MISINGI YA
KIBIBLIA YA ELIMU YA UTETEZI WA IMANI.
Unaweza kujiuliza swali hili je
watu wa nyakati za Biblia walijiingiza katika maswala ya utetezi wa imani?
Manabii na mitume je walikutana na changamoto kama hizi tunazokutana nazo leo
je waliitetea imani au kwa maana nyingine uko ushahidi wa kimaandiko
unaoonyesha swala zima la kuitetea imani? Ni muhimu kwetu kuchukua safari fupi
ndani ya maandiko ili kuthibitisha ukweli na maswali yaliyoko juu yetu
1. Mfano
wa Kitabu kizima cha Ayubu, ni wazi kabisa kuwa bi kitabu kinacho halalisha
Matendo ya haki ya Mungu kwa wanadamu ni utetezi wa kazi sahii ya Mungu dhidi
ya Rafiki ndugu na jamaa waliokuwa wakijaribu kumshawishi Ayubu kuachana na
Mungu ni wazai kuwa mwandishi alikuwa akionyesha kuwa Mungu wa Israel ni
tofauti na Miungu ya kipagani yeye ni mwaminifu
2. Mfano
katika kitabu cha Zaburi, ni wazi kuwa kwa mifano zaburi ya 19 & 119
zinathibitisha wazi kuwa Mungu yupo na
kuwa amejifunua wazi kupitia Neno lake na kazi zake ni wazi kwa mafano katika
Zaburi 19 inaposema Mbingu zatangaza ni wazi kuwa nyota na mbingu ni kazi ya
uumbaji wa Mungu uumbaji unatetea kuwekokwa Mungu.
3. Mfano
katika kitabu cha Warumi, sura ya kwanza na ya Pili kuwa kupitia uumbaji na
dhamiri mwanadamu anao ushahidi unaomuonyesha kuwa anawajibika kwa Mungu bila
kuwa na udhuru
4. Mfano
katika kitabu cha Matendo ya Mitume ni wazi kuwa tunamuona Paulo mtume
akiitetea injili chini ya viongozi kama Felix, Festo na agripa, Kwa ujumla
kitabu cha Matendo kinazungumza kwa upana namna injili ilivyoweza kutetewa.
Kinatetea Ufufuo wa Yesu na uuungu wa Yesu, injili ya neema bila sheria ya
tohara ya Musa na Hotuba ya Paulo mbele ya wanafalsafa wa kiyunani Matendo 17
hali yote hiyo ni Apologetics ni utetezi wa Imani
5. Kwa
ujumla hata nyaraka nyingi ziliandikwa kwa kusudi la kuitetea imani na
kurekebisha mafundisho potofu na kuonyesha njia kupitia mafundisho halali ya
kweli ya injili Wafilipi 1;7 ni wazi kuwa Paulo mtume alifanya kazi ya kuitetea
injili, 1Petro 3;15 “Muwe tayari sikuzote kumjibu (Kujitetea) kila mtu
awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu lakini kwa upole na kwa
hofu” Be ready always to make Defense
(Apologia) ni wazi kabisa kuwa Mitume waliifanya kazi hii ya kuitetea imani
Utetezi wa
Imani nyakati za Mapema baada ya Mitume.
Tangu nyakati
za kanisa la kwanza Mateso yalikuwa yametapakaa na kupamba moto dhidi ya
Kanisa mapaka mnamo mwaka wa 250 hata
hivyo watetezi wa imani wengi waliinuka na kuitetea imani, wengi wao walitumia
mfumo wa mafundisho katika uandihi na baadhi ya watetezi maarufu wa mapema
kabisa ni kama Aristide, Justine Matyr, Tatian, Tertullian, Origen Na Syprian
walitoa hoja zao kwa watatwala wa kirumi, katika bunge la senet na kwa watu
raia wa Rumi
Wao walitoa
miito kadhaa kama miito ya haki.
Mfano Justin
Martyr aliyeishi kati ya 100-165 alikuwa ni Mwanafalsafa, Mwanatheolojia na
moja ya watetezi wa imani wa mapema sana katika kanisa alikata shauri kuikabili
mamlaka kuacha kuwatesa wakristo kwa sababu walikuwa wakristo. Justin alizaliwa
huko Flavia Neapolis ambako leo ni Nabulus ukanda wa mashariki wa miji ya kale
ya Rumi huko shechem Samaria au Israel wazazi wake walikuwa wapagani, alipokuwa
kijana alijitolea kusoma Falsafa kupitia maandiko ya Mwanafalsafa maarufu wa Kiyunani
Plato na falsafa za wastoiki alikutana na Ukristo huko Efeso na baada ya
kuokoka alikwenda Rumi na kustawisha Shule. Aliuawa huko Rome kama shahidi
wakati wa Utawala wa Marcus Aurelius
Marcus Aurelius
Mtawala Marcus Aurelius aliitawala Rumi
kati ya 161 na 180 utawala wake ulitawaliwa na maswala ya vita za marakwa
mara ni katika wakati wake ndipo Justin
Martyr aliweza kuitetea imani.
Mfano wa mtetezi mwingine ni Tertulian
ambaye aliandika miaka 50 baadaye baada ya Justin alukuwa ni moja ya watu
muhimu sana katika ukristo na mwandishi wa vitini vingi vya kitheolojia katika
lugha ya kilatini ambavyo kati ya hizo 30 zimesalia hata leo aliishi kati ya
190-220 ni mwana wa akida wa kikosi cha jeshi cha kirumi alikuwa amesomea
sheria,aliokoka kati ya mwaka 190-95 alirudi kwao Cathage ambaye alioa na
baadaye kuwa mwangalizi wa kanisa alikazia maadili na nidhamu katika kanisa na alikuwa mtetezi wa
imani mwenye kupinga uzushi alijaribu kukebehi miungu ya kipagani pamoja na
sadaka zao za kuteteketeza zilizotolewa kwa miungu hiyo, aliitetea imani kwa
nguvu akithibitisha kuwa Mungu anayetumikiwa na wakristo ndiye Mungu na kuwa
tunamuabudu Mungu mmoja ambaye macho ya kawaida hayawezi kumuona ingawa Yupo.
Utetezi wa imani nyakati za karne ya
Pili.
Wanatheolojia wa Kanisa la
kiorthodox (Imani ye kweli ya Kikristo)
waliitwa watetezi wa karne ya Pili njia yao kubwa ya kiutetezi imekuwa njia
kubwa ya muhimu ya kufuatawa na wanatheolojia na watetezi wengi wa kizazi hiki
njia yao ilikuwa ni Kutoa Tamko, kutafasiri na kukanusha.
a.
Kutoa
Tamko.
Utoaji tamko
wakati wa utetezi unajumuisha Imani na kujiuliza mswali kwamba imani Fulani je inahusiano na kile
tunachokifikiri kuwa kweli kwa wakati huo kujiuliza maswali sio swala zima linalohusiana
na imani na Imani haimaanishi wakati wote ni kujiuliza maswali Imani ni
uhusiano wa mwanadamu na Mungu inampa mtu ujasiri kwa Mungu anayemtegemea hii
ni imani endelevu kwa Mungu na ni Binafsi na inapimika kwani unaweza kuwa nayo
nyingi au chache lakini imani inayozungumzwa katika Yuda ni imani ambayo inaonekana ni mjumuisho wa kweli
kamili iliyofunuliwa na Mungu katika neno lake yaani Biblia na inaaaminiwa na wakristo hii ndio imani
ambayo watetezi huikusanya pamoja kama misingi ya imani ya kweli ya Kikristo.
Kumbuka kuwa
“Haitoshi kujua kile unachoamini, lakini ni muhimu kujua kwa nini unaamini
unachokiamini”
b.
Kutafasiri.
Moja ya kazi
nyingine ya Muhimu ya elimu ya Utetezi apologetics ni kutafasiri kweli ya
Ukristo katika kipimo sahii cha elimu ya kanuni za kutafasiri maandiko.
c.
Kukanusha.
Ni kazi ya tatu ya
elimu ya utetezi wakati wote katika historia kumekuweko na madai yaliyo kinyume
dhjidi ya kanisa kwa kiwango fulani kwa mfano wayahudi waliifikiri imani ya
Kikristo kuwa ni imani iliyokengeuka na kuiasi sheria ya Musa kwa warumi
ilikuwa ni kikwazo, kwa wayunani ulikuwa ni ujinga 1Koritho 1; 21-24 kwa
waislamu wanakataa kabisa swala la Yesu kuwa mwana wa Mungu na kuwa utatu ni
uzushi. Kwa msingi huo uthamani wa Imani ya Kikristo ni Uhakika wa kweli na
ulinzi dhidi ya maadui wa imani au mashambulizi ya kiimani.
MABARAZA NA MATAMKO YA
IMANI. (Councils
& Creeds)
Matamko ya imani Creeds ni Neno la
Kiingereza litokanalo na neno Credo
la kilatini ambalo maana yake ni Ninaamini “Ibelieve” Matamko haya ya imani yalitokana na Mikutano au mabaraza
ya kikanisa yaliyofanyika kwa nayakati tofauti kushughulikia maswala kadhaa ya
kiimani.
1. Mkutano
wa kwanza wa kanisa.
a.
Mkutano mkuu wa kwanza wa kanisa ulifanyika
Yerusalem kati ya mwaka wa 49 na 50 ukishughulikia swala la Wokovu kwamba je ni
lazima mataifa waliookolewa kuishika sheria ya Musa na kupitia tohara ndipo
wahesabike wameokolewa? Paulo na Barnaba walisimama kama watetezi wa imani na
walishinda na kwa sababu hiyo kufungua mlango injili kwa ulimwengu kama matokeo
ya ushindi huo.
b.
Mfumo wa kuweko kwa mamlaka.
Baada ya kufa kwa mitume Mateso pamoja na mafundisho
mengi ya uongo yalijitokeza, Mitume walikuwa wametegemewa sana kama mamlaka ya
mwisho kila kulipotokea tatizo na kanisa liliweza kustahimili mafundisho potofu
na changamoto nyinginezo. Kwa kuwa mitume walikuwa wamekwisha kufa wote kanisa
liliunda mfumo wa mamlaka
1.
Mfumo wa kuwepo kwa Maaskofu
2.
Kupitishwa kwa kanuni ya kupima maandiko
3.
Kustawishwa kwa kiriwa imani na matamko ya
kiimani.
Hata kufikia
mnamo mwaka 250 Kanisa lilikuwa tayari ni Taasisi yenye viongozi wake yaani
Maaskofukatika miji mikuu na majimbo na kutokana na kuweko kwa mafundisho
potofu kanisa lililazimika kuwa na Ukiri wa imani kwani kuweko kwa maaskofu na
kanuni ya kupimia maandiko hakukusaidia kupambana na imani potofu kama imani ya
Gnostics na nyinginezo.
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni