Mathayo 12: 38-42 Biblia inasema “38. Hapo baadhi ya waandishi na
Mafarisayo wakamjibu, wakasema, Mwalimu, twataka kuona ishara kwako. 39. Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na
cha zinaa chatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya nabii Yona. 40. Kwani kama vile Yona alivyokuwa siku
tatu mchana na usiku katika tumbo la nyangumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu
atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi. 41. Watu wa Ninawi watasimama siku
ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watawahukumu kuwa wamekosa; kwa
sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona.
42. Malkia wa kusini atasimama siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki,
naye atawahukumu kuwa wamekosa; kwa sababu yeye alikuja kutoka pande za mwisho
za dunia ili asikie hekima ya Sulemani, na hapa yupo aliye mkuu kuliko
Sulemani.”
Kifungu hicho hapo juu cha
maandiko ni cha muhimu sana na tunapokifanyia uchambuzi yakinifu itatupa mwanga
wa kumfahamu Yesu Kristo kwa kina na upana na urefu zaidi, kifungu hiki ni
matokeo ya mjadala uliokuweko kuhusu Yesu Kristo, Baada ya Wayahudi hasa jamii
ya mafarisayo kumnenea Yesu maneno
mabaya zaidi, Baada ya kuwa Yesu amemponya mtu aliyekuwa ana pepo, kipofu na ni
Bubu, Mathayo 12:22-23, Muujiza huu
uliwashangaza watu na kumfanya Yesu aanze kukubalika miongoni mwa jamii kuwa
“MWANA WA DAUDI” hii ilikuwa ni wazi kuwa walikubali kuwa Yesu ndiye MASIHI, ni
wazi kuwa kwa kazi hii na nyinginezo alizozifanya Yesu zilipelekea watu
kumuamini na kuondoa shaka kuwa ndiye mfalme ajaye kwa JIna la Bwana, Hata
hivyo kwa sababu ya wivu wa Mafarisayo ambao waliona Yesu anaheshimika zaidi na
kuwa gumzo kuliko wao waliamua kwa makusudi kuharibu kibali cha Yesu kwa kusema
kuwa anatoa pepo kwa nguvu za mkuu wa Mapepo Belzebuli (Mathayo 12:24)
Yesu Kristo akitambua hilo alitoa
hutuba kali sana ya maonyo dhidi ya watu wanaopinga kazi ya Mungu Roho
mtakatifu, na zaidi ya yote aliwaonya watu kuhusu kuzungumza maneno yasiyo na
maana kwa vile watatoa hesabu kwa kila neno lisilo na maana wanalolitoa katika
vinywa vyao, Mathayo 12:33-37.
Baada ya hutuba hii ya Yesu
ambayo ilikuwa kali na yenye maonyo baadhi ya Mafarisayo waliogopa sana Lugha
“Hapo” inatumika kuonyesha kuwa iliwalazimu sasa waombe ishara ya kumfahamu
Yesu vema kuwa yeye ni nani, Tupe ishara itakayotusaidia kukutambua wewe ni
nani? Ndipo Yesu aliwajibu kwamba watamtabua kupitia Ishara kuu mbili.
1.
Ishara
ya Nabii Yona.
Yesu aliwaeleza
kwa uwazi kuwa Ishara ya kumtambua Masihi iko wazi, ishara hii ndiyo
iliyowavutia watu wa Ninawi wakatubu na kumgeukia Mungu kupitia mahubiri ya
Yona, Mathayo 12:38-41, Kimsingi Yesu alitaka kukazia kuwa kile kilichomtokea
Yona kilikuwa ni ishara halisi, na kilikuwa ni kivuli cha kumtambua Masihi, ambaye
Yesu alikazia kuwa ni mkuu kuliko Yona, Yesu alikazia kuwa namna njema ya
kumtambua yeye nip ala atakapokufa na kufufuka siku ya Tatu, hii ndio kazia
kubwa ya ukombozi itakayowavuta wengi katika ufalme wa Mungu.
2.
Ishara
ya Malkia wa Sheba.
Yesu aliwapa
Mafarisayo Ishara nyingine ya muhimu. Ambapo sasa anaeleza kuhusu Malkia wa
kusini yaani Sheba kwamba alitoka mbali sana pande zamwisho wa Nchi kuja
kusikiliza Hekima ya Sulemani, Yesu ni kama alikuwa anakazia kuwa njia nyingina
ya kumtambua ni kumsikiliza, usikivu ungeliwasaidia kujua kuwa hakuna mwingine
anayeweza kunena au kutenda katika kiwango kama cha Yesu, Mathayo 12:42 hata hivyo
mahali hapa ndipo paliponisukuma zaidi kufanya Uchambuzi hususani Yesu
alipohitimisha kuwa malikia huyu alisafiri kutoka mbali kusikiliza Hekima ya
Sulemani, hata hivyo Yesu alitamka wazi kuwa Yeye ni mkuu kuliko Sulemani.
Suleimani ni mfalme aliyeishi kwa
anasa na ufahari wa hali ya juu, mfalme huyo alikuwa na Hekima na ufahamu na
maarifa ya hali ya juu sana kuliko wafalme wote ambao wamepata kuweko, Biblia
inasema kabla yake hajakuweko na badala yake hatokuweko 1Wafalme 3:9-13, 4;29-34 unaweza kuona!, wengi waliosikia Hekima ya
Suleimani katika enzi zake walisafiri kutoka mbali ili kwenda kumsikiliza,
Lakini ziara ya kifahari na maarufu sana na iliyoelezewa kwa kina ni safari ya
Malkia wa Sheba au Ethiopia ambaye alikwenda kwa mikogo mingi na mikubwa 1Wafalme
10:1, 2Nyakati 9:1-6 Biblia inasema malkia huyu alikwenda akiwa na maswalai
magumu sana “She came to Jerusalem to test him with Hard Questions” pamoja na
ziara yake ya kifahari na zawadi kibao alizozibeba alipofika Yerusalem kwa
Suleimani alijibiwa maswali yake yote na
mambo yake yote hata aliyokuwa ameyaficha sirini, hakuna kilichofichika kwa
Suleimani, alitosheleza mahitaji yake yote na hisia zake zote zilijibiwa na
kuzidi.
Dunia ya leo ina maswali magumu
mengi yasiyo na majibu, pamoja na kuendelea na kukua kwamaarifa na uvumbuzi wa
kisayansi na Teknolojia, Watu wanazidi kuharibikiwa dunia imejaa hekina ya
uharibifu, wizi,ufisadi,uchochezi,uchoinganishi, majungu na fitina, kuliza
wengine, kutoa mimba udanganyifu, na hakuna majibu ya maswala muhimu katika
matatizo ya watu, Sulemani alikuwa na ujuzi zaidi ya wa kibailojia, Chemistry,
Physics, aliishi kwa anasa kuliko mtu yeyote, mwisho aliona hekina na maarifa
bila ya Mungu ni upuuzi au ubatili,alishauri watu kumkubuka Muumba wao siku za
ujana wao, Muumba huyu ndiye mkuu kuliko Sulemani, Yesu Kristo anatajwa kama
Hekima yetu 1Wakoritho 1:18 kwa
kiyunani Epignosis sofia, Full of wisdom Knowledge and Understanding, yesu
aliposema Hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani alimaanisha Yeye ndiye
aliyemuumba huyo Sulemani, Yeye ndiye mwenye majibu yote hata ya mambo magumu,
Yeye ndiye Masihi, ni zaidi ya mfalme Sulemani, watu watatoka kila pande za
dunia kumjia yeye, na atawahukumu wote waliomkataa yey.
Hapa yupo aliye mkuu Kuliko Sulemani.
Maoni 1 :
Mungu azidi kukutumia pastor Umonifaa sana kama baba kwangu...
Chapisha Maoni