NIKAALIKWA
KAMA MTOTO WA WAZIRI
Mimi ni kijana wa umri wa miaka
34. Malezi na makuzi yangu yalikuwa ni ya wale wazazi ambao kwa siku hizi
wangeitwa machekibobu, hawa ni wazazi ambao wanataka kujionyesha kwa watu wengine kwamba wao ni watu wenye fedha ,waliotoka kwenye
familia bora, waliosoma sana ingawa sio
kweli kwa hiyo name nilikuwa mtu wa aina hiyo mpaka niulipofunzwa na dunia.
Kwa ujumla ni kama nilifundishwa
kujikataa kwamba siyo mimi na nilimudu sana kujikataa kwani katika kukua kwangu
name nimekuwa mtu wa kujikweza mwaka 2000 ni kiwa nimemaliza masomo katika chuo
cha biashara nilipata kibarua kwenye ofisi binafsi katika eneo la viwanda
vingunguti nilianza kazi hapo nikiwa kama karani wa kawaida tu wa kutumwa
shughuli za hapa na pale kujaza fomu za hesabu za fedha na mengine ya aina hiyo
Wakati nikiwapo hapo kazini
nilikutana na msichana mmoja ambaye alikuwa akifanya kazi kampuni ya jirani,
nilikutana na msichana huytu wakati wa chakula cha mchana Lunch hapo eneo la
viwanda. Kwa keli nilimpenda sana ghafla, yaani jicho la kwanza. Lakini Mungu
si Athumani naye alionekana kunipenda ghafla pia, tulijikuta tukiwa marafiki
baada ya mimi kumuanza ingawa kiuoga uoga kwani alikuwa mzuri sana na pia
alikuwa anamiliki usafiri aina ya Rav4 ya milango mitatu, nilipochokoza
alikubali kirahisi tofauti na nilivyotarajia
Rav4 ya Milango mitatu
Kama kawaida yangu katika
kujitambulisha mimi nilijitambulisha kwa
kujilambisha ujiko wa ajabu sana, mimi ni mwenyeji wa Tanga na baba yangu anajuana na mtu mmoja mkubwa
serikalini ambaye hadi sasa ni waziri. Badala ya kusema ukweli kuhusu baba
yangu ambaye kwa maisha ya kichekibobu kama yangu alikuwa amesha chalala sana
nilimtaja mkubwa huyo
Yule binti aliniamini na huko
nyumbani alitangaza bila shaka kwamba amepata mtu ampendaye ambaye baba yake ni
mtu Fulani, siku hiyo binti alinialika niende nyumbani kwao kwaajili ya chakula
cha mchana ilikuwa ni jumapili, nilijitahidi sana hadi nikamudu kukodi gari ya
rafiki yangu kwa shilingi 40,000 ili niendenalo mwenyewe kule wajue kwamba nina
gari unajua kitu gani kilitokea?
Nilipofika nyumbani kwao Yule
binti nilimkuta mama yake, baba yake alikuwa amefariki zamani, lakini pia
nilimkuta mtu mwengine, Hebu otea alikuwa nani? Alikuwa ni baba yangu,
Nilibabaika sana na kujiuliza maswali
mengi ambayo hayakuwa na majibu nilipigwa na butwaa kwa muda na baba baye pia,
nilimsalimia mama wa binti yuile na baadaye kumsalimia baba na kumuuliza uko
huku? Baba alisema nashangaa nawe unaijua familia hii Mama Lewisi tulikuwa naye
kazini zamani. Siku nyingi sijamtembelea leo ndiyo nimeamua kuja kumwona….”
Yuel mama mkwe wangu mtarajiwa aliuliza kwani mnajuana? Baba alisema huyu ni
mwanangu wa kwanza” Halafu palizuka ukimya Yule mama kwaajili ya kuua soo
alinikaribisha lakini ghafla Yule binti alikuwa amebadilika hakuwa na furaha
tena.
Tulikula, lakini katika hali ya
undavaundava tu, tulipomaliza kula
sikutaka kukaa zaidi kwani nilijua kuwa binti Yule na mama yake walikuwa
wakinisanifu sana , du kutoka kuwa mtoto wa waziri hadi kuwa mtoto wa mzee
aliyechezea maisha siku za nyuma, mbaya zaidi ni kuwa baba alikuwa amefika pale
kwa nia ya kuomba msaada, Niliaga
nikimwacha baba akiendelea kupiga mabomu yake. Nilikuwa na uhakika kuwa baba
aliambiwa ishu zangu zote, kwani jioni alinitembelea kwangu na kuniambia kwamba
nimejisanifu sana kwa kujifanya mtoto wa waziri Unataka niendelee kukusimulia?
Unataka kujua kuwa niliendelea na urafiki na Yule demu au La au nilitoa pua
yangu kwa mama mkwe mtarajiwa? Hivi kichwa chako kiko sawasawa?
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni