Kwanini wanaume sio waaminifu?.
Kwa nini wanaume sio waaminifu? Amini
usiamini sio tu katika tendo la ndoa,katika swala la kudanganya wanaume zaidi
ya nusu, wanakiri kutokuwa waaminifu katika ndoa zao kwa vile wanahisi
wamezarauliwa na wake zao, ni asilimia 7% tu wanaweza kufanya tendo hilo nji
pasipo kutamani, kwa hiyo unaweza kuona kuwa tatizo la wanaume kutoka nje ya
ndoa ni kubwa zaidi kuliko la wanawake lakini ni kwa nini ni vema tukapata
sababu za kina ili tujue ni namna gani tatizo hili laweza kushughulikiwa
vyombo vya mawasiliano kama simu vimeongeza maumivu katika mahusiano
1. Hawasikii msimsimko tena kwa wake zao
Baada ya ndoa na muda kupita
kunatokea uzoefu wa nania ataanzia wapi na ataishia wapi, ukweli ni kuwa
msisimko unaisha na inabaki kuwa hali ya kawaida, kila mmoja angependa kuhisi
uhai wa mweziwake katika tendo, lazima ionekane kuwa kila mtu analitaka na
kulifurahia katika mazingira ya Afrika wanawake walijifunza kuficha hisia zao
kuhusu tendo la ndoa hawana njia mbadala, hawajitumi, hawaonekani kusisimuliwa
na tendo hili, mazoea yanatoea na hali inapokuwa namna hii, mwanaume kwa
kukusudia au kwa kuto kukusudia moyo unajiandika kuwa anahitaji kutafuta aina
nyingine ya msisimko nje ya kile alichozoea kupata kwa mazoea katika hali hii
wanawake wanashauriwa kulishabikia tendo la Ndoa, kuonyesha wanawataka waume
zao wanawapenda na wajihadhari kabisa na uchawi wa kuwafananisha waume zao au
kuwalinganisha na wengine ama wale waliowaona katika sinema za kingono na kwa
busara kutoa maelekezo ya kile ambacho wakifanyiwa kitaleta msisimko mkubwa,
badala ya kusubiri mume agundue mwenyewe.
Kwa ujumla sababu hii ndio sababu
inayoweza kuwa ya msingi kwa wanaume wanaopokuwa wameamua kuoa wanakuwa na
msimamo kwamba watatulia katika ndoa zao, lakini mambo yanapobadilika na mara
kwa mara kukaanza kuwa na usumbufu kwa maana ya ugomvi kati yake na mke wake
ugomvi unaojitokeza mara kwa mara na kukosa suluhu, hali ya kukosekana kwa
furaha hujitokeza, na katika hali kama hii mume huweza kuamua kupambana ama
kukimbia kwa maana ya kujiepusha na ugomvi huo na kuanza kutafauta faraja
sehemu nyingine na kwa mtu mwingine, ni katika kutafuta faraja hiyo na
kujihadhari na Usumbufu ndipo Mwanaume hujikuta anaanza zinaa, Kumbuka Mfalme
Suleiman alisema ni afadhali kukaa katika pembe ya darini kuliko katika nyumba
pana pamoja na mwanamke mgomvi yaani mwenye
kelele (mithali 21:9) na pia alisema ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika
kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi.
Baadhi ya wanaume huona kama ni kazi
kubwa sana kutatua matatizo ya ndoa zao, na kuona kuwa nji iliyo rahisi ni
kupata mwanamke mwingine, na huko atajipatia raha na msisimko mkubwa na
kujisikia kuwa mtu, kuliko kazi kubwa ya kufundisha na kuelekeza na kutatua
migogoro katika ndoa, Kutoka nje inakuwa ndio zawadi kubwa wanayoweza
kujipongeza hata kama watakuwa na kazi nyingi na ngumu, inaonekana ni afadhali
lawama kuliko fedheha
4.
Wanaume wanapenda majaribio
Wanaume
wamekuwa na ushawishi wa kimaumbile mioyoni mwao wa kutaka kufanya majaribio ya
kingono, wakati wanaume wengine wanaridhika kufanya ngono na mke wao mmoja kwa
muda mrefu na zaidi katika maisha yake yote, wengine wanaona hapana ni lazima
wafanye majaribio ya kutosha kabala hawajaamua kutulia, wanataka kulala na
wanawake wengi kadiri iwezekanavyo na mara nyingi na hivyo ahawafikiri zaidi
umuhimu wa patano la ndoa na huenda wakajifikiri kuwa ni wenye nguvu katika
ngono kuliko wengine
5. Utoshelevu wa
kihisia
Wakati mwanamke anapokuwa na shughuli nyingi za maisha yao,
kufanya kazi kulea watoti na kuangalia ndugu jama a na marafiki au wazazi,
wanaume wanabakia katika halia ya ukavu na kukosa utoshelevu lakini wanaume ni
wenye kuendeshwa na hisia, wanapenda pia kupendwa kujaliwa na kushukuriwa na
wangependa wake zao wawaonyeshe kuwa wanajali na kutambua kuwa wanajaribu kila
liwezekanalo kuyafanya maisha kuwa mazuri, wengi wa wanaume hawapendi
kukumbushwa yaliyopita ambayo nafsi zao ingependa iyasahahu, kama watalaumiwa
tu nwakati wote itatokea kuwa watafanya mengineyo hata na watu wasaidizi wa
kazini au Bosi zao, na wale wanaowasifia, wamaowahudumia na kuwajali nah ii
ndio sababu inayowapelekea kuona ugumu na uthamani anaoupata nyumbani.
6. Historia ya
kurithi na kujifunza
Baadhi ya wanaume wana kumbukumbu za yake yaliyofanywa na
wazazi wao katika ndoa, jambo hili linakuwa limewapa funzo na kuwajengea utambuzi
tangu utoto kuwa kutoka nje ya ndoa ni jambo la kawaida, Hata kama inawezekana
wakawa wanafahamu kwa undani kuwa wanachokifanya sio sahii, wote tunajifunza
kutoka kwa wazazi wetu, na kwasababu hiyo kwa kujua au kutokujua tunapata
maarifa na kuigiza kutoka kwao, kwa hiyo kutoka nje ya ndoa ni jambo ambalo
wengine hujifunza kutokana na mazingira yote yanayowazunguka Marafiki, wazazi,
jamaa na kila mmoja ambaye umekuwa karibu na mwenye aina hiyo ya maisha, watu
hao kwa kukusudia au kwa bahati mabaya, Baadhi walikuwa na mahusiano na watu
wengi huko nyuma na baadaye historia inajirudia
7.
Kulipa kisasi
Wanaume pia wanatabia ya kulipa
kisasi, na kuamua kuwa na wanawake wengi, hata pale inapotokea kuwa wake zao
walikuwa na hatia na wamekubalia kubadilika na kutubu baadhi ya wanaume hutumia
hi kama njia ya kutokusamehe
8. Wanahitaji
kupendwa
Wanaume pia wanahitaji kupenmdwa,
Mwanaume anapogundua kuwa hapendwi wanatafuta ni wapi wanapendwa na ni wapi
ambapo kuna mtu atawafikiria kuwa wao ni maalumu, na matokeo yake ni kuwa
ataangukia kwenye uhusiano wenye kutimiliza hisia zake na mara wakionyesha
kujaliwa na kupatiwa kile ambacho hawakukipata kwa muda mrefu toka katika ndoa
zao au kwa wake zao wananyoosha mikono yao hewani na kukumbatia uhusoiano mpya
wa nguvu zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni