Sitaki kutaja jina langu ingawa sio vibaya kufanya hivyo, Mimi ni kijana wa miaka 33 hivi Nilikuja Dar es Salaam kutoka Rufiji mwaka 1999 wakati huo nikiwa na miaka 27, kwa hiyo naweza kusema kwamba siifahamu Dar es Salaam vizuri, hata hivyo kutokufahamu Dar haina maana ya kutokufahamu mambo mengine ya kawaida ambayo kwa dunia ya sasa mtu anayeishi mjini kuyajua ni jambo muhimu, lakini pia la kawaida
Siku ninayotaka kuizungumzia ni
Machi mwaka 2001 siku hiyo mjomba wangu ambaye ndiye aliyenilea aliniita na kunituma , aliniambia niende
mjini kwa jamaa yake mmoja nimpelekee fomu zake Fulani, huyo jamaa
azishughulikie, alinielekeza ofisi za huyo jamaa zilipo, mjomba alinipa maagizo
na kumtaja huyo rafiki yake ambaye nikimtaja pengine hata wewe utamfahamu
ukifika pale’Panda lifti ghorofa ya kumi
ulizia ..’, Nilimkubalia na kuondoka ,nataka nikuambie jambo moja ni kwamba
tangu kuja kwangu Dar nilikuwa nimepita majengo kadhaa wa kadhaa na kuona lifti
Nasema kuona, basi nilipojua ni ghorofa ya kumi nilisema iko kazi, nilijiambia
kuwa badala ya lifti ningetumia ngazi tu,Nilipofika kwenye jingo lenyewe ambalo
lilikuwa bado jipya kabisa wakati huo
ilikuwa 2001 nilikwama baada ya kugundua kuwa hata njia ya kupandia ngazi kwa
miguu sikuweza kuiona, Niliona aibu kuuliza kwa hofu ya kuonekana mshamba, Basi
ilibidi nijiunge na watu wengine waliokuwa wakisubiri lifti na kupanda, sikuwa
najua kuwa , nilifikiri labda kungekuwa na dereva na kondakta au mtu Fulani
aliyeniendesha.
Nilioona watu wanadandia name
nikadandia, niliona watu wanaboinyeza kitu Fulani kasha taa inawaka,
Nilijinyamazia, na kiroho kilianza kunidunda, Lifti ikapanda watu wana shuka na
kuingia, mwisho watu wote wakashuka na wakapanda wengine , nilihisi kama lifti
ilikuwa inashuka lakini sikuwa na uhakika nilienda nayo huku nikijaribu
kujiuliza maswal, Niliona watu waliopanda wakishuka tena na wengine wapya
waliingia na lifti ikaondoka kuelekea
huko inakoelekea , Mimi nilibana tu,nilikuwa naangalia watu
wanavyobonyeza lakini sikuwa na uhakika ni kitu gani hasa kinachofanyika ,
Nilitembea na hiyo lifti mpaka nikahisi
kama vile ninjaumwa maradhi ya
moyo au kitu kingine kibaya zaidi Nilikwenda na kurudi kwenda na kurudi tangu kwenye saa tano na nilikuwa na uhakika
kuwa imefika saa nane .
Nikiwa nimefikia hatua ambayo
sasa siwezi kuendelea kuwa bwege yaani kutaka kuuliza, Bwana mmoja mwenye
mavazi ya kaki na bluu aliniuliza vipi hufiki unakokwenda? Tangu asubuhi uko
ndani ya lifti, abiria wa lifti walivunja shingo zao kunitazama kama unavyojua
watanzania masikio yako juujuu kama sungura kutaka kusikiliza ya watu,
Nilibabaika lakini nilijikaza na kusema naenda ghorofa ya kumi lakini sipajui…”
Yule jamaa ambaye kumbe alikuwa ni mesenja kwenye moja ya ofisi kwenye jingo lile
alicheka na kusema ndio maana tangu saa tano hivi nakuona umo humu, naenda
narudi nakuona mzee umo humu, nikadhani unataka kubwedela...” Abiria waliangua
kicheko
Nilitazama chini hasa kwa
kuzingatia kwamba kulikuwa na mademu wengi wakati huo mle kwenye lifti, Yule
mesenja alikuwa kama amepata pa kuonyesha ujuaji wake ‘Ona ukitaka kwenda
ghorofa ya kumi unabonyeza hapa..’ Halafu aliendelea kunifundisha mambo mengine
ya lifti ni tuisheni ya bure lakini!
Nilishuka ghorofa ya kumi na
kuulizia ofisi za Yule jamaa, Nilikuwa nahisi kizunguzugu mtindo mmoja,
Niliambiwa huyo jamaa yake mjomba alikuwa ametoka Ilibidi nimsubiri hadi kwenye
saa kumi aliporejea, Nilimkabidhi fomu na aliponiuliza sababu ya kuchelewa nilimwambia
nilikuwa nimepotea jengo, unadhani wakati narudi nilipanda tena lifti? Kama
unadhani hivyo shauri yako unadhani mbumbumbu niko peke yangu tuko chungu nzima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni