1Samuel 13:13-14 Biblia inasema
hivi “Naye Samweli akamwambia Sauli, Umefanya upumbavu; hukuishika amri ya
Bwana, Mungu wako, aliyokuamuru; kwa maana Bwana angaliufanya ufalme wako kuwa
imara juu ya Israeli milele. Lakini sasa
ufalme wako hautadumu; BWANA AMEJITAFUTIA MTU AUPENDEZAYE MOYO WAKE, naye Bwana
amemwamuru yeye kuwa mkuu juu ya watu wake, kwa sababu wewe hukulishika Neno lile Bwana alilokuamuru”
Daudi alikuwa Mtu aliyeupendeaza Moyo wa Mungu
Paulo Mtume alipohubiri kule Antiokia
katika mahubiri yake aligusia kwa ufupi Historia ya Isarael na kugusa kile ambacho
Mungu alikisema kuhusu Daudi Matendo 13:22 “ ….ambaye alimshuhudia akisema,
Nimemwona Daudi mwana wa Yese, MTU ANAYEUPENDEZA MOYO WANGU,”
Kila mmoja wetu anagefurahi
kuitwa na Mungu “MTU ANAYEUPENDEZA MOYO WANGU”
kila mkristo anapaswa kuhakikisha kuwa anaupendeza moyo wa Mungu, Yesu
aliishi maisha ya ya kumpendeza Mungu kiasi ambacho wakati akibatizwa Mungu
alisema “HUYU NDIYE MWANANGU MPENDWA NINAYEPENDEZWA NAYE” hii ni sifa kubwa
mbele za Mungu Hususani katika ulimwengu huu wa sasa.
Hata hivyo ili sisi nasi tuweze
kumpendeza Mungu na Mungu kuvutiwa nasi kama ilivyokuwa kwa Daudi ni muhimu kwetu kutafakari kwa vipi Daudi
aliupendeza moyo wa Mungu au kujiuliza Daudi alikuwa mtu wa namna gani kiasi
cha kufikia kuitwa mtu aliyeupendeza Moyo wa Mungu, ili sisi nasi tuweze
kufuata nyayo zake: Yako mambo kadhaa ya
kujifunza kutoka kwa Daudi
1. Alilipenda
Neno la Mungu
a.
Aliipenda sheria ya Mungu Zaburi 119:97 (Sheria
ya Mungu ni Neno lake)
b.
Aliliweka moyoni neno la Mungu ili asitende
dhambi Zaburi 119:11(Alilifanya kuwa Muongozo wake)
c.
Neno la Mungu lilikuwa ndio faraja yake wakati
wa Mateso Zaburi 119:50 (kila tatizo alilisuluhisha kwa kuutafuta Uso wa Mungu)
d.
Neno la Mungu lilikuwa ndio chimbuko la amani
ndani yake Zaburi 119:165
Je wewe unaliweka neno la Mungu moyoni, unalisoma,
unalipenda unaliishi unalitafakari? Ni muhimu kulifanya Neno la Mungu kuwa
kinga yetu na dawa yetu kwa kila tatizo hata ikiwemo dhambi.
2. Alipenda
kuomba (Maombi)
a.
Alisema nitaliitia jina la Bwana maadamu
ninaishi Zaburi 116:1-2
b.
Alitambua kuwa Mungu amembariki na atambariki
sana Zaburi 116:12-13
c.
Alitambua kuwa maombi yanamuweka Mungu karibu
naye Zaburi 145:18
d.
Yesu pia alikuwa mwombaji Luka 5:16
Je ni kiasi gani tunapenda maombi, je tunaomba bila
kukoma kama yanenavyo maandiko je tunajilinda katika maombi?
3. Alipenda
Kumsifu Mungu
a.
Alimsifu Mungu kwa sababu ya haki yake Zaburi
119:164
b.
Alimpenda Mungu kwa sababu ya ukuu wake na wema
wake Zaburi 95:1-7
c.
Aliamua kuwa atamsifu Mungu maadamu anaishi Zaburi
104:33
d.
Yesu alipenda kuimba na kumsifu Mungu Mathayo
11:25-26 na 26:30
Je ni kiasi gani unapenda kusifu na kuabudu ni kiasi
gani unajishughulisha na kuimba na kusifu na kuabudu?
4. Daudi
alipenda Umoja miongoni mwa watu wa Mungu
a.
Alipenda ndugu wakae kwa umoja aliona inapendeza
Zaburi 133:1
b.
Alikuwa na ushirika wa karibu sana na Jonathan
1Samuel 18:1
c.
Alitambua pia uchungu wa migawanyiko katika
familia 2Samuel 13
d.
Yesu pia alipenda umoja alituombea tuwe na umoja
Yohana 17:20-23 Alikufa msalabani ili
tuwe wamoja Efeso 2:13-16
Je wewe unapenda umoja, unawafanya watu kuwa kitu
kimoja au unapendelea watu na kuuvunjavunja mwili wa Kristo? Wako watu wengine
leo wanafurahia wengine kupatwa na mabaya, kutengwa na kuwa mbali nao na
kuuharibu mwili wa Kristo
5. Daudi
hakupendezwa na njia za uongo
a.
Alichukia uwongo akiwa na ujuzi wa kutosha
kuhusu mtazamo wa Mungu Zaburi 119:104
b.
Chuki yake dhidi uongo iliathiri shughuli za
uchaguzi wa Marafiki na shughuli zake Zaburi 101:3-4,6-7.
Yesu alichukizwa na uongo na njia zisizo sahii za
mafarisayo
Je wewe unachukia njia za udhalimu? Upendo haufurahii
udhalimu, ni muhimu kwako kuukemea udhalimu kwa Upendo, bila kumsahmbulia mtu,
bali kuishambulia tabia isiyofaa
Biblia inaeleza kuwa Daudi ndiye
awezaye kufanya mapenzi ya Mungu yote, Mtu atakayefanya mapenzi yangu yote,
alikuwa tayari kufanya yote aliyomuamuru Mungu. Moyo wa Daudi ulikuwa tayari
kutimiza kusudi lote la Mungu alilolikusudia. Ni muhimu kuishi Duniani kwa
kulitimiza kusudi lote lile ambalo kwalo Mungu ametukusudia
Mkuu wa wajenzi mwenye Hikima
Rev. Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni