UKIRI
WA IMANI YA MITUME.
a. Maendeleo
ya kuweko kwa Ukiri wa Imani
Ukiri wa zamani
zaidi wa imani katika kanisa la mapema uliitwa imani ya mitume kwa ujumla
haukuandikwa na mitume lakini ulikuwa ni
mkusanyiko wa kiini cha mafundisho yao na ulikusanywa kwa mara ya kwanza kati
ya mwaka 140 na ulikuwa ukitumika kama Katekisimo (Catechism) kwa kila mtu mara anapokuwa anakaribia kubatizwa kama
ukiri wao wa imani
§
Kumuamini Mungu lilikuwa swala la asili kwa
Wayahudi na Wakristo kwa msingi huo kumkiri Kristo katika ukiri wa imani kulitofautisha kati ya Ukristo na Uyahudi na
ubatizo ulikuwa ukifanyika kwa jina la Yesu kama ilivyokuwa katika kitabu cha
Matendo ya Mitume
§
Hata kufikia mwaka 200 A.D. wale waliokuwa
wanataka kubatizwa walikuwa wakiulizwa swali Unaamini? Baaday ilibadilishwa na
hata ilipofikia Karne ya 12th C ilifikia hatua ya juu na kukubalika
kwamba anayebatizwa ni muhimu kukiri ukiri wa imani uliosema hivi
“Namwamini Mungu Baba mwenyezi Muumba wa mbingu na
Nchi na Yesu Kristo mwana wake wa pekee Bwana wetu aliyechukuliwa mimba kwa
uweza wa Roho Mtakatifu akazaliwa na Bikira Mariam, aliyeteswa zamani za
Pontious Pilato akasulibiwa, akafa akazikwa siku ya tatu akafufuka akapaa
mbinguni ameketi mkiono wa kuume wa Mungu baba, toka huko atakuja tena kwa
utukufu kuwahukumu watu walio hai na wafu na ufalme wake ahauna mwisho,
Namwamini Roho MtakatifuKanisa takatifu la Kikristo,Ushirika wa watakatifu
Msamaha wa dhambi,ufufuo wa mwili na uzima wa ulimwengu ujao Amen.”
HISTORIA YA BISHANO KUHUSU UTATU
WA MUNGU.
Kuenea kwa injili ulimwenguni
hususani kwa mataifa kunaifanya injili kuwafikia Wayunani nao wanakuwa sehemu
ya kanisa wasomo, watu wenye uwezo wa kufikiri, wanasheria na kadhalika sasa
wanaingia kanisani na kuchanganua mambo.
Justin Martyr 100-165.
-
Alikuwa mwanafalsafa kutoka Samaria ingawa
wazazi wake waliishi Rumi Kama mwalimu aliuona Ukristo kama Una kitu cha ziada
kuliko falsafa na hivyo aliamini na kuokoka
-
Alifundisha kuwa Yesu ni mwana wa Mungu
aliyeumbwa na Mungu kabla ya uumbaji, kwa msingi huo kabla ya hapo Mungu
alikuwa peke yake ndani ya Mungu kulikuwa na Neno Logos, kwa hiyo Yesu ni mdogo
kwa Mungu na anapaswa kumtegemea Mungu, kwa sababu ya msimamo huo Justin
aliuawa mwaka 165 wakati wa utawala wa Marcus Aurelius huyu alikuwa mwana
apolojetic wa kwanza.
Turtulian 160-220
-
Alikuwa mtetezi wa imani kutoka Misri.
-
Ibu la tatizo alilokuwa nalo Justin lilitatuliwa
na mwanatheolojia huyu alikuwa mtu kutoka Carthage na alikuwa msomi alkuwa
mwana Montanists alikazia utakatifu na kukemea udunia ndani ya Kanisa katiliki
-
-
Alifundisha kuwa Baba na Mwana wanashiriki uungu
mmoja na ni nafsi tofauti zikiwa na kazi maalumu hata hivyo alitoa nafasi ya
Pili kwa mwana kuwa sio wa milele
-
Alisema Baba na Mwana na Roho Mtakatifu ni Mungu
mmoja na kila mmoja ni nafsi na huu ndio
ukawa mwanzo wa msingi wa fundisho hili la utatu kuja kukubalika wakati wa
mkutano wa Nicea.
MKUTANO
MKUU WA NICEA NA TAMKO LA IMANI (IMANI YA NICEA).
-
Nicea ni moja ya miji katika inchi za asia ndogo
-
Mnamo mwanzoni mwa Karne ya Nne moja ya fundisho
muhimu sana liliinuka na kuleta Utata miongoni mwa Kanisa, mijadala iliinuka
kupitia wanatheolojia wakubwa na wenye
nguvu, pia kukiwa na utetezi wenye nguvu na mawazo mbalimbali yaliyopelekea kuitishwa kwa mkutano wa Nicea
a. Arius
wa Alexandria 256-336
Alikuwa ni
kiongozi mkubwa wa imani ya Kikristo na mwanzilishi wa imani ya Arianism moja
ya imani potofi iliyokuwa inapinga uungu wa Yesu Kristo, Arius alikuwa mwana
theolojia aliyesomea huko Antiokia (Antakya ya Leo huko Uturuki) alijifunza
theolojia chini ya Msomi aliyejulikana sana aliyeitwa Lucian na huenda ndiko
alikotoka na fundisho hilo alijulikana kwa kusisitiza maswala ya kihistoria na
njia zanye kujenga na kuzalisha za kidini pamoja na maswala ya utafiti kuhusu
umoja wa Mungu na Utatu mtakatifu shule yake ilijulikana pia kama shule
iliyokuwa ikimuona Kristo kama yuko
chini ya Mungu Baba,.
Arius alizaliwa
Afrika na alikuwa mwangalizi wa Kanisa la Alexandria nchini Misri, alikataa
kuweko kwa ushirika wa milele kati ya Yesu na Mungu usemi wake maarufu unasema
“kuna wakati ambapo Yesu Hakuweko”na kuwa Mungu alimpitisha Yesu kuwa mwana
wake baada ya ufufuo wake na kumpa baadhi ya majukumu ya uungu alisema Yesu
alikuwa na mwili wa kibinadamu lakini hakuwa na Nafsi ya Kibinadamu na hivyo
hakuwa Mungu wala hakuwa mwanadamu wa kawaida Yuko mahali Fulani hapo katikati.
b. Athanasius
Mtakatifu
Athanasius aliishi kati ya mwaka wa 293-373 B.K. Ni mwanatheolojia mkubwa wa
Kikristo na Doctor wa Kanisa Pia alikuwa Askofu ni miongoni mwa watu
walioshindana na kusababisha kuundwa kwa Orthodox katika karne ya 4
akishindania imani dhidi ya Arianism alisimikwa kuwa shemasi akiwa kijana akitumika kama Katibu wa askofu wa Alexandria
na ndipo alipopata nafasi muhimu ya kitheolojia ya kuongoza mapambano dhidi ya
fundisho la Arius ambalo lilijadiliwa katika mkutano wa Nicea mwaka wa 325 na
kwa ujumla alikuwa na nguvu ya ziada ya kupambana na imani hiyo na aliweza
kueleza sawia kuwa mwana wa Mungu Yesu Kristo ni sawa na Mungu Baba ingawa Arius aliendelea kudai kuwa sio sawa
kwani Yesu ni kiumbe tu aliye mkamilifu kuliko viumbe wengine na kuwa alitumiwa
na Mungu katika uumbaji na kazi nyingine za uumbaji.
Mijadala hii
ilipelekea kuzuka kwa mjadala mkubwa kuhusu Utatu wa Mungu mjadala huu ulikuwa
umekita miguu yake katka kutaka kujua kuhusu Uungu wa Yesu kwamba je Yesu I
Mungu? Na kuna uhusiano gani kati ya Roho na Mwili wa Yesu Je Mungu ni Watatu
au mmoja? Na wana uhusiano wa aina gani?
KUITISHWA
KWA MKUTANO MKUU WA KWANZA WA NICEA MWAKA 325
Mkutano huu uliitishwa wakati wa
Utawala wa Constantine ambaye alifuatilia kwa ukaribu sana mjadala mzima wa
maswala ya utatu na uungu wa Yesu ingawa Lengo lake la kuitisha mkutano huu
lilikuwa la Kisiasa zaidi yaani katika kuhakikisha kuwa Himaya yake inakuwa na
amani aliitisha mkutano huo 19th June 325 mpaka Augosti 25th
ni mkutano wa siku kama 67 maaskofu wapatao 300 walihudhuria wengi wao wakiwa
ni kutoka Msahariki.
Constantine the Great
Mfalme Constantine mkuu alikuwa Mtawala wa Kwanza wa Kirumi aliyeokoka
wakati wa utawala wake, mwanzoni aliwatesa wakristo lakiini baadaye akawa
mkristo, alipokuwa Mkristo aliruhusu uhuru wa kuabudu alitoa eneo kubwa sana
Estate na zawadi nyinginezo kwa Kanisa alistawisha mji mkuu jimbo la Mashariki
na kuliita kwa jina lake Constantinopple ambao kwa sasa unaitwa Instanbul huko
Uturuki, aliitisha mkutano mkuu wa Nicea mwaka 325
Mjadala mkuu katika mkutano hu ulikuwa ni kuhusu Fundisho la Arius kuhusu
Asili ya Kristo kwamba je ni mwana wa Mungu na kuwa si sawa na Mungu na kuwa
aliumbwa na kuwa yuko chini ya Mungu Baba
Neno kuu lilkuwa ni neno la kilatini Homo-Ousios yaani wa wa aina moja
Jambo ambalo Arius alikuwa akilipinga
Hitimisho la Mkutano huo lilikubaliana kuwa fundisho la Arius ni la
Uzushi na wazo la kuwa kuna wakati mwana hakuwako lilikataliwa na pia swala la
kuwa aliumbwa kwanza kabla ya viumbe vingine lilikataliwa na Tamko la Nikea
lilikuwa hivi
“Tunamwamini Mungu Baba Mwenyezi Muumba wa kila kinachoonekana na kisichoonekana na Bwana mmoja Yesu risto Mungu kweli kutoka
katika Mungu kweli Mwana wa azali asiyeumbwa mwenye uungu mmoja na Baba ambaye kwa Yeye vitu vyote viliumbwa vya
mbinguni na vya Duniani”
Na hii ndio ikawa imani
liyonyooka Orthodox, swala la Utatu lilikubalika kwa maneno kama hayo kuwa wote
ni ungu katika umoja, Mkutano wa Nicea ulikubaliana kutoa tamko moja ambalo
baadaye lilithibitisha katika mkutano wa Constantonople mwaka 381 na hivyo
imani ya Arianism ikawa imefikia mwisho katika utawala wa kirumi kwa sababu ya
imani iliyonyooka Orthodox.
MASWALA BAADA YA MKUTANO WA NICEA
-
Baada ya mkutano wa Nicea Ukristo ulifanywa kuwa
dini ya kitaifa kwa utawala wa Rumi
wakati huu kuliinuka maswala kadhaa yaliyopelekea kanisa kuwa dhaifu na kulikuweko na mafundisho
kadhaa ambayo yaliingizwa na wanadamu zikiwemo baadhi ya Sacrament
Saint
Augustine wa Hippo Afrika ya Kaskazini (354-430).
Mtakatifu Augustine, alizaliwa huko Souk-Ahras, Algeria, mwaka
354 A.D. Ndiye aliyeleta mpangilio wa
kifaklsafa wa theolojia ya Kikrisro (a systematic method of philosophy to
Christian theology). AugustineAlikuwa mwalimu huko rhetoric mji wa zamani
katika miji ya in Carthage, Rome, na Milan Kabla ya kubatizwa na kuwa Mkristo
mwaka 387. Alijadili Maarifa kuhusu kweli na kuhusu kuweko kwa Mungu kulimvuta
Karibu na Mungu na Biblia na kutoka kwenye Falsafa za kizamani za kiyunani
alikuwa mwanasheria wa Roman Catholicism, Augustine aliendeleza mafundisho
mengi alipokuwa akijaribu kutatua migogoro mingi ya kitheolojia. Ikiwemo imani
za Donatism na Pelagianism, imani kubwa mbili za kizushi zilizokuwa zikiendelea
wakati ule.
Saint Augustine
-
Ni mmoja wa Mababa wakubwa wa kilatini na Daktari wa
Kimagharibi wa Kanisa alikuwa Askofu wa Hippo
-
Alizaliwa November 13th mwaka 354 huko Tagaste,
Numidia kwa sasa (Souk-Ahras Algeria) Baba yake Paticius alifariki mwaka 371
alikuwa mpagani lakini baadaye aliokoka lakini mama yake Monica alikuwa mkristo
aliyejitoa sana na aliyemsaidia mwanae
na hatimaye kukubalika katika kanisa la Roman Catholic, alisoma kati ya umri wa
miaka 15-30 huko Madura na Cathage, baadaye aliishi na mwanamke ambaye jina lake
halikujulikana kati ya mwaka 372 na alimzalia mwana wa kiume aliyempa jina Adeodatus
jina la kilatini lenye maana ya Zawadi ya Mungu
-
Aliishi maisha rahisi naya kimonaki maandishi yake
yaliliathiri kanisa hata katika nyakati
za leo
-
Alifundisha kuwa dhambi inatokana na asili ya uovu
uliorithiwa kutoka kwa Adamu kwa neema ya Mungu
asili ya dhambi inaweza kuondolewa kwa wale walioandikiwa kuurithi uzima
wa milele lakini neema hiyo si kwa wale walioandikiwa kutokuurithi uzima wa
milele
-
Fundisho hilo ndio uliokuja kuwa msingi wa mafundisho ya
John Calvin, Presybyterian na Baptist katika miaka ya baadaye.
Pelagius aliishi kati ya Karne ya nne na Tano (360? - 420?)
-
Alikuwa mwanatheolojia wa Kiingereza (Romano-British) na
mtawa aliyekuja Rumi kati ya mwaka 410, Yeye hakukubaliana na fundisho la
Augustino kwa kudai kuwa kila mwanadamu ana utashi Free will na kwa utashi wake
aweza kuamua kuokoka au kukataa alikataa juu ya dhambi ya asili kutoka kwa
Adamu kuwa ndiyo inayotuamulia alisisitiza kuwa ni utashi ndio unaotuamulia
kufanya mema au kufanya uovu
-
Alisisitiza kuwa Yesu alitusaidia kwa kuonyesha mfano namna
ya kuupata wokovu lakini matendo ya mwanadamu
ni ya lazima
-
Fundisho la Pelegius lilihukumiwa katika mkutano wa Cathage
mwaka 415 na kutangazwa kuwa ni Uzushi na Pope na Mtawala wa Rumi na fundisho la Augustino lilikubalika kuwa
Orthodox mpaka wakati wa Arminius wa Uholanza na John Wesley wa Uingereza.
MKUTANO WA EFESO AD – 431
-
Bishano lingine lilizuka kati ya watawa wa ki Nestorian, Mababa wa mashariki Constantinople
na ki cyxill Mababa wa Alexandria
kuhusu asili mbili za Kristo
Uungu wake na Ubinadamu wake
-
Nestorius alikazia kupita kawaida ubinadamu wa Yersu na
kukataa mafundisho kuwa Mariam ni “theotokos”neno la kiyunani ambalo maana
yake ni Mama wa Mungu yeye aliweka wazi kuwa Mama wa Yesu maana yake ni Mama wa
mwanadamu Kristo Yesu tu
-
Mkutano wa Efeso ulihukumu fundisho hilo la waanestirism na
kumpeleka utumwani Misri jangwani mwaka wa 435.
MKUTANO WA CHALCDON – 451 A.D.
-
Bishano la wa Alexandria na wa Constantinople halikuishia
pale kwani mababa wa ki konstantinople waliendelea kusisitiza kuwa Kristo ana
asili moja tu baada ya kufufuka na asili hiyo ni ya kiungu tu
-
Huu ulikuwa ni moja ya mikutano ya kanisa ya kihistoria
ambapo kanisa liliketi kushughulikia migogoro unaohusu kuilewa asili ya kweli
ya Yesu, Mkutano huu ulifanyika kati ya October 08, 451 - November 01, 451 Fundisho lilianzishwa na
Bynzantine mtawa wa ki Eutiko walioamini katika Monophysitism ambayo ilikuwa
ikisisitiza kuwa asili ya Kristo ni Mungu na sio mwanadamu, fundisho hilo
lilitangazwa kuwa ni Uzushi uamuzi ulipelekea kanisa la Kimisri kugawanyika
miongoni mwa waliokuwa wakiamini hivyo.
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni