UTANGULIZI
Kwa ujumla kujifunza kuhusu watu ni muhimu
sana kuliko kujifunza kuhusu mambo mengine na kwa kuwa wanadamu wana umilele
Mchungaji ni lazima awe na uwezo wa kuwashawishi na kuwavuta ili waufikie
mwisho wao wa kimilele katika njia iliyo njema. Kadiri tunavyojifunza kuhusu
watu ndivyo tunavyoweza kuwa na ujuzi wa kuwashawishi ingawaje kutegemea uwezo
wetu tu wa kawaida bila kutegemea upande mwingine wa maisha yetu ni hatari sana
na sio kusudio la somo hili lakini japo kwa kiwango kidogo ni muhimu kuwa na
ujuzi kuhusu wanadamu Bila kuacha kumtegemea Mungu.
Ingawaje wanadamu wanatofautiana kulingana
na mazingira na tamaduni kwa ujumla wana mambo ambayo kwa kawaida yanafanana
sana au woote huyashiriki na tunapoona mwengine anaenenda Tofauti na tabia
isiyokuwa ya kawaida kama wengine tuna
kuwa na mashaka kuwa ana maumbile
Tofauti kisaikolojia lakini lazima utafiti wa kisaikolojia au Elimu ya
viumbe yaani Baiolojia ifanyike kwa kulinganisha na jamii ya mtu huyo mama yake kabila yake na kadhalika ndipo ithibitike kuwa ni tabia
tofauti kisaikolojia lakini zaidi ya hapo wanadamu katika ubinadamu tunafanana,
Paulo Mtume alisema hivi Matendo 17;26 “Naye alifanya kila taifa la wanadamu
kutoka katika mmoja wakae juu ya uso wa inchi yote akiisha kuweka nyakati
alizoziamurutangu zamani na mipaka ya makazi yao”
Lakini ni muhimu kujibu swali moja la msingi
kabla ya kuendelea je ni muhimu kusoma Saikolojia kwa wakristo? Baadhi ya watu
huamini kuwa Saikolojia ni chombo cha shetani cha kudanganyia watu wenye mapenzi
mema hii inaweza kuwa kweli kwa sababu wengi wa wasomi wakubwa wa Saikolojia ni
watu wasio na wokovu hata hivyo siku hizi kuna watu wengi waliookoka waaminifu
ambao ni wataalamu wa Saikolojia na wanapigia kelele umuhimu wa kujifunza
Saikolojia wakidai kuwa wanafunzi wa Yesu wanaweza kufaidika kwa mengi kupitia
kusomea Saikolojia katika mtazamo wa Kikristo
Somo hili linafanya kazi hiyo na linaweka
japo kwa Muhktasari yale ambayo ni muhimu kwa watumishi wa Mungu kuyajua na
kuwasaidia wakati wa kuhubiri injili hivyo haina kusudi la kumfanya mtumishi wa
Mungu kuwa mwana Saikolojia lakini kukutia moyo na kuyatumia katika maisha yako
na kwa faida ya watu ambao Mungu amekupa uwahudumie hii itakuwa faida kubwa
kwani tunaamini kuwa somo hili litakusaidia pia kuwahudumia watu ambao
wanapitia misukosuko kadhaa ya kimaisha na tabia za binadamu
Kila
sura ya kitabu hiki inatoa mwanga wa kiroho pia kwa aajili ya kweli Fulani za
Kibiblia na mjadala wa kibiblia kuhusiana na jambo linalojadiliwa hapo kwa hiyo
uwe na amani unapopitia somo hili na Mungu akubariki sana Sali sala hii pamoja
nami
“Bwana
mwema wewe ulisema usimwache Elimu aende zake naomba unipe ujuzi huu lakini
uufanye kuwa Baraka kwa mambo ya rohoni kwani Elimu zote na maarifa na Ufahamu
na Hekima vyote vinatoka kwako nasi tunapokea ili tuvitumie kwa utukufu wako
asante Mungu kwa kunipa neema hii ya kusoma somo hili ili niwe msaada kwa jamii
ya watu uliowaita kwa faida ya ufalme wako asante Bwana Yesu kwani kupitia Roho
Mtakatifu utapanua ufahamu wangu na kuzidi katika jina la Yesu Amen”
UFAHAMU KUHUSU SAIKOLOJIA NA ASILI YA
SAIKOLOJIA
Kwa
kawaida wanadamu wanatafuta faraja, maisha mazuri ya amani na utoshelevu hii
ndio maana tunaona hata mtoto mdogo hulia anapokuwa anahitaji jambo Fulani na
hufurahi anapokuwa ametimiziwa haja zake.kadiri mtoto huyo anapokuwa mkubwa
hutoa kipaumbele kwa watu waliokaribu naye na wanaohakikisha anakuwa na
mazingira mazuri. Lakini anapokuwa amekomaa zaidi kuwa mtu mzima anaanza kujitegemea
na kuanza kushughulikia kufanya mambo ya wengine yaweze kuwa mazuri, Pamoja na
umuhimu huu wa ukuaji na maendeleo ya mwanadamu kunakuwa na shauku ya kutaka
kujua kwanini mwanadamu anatenda hivi anavyotenda na kuunda aina ya ushiriki na
hii inaonekana katika kila jamii na tamaduni.mambo haya ni ya muhimu katika
msingi wa Ufahamu kuhusu Saikolojia
MAANA YA SAIKOLOJIA
Kuna
maelezo mengi kuhusu Saikolojia na kila maelezo yanasisitiza sehemu Fulani ya
ya Ufahamu kuhusu Saikolojia maelezo yafuatayo yatakuwa ni muhimu kwa mtazamo
wa somo hili
Saikolojia
ni Elimu kuhusu tabia za mwanadamu, uzoefu na maendeleo ya akili katika
uhusiano wa jamii na mazingira yake.
Saikolojia
ni sayansi inayohusu utendaji wa akili unaohusiana na tabia za mwanadamu katika
kulenga kuielewa, kuona yajayo mbeleni na kuisahihisha hiyo tabia
Neno
Saikolojia limetokana na neno Psychology la kiingereza kinachotokana na Kiyunani
Psyche yaani nafsi na ology yaani logos Ufahamu
kuhusu hivyo saikoloji ni somo lihusulo Ufahamu
kuhusu nafsi. Hata hivyo kuna mkanganyiko kuhusu Saikolojia katika
ulimwengu tulio nao wa leo hivyo ni muhimu kufahamu mambo amabayo sio
Saikolojia
·
Psychic Phenomena – Saikolojia sio kazi za kusoma
Nyakati au utambuzi au usomaji wa nyota kama ifanywavyo na waganga wa kienyeji
wanaodai kuwa na nguvu Fulani ya utambuzi watu hao hudanganya watu kwani ni
kupitia uhusiano wao na mapepo ndipo huweza kutambua mambo fulani na sio
Utafiti wa kisayansi katika shamba la Saikolojia.
·
Common Sense – Kuna uwezekano kabisa kupitia
uzoefu Fulani mwepesi wa watu wenye fahamu au akili wanaweza kuelewa mambo
Fulani kuhusu Saikolojia lakini kuna mipaka katika ujuzi wa kawaida wa
kibinadamu ambao umegawanyika katika vipengele vikuu viwili 1. Utendaji wa
kawaida wa kiakili mara chache hupitia vipimo vya kiutafiti vya kimaabara 2.
Wote tuna ukungu Fulani wa kiufahamu katika mazingira Fulani ya kuwachunguza
wengine na hivyo tunaweza kufikia hatima ya kuamua kitu Fulani kwa sababu
Fulani kwa mfano katika hali ya kawaida wote tunaweza kukubali kuwa wanaume
wana akili nyingi ukilinganisha na wanawake katika Ufahamu wa kawaida Common
sense inaweza kuonekana kuwa sahihi lakini utafiti wa sayansi ya Saikolojia
unagundua Tofauti yake kwamba wanawake wana akili kuliko wanaume
LENGO LA SAIKOLOJIA
Lengo
kuu la msingi la Saikolojia ni mwanadamu kuyamudu mazingira yake au maisha.hii
ina maana ya kuwa uwezo wa mtu na mali alizonazo hauwezi kuwa njia pekee ya
kujitosheleza kuhimili migandamizo au msongo.Mtu huyu anaweza kuwa na umasikini
wa kuhimili msongo au mgandamizo na hivyo akawa anatatizo la kushindwa kuhimili
msongo “Maladjausted” hali hii
inaweza kumlemea mtu, familia na hata jamii, kwa hiyo kazi ya Saikolojia kwa
ujumla ni kugundua kanuni nzuri za
kumfanya mtu astahimili msongo au mgandamizo na kuzitumia kanuni hizo katika
mahusiano ya wanadamu, inafanyika hivyo kwa kufundisha, Kuandika Vitabu au
majarida na kwa kutoa ushauri au nasihi
kwa watu ili waweze kumudu mazingira yao kwa njia hii watu wengi
wataweza kujimudu na kuchukuliana na maisha na kuzijenga jamii zao na
kuwasaidia wengine katika jamii.
UHUSIANO WA SAIKOLOJIA NA SAYANSI.
Saikolojia
inaweza kufikiriwa pia ni sayansi ya tabia “Behavioral science” lakini msingi wake ni wazi uko katika sayansi
ya viumbe yaani Baiolojia na Filosofia ingawaje kuna mwingiliano kati ya
Saikolojia na Nyanja hizi mbili za kisayansi
na Nyanja nyingine kama Elimu ya jamii Sosholojia na Anthropolojia na
Elimu education.
Saikolojia
ni sayansi ihusuyo tabia za mwanadamu kwa ujumla lengo kuu la sayansi likiwemo
la Saikolojia ni
·
Kufanya
uchunguzi – Observation kuchunguza tabia ya mwanadamu kwa makini
·
Kufafanua
Description – Kufafanua kile kilichochunguzwa
·
Kuelezea
explanation – Kuelezea tabia katika msingi wa kufafanua kile ulichochunguza
·
Kukadiria
Prediction - kuweza kukadiria au kutabiri kuhusu tabia hiyo baadaye katika
msingi wa kile kilichoelezewa
·
Kudhibiti
au kushawishi Influence or control – kutumia utabiri kushawishi tabia ya
baadaye au kudhibiti ingawaje wana Saikolojia wengi wa kisasa wanapiga marufuku
kudhibiti tabia ya mwanadamu mwengine.
Ili
kufikia malengo wanasaikolojia wanatumia njia za kisayansi za kiutafiti, njia
hii ndio njia halisi nzuri ya mbinu za kisayansi za kufanya uchunguzi unaofaa
usio na kifungo “Unbiased” kwani
njia za kisayansi zinachunguzika tena na tena na tena utafiti wa kisayansi
lazima uwe wenye lengo, halisi na wenye hitimisho lisiloharibika ingawaje kwa bahati
mbaya uchunguzi kuhusu mwanadamu ni mgumu kutokana na kutokusomeka moja kwa
moja yaani mahitaji ya kiuchunguzi ni magumu lakini hii haimaanishi kuwa
haiwezekani katika kufuata utafiti wa kisaikolojia.
SAIKOLOJIA KAMA SAYANSI.
Kuna
njia kubwa mbili za utafiti wa kisaikolojia ya kwanza ni utafiti wa kimaelezo
na ya pili ni utafiti wa kisayansi Experiment hapa tutajaribu kuzichambua kwa
ufupi.
UTAFITI WA KIMAELEZO
Hii
ni hali ya kutafiti kwa kuchunguza na kujifunza tabia ya mwanadamu, kumbuka
umuhimu wa neno kujifunza na ni huku kujifunza kuna kusababisha uchunguzi wa
kisaikolojia kuwa wenye kufanikiwa badala ya kumchunguza jirani yako. mchunguzaji
wa utafiti wa kimaelezo huchagua tabia fulani kwa umakini zile anazotaka
kuzichunguza na kisha anatafuta namna ya kutunza Kumbukumbu ya yale
anayoyachunguza kwa utaratibu maalumu ingawaje utafiti huu hauna utafiti wa
kisayansi au wa kimaabara lakini faida yake ni kupatikana kwa maelezo yawezayo kumfaa
mtafiti kwa mfano tunataka kujua idadi ya watoto katika kanisa ili kujua kama
kunahitajika mabadiliko fulani katika
madarasa ya shule ya Jumapili au kujua ni idadi gani ya wageni
hutembelea kanisa na kwa nini
wanalitembelea kanisa na nini hutokea baada ya kutembelea Mchungaji anaweza
akaliita jambo hili ufuatiliaji lakini
kwa mwanasaikolojia ni utafiti wa kimaelezo.
UTAFITI WA KISAYANSI "EXPERIMENT"
Tofauti
na utafiti wa kimaelezo utafiti wa kisayansi hufanyika katika maabara za
kisaikolojia vitu vingi muhimu vya kitaalamu vinapatikana humo kupima tabia
fulani kisha kuitolea maelezo na kutafuta njia gani za kisayansi zinaweza
kutumika kudhibiti kwa mfano ni wazi kuwa kama unataka kujua ni sababu gani
hupelekea wanadamu kuwa na kiu unaposhughulika na watu utawauliza kuwa una
kiu? Lakini katika utafiti unaweza
kumtumia mnyama ambao kwa kawaida huwezi kuwauliza hivyo maelezo kuhusu kiu kwa
wanyama yatachukua muda wa kufuatilia ni kwa masaa mangapi au Dakika ngapi
hujisikia kunywa maji utafiti wa kisaikolojia wa kimaabara ni wa muhimu kwa
sababu unatupa kujifunza hii ni ya muhimu hata katika kusaidia kutafuta dawa ya
tabia fulani ya mwanadamu, inaweza kutusaidia kujua mwendo wa Mapigo ya moyo
kupumua na Shughuli nyingine za mwili na namna ya kutibu.
HISTORIA YA WANASAIKOLOJIA WA ZAMANI ZAIDI.
Kwa
ujumla historia ya Saikolojia ni ya zamani sana tunaweza kusema ilianza tangu
kuumbwa kwa mwanadamu tangu wakati huo
mwanadamu ametafuta kujitambua na pia
amejaribu kwa nia mbalimbali kutafuta kujua nini hatima ya tabia yake au nini
kinafuata baadae katika tabia za kibinadamu
katika kutafuta hilo kuliibuka kuweko kwa falsafa mbalimbali.
1.
Mwanzo wa matazamo ya kifalsafa
Mwanafalsafa
wa kiyunani Aristotle 485-322
K.K. aliitwa na wengi kama mwanafalsafa
wa kwanza na mwanasaikolojia mkubwa yeye aliamini kuwa mtu kuwa kichaa ni
matokeo ya aina fulani ya maji katika ubongo kukosa kukaa sawa katika nafasi
yake kutokana na utafiti huu ndipo ilipokuja kusaidia kupatikana kwa aina kubwa
ya makundi ya watu duniani aina zile nne za makundi ya watu tutaziona mbeleni
na kujifunza kwa kina kuhusu makundi hayo ya watu.
Mtakatifu
Thomas Aquinas 1225-1274 B.K aliandika katika matazamo wa kitheolojia kuhusu tabia yeye aliamini kuwa mwanadamu yuko huru kujiundia tabia, analo chaguo
ambalo ni Jukumu la mwanadamu mwenyewe
na hivyo anawajibika kwa kila tendo atakalolifanya anajulikana pia kama
baba wa Rational Psychology. Yaani Saikolojia ya ulinganifu
2.
Viongozi wakuu wa kisayansi
waanzilishi
Saikolojia
haina mlengo mmoja tu na badala yake Viongozi wengi wakuu wa kisaikolojia
waliweza kuendeleza mawazo yao kuhusu matazamo wao kuhusu tabia ingawaje hizi
falsafa zao zinaweza zisikubaliane na hivi ndivyo shule nyingi za mkondo huu wa
kisaikolojia zilipoanzia na shule hizi zinaelezewa pamoja na Viongozi
waanzilishi wake
A.
Wilhelm
Wundt 1832-1920
Huyu
ndiye Mjerumani wa kwanza kuanzisha maabara ya kuchunguza tabia za wanadamu
mwaka 1879 mrengo wake ulihusu mambo ya dhamiri na uzoefu, hisia na sura katika
akili alimtumia mbinu za kiutafiti ziitwazo kitaalamu Introspection ambayo kwayo wachunguzi au watafiti watabia za
wanadamu waliweka rekodi za mawazo yao na hisia zao mtindo huu uliitwa “Structualism”
Ni
mwanasaikolojia wa kwanza wa Marekani ambaye shule yake ilikazia katika mtazamo
wa jinsi tabia inavyofanya kazi katika dhamiri, yeye pamoja na John Dewey
walikuwa na ushawishi mkubwa katika swala la Elimu na kukazia kuwa chochote
kinachofanya kazi ni muhimu kuliko kisichofanya kazi mlengo wao ni kujifunza
C. John
Watson 1875-1958.
Alihisi
kuwa wanasaikolojia wa wakati wake walihitaji utafiti wa kisayansi katika bongo
zao na sio nje ya bongo zao yaani katika ulimwengu halisi hivyo alikazia katika
kufanyia utafiti tabia zenye kuchunguzika tu na sio nini kina msisimua
mwanadamu na kuhamasisha tabia au kuichochea pamoja na kuchunguza miundo ya
mfumo wa fahamu, tezi na misuli kwa hivyo shule hii ilijihusisha na tabia tu na
kuitwa Beheviorism.
D. Wolfgang
Kohler 1887- 1937.
Alikuwa
mwanasayansi wa kijerumani aliyesomea maswala ya namna ya kuipokea mambo Perception mkazo wake ulikuwa ni jinsi
gani akili inafanya kazi katika kutafasiri mambo kulingana na mazingira yetu
hili lilimpatia umaarufu mkubwa hivyo ilisemekana kuwa mambo yote ni zaidi ya
sehemu zake au wimbo ni zaidi ya kukusanya Maneno ya kuimba lakini
tunauchukulia kuwa ni wimbo wote.
E. Humanism
Hii
ni shule ya Saikolojia ambayo Haijulikani haina mwanzilishi lakini ni ya muhimu
sana katika ufahamu kuhusu tabia za wanadamu na iligunduliwa huko Marekani kati
ya mwaka 1950-1960 wakati wa mafanikio makubwa waandishi wake kama Carl Rogers
walikazia katika matazamo chanya wa matazamio ya tabia ya mwanadamu hii
ilijumuisha maswala kama ubunifu, uthamani, kukua na kujitosheleza ni moja ya
shule za kifalsafa zilizodumu sana katika shamba la Saikolojia leo kwa sababu
linalenga kupandisha juu kiwango cha
mwanadamu ambapo shule nyingine hazikuwahi kufanya
Hili
jamaa lilikuwa daktari katika maswala ya madawa na utabibu alikuwa ni mtaalamu
wa maswala ya akili aliamini kuwa tabia ya binadamu inasukumwa na misukumo “Drives” isiyozuilika kidhamiri au
isiyokusudiwa kuelekea kwenye hitaji husika la kistarehe kama tendo la ngono na
endapo halitatimizwa basi linamuacha mwanadamu huyu katika migogoro wa mtu na
mazingira yake na kusababisha tatizo kisaikolojia.
MATAWI YA SAIKOLOJIA.
Saikolojia
ina matawi yapatayo kumi na mbili hivi yoote ni muhimu kulingana na mazingira
na eneo ambalo Saikolojia ya aina hiyo huitajika matawi hayo kitaalami huitwa
Branches of Psychology.
a. Saikolijia ya jamii Social Psychology – hii inahusu
mwenendo wa mtu binafsi kuhusiana na jamii kwa ujumla kwani binadamu ni kiumbe
kisichojitegemea Social being hakuumbwa awe mwenyewe
b. Saikolojia ya maumbile Biological Psychology – hii inahusiana
na Elimu ya viumbe kama mikondo mbalimbali ndani ya mwili wa binadamu au mnyama
na mifumo ya maumbile kama uzazi,urithi,magonjwa na madawa metabolism and
Endrocine System,mfumo wa tezi n.k
c. Children/adolcent/adult
Psychology - hii
ni Saikolojia ya hatua za binadamu na jinsi anavyoweza kutenda kulingana na
umri wake nini kinamtokea wapi anajifunza nini Saikolojia hii ni ya
watoto,vijana na watu wazima
d. Clinical
Psychology – Hii
ni Saikolojia inayohusiana na matatizo ya magonjwa ya akili hapa wataalamu “Psychiatrists” wa magonjwa ya akili
hutumia njia tatu katika kushughulikia maswala ya kutibu akili
·
Psychotherapy – hapa daktari bingwa wa
magonjwa ya kisaikolojia hutimia njia ya mazungumzo na kujenga au kumtia moyo
mpaka aweze Kujiamini au kukubali kukabiliana na hali halisi inayo mzunguka
Reality Therapy n.k
·
During therapy – kutibu kwa kutumia madawa kama
Trangulizers ili kumfanya mgonjwa awe mpole au aweze kulala na kupumzika kwa
muda wa kutosha na kisha kusahau yanayomsibu kwa muda Fulani anajikuta amepona
na anarudi katika hali yake.
·
Shock therapy – ni kutumia njia ya umeme au mipira kushutua mgonjwa ili aweze kurudi
katika hali yake ya kawaida
e. Industrial
Psychology – hii
ni njia inayogusika na utumiaji au uchocheaji utumiaji nguvu ili kazi ifanyike
katika viwanda, ngumi michezo na kadhalika man power
f. Collective
Psychology – hii
ni Saikolojia inayohusu kurekebisha jamii katika makundi makubwa na madogo
kubadilika kulingana au kutoka katika fasheni, kubadilika kitabia, kuonyesha
mwitikio katika mambo mbalimbali mawazo na propaganda mfano kura za maoni kama white paper iliyotumiwa na
serikali kuingia katika vyama vingi 1992 ili kukuandaa kiakili kukubali
g. Applied
Psychology – hii
ni njia ya kufanya utafiti wa kisayansi katika Saikolojia ili kutatua matatizo
ya tabia mbaya za wanadamu katika jamii.
h. Medical
Psychology – hii
ni Nyanja inayoshughulika na swala zima la matibabu ya kisaikolojia kwa ujumla.
i.
Education Psychology – hii ni Saikolojia ya Elimu
ambayo kazi yake ni kuinua viwango vya Elimu, mbinu za ufundishaji, kutafuta
vitendea kazi na kutatua matatizo kujifunza uwezo na maendeleo kwa ujumla
j.
Development Psychology – Hii ni Saikolojia ya kujifunza
mabadiliko, misisimko, usomi na mahusiano ya jamii yanayotokea katika maisha ya
mwanadamu na maendeleo yake life pan
k. Abnomal
Psychology – hii
ni Saikolojia inayohusika na tabia zilizoharibika na watu wasio wa kawaida kama
vile mataahira, vichaa, wavuta unga na matatizo mengine yafananayo na haya n.k
l.
Military Psychology – hii ni Saikolojia ya mambo ya
kijeshi inayohusika katika kuchochea moyo wa kivita Mfano Operation demokras,
operation chakaza, mshike gaidi, Nduli, joka, nk.
MTAZAMO WA KIBIBLIA KUHUSIANA NA SWALA ZIMA LA SAIKOLOJIA
Je
ni namna gani Ukristo unaweza kulinganishwa na sayansi katika mtazamo kuhusu
mwanadamu na tabia? Kunamlingano katika swala ka kujifunza Saikolojia au
tunaweza kusema kila mmoja anataoa matazamo wake na hakuna mgongano isipokuwa
tunaweza kuona tofauti ndogo ndogo sana lakini mtu anapojifunza na kusoma zaidi
kuhusu maswala ya Saikolojia utagundua kuwa tofauti ni ndogo sana na hitimisho
huwa hivi kadiri tunavyojifunza Biblia zaidi ndivyo wakristo wanavyokuwa bora
zaidi kuliko mahitimisho ya kisayansi lakini kwa ujumla wake tunawiana katika wigo
mpana. Lakini ni muhimu kufahamu kuwa kadiri unavyojifunza kuhusu maoni
yatolewayo na wanadamu wawe wakristo au wasio wakristo na tukapuuzia mtazamo wa
kimungu ndipo tunapokuwa hatarini zaidi 2 Timotheo 2; 14- 16 Biblia inasema;-
“Bali
wewe, udumu katika yale uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti, ukitambua ya
kuwa ulijifunza hayo kutoka kwa nani na jinsi ambavyo tangu utoto umeyajua
Maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kwa njia ya
imani katika Kristo Yesu. Kila andiko, lililovuviwa na Mungu lafaa kwa
mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika
haki ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila kazi njema.”
Hatupaswi
kujisahau na kuyategemea zaidi mawazo ya kibinadamu na tukasahahu kuwa sisi ni
watu wa Mungu tunajifunza mengi kuhusu mawazo yetu, hisia, tamaa, misukumo nk.
Kupitia katika neno la Mungu katika namna ambayo tunaweza kuwa na ufahamu
mkubwa katika tafiti zinazofanywa na wana Saikolojia Ugunduzi unaonyesha kuwa
wanasaikiolojia wa Kikristo wanauwezo mkubwa wa kutatua matatizo ya wanadamu
kuliko hata wale wa kitabibu kwani wao hawagusi roho ya mwanadamu zingatia
kielelezo kifuatacho kinaonyesha kuwa mwanadamu ana maeneo makuu matano
Mwanadamu ambaye tunashughulika
naye ana mapito mengi na Saikolojia inaweza kugusa yote lakini inashindwa
kugusa mahitaji ya kiroho ya mwanadamu ambapo hapo ndio chanzo cha matatizo
yoote wanasaikolojia wa Kikristo wanaweza kugusa eneo hilo la muhimu, kwa vile mwanadamu ni zaidi ya mwili na akili
SAIKOLOJIA YA KUJIFUNZA
Tunaweza kuona
kuwa ni mambo gani yanachochea mazingira ya tabia ya mwanadamu kupitia kusoma
au kujua nini anajifunza na anajifunza vipi kwani karibu kila jambo katika
tabia ya mwanadamu imechangiwa na tulivyojifunza, maarifa, mbinu, mtazamo,
imani na tabia ya mchakato mzima wa mabadiliko ni matokeo ya kujifunza,
mchakato huu wa kujifunza pia ni mchakato wa mabadiliko unaoanzia tangu wakati
wa Kuzaliwa na unaendelea mpaka wakati wetu wote wa maisha ya duniani.
KUJIFUNZA NI
NINI?
Kujifunza ni
uhusiano wa kudumu wa mabadiliko ya tabia inayojitokeza kwetu kama matokeo ya
mazoea.na msingi wa muhimu wa kujifunza ni kubadilika kwa mfano mwalimu
anapoona wanafunzi wakionyesha muitikio wa maswali yake kwa ufahamu na maarifa
anajua kuwa wanafunzi wake wamejifunza kwa sababu tabia hiyo ya ujibuji maswali
kwa usahihi inaonyesha kuwa wamebadilika mchakato huu wa kujifunza unaweza
kupimwa katika mazingira makuu matatu
1.
Kuendeleza
mbinu mpya au kuboresha ile ya zamani
2.
Kuifundisha
mbinu hiyo mpya kwa wengine na
3.
Kuendeleza
mtazamo mpya na kuonyesha shauku ya kubadilika na kutumia mbinu mpya
Ili mtu aweze
kujifunza yako mambo ya msingi yanayosababisha kujifunza kuweza kutokea
·
Kuhamasika
au kuwa na shauku motivation – mtu
hawezi kuwa na moyo wa kujifunza kama hakuna hamasiko hii ni ile hamu kama ya
kuwa na daraja zuri baada ya Kujisomea au kupania kufaulu au ujuzi kwanini
unasoma hivyo shauku ikiwa juu
itakufanya uwe makini katika Kujisomea na kukumbuka kile ulichojifunza
·
Kushirikiana
Association – unapokusanya vitu
viwili au zaidi vinavyofanana na kusisimua katika akili huo ushirikiano kwa
kweli ni moyo wa kujifunza kwa mfano nikitumia neno KUSOSA kumaanisha kanuni ya
kula sana, soma sana na Sali sana neno hili kusosa ni ushirikianio wa neno hili
kubwa hivyo maana halisi ya jambo hupatikana na hivyo kujifunza hutokea, kule
kuweko katika jamii kunakufanya ujifunze, tabia za wanafunzi wa shule za kutwa
zaweza kuwa tofauti na za wanafunzi wa bweni kutokana na kuwa na ushirikiano
wanajifunza kitu cha ziada zaidi
·
Kuchochea
reinforcement – hali ya kuchochea
kitu ambacho umekwisha kujifunza inaleta matokeo ya kukifanyia kazi kile
ulichojifunza hii ni kwa sababu wakati mwingine usipokichochea kitu kinaweza
kisitokee tena lakini ukikichochea basi kitatokea hali ya kuchochea inaweza
kufanya kazi katika mazingira yote mazuri na mabaya rafiki kazi nzuri endelea
na kazi safi! Hii inachochea wakati wa
kampeni ni wakati wa kuchochea pia wakati wa mahubiri ya kiuamsho
Namna
kuu tatu za kuelewa namna ya kujifunza
Haiwezekani kwakweli
kufahamu kuhusu namna ya kujifunza bila kuelewa mambo machache kuhusu mawazo
kuhusu kujifunza na utafiti unaolingana na mawazo hayo ingawaje hatuhitaji
mawazo hayo au utafiti huo uweze kuathiri namna kuu tatu za kuelewa kujifunza
Kujifunza
katika hali ya kawaida Classical condition
Hii ndio namna
nyepesi zaidi ya kujifunza inahusisha mabadiliko katika kuakisi tabia nyepesi
na hisia mgunduzi wa mawazo haya ni Ivan
Pavlov aliyegundua kanuni muhimu baada ya kufanyia utafiti kupitia mbwa na
jinsi anavyoweza kudondosha ute baada ya
kumpima kuwa kila alipokuwa akimpa chakula alipiga kengele na siku moja kwa
bahati mbaya kengele ililia na mbwa akatokwa na mate mengi akifikiri kuwa
angeletewa chakula hivyo mbwa alijifunza
kutokana na hali ya kawaida kwamba kula
kwake kuliendana na mlio wa kengele hivyo ilipolia wakati hakuna chakula mate
au ute ulimtoka kwa wingi . hali kama hii inaweza pia kuaathiri binadamu kwa
mfano tunapoogopa mahali ambapo wala hapatishi kama vile tunapoona makaburi
tumejifunza katika hali ya kawaida kuogopa au kama kuna wimbo unapigwa wakati
sisi tukiwa katika hali fulani ya kihisia basi tunaweza kuwa na hisia zile kila
tuusikiapo wimbo huo, kama ulikuwa wakati wa vita au lolote hisia zetu zitakuwa
kama wakati huo na kwa hivyo tunaposisimuliwa na kitu ni kwa sababu tumejifunza
katika hali ya kawaida inayotufanya sasa tujisikie kama vile tulipojifunza
Kujifunza
kupitia Shughuli mbalimbali Operant condition
Dhana hii
inaamiini kuwa tabia hujengeka kupitia Shughuli mbalimbali njia hii ni ngumu
kwani inaingiza tabia kupitia nyenzo mbalimbali kwa mfano mbwa anaweza tena
kufundishwa aokote kijiti na asipokiokota anachapwa kiboko na bwana wake na
anapofanya vizuri anapewa zawadi chakula na upendo toka kwa bwana wake hivyo
anajifunza kupitia Shughuli mbalimbali na wanadamu pia huweza kujifunza kupitia
njia kama hizi kwa mfano watu wageni wanapokuja Kanisani wakapokelewa kwa
furaha na kupewa zawadi wanaweza
kujifunza kuja Kanisani na kijijengea tabia kuanzia na wakati huo.
Kujifunza
kupitia utambuzi au ufahamu au akili Cognitive learning
Dhana hii
imegunduliwa na mwanasaikolojia wa kijerumani mapema katika karne hii yeye
aliwafanyia watu utafiti na kugundua kuwa watu hujifunza au kuelewa vitu
kutokana na mazingira yao hivyo alihitimisha kwa kusema kujifunza kunatokea
mara mtu anapokuwa amepatwa na tatizo, ufahamu wa kuyajua mambo unatokana na
uhusiano kati ya mambo mbalimbali yanayoungana kutengeneza picha nzima ya mambo
kamili kwa mfano kama watu wameona Jengo kubwa kama Godauni na pakaweko Bwana
shamba, Mchungaji na Dj wa muziki jengo hilo litatafasiriwa kwa haraka
kulingana na ufahamu wa mtu Mchungaji ataliona linafaa kuwa kanisa,bwana shamba
ataona linafaa kuwa ghala la kuwekea chakula na Dj ataona linafaa kuwa hall la
kupigia muziki hii inatokana na utambuzi wao au ufahamu wao.
Kumbukumbu.
Tendo la kukumbuka
linategemea na namna mtu anavyokuwa amejifunza, kujifunza kwenyewe
kunategemeana na msukumo wenye kuleta athari kwa tabia hivyo kujifunza
kunapokuwa kwa nguvu basi kunaifanya tabia ijengeke
Namna
tabia inavyojengeka
Tunajua kuwa tabia
imejengeka kutokana na tendo analolifanya mtu linapokuwa limejitokeza bila
kupangwa katika hali kama hiyo tunasema tendo limekuwa tabia au mtu
amejifunza ingawaje tabia nyingine ni
zile zisizo faa kama kuvuta sigara,
nyingi huwa tabia hasi au chanya
kama kutembea au kuchukua mazoezi, tabia nyingi huendelezwa pasipo
kukusudia ingawaje nyingine zinapokelewa bahati mbaya katika kufanyia kazi
mbinu mpya au ujuzi mpya, mazoea yanafaa kwa sababu hututoa katika kufikiria
mambo madogo madogo na hivyo tuko huru kutoa muda wetu na nguvu zetu katika vitendo vya ubunifu, na
ni mpaka hali mpya inapoinuka usiyoitaka ya ina ile ya tabia ndipo inaposhindwa kufanya kazi ipaswavyo na
msukumo wa kidhamiri utahitajika.
Kukumbuka
Kukumbuka ni
mchakato wa akili kutunza katika fahamu zetu Maneno, picha na mbinu na
tunapokumbuka maana yake ni kuwa akili
inakurejesha katika ile picha au Maneno au mbinu uliyojifunza mwanzoni, kuna
mabadiliko yanayoelezeka ya muundo wa mfumo wa ubongo na chembechembe zake
ambao unahusika katika kufanya Kumbukumbu iweko mfumo huu unaitwa “Memory traces” kuhifadhi na kutafuta
kilichohifadhiwa ndio unaofanya mchakato wa kukumbuka uweze kukamilika kwa sababu ya muitikio wa chembechembe zinazo
fanya umoja uwepo wakati wa tendo la
kukumbuka linapofanyika
Lakini ni muhimu kufahamu kuwa kuna namna
mbili kuu za kukumbuka Kumbukumbu za muda mfupi Short term memory na Kumbukumbu za muda mrefu long
term momory kwa mfano wengine kwa wanafunzi ni Hodari kuweka Kumbukumbu kwa
ajili ya kujibu maswali katika mtihani lakini mara baada ya mtihani kila kitu
kinayeyuka kwa sababu hakujifunza namna ya kuhifadhi katika mfumo wa kukumbuka
wa muda mrefu lakini ili mtu awe na Kumbukumbu za muda mrefu anapaswa kuwa
na kujifunza zaidi Over learned au kurudia
rudia na kuyatumia kwa msingi huo mfumo
wa Kumbukumbu wa muda mrefu utaumbika na ikifanikiwa hivyo basi
kilichohifadhiwa hakiwezi kufutika kwa urahisi au kusahaulika kwa msingi huo
basi ili mtu akumbuke ni muhimu kuwa na ufahamu kuhusu mambo ya msingi matatu
yafuatayo
·
Recall
hii ni Kumbukumbu ya kawaida na mwanafunzi anaweza kuigiza tabia na vituko vya
mwalimu Darasani au kuweza kukariri kile alichojifunza kwa mwalimu wake amekariri
tu!
·
Recognition
hii ni kiwango cha juu sana katika kukumbuka wakati huu mtu huweza kutofautisha
anachokijua na asichokijua na kufanya unyambulisho.
·
Relearning ni jaribio la kukusanya mbinu au ujuzi wa
jambo fulani ambalo umelisahau kabisa
Kusahahu
(forgetting).
Kusahau ni tatizo
la ulimwengu mzima hii ni hali ya kushindwa kukikumbuka kitu ambacho
ulijifunza, swala hili hutokea wakati mwingine kwa sababu ya upungufu wa
vichocheo vinavyohitajika kuufanya mfumo wa Kumbukumbu kuwa kazini, na wakati
mwingine hutokana na mwingiliano wa jambo jipya ambapo mtu anapokuwa amejifunza
jambo jipya jambo hilo husababisha uwezo mdogo wa kukumbuka ya zamani tatizo
hili huitwa retroactive inhibition
au interference. Lakini unapojifunza lile la zamani kwa nguvu inakuwa ngumu pia
kushika jambo jipya hii nayo inaitwa Proactive
inhabition au interference wakati tukiwa tunalitafakari hili katika kanuni
za ujumla tunaweza kusema yafuatayo
·
Watu
wazima husahau zaidi kwa sababu wana mambo mengi ya kushughulikia katika maisha
yao mengi yakiwa ni ya zamani na ni vigumu kwao kupokea jambo jipya.
·
Watu
wazima wana tabia ya kufanyia kazi mambo yanayoonekana kama Yanastahili na kushughulikia kidogo sana na mambo
yanayoonekana kama hayastahili katika fahamu zao
·
Matatizo
ya kihisia na kimwili pia yaweza kuchangia katika swala zima la kusahau mambo
fulani ili mtu akumbuke anatakiwa kushituliwa
kwa umeme “Electric shock to the brain”
hii labda ni kwa sababu ya kuwa na
msongo wa mawazo depression na mtu anaweza asikumbuke tukio lililomfanya akawa
na msongo wa mawazo tiba yake ni hiyo.
·
Jambo
lingine linaloweza kumfanya mtu akasahau ni kukandamiza Repression hii ni hali ya mtu kutokutaka kukumbuka jambo baya la
kuumiza lililompata mtu kimaadili au kutishwa au kupitia uzoefu na hovyo
anajaribu kulipotezea na anasahau linapokumbushwa kwake linakuwa ni la
kuchukiza ama kutokana na kujeruhiwa nalo anakuwa mpiganaji wa tukio husika
kuliko.
·
Jambo
linguine ni suppression hii ni hali
ya dhamiri kujaribu kusahahu au kujihadahari kukumbuka na hivyo anatumia nguvu
nyingi ili asikumbuke jambo hilo na hii inaweza kufanyika bila mtu huyo
kujitambua kuwa amejilazimisha kusahau tukio asilotaka likumbukwe.
Namna
ya kujiendeleza au kukuza hali ya kujifunza Improving Learning Perfomance
1.
Kusoma
katika makundi group discussion hii
ni njia ya kujihamasisha kupitia wengine na kujichochea katika kuleta motisha
ya Kujisomea.
2.
Kurudia
rudia Recitation huu ni usomaji kwa
sauti kubwa ni usomaji mzuri kwani
unahusisha na namna nyingine za milango ya fahamu kama kusikia unaweza pia kujaribu kuelezea swala hilo kwa
mwengine napo pia ni kujifunza kuliko kuzuri
3.
Kusudia
kusoma kwa bidii mfano usilale wakati unaposikiliza kaseti fulani kwani
hutajifunza
4.
Kujirekebisha
soma kwa makini kisha jifanyie masahihisho kwa kurudia majibu sahihi
5.
Na
namna ya Kujisomea kitabu kwa mfano kipitie kwanza kabla ya kukisoma, jiulize
maswali, kisha soma, kariri au tamka kwa sauti, kisha pitia kwa upya hii ni
njia nzuri.
Mwanga
wa kibiblia kuhusu kukuza hali ya kujifunza
Biblia ina mambo
mengi ya kuzungumzia kuhusu swala la kujifunza hii inaonekana kwanza katika
majukumu aliyopewa mzazi ya kuwafundisha watoto wake Kumbukumbu 6;6,7 wana Saikolojia wanasisitiza watu kujifunza
wakiwa wamehamasika, kibiblia tunaambiwa kuwa wana wa Israel walikuwa na
masikio lakini hawakusikia hii ina maana kuwa watu hawakuwa na hamasa ya
kujifunza, lakini iko wazi kuwa alipokuja Kristo watu walikuwa wamehamasika
kusikia habari njema za ufalme wa Mungu mwanadamu aweza kujifunza kivitendo
hata kupitia mifano 1Koritho 4;16 Yohana 13;12-15 bado Biblia inaonyesha kuwa
ili mtu ajifunze anahitaji bidii na kurudia tena na tena mpaka aweze kusema
kama Daudi moyoni mwangu nimeliweka neno lako ili nisikutende dhambi. Watumishi
wa Mungu hawapaswi tu kuhubiri jumbe mpya kila wakati na kusahahu kuwakumbusha
watu makusudi ya Mungu kwa kuyarudia tena na tena kwa namna nyingine.
Misingi
ya maendeleo ya ufahamu na tabia ya mwanadamu
Jukumu la kutaka
kujua maendeleo ya tabia ya mwanadamu ni Shughuli ya kila siku kwa mfano kama
unataka kujua kwanini baadhi ya watu huwa na furaha kila siku na baadhi ni
wakali au wahalifu au Walevi? Kujua jibu la maswala kama hayo inakupasa kwanza
uanze kujifunza au kusoma kanuni za maendeleo ya mwanadamu tangu anapotungwa
mimba anapokuwa mtoto mpaka anakuwa mtu mzima kadiri unavyo yafahamu mambo hayo
ndivyo unavyopata ujuzi mzuri kuwahusu wanadamu na tofauti zao na kwa msingi
huo ili tuweze kuelewa vema swala hili ni muhimu kwetu kuwa na ufahamu juu ya
maswala ya kurithi na mazingira yanayojiumba katika wiki za mwanzoni na miezi
ya mwanzoni ya ukuaji katika tumbo la mama yake
Maswala
ya kurithi Heredity
Huu
ni ufahamu kuhusu maswala ya kibaiolojia ya namna kila mwanadamu anavyorithi
kutoka kwa wazazi wake wakati anapokuwa anatungwa mimba, kwani uwezo wetu wa
kimwili na kiakili na upekee unaamuliwa
na namna tunavyorithi, hali hizo zitaamua
tuwe na nywele za aina gani? Rangi gani? Macho ya rangi gani urefu au ufupi na
mengineyo mengi huamuliwa na namna tunavyorithi kutoka kwa wazazi wetu aina
hizi za urithi wa mambo kutoka kwa wazazi wetu unaamuliwa na chembechembe
zinazobeba siri ya chembechembe za mwili zitakavyokua hizi huitwa “genes au genetics codes” DNAs deoxyribonucleic acid hizi huamua jinsi chapa ya mwili
itakavyokua na kila chembechembe ya mwili itakavyokua hizi hutofautiana kati ya
mtu mmoja na mwingine hali hii ndiyo inayoamua mwili uweje na tabia pia
inadaiwa na wataalamu kuwa karibu asilimia 80% ya uwezo wetu wa kiakili ni wa
kuurithi hii haijalishi kuwa mtu ni masikini kiasi gani au ni tajiri kiasi gani
kwani Elimu huchukua asilimia 20% tu ya maswala ya jinsi tulivyo huku tukizingatia
kuwa mazingira pia yanachangia katika maendeleo ya mwanadamu
Maswala
ya mazingira
Wakati ambapo
wengi ni rahisi kufikiri kuwa mtoto anajifunza tabia anapokuwa amesha zaliwa au
mara baada ya Kuzaliwa lakini ukweli unabaki kuwa mtoto anaanza kuathiriwa na
mazingira hata tangu akiwa tumboni jambo hili kitaalamu huitwa Prenatal environment mtoto ambaye bado
hajazaliwa anaanza kuathiriwa na kemikali za mabadiliko katika tumbo la mama
yake kwa mfano kama mama anakunywa pombe, anavuta sigara, na mabadiliko
yanayosababishwa na maumivu au migandamizo huweza kusababisha watoto wengine
Kuzaliwa na athari za vilevi na baadhi ya magonjwa anayoambukizwa kutokana na
mazingira ya mamaye mtoto akiwa tumboni. Inaaminika kuwa mtoto ambaye
hajazaliwa anauwezo wa kuisikia sauti ya mama yake akiwa tumboni, mwanga, joto
na maswala mengine ya mazingira ingawaje haikubaliki na wengi sana lakini wengi
huamini kuwa pamoja na kuurithi mpaka mtu apatikane kuwa kama alivyo jamii
familia tamaduni vina sehemu kubwa ya kuufanya utu wa mtu kuliko kuurithi.Lakini
kisayansi inakubalika kuwa mtu hujifunza mambo tangu akiwa tumboni.
Maendeleo
ya kimwili ya mwanadamu
Kuna dhana kama
nne hivi zihusuzo ukuaji wa kimwili wa mwanadamu na hizi huanzia tangu wakati
ule anapaokuwa anatungwa mimba mpaka anapokuwa mtu mzima
Kutoka
kichwani mpaka mkiani
Inasadikiwa kuwa
unapojifunza kuhusu ukuaji wa mtoto akiwa tumboni katika wiki za mwanzoni mtoto
hukua kuanzia kichwani wakati huu kichwa ndicho huumbika kwanza kuliko
kiwiliwili hivyo kiumbe ambacho hakija zaliwa huwa na kichwa kikubwa kuliko cha
mtu mzima hivyo katika wakati huu basi ndio wakati wa makuzi ya ubongo kwani
wenyewe ndio unaoongoza utendaji mzima wa mwili
kuanzia na Mapigo ya moyo na mzunguko wa damu hivyo ukuaji wa ubongo
ndio unaoruhusu ukuaji wa mwili mzima na kuufanya ukue kwa asili hii ndio maana
mtoto huweza kusema japo vitu visivyoeleweka kabla ya kujifunza kusema kabisa
Kutoka
karibu kuelekea mbali.
Usemi huu kutoka
karibu kuelekea hutumika kuelezea ukuaji wa viungo vilivyo karibu na uti wa
mgongo ambavyo hukua kwa haraka zaidi kuliko mikono na miguu na baadhi ya
viungo vya mbali zaidi kama vidole na viungo vingine hivyo ukuaji wa kichwa
kuelekea kiwiliwili na ukuaji wa kutoka karibu kuelekea mbali unathibitisha
kuwa mwanadamu huanza kukua viungo vile ambavyo ni muhimu kwa uhai kwanza kabla
ya vile ambavyo vinatoa uimara na kumuwezesha au kuuwezesha mwili kutenda na kutembea
Mtoto wa miezi mitatu na nusu mpaka miezi minne tumboni anaweza kusikia na kujifunza kinachoendelea ulimwenguni
Tendo
la kujitofautisha differentiation
Hii ni hatua ya tatu
katika ukuaji wamwanadamu ambayo hutokea tangu mtu akiwa tumboni wakati ambapo
viungo vidogo sana huanza kukua kwa kasi sana na kujichanganua katika namna ya
kushangaza kwa mfano moyo huanza kama kijiungo kidogo sana kisicho na kazi
lakini katika siku chache za ukuaji huko tumboni hukua kwa kasi na kuanza kujiumba
katika maeneo yake makuu manne na kuanza kuongoza mtiririko wa damu inayoingia
na kutoka
Ukuaji
mwingineo Growth spurts
Katika namna ya
kushangaza sana tangu kutungwa kwa mimba kunakuwa na ukuaji unaojitokeza na
unaokwenda na mgawanyo sawia wa chembechembe za mwili katika kila sehemu lakini
wakati huu zikiwemo sehemu za via vya uzazi via vya kike au kiume ukuaji wa
viungo hivyo baadae huongezeka katika umri wa miaka miwili na kisha wakati wa
ujana kati ya umri wa miaka 12 kijana huanza kuwa mrefu sana na kuanza kupevuka
zaidi viungo vyake vya uzazi na kukoma kukua katika umri wa miaka 20
Maendeleo
ya ukuaji wa kisaikolojia na kijamii Psycho-social Development
Mwanasaikolojia
maarufu sana Erik K. Erikson alitoa maelezo ya kushangaza na kuvutia kuhusu
hatua za ukuaji wa mwanadamu na namna unavyochukua nafasi yeye anatoa wazo
linalobeba hali chanya na hasi katika kushughulikia ukuaji wa mwanadamu
Kujiamini
na kutokujiamini trust & mistrust
Jambo hili
hujifunza watu wa umri kati ya mwaka tangu Kuzaliwa mpaka mwaka mmoja au
Kuzaliwa mpaka miezi 18 katika wakati huu mtoto huanza kupima ulimwengu kama ni
mahali salama kwa ajili yake au la anapohisi kuna usalama anajijengea Kujiamini
na inapokuwa anahisu si salama anajijengea kutokujiamini, Kujiamini hutokea
pale mzazi anapomtimizia mtoto mahitaji yake yoote kama chakula na kumuonyesha
upendo na wazazi wanapokuwa wanawasiliana kwa amani mtoto anahisi kuwa
ulimwengu ni salama kwa ajili yake na anapohisi kinyume chake huanza kuingia
hofu na kuhisi ulimwengu kuwa si salama kwa ajili yake lakini haitokei kuwa
akajiamini au kutokujiamini kwa asilimia zote hili hutokea kiasi katika kipimo
fulani lakini hili ndilo linaweka msingi wa maswala mengine yote ya kujiamini.
