ALFA NA OMEGA.
“Alfa” ni herufi ya kwanza katika alfabeti
za lugha ya kiyunani kama ilivyo “A”
katika alfabeti za Kiswahili na Vivyo hivyo “Omega” ni herufi ya mwisho katika
alfabeti za kiyunani kama ilivyo “Z” katika alfabeti za Kiswahili. Yesu Kristo anaposema hivyo anamaanisha kwa
undani sana kwamba hata herufi zote za Alfabeti
zinamzungumza yeye katika lugha yoyote duniani na siyo kiyunani pekee
Yesu ni Mwanzo na mwisho wa alfabeti zote zote humtaja yeye na kumtukuza hii
pia humaanisha ya kuwa yeye ni yote katika yote.
YESU NI A.
Yesu
kristo anaitwa A yaani ni Afya yetu Zaburi 42;5.11, 43;5 Yeye ni Afya yetu na Mungu wetu tunapokuwa na
upungufu wowote katika Afya zetu yeye3 alikuja ili sisis tuwe na uzima tena
tuwe nao tele Yohana 10;10 Yeye pia ni Ahadi ya uzima 2Timotheo 1;1 mganga
yeyote akikuhaidi uzima ahadi hiyo
inaweza isiwe na uhakika lakini ahadi za Yesu ni ndiyo yaani ni hakika
2Wakoritho 1;19-20 Hesabu 23;19. Anaitwa pia Aliye juu Zaburi 46;4 wengine wako chini Yeye yu juu ya yote Yeye
pia ni Aliyeko,Aliyekuwako na Atakayekuja Ufunuo
1;8,Yeye pia ni Amani ya Bwana.
Zaburi 129;8 Yeye ni Amina Ufunuo
3;14. Anaitwa Arabuni ya roho zetu Efeso 1;14 yaani ni muhuri au uhakika.
YESU NI B.
Yesu
huitwa Bwana wa mabwana Ufunuo 19;16 na pia huitwa Bwana mkubwa Luka 8;24 Huitwa pia Baraka ya Bwana Kumbukumbu
33;23 ni Bwana wa vita Yoshua 10;14 kutoka 15;3 ni Bwana harusi wa kanisa Mathayo 9;15
YESU NI C.
Ni
chakula cha uzima Yohana 6;35 vyakula
vingine hutupa uzima wa muda tu chakula hiki hutupa uzima wa milele yeye ni Chanda cha Mungu Kutoka 8;19 huitwa chapa ya nafsi ya Mungu Waebrania 1;13
na ni chemichemi ya maji ya uzima
Yeremia 2;13 pia huitwa Chipukizi la
haki Zekaria 6;12
YESU NI D.
Yesu
Kristo ni dhabihu yetu Waefeso 5;2
alitolewa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu na kwa kupigwa kwake sisi
tunmepona Isaya 53;5 hatuna haja tena ya kutoa kafara nyingine kama mbuzi kuku,
na kuwapelekea waganga wa kienyeji
YESU NI E.
Yesu
pia huitwa Elimu ya utukufu wa Mungu angalia katika 2Koritho 4;6
hakuna aliye na Elimu yenye utukufu kama Kristo wanadamu wenye madigrii kibao wana
sehemu ndogo sana ya maarifa ukilinganisha na Kristo mwenye maarifa yote,
ikumbukwe kuwa maarifa yote yanatoka kwake.
YESU NI F.
Yesu
anapotajwa kama F katika Maandiko yeye ni Fadhili
za Mungu Zaburi 57;3 tukikosa fadhili kwa wanadamu tumwendee Yesu yeye ni
mfadhili wa ajabu atatupa mahitaji yetu yote Bure bila ya masharti.Huitwa pia Fahari ya Yakobo Zaburi 47;4 Yeye ni
fahari yetu hatupaswi kumuonea aibu yeye pia ni Faraja Yetu au faraja ya Israel Luka 2;25,Ni fimbo ya Mungu Kutoka 4;20 na ni furaha ya bwana Nehemia 8;10
YESU NI G.
Yesu
Kristo huitwa Gumegume Isaya 50;7 Gumegume
ni aina Fulani ya jiwe ambalo ni gumu sana kwa kiingereza huitwa Flint mtu
aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjikavunjika na yeyote ambaye litamwangukia
jiwe hili litamsagasaga tikitiki Mathayo 21;44 Chochote kilichokigumu magonjwa
mikosi balaa tuvilete kwa Yesu vitapondwapondwa kabisa
YESU NI H.
Yesu
Kristo anatajwa pia kuwa ni Haki ya
Mungu 2Koritho 5;21 hakuna mtu yeyote atakayehesabiwa haki mbele za Mungu
isipokuwa katika Yesu Kristo aliye haki ya Mungu Warumi 3;26,5;1 Yeye pia ni Hakimu
Zaburi 50;6 ndiye atakaye uhukumu
ulimwengu Kristo pia ni Hekima yetu kwani huitwa Hekima ya Mungu 1Koritho 1;30iwapo
tunalo hitaji la Hekima leo
YESU NI I.
Yesu
huitwa pia Immanuel Mathayo 1;23
yaani ni Mungu pamoja nasi anatajwa pia kuwa ni Ishara Yesu ni udhihirisho wa uwezo wa Mungu mahali alipo kuna
ishara Isaya 11;10
YESU NI J.
Jina
la Yesu ni Jina lipitalo majina yote Wafilipi 2;9 si hilo tu
Yesu ni Jiwe kuu la pembeni Matendo
4;11 Jiwe lililo hai 1Petro 2;24.
Uimara wetu unatokana na jiwe kuu la msingi la pembeni na lililo hai yaani Yesu
Kristo bila yeye hakuna uimara wowote
YESU NI K.
Yesu
anaitwza kichwa cha kanisa Waefeso
5;23 yaani ndiye kiongozi mkuu wa kanisa lote,huitwa pia kiongozi mkuu wa wokovu wetu Waebrania2;10. Katika Waebrania 7;17;10;21
Ni Kuhani mkuu maana yake ndiye
mpatanishi wetu mkuu 1Timotheo 2;5 yeye pia huitwa kweli Yohana 14;6 pia ni Kimbilio letu
YESU NI L.
Yesu
Kristo ni Lulu moja ya thamani kubwa
Mathayo 13;46 tukimpata katika maisha yetu tumepata lulu moja ya thamani kubwa
yeye ndiye wa kumshika na sio dini Ufunuo 3;11 Dini au dhehebu Fulani sio lulu
moja ya thamani
YESU NI M.
Ni
Mfalme wa Wafalme Ufunuo 19;16
yapasa tumuogope na kumtii na kumuheshimu Ni Mfinyanzi wetu Isaya 64;8,Yeremia 18;1-6. Huitwa Mchungaji mkuu wa kondoo Waebrania
13;20 ni Mchungaji mwema Yohana
10;14. Ni Mlango wa kondoo Yohana
10;7 ni Moto ulao Waebrania 12;29,
ni Mungu mkuu Tito 2;13 ni Mwana wa Mungu Yohana 9;35-37 ni Mwana wa Adamu Mathayo 26;64 Ni Mwokozi Tito 1;4,Mwalimu Yohana 3;2,na Muhukumu
wetu siku ya mwisho Yohana 5;22
YESU NI N.
Yeye
ndiye Nabii yule Yohana 6;14 huitwa
pia Njia pekee ya kuingia mbinguni
Yohana 14;6 ndiye Nyota ya kung’aa
asubuhi Ufunuo 22;16 au Nuru ya
ulimwengu Yohana 8;14 akiwa ndani yetu hatuta kwenda gizani kamwe yeye ni Neno Yohana 1;1
YESO NI O.
Yeye
hutajwa kama Ondoleo la dhambi zetu
Matendo 10;43 tukimuamini hutupa ondoleo la dhambi
YESU NI P.
Pendo la Mungu Warumi 5;5 ni chimbuko la
upendo la kweli
YESU NI R.
Ni Rafiki Luka 12;4.pia ni mwalimu mkuu
sana anayeheshimika Rabi au Rabon Yohana 20;16
YESU NI S.
Yeshu
huitwa Shahidi aliye mwaminifu
Ufunuo 1;5 ni Simba wa kabila la Yuda
Ufunuo 5;5
YESU NI T.
Tabibu mkuu Mathayo 9;11-12,Yeye ni Tumaini letu kuu Zaburi 71;5 ni Taraja
letu Zaburi 71;5 ni Tegemeo letu
Yeremia 17;5-8.
YESU NI U.
Yesu
Kristo ni uzima wa milele Yohana
14;6 na ukombozi wetu 1Timotheo 2;6
na ndiye upanga wa utukufu Kumbukumbu 33;29 upanga huu
unaweza kushughulikia na yeyote anaye kutesa
YESU NI V.
Yesu
ni Vazi jipya Luka 5;36 Torati ni
vazi kuu kuu lakini Kristo ni vazi jipya
YESU NI W.
Ni
Wokovu wetu Zaburi 27;1 tukiwa na
Yesu hatupaswi kumuogopa mtu awaye yote Hesabu 23;23 hata wachawi hatupaswi
kuwaogopa kwani Yesu ni wokovu wetu
YESU NI Y.
Huitwa
Yesu Mathayo 1;21 yeye ndiye
aokoanye watu wake na dhambi zao bila Yesu hakuna wokovu.Yeye ni Yeye
yule jana leo na hata milele,ni Yeye ajaye wala hatakawia Ebrania 10;37.
YESU NI Z.
Yesu
ndiye Zeri ya Gileadi Yeremia 46;11 nyakati za Biblia kulikuwa na dawa
iliyoitwa zeri ambayo ilikuwa ikipatikana huko Gileadi dawa zote zikishindwa
ndipo ilibidi itumike zeri ya Gileadi ilikuwa ni dawa isiyoshindwa ni zaidi ya
muarobaini Zeri ni Yesu Kristo dawa isiyoshindwa kila kitu kinaposhindikana
ndipo tumuitie Yesu yeye hashindwi kitu.
Na mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni