Nilipokea msichana mzuri sana wa kazi hausigeli ambaye nilimpata kupitia rafiki yangu, Huyu rafiki yangu alikuwa na uhitaji wa hausigeli kwa siku nyingio kwa hiyo alitumia watu mbalimbali ili kupata hausigeli, wakati mmoja majibu yalipokuja alipata mahausigeli watatu, kwa kuwa alijua kuwa na mimi ninahitaji alinipa na mimi mmoja kati ya hao
Chui akiwa Mawindoni
Binti huyu alikuwa anatokea Tanga
wilayani Handeni, Alikuwa anataja vijiji tofauti tofauti kila akiulizwa kijiji
anachotokea, mara Kwedizinga, kwediboma, kwedibangala, kwedibago,kwedikwazu n.k
Hilo halikutusumbua kwani kuna watu wengine ni waongo mpaka wanajidanganya
wenyewe.
Alianza kazi juni mwaka 2004, na
hakuwa anajua kupika vyakula vingi, lakini nilijitahidi kumfundisha, pamoja na
maswala ya chooni matumizi ya friji na jiko la umeme kwani kwake vilikuwa vitu
vipya nilimfundisha vyote
Kumbe mwenzangu alikuwa anajua
kila kitu hadi kucheza na intaneti kwa nini sasa akaja kufanya kazi za
uhausigeli hapo ndipo penye habari
Msichana huyu ambaye kweli kwa umbo alikuwa mzuri kumbe kazi yake
ilikuwa ni kuajiriwa kwenye nyumba ambazo anaziona ni alihamdulilah kiuchumi,
halafu baada ya muda anaanza kuwatongoza
baba wenye nyumba , tulikaa naye mwezi mmoja
na mume wangu akaniambia hapa hauna mtoto wa kazi, Awali sikumuelewa
alikuwa anamaanisha nini kumbe binti huyu alishaanza kumuwangia, baadaye
tulikuja kuambiwa kwamba binti huyu akimtafuta mwanaume akishindwa huzua visa
vikubwa, alipoona mume wangu ana
msimamo alianza visa, siku moja
aliniambia kuwa angependa kuondoka kwa sababu hakuja hapo kuvunja ndoa yangu, nilipomuuliza ana maana gani
aliniambia mama wewe ni mtu mzima najua unaelewa, vitu vingine ni aibu hata kuvisema, kwa kweli niliumia sana ,
Nilimwambia avumilie kidogo, Mume wangu alipokuja nilimvaa, Nilipomvaa kwamba
kamtongoza hausigeli mume wangu alicheka na kusema yaani huyo naye ni wa
kutongozwa?
Kama ameshindwa mbinu zake sasa
ndo anataka kutuvunjia ndoa, nitamsweka ndani mwambie’Mume wangu aliniambia
lakini hakunishawishi, vya kutosha, Hatimaye mume wangu aliniambia visa ambavyo
huyu binti alishawahi kumfanyia ikiwemo kumfuata chumbani na kumfunulia nguo
akijidai eti ameumwa na nge kwenye mapaja ili eti mume wangu ajaribu kumtoa
mwiba wa nge huyo, aidha wakati mwingine alijaribu kumshika mabega wakati mume wangu alipoingia jikoni, aidha
mara nyingi alikuwa akimkalia vibaya na kumkonyeza kila wakati
Ilibidi nimfungishe virago siku
hiyo hiyo, Kesho yake nilimfuata Yule rafiki yangu na kuulizia kwa undani kuhusu binti Yule,
akasema ilikuwa leo nikuulize habari za huyo binti maana nimepata habari zake juzi tu hadi nikashindwa kuamini nikasema nikuulize
leo ili ufanye uamuzi nilibaki nimeduwaa Niliambiwa binti huyo alishavunja ndoa
tatu za watu hapa dar katika moja ya
hizo alishaolewa yeye badala ya mama
mwenye nyumba na akamfilisi kabisa mwanaume
Yule na kumwacha kwa hiyo ndoa yangu ilikuwa iwe ya nne kufisadiwa “lo kumbe kalijifanya kapaka kumbe ni chui”
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni