Jumanne, 26 Januari 2016

UJUMBE: UPIGANE NAO WANAOPIGANA NAMI!




Zaburi 35:1-38
     Zaburi ni mojawapo ya vitabu vya kipekee sana katika Biblia ni moja ya kitabu maarufu kilichoko katika kundi la vitabu viitwavyo vitabu vya mashairi ya kiebrania na ndicho kitabu kirefu kuliko vyote katika Biblia kwani kina sura karibu 150 zilizogawanywa katika vitabu vitano, inaaminika kuwa ndicho kitabu kinachosomwa zaidi na kuhubiriwa zaidi kuliko vyote katika agano la kale, aidha waimbaji wengi sana  na watunzi wa nyimbo hutoa nyimbo zao katika zaburi, sababu moja kuu inayovutia wengi katika zaburi ni kwa sababu zinagusa hisia za watu
·         Zaburi ziliandikwa kwa sababu mbalimbali za kihisia kama vile watu walipokuwa na furaha, huzuni, nk, Mfano mwandishi wa wimbo nionapo amani kama shwari kwa hiyo kuna sababu nyingi zilizopelekea zaburi kuandikwa kati ya hizo ni pamoja na
1.      Zaburi kwa ajili ya hekima na maadili mfano zaburi ya 1
2.      Zaburi kwa ajili ya shukurani nyingi huanza kwa kusema mshukuruni Bwana!
3.      Zaburi za kujitia moyo mfano zaburi ya 27
4.      Zaburi za kifalme au za kimasihi
5.      Zaburi za kihistoria au za kukumbuka matukio maalumu
6.      Zaburi za kusifu au “Halel Psalms” ambazo huanza na neno Haleluya
7.      Zaburi za maombolezo
8.      Zaburi za dua na maombi pamoja na kulaani Mfano Zaburi ya 35 : 1-8
Leo nataka tuchukue Muda kuitafakari zaburi hii ambayo huangukia katika kundi la zaburi za kulaani, au zaburi za maombi lakini wakati huu mwandishi wa zaburi hii anaomba mabaya au hukumu ndhidi nya adui zake! Ni zaburi ngumu wakati mwingine kuitafasiri ukilinganisha na Mafundisho nya Bwana Yesu kuwa tusiwalaani maadui zetu bali tuwaombee mema hata wale wanaotuudhi! Luka 23:34 na Mathayo 5:39,44. Hata hivyo ni muhimu kujiuliza Kwanini Roho Mtakatifu ameruhusu Zaburi hii kuweko!
1.      Kila mtu aliyeokoka anayo haki ya kudai ulinzi wa Mungu dhidi ya watu waovu na wanaotuonea, Mungu hakutuita duniani tu ili tutukanwe na kudhulumiwa na kusemwa vibaya na kuteswa na kuonewa na kuuawa na kuchukuliwa wake zetu, waume zetu, kujaziwa mimba watoto wetu, kusemwa vibaya kukandamizwa kuzibwa vinywa eti kwa vile sisi ni walokole Hapana! Simama na kuitetea haki yako!
2.      Mwandishi wa zaburi hii hatufundishi kujichukulia sheria mkononi na kujilipia Kisasi lakini anatufundisha Kumtegemea na Kumsihi Mungu awaadhibu waovu kulingana na uovu wao anayeteta name Bwana atete naye!, anayepigana nani Bwana apigane naye! Hatuwezi kama wakristo kukaa kimya pale uonevu unapofanyika kisha Mbingi ziko kimya na serikali iko kimya Biblia inatufundisha kuidai haki, naweza kushindwa kuandamana, kubeba silaha, kujitetea mwenyewe, kwenda mahakamani n.k lakini siwezi kushindwa kuingia Magotini na kuidai haki yangu Mungu ni Lazima anilipie Zaburi 28:4 Unasema Hivi “ Uwape sawasawa na Vitendo vyao Na kwa kadiri ya Ubaya wa kufanya kwao, Uwape sawa sawa na Kazi za mikono yao Uwalipe stailizao”
3.      Biblia kupitia Zaburi hii inatufundisha kuwa kiko kiwango cha uvumilivu lakini kama uovu utaendelea kupita kiasi na kufikia kilele Ni lazima Kumkumbusha Mungu katika Haki yake kutoa haki na hukumu, ni lazima tusimame kuhakikisha kuwa Uonevu na ukatili vinakomeshwa na kuharibiwa Yesu Mwenyewe alifundisha Mfano wa Mwanamke mjane Katika Luka 18:3 aliendelea kuomba bila kukata tama mpaka haki yake ikapatikana tena Kristo alihahidi kuwa Mungu hataacha kuwapatia haki wateule wake wanaomlilia Mchana na Usiku Luka 18:7
4.      Zaburi hii inatufundisha kuwa ingawa tunatamani kuona watu wanamgeukia Mungu na kuja kwake kupitia Upole wetu, upendo na Unyenyekevu, Lakini pia tutamani kuona Uovu ukiharibiwa na watu wakatili wakishughulikiwa, Nimlazima tumuombe Mungu ashughulikie adui zetu ndio adui yetu mkuu ni shetani lakini na wale anaowatumia kutuonea na kutubughudhi na kutukerehesha ni muhimu kumsihi Mungu ashughulike navyo ni lazima tumuulize Mungu Maswali ambayo hata Daudi na upendo wake na huruma na rehema alimhoji Mungu!
Mbona Mataifa wamefanya ghasia
Na kabila za watu wametafakari Ubatili?
Wafalme wa Dunia wamejipanga
Na wakuu wamefanya shauri pamoja
Juu ya Bwana na juu ya Mpakwa mafuta wake.
Ni wakati wa kusimama na kudai haki yako dhidi ya Udhalimu wa kila aina, lazima umwambie Bwana ashughulike na kila kinachokukosesha raha na amani hapa duniani, kama ni magonjwa, Mapepo, Mateso, Ugaidi, Uonevu, Dhuluma, Kunyanyaswa n.k. Usikubali ukaonelewa Yuko awezaye Kupambana navyo mweleze ashughulike navyo!

Ujumbe:
Na Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.

Hakuna maoni: