Kutoka 3:1-4:17
1.
Mungu
alipomtokea Musa katika kijiti kilichokuwa na utukufu
a.
Alimuita
Musa ili kuwaongoza Israel kutoka katika Inchi ya Utumwa Misri
b.
Musa
alionyesha Mashaka yake wazi na kutoa sababu zinazodhihirisha kwa nini hafai
kwa kazi hiyo
2.
Musa
alionyesha Mashaka yake wazi na Bwana Mungu alikuwa akimjibu Musa, Mashaka ya
Musa ndio somo kubwa sana kwetu
a.
Kwa
sababu ni katika njia inayofanana watu wengi sana leo hupewa na Mungu wajibu
Fulani na hata wito wa kumtumikia Mungu
b.
Si
kwaajili ya kuwatoa watu katika utumwa kama ilivyo kwa Musa kule Misri, lakini
kwa Ulimwengu kwaajili ya kuwahubiri habari njema Marko 16:15 1Petro 2:9
ili waokolewe
c.
Kama
ilivyokuwa kwa Musa wengi wetu tunatoa Udhuru na kuonyesha Mashaka, Mashaka ya
Musa yanaweza kugawanywa katika maeneo Matano yafuatayo;-
A.
Mimi ni nani? Kutoka 3:11 Musa akamwambia Mungu, Mimi ni nani……
1.
Ingawa
Musa aliwahi kuishi katika Ikulu ya Farao mtawala wa Misri
a.
Sasa
alikuwa mchungaji wa mifugo ya mkwewe akiwa mtu duni
b.
Miaka
40 ilikuwa imepita tangu alipoondoka kwa Farao
c.
Sasa
alikuwa mtu mzima mzee wa miaka 80, nguvu za ujana zimekwisha na yuiko na fimbo
tu Musa aliweza kuwa na sababu za haki za kufikiri kuwa huenda yyeye si mtu
sahii
2.
Mungu
alimjibu Musa Kutoka 3:12 asiwe na Mashaka kwani yeye atakuwa Pamoja
naye
a.
Bila
shaka mimi nitakuwa Pamoja nawe
b.
Mungu
anapomuahidi mtu atakuwa Pamoja naye maana yake Yeye mwenyewe Mungu ni
Utoshelevu wetu
c.
Paulo
mtume alisema kama Mungu akiwa Upande wetu yaani pamoja nasi ni nani
atakayeweza kusimama kinyumenasi Warumi 8:31
B.
Baadhi
yetu leo tunatoa Udhuru au kuonyesha Mashaka kama Musa
1.
Tunajiangalia
wenyewe na kujipima na kuona kwamba hatutoshelezi/hatustahili kwa vigezo vya
kuwa watumishi wa Mungu
a.
Ni
kweli kabisa hakuna mwanadamu anayetosheleza katika utumishi na huduma hii
kimsingi hata mimi pamoja na kujiita Mkuu wa wajenzi katika Huduma hii kila
siku najigundua kuwa sistahili kabisa kumtumikia Mungu, sio hivyo tu huwa namshangaa
Mungu kwa nini anitumia mtu kama mie
b.
Lakini
Mungu ni Utoshelevu wetu 2Wakoritho 3:5-6 “ Si kwamba twatosha sisi
wenyewe kufikiri neno lolote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu
watoka kwa Mungu, Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya”
c.
Unaudhuru
gani Elimu? Angalia kuwa Mungu aliwatumia mitume ambao wengi wao walikuwa wasio
na Elimu Matendo 4:13
d.
Kama
ilivyokuwa Mungu kwa Musa, Yesu Kristo anakutia moyo leo usiogope atakuwa
pamoja nasi hata ukamilifu wa Dahari Mathayo 28:20
e.
Kwa
msaada wake tutayaweza yote Wafilipi 4:13.
C. Niwaambie
Nini? Imekaa vema
kwa kimombo what shall I say? Kutoka 3:13
1.
Musa
alijua kwamba anapaswa kuwaendea Israel, na wako kifungoni wakiwa na maswali
lukuki
a.
Wangemuuliza
Mungu yupi aliye kutuma?
b.
Kwa
nini tuondoke hapa tumekuweko kwa miaka 400, tumezaliwa hapa haya ndio maisha
yetu na tamaduni zetu
c.
Ni kama
Musa alukuwa akijiuliza ninaanzia wapi?
2.
Mungu
alilazimika tena kumjibu Musa, mwenye mashaka
a.
Mimi
niko ambaye niko, Utawaambia Kutoka 3:14-15
b.
Mungu
alikuwa na majibu kwa Musa kuhusu nini cha kusema
D.
Baadhi
yetu tunaweza kuwa na mashaka kuhusu nini cha kusema
1.
Tuna
mashaka kwa sababu wakati mwingine tunafikiri kuhusu maarifa yetu yasotosheleza
2.
Lakini
Mungu ataweka maarifa na nini cha kusema
a.
Atakupa
neno rahisi Marko 16:15-16
b.
Na ni
jinsi gani itakuwa Rahisi 1Koritho 15:1-4,2:2
c.
Hata
Musa alipokuwa ameelekezwa nini cha kusema akaibuka na sababu nyingine
E. Je
wasiponiamini wala kunisikiliza?
1.
Musa
sasa amepewa Maarifa na anajua nini cha Kusema lakini anawasiwasi hawatamuamini
walakumsikiliza?
a.
Ni dhahiri
kuwa Musa alikuwa anaogopa kukosea
b.
Anaogopa
matokeo magumu na amesahau kuwa Mungu alisema atakuwa Pamoja naye
2.
Mungu
alimsaidia Musa kuondoa mashaka na kumuaminisha kuwa yuko naye
a.
Fimbo
ya Musa iligeuka kuwa nyoka Kutoka 4:2-5
b.
Mkono
wake ulipatwa na ukoma
c.
Maji
yaliyogeuka Damu Kutoka 4:9.
F.
Wengi
wetu tunamashaka na majukumu na wajibu tuliopewa kuutumikia na kwa watu wa
Mungu wana mashaka kama wanafaa kuwa chombo cha kuhubiri injili
1.
kumbuka
woga ni adui anayekuzuia katika kujaribu
2.
Kama
Mungu alivyomjibu Musa na kuondoa mashaka aliyokuwa nayo tunao ushahidi
unaoweza kututhibitishia na kutuondolea mashaka juu ya kile Mungu anataka
tukitimize
a.
Neno la
Mungu liko kwaajili yetu Warumi 10:17, Yohana 20:30-31
b.
Yesu
alikufa na maefufuka Yuko hai ni yeye anayetenda kazi ndani yetu
c.
Migandamizo
na kelele kutoka nje isikutie mashaka ukaacha kumuamini Mungu kuwa yu aweza
kukusaidia na kuwa yuko pamoja nawe na kuwa vita si yako ni yake yeye na kuwa
hata wajibu na kazi tuliyopewa ni kwa utukufu wake.
G. Mimi
sio Msemaji, Mimi sio mwepesi wa Kusema!
1.
Tunaona
mashaka haya katika Kutoka 4:10
1.
Musa
alisema mimi sio mnenaji Mzuri? Je umeshawahi kuwasikia baadhi ya viongozi
wakisema neno mimi sio Mwanasiasa? Unajua wanamaanisha nini? Wao sio wasemaji,
sio wazungumzaji wazuri
2.
Mungu
hasukumwi na Udhaifu wa Mwanadamu anatujua tulivyo hata kabla hajakuita au
kukupa wajibu
3.
Anaujuzi
wa kuwatumia hata waliodhaifu ndio si tuliumbwa kwa kusudi lake uwe na uwezo
usiwe na uwezo yeye akiamua anakutumia
a.
Mungu
alimsaidia Musa kujua Yeye ndiye Muumba ndiye anayeruhusu mtu kuwa Bubu au kuwa
msemaji, Mungu alikuwa anaelewa wazi udhaifu wake na kama udhaifu wake ungekuwa
ni sababu ya yeye kushindwa kumtumia asingelimfuata
b.
Mungu
anauwezo wa kumsaidia kila mtu katika madhaifu yake
c.
Mungu
alimuahidi tena Musa kuwa atakuwa pamoja naye Kutoka 4:11
d.
Mungu
alimuandaa haruni kwaajili ya kumsaidia Musa Kutoka 4:14-16 Mungu wakati wote
ataandaa watu wa kututia moyo na kufanya kazi pamoja nasi.
H.
Sisi
nasi tunaweza kuwa na mashaka na kutoa udhuru kama huu wa Musa,
1.
Paulo
mtume Hakuwa na ufasaha wa Maneno wala hekima kama zile za wagiriki, alikuwa
dhaifu, mwenye hofu na mwenye kutetemeka sana 1Koritho 2:1-5, Lakini pamoja na
hayo alimtegemea Mungu na sio hilo tu aliwatia moyo na wengine
“Imani yetu isiwe katika Hekima za wanadamu bali
katika nguvu za Mungu”
Musa
aliogopa kuwa mnenaji eti kwa vile alikuwa na Kigugumizi Kutoka 4:13 Mungu
hakukiondoa kigugumizi kila japo angeweza kufanya hivyo Mungu alikusudia
kumtumia pamoja na udhaifu wake
I. Tuma huyo utakayemtuma! Kutoka 4:13.
Mungu
alikubaliana na Mashaka yote ya Musa na kila mashaka yake yalikuwa na Majibu
lakini sasa Mungu anakasirishwa na tabia ya Musa wakati huu, Sasa Musa hataki
kabisa kwenda!
1.
Mungu
ametuumba kwa kusudi lake ni lazima tutmika bila kujali udhaifu tulionao kwa
vila kila aina ya udhaifu una majibu kwa Mungu
2.
Ukikataa
kumtumikia Mungu au kulitumikia kusudi la Mungu unajiweka katika wajibu wa
kumtumikia shetani
3.
Hasira
za Mungu kwa Musa zilikuwa za upendo, Mungu alikuwa anataka kumtumia Musa ndiye aliyekuwa amamemuandaa kwa Muda mrefu
kwa kusudi hilo
Ndugu zangu
a.
Kila
udhuru na kila sababu utakayoitoa kukwepa kutokumtumikia Mungu ni Upotoshaji wa
haki ya Mungu
b.
Ni
kweli tungetamani kama Mungu angelimtumia mtu mwingine mbadala
c.
Ni
kweli hatupendi kutenda kila Mungu anachokitaka
d.
Lakini
ndugu hapo ndipo hasira za Bwana zinapowaka na kuwa kinyume nasi, hatuwezi
kuacha kulitumikia kusudila Mungu wetu hata kama kuna hali zinazokataa endapo
hali hizi zimetokea kwetu kutoa udhuru tunahitaji kutubu
Hatimaye!
Wote tunajua kuwa Musa alikubali, wito wa kwenda Misri
Wote tunajua kuwa Mungu alikuwa pamoja naye na kumsaidia
Wote tunajua dhahiri kuwa Musa sasa anaheshimika na kukubalika na watu
wote kama kiongozi mkubwa sana wa manabii na baba wa taifa la Israel, Ukiondoa
shaka na kumuamini Mungu atakutumia kwa viwango vya juu kwa utukufu wake.
Mungu
hatuimii watu maalumu sana, Tunakuwamaalumu Mungu anapokuwa Pamoja nasi
God
never use the superman, we became the superman when God is with us
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
0718990796
0784304550
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni