Jumanne, 26 Januari 2016

MFULULIZO WA MASOMO YAHUSUYO UTETEZI WA IMANI (APOLOGETICS) 1


Apologetics ni nini?
    Apologetics ni tawi la Theolojia linalohusiana na elimu ya Utetezi wa imani ya kweli ya Kikristo, ni neno linaltokana na asili ya kiyunani Apologia ambalo maana yake ni kulinda au kutetea au kujitetea ni neno lenye asili ya kimahakama sawa na utetezi unaotolewa mahakamani katika misingi ya Kisheria, kwa msingi huo Mteteaji huitwa Apologist jina ambalo lilitolewa kwa waandishi wa Karne chache za mwanzoni baada ya Kristo waliojitetea mbele ya Mtawala wa Kirumi na jamii kuonyesha kuwa Ukristo ni Falsafa na Maadili yaliyo juu zaidi ya Upagani ambao kwa asili ulikuwa ukiabudu asili wanautetezi wa Mwanzoni kabisa ni kama Aristides, Anthenagoras, Saint Justin Martyr, Minucius Felix, Tatian na Tertullian.

Ø  Tangu mwanzoni kabisa  mwa Karne ya Kwanza Kanisa lilipatwa na tishio la kuweko kwa Imani potofu
Ø  Jibu kubwa la kanisa lilikuwa ni kujibu hoja hizo kwa kuleta fundisho sahii na kushambulia fundisho lisilo sahii jambo hili ndio linaitwa Apologetics
Ø  Yuda anazungumza swala hilo la utetezi wa Imani katika Yuda 1;3 “Wapenzi nilipokuwa nikifanya bidii kuwaandikia habari ya Wokovu ambao ni wetu sisi sote  naliona imenilazimu kuwaandikia ili niwaonye kwamba muishindanie Imani  waliyokabidhiwa watakatifu  mara moja tu

Kwa kiingereza cha kisasa inafikiriwa kuwa neno Apology ni kuthibitisha ukweli pia inamaana ya kuitetea sheria au mtu ni utetezi wa Imani ya Kikristo au kanuni za kuitetea imani ya Kikristo ni taaluma inayohusu kupinga mawazo au imani hususani zilizo kinyume na Ukristo kwa hoja za Kikristo zinazokubalika
Ni tawi la Theolojia ya kikristo linalojihusisha na kuuthibitisha ukweli wa Imani ya Kikristo.

Tofauti ya Apologetics na Polemics.

Polemics ni neno la Kiyunani lenye maana ya Vita au shambulizi dhidi mawazo ya mtu mwingine maana nyingine ni pamoja na utetezi wa Imani dhidi ya upinzani kutoka ndani ya Kanisa Wakati Apologetics ni utetezi wa Imani ya Kikristo dhidi ya upinzanikutoka nje ya kanisa

Ufahamu kuhusu Maana ya Maneno mbalimbali yatumikayo kwenye somo hili.

*      Uzushi (Heresy) – Ni Mawazo yasiyo sahii au yasiyozingatia ukweli wa kimaandiko na ambao unapingana na misingi ya imani na amafundisho ya Kikristo
  Nyakati za kanisa la Kati Medieveal Church Wazushi walikuwa wanatengwa  na kanisa au kuuawa hata ingawaje mawazo yaliyofikiriwa kuwa ni uzushi kwa sasa ni moja ya misingi muhimu ya Imani kwa mfano Fundisho la Kuhesabiwa haki kwa Imani Justification by Faith ambalo ni fundisho linaloaminiwa na makanisa jamii ya kiprotestant.
*      Dini za uongo (Cults) – Neno Cults limetokana na Neno Cultus ambalo kwaasili maana yake ni ibada za uongo au ibada katika vitu visivyo halisi kwa mfano kuabudu jua n.k. Dini za uongo pia inaweza kuwa imani ya Kikristo na ambao wanakiri kuwa ni Wakristo lakini katika mafundisho yao kuna Imani za Uzushi ingawa kwa nje wanaweza kuonekana kubeba alama za Kikristo Linaweza kuwa kundi la watu wakristo lakini wanaoamini Mafundisho yanayotokana na Tafasiri za  mtu Fulani na kusababisha kumeguka au kuondoka katika mafundisho ya Msingi.
-          Cult ni mfumo wa kidini au imani ya Kiroho ambayo haiku sawa na misingi ya kweli ya imani , au watu waliokengeuka au imani potofu ambayo inafuata mafundisho ya mtu Fulani
-          Ni kundi la dini au watu wanaoshiriki imani Fulani za kiroho ambayo ni wazi kwa wengine kuwa ni potofu
-          Ni kundi la watu wenye Imani iliyopituka Extremist ambayo ina mlengo wa kumuamini mtu au kufuata falsafa za mtu Fulani mtindo wa maisha na tabia pia inaweza kuwa ibada ya sanamu au mashetani ibada za kichawi pia zaweza kuitwa Cults.
*      Dhehebu la uongo (Sect) – Kwa ujumla kuna tofauti ndogo na Cults  lakini sect ni dhehebu na linakuwa kubwa kuliko Cults na linawezxa kuwa na miaka mingi  lakini wao huziona imani kama za kipentekoste kuwa kama madhehebu ya uongo mfano wa Sect ni kama SDA. (Wasabato).
*      Orthodox – Ni neno la Kiyunani lenye maana ya wazo lililonyooka ni Imani ya asili na mafundisho ya kweli ya Dini mfano ni Wayahudi wenye imani kali Orthodox Judaism.
*      Dogma – Ni mafundisho ya Imani au Usemi wa kimaadili uliowekwa katika utaratibu maalumu  ambao umetamkwa na kanisa au kundi Fulani wakiamini kuwa ndio mafundisho yao ya Imani
- Ni utaratibu wa mafundisho ya Imani uliokusanywa naDini au dhehebu Fulani wakiamini kuwa ndio kweli zao kuu. Mfano ni Imani ya Nikea au mitume N.K.
- Ni itikadi au Falsafa au maadili au sera za kisiasa au kundi la kidini zinazoaminika kuwa kweli.
Kwa mfano Mwaka 1850 ilitangazwa na Pope wa wakati huo kuwa Mariamu alizaliwa pasipokuwa na dhambi kwa msingi huo hiyo imekuwa Dogma kwa wakatoliki.

Kazi za Apologetics.
§  Nyakati za Karne ya Pili kazi kubwa iliyofanyika ilikuwa ni kuutetea na kuulinda Ukristo na kuondoa madai
§  Kazi kubwa ya apologetic ilikuja kupata nguvu baada ya miaka kadhaa iliyofuata
§  Jukumu la kiapologetic kwa mfano lilidhihirishwa na Mtakatifu Agustino kwa kudhihirisha kuwa kazi ya kuutetea Ukristo haikuwa tu kwaajili ya kushughulika na Madai bali ni zaidi ya hapo
§  Dr. Ramm aliidhinisha wazi kabisa kwa kuonyesha kuwa Apologetic ina kazi kuu tatu
-          Kuonyesha Imani ya Ukristo jinsi ilivyo ya Kweli na kuwa imani nyinginezo nje ya Ukristo ni kama Hadithi
-          Kuonyesha Nguvu ya Ukristo katika tafasiri sahii za maandiko
-          Kukanusha fundisho lolote ambalo liko kinyume na Ukristo
Matawi makuu ya Apologetic.

Tunaweza kuligawa shamba la Utetezi katika maeneo makuu mawili
a.      Utetezi wa Kifalsafa (Philosophical Apologetics) – hii ni hali ya kuwasilisha mtazamo wa Kikristo kwa kutumia mawazo ya msingi na yaliyo sahii ni sawa na kuonyesha uungwana wa Kikristo
b.      Utetezi wa kihistoria (Historical Apologetics) – Hii kazi yake kubwa ni kutoa Ushahidi  kwa kuonyesha jinsi Ukristo ulivyokumba na Vikwazo mbalimbali na jinsi walivyoweza kujibizana navyo na kukabiliana navyo na kuwa matokeo yake yalikuwa nini

Katika somo letu hili tutakuwa tukiangalia kwa upana kuhusu tawi lile la kwanza la utetezi wa Kifalsafa

Kazi kubwa ya Apologetic Elimu ya Utetezi.
 Ni muhimu kufahamu kuwa kazi kubwa ya elimu ya utetezi sio kupinga tu bali ni pamoja na kujenga, kutoa msaada, kutoa ujasiri na kupinga mawazo ya kuchukuliana na ybatili na kuwasaidia wakristo katika swala zima la kuitetea imani yao.
 Kwa hiyo kazi ya utetezi sio kupinga tu ni kuwasilisha mawazo sahii kuhusu Kristo, kuilinda imani kutoka katika ujinga, kutokueleweka,na mashambulizi ambayo yanaweza kuharibu imani yetu
Kwa msingi huo ni muhimu kufahamu kuwa Elimu ya utetezi katika Ukristo kamwe haitii moyo swala la Kumashjambulia mtu bali ni kushugfhulika na Mawazo au mafundisho yasiyo sahii ndani ya mtu Waebrania 3;12 Biblia inasema Ndugu zangu, angalieni, asiwepo miongoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, unaojitenga na Mungu aliye hai.
Kama watu wa ulimwengu watakuwa ni wenye kutafuta ukweli Apologetic itakuwa hainakazi kwao lakini wanapoupinga Ukristo na kuiharibu imani ni wazi kuwa apologetics itafanya kazi kwao.

CHIMBUKO LA ELIMU YA UTETEZI.

Kwa ujumla chimbuko la elimu ya utetezi linatokana na sababa kubwa Tatu zifuatazo
1.      Mabadilio makuu matatu katika kanisa.
-          Kanisa katika hatua za mwanzoni lilikuwa ni kanisa kama shirika lisilo na sheria au kanuni au makusudi ya kimaadili au kimuuundo
-          Hakukuweko na Muundo maalumu wa kimaongozo wala wa kitaratibu nabaadaye lilikumbwa na mabadiliko hususani katika karne ya pili ambapo waamini walianza kufikiri kuhusu ushirika na kuweka viwango vya kimaadili na mafundisho ya msingi sababu zilizopelekea mabadiliko hayo ni pamoja na
a.      Kufa kwa Mitume wa Bwana.
Mwishoni mwa Karne ya kwanza Mitume wote wa Bwana walikuwa wamekwisha kufa wao walikuwa ni kama Mamlaka ya juu kabisa ya Kanisa na kila kulipotokea tatizo walikuwa wakitoa suluhisho je nanai atakuwa mwenye mamlaka kama ile?
Je kanisa lingewezaje kutunza umoja wake wa imani bila kuweko kwa Mitume? Ilikuwa ni lazima na muhimu jibu lipatikane na zaidi sana Mchanganuo wa majibu ya Misingi ya Imani ilikuwa lazima Isitawishwe.
b.      Mateso dhidi ya Kanisa.
Wafalme wengi wa Kirumi makaisari walitaka kuabudiwa wao kama miungu, aidha wayahudi walianza kuwaona wakristo kama dhehebu lililo kinyume na sheria ya Musa na kuwa ni imani pinzani au tishio Kanisa lingeweza kukabili vipi dharula hizo zilizojitokeza ndipo ilipoonekana haja ya kuwepo na Ushirika thabiti pamoja na sauti kamili ya kimafundisho au mafundisho sahii ambayo ungekuwa ndio msingi wa Imani ya wakristo wote.
c.       Kuweko kwa mafundisho ya uongo.
Mafundisho ya Mitume yalikuwa yanakubalika na kuheshimika kama Mamlaka ya mwisho hususani walipokuwa wakiwa hai, Lakini baada ya wao kufariki waalimu wa uongo wengi walitokea je ni nani angesimama na kuzungumzia maswala ya imani na misingi ya mafundisho ya kweli ya kanisa? Hapa ndipo tunapoiona elimu ya utetezi ikihitajika
Tatizo lilikuwa kubwa zaidi wakati jamii ya wakristo wa Mataifa walipoamini na kuingia kanisani kulizuka mawazo tofautifalsafa tofauti na migogoro iliinuka 

Na mkuu wa wajenzi mwenye hekima!
Rev. Innocent Kamote

Maoni 2 :

Paul Salim Ramadhani alisema ...

Nashukuru sana nimejifunza kitu hapa kwakweli kuhusu utetezi wa imani ya kikristo kutoka mashambulizi yatokayo nje ya kanisa la kristo.

Unknown alisema ...

Mafundisho mazuri sana. Mungu akubariki mtumishi wa Mungu kwa elimu tunayopata hapa hasa sisi wanafunzi wa theolojia tunapata madini ya kutosha sana. Baba usiache kuchambua kitabu baada ya kitabu tafadhali Askofu. Nimefurahia sana uchambuzi wa kitabu cha Ufunuo. Ubarikiwe