ZABURI 71:1-24.
Utangulizi:
Zaburi ya 71 ni zaburi
inayofikiriwa kuwa ni zaburi yatima kwa vile mwandishi wake hajulikani, hata
hivyo naweza kuifikiri zaburi hii kuwa ni ya Daudi kwa vile ina muungano na
Zaburi ya 70 ambayo tuna uhakika kuwa imeandikwa na Daudi, Zaburi hii ni zaburi
ya Maombi na inaonekana kuwa ni maombi yanayofanywa na mtu mzima au mzee,
akililia msaada wa Mungu kwa Haraka.
Zaburi 71:1-4.
Mwandishi amekuwa mtu mzima
lakini maisha yake ya uzee yanasumbuliwa na adui, adui mwenyewe ni mwovu,
katili na mdhalimu hana huruma, anachokitaka ni kusambaratisha na kuangamiza
maisha ya mtu huyu, Mzee anaona ni kama ataaibishwa hapa, Uzee hapa pia unaweza
kutumika kama uzoefu. Kutokana na mazingira haya magumu ya kuzungukwa na adui,
mwovu na mdhalimu, Mwandishi anaonyesha kuwa ana uzoefu kuhusu Mungu na jinsi
alivyoweza kumshindia vita za aina mbalimbali katika maisha.
Mstari 4 “Ee Mungu wangu uniopoe
mkononi mwa mkorofi, Katika mkono wake mwovu Mdhalimu”
Mwandishi wa Zaburi anajua kuwa
hakuna njia nyingine, namna iliyoko mbele ni kumuomba Mungu na hivyo
anajitegemeza katika kuomba na kumkumbusha Mungu namna alivyomshindia vita za
aina mbalimbali, tangu ujana wake na jinsi Mungu alivyokusudia mema tangu
kuzaliwa na tangu tumboni mwa mama yake Zaburi
71:5-9.
Mwandishi anaangalia mpango wa
adui wa sasa “Mstari wa 10-11” “kwa
maana adui zangu wananiamba nao wanaoniotea roho yangu hushauriana , wakisema ,
Mungu amemwacha, Mfuateni mkamateni, hakuna wa kumponya”
Adui ana mpango mbaya juu ya maisha
ya kila mmoja wetu, anataka kuivizia roho yetu anataka kutuua, anafikiri Mungu
ametuacha, anafikiri ni kipindi cha kutukandamiza,kutukamata na hakuna namna
tunavyoweza kuponyoka. Haya ndio yalikuwa mazingira ya mwandishi wa zaburi hii
na wakati mwingine huwa ndio mazingira yanayokuzunguka.
Mst 12-24 mwandishi kupitia
uzoefu alionao anatabiri kuwa Mungu hatamuacha aaibike milele na kuwa Mungu atakuwa upande wake na kuwa Mungu
atampigania na kuwa atasimulia na kushuhudia Matendo makuu ya Mungu na na sifa
zake na haki yake kwakuwa wameaibishwa wametahayarika walionitakia mabaya,
waliokusudia kumuaibisha wameaibishwa wao.
Msomaji wangu Ukimtumaini Bwana
hutatahayarika!, Mungu ndio kila kitu katika maisha yetu ni lazima tumkimbilie
na kumtegemea yeye kwake kunalipa tukimtegemea Mungu, hatatuacha tuaibike,
Bwana atakushindia kutoka vita moja kwenda nyingine aina yoyote ya udhalimu wa
kishetani, kiafya, kiuchumi, kikazi, na mengineyo Mungu atatutetea yeye alisema
nitawapigania nanyi mtanyamaza kimya Neno la Mungu ni dhahiri na tujikinge
kwake
Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima.
Rev. Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni