Ni mwaka 1994 wakati nilipoingia kwenye kasheshe kubwa
ambayo nusura iniingize jela, nikiwa ndio nina mwaka wa pili tangu nimeanza
kazi nilimpachika binti mmoja mimba alikuwa ni binti wa shule akisoma darasa la
sita wakati ule ,mwili wake ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ukiambiwa kuwa yuko
darasa la nne ungebisha lakini alikuwa bado mdogo ,baada ya kumpachika mimba
mjomba wake ambaye ndiye aliyekuwa
akiishi naye alilifungia kibwebwe suala lile akitaka nipelekwe mahakamani,
ndugu zangu na jamaa zangu walijitahidi kwa kadiri wawezavyo kuzuia jambo lile
kufikishwa mahakamani, Mjomba wa binti alikubali lakini kwa sharti moja tu la
mimi kumuoa mpwa wake mara moja
Kumpa mwanamke mimba Ni neema au Karaha hasa inapokuwa sio mwanamke halali
Nilikubali kufanya hivyo haraka
kwani nilishauona mlango wa ukonga ukiwa wazi mbele yangu, Nilimuoa binti Yule
kwa ndoa ya mkeka wazazi wake hawakuweko kwani wanaishi vijijini mkoani Ruvuma,
mwezi huo huo nililazimika kwenda mbeya kikazi , ambapo nilitakiwa kuishi kwa
miezi mitatu kwa ajili ya kazi ya mkataba
ambayo kampuni yetu ilipata, Nilipokuwa Mbeya nilipata mwanamke ambaye
alionekana kuwa ana adabu za kule kijijini kabisa , huyu nilimpata hospitalini
nilipokuwa nimekwenda kutibiwa maralia , wiki ya tatu tangu kufika pale ,
Mbeya.
Sijui tulizoeana vipi Lakini
alikuja kuwa rafiki yangu, alikuwa ni mwenyeji wa Ruvuma na pale Mbeya alukuwa
amekuja kumuuguza kaka yake ambaye alilazwa katika hospitali ya rufaa pale
mbeya nilimpenda kwa kweli hasa nidhamu yake na hekima kiumri alikuwa amenizidi miaka mine, yaani
mimi nilikuwa na miaka 29 na yeye 33, lakini kwa kutazama mimi ndiye
nilionekana mkubwa, niliishi naye kama mke wangu hadi miezi mitatu ikaisha.
Nilirudi Dar nikimuacha bado anauguza mgonjwa wake, wiki mbili baadaye
alinijulisha kuwa Yule kaka yake amefariki na walikuwa wanakwenda kuzika Ruvuma
, Bahati mbaya ni kwamba, siku hiyo hiyo , tuliletewa taarifa Baba wa mke wangu
alikuwa amefariki, nilisahau maswala ya hawara yangu na nikaweka nguvu kwenye
kifo cha baba mkwe.
Tuliamua kusafiri kwenda Ruvuma
mke wangu wakati huo ana mimba ya miezi sita, tuliondoka mimi yeye na ndugu yangu
mmoja, tulifika kijijini kwao jioni ambapo tulikuta mazishi yakiendelea ,
tulikwenda makaburini , tukimwacha mke wangu nyumbani kutokana na hali yake,
tulipofika makaburini tulikuta ndiyo zamu ya kuweka mashada ya maua ikiwa
inaendelea ilikuwa kama ndoto Fulani
kwani nilimuona Yule hawara yangu wa mbeya akiweka shada la maua huku akitajwa
kama mke wa marehemu. Nilihisi kama nataka kupoteza fahamu Nilijikaza ingawa
nilikuwa natoka jasho sana
Baada ya mazishi tulirudi
nyumbani ambapo ilibidi nitambulishwe kwa mzazi wa mke wangu na ndugu zake
Nilitambulishwa kwanza kwa mama mkwe ambaye kumbe kule Mbeya alikuwa ni hawara
yangu kila mmoja kati yetu alijikaza ili
isifahamike kinachoendele, lakini hiyo haikudumu kwa muda mrefu kwani mama mkwe
wangu alilazimika kusema kwa wazazi wake ati akiogopa mkosi utokanao na jambo
hilo, ilibidi siku ya nne baada ya msiba tufanyiwe tambiko la kiasili kuondoa
laana, nataka nikuambie katika maisha
yangu huu ulikuwa mtihani mgumu, ninaye bado mke wangu na tumayasahau
yaliyopita mama mkwe hajawahi kuja kwetu, ingawa sisi huwa tunaenda na kukaa
siku chache kwake kila mwaka
na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni