UJUMBE: KAMA SI BWANA ISRAEL NA ASEME SASA
Muhubiri;
Mchungaji Innocent kamote
Zaburi ya 124;1-8.
Zaburi ni mojawapo ya vitabui vya kipekee
sana katika Biblia ni moja ya kitabu maarufu kilichoko katika kundi la vitabu
viitwavyo vitabu vya mashairi ya kiebrania na ndicho kitabu kirefu kuliko vyote
katika Biblia kwani kina sura karibu 150 zilizogawanywa katika vitabu vitano,
inaaminika kuwa ndicho kitabu kinachosomwa zaidi na kuhubiriwa zaidi kuliko
vyote katika agano la kale, aidha waimbaji wengi sana na watunzi wa nyimbo hutoa nyimbo zao katika
zaburi, sababu moja kuu inayovutia wengi katika zaburi ni kwa sababu zinagusa
hisia za watu
·
Zaburi zilia ndikwa
kwa sababu mbalimbali za kihisia kam avile watu walipokuwa na furaha
,huzuni,nk, Mfano mwandishi wa wimbo nionapo amani kamqa shwari kwa hiyo kuna
sababu nyingi zilizopelekea zaburi kuandikwa kati ya hizo ni pamoja na
1. Zaburi kwa ajili ya hekima na maadili mfano zaburi ya 1
2. Zaburi kwa ajili ya shukurani nyingu huanza kwa kusema
mshukuruni Bwana
3. Zaburi za kujitia moyo mfano zaburi ya 27
4. Zaburi za kifalme au za kimasihi
5. Zaburi za kihistoria au za kukumbuka matukio maalumu
6. Zaburi za kusifu au Halel Psalms ambazo huanza na neno
Haleluya
7. Zaburi za maombolezo
8. Zaburi za dua na maombi pamoja na kulaani Mfano Zaburi ya
35 : 1-8
Zaburi
ya 124 ni zaburi ya kihistoria ni ya kukumbuka matukio na ni zaburi inayokisiwa
kuwa ya Daudi au mtu wa karibu na Daudi Kwani Zaburi zimeandikwa na watu wengi
akiwemo Musa, Sulemani wana wa kora n.k na Daudi anazo zaburi kama 73 hivi na
nyingine ni zaburi yatima Zaburi hii ya
124 inakisiwa ndiyo iliyonukuliwa na Paulo katika Warumi 8;31 “Mungu akiwa
upande wetu ni nani atakayekuwa juu yetu?” Inaonekana mwandishi wa zaburi hii
alikuwa akitafakari kwa niaba yake na kwaniaba ya Taifa la Israel jinsi hasira za adui shetani zilivyokuwa juu
yao jinsi alivyokusudia kuiangamiza Israel kwa moto, maji, mitego na mbinu
mablimbali, jinsi alivyokusudia kutumaliza lakini hatimaye anaanza na hitimisho
kuwa kama Bwana asingelikuwa pamoja nasi
Tungeliangamia huku Israel wakiwa mashahidi ya wema wa Bwana na utetezi wa
Mungu Hivyo kama si bwana Israel na aseme sas!
Israel
ni taifa linalotetewa na Mungu hata leo ni mara kadhaa wamepitia misukosuko ambayo isingelikuwa rahisi
kuiepuka kwa hali ya kawaida, wakristo wengi wasio na ufahamu hufikiri kuwa
kanisa ni mbadala wa Israel, Warumi
11:1-2 Israel ni kijiti kinachowaka moto lakini hakiteketei!
1948 – wayahudi
walipopata uhuru wakiwa kiasi cha wayahudi laki sita hivi kuhesabu wanawake na
watoto Waarabu wakiwa miliono 80 walikusudia kuwa futilia mbali lakini kwa
uweza wa ajabu Israel Iliwapiga vibaya wqaarabu na kufanikiwa kupanua mipaka
yao kutoka Tell Avivi Jaffa mpaja ukanda wa gaza, milima ya Golan, na kuuteka
mji wa Yerusalem
1950 – Wafaransa
walikuwa ndio wafadhili wakubwa wa kuuza ndege za kivita kwa Israel lakini
katika vita ya Six days War Israel walionyesha kipigo kikali sana kwa maadui
ambacho wafaransa walisema kipigo hicho hakiwezi kusababishwa na ndege zao kwa
hivyo uhusiano na Isarael kijeshi ulisimama kwani Israel walikuwa wakiziboresha
ndege hizo na zikatoa kichapo kikali
June 5 1967 – Isarel
kwa dakika 3 tu walizipiga ndege za maadui 451 zilizokuwa zimeandaliwa kwa
ajili ya kuifuta Israel ndege hizo mpya zilizonunuliwa na wamisri na nyingine
za Jordani na Syria zilitandikwa vibaya
na hivyo kupelekea Misri na Jordani kuweka mkataba wa kudumu wa amani na
Isarael kuwa hawatapigana tena milele
1969-1970 – Ndege 111
za maadui ziliwekwa chini pamoja na msaada wa warusi katika vita hiyo waarabu
waliaibiika
Jeshi la anga la
Israel limefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na katika operation mbalimbali
waliweza kuwalenga viongozi wa kigaidi wa palestina kwa vipimo vilivyoweza
kuwapata na kuwaua mmoja mmoja viongozi hao ni pamoja na Abu ali Mustafa, Ahmed
Yasini na Abed al azizi Rant iss aliyeuawa punde akitokea msikitini wakati wa
ibada ya ijumaa
1976 walifanikiwa
kuokoa wayahudi kadhaa waliokuwa
wakitishiwa kuuawa na Iddi amini dikteta aliyetawala Uganda katika operation
iliyoitwa operation Entebe
1991 – Jeshi la anga
la Israel lilifanikiwa kuwaokoa wayahudi wenye asili ya kiafrika huko Ethiopia
wanaoshukiwa kuwa ni watoto wa mfalme suleimani
Katika operation iliyoitwa operation Solomon
Sisi nasi tunapotafakari maswala ambayo adui ameyakusudia
kwetu na kuona ushindi wa ajabu ni muhimu kufahamu kuwa kama si Mungu kuwa
upande wetu tungelifutiliwa mbali kweli Kama si Bwana Israel na aseme sasa!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni