ANDIKO LA MSINGI MARKO 5:1-20.
Jacob Koshy alikulia katika mji mkuu wa
Singapore akiwa na maono ya kuwa Dereva na kuwa na mafanikio makubwa sana
katika maisha, alikuwa na ndoto za kupata fedha na kumiliki mali, Hata hivyo
mpango wake huo ulimpelekea kujiunga na mtandao wa kimataifa wa kusambaza
madawa ya kulevya Duniani, mwaka 1980 alikamatwa na seriakali na kuwekwa
Gerezani.
Alikata tamaa sana, alichoka kabisa, kwa
vile ndoto zake, makusudi na mipango ya maisha aliyokuwa nayo iliharibika
kabisa hakukuwa na tumaini tena na alivunjika moyo, alijiingiza katika uvutaji
mkubwa wa sigara na tumbaku, hata ingawa havikuwa vinaruhusiwa huko Gerezani, alipopata
tumbaku ili aweze kuivuta alitumia karatasi za Biblia ya GIDEON ili kusokotea
tumbaku na kuvuta, siku moja alipitiwa na usingizi huku akiwa anavuta,
aliposhituka aliona karatasi yote ya sigara imeungua na kimebaki kipande kidogo
cha karatasi, alipoamua kukikunjua alikuta kimeandikwa “Saul Saul Mbona
waniudhi?” Jacob aliomba Biblia nyingine
na kuisoma habari ya Saul kwa undani zaidi, kisha akajisemea Kama Yesu anaweza
kubadili mwelekeo wa mtu katili namna hii, bila shaka anaweza kubadili mwelekeo
wangu, aliamua kupiga magoti na kumkubali Yesu akiwa Gerezani, Maisha yake
yalibadilika alikuwa ushuhuda kwa wafungwa wengine, alitolewa gerezani kutokana
na badiliko kubwa, alijiunga na kanisa na kufanya kazi za kanisa alioa mke wa
Kikristo, kwa sasa Jacob amekuwa Mmishionari anayehubiri njili huko Mashariki
ya mbali akiwaeleza watu, Yesu ni Mwana wa Mungu aliye Juu.
Marko 5:1-9 Biblia inasema “ Wakafika
ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi.
Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka
makaburini, mwenye pepo mchafu; makao yake yalikuwa pale makaburini; wala
hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa
pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala
hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. Na sikuzote, usiku na mchana, alikuwako
makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe. Na alipomwona Yesu kwa mbali, alipiga mbio,
akamsujudia; akapiga kelele kwa sauti kuu, akasema, Nina nini nawe, Yesu, Mwana
wa Mungu aliye juu? Nakuapisha kwa Mungu usinitese. Kwa sababu amemwambia, Ewe pepo mchafu, mtoke
mtu huyu. Akamwuliza, Jina lako nani?
Akamjibu, Jina langu ni Legioni,”
Ndugu Msomaji wangu nafahamu kuwa husomi
ujumbe huu kwa bahati mbaya Nguvu zake Mjenzi mkuu wa Mbinguni zimekuvuta ili
apate kukuganga na kukuponya moyo wako, inawezekana umepigika, huna amani,
umepoteza kiu na shauku ya maisha, ndoto zako na mitazamo yako imepotea, unaona
giza kila inapoitwa leo, hujui hata kesho itakuwaje, hupendi kufa lakini unaona
heri hata ya kifo, unashindwa uchague nini unaona heri kusikuche, ni giza
linakuzunguka kila kona unajuta laiti ningefanya hivi au vile na unaweza
kumchukia Mungu na kuona ni kama anakuleta katika hatima ngumu na ya aibu kila
kitu kinakataa!
Hali hii ndio inayomkuta Kichaa tunayesoma
Habari zake katika Marko 5:1-7 mtu huyu aliishi makaburini, ni kama alikua
anawaza kufa au alizungukwa na mauti na akawa anatamani kufa ama alikuwa
akiwajutia ndugu zake waliokufa zamani, au mapepo yalimuongoza kushinda
makaburini, alijitenga na ulimwengu wa walio hai, alijiona hastahili kuwa
miongoni mwao, alijawa na huzuni, maisha yake yalisikitisha, aliishi maisha ya
upweke, hakuwa na mtu wa kumtia moyo, alikuwa amekwazwa na jamii na jamii
imechoka naye, amaumizwa ni muhitaji, hakuwa na mtu wa kumuonyesha upendo,
hakuna aliyesema dally wala honey hakuna mtu aliyetamani kuwa naye wala kupiga
naye story hali yake ilikuwa mbaya, alikuwa ni picha ya mtu aliyetengwa mbali
na huruma za Mungu, amekatiliwa mbali na Mungu na watu wake pia hali ya mtu
huyu ilikuwa ya kusikitisha hakuwa na nguo mwili wake haukujua jua wala baridi
aliishi maisha ya kusikitisha mnomno.
Mstari
3-5 hakuwa na msaada biblia inasema hakuna mtu aliyekuwa na uwezo wa kumfunga
tena kwa minyororo, ilikuwa ngumu kumdhibiti tena mtu huyu, alikuwa anauwezo wa
kukata kila aina ya minyororo, alijichukia alitamani kufa alijikatakata na
kupiga makelele ukichaakichaa ulimvamia hii ilikuwa ni picha ya mtu aliye
katika vifungo vya Ibilisi, hata watu waliojaribu kumsaidia walichoka naye,
alibaki na huzuni na kukosa msaada ni kama alikuwa katika gereza la Mateso na
uonevu na katika mikono isiyo na huruma ya mashetani.
Mstari
wa 5 Mateso yake yalikuwa endelevu ilikuwa usiku na mchana, alijikatakata na
kujijeruhi kwa mawe, hakuwa na uzuzi wala ngozi nzuri, angeoga saa ngapi,
aligeuka kuwa kama mnyama, huenda alirushiwa chakula kwa mbali na alikula kama
mbwa, hii inaonyesha hali zinazowazunguka walimwengu wengi, huwezi kujua kwa
nini wengine wanajiingiza katika ukahaba wa hali ya juu, uvutaji wa bangi na
madawa ya kulevya, ulevi na ujambazi uliokithiri na hawawezi kujitoa kamwe huko
kwani ziko nguvu za manyanyaso zinawakandamiza huko na wakati mwingine
hawafanyi kusudi, hawawezi kujiweka huru na wanamezwa na huzuni za historia ya
maisha yao yasiyo na msaada
Akiwa
katika hali ya kusikitisha na amekosa msaada mji mzima siku moja Yesu alifunga
safari kwenda katika nchi ile, iko wazi kabisa kuwa Yesu hakuwa na jambo lingine
lolote la kufanya katika mji ule alikwenda akiwa na jambo moja tu, kutoa msaada
kwa mtu huyu, hatujui kama akili zake ziliweza kutambua chochote maana alikuwa
amepagawa na mapepo yaliyojiambulisha kwa jina la Legion la kirumi ambalo maana
yake ni kikosi cha jeshi la askari 6000, askari hao au mapepo hayo ndiyo
yaliyoweza kumtambua Yesu, walipiga mbio wakiwa katika mwili wa mtu huyu na
kusujudu na kupiga kelele NINA NINI NAWE, YESU, MWANA WA MUNGU ALIYE JUU?
Kumbuka jinsi ambavyo hata safari ya Yesu ya kufika nchi ile ilikuwa ngumu
kulikuwa na upepo mkali ambao Yesu aliukemea ni wazi kuwa mazingira ya mji ule
na nchi ile ya wagerasi yalikuwa na nguvu za giza tupu, yalikuwa ni ngome ya
shetani yalikuwa hayapenyeki kirahisi, ilikuwa ngumu hata mapepo yale kuhama
nchi ile kwani yaliomba yasihamishwe katika nchi ile yalikuwa na madai maalumu,
yalikuwa na miliki maalumu, yalikuwa yameufanya mji ule kuwa kiti chao cha
enzi, Lakini hata hivyo mapepo yale yalikuwa na uelewa maalumu kuwa Yesu ni
nani Yalimuapisha Yesu kwa Mungu kuwa asiwatese Biblia inasema mashetani huwa
yanatetemeka Yakobo 2:19 Yalitetemeka na kusujudu yalipomuona Yesu ambaye ni
kiboko yao.
Leo
ni siku yako ya kuwekwa huru ninakutangazia ukomo wa misiba na majanga na
mikosi na balaa na nuksi na laana na mitazamo na manuizo na matamshi mabaya
uliyotamkiwa kwa mamlaka niliyopewa kama myumishi wa Mungu aliye hai namuomba
Mungu abadilisha maisha yako, iwe ghafla au kidogokidogo Mungu akubadilishe
kabisa imetosha mateso yako, vifundo vya kichawi na nguvu za kiza ziharibiwe na
uwe huru kwa Damu ya Yesu Kristo matatizo yako yapige kelele nina nini nawe
Yesu mwana wa Mungu aliye juu!
Ashukuriwe
Yesu mwana wa Mungu aliye hai kijana huyu aliyefungwa kwa miaka alijikuta akiwa
katika mikono salama ya Bwana na mwokozi mwenye wingi wa huruma na neema Yesu
alitoa msaada Yesu hakufanya jingine katika nchi ile zaidi ya kumponya mtu huyu
na kumuweka huru!
Hali
ya mtu huyu mwenye kuteswa na mapepo na Jacob Koshy zinafanana na hali za wengi
wetu kwa mazingira tofauti, kumbe Bwana anatujali anajishughulishja na maisha
yetu, hajabadilika Yesu Kristo ni Yeye Yule jana leo na hata milelel
amaegharimika kwaajili yetu, yuko tayari kubadili maisha yetu, kutoka katika
hali ya kutokuheshimika kutupeleka katika hali ya kuheshimika, kutoka katika
kupoteza tumaini kutupeleka katika tumaini, kutoka katika hali ya ukichaa kuwa
wapeleka habari njema, kutoka katika kufanyika kuwa nyumba ya shetani kutufanya
kuwa nyumba ya Roho Mtakatifu, maisha ya mtu huyu yalibadilishwa na kujaa neema
ya Mungu angalia kuwa
Mtu
huyu aliponywa, akili zake zilirejea
1.
aliketi akiwa salama
2. alivaa mavazi
3. alirudiwa na akili zake
4. alikuwa tayari kumfuata Yesu
5. alifanyika Muhubiri wa Injili
6. na Mungu alitukuzwa kwaajili yake.
Yesu
alimkomboa kwa gharama kubwa Machoni pa Yesu mtu huyu alikuwa wa thamani kuliko
wanyama wa kufugwa waliokuweko katika mji ule, ni muhimu kufahamu kuwa watu
waliofuga nguruwe hawakuwa Wayahudi
wayahudi waliamini kuwa nguruwe ndiye moja ya wanyama wachafu zaidi
walio najisi hivyo ni wazi wafugaji walikuwa ni mataifa hivyo ni wazi kuwa
walishiriki maswala ya kichawi na Yesu aliwatia hasara, kwani ni wazi pia ya
kuwa mtu huyu alirogwa! Wachawi hao waliogopa kupata hasara kwani walimsihi
Yesu aondoke katika nchi yao
Gharama
ya ukombozi wake Mapepo yaliyotoka yaliomba yawaingie Nguruwe, mapepo
yaliwaingia Nguruwe 2000, kilo moja ya nguruwe leo ni 6000-7000 kama kila
nguruwe alikuwa na kilo 200 chukua 7000 x 200 x 2000 = 2,800,000,000/- Bilion 2
na milioni mia nane ilikuwa ni thamani ya kichaa Yule aliyeokolewa na Yesu
Ndugu
yangu thamani yako katika macho ya Mungu Baba na Mikono ya Yesu kristo ni kubwa
sana, haijalishi wewe ni kahaba, kichaa, mvuta bangi, shoga, mla madawa ya
kulevya, uliyekataliwa, chokoraa, usiyesoma, mwenye ukoma, mwenye ukimwi,
unaishi na hiv, una sukari, huna thamani kwa mumeo, mkeo, ndugu zako,
unaonekana mzigo na kadhalika wewe kwa Yesu sio mzigo kwa mjenzi mkuu mwenye
huruma wewe ni wa thamani, unamuhitaji Yesu tu abadilishe maisha yako yeye Yuko
tayari kubadili historia yako na kukupa msaada ikiwa uko tayari fuatilia maombi
haya ninayokuombea kwa kumaanisha kabisa kutoka Moyoni
Mungu
mwema! Na Baba yangu! mtumwa wako ninaomba kwa unyenyekevu mkubwa nikibubujikwa
na machozi, ninajishusha chini ya magoti yangu najiinamisha katika miguu yako
kwaajili ya msomaji na msikilizaji wa ujumbe huu Eeeee Bwana Mungu wangu hakuna
mwanadamu aliye mbaya sana duniani kiasi ambacho asihitaji au asisitahili
kupata rehema zako nakuomba leo eeeeee bwana Mungu wangu katika Jina la Yesu
Mwana wa Mungu aliye Juu umponye na kumuhurumia msomaji wangu ili ajue ya kuwa
nguvu zako zipo hata katika maadnishi haya badili kabisa maisha yake nakulilia
ee mwokozi usiitazame dhambi yake wala ya jamaa zake wala ukoo wake, wala
makosa yake, kumbuka rehema zako hata katika hasira zakoooo oooooh ohhhhho Bwana mtumwa wako ninakusihi
badili kabisa maisha ya mtu huyu leo aliyekosa msaada ufanyike msaada kwake
katika Jina la Yesu Kristo ameeen!
Baada
ya sala hiyo nilikuwa nalia machozi nilipokuwa nakuombea naamini umetembelewa
na Mungu huyu tumwabuduye niandikie ili nimshukuru mungu pamoja nawe au acha
ujumbe wako chini ya ujumbe huu katika face book
Rev.
Innocent Kamote
0718990796
MKUU
WA WAJENZI MWENYE HEKIMA
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni