Imepita miaka mine sasa tangu
nilipopatwa na mkasa huu , wakati huo nilikuwa mkoani ambako nilikwenda
kusalimia ndugu na jamaa kufuatia kupata vijisenti kidogo kwani nilikuwa
sijakwenda huko kwa mia karibu mitano, kwa sisi wengine ambao maisha yetu ni ya
kubahatisha kwa kiasi Fulani inabidi
ujiwekee vijiakiba vya kubahatisha kwa muda mrefu kabla hujapata kiasi ambacho kwa hicho
unaweza kwenda kusalimia nacho kwenu bila kuadhirika, kuna wakati inaweza
kukulazimu kukomba hata nauli ya kurudia
huko sasa ndo kuadhirika kwenyewe.
wasema kweli huitwa wapondaji/wanafiki
Ninaishi Dar es Salaam kwa muda
wa miaka 16 hivi sasa na shughuli zangu ni kubangaiza. Lakini kijijini kwetu
wote wanajua kuwa kwamba mimi ni mfanya biashara maarufu huku Dar.Kwa hiyo
ninapoenda najitahidi kuwaonyesha wana
kijiji kuwa mambo yangu si haba , ingawa kwenye familia yetu wanajua kuwa mimi
nimechoka vilivyo, siku hyo nikiwa hapo kijijini nimewanunulia jamaa bia huku nikiwa natamba sana mara akatokea jamaa mmoja ‘ Du umekuja lini
mshikaji mimi niko hapa tangu wiki jana alisema’ jamaa huyu huwa tunabangaiza
wote kule mjini lakini sikuwa na jua kuwa ni mwana kijiji wa pale ingawa najua
kuwa ni mwenyeji wa wilaya yetu, siku hizi mimi ni mwana kijiji mama aliolewa
hapa na mzee, alimtaja moja ya wazee hao, Sasa mzee lete stori maana ngalambe
zetu mjini tunazijua wenyewe alianza kusema na taratibu nilihisi hatari ikija
halafu aliendelea , Washikaji huyu jamaa yangu kabisa wiki iliyopita tu tulikuwa tuna kabiliana na mwenye nyumba ,Jamaa
akaanza kuponda hasa, kwani tumepewa notisi geto yetu si unajua maisha ya bongo
yalivyo mtu sita chumba kimoja mambo
magumu washikaji msije mjini kabisa asiwadanganye mtu…’ Kila nikifanya bidii ya
kumzuia asizungumzie naona mwenzangu anazidi kuchanja mbuga na kumwaga siri za
maisha yetu kule Dar , mwsho wale wapambe wangu wakaanza kuhoji kuhusu
anachosema Yule jamaa, jamaa aliendelea
kusema ukweli kuhusu maisha yetu kule mjini, nilipoona vile na kwa
sababu namjua ni mgomvi niuliona bora niondoke badala ya kubishana naye kwa
kweli kesho yake nikakuta taarifa
zimeenea kijiji kizima kwamba huko Dar niliko ninabangaiza tu ilibidi niondoke
siku hiyohiyo na kwenda kulala kijiji kingine na kusafiri siku iliyofuata kurudi Dar Lakini nashukuru jamaa alinisaidia
kwani baada ya pale niliamua kuwa
mkweli, leo hii hata hivyo maisha yangu yamebadilika na yamekuwa mazuri kiasi
cha kutosha lakini siku zote sasa nimejifunza kuwa mimi tu na sitaki
kujipandisha zaidi ya nilivyo katika hali halisia
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni