Ndugu wawili walipanga kuwa na safari, na siku moja jiono waliamua kujipumzisha katika moja ya misitu mikubwa, walipokuwa wakiangalia huko na huko humo waliona jiwe lililokuwa na maandishi yafuatayo;-
"Ulimwengu wa Mafanikio uko na wale wanaothubutu"
“Yeyote atakayeliona jiwe hili” walilisoma “ na aingie moja kwa moja
msituni wakati wa jua kupunga yaani jioni, Ndani ya msitu mto utatokea ogelea
mto huo mpaka ufike upande wa pili, hapo utaona gari zuri na ufunguo wake
endesha gari hilo mpaka kwenye kilele cha mlima bila kuangalia nyuma,
utakapofika mlimani utaona nyumba na ndani ya nyumba niyo Utapata furaha kuu”
walipomaliza kusoma habari hii katika jiwe Kaka mdogo akasema Kaka tafadhali
twende….. tunaweza kuogelea na kuuvuka mto huu na kuchukua gari na kupata
nyumba na huko mlimani tutaipata furaha kuu!
Sitakwenda sitaingia msituni na
kuogelea sita vuka huko alisema Kaka mkubwa na kisha akamsahauri nduguye,
“fikiria labda yaliyoandikwa humu ni fumbo, au labda tunaweza kuwa hatujasoma
sawasawa, au tumesoma na hatukuelewa, na hata kama yaliyoandikwa hapa ni kweli
jaribu kuwaza kama tutavuka na tusiuone mto au kama tunaweza kuuona na
tukashindwa kuogelea au kama tutaogelea
na kuvuka nay ale yaliyoahidiwa upande wa pili yakawa hayako na badala ya
kupata furaha kuu, tukajikuta tunaangamia, tutawezake kuupanda mlima bila
kupumzika wala kugeuka nyuma inawezekana ile furaha kuu tunayoitazamia ikawa ni
msiba mkuu sana kwetu
“Kwa maoni yangu” alisema kaka mdogo “Hauko sahii”
Yaliyoandikwa katika jiwe hili hayangelikuweko hapa pasipo sababu, Na ni wazi
kwamba Hakuna madhara yanayoweza kutupata endapo tutajaribu kama tutajaribu,
aidha kwa upande mwingine kama hatutalifanyia kazi hili kuna mtu mwingine
atasoma na kulifanyia kazi yaani haya yaliyoandikwa kwenye jiwe na atapata
furaha kuu, sisi tutapoteza na mimi sitaki tupoteze nafasi hii”
Kaka mmkubwa alijibuna kusema
kuna mithali isemayo “ Mtaka cha uvunguni shurti ainame” yaani katika kutafuta
furaha kuu tutapata majaribu na maumivu, na pia mithali nyingine inasema “Ndege
aliye mkononi ni bora kuliko wawili walioko Porini” Kaka mdogo akajibu na
kusema nimesikia Basi yeye anayeogopa asiingie msituni, Basi kaka mdogo
akaingia msituni na kuanza safari na mkubwa akabaki nyuma, ndugu mdogo aliingia
msituni usiku na akauona mto uliokuwa umeelezwa, akaogelea na kuvuka nga’mbo na
akaiona gari na ufunguo wake na kuingia na kuiendesha akapanda mlimani bila kuangalia nyuma alienda
kwa muda mrefyu na hatimaye aliiona nyumba, kaka mkubwa alirudi nyumbani.
Aliingika katika nyumba ile na
kuikuta iko vizuri sana imeandaliwa vema na alipoingia mara kundi kubwa sana la
watu wakaja kumpokea kwa ujasiri, wakamkaribisha katika mji wao wakampaka
mafuta na kumtawadha kuwa Mfalme wao akaishi kwa furaha kuu akitawala kwa miaka
mitano, mwaka wa sita aliinuka mtawala mwingine wa mji mwingine mwenye nguvu na
wakafanya vita na ufalme wake na katika vita ile mfalme huyu alishindwa na kila
kitu kilitawaliwa na Yule mfalme mwenye nguvu, kwa kuwa hakuuawa aliamua kurudi
kwa kaka yake
Kaka yake alikuwa akiishi
kijijini na hakukuwana mabadiliko yoyote katika maisha yake hakuwa tajiri wala
masikini aliishi kawaida tu, Kaka mkubwa alifurahi kumuona ndugu yake
wakakumbatiana kwa furaha hasa kwa kuonana katika maongezi yao Kaka mkubwa
alimwambie ndugu yake unaona nilikuambia nilikuwa sahii mimi nimeishi kwa raha
mustarehe japo maisha yangu yalidumaa niko vilevile, wewe umerudi duni ingawa
ulikuwa mfalme na umekutana na taabu kubwa sana na vita kaka mdogo alijibu, “Sijutii niliyokutana
nayo nimevuka mto na nimepanda mlima, nimekuwa mfalme na nimetawala inawezekana
nimerudi nikiwa sina kitu sasa lakini
nina cha kukumbuka na kuelezea watu wewe huna cha kuelezea wala cha
kukumbuka” – wise man Leo Tolstoy interpreted by wise Master mason Rev.
Innocent Kamote.
"Ulimwengu wa Mafanikio uko na wale wanaothubutu"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni