MAFUNDISHO POTOFU WAKATI WA KARNE YA
PILI.
Marcionites.
Ni imani iliyoanzinswa na mtu
aliyeitwa Marcion aliyeishi kati ya
Mwaka wa 100-160 alizaliwa huko Sinope-Pontus yaani Uturuki ya Leo inaaminika kuwa
huenda alikuwa mtoto wa askofu wa mji huo Imani yake ya uzushi ilianzia huko Rome
kati ya mwaka 140 hivi Yeye alisisitiza
zaidi sana kuhusu Upendo wa Mungu kuliko
haki yake na alilipinga vikali agano la
kale
Alikuwa mpinzani mkubwa wa
wayahudi na pia alikataa sehemu kubwa ya agano jipya ambayo alifikiri kuwa
inawapaka mafuta wayahudi au ina uhusiano na imani ya kiyahudi aliamua kuandika
Injili yake ambayo ilikuwa ikifanana sana na ile injili ya Luka ingawaje
alikuwa ameruka Karibu 1/3 ya injili hiyo.
Alitengwa na kanisa kama mzushi na alianzisha
imani yake hiyo watu wake walijikana na waliacha kuoa , imani ilikuwa ana kupata nguvu ikiwa na askofu
wake pamoja na sacrament ya Ubattizo na
meza ya Bwana lakini hawakutumia kabisa mvinyo wa divai. Walipinga swala la
Incarnation na maswala ya Yesu kusulubiwa, aliamini katika umilele wa vitu
vyote, waliendelea kuweko mpaka mnamo karne ya nne na imani hizi zilipingwa
vikali na wakristo akiwemo Justin,
Irenaeus, and Tertullian.
Montanists.
Ni mojawapo ya imani ya kizushi iliyoanzia wakati wa karne
ya pili imnani hii ilianzshwa na Nabii Montanus aliyeishi huko Phyrigia ambayo
sasa ni sehemu ya uturuki imani hii ilianza mnamo mwaka 156, Bwana Montanus
alitokea katika kijiji kidogo na alianza kutoa unabii akidai kuwa amesikia
sauti ya Roho Mtakatifu,Yeye na vijana wawili wa kike Prisca na Maximilla
alizunguka akihubiri na kufundisha katika Asia ndogo, alifundisha kuwa mtu
akianguka katika neema hawezi kukombolewa tena, waamini walitiwa moyo
kuyatafuta mateso na sio kuyakimbia,
Imani hii iliweka mkazo na kukemea ubaridi katika kanisa
kwani wakati huu kanisa lilianza kupoa na kuchukuliana na ulimwengu walikuwa
wakijiandaa na ujio wa Kristo wa mara ya pili na hawakujali maswala ya kawaida
zaidi ya kujiandaa na kuja kwa Bwana mnamo mwaka 177 kiongozi wa kanisa
alihofia mgawanyiko wa kanisa na hivyo aliitenga imani ya Montaninism imani hii
ilipata nguvu kwa sababu iliungwa mkono na mwanatheolojia wa kipoman Tertulian
mpaka karne ya 6 imani hii ilikuwa imetoweka.
Gnosticism.
Ni moja ya imani potofu ya kale na ya zamani zaidi au ya
muda mrefu zaidi, Neno Gnosticism lina tokana na neno la kiyunani Gnosis ambalo
maana yake ni Maarifa au ujuzi, imani hii ilichanganya maswala ya kipagani na Ukristo.
Walifundisha kuwa baada ya Mungu mkuu kuna miungu mingine
mingi midogomidogo ambayo baadhi yao ni mibaya na baadhi ni wema na kuwa
kupitia wao ulimwengu uliumbwa ukiwa na Mchanganyiko wa mambo mema na mabaya
Wanafundisha kuwa Kristo ni miongoni mwa miungu hiyo na kuwa
uweza wa uungu ulikuwa juu yake kwa muda, waliamini kuwa maandiko ni hadithi na
kuwa unaweza kutafasiri maandiko haya kama kila msomaji apendavyo na aonavyo
KWA NINI IMANI POTOFU HUTOKEA?
Jibu moja jepesi kwa nini imani
potofu hutokea ni kwa sababu kanuni za kutafasiri maandiko hazikuweko au
haizizngatiwi, kwa msingi huo ni Ushauri wa somo hili kwamba kila mwanafunsi wa
Biblia ni lazima ajifunze kanuni za
kutafasiri Biblia na kufahamu kuwa maandiko hayawezi kutafasiriwa kama kila mtu
apendavyo Paulo alimwambia Timotheo katika 2Timotheo 2;15 kuwa ni muhimu kwake
kulitumia neno la Mungu kwa halali kwa msingi huo hapa tunaelekeza maswala
kadhaa ya kuzingatia wakati tunapotaka kulitafasiri neno la Mungu.
1.
Ni
lazima uzingatie Mazingira.
Ni muhimu
kufahamu kuwa Biblia kwa mfano Agano la kale liliandikwa zaidi ya Miaka 3500
hivi iliyopita na huku wakati Agano jipya liliandikwa zaidi ya miaka 2000
iliyopita kwa msingi huo Mtafasiri wa
maandiko anapaswa kuzingatia swala zima ka Historia,
siasa, Falsafa na Tamaduni za
wakati huo kuwa zinatofautiana na za sasa
kwa msingi huo ni lazima Mtafasiri afikiri kuwa kifungu Fulani cha
maandiko kliwezaje kuwafaa watu wa nyakati zile na baadaye kuangalia kinawezaje
kutumiwa katika wakati tulio nao.
2.
Ni
lazima uzingatie Mabadiliko ya Lugha.
Ni muhimu
kufahamu kuwa lugha za asili pia zilizotumiwa kuileta Biblia kwetu zilikuwa
Kiibrania na kiyunani na sehemu chache kiaramu kwa msingi huo ni muhmu kufahamu
lugha hizo zilimaanisha nini kwa wakati ule na ukumbke kuwa maana ya meneo hubadilika
baada ya Karne kadhaa.
3.
Ni
lazima Uzingatia sheria ya Muktadha Context.
Watu wanaweza
kukengeusha maana halisi ya maandiko na kupata mafundisho ya uongo kama
Muktadha yaani kifungu cha maandiko hakitazingatiwa unapotaka kuchanganua maana
ya aya Fulani lazima uanze kujisomea kutoka juu ya aya hiyo na pia chini ya aya
hiyo kwa mfano katika Zaburi ya 116; 11b “Biblia inasema Wanadamu wote ni
waongo” lakini unaposoma andiko hilo vema kuanzia 11a utaweza kuona mwandishi
akiweka wazi kuwa “Mimi nalisema kwa haraka yangu” unaona?
4.
Ni
lazima maandiko unayotumia yawe yanaungwa mkono na maandiko mengine (Harmony).
Mara nyingi
waalimu wa uongo hujitungia Mafundisho yao
kwa tafasiri zao kumbuka kuwa 1Petro 1;20-21 Biblia inasema unabii
haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwanadamu
kwa msingi huo ni lazima maana ya ujumla ya neno la Mung iweze
kuzingatiwa na sio kamstari kamoja tu Zaburi 119;160 Unasema Jumla ya Neno lako
ni kweli.
5.
Ni
lazima ufanye kazi ya kutafuta maana iliyokusudiwa kisha uitumie. (Exegesis)
Neno la asili la
kuelezea au kutafuta maana linatokana na asili ya kiyunani Exegeisthai ambalo maana yake ni kuelezea kwa hiyo mtafasiri ni
muhimu kutafuata maana iliyokusudiwa na waandishi na andiko na kulinganisha
ukweli na maandiko mengine na kasha kuelezea maana inayokusudiwa na Biblia au
neno la Mungu na hapo ndipo mtu anakuwa amehubiri neno la Mungu na sio
kulisingizia neno la Mungu Eisogesis.
Kujitafutia maana yako mwenyewe na kuyasingizia maandiko.
6.
Ni
lazima uzingatie swala la kujirudia kwa unabii (Multiple Fullfillment.)
Baadhi ya unabii
una tabia ya kujirudia katika kutimizwa kwake kwa zaidi ya mara moja kwa mfano swala la kurudi kwa Yesu Mara ya
pili liko katika mazingira makuu mawili
Unyakuo na Ufunuo, au kunaweza kuwa na wapinga Kristo wengi katika historia
lakini hatimaye kutakuwa na mpinga Kristo mmoja tu.
7.
Ni
lazima wakati mwingine ukubaliane na maandiko kama yalivyo (Simplicity.)
Wakati wote ni
muhimu kuzingatia kwanza Tafasiri iliyowazi katika maandiko kabla ya kuanza
kufikiri kuwa ni mafumbo chagua maswala rahisi kuliko kujichagulia maswala magumu.
Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev Innocent Kamote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni