Vijana
na Ufahamu kuhusu viungo vya uzazi.
Viungo vyetu tulivyopewa na
Mungu ni zawadi ya pekee sana ambavyo vinaweza kutumiwa kwa utukufu wa Mungu na
kutupa baraka duniani pia vinaweza kutumika vibaya na vikasababisha madhara
ikiwemo kupoteza maisha, si dhambi kuzungumzia viungo vya uzazi na matumizi
yake kwani kwa haraka sana vijana wanaweza kudhani kuwa wanaelewa na pia
wanajua kuvitumia viungo hivyo vya uzazi, inawezekana dhana hiyo ikawa kweli
lakini bado tunahitaji kujifunza biblia insema nini juu ya hilo, mtu akidhani ya kuwa anajua neno
hajui bado kama impasavyo kujua. (1Koritho
8;2).tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitatu vifuatavyo;-
- Ufahamu kuhusu viungo vya uzazi.
- Dhana potofu kuhusu viungo vya uzazi
- Jinsi ya kutumia viungo vya uzazi kwa halali.
Ufahamu kuhusu viungo vya uzazi.
(Mathayo
19;4) Mungu alipoumba mtu mume na mtu mke maana yake aliumba mtu mmoja akiwa na jinsia ya kike na
mwingine akiwa na jinsia ya kiume ili kupitia muunganiko wao waweze kuzaliana
na kuongezeka na kufurahiana au kuyafurahia maisha kupitia tendo hilo ambalo ni
zawadi (Mwanzo 1;26-28) baraka ile
yakuzaa na kuongezeka ni tofauti na ile ya kulima bustani ya eden na kuitunza (Mwanzo 2;15) kazi ya kuitunza bustani
iliweza kufanyika kwa mikono lakini ile ya kuzaliana na kuongezeka hufanywa na viungo hivi maalumu
ambavyo Mungu ametupa, Bahati mbaya viungo hivi vinafichwa sana na havionekani
hovyo vinaitwa vya siri, na vinapotajwa watu hushituka na kuona ni dhambi kwa
mtindo huu hata kuvizungumzia
kunaonekana ni kinyume na maadili na watu wengi huinama vinapotajwa hivyo ujuzi
kuhusu viungo hivi ni unakuwa mdogo na
unapovielezea watu wanataka umalize kwa haraka. Viungo hivi tutavichambua kwa
picha na baadae kuelezea kazi za kila kiungo.
Pichani ni mfumo wa kiungo cha uzazi
cha mwanaume, mboo inapokuwa imekatwa
katikati, mfuko mweupe juu kabisa ni kibofu cha mkojo Bladder, Mrija mweusi ni (tube)
njia ya mkojo na shahawa ambayo huitwa Uretha, Mfuko unaobembea chini kwa ndani
ni Testicals, mapumbu au makende, na Mfuko unaobeba kwa nje ni kifuko cha mapumbu
scrotum, Nyuma ya kibofu na mrija wa shahawa na mkojo ni tezi maalumu
zinazotengeneza majimaji yanayobeba mbegu au ghala ya shahawa hii huitwa Seminal vesicle, Mbele ya mapumbu na
mfuko wake ni Mboo yenyewe Penis. (Picha na maelezo kwa hisani ya maktaba ya
mwandishi Innocent Mkombozi Kamote)
Pichani ni mfumo wa kiungo cha uzazi
cha mwanamke,kuma inapokuwa imekatwa katikati,Pale kilipo kidole ndio kuma
vargina ni mahali panapotumikazaidi
wakati wa kujamiiana,kutoa damu ya hedhi,kuzalia na kukojolea,Juu kwa pembeni
ni kibofu cha mkojo bladder,Mfuko uliolala kuegemea kulia ni mji wa uzazi
uterus ni eneo linalotumika kukuzia mtoto wakati wa ujauzito,
Juu ni Mfumo wa kiungo cha uzazi cha
mwanamke kikiwa kwa sura ya mbele,kuma ikiwa katikati ya mapaja juu ni mji wa
uzazi na matawi tuyaonayo kwa pembeni ni mirija ya kulia na kushoto ya
kupitishia mayai pembeni mwake kulia nakushoto ni ni kokwa za kubebea mayai yai
la mwanamke ukubwa wake ni kama punje yamtama hivi.
Jinsi
ya kutumia viungo vya uzazi kwa halali.
Viungo hivi ambavyo muumba alitupa kama zawadi
pia alitoa vidokezo kadhaa katika Biblia namna ya kutumia viungo hivyo kwa
mfano wakati wa agano la kale Mungu alitoa maelekezo haya yenye uhusiano wa
moja kwa moja na Viungo vya uzazi ilikuwa ni najisi kumbikiri bint na endapo
mtu angefanya hivyo angelazimika kumuoa (Kumbukumbu
22;13-18). Mtu aliyebaka alipaswa kuuawa (Kumbukumbu 22;25),Kutokupiga kelele ni dhambi kama unabakwa (Kumbukumbu 22;23). Mtu kahaba hakupaswa
kuwepo (Kumbukumbu 23;17),ilikuwa
kuumizana sehemu za siri ni dhambi (kumbukumbu
25;11-12),Viungo hivyo pia viliwekewa sheria kama vile kutokulala na
wanyama (Lawi 20;15-16) kuvitumia
watu wa jinsia moja kama wanaume kwa wanaume ilikatazwa na imekatazwa katika
agano jipya pia (Lawi 18;22,Rumi 1;18-27) aidha
wanawake kwa wanawake pia si halali (Rumi
1;18-27). Na pia haikuwa halali kuvitumia kwa wanandugu walio karibu (Lawi 18;6-29).Unaweza kuona kama Mungu
ni muumba na alitupa viungo hivi pia alitupa namna ya kuvitumia kwa halali
kutumia viungo hivi kinyume na mpango wa Mungu kunaweza kusababisha madhara ya
aina mbalimbali ikiwa Mungu anaguswa na viungo hivi basi kuvitumia isivyo
halali kunaweza kutupelekea kuhukumiwa na Mungu kwani kunaweza kuharibu mfumo
na utendaji uliokusudiwa na Mungu aidha kwa sababu hii pia kisheria kuna hukumu
za uhalifu wa kimapenzi katika nchi mbalimbali “Sexual Crimes” hizi zimetungwa
ili kulinda utendaji ngono usio sahihi hii yote ni kwa sababu Mungu hapendi
tutumie isivyo halali.
Hakikisha
unakua msafi kwa viungo vya uzazi.
Kwakuwa viungo hivi vya uzazi viko sirini
vinafunikwa na Nguo hatuna budi kuhakikisha kuwa tunavitendea haki kwa
kuvifanyia usafi,oga mara kwa mara safisha viungo vyako vya uzazi ili kuvilinda
na bacteria na vipele vya joto au vya uchafu,ili kujikinga na harufu,aidha
hakikisha kuwa unajikausha vizuri kwa taulo na kama unaweza kupaka poda ni
vema,Fua chupi zako na nguo za ndani mara kwa mara hasa wanaume kwani wanawake
wengi hufanya usafi wa nguo zao za ndani mara kwa mara,lakini sivyo ilivyo kwa
wanaume,Biblia inaunga mkono swala zima la usafi wa viungo hivi ikikazia swala
zima la kutokwa na vitu najisi kama damu
ya hedhi na shahawa (Lawi 15;16-18,19).
Hivyo ni muhimu basi kwa vijana kuhakikisha wanakuwa wasafi, kama ni damu ya
hedhi tumia vitambaa safi vilivyokaushwa
vizuri na kupigwa pasi,na kama una uwezo tumia vitu kama always n.k vifaa vya
dukani vya kuzuia damu ya hedhi, Kwa wanaume kama umetokwa na shahawa hakikisha
unaoga na kufua chupi na mashuka,vijana ni muhimu wakajifunza kuwa na tabia ya
kunyoa vikwapa vyao na mavuzi katika sehemu za siri na maeneo mengine,
hakikisha unakua smart Mungu anapenda tuwe wa safi Biblia na hata Quran
zinakazia sana usafi wa mwili pia chumba chako na kitanda chako na maeneo
mengine yote yawe safi uwe na tabia ya kupenda usafi kwa gharama yoyote.
Dhana
potofu kuhusu Viungo vya uzazi.
Ni muhimu kufahamu kuwa yako mafundisha
potofu duniani yahusuyo viungo vya uzazi ambayo yanaweza kujenga dhana potofu
kwa vijana kuhusu matumizi ya viungo vya uzazi ambayo mengine yako kinyume na
neno au muongozo wa kimungu.
Iko dhana kuwa endapo utakaa muda mrefu
bila kuvitumia viungo hivi vitumikavyo
kwa kujamiiana kunakuwa na madhara,Madhara yanayotajwa ni kama vile ,kutoka
chunusi nyingi usoni,Kuchanganyikiwa,kuwa na ugonjwa wa kisaikolojia wa kukosa
mwanaume,kuumwa na tumbo wakati wa kuingia katika hedhi,nk. Dhana hii haina
ukweli kwani biblia inatia moyo watu vijana kusubiri hta wakati wa kuolewa(1Koritho 7;1,36),kuishi maisha ya
kujitunza ilikuwa ni Desturi ya kawaida kwa waisrael na nyakati za kanisa la
kwanza,na ilikuwa ni upumbavu mtu kuharibu ubikira wake (Mwanzo 34;1-9,2Samuel 13;10-15). Kwa msingi huu vijana wa kike na
wa kiume wanaweza kuishi maisha ya ubikira hata zaidi ya miaka 30 hivi yusufu
aliishi na hata kupewa mke akiwa na Umri wa miaka 30 na alizaa watoto watu
wanaotia moyo dhana hii wanataka kuwaongoza vijana nje ya mpango wa kimungu
biblia inasema jinsi gani kijana aisafishe njia yake ni kwa kutii neno la Mungu
akilifuata daima (Zaburi 119;9).
Ni muhimu kufahamu kuwa chunusi si sababu
inayotokana na kutokushiriki mapenzi,lakini mtu anapo anza kuwa mtu mzima yaani
anabalehe mwili huwa katika mchakato wa
mabadiliko ya aina mbalimbali katika wakati huu ngozi huwa inapokea vinururisho
vya kuifanya ionekane nzuri hivyo kunakuwa na kusambazwa kwa aina Fulani ya
mafuta mwilini ukiwemo uso,hii hupelekea baadhi kuwa na ngozi yanye mafuta mengi na wengine kuwa na ngozi
kavu kwa wale wenye ngozi yenye mafuta
yanayozalishwa kwa wingi ndio hukumbwa na tatizo la kuweko kwa chunusi nyingi
hivyo tatizo hili haliwezi kumalizwa kwa kufanya ngono bali kwa aina za mafuta
tunazozitumia kama ni lotion basi inashsuriwa wale wenye tatizo hili kutokupaka mafuta au kupaka
lotion yenye griselini nyingi lakini griselini nyingi itawafaa wale wenye ngozi
kavu, pia inashauriwa kutumia poda kwa watu wenye nyuso zenye mafuta
mengi,kutumia maji ya vuguvugu na njia nyinginezo.
Dhana nyingine ambazo huongoza katika
matumizi mabaya ya viungo vya uzazi ni kupunguza hamu ya mapenzi kwa
kubusiana,kushikana shikana,kugusana uume au uke au kwa kujichua yaani kupiga
punyeto master bathion, nia hizi hufaa kupunguza ashki za kimapenzi bila
kufanya ngono dhana hii ni sahihi kwa vijana wa kawaida kama ifundishwavyo
mashuleni hata hivyo si njia sahihi kibiblia mapenzi ni kama moto na huwezi
kufanya mahaba haya kisha ukatoka salama (Mithali
6;27-28),Biblia haishauri kutumia njia zenye kuchochea mapenzi kabla ya wakati
sahii akisisitiza hilo Sulemani anasema hivi “Nawasihi enyi Binti za Yerusalem
kwa paa na kwa ayala wa porini Msiyachochee mapenzi wala kuyaamsha hata yatakapoona vema yenyewe”(Wimbo ulio bora 2;7,3;5).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni