Mstari wa Msingi: 1Samuel 16:7 “Lakini Bwana
akamwambia Samuel, Usimtazame uso wake wala urefu wa kimo chake ; kwa maana
mimi nimemkataa. Bwana haangaliikama binadamu aangaliavyo; Maana wanadamu
huitazama sura ya nje, bali bwana huutazama moyo”
Mfalme Daudi alipatikana kwa Mapenzi ya Mungu na sui kwa shinikizo la Wanadamu
Utangulizi:
Hivi Karibuni Nchi yetu itakuwa na uchaguzi mkuu wa
Rais, wabunge na madiwani, na kwa upande wa uchaguzi wa Rais ni wazi kuwa
nafasi hii inahitaji Rais mpya kwa mujibu wa utaratibu tuliojiwekea, ni wazi
kuwa kwa Tanzania, Marais hutokana na vyama vya kisiasa na hivyo vyanzi
vinavyoweza kuleta Rais ni vyama vya siasa, na iko wazi kuwa kuna vyama vya
siasa kama CCM, CUF, NCCR, CHADEMA, UDP, DP, ADC, na kadhalika, wote tunakubali
kuwa moja ya chanzo kikubwa kinachoweze kutupatia viongozi katika Tifa hili ni
CCM, hili halina ubishi kutokana na mfumo mzima ulivyo kwa taifa hili, ingawa
inaweza kutokea tofauti wakati mwinginine lakini kwa Tanzania sio sasa
Katika wakati huu wa uchaguzi kuna mambo mengi ya
kujifunza, au ambayo tunaweza kuwa wote tumejifunza na ni dhambi kuyakalia
kimya bila kuyatafakari, vinginevyo Historia itatuhukumu!
Katika chaguzi za nyuma zilizopita, vituko kadhaa
vilivyopata kushuhudiwa ilikuwa ni pamoja na kutabiriwa kumwagika kwa Damu,
tetesi za vita, maonyo dhidi ya taifa, na pia baadhi ya watu kutabiri kuwa
Fulani ndio chaguo la Mungu n.k.
Uchaguzi wa mwaka huu pia kupitia ndani ya mchakato
wa CCM wengi wetu, tuliona na kushuhudia watu walionyesha wazi kuwa ni nani
amechaguliwa na Mungu kuiongoza Tanzania kupitia CCM, watumishi wa Mungu,
wachawi, wanajimu na Mashehe kila mmoja alikuwa na majibu kuwa ni nani anafaa
kuwa kiongozi wa Taifa hili wakati Kikwete akiondoka Madarakani
Neno la Mungu lina majibu ya kutosha kuondoa utata
huo uliojitokeza, kwa kurudia Historia ambayo watanzania lazima tuikumbuke kila
wakati na kujifunza kutoka katika Neno lake namna na jinsi MUngu anavyojipatia
viongozi.
Biblia imejaa Mifano mingi jinsi Mungu alivyojipatia
viongozi wa aina mbalimbali wengi wao wakiwa ni hodari, viongozi hao wanaume
kwa wanawake, wafalme, waamuzi, makuhani, manabii na Mitume Je Mungu
aliwapataje viongozi hao ni mfumo gani Mungu aliutumia kupata viongozi? Njia
hii ya Mungu kujipatia viongozi ikitumika katika taifa letu tutaona viongozi
wazuri na watakaotimiza mengi makubwa katika Taifa letu wakiendelea kupatikana
Jinsi Mungu anavyochagua viongozi
Katika
Mstari wetu wa msingi pale juu tunaona kuwa Daudi ni moja ya mfano wa viongozi
waliopata kuiongoza Israel na kuiletea heshima kubwa sana, aliongoza Israel kwa
miaka 40, Isamuel 16. Israel walikuwa chini ya utawala wa Saul ambaye sasa
alikuwa anafikia ukingoni, Na Mungu anamtuma Nabii Samuel katika Familia ya
Yesse akimueleza wazi kuwa amejipatia mfalme katika wanawe ! 1Samuel 16:1.
Hakuna mtu alimjua si Samuel wala hata Yese mwenyewe ambaye alikuwa ndio chanzo
kikuu cha kumleta mfalme!
Kumbuka
kuwa hakukuwa na uteuzi wa kiofisi, hakukuwa na Kampeni, wala mijadala wala
kujitangaza kwa mbwembwe, wala kwa kueleza sera mipango na mikakati au nini
wataufanyia utawala wa Israel, Bali Mungu mwenyewe aliangalia na kuchagua ni
nani atakuwa mrithi wa Sauli, sio hivyo tu lakini hebu chunguza njia ambayo Mungu
anaitumia kumpata kiongozi ambaye ni chagua lake!
Wakati
Samuel anafika nyumbani kwa Yese, Yese ambaye ni chanzo kikuu cha kutoa
kiongozi anawaleta mbele ya nabii wanae wote wakubwa akiwa na furaha sana,
Kumbuka kuwa hata Samuel hakuwa anajua kuwa ni nani atakuwa mfalme licha ya
kuwa Nabii mkubwa na mwenye uzoefu na ujuzi kuhusu sauti ya Mungu Mungu
alimwambia wazi “USIMTAZAME USO
WAKE,WALA UREFU WA KIMO CHAKE, KWA MAANA MIMI NIMEMKATAA” Ni maneno magumu
sana haya kutoka kwa Mungu hasa kama yanaelekezwa kwako kukataliwa Mh? Ni kama
ukatili Fulani hivi lakini Mungu yuko kazini tena makini kuhakikisha kiongozi
bora anapatikana, kwa sababu yeye haangalii mbwembwe za nje anaangalia Moyo!
Ni
wazi kuwa wana wote wa Yese waliopitishwa kwa Samuel Mungu aliwakataa Mstari
8-10 Mungu anauwezo wa kuchunguza moyo Ayubu 34:21, Waebrania 4:13, 1Yohana
3:10. Mungu ana namna yake ya kuangalia
mambo katika namna iliyo njema kabisa nay a kiungu, na hivyo wana wote wa Yese
waliopitishwa hawakuwa wanafaa kwa kwa nafasi ya Ufalme, Mwisho Yese alimuita
mwanae mdogo Daudi ambaye hakuna hata mmoja alidhania kuwa angefaa hata kuletwa
mbele ya Samuel
Hakika
Mungu huchagua viongozi katika namna tofauti kabisa na sifa na mitazamo ya
kibinadamu
Kila
mahali katika Biblia tunaweza kuona mifano hii ya jinsi Mungu alivyojipatia
viongozi, Musa aliyekuwa na miaka 80 akichunga kondoo wa mkwewe jangwani,
Malaika wa Bwana alimtokea na kumuagiza awaongoze Israel kutoka Misri Kutoka 3.
Elisha alikuwa akilima kwa ngo’mbe kwa jozi 12 na Eliyanabii alipita na
kumtupia vazi kama ishara ya kuwa mrithi wake (1Wafalme 19:15-21) kumbuka kuwa
Eliya aliambiwa watu ambao alipaswa kuwatia mafuta ambao Mungu alikuwa
amewachagua, wakiwemo wafalme wa Israel na Syria
Katika
agano jipya mitume walichagua mtume mwingine ili kujaza nafasi ya Yuda
aliyemsaliti Yesu, kwa kura lakini waliomba Mungu awaonyeshe ni nani
aliyemchagua kati ya wawili waliopendekezwa Matendo 1:24-25 waliomba Mungu
anayejua mioyo ya watu awaonyeshe. Hilo ni la Muhimu sana!
Mungu
pia aliamua kumchagua mtu mwingine aliyeitwa Sauli ili awe Mtume yeye mwenyewe
Matendo 9 Sauli yaani Paulo alitambua mara moja kuwa alikuwa akiwatesa watu wa
Mungu, aliokoka na kubatizwa na akawa mtume mkubwa sana ilileta mashaka sana
kwa watu wa kanisa wakati huo lakini kumbuka maneno haya Matendo 9:15 “ Lakini
Bwana akamwambia Nenda tu kwa maana huyu
ni chombo kiteule kwangu alichukue jina langu mbele ya mataifa , na wafalme na
wana wa Israel”
Mtu
anaweza kudai kuwa hawa walikuwa viongozi wa kiroho, na labda Mungu hajihusishi
na uchaguzi wa viongozi wa kisiasa na wakuu wa serikali kwa nnjia hizo! Jibu ni
Hapana Mungu pia hujihusisha kuchagua viongozi wa kisiasa kama tulivyoona
kuhusu mfalme wa Israel na Syria pale juu Biblia iko wazi kabisa kuwa aliye juu
ndiye anayetawala katika falme za wanadamu Daniel 4:17 “hukumu hii imekuja kwa
agizo la walinzi, na amrihii kwa neno la watakatifu: kusudi walio hai wapate
kujua ya kuwa Aliyejuu anatawala katika ufalme wa wanadamu naye humpa amtakaye
tena humtawaza juu yake aliye myonge
(myenyekevu)”
Hata
inapotokea kuwa wanadamu wanalazimisha kiongozi wa aina wanayemtaka Bado Mungu
huchagua yeye mwenyewe lakini mabaya yatakayowapata yatakuwa ni matokeo ya
kutaka kwenu, Mungu aliwafanyia Israel walipotaka ufalme kama mataifa mengine
kinyume na Samuel 1Samuel 10:23-24 Mungu akiruhusu wanadamu wakajichagulia
atakuacha upate somo kuwa uchaguzi wa mwanadamu ni wa kipuuzi na tutaumia!
1Samuel 9: 15-17
Ni
muhimu kufahamu kuwa Mungu anapochagua wala haiitajiki kampeni wala uchaguzi
kwa vile sio DEMOCRACY lakini ni THEOCRASY yaani sio Mfumo ambao watu wengi au
wote wanapata nafasi ya kuchagua MKUMBO bali ni mfumo ambao Mungu anaibua
kiongozi kwa jicho lake kutoka kusikotarajiwa, uchaguzi wa Mungu hautokei chini
kwenda juu bali juu kuja chini, HIVYO SAUTI YA WENGI SIO SAUTI YA MUNGU!
Nakazia tena SAUTI YA WENGI SIO SAUTI YA
MUNGU mwisho wa kujinukuu.
Kampeni
na uchaguzi wa kupiga kura uko kwaajili ya kuendeleza tabia ya kiongozi na
kutekeleza mapenzi ya Mungu, lakini ukweli Mungu anapochagua huitaji
kuwashawishi wanadamu kwa namna yoyote wala kwa sera na mipango utakayoifanya
Mungu anawaweka katika ofisi na watu wanatakiwa kumfuata.
JINSI
GANI VIONGOZI WANAWEZA KUFANIKIWA?
Hili
ni swali muhimu Je kila kiongozi anayetokana na Mungu anaweza kufanya vizuri
jibu ni ndio ikiwa wataendelea kumfuata Mungu na maagizo yake “Yoshua 1:5-9, 1Wafalme 1:1-3” Hata baada ya kufa kwake Daudi
ingawa aliwahi kufanya dhambi katika maisha yake anasifiwa na Mungu kama mtu
aliyeupendeza Moyo wa Mungu Matendo 13:22, Musa pamoja na makubwa
aliyoyafanya na madhaifu aliyokuwa nayo anatajwa kuwa mtu mnyenyekevu zaidi
kuliko wote waliokuwa juu ya uso wa duni Hesabu 12:3, Mungu hutuchagulia
viongozi wazuri wenye kuleta ufanisi mkubwa, wenye moyo na uzalendo
atakaowatumia kwa namna ya kupita kawaida na kuleta mafanikio makubwa ambayo
kila mtu anayataka na watu hupata faraja kubwa na kufurahi
Mithali 29:2 “ wenye haki wakiwa na amri watu
hufurahi bali mwovu atawalapo watu huugua”
Je ungependa nani akuchagulie kiongozi ? Mungu
huchagua viongozi
Kumbuka.
·
Kiongozi anayetoka kwa Mungu ni
vigumu kumtambua mpaka Mungu amfichue, Samuel alikuwa nabii mkubwa lakini
ilikuwa ngumu kwake kujua Mungu anamtaka yupi katika shina la Yese
·
Tuwasamehe viongozi wote wa dini
waliotabiri na kutamka kuwa mtu Fulani ni chagua la Mungu na wengine Fulani
asipokuwa Raisi mniue kwa vile hao ni wanadamu na huenda hawajui Mungu
anajipatiaje viongozi
·
Tuwasamehe watabiri na wanajimu kwa
vile inawezekana uwezo wao wa kuona uliishia kwenye nyumba ya Yese yaani
walitabiri wale walioishia kwenye tano bora ua wengine waliokatwa mapema
tuwasamehe kwa vile ni wanadamu na hawajui mapenzi ya Mungu
·
Tuache kujivuna na kujifikiri kuwa
sisi ni watu maalumu tunayoweza kuyajua mapenzi kamili ya Mungu aidha tuache
kwenda kwa Mkumbo kwa vile Mungu hachukuliwi na umati wa watu
·
Acha kuwaombea na kuwalilia wale
ambao Mungu amewakataa Mungu hutazama Moyo, wajibu wetu siku zote ni kumuomba
Mungu atuonyeshe ni nani aliye katika mapenzi yake na kujiandikisha na kwenda
kupiga kura ya kumkubali Yule ambaye Mungu amemchagua, Niliwahi kusema katika
mahubiri yangu kuwa Yule ambaye anatoka kwa Mungu atakuwa ni Yule ambaye
wanadamu hawakumtarajia wala kumfikiria.
Haya
ndio niliyojifunza katika mchakato mzima wa kupatikana kwa wagombea Urais
katika Taifa letu na huku tukiyaangalia mapenzi ya Mungu Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
Mkuu
wa wajenzi Mwenye Hekima
Rev.
Innocent Kamote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni