Zaburi
92:12-15.
Nyakati hizi tulizo nazo
kumekuwepo na wimbi kubwa sana na shauku ya watu kutakakufanikiwa, na watu wengi sana wanafanikiwa kwa vile
wana nia ya kufanikiwa, hata hivyo, mafanikio ya watu wengi sana hustawi kwa
muda mfupi na baada ya muda hufilisika na kuishiwa kabisa au kubakiwa na
historia ya jinsi walivyofanikiwa!
Mungu katika mapenzi yake
anataka tufanikiwe sana, lakini zaidi anataka tufanikiwe na mafanikio yetu
yaweze kudumu kizazi na kizazi, Biblia inapozungumzia ustawi wa kudumu
inazungumzia miti miwili yaani mtende na Mwerezi wa Lebanon, hii
ni miti inayotumiwa na biblia kutufundisha mafanikio ya kudumu, lakini katika
somo hili leo tunauangalia zaidi MTENDE tutajifunza somo hili kwa
kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo
- · Ufahamu kuhusu mti wa Mtende
- · Mambo ya kujifunza kutokana na Mtende
- · Jinsi ya kusitawi kama Mtende.
Ufahamu
kuhusu mti wa Mtende.
Kwa kawaida miti jamii ya mitende iko Mingi sana, kuna jamii zaidi ya 2600
ya mitende, lakini iliyo maarufu ni miwili, acacias palm tree na coconut
palm tree kwa msingi huo miti jamii ya minazi ni jamii ya mitende, Mawese
ni jamii ya mitende. Kama utataka kujua kwa undani kuhusu miti hii unaweza
kutafuta google Palm tree/Wikipedia. Kwa Kiaramu na Kiethiopia mtende unaitwa
“TAMAR” Kiarabu “Date” na wengine huiita Phoenix.
Mti huu katika Biblia umetajwa kama moja ya miti Maarufu sana ambao
hutumika kuelezea Ushindi, amani na Ustawi. Katika Israel mti huu huhesimika
sana na unatumika kama moja ya nembo ya Taifa ukihusihwa na Taa ya vinara Saba.
Biblia inautaja mti huu kwa sababu ya mafundisho kadhaa
1.
Ushindi na amani na Ustawi Kutoka 15:27
watu wa Mungu waliburudika baada ya Ushindi
2.
Ni Malimbuko ya Canaan Mji wa kwanza kupewa na Mungu
kwa Israel Yeriko ulikuwa na mitende mingi sana na uliitwa mji wa mitende
Kumbukumbu 34:1-3, Waamuzi 1:16
3.
Mtende unazungumzia Faraja na furaha na kurejeshwa
2Nyakati 28:15
4.
Katika Biblia kama mtende umekauka ilihesabika kuwa Furaha
imeondokwa kwa wanadamu Yoeli 1:10-14 na ilihitajika maombi na toba kurejesha
furaha hiyo
5.
Mitende ilitumika kama mapambo na sifa ya uzuri
1Falme 6:28,32, wimbo bora 7:7
6.
Ni alma ya Ushindi wa sasa na ujao Yohana 12:12-12,
Ufunuo 7:9-10
Mambo ya
Kujifunza kutoka na Mtende.
1.
Jamii ya mitende ni miti inayostawi popote na
hustahimili ukame Inazungumza kuhusu Uvumilivu.
2.
Miti jamii ya mitende haina muda wa kubughudhi
miti mingine, inakua kuelekea juu
3.
Mitende Haiweki kinyongo inapukutisha Majani
ya zamani na kuzalisha Mapya Inazungumzia kusonga mbele bila kujali ni magumu
gani unayapitia
4.
Miti ya mitende inawafanya watu waangalie juu,
inakumbusha kuabudu, inaelekeza kwa Mungu inakumbusha watu kumtegemea Mungu.
5.
Mitende inawapa watu Burudani, inawapa watu makazi,
inafunika inazungumzia Amani
6.
Miti mingi ya mitende Imenyooka Straight,Upright
Inazungumzia Unyofu wa Moyo,Ayubu 1:1 na Joshua 1:7-10
Jinsi ya
Kustawi kama Mtende
1.
Ishi maisha ya Haki, unaweza kujiuliza mtu wa haki
ni Mtu wa namna gani
a. Hawana muda wa
Kuaibisha wengine Mathayo 1:19
b. Hukaa katika
maagizo ya Bwana bila lawama Luka 1:5-6
c. Anakuwa Mcha Mungu
Luka 2:25
d. Utamtegemea Mungu
katika hali zote ziwe njema au mbaya na hatima yako ni suhindi
Warumi 8:33-39. (Yesu alipoingia Yerusalem
alishangiliwa kwa matawi ya miti ya mitetende kumaanisha Ushindi, utawala na
Amani ya Mungu wa Kweli)
Mwisho wa Yote, Utaishi Maisha Marefu, ukiwa na Matunda wakati wote, na
hutayumbishwa na upepo wakati wote bila kujali ukame au mvua utazaa matunda na
haya ndio mafanikio ya Mtende.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni