Jumatano, 10 Februari 2016

Samuel Jumaa Kamote.


Samuel Jumaa Kamote ni nani?

Samuel Jumaa Kamote ni moja ya Viongozi Mahiri ambao, wamewahi kulitumikia taifa hili katika nyanja na nyadhifa Mbalimbali, kuanzia ngazi ya ualimu mpaka katika ngazi ya mkuu wa wilaya mbalimbali, kwa Bahati mbaya watanzania wengi wetu hatuna tabia ya kutunza na kuandika kumbukumbu mbalimbali zikiwemo za viongozi wetu waliowahi kulitumikia taifa hili katika nyadhifa mbalimbali, Ni kutokana na kutambua umuhimu wa swala hili, kwa vile Samuel Kamote ni moja ya viongozi ambao mimi nimemfahamu kwa karibu sana na kushuhudia utendaji wake wa kazi, na moyo wake katika kulitumikia taifa hili naliona si vema kuto kuandika habari zake ili kwamba yamkini vizazi vilivyopo na hata vijavyo viweze kutambua na kujifunza kutoka kwa wengine. Akiwemo mzee Samuel Jumaa Kamote.

Maana ya Jina Kamote
Jina Kamote ni jina linalopatikana miongoni mwa waseuta (yaani jamii ya makabila ya watu wa Tanga). hususani wa jamii ya Wabondei,Wasambaa  na wazigua, ingawa wengi hata wanaoitwa jina Hilo  KAMOTE hawana ufahamu kuwa jina Hilo lina maana gani, katika utafiti wa uandishi wa Makala hii nilijaribu kutafuta maana ya jina hili na penginepo ukoo huu ulikuwa na asili gani Mzee mmoja wa sikunyingi ambaye ni mzigua aishiye Pongwe ambaye ni Shekh wa dhehebu la Sunni mjini Pongwe mtaa wa Misufini anaeleza kuwa Kamote ulikuwa ni ukoo wa kikuhani ambao ulikuwa unahusika na maswala ya kuombea watu kwa Mungu na kuwapatanisha na Mungu kwa sadaka na maswala ya kuombea Mizimu ni wazi kuwa Hata chifu Kimweri na wengineo walikuwa hawahusiki sana na maswala ya matambiko lakini swala hili lilikuwa linashughulikiwa na wataalamu hao ambao walikuwa ni wa ukoo wa Kamote jina. Hili Kamote linapatikana kwa jamii ya wasambaa na wabondei  na wazigua katika maeneo yafuatayo Korogwe, Lushoto, Muheza mjini, Kicheba, Bombani na maeneo ya Maramba, Kamote walio wengi ni wasambaa na inasemekana hata Amboni wako kina Kamote ambao ni wabondei lakini wamepotelea digo.

Jina Kamote pia linaonekana katika sehemu kadhaa za inchi ya Ugala huko Kenya ambako waseuta walikaa kwa Muda, kuna asili za majina Kamote yanayoweza kupatikana katika kabila nyingine mfano Kameta huko Unyakyusani, Kamau huko Kenya, Kamota huko zigua na Kamote huko Philippines  bara la Asia.

Kwa mujibu wa watu wa Iringa Kamote ni kitu kitamu sana au kitu kilicho kizuri hii ni kwa mujibu wa Mhehe mmoja aitwae Kelvin Josephu Nyalusi, Pia kwa Mujibu wa Kabila ya wagogo Huko Dodoma Kamote ni kitu kitamu mfano wa Pipi, ni wazi kabisa kuwa makabila hayo yana tafasiri ya kweli kuhusu jina Kamote ambalo inawezekana wasambaa na wabondei  na hata wazigua wakawa hawajui, Maelezo mengine kuhusu Kamote niliyapata kutoka kwa mzee Samuel Jumaa Kamote ambaye alinieleza kuwa jina hili kwa asili ni sawa na jina Kamota linalotumika huko uziguani likimaanisha Kapata au Kauchinja au mtu aliyefanikiwa au kushinda, alieleza pia kuwa huko kanda ya ziwa pia kuna moja ya kabila ambalo hutumia jina Kamote kumaanisaha Kupata Kitu kizuri au kupata kitu kitamu au kuuchinja inasemekana kuwa pia yuko samaki aina ya sato katika ukanda huo wa ziwa Victoria ambaye ni mtamu sana naye huitwa Kamote kwa msingi huo jina hilo ni kweli kuwa lina uhusiano na kitu kizuri au kitamu, Huko Philippines ndiko kuna matumizi makubwa ya jina hili Kamote wao hulitumia kwa kumaanisha Viazi vitamu ambavyo huitwa Kamote, Kwa msingi huo utaweza kuona kwa asili jina Kamote limetokea Philippines ambako huko hutumika kama jina la kawaida kuhusu viazi vitamu mmea wake na chakula chake ambacho huzaliwa chini ya ardhi mmea huo na hususani chakula chake kitamu sana kinapochemshwa au kukaangwa huitwa Kamote sawa na Kabila ya Wahehe na Wagogo mmea huo wa Kamote una ngozi nyembamba sana na chakula kingi sana nje ina rangi ya zambarau na ndani manjano na wanga wa kutosha wenyewe wafilipino hukiita kiazi hicho “Morning Glory” yaani utukufu wa asubuhi, aidha maua ya kiazi hiki ni yenye mchanganyiko wa rangi nyeupe na zambarau yenye urefu wa cm 5 na umbile la mjali wa kuchujia mafuta yasimwagike “funnel-shaped” na ni kutokana na uzuri wa ua hili wafilipino waliuita mmea huo Utukufu wa asubuhi na pia kutokana na utajiri wa Vitamini A, B na C. pamoja na madini ya chuma na calicium na huliwa asubuhi licha ya kuwa na wanga mwingi kutokana na uzuri na utamu wa maua hayo na kiazi chake kiazi hiki kinaitwa Kamote. Na hii ndio asili hasa ya jina Kamote utamu wa kiazi na uzuri wa ua la kiazi kitamu au utukufu wa asubuhi kwa kifilipino.


 Mmea wa viazi vitamu, maua yake na majani yake  na kiazi cheke chenyewe huitwa Kamote katika Mataifa Mbalimbali ikiwemo Ufilipino na Urusi.

Mmea huu wa viazi vitamu huko Philipines na Kiazi chenyewe huitwa Kamote hususani utamu wa kiazi chenyewe ambacho huliwa asubuhi na kunywewa na chai na wafilipino huita Morning glory.
Kwa msingi huo maana ya Kamote ni kitu kitamu au kizuri kutokana na asili ya jina hilo, Huko Philipines, hatujui ni kwa namna gani jina hili liliweza kufika Tanga hususani kwa wabondei kwani wafilipino pia hatuna historia kamili kama waliwahi kufika hapa nchini na hakuna historia inayoonyesha kama kuna moja ya mkale wa ukoo huo aidha alifanya kazi ya Ubaharia au vipi lakini ni wazi kuwa huenda kama ilivyokuwa kwa mazao ya kigeni yaliyoletwa Afrika mashariki na wageni kutoka Ureno yalikuwa ni Mananasi, Ndizi, Muhogo na mahindi, kwa hiyo kuna uwezekano kuwa zao la viazi vitamu lilikuja Afrika mashariki kutoka Filipino na huenda ukoo wa kibondei au wazigua uliopokea zao hilo na ulianza kutumia jina hilo Kamote kama jina la mtu aliyelima viazi vitamu na jina hilo likampata mtu, huku maana ya jina hilo ikisahaulika kwa wabondei na wasambaa na wazigua  lakini wahehe na wagogo wana maana halisi kabisa sawa na ile inayotumika ufilipino.
Vyovyote iwavyo hii ndio maana ya jina Kamote na asili yake, hata hivyo pamoja na uhalisia wa jina wengi wa jamii ya Kamote ni wapole, na waungwana sana, na hata kama wanakunywa huwa hawasumbui sana watu, ni wanyenyekevu hawapendi kuonewa hupenda sifa, wana mafanikio makubwa ni wana dini na huheshimika kwa hiyo kweli Kamote wana sifa nzuri au tamu, wana upendo na hawapendi kuonelewa hizi ndio tabia zao na ukiwakorofisha ni wakorofi tabia hizi zinaashiria kuwa kuna uwezekano wa kweli kuwa walikuwa makuhani wa mila za wabondei na wasambaa au kutolewa kwa jina hili kunaonekana kabisa kulitokana na mmea wa kiazi kitamu cha kifilipino.

 viazi aina ya Kamote

UKOO WA KAMOTE-

Ukoo wa Kamote kwa maelezo ya wazee wetu ulitokea maeneo ya kwamgumi huko handeni na hivyo kwa asili ni wazigua walikuja wanaume kadhaa wa ukoo huo na kuomba ardhi ya kilimo katika nchi ya wabondei na kupata maeneo ya SEMNGANO na KWEMKABALA maeneo ya Masuguru Muheza mjini ambako ndiko ilikokuwa asili ya ukoo huu, Kamote mkubwa kabisa kwa asili alifariki katika inchi ya zigua akiwa hana mtoto na ndugu zake kwa heshima waliona kuwa jina hilo lingepotea na hivyo waliona kuwa wamwite moja ya watoto wao Kamote, na ama wakizaa watoto wawaite Kamote ili jina la ndugu yao lisipotee, Huko Semgano/ Kwemkabara ndiko yaliko makaburi mengi ya wazee kwa asili  Baadhi ya ndugu watoto wawili walikuwa wakifanya Biashara katika maeneo ya Pwani kupitia Misozwe na Kwatango na njia za Maramba, Amboni na kadhalika ukoo huu kwa asili walikuwa wazigua wa asili ya ukoo wa Mngumi, watoto hao wawili katika pitapita zao walivutiwa sana na Mabinti wa kibondei waliokuwa wakiishi kati ya Muheza na Misozwe ambapo palikuwa na Mashamba na korona za mikonge, mabinti wengi wa kibondei walikuwa na Rangi ile ya asili ya waseuta au mbega yaani walikuwa weupe kama wazungu, Kaka mkubwa kabisa aliamua kununua shamba na kupanda migomba kwa wingi kaka huyu aliitwa Semmea (Wasambaa walimuita Shemmea) na kaka wa pili aliyekuwa anaitwa Athumani Kamote naye aliungana na kaka yake na kukaa pamoja katika kijiji jirani kilichoitwa Mlingoti ambayo ndio Kicheba ya leo na Misozwe, watu wengi maarufu walihamia katika kijii hiki ikiwa ni pamoja na ukoo wa kidungwe, Semwaiko, Kihampa ambao wengi walitoka pande nyingine za wilaya ya Muheza kuja katika kijiji hiki cha mlingoti na maeneo ya shamba la mkonge la Kibaranga na shamba la mlingoti.

Athumani Kamote aliendelea kuwa mtu wa Biashara na Semmea alikaa Bonde akiendeleza kilimo baada ya kuoa mkewe wa Kwanza Athumani alipata mtoto wa kike na akaitwa Kivunga na hivyo Mzee Athumani aliitwa Sekivunga (Wasambaa walimuita Shekivunga), shekivunga aliendelea kufanya biashara zake huku akinunua mashamba na minazi, kwa muda wa miaka kadhaa hakufanikiwa kupata watoto na hususani watoto wa kiume ilikuwa kila anapozaliwa mtoto wa kiume anakufa katika hatua za utotoni jambo lililokuwa likimuhuzunisha na hatimaye mkewe naye alifariki Mzee Sekivunga yaani Athuman Kamote alioa mke mwingine kutoka maeneo ya kwemahuza ambako zamani kulikuwa na mji na mwanamke huyo pia alikuwa akizaa watoto na walikuwa wakifariki katika utoto wao  siku moja alipokuwa akitoka safari aliambiwa kuwa mkewe amejifungua mtoto wa kiume na alipoulizia alijua kuwa naye atakufa tu na aliuliza leo siku gani wenzake walimwambia ijumaa hivyo akasema Mtoto huyu ataitwa Jumaa kwa bahati nzuri Jumaa alikua lakini akiwa katika umri wa utoto mama yake mzazi alifariki, Mzee Athumani Kamote Sekivunga alioa mke mwingine ambaye alimlea Jumaa mpaka alipokuwa kijana wa makamo, mama huyo alifariki mapema na hivyo Sekivunga kubakia na watoto wawili Kivunga na Jumaa, Kivunga aliolewa huko Mkuzi katika kijiji kijulikanacho kama KWASEMWAIKO na kuzaa wana wa kiume na wakike, hivyo huko wako jamaa zetu wengi waliozaliana na kupotelea huko, Kivunga alifariki mwaka 1985 na kuzikwa Mzambarauni kwa Semmea huko bonde Kicheba. Kutokana na kuhama kwa Semmea na Sekivunga kuja Bonde Mlingoti jina la zamani la kijiji hicho katika maeneo haya ya mlingoti wamishionari walifungua kanisa na shule ambayo vijana wengi walipata elimu.

ASILI YA JINA MLINGOTI
Kutokana na maelezo niliyoyapata kutoka kwa mzee Samuel Jumaa Kamote ni kuwa Nyakati za nyuma kidogo Waingereza walipotawala walipenda kuwatumia viongozi wa kiafrika waliokuwa na ushawishi katika jamii kuwa majumbe Mazumbe ili kuwatawala wanachi katika njia isiyo ya moja kwa moja “Indirect rule” Zumbe wa wabondei aliyekuweko mlingoti aliitwa SEKIKWAUTO huyo ndiye Jumbe au Zumbe aliyetawala bonde ya Kicheba au Mlingoti. Asili ya jina MLINGOTI ilitokana na Mlingoti wa bendera uliosimamishwa na wakoloni wa Kiingereza na kutokana na mazumbe kuwa walikuwa ni waamuzi wa maswala mbalimbali ya kiamii wengi walitamka kuwa wanakwenda huko mlingotini na jina Mlingoti likastawi hata leo, Kwa hiyo mlingoti ilikuwa ni  nguzo ya kusimamishia bendera na hivyo wabondei waliokuwa wakielekea huko wakiulizwa Waita kuhi? Yaani unaenda wapi walijibu Kwe - Mwingoti yaani huko kwenye mlingoti yaani akaako zumbe na hivyo eneo hilo katika mji wa Kicheba huitwa Mlingoti hata leo. aidha katika maumbile ya mji wa Kicheba mlingoti ni juu na kicheba ni mlimani na kwa lugha ya kibondei mtu alipokuwa anapandisha juu husema Naita Kenya Yaani naenda huko juu, watoto wa kizazi kipya wakaita Nairobi na hivyo mazingira ya kijiji cha Mlingoti yana mtaa uitwao Nairobi hata leo.
Kumbuka kuwa wakati wa Utawala wa Waingereza sultani alipewa kutawala ukanda wa Pwani kwa kilomita zisizozidi 45 hivi kwa hiyo maeneo mengi ya Muheza na vijiji vyake yaliangukia chini ya utawala wa sultani, Kwa mujibu wa maelezo ya wazee wetu Muheza ilikuwa na Jumbe au Zumbe Mkuu wa wabondei aliyekuwa anaitwa "ASHARAFU" ambaye alikuwa anaishi Muheza mjini, Kwa kawaida kulikuwa na Majumbe wengi au Mazumbe wengi Lakini zumbe mkuu alikuwa ASHARAFU, Aliyeishi Muheza mjini, na kuanzia mwaka 1959 Baada yake wabondei walimteua  na kumtawaza Erasto Mang'enya kuwa chifu wa wabondei, Erasto Mangenya alichaguliwa na Mazumbe wote kuwa chifu wa Kwanza na wa mwisho wa Wabondei.

ASILI YA JINA KICHEBA.
Moja ya Kijiji maarufu sana ambao ukoo wa Kamote wametokea kinaitwa Kicheba kijiji hiki ni cha zamani sana na mwanzoni kiliitwa mlingoti ikiwa ni maeneo ya shamba la mkonge la Kibaranga,na Mlingoti wakoloni walifikisha umeme mapema sana, Baada ya azimio la kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa mlingoti ilichaguliwa kuwa moja ya kijiji cha ujamaa, Jina kicheba likawa ndio jina la kijiji hiki, jina hili lilitokana na ndege mdogo ambaye alikuwa maarufu sana kwa kula ndizi kwa kuwa Semmea alikuwa na shamba kubwa sana la ndizi ambazo wakati mwingine zilikuwa zinaivia juu ndege wadogo aina ya mtongo walitua na kutafuta kwa kudonoa Ndizi na mzee Semmea akawa anaviita vijidege hivyo vicheba, na kikiwa kimoja ni Kicheba kwa hiyo jina Kicheba linatokana na ndege mdogo aitwae kicheba jina lililotokana na mzee Semmea alipokuwa akiulizwa na watoto wake ni ndege gani wanadonoa ndizi zake alisema ni Kicheba hii ndio asili ya jina Kicheba ambacho ni kijiji maarufu sana na kikubwa kuliko Misozwe.

Kijiji cha kicheba kilikuwa na umaarufu mkubwa kutokana na kuwa katikati ya mashamba mawili ya mkonge, likiwemo shamba la mlingoti na kibaranga, mji huu baadaye ulikuwa mji mkubwa wa kibiashara ukiwa na mchanganyiko wa watu wengi na jamii nyingi wakiwemo watu kutoka Sehemu Mbalimbali  za ndani na nje ya nchi mfano wa miongoni mwa watu waliokuja kicheba wakiletwa na Serikali ya wakoloni wa kijerumani kama manamba ili kukata mkonge ni pamoja na WARUNDI, WANYARWANDA kutoka Rwanda, WAMAWIA au WAMAKONDE kutoka Msumbiji, WANYASA Kutoka Malawi, WABEMBA kutoka Zambia, WAMANYEMA NA WABEMBE Kutoka Kongo, aidha kutoka hapa nchini ni pamoja na makabila ya WAHA, WANYAMWEZI, WABENA, WAYAO, WAPANGWA,WAMAKUA,WASUKUMA, WAMWERA, WAFIPA,WANYAMWANGA,WAHEHE
na Kadhalika waliokuja kukata mkonge na pia kujichangana na jamii ya wakazi wa mji huu, WABONDEI waliwaita watu hao WANYIKA kwa jina la ujumla wakimaanisha yaani watu kutoka BARA.

Kutokana na kijiji hiki kuwa kitovu kikubwa sana cha biashara, watu kutoka Arabuni yaani waarabu wengi sana walijongea na kuishi katika kijiji hiki wakifanya Biashara na kufungua maduka ya biashara mbalimbali, mzunguko wa fedha na biashara uliokuweko uliwawezesha baadhi ya waarabu waliokaa kicheba kuweza kufikia hatua ya kununua mabasi, Waarabu waliotajirikia, kicheba ni pamoja na wamiliki wa mabasi ya RAHALEO,  SHENGENA, na SATELITE ambayo wamiliki wa mabasi hayo wako hata leo, kutokana na kuweko kwa waarabu wengi katika kijiji cha kicheba mjii huu ulipata umaarufu mkubwa na kuitwa "MUSCUT" kwa jina la utani kwa sababu waarabu wengi kutoka maeneo mengine walikuwa wakifariki wanakuja kuzikwa Kicheba kwa jamaa zao.

Ndege ajulikanaye kwa Jina La Kicheba kama anayoonekana pichani
 
Historia ya Mzee Andrea Jumaa Kamote.

Mzee Andrea Jumaa Kamote alizaliwa Mwaka 1924 Katika kijiji cha Mlingoti Kicheba wilayani Muheza mkoa wa Tanga, alisoma shule ya Msingi ya Mtakatifu Barnaba. Mlingoti wakati huo ikijulikana kama KWEMNKONGOO alipohitimu Darasa la nne mwaka 1935 alijiunga na shule ya kati Mwaka 1936 huko St Martin Hemvumo Magila na kuhitimu Darasa la sita mwaka 1937. Alifaulu vizuri masomo yake katika shule ya kati Mwaka 1937 lakini kwa bahati mbaya Mzazi wake Marehemu mzee Athumani Kamote "Sekivunga" alishindwa kumuendeleza kwa kumlipia ada ya shlingi Mbili 2 na sent 50 ili aendelee na Masomo ya sekondari huko Minaki.

Hata hivyo kutokana na kiwango cha Elimu alichokuwa nacho aliajiriwa na shirika la Posta na simu kama Telephone Operator pale Ngomeni kati ya mwaka 1938-1942, Mwaka 1943 alijiunga na kazi ya ukarani wa mahesabu katika mashamba ya mkonge alikotumia kwa miaka 50 hadi alipostaafu mwaka 1993, Alifunga ndoa na Mama Agnes Chonge Mwaka 1944 Bibi Huyu alifariki mwaka 2007 Deceber 30th  Mpaka anafariki mzee huyu ambaye makala hii  kimeandikwa kwa Heshima yake alijaliwa kupata watoto nane ambao wawili walifariki kabla yake, jumla ya watoto wa kiume ni sita na wawili wa kike, wajukuu walikuwa jumla ya 34 na vilembwe 25 na vitukuu 2 Mzee Kamote alifariki kwa Mshituko wa Moyo (stroke) na Maralia kali usiku wa kuamkia tarehe 18 November na kukimbizwa Hospitali teule Muheza ambako alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi hadi alipofariki dunia  asubuhi 24 November 2009.Ttulimzika mzee huyu katika shamba lake huko Tongedigwa tarehe 26 November 2009 saa tisa alasiri, jumla ya miaka ya uhai wake ni miaka 85 Mazishi yake yalihudhuriwa na mkuu wa Wilaya ya Muheza Mathew Nasei ambaye pia alikuwa akimtembelea Hospitalini Teule Muheza na Katibu Tawala wilaya ya Muheza Bwana Paulo Moshi na DC Samuel Kamote Mwanae akiwa mkuu wa wilaya Bukoba wakati huo.

Mzee Andrea  alikuwa mtu makini mchapa kazi, Mvumilivu  na mtu asiyekata tamaa mwenye uwezo wa kufanya mambo kutokea na mwenye maono na ndoto za mbalimbali, wakati wa uhai wake alionekana kuwa mtu makini mwenye akili na elimu aliyokuwa nayo aliitumia kwa faida, alitembea kwa miguu kuelekea kazni kila siku na kurudi kwa miguu kutoka Kicheba hadi Muheza alikokuwa akifanya kazi, pamoja na hayo alikuwa mchumi mzuri na mwenye kujua Biashara hakuacha kuuza Papa, kukusanya makuti na kusuka viungo na kuna wakati alikua anakwenda kukusanya sufi kwenye shamba lake huko Tongedigwa, na kuuza sufi, aidha alikuwa na shamba la mikorosho, minazi na viwanja, alipenda kujadili maswala ya siasa na Neno la Mungu, alikuwa anasoma sana Biblia na kufanya maombi kila siku asubuhi na usiku anapokwenda kulala au anapoamka, alifuatilia habari katika redio na televisheni pia vipindi vya dini, na alikuwa msomaji mzuri wa Magazeti, alikuwa mpigania haki, hakupenda uonevu, aliwapenda watoto wake na wajukuu wake alikuwa na upendo wa kweli kwa marafiki na ndugu na jamaa, aliweza kuwatembelea watu kokote waliko na kujua shughuli za maendeleo, alichukizwa na tabia mbaya ikiwa ni pamoja na wizi, maisha yake yote alikuwa ni muhudumu mwema wa kanisa akihudumu madhabahuni na kutunza sadaka za kanisa ni washirika waamiifu wa kanisa la mlingoti, aidha alipotembelea watu kokote hakuacha kusali na kuomba kwa kuhudhuria Ibada alikuwa muanglikana kweli kweli mweye uwezo wa kuitetea imani na kuhoji maswala ya imani, ndoto zake zilikuwa ni kuona wau wanapata maendeleo, alikuwa tayari kuwajibika kutoa msaada hata pale inapotokea wengine wameshindwa kutoa msaada, Mzee Andrew alikuwa mfuasi mzuri sana wa siasa na utendaji wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kutokana na upenzi wake huu wa siasa si ajabu kuona watoto wake na wajukuu, wakitumika katika serikalia na vyama vya siasa Kamote aliacha watoto wake wakiwa watawala, wanasheria, Askari, Mafundi, wahandisi na watumishi wa Mungu,

Historia ya Agness Chonge Kamote.
Agness Chonge Kamote alizaliwa mwaka 1925 katika kitongoji cha Miembeni/Kicheba, alifunga ndoa ya kimila na Mzee Andrea Kamote mwaka 1943 na hatimaye ndoa ya kikristo mwaka 1953 alijaliwa kupata watoto nane  wakiume 6 na wakike wawili, mtoto wa kwanza alizaliwa mwaka 1945 na wa mwisho 1967 watoto wawili walitangulia mbele za haki wakati Chonge mkuu akiwa hai, Naye aliugua Ghafla jumamosi 29 December 2007 na asubuhi alikimbizwa Hospitali teule ya Muheza ambako  alilazwa kaika wodi ya wagonjwa mahututi na jumapili 30th 2007 saa 6;30 Mchana alifariki Dunia wakati anafariki aliacha wajukuu 36, vilembwe 21 na kitukuu 1, Mazishi yake yalihudhuriwa na wakuu wa Wilaya za Pangani wakati huo DC. ZIPORA PANGANI, Mkinga DC. KINAWIRO, Muheza ZAINAB KONDO na Katibu tawala wilaya ya Muheza Ndugu Paulo Moshi, pia Chonge mkuu alizikwa na DC. Samuel Kamote mwanae akiwa mkuu wa wilaya Ilemela, Chonge mkuu alizikwa huko miembeni Kicheba Muheza jumla ya miaka ya uhai wake ni 82.

Chonge alikuwa ni mwanamke Jasiri mwenya kujiamini na mchapa kazi ingawa hakubahatika kupata elimu lakini alisisitiza watoto wake kusoma na alichukizwa pale walipoonyesha kutoroka shuleni au kuharibu mambo huko shuleni, alijikita katika swala la kilimo jambo ambalo mwenyewe alikuwa akisisitiza kuwa ndilo alilorithishwa na Baba yake, alijituma katika kilimo na wakati wa uhai wake alihakikisha analima mahindi, mihogo, na hata matunda na mengineyo, alikuwa ni mwanamke mwenye kuamka asubuhi na mapema na kuelekea shambani kwake huko kwapisholi, na kwa mahuza na tongedigwa, mara chache alilazimka kutembelea mijini kwa watoto wake lakini akiisha kutimiza majukumu yake hakuwa mwenye kupendelea kukaa kwa watu bila kujishughulisha na wakati wote aliwaza mashamba yake, katika maisha yake hakupenda kuonewa wala kupenda uonevu, alichukia maswala ya utoaji mimba alipendelea Ibada, aliheshimu watu, alikuwa mlezi mwema na mwenye kuwapenda watoto wake na wajukuu wake, alikuwa ni mtu mwenye kuridhika na kukumbuka fadhila, mwingi wa shukurani, alitunza nguo mpya alizopewa na alijua ni wakati gani wa kuzivaa, ingawa kwaajili ya shamba alipendelea kaniki, kwa umjula alikuwa anapendela kufuga kuku na ilikuwa vigumu katika uwepo wake kulala na njaa hata pale ambapo babu angekuwa hana hela, alipenda usafi na kuhakikisha kuwa familia inapata maji safi ya kunywa na kuoga na wakati maji yakiwa yanapatikana mbali alihakikisha anajihimu kwenda kuchota, mpaka anafariki alikuwa bado ni mchapa kazi na alikuwa akimsaidia mjukuu wake kuvuna mahindi ni mwanamke shujaa ambaye ni mfano wa kuigwa kwa mwandishi wa kijitabu hiki ni wazi kuwa nimefaidika na malezi ya Bibi huyu kwa zaidi ya miaka miwili 1984 – 1986 tulipokuwa tumefiwa na mama yetu na mzee wetu Samuel Kamote kwenda Ujerumani kwa masomo tulikaa na bibi huyu na kufaidika sana .
 
Samuel Jumaa Kamote ni nani?

Kutokana na maelezo marefu yaliyotangulia bila shaka sasa utakuwa umepata Picha ya chimbuko la Samuel Jumaa Kamote ambaye ninataka kumuelezea sasa Habari zake imenilazimau kuanzia mbali ili kutunza kumbukumbu zote muhimu na nili kwama uweze kufaidika na Historia hii ya kipakee na yenye kusisimua.

Samuel Jumaa Kamote ni Mzaliwa wa Kijiji cha Kicheba, wilayani Muheza Mkoani Tanga,  Ni moja ya viongozi maarufu sana Nchini, ambaye ameitumikia nchi hii na taifa hili katika Nyadhifa mbalimbali za chama na serikali, anajulikana sana kama mtu Mchapa kazi, mwaminifu, mwadilifu, mpenda watu, mcheshi, mvumilivu ambaye hana kashifa ya Ufisadi wala Rushwa, njia ya kidiplomasia ilikuwa ni kanuni yake muhimu katika kuamua na kuhitimisha migogoro katika jamii.

 Pichani ni Jengo la zamani sana ambalo ni Ofisi ya CCM katika kijiji cha Kicheba


Samuel Jumaa Kamote alizaliwa tarehe 3th July 1949. akijulikana kijijini Kicheba Kama Hamza Jumaa Kamote, Baba yake alijulikana kama Jumaa Athumani Kamote na Babu yake ni Mzee Athumani Kamote Maarufu kama Sekivunga. Jina la Samuel lilipatikana baada ya Kubatizwa kwa familia yao na kuamua kuwa wakristo wa Kanisa la Anglikana, Imani hii ilitokana na Mzee Jumaa Kamote aliyesoma huko Magila Kuamua kuwa Mkristo na kubatizwa akiwa na Jina la Andrew Kamote, na hivyo watoto wake waliozaliwa wakati huo Zaina kuitwa Marry na Hamza kuitwa Samuel, Mwanaidi aliyebatizwa kuwa  Herrieth na Jumanne aliyebatizwa kuwa Dismas, Samuel Jumaa Kamote alikulia katika malezi ya kawaida na alikuwa akienda shuleni bila viatu kwa wakati huo. Samuel alianza kuvaa viatu baada ya kufaulu kwenda shule ya Sekondari Minaki, alijulikana pia kama kijana mpole na mwenye upendo na huruma na hakupenda Ugomvi kabisa.
 Pichani Kutoka Kushoto aliyeketi ni Dismas Jumaa Kamote, (Mratibu wa Elimu Magila Mstaafu), Julius Jumaa Kamote (Engineer), Samuel Jumaa Kamote aliyesimama, Peter Jumaa Kamote Mezani Picha hii ilipigwa mwaka 1963, (Zaina Marry) na (Mwanaidi Herrieth) hawakuweko pichani na Frank Jumaa Kamote alikuwa hajazaliwa

Jumla ya watoto wa Mzee Andrew Jumaa Kamote kwa kufuatia kuzaliwa kwao ni jumla ya watoto nane huku wa kike wakiwa ni wawili tu, watoto hao wa mzee Andrew Jumaa Kamote ni pamoja na  Marry Kamote, Samuel Kamote, Herrieth Kamote, Dismas Kamote, Julius Kamote, Jacob Kamote, Peter Kamote na Frank Kamote.

Samuel Jumaa Kamote: -Alijiunga na shule ya Msingi Mlingoti mwaka January 1956 na kumaliza darasa la nne mwaka 1960, Samuel Jumaa Kamote alifaulu masomo yake ya darasa la nne na kujiunga na shule ya kati St. Martin iliyoko Magila Msalabani 1961-1964 shule za kati zilihusisha Darasa la 5-8, wakati huo Magila pakijulikana sana kama Hemvumo ambapo alihitimu darasa la Nane na kuchaguliwa kwenda shule ya Sekondari ya Minaki  1965-1968 wakati huo ikijulikana kama St Andrew Huko Dar es Salaam. Maeneo ya Kisarawe siku hizi Pwani. na kuhitimu Darasa la 12.

Kanisa la Anglikana lililoko Magila Msalabani, Muheza mkoani Tanga, Hapa ndipo waliposomea Mzee Andrea Kamote na Samuel Kamote na Kupata Elimu ya upili au shule ya kati kwa wakati huo

Shule ya Sekondari Minaki kama unavyoweza kuiona kwa sasa zamani ST. Andrew


Samuel Jumaa Kamote alihitimu masomo yake Katika sekondari ya Minaki, iliyokuwa Kisarawe Dar es salaam wakati huo ikijulikana kama ST Andrew,  na alifaulu  kwa kiwango cha juu sana na kupokea Cheti cha kuhitimu Masomo hayo Kutoka Uingereza kwa wakati huo, Kutokana na umahiri wake katika elimu alipendekezwa kuwa Mwalimu na hivyo kuchaguliwa moja kwa moja kujiunga na chuo cha ualimu  Marangu mwaka 1969-1970 Na kuhitimu mafunzo ya Ualimu Daraja "A" wakati huo CSE. Samuel Jumaa Kamote alijiunga na kupata Mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa sheria Mwezi October 1969-1970 Katika kambi mbalimbali zikiwemo Kambi za Mafinga, mkoani Iringa kwa wakati huo na Oljoro  iliyoko Arusha,

Samuel Jumaa Kamote alianza Kazi ya Ualimu December Mosi 1970 Katika shule ya Msingi Mwambao Iliyoko Pwani Bagamoyo mjini, Kamote alifundisha shule zipatazo nne wilayani Bagamoyo, Baada ya Mwambao mwaka 1970 ambayo iko Bagamoyo mjini, alihamishiwa shule ya Msingi Mapinga mwaka 1972 na baada ya Mapinga alihamishiwa Fukayosi 1973 na baada ya Fukayosi alihamishiwa  Kikaro/Miono 1976  Zote za wilayani Bagamoyo na kurudishwa tena Mwambao 1978 Mjini Bagamoyo na badaye kupandishwa cheo na kuwa afisa elimu vifaa na takwimu wilayani Rufiji 1979.na Baada ya hapo kuwa mwalimu wa Siasa.

Samuel Jumaa kamote alioa mke wake wa kwanza mnamo tarehe 2 mwezi April 1972 na kumpata mke wake mpendwa Margareth Sengwaji ambaye alikuwa mwalimu mahiri wa kiingereza na maswala ya Sayansi kimu wakati huo, Yeye pia  Margareth kutokana na umahiri wake amewahi kuwa mwalimu mkuu katika shule mbalimbali za msingi hapa nchini Margareth Sengwaji alifariki mwaka 1984 tarahe 19 mwezi wa July  katika Hospitali ya Sokoine mjini Lindi baada ya kufanyiwa Upasuaji wa kidole tumbo na baadaye upasuaji huo kusababisha kifo cha Margareth Sengwaji, Mama Margareth Sengwaji alifariki akiwa ameacha watoto wanne ambao wakiume waili na wakike ni wawili, watoto wa Marehemu Margareth ni kama Ifuatavyo Francis Mwangoto Mwehuti Zumbe Kamote, Rev. Innocent Mkombozi Kamote  mwandishi wa makala hii (Mkuu wa wajenzi mwenye hekima). Rosefaith Joyce Kamote na wa mwisho ni Lilian Chonge Kamote.


Samuel Jumaa Kamote na Margareth Mourice Sengwaji katika Harusi yao Apil 2 1972.

Baada ya kumaliza Masomo yake alichaguliwa kuwa Mwalimu wa shule ya msingi Mwambao iliyoko Bagamoyo Pwani ambapo pia alikuwa mwalimu mkuu, December 1 1970 baadaye alihamishiwa Fukayosi huko Pwani, akiwa mwalimu mkuu na kurejea Bagamoyo akiwa mwalimu mkuu katika shule Mwambao na kupandishwa cheo kama Afisa elimu vifaa na tawkimu wilaya.

Samuel Jumaa Kamote akiwa na Mkewe Margareth Sengwaji, na wanawe wakubwa wa kiume Francis Mwangoto Kamote na Innocent Samuel Kamote aliyepakatwa ilikuwa December 25 1976.


Mwalimu Margareth Mourice Sengwaji Mke wa Mzee Samuel Jumaa Kamote akiwa na wanawe wote aliobahatika kuwazaa, Mkubwa wa Kiume ni Francis Mwangoto mwehuti Kamote (Zumbe) anafuatiwa na Innocent Mkombozi Kamote (Mkuu wa Wajenzi Mwenye Hekima) kisha Rosefaith Msekwa Kamote (Mwalimu) na aliyepakatwa ni Lilian Chonge Kamote (Mwalimu).Picha hii ilipigwa mwaka 1983mwaka mmoja kabla ya kifo cha Mwalimu Margareth Sengwaji.

Baadaye alipandishwa cheo na alikuwa Afisa Elimu vifaa na Takwimu 1979 katika wilaya ya Rufiji. na kutokana na ushawishi wa chama kimoja kilichokuwa kikitawala wakati huo  Mzee Samuel Kamote alichaguliwa na Chama cha Mapinduzi kuwa mwalimu wa siasa na kuanza kazi ya kufundisha siasa katika maeneo mbalimbali akikitumikia chama cha Mapinduzi 1980, pia alihamishiwa katika kisiwa cha Mafia 1982 akiwa Mwalimu wa siasa, alifanya kazi hiyo na baadaye kwenda Chuo kikuu cha Chama Kivukoni na kusomea Siasa uongozi na itikadi, Samuel Jumaa Kamote alihamia Liwale 1983 na baadaye Lindi mjini 1983-1984 akiwa Katibu wa CCM msaidizi mkoa wa LINDI, kote huko akiwa katibu mtendaji mwandamizi wa Chama cha Mapinduzi na kada mahiri aliyebobea katika fani ya siasa, kwa mujibu wa maelezo ya kina alipelekwa Liwale na aliyekuwa katibu wa chama wakati huo Mzee Rashid Mfaume Kawawa kwa kusudi la kuimarisha chama wilaya alikozaliwa Mama yake mzee Mfaume Rashid Kawawa. Mpaka anaondola Lindi alikuwa ni Katibu wa chama Msaidizi mkoa.

Samuel Jumaa Kamote katika Ubora wake mnamo miaka ya  1985

1984 -1985 Kamote alichaguliwa kuwa miongoni mwa Makada wa chama waliopelekwa Ujerumani Mashariki wakati huo kwaajili ya kujifunza maswala kadhaa ya kiitikadi Katika chama cha mapinduzi, yaani (KOZI YA SIASA) akiwa nchini Ujerumani Mashariki walitembelea miji mbalimbali  ikiwa ni pamoja na kuonyeshwa mahali alipozaliwa mwanzilishi wa Kanisa ka Kiluetheri Martn Luther Kijiji hicho kinaitwa "EICELEBEN" na pia walipata nafasi ya kwenda Urusi kwa ziara ya kimafunzo, Samuel Kamote alirejea Nchini na kuhamishiwa Ofisi ya  CCM mkoa wa Tanga  1986-1990 Akiwa Katibu Msaidizi wa CCM mkoa, alihamishiwa kijiji cha Ujamaa Magamba Kwalukonge, wilayani Korogwe na kuwa Katibu wa wilaya ndogo za Chama au makada wa kusukuma maendeleo wakati huo wakijulikana kama makada wa CCM, 1991-1992 alirudishwa Tanga mjini akiwa kama Katibu wa Chama wilaya ya Tanga, Mzee Samuel Kamote Msaidizi wakati huo wakuu wa wilaya walikuwa pia ni makatibu wa chama, chama kilipojitenga na serikali baada ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi Samuel Kamote akawa katibu wa wilaya ya Tanga wa chama cha mapinduzi CCM kutoka 1992-1996 na Dodoma mjini, Baada ya Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi 1995 ambapo Mkapa alipita na Mwapachu kama Mbunge wa Tanga mjini Samuel Kamote alihamishiwa Dodoma akiwa katibu wa Chama na mwaka huo huo alichaguliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro huko Arusha kwa sasa Manyara, Samuel Kamote alikaa Simanjiro kwa 1997-2002 alipohamia Wilaya ya Mvomero mpaka wakati wa Uchaguzi mkuu uliomuingiza Kikwete Madarakani 2002-2006 alihamishiwa Mvomero na kwenda wilaya ya Ilemela Mwanza, 2006-2009,  Baadaye alihamishiwa wilaya ya Bukoba mjini 2010 -2012 ambako ndiko alikomalizia mkataba wake kama mkuu wa wilaya, na Kustaafu. Samuel Kamote alistaafu ukuu wa wilaya mwaka 2012 akiwa na umri wa miaka 63, huku akionekana mwenye nguvu na bado akiwa anaonekana kijana kuliko hata wanafunzi wake aliowafundisha miaka ya 1970.Jumla ya miaka yake ya utumishi katika chama na serikali ni miaka 42

Samuel Jumaa Kamote Katika matukio Mbalimbali katika Picha

 Samuel Jumaa Kamote akiwa Ujerumani 1984

 Samuel Jumaa Kamote akiwa Nchini Urusi 1985


 Samuel  Jumaa Kamote Nchini Urusi wakati wa baridi
 Samuel Jumaa Kamote Nchini Urusi
Samuel Jumaa Kamote Mwenye Kamera anayejigusa jicho akiwa na wenzake huko Ujerumani

Samuel Kamote Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanga mjini
Akiwa Katibu mkuu wa wilaya wa chama cha Mapinduzi CCM Samuel Kamote, alifanya kazi zake kwa umahiri ikiwa ni pamoja na kukiimarisha chama cha mapinduzi hususani katika wakati wa mpito kutoka kuelekea mfumo wa  chama kimoja kiutawala na kuelekea katika mfumo wa vyama vingi  vya kisiasa, Mageuzi haya yalifanyika mwaka 1992 ambapo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wakati huo pia alikuwa ndio Katibu mkuu wa Chama, Isdori Shirima alikuwa Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi mkoani Tanga,  Mama Carona Faida Busongo aliwa katibu wa wilaya na mkuu wa wilaya ya Tanga na pia aliyewahi kuwa mbunge wa Tabora mjini, kutokana na mageuzi ya kisiasa Samuel Kamote aliteuliwa kuwa katibu wa CCm wilaya ya Tanga na Kumrithi Mama Busongo, Mafanikio Makubwa aliyoyafanya katika wakati wake ni pamona na ujenzi wa Nyumba mbili za CCM wilaya na Ofisi ya CCM wilaya iliyokuwa ijengwe kwa Ghorofa, Nyumba hizo mbili za Chama zilijengwa eneo la Masiwani mjini Tanga na Kamote akawa Katibu wa CCm wa Kwanza kukaa katika nyumba hizo, mbili moja ilikodishwa kwaajili ya kipato cha chama, Fedha na vifaa vya ujenzi wa nyumba hizo za chama zilichangishwa na wahisani wa CCM Bandari ya Tanga, kupitia tawi lao la CCM sehemu ya kazi, Enzi za mfumo wa chama kimoja cha Siasa, Baada ya Uhamashishaji uliotukuka uliofanywa na  viongozi hao, Lengo lao kubwa likiwa ni pamoja na kujenga Ofisi ya CCM ya Ghorofa ya wilaya ambayo kwa bahati mbaya ujenzi wake umesimama mpaka sasa.Baada ya Kamote Kuhamia eneo Lingine la kazi.


Samuel Jumaa Kamote Pichani akiwa na Mama Corona Faida Busongo aliyekuwa mkuu wa Wilaya na Katibu wa Chama Cha mapinduzi wilayani Tanga kabla ya 1992 wakati wa mageuzi ya mfumo wa Kisiasa,

Kada wa Chama cha mapinduzi Samuel Jumaa Kamote, akimpokea Rais wa awamu ya Pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi alipokuja kufanya ziara na kufungua nyumba za Chama zilizoko masiwani mjini Tanga, aliyejishika Uso  mwenye koto na Kanzunni aliyekuwa mwenyekiti wa Chama mzee Abdulrahiman Magambo Marehemu kwa sasa .
Kada wa Chama cha mapinduzi Samuel Jumaa Kamote akisalimiana na Rais wa awamu ya Tatu Benjamin Willium Mkapa wakatai wa Kampeni mwaka 1995 na aliyekuwa Mgombea Mwenza Dr. Omar Ally Juma (Marehemu kwa sasa). Uchaguzi huu ulimpa Mkapa ushindi wa Kishindo na Tanga ikiongoza kwa kumpa Kura nyingi na Harith Bakari Mwaachu akawa mbunge wa Tanga, wote walikiri kuwa Umahiri wa Samuel Jumaa Kamote katika ufanyaji Kampeni ulikuwa na Mchango mkubwa kwa Chama cha Mapinduzi.

 Samuel Jumaa Kamote akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa baada ya kuteuliwa naye kuwa mkuu wa wilwyw ya Simanjiro mwaka 1997 (Picha kwa hisani ya maktaba ya Rev. Innocent Kamote Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima)

Samuel Kamote Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro

Samuel Jumaa Kamote alianza kupata umaarufu mkubwa na kutajwa sana katika vyombo vya habari alipoteuliwa na rais Benjamin Mkapa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, wakati huo ikiwa mkoani Arusha na mkuu wa mkoa huo alikuwa Muheshimiwa Daniel Ole Njolay, Wilaya hii ndio ilikuwa wilaya yake ya kwanza kuiongoza Kamote alifanya kazi mbalimbali kwa umariri akitumia busara na diplomasia katika uongozi wake hivyo kuweza kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zinaikabili wilaya hiyo kubwa na yenye utajiri mkubwa wilaya ya Simanjiro ilikuwa na changamoto za Fujo na uhalifu katika eneo la Mererani kutokana na kuweko kwa watu wa tamaduni mbali mbali walioko kwenye migodi ya Tanzanite, aidha wilaya hii ilikuwa pia inakabiliwa na tatizo la miundo mbinu mibaya , uhaba wa maji na mapigano ya wafugaji na wakulima, migogoro ya ardhi ukosefu wa maji, elimu duni, na mimba za utotoni pamoja na ukeketaji kutokana na wakazi wengi wa Simanjiro kutoka katika jamii ya wamasai, Kamote alichangia kwa kiwango kikubwa uanzishwaji wa Hospitali ya Wilaya, shule ya sekondari ya Simanjiro na utatuzi wa migogoro ya aina mbalimbali pamoja na kuimarisha kazi za Ulinzi na Usalama


Samuel Kamote Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro akifungua Mafunzo ya Mgambo wilayani humo kwa kusudi la kuimarisha Ulinzi na Usalama wilayani humo Hapo akilenga shabaha kwa kutumia silaha aina ya SGM

Samuel Jumaa Kamote Mkuu wa wilaya ya Mvomero

Kamote akiwa mkuu wa wilaya ya Mvomero, iliyoko Morogoro aliendelea kufanya kazi yake kwa bidii na uangalifu mkubwa pia akitumia busara, Wilaya ya Mvomero ni moja ya wilaya ambazo licha ya kuwa na ardhi yenye Rutuba pia inakabiliwa na changamoto za migogoro ya ardhi swala kubwa likiwa ni swala la wakulima na wafugaji, Kamote alimudu kupambana na changamoto hizo, kutokana na umahiri wake wa kuwahi punde inapotokea Migogoro na kwa njia ya mazungumzo aliweza kuitatua Migogoro hiyo katika kipindi chake, Aidha mgogoro mwingine unaojitokeza katika wilaya hii ni kuwepo kwa migomo na kuibuka kwa migogoro ya wafanyakazi wa kiwanda cha sukari na uongozi wao, au swala la wamiliki wa mashamba ya miwa kuto kuto kulipwa stahiki zao aina yote hiyo ya Migogoro Samuel Jumaa kamote aliweza kukabiliana nayo, huku akishirikiana na viongozi wengine wa wilaya hiyo wakiwemo wabunge waliokuweko wakati huo akiwemo Amosi Makala. Jambo kubwa ambalo Muheshimiwa Samuel Kamote atakumbukwa kuwa walilisimamia na likatimia katika wakati wake ni Ujenzi wa Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Mvomero, wakati Kamote akikabidhiwa wilaya hii Ofisi za wilaya hii zilikuwa Morogoro mjini kwa Muda, Mzee Kamote aliweza kusimamia upatikanaji wa Mahali ambapo wenyeji walipendekeza Ofisi ijengwe na makao hayo makuu ya Ofisi yalijengwa
katika kujihusisha na maisha ya mtu mmmoja mmoja na kuwahurumia alijihusisha na kuona numuhimu wa kutunza mahali alipofia waziri mkuu Edward Moringe Sokoine amapo pao katika wilaya ya Mvomero, Mzee Mpandacho aliyekuwa mlinzi wa mnara wa mahali alipofia sokoine anamkumbuka kamote kama mtu aliyeonyesha kumjali na kumuahidi kupata kazi ya ulinzi katika ofisi yake lakini alipohamia mwanza "Dili likaharibika" anaeleza mzee Hamis Mpandacho


Pichani Mzee HAMISI MPANDACHALO aliyejitolea kulinda Mnara wa Sokoine bila Kujaliwa na mtu Samuel Kamote aliahidi kumpa kazi ya ulinzi Makao makuu ya wilaya ya Mvomero, na alipohamishiwa Mwanza Mzee huyu kwake ilikuwa ni Mkosi, Moyo wa kujali mtu mmoja mmoja huruma na kutia moyo ni moja ya tabia za Samuel Jumaa Kamote.

Mzee Samuel Jumaa Kamote akimpokea Waziri Kagasheki Mjini Bukoba kwa furaha Kamote ni Mtu wa watu

Samuel Jumaa Kamote Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mwanza.
Wilaya ya Ilemela mjini Mwanza ni moja ya eneo la tatu kwa Muheshimiwa samuel Jumaa Kamote kulitumikia Taifa hili, Mapema tu mara baada ya Uchaguzi mkuu, Rais Kikwete alifika Mwanza na kukutana na mkuu wa mkoa na wakuu wa wilaya za Mwanza Samuel Kamote akiwemo. Katika mji wa Mwanza mara kwa mara Mzee Kamote alipata nafasi ya kukaimu Ukuu wa Mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa Eng. Dr, James Msekela, shughuli nyingi sana za maendeleo zilifanyika mjini mwanza, ikiwa ni pamoja na ufunguzi wa Mabenki,shughuli za sikuukuu za wakulima kikanda na matukio mengine mengi ya Maendeleo, Mzee Kamote alifanya kazi bega kwa bega na James Nsekela na wakuu wa wilaya nyingine kwa ufanisi mkubwa sana

Mkuu wa wilaya ya Ilemela wakati huo Samuel Jumaa Kamote akipokea Msaada wa Vitabu kwaajili ya shule ya Sekondari Mojawapo mjini Mwanza zawadi iliyotolewa na Kampuni ya Vodacom Ilemela mwanza.
Kiongozi wa Kampuni ya vodacom akichezesha bahati nasibu kuchagua shule itakayoshinda ili kupatiwa zawadi ya vitabu Huku mkuu wa wilaya ya Ilemela Samuel Kamote akifuatilia kwa ukaribu

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wakati huo Injinia Dr. James Nsekela akiwa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela mjini Mwanza Samuel Jumaa Kamote wakipata Futari pamoja na viongozi wa dini ya Kiislamu mjini Mwanza

Samuel Kamote akiwa Ilemela pia alijishughulisha na uhamasishaji wa michezo, akiwa amepaniku kukuza michezo na akiwa mlezi wa timu ya Ngumi ya mkoani humo, jambo lililopelekea mafanikio makubwa na wanandondi hao Pamoja na mlezi wao kupata nafasi ya kutembelea Kisiwa cha Madagasca.

Samuel Jumaa Kamote Mkuu wa wialaya Bukoba.
Wilaya ya Bukoba  ina Halmashauri mbili Halmashauri ya Manisapaa ya Bukoba na  Halmashauri ya wilaya ya Bukoba, Akiwa Mkuu wa wilaya Bukoba, Samuel Jumaa Kamote alifanya kazi nyingi, ikiwemo utatuaji wa Migogoro ya kidini, huku malengo yake makubwa yakiwa ni kuinua tena Historia ya Elimu ambayo watu wa kagera walikuwa nayo katika miaka ya nyuma na kuitwa  "Ishomile" Kamote anasema katika miaka ya hivi karibuni morali ya kusoma kama zamani imeshuka mkoani humo na Lengo lake ilikuwa ni kuhamasisha maendeleo na kuhakikisha kuwa watu wa Bukoba wanajituma tena kwa bidii ili kuinua Heshima yao, aidha kama ilivyokuwa kwa Ilemela mara kadhaa alipata nafasi ya kukaimu Ukuu wa Mkoa mara nyingi wakati huo Mkuu wa Mkoa huo alikuwa Mohamed Babu na baadaye Fabian Masawe, Kamote akiwa Bukoba kama mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama alifanya kazi ya kuwatia moyo askari waliofanya kazi vizuri na kufanikiwa kukamata wahalfu.

 Kaiumu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Samuel Jumaa Kamote akimkabidhi zawadi ya Laki tano Mkuu wa Upelelezi mkoani Kagera Bwana Peter Matagi kutokana na Kazi nzuri aliyoifanya ya kufanikisha kukamata silaha 8 za kivita. (picha kwa Hisani ya Michuzi Blog)

Kamote pia alipokuwa Kagera aliimarisha uhusiano baina ya serikali na vyombo vya habari, alikuwa ni rafiki wa wanahabari, kwani wanaisaidia serikali katika kuhamasisha uenezi wa maswala ya Maendeleo, tofauti na ilivyo kwa watu wengine huwaona waandishi kuwa kama adui zao kwa Kamote waandishi wa habari walikuwa ni rafiki zake wakubwa kama unavyoweza kuona Pichani chini


Samuel Jumaa Kamote mwenye koti na tai akiwa pamoja na waandishi wa Habari Mjini Bukoba baada ya kufungua semina yao mjini humo Magazeti mbalimbali yaliyandika haya kwa ufupi kuhusu Habari hizi Nanukuu

"WAANDISHI wa habari  Mkoani Kagera wametakiwa kuwa makini katika kuelimisha jamii juu ya rushwa kutokana vitendo hivyo huathiri  zaidi wananchi masikini kwa kushindwa kupata haki zao.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Bw. Samuel Kamote wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya waandishi wa habari wanachama wa Kagera Press Club (KPC) wapatao 34 yanayodhaminiwa na Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) yanayofanyika mjini Bukoba."
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Bukoba mjini Bwana Samuel Kamote, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanal Fabian Massawe Katikati na Balozi Hamis Sued Juma Kagasheki Naibu waziri wizara ya Mambo ya ndani wakati huo wakishiriki katika mazishi ya Nuru Sued Kagasheki Ndugu wa waziri Kagasheki Mjini Bukoba.
Mhe. Samuel Kamote akizungumza Neno wakati wa sherehe iliyoandaliwa na Muheshimiwa Kagasheki kwaajili ya walemavu mjini Bukoba, viongozi mbalimbali wa dini walhudhuria pia katika sherehe hiyo

Meneja wa tawi la Benki ya Posta TPB Makoye Maduhu akitoa taarifa Fupi kuhusu utendaji wa Benki hiyo mbele ya kaimu Mkuu wa mkoa wa Kagera, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Ndugu Samuel Jumaa Kamote Mwenye Koti na tai Mjini Bukoba, wakati wakifungua huduma ya ulipiaji bili za maji kwa njia ya Benki hiyo mjini humo.

 Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bwana Samuel Jumaa Kamote, akiongea na waandishi wa habari hawako Pichani akitoa agizo la kufungwa kwa chuo kilichopo mjini Bukoba kinachodaiwa kuwa tawi la chuo cha Victoria Institute of Tourism and Hotel management kilichoko jijini Mwanza, kwa madai kuwa ni cha kitapeli na hakina vigezo vya kuitwa chuo, Kamote hakutaka ubabaishaji katika swala zima la Utoaji Elimu.
 Thadeo Ryemamu afisa mfuko wa Penisheni kwa watumishi wa umma (PSPF) akimuelezea Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bwana Samuel Jumaa Kamote, Namna mfuko hio unavyonufaisha wastaafu.
 Mtafiti mwandamizi wa taasisi ya zao la kahawa (TACRI) Bwana Malyatabu Ngh'oma Akimwelezea Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bwana Samuel Kamote namna wakulima wanavyoweza kufaidika na zao la kahawa wanayoizalisha, wakati Mku huyo wa wilaya alipotembelea shughuli za sherehe ya wakulima nane nane mjini humo
Mmoja wa watumishi wa taasisi ya utafiti wa zao la kahawa (TACRI)iliyoko katika kituo cha utafiti Maruku akimuonyesha Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bwana Samuel Jumaa Kamote namna kituo hicho kinavyozalisha miche bora ya Kahawa inayostahimili magonjwa alipotembelea  Banda la taasisi hiyo lililipo katika viwanja vya nane nane mjini humo.


Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Samwel Kamote(kushoto)na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Omary Nundu(mwenye miwani kifuani) siku walipotembelea Bandari ya Kemondo,anayetoa maelezo ni Meneja wa bandari hiyo Bwana Minja

Kamote Astaafu 
Baada ya kulitumikia Taifa kwa muda wa Kutosha akiwa na umri wa miaka 63 Samuel Kamote alistaafu, Mzee Samuel Kamote sasa yuko Nyumbani kwake mjini Tanga katia eneo la mwangombe, kutokana na utendaji wake wa kazi na uhodari wake aliagwa kwa furaha kuu na wananchi wa Kagera kama unavyoweza kuona katika picha
Mzee Samuel Jumaa Kamote akiagwa baada ya kustaafu Ukuu wa wilaya mjini Kagera Bukoba akiwana miaka 63,  Mzee huyu amekitumikia chama na serikali kwa ujumla wa miaka 42 amestaafu akiwa na nguvu na anaonekana kuwa bado kija na hata kuliko wanafunzi wake aliowafundisha miaka ya 1970.Kamote sasa anajishughulisha na kilimo na ujasiriamali, huku akiwa ni mshauri mzuri wa maswala ya kisiasa, Aidha baada ya kustaafu kwake Askofu wa kanisa la anglican Dayosisi ya Tanga FatherWilliam Mahimbo Mndolwa wa  alimteua kuwa Makamu mwenyekiti wa Bodi ya shule ya sekondari ya Hegongo Magila, Muheza. Kamote sasa anajishughulisha na maswala mbalimbali ya ujasiriamali mjini Tanga huko Nyumbani kwake Mwangombe njia ya kuelekea Pangani.

Samuel Jumaa Kamote ateuliwa kusaidia Utawala Hospitali Teule wilaya Muheza

Akiwa katika majukumu yake baada ya kustaafu Mzee kamote aliombwa na Askofu mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania Mhashamu baba askofu Maimbo Mndolwa ili kwamba aweze kusaidia kazi za utawala katika Hospitali ya Teule iliyoko Muheza Mkoani Tanga, Mzee kamote alikubali ombi hilo na kuifanya kazi hiyo kwa uaminifu kama  sehemu ya kumtumikia Mungu kwa huduma za jamii, Akiwa katika wakati wa uongozi wake Hospitali hiyo iliweza kutunukiwa tuzo ya utopaji huduma bora za afya ukilinganisha na hospitali nyingine mkoani Tanga


 Pichani Baba Askofu William Maimbo Mndolwa akiibariki tuzo aliyokabidhiwa na serikali kwaajili ya kutambua mchango wa huduma bora za jamii kwa Hospitali teule ya wilaya ya Muheza, Hospital hii ni mali ya kanisa la Abglican Tanzania na huendeshwa kwa ubia na serikali ili kukidhi vigezo vya kihuduma kwa wakazi wa wilaya ya Muheza na sehemu nyinginezo


Pichani Mzee Samuel Jumaa Kamote akiwa ameshikilia tuzo ya huduma bora kwa jamii katika swala la matibabu kwa hospitali ya teule wilayani Muheza, Mzee Kamote ndiye Afisa Tawala wa hospitali hiyo, Kushoto kwake ni Dr. Aubrey Aonga Mganga mkuu wa hospital ya teule wilayani Muheza. Aubrey pia ni Mzee wa Kanisa la Tanzania assemblies of God (TAG) Majani mapana mjini Muheza


Samuel Jumaa Kamote asimikwa kuwa Shemasi wa heshima

Mungu hakawii wala hachelewi, katika namna ya kushangaza Mzee Samuel Jumaa Kamote kumbe ndani yake Mungu ameweka vipawa vya namna mbalimbali, ukiacha maswala ya uongozi, ualimu, siasa, hekima na busara lakini Mungu alioja kuwa ndani yake kuna ukuhani hivyo kupitia Mtumishi wake Mhashabu Baba askofu Maimbo Mndolwa alisimikwa kuwa Shemasi wa Heshima katika  Kanisa la anglican, Ibada hiyo ilifanyika mnamo tarehe 5/5/2019


Pichani Mzee Samuel Kamote baada ya ibada ya kuwekwa wakfu kuwa shemasi wa Heshima iliyofanyika huko Korogwe mnamo tarehe 5/5/2019 na kuongozwa na Askofu mkuu na askofu wa Dayosisi ya Tanga Rev. William Maimbo Mndolwa, Pichani kutoka kushoto Janeth Kayamba, (mjomba wa Mzee Kamote) Mjomba Muhina mkumbukwa (Shemeji wa Mzee Kamote) Rev. Innocent Kamote mwenye suti nyeusi (Mtoto wa pili wa Mzee Kamote na mwandishi wa makala hii), Mzee Kamote mwenyewe na  Mama Esther Mkumbukwa Kamote mke wa Mzee Kamote, wengineo ni ndugu na jamaa waliokuwepo katika kusindikiza tukio hilo lenye kusisimua.


Mzee Samuel Jumaa Kamote, Mkuu wa wilaya Mstaafu tarehe 5/5/2019 alipata neema ya kusimikwa na kutawazwa rasmi kuwa SHEMASI WA HESHIMA, Katika kanisa la Anglican. Katika ibada iliyoongozwa na Askofu mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania Mhasham Maimbo Mndolwa, Ibada hiyo ilifanyika jana tarehe 05/05/2019 katika kanisa St. Michael lililoko Old Korogwe, ambalo ni kanisa la Kiaskofu, Ibada hii ilihudhuria na viongozi mbali mbali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Muheza Hajat Mwanasha Tumbo ambaye alimuwakilisha mkuu wa Mkoa na Tanga ndugu Martin Shigela. Na katibu tawala wilaya ya Korogwe aliyemuawakilisha mkuu wa wilaya ya Korogwe ambaye alikuwepo kanisani lakini aliondoka kwa dharula.
Samuel Jumaa Kamote waliapishwa jana pamoja na mashemasi wengine kadhaa, akiwemo mmoja amnbaye aliapishwa kuwa Kasisi

Kwa mujibu wa Kanisa la Anglican Shemasi ni moja ya ngazi kubwa na ya heshima katika kumtumikia Mungu kama ilivyo kwa uchungaji, Kila kanisa lina taratibu zake kaytika matumizi ya cheo cha shemasi kama inavyofafanuliwa na mkuu wa wajenzi mwenye hekima:-
*Shemasi:*
Neno *shemasi* limetokana na neno la Kiingereza *DEACON* ambalo kwa asili limetokana na neno la kiyunani au kigiriki DEAKONOS *(διάκονος)*, ambalo maana yake ni *Mtumishi* Hawa ni watu wanaochaguliwa na kanisa au uongozi wa kanisa kwa kusudi la kusaidia kazi zinazofanywa na viongozi wakubwa wa kanisa, Shemasi ni Mchungaji mdogo, ni wahudumu wanaofanya kazi za kichungaji, au wenye kuwasaidia wachungaji
Kwa asili neno hili linaanza kuonekana katika Matendo ya *Mitume 6:1-6* ambapo Biblia inasema  “*Hata siku zile wanafunzi walipokuwa wakiongezeka hesabu yao, palikuwa na manung'uniko ya Wayahudi wa Kiyunani juu ya Waebrania kwa sababu wajane wao walisahauliwa katika huduma ya kila siku.  Wale Thenashara wakawaita jamii ya wanafunzi, wakasema, Haipendezi sisi kuliacha neno la Mungu na kuhudumu mezani. Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili;  na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno. Neno hili likapendeza machoni pa mkutano wote; wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, na Prokoro, na Nikanori, na Timoni, na Parmena, na Nikolao mwongofu wa Antiokia; ambao wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao*”
Katika kifungu hicho cha Mistari utaweza kuona wale waliochaguliwa na Mitume katika kanisa ili wawasaidie kazi za kitume ndio baadaye walikuja kuitwa “*MASHEMASI*”
Katika makanisa mashemasi hutafasiriwa tofauti tofauti kulingana na dhehebu husika na mitazamo yao ya kitheolojia
Lakini katika kanisa katoliki na Othodox pamoja na kanisa la Anglican *SHEMASI* ni padre Mdogo, Mtu anapopewa heshima ya kuwa shemasi na kusimikwa au kupakwa mafuta anakuwa amepewa heshima ya kuwa miongoni mwa wahudumu wa kanisa mwenye cheo kinachosimama kati ya Wachungaji na washirika, anahudumu kwa niaba ya wachungaji, ana heshima ya kichungaji ana daraja la kichungaji anaweza kufanya kazi za kichungaji na hata kuendesha ibada pale mchungaji anapokuwa hayupo.
Kwa jamii ya wapentecoste shemasi ni mtu wa kawaida, Lakini kwa jamii ya makanisa ya Kitoliki, Othodox na Anglican shemasi ni Mchungaji kamili ni daraja la kihuduma la juu kabisa, chini kidogo ya makasisi na wakati mwingine sawa na kasisi.
Nyakati za kanisa la kwanza Mashemasi walihubiri injili waliombea wagonjwa waliongoza ibada na Mtakatifu Stefano alikuwa mojawapo ya waliofanya kazi nzuri kiasi cha kuuawa na kuwa shahidi wa kwanza kumfia Yesu hata kabla ya mitume, *The first Christian Marty* hivyo unaposimikwa kikanisa kuwa katika ngazi hii wewe ni mtu mkubwa na una wito kamili wa kumtumikia Mungu kama ilivyo kwa wachungaji, na Mungu nanakuwa amekuheshimu mno.
Mashemasi wameainishwa wazi kuwa na sifa muhimu kama zile wanazopaswa kuwa nazo wachungaji na maaskofu

1Timotheo 3:1-8 “*Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema.Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi. Vivyo hivyo mashemasi na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana,si watu wanaotamani fedha ya aibu.wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi. Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia. Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote. Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao. Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu*.”
Kwa niaba ya familia namtakia mzee afya njema na kazi njema katika kumtumikia Mungu katika daraja hili la ushemasi, Na kama mtumishi wa Mungu namkaribisha rasmi sasa katika kumtumikia Bwana, yeye alikuwa akiniambia nimechagua fungu lililojema na sasa kwa pamoja tunamtumiakia Mungu na familia yetu imekuwa ya kikuhani kwa vile Babu Mzee Andrew Jumaa Kamote pia alikuwa shemasi.
Kila la Kheri DC Mstaafu katika kumtumikia Mungu.

*Muonekano mpya wa Mzee samuel Jumaa Kamote baada yakuwa Shemasi wa Kanisa, Siasa bai bai, sasa msalaba mbele katika kumtumikia Mungu Pichani Samuel Jumaa kamote akiwa na mkewe Esther Mkumbukwa Kamote, Baada ya kukamilika kwa ibada ya kusimikwa kuwa shemasi iliyofanyika huko Koreogwe



Tunamuombea maisha marefu na mafanikio mema mengi katika wakati wake huu wa Kustaafu

Imekusanywa kufanyiwa utafiti na kuandikwa na
kwa maoni na ushauri tafadhali niandikie 0718990796.
Rev. Innocent Samuel Kamote
Mkuu wa Wajenzi mwenye Hekima


Hakuna maoni: