MJENZI: Mchungaji Innocent Kamote
Moja ya matatizo makubwa na
yanayokuwa kwa kasi siku hadi siku na hususani siku hizi ni tatizo la
migandamizo (depression) Hili ni
tatizo la kisaikolojia na kiroho pia. Tatizo hili linapopita kiasi huweza
kupelekea mwanamke au Mwanamume kujiua, na kwa vijana ambao uwezo wao wa
kuhimili mihemko ni wa kasi zaidi wengi huweza kujidhuru, kumbuka kuwa wengi wa
watu wanaofikia ngazi ya kujiua
wenyewe wakati mwingine hufanya
hivyo kwa sababu ya migandamizo depression
hali ya migandamizo hii wakati mwingine haielezeki lakini huweza kujumuishwa
hali za kukata tamaa, kukosa furaha au faraja na, kuvunjika moyo,kufiwa na
mpendwa mwanao, mkeo, mumeo au ndugu na rafiki, kujiona duni, kukosa rafiki, kusalitiwa,
kupoteza tumaini ndani ya ndoa, kuudhiwa na jamaa waliokaribu, kusalitiwa,
talaka, ndoa iliyovunjika, au kuchoshwa na vikao vya upatanishim kazi nyingi na
maudhi, kukosa furaha kuwa na huzuni na kujisikia hali nzito sisi kama wanadamu
wakati mwingine hufikia hatua ya kuwa na hali kama hizo Zaburi 34;17-19 inasema hivi:-
“17. Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote. 18.
Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa. 19.
Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini Bwana humponya nayo yote.”
Unaona watakatifu waliotutangulia pia walipitia Matatizo haya
waliovunjika moyo, na waliopondeka roho hii ni lugha ya zamani inayozungumzia
stress na depression wakati huu biblia inazungumzia kuvunjika Moyo Broken
hearted na roho iliyopondeka crushed in spirit
Ø
Tatizo hili kwa mujibu wa wanasaikolojia ni
tatizo la ngazi ya juu sana ya maumivu ya moyo wa mwanadamu au tatizo la akili
la kibinadamu, Tatizo hili wakati mwingine linaweza kumpata mtu kwa sababu
ameshindwa kuipokea taarifa mbaya nzito kama kupoteza mchumba, kufiwa na
uliyempenda, na inapofikia ngazi ya akili za mwanadamu kushindwa kulibeba
tatizo hilo mwanadamu huweza hata kupoteza maisha au kupata ugonjwa wa kiharusi
stroke mfano 1Samuel 4;12-22
“12. Basi, mtu mmoja wa Benyamini akapiga mbio
kutoka mle jeshini akafika Shilo siku ile ile, hali nguo zake zimeraruliwa, na
mavumbi kichwani mwake. 13.
Alipofika, tazama, Eli alikuwa ameketi kitini pake kando ya njia, akingojea;
maana moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Na yule mtu
alipoingia mjini, akatoa habari, mji wote ukalia. 14. Naye Eli aliposikia
kelele za kile kilio, akasema, Maana yake nini kelele za kishindo hiki? Yule
mtu akafanya haraka, akaenda, akamwambia Eli. 15. Basi Eli umri wake umepata
miaka tisini na minane; na macho yake yamepofuka hata asiweze kuona. 16. Yule mtu akamwambia Eli, Mimi ndimi
niliyetoka jeshini, nami leo hivi nimekimbia toka jeshini. Naye akasema,
Yalikwendaje, mwanangu?
17. Yeye aliyeleta
habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi
sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na
sanduku la Mungu limetwaliwa. 18.
Ikawa alipolitaja sanduku la Mungu, Eli akaanguka kitini pake kwa nyuma, kando
ya mlango, shingo yake ikavunjika, akafa; maana alikuwa mzee, tena mzito. Naye
alikuwa amewaamua Israeli miaka arobaini.
19. Tena mkwewe,
mkewe huyo Finehasi, alikuwa mja-mzito, karibu na kuzaa; basi, aliposikia
habari ya kutwaliwa sanduku la Mungu, na ya kwamba mkwewe na mumewe wamekufa,
akajiinamisha, akazaa; maana utungu wake ulimfikilia. 20. Hata alipokuwa katika kufa, wale wanawake waliohudhuria
karibu naye wakamwambia, Usiogope; kwa maana umezaa mtoto mwanamume. Walakini
hakujibu, wala hakumtazama. 21. Akamwita mtoto, Ikabodi, akisema, Huo utukufu
umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na
kwa sababu ya mkwewe na mumewe. 22. Naam, akasema, Huo utukufu umeondoka katika
Israeli; maana sanduku la Mungu limetwaliwa.
Unaona si kila mtu
duniani anaweza kuvumilia taarifa ngumu na mbaya kama hizo, Moyo ulioshambuliwa
na roho iliyopondwapondwa huweza huweza kusababisha Mauti! Wako wengi wanalia
kwa sababu ya matatizo mbalimbali duniani ni Ngumu sana
Ø
Inahitajika Mungu kuingilia kati wakati mwingine
ili mtu ashinde migandamizo hii katika maisha, wakati mwingine shetani huruhusu
migandamizo hii kwa kutushambulia kwa matatizo mengi ili kutupata na kufanikiwa
kutuua kimwili na kiroho au hata kimafanikio
Ø
Daudi mtu wa Mungu ni moja ya watu waliopitia
tatizo la migandamizo kwa zaidi ya miaka 25 ya maisha yake, Mfalme Sauli
alikuwa anataka kumuua, aliishi mbali na ndugu zake pamoja na kuwa Mungu alikuwa amempaka mafuta
lakini alikutana na matatizo mengi mbali na nyumbani, mbali na marafiki, uchumi
duni watu duni wenye madeni kwa ujumla aliishi kama yatima na wakati mwingine
matatizo yenye kutatanisha 1Samuel 30;3-8
Ø
Hatujui wewe unapitia migandamizo ya aina gani
pengine mchumba wako amevunja uhusiano nawewe, Mumeo anaweza kuwa sio muaminifu
au amekuacha, watoto wanaweza kuwa sio watii, ndugu na jamaa hawakuoni kuwa wa
maana na wakati mwingine hata ndugu zako wa Kanisani wako kinyume nawewe, umezungukwa
na taarifa mbaya kila mahali, unahangahika tu na unashindwa ni wapi pa
kusimamia inakuumiza lakini huna jinsi, maisha hayaonyeshi kufanikiwa
unachokipata hakitoshelezi mahitaji yako kibinadamu kila ukipiga akili
inakataa, malengo yako na ndoto zako katika maisha hazionekani kuwa na
mafanikio je unafanya nini kukabiliana na hali hizi wakati mwingine unalia
kitandani unatembeatembea na huoni faraja yoyote hali yako ni ngumu unahitaji
kushinda mgandamizo huo wa mawazo kwani maisha yako yanathamani sana wala
usifikie hatua ya kujiombea kufa au kutamka heri nife!
Ø
Migandamizo mingine inatokana na mitatizo sugu
katika ndoa wengine wanajuta wanasema heri nisingeolewa au heri nisingeoa
matarajio na matumaini uliyoweka kwa mwenzi wako picha yake imekuwa kinyume na
ndoto zako, sasa umekata tamaa, wengine wametamani kufa au wapenzi wao wafe au
wamepoteza uaminifu ili kutafuta faraja nje ni matatizo matupu ni maumivu juu
ya maumivu upweke wako haujaondoka kamwe nyumba imekuwa kama kituo cha polisi
huna rafiki nyumbani hali hizi zote zinasababisha moyo kupondeka na roho kuumia
unahitaji uponyaji.
JINSI YA KUSHINDA MIGANDAMIZO
·
Samehe wote walio kinyume na wewe 1Samuel
24;1-6, Jifunze kuwa Komandoo wa kusamehe na sio wa kulipiza kisasi usiwe kama Van
dame alisema “No retreat no Surrender” hata kama kuna uonevu wa kupita kawaida
Mungu na atupe uvumilivu na uwezo wa kusamehe Yesu aliweza kusamehe waliomtesa
Msalabani, Stephano aliweza kusamehe walimpiga kwa mawe unahitaji Kusamehe ili
uchungu uondoke Moyoni mwako linaweza kuwa jambo gumu lakini uliomba Roho
Mtakatifu atakuwezesha.
·
omba toba kwa Mungu Zaburi 38;4 toba ni jambo la
msingi sana sisi sote tunakosea, yeye asiyekosea huyo ni mtu mkamilifu,
tunapokosea lazima tukimbilie toba, omba radhi kwa Mungu Mungu ataondoa uchungu
mioyoni mwetu
·
Lia kwa machozi ya furaha na kupiga kelele za
shangwe kumsifu Mungu Ayubu 1;20-22,Marko 14;26,matendo 16;25, kisaikolojia
kulia kunaleta nafuu, usipolia jeraha la moyo linaweza kuwa kubwa hivyo ni vema
ukalia, ukimaliza imba zaburi, sikiliza nyimbo za kwaya na neon la Mungu furahi
na kama unaweza kucheza mpira nenda furahi na uponyaji wa Bwana utachukua
nafasi
·
Jitie nguvu katika Bwana na kuomba na kuutafuta
uso wake 1Samuel 30;6-8 mtwike yeye fadhaa zako maana anajishughulisha nazo
1Petro 5;6-7 soma neno la Mungu hususani zaburi
Kuna wakati hutapata mtu wa kukutia moyo
hata kidogo, huu ni wakati wa kujitia nguvu katika Bwana, tumia upweke
kujiimarisha kwa Bwana na kuomba manabii wengi waliishi katika migandamizo lakini
waliamua kutafakari, kukaa peke yao kuomba na kukesha na Mungu akashughulika na
matatizo yao
Kumbuka Mateso ya mwenye haki ni mengi, Lakini
Bwana humponya nayo yote. Ni imani yangu kuwa Umejengeka na bwana amekuganga
ikiwa yako mambo zaidi maswali au ushauri nipigie simu 0718990796 nitaomba
pamoja nawe na kukushauri
Maana Msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka isipokuwa ni ule
uliokwisha kuwekwa yaani Yesu Kristo –
Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima Rev. Innocent Kamote
+255784394550
+255718990796
Box. 100 Muheza, Tanga
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni