Mstari wa Msingi Kutoka 7:4-5
“Lakini Farao hatawasikiza ninyi, nami nitaweka mkono wangu juu ya Misri, na
kuyatoa majeshi yangu, watu wangu, hao wana wa Israeli, watoke nchi ya Misri
kwa hukumu zilizo kuu. 5. Na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, hapo
nitakapounyosha mkono wangu juu ya Misri na kuwatoa wana wa Israeli watoke kati
yao”.
Hii ni lugha nyingine ya Kibiblia
“NITAWEKA MKONO WANGU JUU YA MISRI” Maana yake ni nini ? Mungu ataihukumu Misri
kwa sababu ya kiburi cha maendeleo yao ataleta anguko kubwa kwa vile Pharao
amekuwa jeuri ana moyo mgumu hataki kuwaachia Israel Mungu napoihukumu Misri
ana hukumu nini ni muhimu kulichambua hili!
Hali ya kiroho ya Taifa la Misri
ilikuwa mbaya sana ingawa walikuwa na maendeleo makubwa sana, Mungu atalihukumu
taifa lolote na kusababisha anguko kwa Dola hata kama ina nguvu kiasi gani endapo
tu itamuacha Mungu, Historia inaonyesha sababu nyingine za kuanguka kwa dola la
Misri
· Mpaka miaka ya 1550 – 1200 hivi Utawala wa Misri
ulikuwa umeenea mashariki ya kati na mbali mpaka mto Frat
·
Hata hivyo kwa haraka sana utawala huu ulianza
kuanguka na kupoteza uwezo baadaye ukifuatiwa na tawala nyingine kama Ashuru
Syria mwaka 750 KK
·
Kisha Babeli 606 BC
·
Kisha Uamedi/uajemi au Iraq na Iran 530 BC
·
Kisha uyunani au Ugiriki 332 BC
·
Kisha Rumi mwaka wa 30 BC
Dola zote zilizofuata baada ya
misri hazikudumu kwa miaka mingi kama Misri, kwa mujibu wa kihistoria kuibuka
kwa Dola hizo nyingine ndio ulikuwa mchango mkubwa wa kuanguka kwa Misri,
ushahidi wa kibiblia unaonyesha kuwa taifa linalomuacha Mungu Mungu huweka
mkono wake juu ya taifa hilo kwa hukumu Mungu ndiye aliyeihukumu Misri na
mataifa mengineyo!
Ni lazima kila taifa litambue
kuwa Mungu ndiye anayetawala na kuwa ndiye anayeweka wafalme na kuondoa na tena
ndiye anayeyainua mataifa kwa makusudi yake na kuyasimamisha kwa kusudi lake na
kuyaangusha kwa kusudi lake na utukufu wake
Warumi 9:17. Biblia inasema hivi
“Kwa maana maandiko yasema juu ya Farao ya kwamba nilikusimamisha kwa kusudi
hili, ili nionyeshe nguvu zangu kwako jina langu likatangazwe katika inchi
yote” unaona kumbe kusimama kwa Misri ilikuwa ni kusudi la Mungu ili Mungu
atangaze nJina lake Duniani
Ni vema neno la Mungu likawa wazi
kwa kila kiongozi na kila taifa kuwa mtu akiwa na madaraka au akiinuliwa
akubali na kutambua kuwa kuna kusudi la Mungu nyuma yake, hivyo kila Mtu na
kila taifa linapaswa kumuheshimu Mungu na kumpa Mungu kipaumbele, na kuwa na
utambuzi na kunyenyekea na kuacha majivuno Lazima kila mtawala ajue yuko kwa
kusudi la Mungu, na kuwa kama hatalitimiza Mungu ataweka Mkono wake na
kuhukumu!
Biblia inasema Hivi Daniel 4:17 “Hukumu
hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi
walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu,
naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge”. Unaweza kuona?
Mungu anatumia wanyonge na
kuwainua Mungu hapendezwi na kiburi na majivuno alimshughulikia Mfalme
Nebukadreza kwa kusudi la kumyemyekesha ili ajue kuwa aliye Juu yaaani Mungu
ndiye anayetawala, Mwisho mfalme wa
Babeli alisema Hivi katika Daniel 4:37 “….Basi mimi Nebukadreza namhimidi
mfalme wa Mbinguni namtukuza na kumuheshimu maana matendo yake yote ni kweli na
njia zake ni za adili na wale waendao kwa kutakabari (kiburi) yeye aweza
kuwadhili! Unaoana
Biblia inaonyesha kuwa kiongozi
jeuri asiyemnyenyekea Mungu, Mungu anauwezo wa kumuadhibu ni kwa sababu hizi
Mungu aliweka mkono wake wa Hukumu dhidi ya Misri kwa sababu ya viongozi wake
ambao walijichukulia heshima ya Mungu na kusahau kuwa wao ni binadamu tu Farao
na majeshi yake yalifutiliwa mbali na Misri ilianguka, Historia kamwe haiwezi
kuonyesha sababu hizi za kiroho, Ushahidi uliowazo kuwa Farao alikuwa na kiburi
ni jinsi mara nyingi alikaidi agizo la Mungu la kuwaachia Israel waende zao
mfalme huyu aliwahi kumjibu Musa kuwa Huyo Bwana ni nani? Kutoka 5:1-2 Biblia
inasema hivi …..Bwana ni nani hata niisikilize sauti yake na kuwapa Israel
ruhusa waende zao? Mimi simjui Bwana wala sitawapa Israel Ruhusa waende zao! Ni
maneno ya Kiburi dhidi ya Mungu aliye hai hii ni kwasababu wamisri walimtukuza
sana Farao na kumuabudu wakiamini ni mwana wa Mungu jua aliyeitwa Re akiwa
katika mwili wa kibinadamu, Hivyo, kuwatumikisha Israel ilikuwa ni kashfa kwa
Mungu wa Israel kwa vile farao anajilindanisha naye huku akiwa hatambui uwepo
wa Mungu aliye hai ni kwa sababu hii Mungu alisema Nitaweka Mkono wangu juu ya
Misri yaani nitaihukumu Misri, Kitu chochote kile kinachomdhalilisha mtu wa
Mungu na kumtesa ni wazi kuwa kimejitukuza dhidi ya Mungu aliye hai Bwana na
aweke mkono wake juu ya kila kitu kinachokusumbua na kukutweza na kukuonea na
kukutawala huku kikiwa hakitaki kukuachia natangaza kuwa wakati umefika lazima
vilivyojiinua vishushwe Bwana anaweka mkono wake juu ya usumbufu wote na
kuhukumu kwaajili ya utukufu wa Jina lake Kutoka 14:3,17-18
Ujumbe na Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev Innocent Kamote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni