Ilikuwa mwaka jana nasafairi
kutoka Dar kwenda Arusha kwa ajili ya kwenda kula sikukuu ya Krismasi, wale
wanaosafiri na magari hayao nafikiri wanafahamu kuwa wakifika katikati
kwenye safari wenye mabasi hayo
huyaingiza hoteli iliyoko karibu na
njiani ambayo sipendo kuitaja jina
na kondakta akaamuru abiria washuke wakapate chochote lakini kwa
dakika kumi , kama kawaida kwa sababu mimi nilikuwa karibu na mlango nilikuwa wa kwanza kushuka nikawahi hotelini na kuangiza bisikuti pakiti mbili na
soda nikawa nimekaa kwenye kiti
naendelea kula taratibu huku nikiangalia saa yangu ya kwenye simu ya mkononi ili niende na muda
wa kondakta wa basi.
Tumbo la kuhara huwa halina Adabu!
Wakati naendelea ghafla nikasikia sauti ya dada mmoja akiita anko samahani naomba hiyo chumvi hapo
mezani kwako, nilipogeuka nyuma ghafla
nikamwona aliyekuwa akinisemesha
ni dada mmoja aliyekuwa akila wali kwa mchguzi wa nyama pamoja na
kachumbari, alikuwa ni msichana mrembo kwa kweli jambo lililonifanya wakati nanyanyua
ile chumvi kuimpa nikodoe macho kidogo kwa maana nyingine ni kama nilihamaki,
muda wa kuondoka gari ukawa
umewadia kwani gari lilishaanza
kupiga honi nami nikaelekea kwenye basin a likaanza safari kuelekea Arusha Baada ya safari kwa masafa ya kutosha
nilimuona Yule dada akizungumza na kondakta wa basi jambo Fulani, Kondakta
aliondoka na kumfuata dereva ambaye aliongea naye kwa sekunde kadhaa, basi
lilisimama na ikatangazwa kwamba abiria wakajisaidie Nilijua Yule dada anataka
kujisaidia, Abiria walirudi basini na
basi likataka kuondoka , lakini abiria mmoja alitahadharisha kuwa Yule dada
aliyeomba basi lisimame alikuwa hajarudi na , ilibidi akina mama watumwe kwenda
kuangalia kulikoni.
Baada ya muda tukaona wale akina
mama waliokuwa wakienda kumfuatilia wakirudi na Yule dada aliyeniomba chumvi taratibu
wanarudi kutoka nje na kuingia kwenye
basi, Na alipoingia alikwenda moja kwa moja kukaa kwenye siti yake huku abiria
wengine wakimpa pole na wengine wakimwangalia tu bila kusema chochote na basi
likaanza safari yake, lakini basi lilipotembea kama dakika hamsini hivi
nikamwona Yule dada akinyanyuka tena kumwendea kondakta, na kwa sababu nilikuwa
karibu na mlango niliposikia maongezi ya
safari hii kwani kondakata alikuwa akiongea na Yule dada kwa sauti kubwa baada
ya kumuomba kuwa gari lisimame tena aende kujisaidia kondakta akaijbanza naye kwa kumwambia haiwezekani bwana tukimbize gari tukuwahishe hospitali,
sisi tunakwenda kwa ratiba na kwa muda njiani trafiki watatukamata, Ghafla
nikaona Yule dada akirukia mlango wa basi na kutaka kuufungua huku basi linakwenda, ndipo abiria wengine wa
basi wakataharuki kulikoni huku wengine
wakisimama kwenye viti vyao baada ya kuona tukio lile wakati Yule dada
akiurukia mlango na kujaribu kuufungua
na kondakta kujaribu kumzuia,
nikamwona amechuhumaa chini na
huku amejiinamia na baada ya muda mfupi hariufu ya kinyesi ikatanda ndani ya
basi zima na hususani kwa siti za mbele
, Na baadaye ikaonekana kuwa amejiharishia
tena vibaya mno, Ndipo tena wasamaria wema walipojitokeza na kwenda
kumsaidia na kubadilisha zile nguo kwa
kumtaka atoke nje ya basi lakini safari
hii basi lilikuwa kwenye maeneo ya watu na sio zile sehemu maarufu za uchimbaji
dawa, ndipo wakati huo ukazuka mjadala , wengine wakisema ashushwe
akabadilishwe hivyohivyo mbele za watu nje ya basi, wengine wakisema asaidiwe
ndani ya basi, wengine wakisema basi liwahishwe mpaka porini, wengine
wakafungua mabegi yao kutoa mashati kumfunika wengine wakarudi viti vya nyuma
kukimbia harufu ilimradi ilikuwa vurugu tupu tu.
Wakati hayo yakiendelea
kukasikika kilio kingine cha sauti Para! t Para! Prataaaaapaa! Kumbe alikuwa
amefanya tena vitu vingine palepale mlangoni, hayo yote yakiendelea akatokea
mzee mmoja wa makamo ndani ya basi
akapaza sauti kwa nguvu nyie akina mama watu wa ajabu sana Yaani mwenzenu
anaadhirika , badala ya kutoa khanga zenu mkaweka uzio wa dharula hapo nje na kumsaidia mnaangalia tu, Kweli wazo lile likafanya kazi kwa wengine
hasa akina baba kufungua mabegi yao na kujitolea shuka na wengine waliotoa dawa
ambazo walisafiri nazo wakati huo wakazi wa eneo lile walipoona uzio wa akina
mama wamezunguka wakajazana kuona au kutaka kujua kulikoni, zoezi lile
likakamilika na safari ikaendelea ambapo
dada Yule dada alishuka Moshi name nikaendelea hadi Arusha huku nikijiuliza fedheha yote ile
ya kujiharishia kwa Yule Dada huenda
shauri ya mikachumbari ile jamboa ambalo linanifanya hadi leo kuwa
mwangalifu na kula hovyo hovyo njiani niwapo safarini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni