Siku hizi huwa nashindwa
kujiuliza sana kuhusu maisha, najiuliza kuhusu watu kushindwa kuwajibika kwa
matendo yao na maisha yao kwa ujumla, Maswali haya najiuliza baada ya kujifunza
kupitia uzoefu mmoja na ambao ningependa
kuushiriki na wengine leo hii
Ilikuwa mwaka 1995 nilikuwa
nimepata uhamisho kutoka wilayani mpanda
kuja Dar ni lazima niwe mkweli kwamab siku hiyo ilikuwa ni mara yangu ya
kwanza kuja dar kuishi mara nyingine
kama mbili tatu hivi nilikuwa napita tu
kiofisi, nakuja ofisini kwetu na siku ya pili narudi mkoani, Nilipofika
nilitafuta nyumba na kupata katika maeneo ya mwenge, sikuja na familia yangu kwa sababu ilinibidi
kuja kutafuta nyumba kwanza na kasha
familia yangu ifuate baada ya
kuhakikisha kuwa nimepata nyumba , nikiwa bado mgeni wiki ya pili tu, niliotoka
siku moja kwenda kutembea na kunywa
kidopgo, wakati huo tulisha kubaliana na familia yangu kwamba wajiandae na kuja Dar baada ya wiki
mbili.
Siku hiyo nilikwenda kutembea
katika baa moja maarufu wakati ule pale Mwenge-Sinza najua unanielewa vema kama
unaipata vilivyo mitaa na vitongoji vya Dar ilivyo na utata kubainisha , Basi
wakati nakunywa akatokea dada mmoja
akanizoea palepale.Kule kwetu Mpanda mwanamke kukuzoea haraka ni lazima awe anakupenda hasa kwa hiyo nilitafasiri
kuwa huyu dada kanizimia haswa tulikunywa naye na kuzoeana usiku huo huo.
Hatimaye nilikwenda naye kwangu
na kupitisha usiku naye kiibilisi, kosa namba moja likawa hili, nilimwambia
kwamba sijaoa, kwa ushamba wangu nilidhania kumwambia msichana wa Dar kwamba nimeoa ingekuwa ni kujiangusha
sana kwa hiyo Yule changudoa ambaye mimi nilimuona kuwa mwanamke wa maana
sana baada ya kunidanganya kwamba
anafanya kazi ubalozini na ametokea kunipenda, kusikia sijaoa nadhgani alijua
amejipatia bwana, kwa sababu hiyo akawa amepata pa kulala , Zile pesa zangu za
uhamisho nilianza kuzimwaga kwa matumizi
ya kijingakijinga. Nilikuwa sijui mambo ya bilicanas au FM, nikayajua kupitia
kwake Ilibidi mke wangu anishitue akiwa ofisi ya basi pale Kariakoo, Nilikuwa
nimekwisha sahau kabisa hata kuhusu kuja kwake, nilifanya utaratibu wa kwenda
kumpokea, kwa habari ya yuel changudoa nilishindwa kumjulisha kuhusu ujio wa
familia yangu, nilitaka nimfahamishe kwamba mke wa kaka yangu na watoto
wamekuja na hivyo itabidi tusikutane nyumbani kwanza kwaajili ya kulinda
heshima.
Lakini ningempata wapi? Mtu
anakwambia anafanya ubalozini ukimwambia nipeleke anakwambia anafanya hazina ,
ukimwambia nipeleke ofisini kwako
anabadilika na kukwambia kuwa yuko Usalama wa Taifa, aha Niliamua kwenda
kwanza kituoni kuwachukua watu wangu,
nilifika kituoni na kukuta pamoja na mke
wangu na watoto wawili alikuwemo mama mkwe wangu, niliwachukua na kuwapeleka
nyumbani Mwenge muda ulikuwa ni kwenye saa tano asubuhi siku ya jumapili,
Nilimwambia mke wangu kuwa ninaenda kazini, kuna kazi maalumu huko,
niliondoka kwenda kumsaka Yule changudoa lakini sikuweza
kumpata . Ilibidi nirejee nyumbani na kuamua kwamba , nikisikia hodi tu nitakuwa wa kwanza kwenda mlangoni ili kuuwa soo hukohuko,Ni kweli
jioni iliingia na usiku ukaingia kwenye saa mbili hivi wakati tunakula ndiyo ikatokea Mlango mkubwa ulikuwa umesindikwa tu kama
unavyojua watu wa Bushi kufunga milango
kwao sio Issue, Ghafla tuliona mlango ukifunguliwa na mwanamke aliingia, Mwanamke
Yule akiwa amelewa alipiga kelele “Haroo
daring izi faini yuu welikamu” Halafu alikuja pale mezani na kuniinamia
na kunibusu. Kumbe una wageni daring wangu mbona hujasema ndiyo maana
sikukuona sehemu sehemu…’ Ehee Hebu tulia bwana wewe unaona kuna wageni halafu
unaanza kuleta fujoi zako, Huyu hapa ni mke wangu hawa ni watoto wangu na huyu
ni mama mk…” Nilisema kwa kelele.
Alinikatisha karibu mke mwenzangu
mimi pia ni mke wa huyu bwana tulikuwa hatujuani…” Niliinuka kutaka kuangusha
kipigo lakini kabla sijarusha ngumi au kibao nilijikuta niko chini Mke wangu ni
wale ambao hawakuja duniani kuchezewa na wanaume. Alimvaa changudoa Yule na kushughulika neye vilivyo kuna kupigwa na
kusuuzwa, Yule changudoa alisuuzwahaswa, ilibidi mama mkwe aingilie kati na
kumsihi mwanawe aache vurugu, changudoa
Yule alitumia nafasi hiyo kuiona njia
kwa kukurupuka kama guruwe pori
lililokoswakoswa mshale, huku akisema tutaonana, kasha ikafuata zamu
yangu nakwambia mkioa muwe mnatazama vizuri kuna wanawake wengine bwana
wakikasirika, wana kuwa kama nyati majeruhi, Kama isingekuwa kelele za ‘Mama
unamuua baba‘ ya watoto na mama mkwe
kuingilia kati apigwe yeye badala yangu
huenda ningefikishwa Muhimbili kitengo cha kuunga mifupa MOI nikiwa unga
wa dona. Najua ungependa niendelee sawa
si unapenda kuona wengine wakiadhirika ili upate nyuzi ehe! Ngoja yaje kukupata
hutakuwa na hamu hata ya kusikiliza ya wenzio!.
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev Innocent Kamote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni