Jumanne, 26 Januari 2016

Kupenda sifa nako ni kazi !


KUPENDA SIFA NAKO NI KAZI
Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1995 na ilikuwa ni hapa Daresalaam, wakati huo tulikuwa tukiishi Magomeni Makanya. Nilikuwa nimemaliza masomo kidato cha nne sekondari ya Pugu, ambako sikufanikiwa kufaulu kwani nilipata Division ziro. 

Kwa hiyo nikiwa nyumbani  nilizongwa zongwa na baba na mama pamoja na ndugu zangu  kwa nguvu zao zote  kutokana na kufeli kule, nakumbuka siku ya tukio hili la fedheha ilikuwa ni mkesha wa Krismasi, nilitoka nyumbani  na kwenda kwa jamaa yangu kinondoni jamaa huyu alikuwa ni rafiki yangu  toka shule ya msingi, naye alianguka masomo ya kidato cha nne kama mimi yeye alikuwa anasoma shule moja ya kulipia kule mbeya, lakini yeye wazazi wake, walikuwa wanajimudu kidogo kwa hiyo mara nyingi hata tukienda outing yeye ndiye anakuwa kibosile  yaani anakuwa tajiri tangu kumaliza masomo hadi majibu kutoka tulikuwa watu wa kutanua sana 


 Dar es Salaam
 Siku hiyo tuiliamua kwenda bichi ambapo jamaa yangu alikuwa ametafuta wasichana wawili, Ile jioni tulipokutana aliniambia kwamba itabidi nichukue msichana mmoja na akaninong’oneza, inabidi ujifanye mtoto wa mtu mkubwa maana demu mwenyewe ni mtoto wa kigogo.Bila kumuuliza ni mtoto wa nani, niulichangamkia tenda  na jamaa yangu alinipa shilingi 6,000 na mimi nilikuwa na 1,200 kwa kipindi kile hizo ni fedha nyingi, halafu yeye jamaa yangu akamchukua demu wake  name nikamchukua wangu,tukaenda kila mmoja njia yake humohumo ukumbini, Yule msichana aliniuliza mimi, ni nani  yaani akitaka kunijua vema 

Harakaharaka nilitafuta jibu, Nilimtaja kigogo mmoja wa serikali wakati ule alikuwa ni naibu waziri, Yule msichana aliniambia nakuuliza ukweli siyo mzaha. Mimi nilikazana kumtaja mzee Yule kwamba ndiye baba yangu. Yule msichana alionekana kukereka na alisema sasa mbona sikufahamu, wakati huyo mzee ni baba yangu mdogo na ninaishi kwake? kwanza nilizani ni mzaha  lakini aliponikazia macho kuzidi kuniuliza nilijikuta nikianza kuchanganyikiwa, nilimwambia kwamaba huyo ni mlezi wangu ndiye aliyenilea ingawa ninaishi na mama yangu, aliniuliza kama nawajua watoto wake  Niliropoka kwamba nawajua, aliniuliza kuhusu Yule mtoto wa Yule mzeeambaye amefariki miezi miwili iliyopita sikuwa na jua lolote na Mkwaju ule ulianza kunituhumu kwa kujikweza Kama umetoka familia masikini si unasema tu kwani mapezni unadhani ni laziam  mtu awe na fedha  au umaarufu! Alianza kunisomea  na kwa sababu alikuwa amekunywa kidogo aliongea kwa kelele kubwa ilibidi jamaa yangu na mkwaju wake waje kujua kulikoni Yule binti alimwambia jamaa yangu nini bwana unanipa jamaa mshamba huyu anajipaka zia ukubwa kwa nguvu jamaa yangu alinivuta  kando na kuniuliza kulikoni Nilipomsimulia  alishika mdomo Ahaya! Umeharibu, huyu binti huyo mzee ni baba yake mdogo na ameishi naye tangu akiwa mdogo, unafikiri ilinibidi nifanye nini? Najua uasubiri umbea kwa hamu kubwa Watanzania bwana! 

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev Innocent Kamote

Hakuna maoni: