Jumapili, 31 Januari 2016

Nguvu ya Kufunga 1-3




SOMO namba 1; NGUVU YA KUFUNGA
Muhubiri ;Mchungaji Innocent Kamote

     Katika Mathayo 17;14-21 tunajifunza juu ya nguvu itokanayo na kufunga, Biblia inatufundisha kuwa yako mambi ambayo hayawezekani kama kuomba hakutaambatanishwa na kufunga ni kwwa sababu hii basi ni muhimu kwa kila mkristo kuchukua muda  na kutoa kipaumbela na uzito mkubwa sana  katika mfululizo wa masomo haya yahusuyo kufunga  na tutajifunza somo hili nguvu ya kufunga kwa kuzingatia vipengele vine vifuatavyo;-

·         Maana ya kufunga
·         Umuhimu wa kufunga
·         Mifano ya watatkatifu waliokuwa wanafunga
·         Nguvu ya kufunga

Maana ya kufunga
    Neno kufunga limetokana na neno la asili la kiyunani “Nestevo” ambalo nalo limetokana na muunganiko wa maneno mawili ya kiyunani “Ne” na “Esthio”. Neno “Ne”maana yake ni bila au pasipo kwa kiingereza ni “No” au “Without”na Esthio  maana yake ni kula chakula au kinywaji kwa kiingereza “To eat solid or liquid food”Kwa msingi huo Neno Nestevo sasa linaunganisha maneno hayo mawili ya kiyunani  Ne na Esthio na lina maana ya Bila kukla chakula au kunywa kinywaji chochote kwa msingi huo basi maana kamili ya neno kufunga ni Bila kula au kunywa chochote. Without eating solid or liquid food
      Hiyo ndiyo maana ya kufunga kufunga sio kuacha kusoma magazeti tuliyoyazoea,au kuacha kuchana nywele n.k ni kuacha kabisa kula na kunywa maana hii ya kufunga inathibitishwa na maandiko kadhaa yafuatayo Ezra 10;6,Yona 3;7,2Samuel 3;35,Esta 4;16 Kumbukumbu 9;9 Matendo 9;9 ni muhimu kufahamu pia kuwa kufunga sio kuacha kula aina fulani ya vyakula na kula aina nyingine ya vyakula  kwa mfano labda mtu aache kula ugali au wali lakini anakunywa maji au kunywa soda,au maziwa au uji na matunda n.k kufunga maana yake ni kuacha kula chochote, wako watu wanaofundisha funga ambayo sio ya kibiblia Partial Fasting na hutumia andiko la Daniel 10;2-3 katika kuhalalisha fundisho hilo katika andiko hili kuna maneno “Sikula chakula kitamu” chakula kitamu ni Dessert kwa kiingereza au Pudding yaani ndizi ,nanasi,papai ,machungwa  jamii za matunda n.k Daniel anachokisema hapo ni mkuwa hakula kabisa chakula chochote ikiwemo na hivyo hakula kabisa na hata kama ingekuwa ndivyo ni muhimu kufahamu kuwa huwezi kufanya fundisho kupitia mstari mmoja tu kwa kanuni za matumizi halali ya maandiko hivyo fundisho hilo sio halali

Umuhimu wa kufunga
     Mathayo 6;16-18, Yesu Kristo anamtazamia kila mtu aliyeokoka kuwa na maisha ya kufunga hili liko wazi kupitia lugha inayotumika katika maandiko  “Tena mfungapo”au “Bali wewe ufungapo”hii maana yake Yesu anamtazamia kila mtu aliyeokoka kuwa na wakati wa kufunga katika msingi uleule wa wakati tunapoomba Tena wewe usalipo Mathayo 6;5-6, katika mistari hii tunajifunza kuwa Mungu huwajazi wale wafungao , maana yake huwapa thawabu au huwapa zawadi au kuwajazi pale palipopungua kwa msingi huo  Mungu hutuongeza imani inayopungua kwetu tunapofunga ,wanafunzi hawakuweza kumtoa pepo kwa sababu ya upungufu wa imani yao na wakaelezwa kwamba hawana budi kufunga na kuomba ili wawe na imani hiyo Mathayo 17;14-21 hivyo kufunga hutuongezea imani.

Mifano ya watakatifu waliokuwa wanafunga
·         Yesu Kristo  - mara baada ya kujazwa na Roho alifunga siku arobaini baada ya mfungo alirudi akiwa kwa nguvu za Roho Luka 4;1,14.
·         Musa – Kutoka 34;28
·         Ezra – Ezra 10;6
·         Eliya – 1Falme 19;8
·         Daudi – Zaburi 109; 24
·         Paulo na Barnaba Matendo 14;23
·         Kanisa la kwanza Matendo 13;1-3
     Ikiwa watakatifu wengi tunaowaona katika Biblia walifunga na tunaona jinsi mambo yalivyobadlika baada ya kufunga sisi nasi hatuwezi kupuuzia kufunga na tukadai kuwa ni wakristo kibiblia, kupuuuzia kufunga kutatufanya tuwe dhaifu kiimani tukilinganishwa na watakatifu wa zamani

Nguvu ya kufunga 
Sehemu nyingi sana katika Biblia tunaona jinsi ambavyo mambo yalivyobadilika baada ya kufunga na kuomba , Mifano  mitano ifuatayo inatufundisha juu ya nguvu ya kufunga
·         Wana wa Israel  walipigwa mfululizo katika vita na wana wa Benjamini na baada ya kupigwa mfululizo wakaamua kufunga na kuomba  Waamuzi 20;20-22,24-26baada ya kufunga na kuomba matokeo tyalibadilika ,Benjamini wakapigwa sana  na wana wa Israel wakashinda  kwa kuiteketeza miji ya maadui zao kwa moto waamuzi 20;34-35,41-45,48 tunaweza kuitia moto miji yote ya shetani katika ulimwengu wa kiroho kama tukiwa wafungaji
·         Ezra hakutaka kumtegemea Mfalme na badala yake walifunga  na mkono wa bwana ukawa pamoja naye  nay eye na wenzake wakaokolewa na mikono ya adui  Ezra 8;31-32 ikiwa tunahitaji kuokolewa katika mikono ya adui kama kanisa ni muhimu kuzingatia swala la kufunga
·         Yehishafati alipata taarifa za kuwako kwa jeshi kombainia ya maadui waliotaka kumpiga akatangaza kufunga  na kuomba  2nyakati 20;1-4 matokeo yake wakashinda vita kirahisi kwa kuimba sifa tu 2Nyakati 20;22-25
·         Nehemia alivyopata taarifa za kubomolewa kwa ukuta wa Yerusalem na malango yake  kuteketezwa kwa moto alifunga na kuomba nehemia 1;3-4 na matokeo yake ukuta ulijengwa tena kwa muujiza mkubwa Nehemia 6;15-16
·         Hasira ya Bwana inapowaka kwaajili ya taifa au kanisa kutokana na uovu wa watu inaweza kufanywa kuwa amani kwa kufunga na kuomba 1Falme 21;27-29,Yona 3;7-10,Ezra 10;6
                                 Namna hii haitoki ila kwa kufunga na kuomba mathayo 17;21

 Yesu alifunga siku 40 akiongozwa na Roho Mtakatifu Nyikani

SABABU   ZA KUFUNGA somo  na 2
Muhubiri ; Mchungaji Innocent Kamote
Tunaendelea na mfululizo wa masomo yahusuyo kufunga na sasa au leo tunaingia katika somo la pili linalozungumzia sababu za kufunga tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo;-

·         Kufunga ni mapenzi ya Mungu
·         Kila mtu aliyeokoka anaweza kufunga
·         Sababu za kufunga

Kufunga ni mapenzi ya Mungu
    Katika mathayo 6;16-18  tuliona Yesu akitumia neno tena mfungapo na Bali wewe ufungapo hasemi kama wewe ukipenda kufunga au tena mkipenda kufunga hii maana yake  ni kuwa Yesu anatarajia kuwa kila mtu aliyeokoka awe na maisha yaliyojawa na kufunga ,kuna wakatui mungu hufurahia kutuona tumemfungia yeye ,tunapokula na kunywa tunafanya hivyo kwa ajili ya nafsi zetu na tunapoacha kula na kunywa tunakuwa tumeacha kwa ajili ya Mungu yaani tunafanya hivyo kwa ajili ya nafsi yake Mungu Zekaria 7;4-6 yako mambo kadhaa ambayo hatuwezi kuyapokea kwa Mungu ikiwa hatumwendei kwa kufunga Yoel 2;14 kwa nini inakuwa hivyo tutapata majibu ya maswali hayo tutakapoangalia sababu za kufunga

Kila mtu aliyeokoka naweza kufunga
    Mtu yeyote aliyeokoka mwenye afya timamu anaweza kabisa kufunga, kwa msingi huo hatupaswi kujiona kuwa hatuwezi na kuruhusu woga, ikiwa wafuatao katika biblia walifunga  ni wazi kuwa kila mmoja wetu anaweza kufunga
a.       Ana Bint Fanuel – Huyu alikuwa mjane mwenye umri wa miaka 84 hata hivyo alikuwa mfungaji mkubwa sana ,ikiwa mzee wa jinsi hii aliweza kufunga  ni muhimu kufahamu kuwa sisi nasi tunaweza kufunga luka 2;36-37.
b.      Watu ambao hawajaokoka – watu ambao hawajaokoka waliweza kumsikiliza Yesu akiwafundisha bila kula wala kunywa kwa siku tatu Mathayo 15;32 ikiwa hawa waliweza bila shaka sisi nasi tunaweza
c.       Ng’ombe na kondoo – wanyama kama ng’ombe na kondoo waliweza kufunga wakati wa Yona ona katika Yona 3;7 ikiwa hawa waliweza sisi hatuna udhuru kabisa
Watu wanaoweza kuepuka swala la kufunga ni wale ambao wana afya mbaya au wajawazito wao sio vema kufunga katika halui kama hizo na pia ni muhimu kuzingatia kutokuwalazimisha watoto wetu kufunga bila hiyari yao Ni muhimu kukumbuka kuwa kufunga ni kuacha kula na kunywa  hivyo tunapopiga mswaki na maji yakaingia kinywani au wakati wa kuoga matone yakakudondokea kinywani bila kukusudia huko sio kula na kunywa kwa hiyo kufunga kuko palepale Mume na mke watazingatia kupatana ili kuwa na kiasi katika swala hili  1Koritho 7;5 biblia inasema hivi “Msinyimane, isipokuwa mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda fulani ili mweze kujitoa kwa maombi, kisha mrudiane tena ili Shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kutokuwa na kiasi.” Hii ni kwa sababu mmoja wa wanandoa asipokuwa radhi na mfungo wako hususani Mume ambaye ni kichwa basi mfungo huo unaweza kuwa batili. Ni muhimu pia kila mfungaji kuzingatia  kumuomba Mungu neema ya kumwezesha kufunga kabla ya kuanza kufanya hivyo kwa kufanya hivyo Mungu anatupa neema ya kutuwezesha kufanya yale tuliyokuwa hatuwezi kuyafanya zamani  neema hii itatuwezesha kufunga Yohana 15;5,Wafilipi 4;13,Yohana 1;16-17 Wakolosai 1;10-11

Sababu za kufunga
     Kuna sabau kadhaa za kutufanya sisi kufunga
1.       Kutokufunga ni sawa na kuabudu sanamu au miungu mingine
     Biblia inatufundisha kujilinda nafsi zetu na ibada za sanamu na kuikimbia ibada ya sanamu 1Yohana 5;21,1Koritho 10;14 sanamu katika Biblia ni zaidi ya vinyago vya kuchonga vya miti na fedha n.k  lakini pia ni kitu chochote au jambo lolote au mtu yeyote ambaye umempa moyo wako  wote , akili zako zote na roho yako yote  na kuruhusu ichukue nafasi ya Mungu kwa msingi huo sanamu inaweza kuwa Elimu, Mkeo, akili zako,cheo , kazi au kutamani chochote au kukitumikia  kuliko Yesu Kristo hiyo ndiyo ibada ya sanamu Kwa msingi huo kama mtu atakuwa anaendekeza kula basi mungu wake ni tumbo Wafilipi 3; 17-19 mtu wa  namna hii anawekeza nguvu zake katika maswala ya lishe na fedha na akili kwa ajili ya kula inasemekana ya kuwa mtu a anayetumia dakika 30 kunywa chai  na dakika 45 kwa chakula cha mchana ,dakika 20 chai ya jioni,dakika 45 chakula cha usiku na dakika 40 nyingine katika  kunywa soda ,juice,kutafuna karanga  au machungwa njiani .n.k mtu wa namna hiyo muda anaoutumia kula kwa siku ni dakika 180 sawa na masaa matatu hivyo kwa mwezi mtu huyo anatumia saa 90 au 93 ambazo ni karibu  siku nne nzima kwa hiyo kwa mwaka  mmoja anatumia siku 48 kula tu  kama mtu huyu ataishi miaka 75 atakuwa ametumia siku 3600 au miaka kumi 10  mchana na usiku kula tu  kwa msingi huo mtu huyo atakuwa anajaribu kuishi kwa mkate tu na analisujudia tumbo Yesu alisema mtu hataishi kwa mkate tu .

2.       Kufunga ni kushinda jaribu la kwanza la shetani lililoleta maafa kwa mwanadamu
    Adamu wa kwanza alijaribiwa na shetani kwa chakula Yaani kwa kula lile tunda na akaanguka  dhambini Adamu wa mwisho yaani Yesu Kristo alipojaribiwa na ibilisi jaribu la kwanza lilikuwa ni  chakula pia Mathayo 4;3-4, nguvu za Roho wa Mungu zinapatikana kwa mtu ambaye hatiwi chini ya chakula 1 Koritho 6;12 Luka 4;1-2,14 chakula nmdicho kinachoweza kumfanya mtu aibe, afanye uasherati ,atoe au kupokea rushwa  na kufanya dhambi nyinginezo kwa msingi huo kushinda jaribu la kula ni kuwa kama Yesu  na ni kumshinda shetani  na kupata nguvu za Roho wa Mungu  Yesu hakutiwa chini ya uwezo wa chakula ,Pamoja na kuletewa chakula na wanafunzi wake aliendelea  kuifanya kazi ya Mungu bila kula Yohana 4;6-8,31-34

3.       Kufunga ni kuomboleza mathayo 9;14-15
       Mtu huomboleza baada ya kuondokewa na mtu ampendaye   na huwezi kufurahia kunywa na kula  2samuel 1;11-12,3;31-35,37-38 Yesu tumpendaye hayuko nasi kimwili ,tunaomboleza kwa kumkosa na kumtafuta katika maombi, na tunapompata katika maombi ndipo furaha yetu inapotimilika , aidha pia kwa sababu yaq maangamizo yatakayowapata ndugu zetu au sisi kama tumefanya dhambi  tunaomboleza na kutamani kuwa huru kumbukumbu 9;18-19

4.       Kufunga ni kujinyenyekeza mbela za Mungu
1Falme 21;27-29,Ezara 8;21.luka 14;11 na yakobo 4;9-10 kufunga ni ibada kwa Mungu ni ishara ya kutafuta kunyenyekea na ni kujinyenyekeza kwa Mungu hii ni kwa sababu  kula na kunywa ndiko kunakoleta kiburi cha uzima hata awe mbali  na mungu na kuwasahahu hata watu wengine , kushiba na kusaza  kunamfanya mtu aone  kwamba hana haja ya kumtafuta Mungu kumbukumbu 32;13-15 Isaya 22;13 mtu anapokuwa amefunga kiburi cha uzima kinanyonywa  na anajifunza kumtumainia Mungu katika udhaifu wa mwili.

5.       Kufunga ni kwa ajili ya afya zetu
Maandiko na kitaalamu inashauriwa na kupendekezwa kuwa ni muhimu sana kufunga pia kwa ajili ya afya zetu Mungu alipoweka mpango wa kufunga na kukataza mambo kadhaa wa kadhaa hakufanya hayo kwa ajili yetu lakini zaidi sana kwa ajili yetu

SOMO namba 3; MUDA   WA KUFUNGA

Tunaendelea na mafululizo wa masomo yahusuyo kufunga  na sasa tunaliangalia somo namba tatu ambalo tutalichambua kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo

·         Aina mbili za wito wa kufunga
·         Muda wa kufunga
·         Vizuizi vya nguvu ya kufunga
Aina mbili za wito wa kufunga

Kuna aina mbili za wito wa kufunga  ambazo mtu aliyeokoka anapaswa kuzishiriki

1.       Kufunga kunakotokana na mbiu ya kufunga
2Nyakati 20;3-4,Yona 3;7-8 na Ezra 8;21 Huku ni kufunga kunakotokana na mbiu inayoweza kulatwa kwetu  na kiongozi wetu wa kanisa  au taifa n.k kiongozi anapolieleza kanisa kwamba lifunge  kwa siku kadhaa kwa ajili ya jambo fulani na kisha kukutana mahali fulani kwa ajili ya kilele cha maombi hiyo ni mbiu ya kufunga  na inaweza kutanga zwa aidha na kiongozi wa kundi la maombi au shemasi wqa eneo husika viongozi wa zone au section  kwaya ,vijana ,wamama n.k.kiongozi atatelezea sababu ya kuitisha mbiu hiyo ya kufunga na kama watu wana shiriki inaleta baraka kwa jinsi ambavyo inajumuisha watu wengi kwa pamoja kwani Biblia inasema wawili wenu ama watatu wakipatana katika jambo lolote watakalomuomba Baba wa mbinguni watatendewa Mathayo 18;18-20

2.       Kufunga kunakotokana na uamuzi Binafsi
Katika maisha binafsi ya mtu aliyeokoka ni muhimu kujipangioa muda wa kuwa na vipindi vya kufunga na kuomba ili kujichotea baraka mbalimbali kutoka kwa Bwana ,kama kila mmoja anavyoweza kujipangia muda wake binafsi wa kuomba bila kungojea maombi ya kikanisa basio hali kadhalika ni muhimu kujipangia siku za kufunga na kuomba binafsi , na tutaweza kuiomba kwa ajili nya mahitaji BINAFSI na mahitaji ya kifamilia kanisa na kazi ya Mungu 

Muda wa kufunga 
 Je ni muda gani unaofaa kwa kufunga? Biblia haiweki muda maalumu wala sheria juu ya siku za kufunga kwamba ziwe ngapi lakini tunapoangalia vipindi vinavyotajwa katika Biblia kuhusu kufunga basi tutajifunza mambo kadhaa ya msingi , mifungo mingi inayotajwa katika Biblia haiweki siku za kufunga  lakini tutaangalia hapa ile inayotaja siku za mfungo na sababu za kufunga

MUHUSIKA  KUFUNGA
KIPINDI CHA KUFUNGA
SABABU ZA KUFUNGA
MAANDIKO
1.Daudi
Siku 1
Kuomboleza kwa ajili ya aliyekufa
2samuel 3;35
2. Israel
Siku 1
Kumuuliza bwana kwa ajili ya kushindwa vita
Waamuzi 20;24-27
3.Daudi
Siku 1
Kumlilia aliyekufa
2samuel 1;12
4.Yuda
Siku 1
Kuutafuta uso wa Bwana
Nehemia 9;1-4
5.Yuda
Siku 1
Kuutafuta uso wa Bwana
Yeremia 36;6
6.Farisayo
Siku 2 kwa kila juma
Sababu za haki za kudini
Luka 18;9-12
7.Israel
Siku 1
Kumlilia Bwana waokolewe na wafilisti
1samuel 7;6-14
8.Esta/Mordekai
Siku 3
Kumuomba Mungu kwa ajili ya taifa la kiyahudi huko uhamishoni wasiuawe
Esta 4;13-16
9.watu wengi
Siku 3
Siku tatu kusikiliza mafundisho ya Yesu
Mathayo 15;32
10.Paulo
Siku 3
Wokovu na wito wa paulo
Matendo 9;9
11.Daudi
Siku 7
Kumuombea uhai mtoto wake
2samuel 12;16-18
12.Israel
Siku 7
Kuomboleza kifo cha sauli na wanae
1samuel 31;13
13. Paulo na watu 276
Siku 14
Kwa ajili ya safari iliyojaa misukosuko
Matendo  27;33,37
14.Daniel
Siku 21
Kumuomba Mungu  kwa ajili ya Taifa baada ya kufunuliwa neno
Daniel 10;1-3
15.Musa
Siku 40
Kuketi mlimani mbele za Mungu na kuombea Israel
K/Torati 9;9.18.25-29.10;10
16.Yoshua
Siku 40
Kuketi mlimani mbele za Mungu
Kutoka 24;12-15
17.Eliya
Siku 40
Safari ndefu baada ya chakula maalumu
1falme 19;5-8
18. Yesu
Siku 40
Kuongozwa na Roho ili kujaribiwa nyikani
Mathayo 4;1-2

Kutokana na Jedwali hilo hapo juu tunajifunza mambo ya msingi yafuatayo;-
1.       Kipindi cha kufunga katika kumtafuta Bwana kwa maombi kinapaswa kiwe sio chini ya siku moja yaani saa 24
2.       Kipindi cha kawaida cha mfungo kinapaswa kuwa siku tatu nzima  ni katika hali ya uzito usiokuwa wa kawaida  ndipo tunazidisha hapo tena kwa muongozo wa Roho Mtakatifu  na hata ikiwa hivyo basi hazitazidi siku saba
3.       Kufunga siku zaidi ya saba  ni lazima kuambatane na kufunuliwa Neno,Daniel,Musa ,Yoshua ,Yesu na Eliya walikuwa katika hali ya kupokea ufunuo wa Neno la Mungu na kwa ajili ya taifa na ulimwengu kwa msingi huo mtu hawezi kufunga siku 40 bila kula na kunywa kama hakuna muongozo maalumu wa Roho Mtakatifu  yeye anapoongoza ndipo inapotokea neema maalumu kukuwezesha kufanya hivyo 1falme 19;8

Vizuizi vya nguvu ya kufunga
1.       Nia ya kufunga Warumi 12;2 Nia yako ya kufunga ni ya muhimu sana kuliko hata kufunga kwenyewe ikiwa nia yako haiku sawa na neno la Mungu itazuia upatikanaji wa nguvu itokanayo na kufunga
2.       Kufunga katika dhambi Yeremia 14;10-12,Isaya 58;3-5 dhambi huzuia maombi na nguvu itokanayo na kufunga kwa msingi huo toba ni ya muhimu sana kabla ya kuingia katika mifungo
3.       Kufunga Bila kuomba 2Nyakati 20;3-4,Ezra  8;21,Mathayo 17;21 Kufunga mara nyingi ni lazima kuambatane na kuomba  kama unafunga kisha unapoteza muda katika shughuli nyinginezo basi nguvu itokanayo na kufunga hutaiona
4.       Kufunga hakupaswi kuchukua nafasi ya imani. Ni muhimu kufahamu kuwa kufunga ni ibada kwa Mungu na huchiochea imani lakini hatupaswi kufikiri kuwa kila jambo jhaliwezekani mpaka tufunge kwanza pasipo imani hatuwezi kumpendeza Mungu waebrania 11;6,yakobo 1;6 kufunga kunachochea imani tu na sio sababu ya kumlazimisha Mungu kufanya jambo.

Maoni 6 :

Unknown alisema ...

Ahsante

Bila jina alisema ...

Tuendelee kujifunza neno la Mungu ili tukue kiimani

Bila jina alisema ...

Asante sana , nimebarikiwa sana

Bila jina alisema ...

Ubarikiwe sana🙏🙏

Bila jina alisema ...

Nimeona mafindisho Mazurie

Bila jina alisema ...

Nimebalikiwa sana