maombezi yanayosababisha miujiza kutokea ikiwemo kutoa pepo mfano ni Mathayo 4;23,8;16,10;1,8,13;54,Marko 1;32-33,3;15, 6;13,16;17,Luka 4;40-41,9;1,10;17,Yohana 7;3,10;25 Matendo 2;22,4;30,Galatia 3;5,n.k
Neno miujiza katika Lugha ya kiyunani Greec linagawanywa katika makundi makuu manne

1.       Semeion – ambalo maana yake ni Ishara Luka 23;8, Matendo 4;16.
2.       Teras – ambalo maana yake ni  Maajabu,Mambo ya kushangaza Matendo 6;8
3.       Dunamis - ambalo maana yake ni miujiza ya kupita kawaida Matendo 19;11,Matendo 2;22
4.       Paradoxon – ambalo maana yake ni Mambo mageni au ya ajabu Luka 5;26

Uchambuzi wa karama za mafunuo.

Neno la hekima
   Hii ni Karama kwa mtu aliyeokoka inayowekwa na Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kulitumia neno la Mungu au ujumbe wa hekima kwa ajili ya kutatua tatizo Fulani lenye utata mfano matendo 6;3,1koritho 12;8 13;2,9,12 au Marko 12;13-17.

Neno la Maarifa.
  Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kwa Roho Mtakatifu kuwa na uwezo wa kufahamu jambo lililofichika katikamaisha ya binadamu na kuleta ufumbizi katika mazingira ya kweli ya kibiblia Matendo 10;47-48,13;2,15;7-11 Matendo 5;9-10 n.k

Kupambanua roho.
   Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo kupitia Roho Mtakatifu kutambua kuwa ni roho gani inatenda kazi kati ya roho ya mwanadamu, ya Shetani na Roho wa Mungu ili kuhakiki kama kinachotenda kazi ni cha kimungu? 1koritho 12;10,14;29 Matendo 2;4-11, Matendo 13;8-12; 16;16-18.

Uchambuzi wa karama za usemi.

Aina za lugha
   Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka chini ya uweza wa Roho Mtakatifu kumwezesha mtu huyo kuongea au kusikia Lugha mpya ya wanadamu au ya malaika ambayo hajawahi kujifunza 1koritho 12;10,28,30,13;1Matendo 2;4-11

Tafasiri za Lugha.
   Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka inayowekwa na Roho Mtakatifu kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kufasiri lugha au kinachoongelewa ambacho watu na yeye hawakijui bila kutumia akili 1Koritho 12;10,30,14;5,13,26-28 mfano Daniel aliweza kusoma maneno mene mene …………

Unabii
    Hii ni karama kwa mtu aliyeokoka kumuwezesha mtu huyo kuwa na uwezo wa kupokea na kutoa ujumbe kwa kanisa kupitia Roho Mtakatifu kwa kusudi la kujenga au kutia moyo au kuonya bila kutumia akili Luka 1;40-45,Luka 1;46-55.luka 1;67-79 Matendo 2;14 21;9,10-11

MUHKTASARI KUHUSU ROHO MTAKATIFU
Kwa muhktasari tunaweza kusema kuwa Roho Mtakatifu ni Suluhisho la matatizo yoote katika kanisa au kiboko cha matatizo yoote na hii ndio maana nyakati za kanisa la kwanza alipewa kipaumbele kinachostahiki Luka 24;49 Matendo1;8 nyakati za kanisa la kwanza swala la Roho Mtakatifu lilipewa kipaumbele kama swala la sala ya toba Matendo 8;14 na 19;1-7 kama kuna upungufu wa aina yoyote leo katika kanisa basi tunapaswa kurudi kwenye msingi na kujiuliza kwa ni nini wenzetu walimpa kipaumbele hii ni kwa sababu walijua kuwa;-

Ni suluhisho kwa tatizo la Kimaongozi
     Kama kuna jambo lina shida kubwa hapa duniani basi swala la maongozi linashida kubwa na ndio maana tunashuhudia leo migogoro mikubwa ya kimaongozi dunia haitaweza kusahau viongozi waovu waliopata kuweko kama Mao, Hittler Idd amin Nimrodi sadaamu na Osama n.k ambao wameiongoza dunia au mataifa yao katika maumivu na kuuwa wengi suluhishi ni kuwa na viongozi waliojaa Roho Mtakatifu “Spirit Filled Leaders” hili Farao aliliona Mwanzo 41;38, Daniel 5;5-12,Hesabu 11;10-17 Isaya 63;10-14. Makuhani Manabii na wafalme katika Israel ilibidi wapakwe mafuta ili wapokee Roho ndipo waongoze.

Ni suluhisho la uadui
     Roho Mtakatifu pia ana uwezo mkubwa wa kuwadhibiti maadui na kuhakikisha usalama wetu hasa pale wanapotuandama na kutusakama 2 Falme 6;8-12,1Samuel 19;18-24 hivyo mahali alipo Roho wa Mungu pana usalama

Ni suluhisho la uonevu
     Nyakati za agano la kale wana waisrael walipoonewa na maadui walio wazunguka Mungu aliwainulia waamuzi na kuwajaza kwa Roho ili kukomesha uonevu Waamuzi 14;5,6,15;3,14-16. Watu wanapoonewa na shetani msaada wa pekee utaupata kwa mtu mwenye Roho wa Mungu

Ni suluhisho la upinzani wa kidini
    Tunaishi katika wakati mgumu ambapo kuna changamoto za aina nyingi zikiwemo za kidini uislamu unakua kwa kasi na huku wanawashambulia wakristo kwa namna nyingi sana huko ulaya uislamu unakua kwa kasi hakuna namna yoyote ile tunaweza kukabiliana na changamoto hizi isipokuwa kwa Roho Mtakatifu Matendo 6;8-10,7;55 mitume walipokutana na upinzani wowote wa kidini hawakuogopa kwani walikuwa wakijaa Roho Matendo 5;17;-29,4;5-14

Ni suluhisho dhidi ya nguvu za giza uchawi.
   Nyakati hizi tulizo nazo ni nyakati ambazo pamoja na maendeleo yoote yaliyoko bado uchawi unakua kwa kasi sana huko ujerumani watu wanakusanyika katika misitu mmoja ili kujifunza uchawi pia ziko website ambazo zinafundisha uchawi katika mitandao ya intrenet  
                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                Biblia inaamini kuwa uchawi upo na namna ya kukabiliana nao lazima ujae Roho Mtakatifu kutoka 7;10-13,Daniel 5;7.Hesabu 23;7-8,22-23 matendo 8;4-21,13;6-12 tusipokuwa makini tunaweza kuabudu na wachawi hata katika makanisa ya kiroho

Ni suluhisho dhiidi ya mateso na uonevu wa ibilisi
Roho Mtakatifui anapokuwa juu ya mtu hushughulika pia na maonevu yawapatayo watu Yesu alifanya kazi duniani kama mwanadamu akimtegemea Roho Mtakatifu watu wa Mungu wanateseka huduma mahospitalini haziridhishi inahitajika kanisa liwe na majibu ya matatizo na shida za watu Ni kwa Roho wa Mungu tu tunaweza kufanya hivyo Luka 4;18-19,Matendo 10;38.

Ni suluhisho kwa woga kukata tamaa na kukabiliana na changamoto za ulimwengu huu
 Matendo 2;1 Petro aliyekuwa muoga sasa anaonekana kusimamia kwa ujasiri kwa sababu amejazwa Roho,anatusaidia katika kuishi maisha matakatifu na kuwa mbali na sheria ya dhambi na mauti warumi 8;2

Nisuluhisho la hekima tunapokuwa katika hali ya kutokujua nini cha kufanya
     Mara nyingi katika ulimwengu huu tumekutana na changamoto nyingi kiasi cha kuchanganyikiwa na hata kufikia hatua ya kutokujua nini cha kufanya tunamuhitaji roho mtajkatifu katika kutusaidia kutatua matatizo 1 falme 3;16-27 matendo 15,Kufanya uamuzi 1falme 12;4-11 kuhimili migandamizo kama ya Ayubu Ayubu 1.

Hitimisho
 Nina mshukuru Mungu aliyenisaidia kuandaa mafundisho haya kuhusu Roho Mtakatifu ni imani yangu kuwa yatakuwa msaada mkubwa kwa kanisa la Mungu Hapa nchini na nje ya nchi Yatendee kazi yaliyomo humu na hii itatufanya sisi waalimu kufurahia Baraka za Mungu pale tunapoona kile tunachokifundisha kikifanyiwa kazi na kuzaa matunda yanayo kusudiwa Mungu na akubariki Endelea kuniombea kwa habari ya huduma hii ili niweze kuwa Baraka kubwa zaidi kwako na kwa kanisa la Mungu Ubarikiwe sana Wako katika utumishi Mchungaji Innocent Mkombozi Kamote

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Unavitabu ulivyochapisha Mason haya