Kujitegemea
na kuwa na mashaka Autonomy & doubt-Shame
Jambo hili huanza kuumbika kutoka katika umri
wa miezi kumi na nane mpaka miaka sita wakati huu ni wakati ambapo mtoto
anaanza kujishughulisha na jamii wakati huu ndipo anapojifunza maswala ya kuvaa
nguo na kuanza kufanya mambo mengine bila msaada wa mtu katika wakati huu mtoto
atataka kufanya vitu vingi sana hata vile ambavyo haviwezi wazazi wakiwa makini
wakati huu kumtia moyo kuwa anaweza anajijengea hali ya Kujiamini lakini
anapokuwa anakemewa anaanza kuingia mashaka na kutokujiamini na kuwa na aibu ya kufanya mambo
Uwezo
wa kuamua bila kumtegemea mtu na kuwa na hatia Initiative & Guilt
Jambo hili hutokea
kati ya umriwa miaka 4 -5 katika wakati huu mtoto hujishughulisha katika
vitendo zaidi vinavyo msaidia kujitegemea zaidi wakati huu anaongea anaongezeka
nguvu na anatamani aujue ulimwengu zaidi na wakati huu wanakuwa na maswali
mengi yakiwemo kuuliza mtoto anatoka wapi n.k wakati huu kama atajibiwa maswali
yake kwa usahii basi mtoto ataendeleza tabia ya Kujiamini na kuwa na uwezo wa
kuamua au kuanzisha kitu bila kutegemea msaada wa mtu lakini akivunjwa moyo
huanza kuwa na hatia ya kujihisi kuwa anaweza kusema au kutenda kisichofaa na
ataogopa kufanya mambo yake mwenyewe
Kujijenga
na kuzalisha au kujiona duni na kushindwa Industry & inferiority
Jambo hili
hujitokeza kati ya umri wa miaka 6-11 katika wakati huu mtoto huanza kusahau
ndoto zake na matarajio yenye matumaini na kuanza kujishughulisha kubuni na
kutenda kwa bidii ili kuzalisha anajitahidi kuwa bingwa wa kuanzisha jambo na
mbinu zake hukua na huumbiwa shauku ya kutimiza mambo anajifunza kuchukuliana
na matatizo au maswala ya kifamilia na shuleni anapotiwa moyo wakati huu
anajijengea moyo wa kukamilisha yale aliyoanza na anapovunjwa moyo anajiona
duni
Kujitambua
au kujichanganya Identity & Role confusion
Hali hii huwapata
watu wenye umri kati ya miaka 12-18 katika kipindi hiki kundi hili hukumbana na
mapinduzi ya kisaikolojia katika wakati huu kijana huanza kujitambua na kwa
kawaida huanza kujitenga mbali na wazazi na kujijumuisha na kundi rika la
wenzake wakati huu wa mpito wao hujitahidi kujistawisha mwenyewe mbali na
wazazi wakati huu kijana hujitambua kuwa ni mwanamke au ni mwanaume katika
wakati huu kijana asiposaidika kujitambua vema atajichanganya katika kuelewa
Jukumu lake na inaaminika na watafiti wengi kuwa hali ya usagaji au ushoga
hujitokeza katika wakati huu katika kundi hili linaposhindwa kujitambua
Mwingiliano
au upweke. Intimacy & Isolation.
Hali hii hujitokeza wakati wa ujana wakati
huu kijana anahitaji kujichanganya na kuingiliana na vijana wenzake mwingiliano huu pia hujengeka kutoka katika
ngazi ya kujitambua ambapo kama ngazi ya kujitambua kwa kijana haijajengeka
vema au akasumbuliwa katika kujua namna ya kujichanganya na watu wengine
anaweza kupata tatizo la kuwa tayari kujitambua au kuingiliana na wengine na
hivyo anaweza kushindwa kujichanganya hata na watu wa kundi la jinsia yake au
ile nyingine na matokeo yake ni kuwa mpweke akijifunza vizuri anakuwa tayari
kushiriki na wengine kimwili kimawazo na kihisia lakini inapokuwa kinyume chake
mwingiliano na watu wengine litakuwa swala tishio kwake na upweke utatokea hii haimaanishi kuwa mtu wa
jinsi hii hataoa au kuolewa lakini hata
ndoa yake haitakua au kuendelea na hatakuwa na ukaribu na mwenzi wake matokeo kila
mmoja atakuwa kivyakevyake
Kujumuisha
na kujisahau Generativity & self-Absorption, au stagnation (Middle age)
Hali hii hujitokeza katika umri wa kati
wakati wa kazi za uzalishaji wakati huu akili inafikiri zaidi maswala ya
kustawisha kizazi kijacho, atawaza zaidi juu ya familia yake na wengine kwa
ujumla katika kufikia wawe na hali nzuri kwa ujumla wakati huu anaweza kuacha
hata jambo la muhimu kwa ajili ya jambo analofikiri kuwa litakuwa la muhimu
zaidi anakuwa na miaka mingi ya kazi na kusumbukia maisha jambo hili
linaposhindikana mtu huyu anaathirika na kukata tamaa au kudumaa au kujidharau.
Kujikubali
na kukata tamaa Integrity & Despair
Hali hii hujitokeza katika umri wa utu
uzima ambapo mtu hujikubali au hukubaliana na hali zilizoko za mizunguko ya
maisha kwamba ndivyo yalivyotakiwa yawe katika wakati huu kama mtu hajafanya
mambo ya maana huona kuwa muda ni mfupi kukamilisha jambo lolote na hivyo
hukata tamaa na kuona kua amechelewa na wakati huu hujiandaa kuridhika na
kujiandaa kwa safari ya kuondoka duniani wakati huu nguvu za kimwili zinakuwa
zimepungua na anaanza kuakisi aina za maisha walizoishi enzi hizo kama
alifanikiwa kujiandaa vizuri na kuwafanikisha wanawe atajiandaa kufa katika
hali nzuri lakini kama hukufanya mambo vizuri anatamani angeongezewa muda ili
arekebishe mambo lakini muda ndo hivyo tena katika wakati huu uzee wa mtu huyo
utakuwa uliojawa na uchungu na wenye
kukatisha tamaa Paulo mtume aliyefanikisha kazi ya Mungu vema anasema katika
1Timotheo 4;7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri na kwa furaha anatazamia mwisho
mwema, kwa walioshindwa wanabaki kusema ningelijua ningelijua! Huu ni wakati wa
majuto wa aina za maisha Mwanzo 47;8-9.
Maendeleo
ya uwezo wa akili za mtoto
Mwanasaikolijia wa
Ki Swiss Jean Piaget alitoa mchango mkubwa sana wa ufahamu kuhusu makuaji ya
watoto kiufahamu na kifikra alimtumia zaidi ya miaka 50 hivi katika utafiti
wake na kwa umakini alichunguza watoto na ukuaji wao mchango wake una msingi
mkubwa katika kuwafahamu watoto na kujua namna wanavyojifunza na kuwaelimisha
yeye aligawanya vipindi vikuu vinne ambavyo haviwezi kujitokeza mpaka mtoto
amefikia hatua ya tatu ingawaje watoto
hujifunza katika mtiririko wa maswala matatu Kibaiolojia, kihamasa na uzoefu wa
kujifunza lakini yako mambo yanayoweza kuchangia kitu katika makuaji ya mtoto
Chati
ifuatayo inaonyesha hatua za mtoto katika kukua kiakili
HATUA
ZA UKUAJI KIAKILI
|
MUDA
MUAFAKA
WA
KUJIFUNZA
|
SIFA
ZA NAMNA ANAVYOJIFUNZA
|
Kipindi cha kuhisi sensorimental
stage
|
Kuzaliwa – miezi 18
|
Wakati huu hugusa kile
kinachoonekana mbele yake vinavyofichika hawezi kujua wala kuviona, hufuatilia
lolote linalomjia au analoliona huweza kushika hiki au kuacha na kuamua
kufuatilia kingine
|
Kipindi kabla ya
kujishughulisha
Prioperation
|
Miaka 2- miaka 7
|
Hutatua tatizo kwa kujaribu na
kushindwa, anafungwa na kile anachofikiri tu na kukiona hawezi kutofautisha mambo baina ya vitu
viwili mfano maji na chupa au chupa tupu
|
Kipindi cha kuumba au
kuchanganuamambo
Concrete operations
|
Miaka 7-miaka 11
|
Anaanza kufikiri kwa usahihi hata vitu vilivyochanganyika, kujua vipimo
vya kitu au vitu kujaa au kupungua
|
Kipindi cha kujua
mambo kwa usahii zaidi
Formal operation
|
Kuanzia miaka 11 na
kuendelea
|
Anaweza kufumbua mafumbo na
kuhusika na vitu na uchambuzi wa mambo anajifunza kufikiri kabla ya
kutenda na kupangilia au kuoanaisha
|
Maendeleo
ya kimaadili ya mwanadamu
Mwanasaikolojia
Lawrence Kohlberg naye alichanganua hatua sita za ukuaji wa kimaadili wa
mwanadamu ambapo alidai kuwa kabla mwanadamu hajafikia hatua ya juu kabisa ya
kimaadili lazima apitie hatua hizo mtu anapokuwa na hatua ya juu zaidi ndipo
anapoweza kuonyesha sifa za hatua ya chini yake ingawaje mtu aweza kuwa na
hatua ya juu zaidi kuliko nyingine lakini kadiri anavyokuwa katika hatua ya juu
zaidi ndivyo anavyokuwa na uwezo wa chini wa kutambua hatua alizoziruka
kimaadili
|
||||||||||||
Hatua ya 4 kipindi cha kujitibu kitabia wakati wa kuwa chuoni 20
|
SAIKOLOJIA YA ASILI YA MISUKUMO YA
MWANADAMU
Tunawezaje
kuelewa mahitaji, hamu, tamaa, matakwa na shauku zinazosababisha watu kuwa na
tabia fulani? Kwa nini baadhi ya watu wana misukumo inayowahusisha na jamii au
matakwa ya jamii na wengine wanaweza kuwa wahalifu na hata kupoteza maisha?
Majibu ya maswali haya yanatupa au yanafunua nguvu au ugumu wa kuelewa misukumo
ya mwanadamu katika maisha kwa msingi huo tunapojifunza kuhusu misukumo
tunapaswa kujifunza katika Nyanja mbalimbali za maisha ikiwemo utendaji wa
mawazo, misukumo, migawanyo ya mwili na utendaji mzima wa ubongo wa mwanadamu.
Misukumo na Mihemko
Kujifunza
kuhusu misukumo ni kujifunza namna tabia inavyoanza kujijenga. Kimsingi hapa
tunajifunza jinsi utendaji wa ndani wa mwili wa mwanadamu na mahitaji ya ndani
ya kibaiolojia mihemko vichocheo vya kimazingira na hamasa za ndani za mwanadamu zinazo sababisha mwanadamu kuwa na tabia
fulani ili kutimiliza mahitaji matakwa na malengo mengine ya baadaye
Mihemko
hufanya kazi kama vichocheo vya ndani ambavyo huathiri uwezo wa kufukiri kuhisi
na kutafasiri uthamani na kujenga tabia mihemko ya kibaiolojia inatokana na
maumbile ya kawaida ya mwili kukosekana kwake kunachochea mwanadamu aweze kuwa
na tabia fulani ambayo huamini kuwa itaondoa hali aliyo nayo, mihemko ya
kijamii inaambatana na vichocheo vitokavyo katika mazingira kwa mfano kusikia
harufu ya chakula kunaweza kusababisha wewe kusikia njaa hata kama bado ulikuwa
hujasikia njaa
Ufahamu
kuhusu mihemko yetu na mahitaji yetu
kutahamasisha kujitosheleza katika mahitaji yetu kama mtu atakuwa na uwezo
na akafanikiwa kutosheleza mihemko yake
hisia za kupendeza zitafuatia na asipofanikiwa atajijengea tabia ya kutoridhika na kuendelea
kutafuta kujitosheleza inagawaje mihemko
hiyo na matakwa hayatakuruhusu wakati
wote kufanya mambo kwa usahii kwa mfano mtoto anaweza kulilia chakula hata kama
ameshakula chakula cha kutosha tu na mtu mzima aweza kuvutiwa kununua nguo mpya
hata kama anazo nguo za kutosha
Tendo
hili linapojirudia rudia linaweza kujenga tabia na linaweza kutabirika
kisaikolojia lakini likidumu zaidi linaweza kumsababishia desturi au mazoea ya
kudumu ambayo ni vigumu kuyabadili lakini hili linategemeana pia na uwezo wa
kiakili wa mwanadamu huyo na utayari wake katika kubadilika kwani kama
mwanadamu hajataka kukubali kuibadilika hatuwezi kusaidia kubadilika kwake
hivyo hapa tunaona mabadiliko au mchakato wa hali ya misukumo inavyoweza
kupelekea tabia kujengeka
Hata
hivo ni muhimu kufahamu kuwa misukumo haiwezi kuchunguzwa katika hali ya moja
kwa moja bali inachunguzwa kwa kupitia tabia iliyozaliwa ingawaje kuna njia kuu
tatu za kupima nguvu ya misukumo
·
Nguvu
inayozalishwa – katika kumpatia mtu hali yoyote ya Shughuli je ni namna gani
mtu huyo ni mgumu katika kutekeleza Jukumu fulani alilopewa kulikamilisha
·
Uvumilivu
– Je pamoja na vikwazo anavokutana navyo je mtu huyu ni mvumulivu kiasi gani
katika kukamilisha malengo aliyopewa?
·
Matumizi
ya tabia mbalimbali na kuingilika – kama hizo za kwanza hazionyeshi matokeo je
ni ubunifu kiasi gani alionao mtu katika kujaribu kuyafikia malengo?
Kama
malengo ya chuo ni mtu kupata Diploma tunaweza kupima ni jinsi gani Mwanafunzi
anajitihada kila wiki anaendeleaje katika kusoma ni mbunifu kiasi gani katika
usomaji wake ili kufikia lengo la chuo? Lakini njia hii ya tatu itapimwa kama
ile ya kwanza haijaonyesha matokeo
Misukumo
ya msingi na ya asili
Mwanadamu pamoja
na wanyama woote wanayo misukumo ya kibaiolojia inayo usisimua, mfumo wa fahamu
pale inapokosa kutimizwa au inapopungua hali ya kuhitaji hujitokeza misukumo
hii inaweza kuzalisha tabia, mihemko, hisia au uhitaji misukumo hii ni kama
vile;-
1.
Njaa – husababishwa na kemikali
zinazozalishwa katika damu kupitia maumbile ya tumbo na hivyo kuzalisha hisia
ya njaa au kuhitaji kula kutokana na taarifa hizo kuufikia ubongo.
2.
Kiu – Cell zote au chembechembe zote
katika mwili wa mwanadamu zinahitaji maji hitaji hili linazalisha kusikia kiu
au hitaji la maji mara kiwango cha mahitaji ya maji kinaposhuka au kuwa chini
ya kiwango kinachohitajika taarifa huufikia ubongo na akili huanza kujua hitaji
la maji
3.
Hali joto – mabadiliko katika mazingira
lazima yatokeapo mwili huitaji kiasi cha joto lake kikae sawa kulingana na
mazingira husuika hivyo mwili huzalisha hali ya kutaka kuweka hali joto ya mwili
sawa kulingana na mazingira “Tempereture
adjustiment mechanism” katika wakati huo mtu huweza kusikia joto au baridi
n.k mishipa ya Damu hupanda juu kama kuna joto au kuzama chini kama kuna
baridi, hizi ni hali zinazojizalisha zenyewe katika mwili bila kutumia akili.
4.
Kujisaidia – Mwili unahitaji kutoa uchafu
au mabaki ya vitu visivyofaa baada ya matumizi yake au baada ya kuondoa
virutubisho vinavyohitajiwa na mwili kutoka katika vitu tulivyokula vinapotaka
kutoka mwanadamu hujisikia hali ya kutaka kujisaidia baada ya ubongo kufasiri
5.
Ngono – Tezi katika mwili wa mwanadamu
huzalisha estrogen kwa mwanamke na androgen kwa mwanaume vinavyoamsha
vichocheo katika mwili wa mtu na kuleta mhemko unaohitaji tendo la ngono ili
kupunguza msukumo huo wa hitaji la kingono wakati mwingine vichocheo hivyo
huweza kuamshwa kwa mazingira, mazungumzo, kuguswa au kusikia na ubongo kuelewa
na kutafasiri hitaji hilo na kuzalisha nguvu za kutaka kutimiza shauku ya
kingono.
Misukumo
ya msingi ya kijamii
Kila mwanadamu
anauhitaji wa kuwa na wanadamu wenzake kuliko kuwa peke yake hali hii huzalisha
msukumo wenye nguvu wa kuwa na wengine, katika hali hii ya kuhitaji
kujichanganya yako mahitaji ya msingi ya mwanadamu ya kimisukumo katika jamii
misukumo hii ni kama ifuatavyo;-
·
Kutaka
kuwa juu - hii ni hali ya kukataa kujiona duni miongoni mwa watu kwa mujibu wa
Dr Alfred Adler aliamini kuwa ni hali
inayojitokeza ili kuziba ile hali ya kujiona duni au hisia zisizozuilika za
kujiona duni na hii hutokea kimaumbile wala si kama watu watakavyo
·
Kutaka
Kutambulika – hii ni hali ya kutaka wengine watambue kuwa tumefanya nini katika
maisha yetu ili kukubalika au kusifiwa au wajue tu kuwa upo na wewe
·
Kutaka
ulinzi – Dr Erick aliamini kuwa kuishi katika jamii ni asili ya mwanadamu
katika maisha kwa ajili ya mahitaji ya kisaikolojia na kujihisi salama au kwa
ajili ya usalama unaotokana na kuwa katika kundi au jamii
Matokeo
ya mahitaji ya kuwa juu kimaendeleo
Inapotokea mtu
amekuwa juu kimaendeleo kulingana na tamaduni za kila mahali zenye kumaanisha
kuwa mtu amefanikiwa kuwa zaidi ya wengine kwani hili ni lengo la kila mwanadamu
wanayo hulka ya kuataka kufikia kiwango fulani na wanapokuwa wamefanikiwa
kukifikia, Winterbotton aliwasoma wanadamu mwaka 1953 na kugundua kuwa
wanapokuwa wamefanikiwa wanakuwa na tabia ya kushindana kuzuri na kuwa na
marafiki wengi lakini mambo haya pia hujitokeza
a.
Wanakuwa
na tabia ya kujilinganisha need for social comparison
b.
Anahitaji
la kusikilizwa na kuwa na au kujiunga katika kundi na haitaji kuwa peke yake
c.
Anahitaji
kuwasaidia wengine hii ni tabia inayoumbika wakati mwingine kwa ajili ya kutaka
sifa au kuitambulika au kutambua kuwa kuna wengine baada ya wewe kuwa
umenusurika 2Falme 7;3-11
d.
Anatafuta
kujilinganisha kulingana na uzito wake hii ni hali ya kuwa na jamii ya watu
wenye hadhi kama yake kwa kawaida kama mtu amefanikiwa atahama manzese na
kwenda masaki au mwakizaro kwenda Raskazone ili kujijumuisha na watu wa hadhi
yake au kundi lake hii ipo hivyo kielimu na katika mafanikio mengine watu wenye
degree hujitenga na wa diploma waalimu na wanafunzi ili kujazia ulinganifu wao
Kilele
cha mahitaji ya msingi ya misukumo ya mwanadamu
Kwa mujibu wa Dr. Abraham Maslow aliamini
kwamba mahitaji ya mwanadamu yana jiorodhesha yenyewe hadi kileleni kama ngazi
unayoweza kuipanda kutoka katika mahitaji muhimu mpaka kujitambua au
kujitosheleza kwa maana nyingine ni kuwa wanadamu wana tabia ya kutafuta
kujiridhisha katika hitaji moja la ngazi ya chini kabla ya kufikia lile la
ngaji inayofuata kwa mfano kama mahitaji ya kimwili ya kawaida kama chakula, maji, hayajakamilishwa kwa kawaida nguvu kubwa ya mwanadamu
itaelekezwa katika mahitaji hayo kwanza ambayo ni mahitaji ya kisaikolojia, (Psychological Needs) hayo yanapokuwa
yametoshelezwa mwanadamu huamia katika hitaji lingine na kwa haraka atapata
misukumo ya kutaka kuwa na mahali salama pa kukaa (Safety Need) na baada ya hilo kutimia ndipo linapokuja hitaji la
kupenda watu wengine au mtu mwengine (Love
Need) baada ya hapo ndipo mwanadamu huitaji kujiona kuwa anastahili/anajitambua
(Esteen Need) na mwisho ndipo
mwanadamu hujiona anaweza kufanya chochote awezacho kukifanya kupitia vipawa
vyote na uwezo woote ambao Mungu amempa kwa nguvu zote hapa mwanadamu hujiona
kuwa amejitosheleza (Self Actualization Need). Hivyo katika mahitaji haya ya kilele cha
mwanadamu tunaona jinsi mahitaji ya kimwili na kisaikolojia yanavyo chukua
nguvu kubwa ya mahitaji ya misukumo ya mwanadamu na mahitaji yale mengine
yanahitaji mwingiliano na watu wengine na hivyo huwa ni mahitaji ya kijamii
zaidi na hivyo mengi ya nayozalishwa na tabia zetu yanalenga kufikia malengo
hayo tuliyo nayo katika akili au fahamu zetu.
Kilele cha ubora wajuu zaidi wa Mwanadamu ni kujitambua
Hivyo katika
mahitaji haya ya kilele cha mwanadamu tunaona jinsi mahitaji ya kimwili na
kisaikolojia yanavyo chukua nguvu kubwa zaidi ya mahitaji ya misukumo ya mwanadamu
na mahitaji yale mengine yanahitaji mwingiliano na watu wengine na hivyo huwa
ni mahitaji ya kijamii zaidi na hivyo mengi ya nayozalishwa na tabia zetu
yanalenga kufikia malengo hayo tuliyo nayo katika akili au fahamu zetu.
Asili
ya misisimko ya mwanadamu
Misisimko katika hali
ya mwanadamu hutofautiana kutokana na mabadiliko ya mwili na hali ya akili
misisimko inafanana sana na misukumo lakini misisimko ni ya ndani zaidi na
inahusika zaidi katika kuyafikia malengo,Tunaweza kufikiri kuwa misisimko ni mahitaji
ya kimwili na kisaikolojia mwili unabadilika hali kutokana na hali fulani
zinazoamka katika vichocheo au kutokana na mabadiliko ya damu au hali fulani ya
kiakili inapopata usumbufu lakini pia inaweza kusababisha mabadiliko katika
hali ya kisaikolojia kwa mfano unaona umuhimu wa kumalizia sura hii ya kitabu
lakini sina msukumo wa kuendelea hili linaweza kutokea kwa sababu ya kuchokozwa
au kusumbuliwa kwa hisia
Maendeleo
ya Misisimko
Kwa kawaida
tunazaliwa tukiwa na uwezo kamili wa kuwa viumbe wenye misisimko lakini baadhi
ya misisimko huchukua Muda kuumbika kwa mfano mtoto mdogo anazaliwa huku akiwa
na uwezo wa kuonyesha kabisa kusisimkwa kimwili na kiasaikolojia lakini baada
ya miezi kadhaa mtoto huanza kuonyesha mabadiliko ya kimsisimko kwa namna pana
zaidi hii inatokana na ukuaji wa ubongo na kadiri mwanadamu anavyokua ndipo
anapojifunza kiwango fulani cha kusisimkwa kutokana na yale aliyojifunza tangu mapema.
Mabadiliko
ya mwili katika mabadiliko ya kihisia
Ni wazi kuwa maswala ya misisimko si ya
kisaikolojia tu bali ni ya kimwili pia kwa sababu hisia zinazo inuka juu ya mtu
si zote zinachochewa na hali halisi za kimwili kama zifuatazo
·
Ukuaji
wa moyo
·
Mfumo
wa ulainishaji chakula kuwa chini au kutofanya kazi kabisa
·
Tezi
zilizoko katika ini ziitwazo kitaalamu adrenal
glands zinapofanya kazi kwa kasi sana na kuzalisha vilainisha chakula kwa
wingi adrenalin
·
Mtiririko
wa damu katika mikono na miguu unapoongezeka
Hali hizi zote za
mabadiliko katika mwili zinaruhusu mchakato wa kumuinua mwanadamu katika hali
fulani ya nguvu ya kuitikia mambo au misisimko katika wakati huo huo mtu huyo
akihitaji mabadiliko kwa hivyo mwili utajiandaa kucheza au kufurahia au
kujilinda au kufanya chochote kulingana na hali ambayo mwili unaokabiliana nayo
ndipo tunapata vitu kama woga, hasira, au furaha n.k.
Hisia
na Misisimko
Hisia na misisimko ni nyanja zinazo angukia kwa wingi katika
dimbwi la kisaikolojia zaidi kuliko kimwili ingawa vinaingiliana lakini vingine
husababishwa na vichocheo fulani vinapoamshwa au kuchochewa hata hivyo utendaji
huu mzima wakati mwingine una uhusiano na utendaji wa mfumo wa ubongo
Ufahamu
wa jumla kuhusu ubongo
Una sehemu kuu
tatu yaani
·
Medula Oblangata huu ni ubongo unaopokea taarifa
kutoka katika mishipa ya fahamu Nevers kupitia katika uti wa mgongo
·
Cerebllum huu ni ubongo wa pili unaopokea
taarifa kutoka ubongo wa kwanza na kuzirekebisha ili kuzipeleka katika ubongo
wa tatu ili kutafasiri na kupata majawabu au nini cha kufanya
·
Cerebrum huu ni ubongo wa tatu unaopokea
taarifa toka ubongo wa pili Cerebllum na
sehemu nyingine za karibu za ufahamu kama macho, pua na masikio na kutoa majawabu
kwa kupeleka viashiria Signals kwa viungo husika ili kutafasiri au kutoa uamuzi
nini kifanyike mfumo huu hufanya kazi kwa kasi ya ajabu kupitia mifumo miwili mikuu
ifuatayo
·
Mfumo
wa mishipa ya fahamu Nervours system
mishipa hii iko kwa mamilioni ya nyuzinyuzi za nyama zinazopeleka taarifa
kutoka kila eneo la mwili wa mwanadamu kwenda katika ubongo na kutoka katika
ubongo kwenda katika viungo husika
·
Mfumo
wa utendaji wa tezi Endrocine System
hizi ni aina za tezi glands ambazo humwaga aina fulani ya dawa hormones na
kusambaza katika mishipa ya damu ili kutayarisha mwili kwa huduma au tukio
maalumu
Utendaji huu wa
mfumo wa ubongo na mwili na mahitaji ya kisaikolojia vyote vinahusika katika
utendaji wa hisia na misisimko
Woga.fear.
Msisimko wa
kihisia unaotokea ili kukabiliana na hali zenye kutosha au kuogopesha kwa kawaida woga huwa tunazaliwa nao mfano
mtoto mdogo anaposikia sauti ya kitu kikubwa ghafla au kilichoanguka na kutoa
mlio huweza kuogopa huu ni woga wa Kuzaliwa hata hivyo Matendo mengine ya woga
au yanayochangia woga hivyo huo utakuwa
ni woga wa kujifunza kutokana na mazingira ambao hujengeka hata kufikia hatua
ya kuogopa kufanya jambo katika jamii kwa kuogopa kukosea lakini woga wa
kuogopa kufa huu ni woga wa kawaida
Wasiwasi
Anxiety. Tunasikia
woga kwa sababu fulani au katika Matukio maalumu ya kututisha lakini tofauti na
woga wasiwasi ni hali inayo fanana na woga ingawa wakati mwingine hali ya
wasiwasi inaweza isiwe rahisi kuelezeka ni kama woga unaoelea hujulikani sababu
au ni hisia za hofu inayotokana na jambo lililo tokea au litakalotokea wasi wasi husababisha ubongo Cerebrum
kuzalisha nguvu nyingi katika mfumo wa damu unaofanya damu nyingi kuhitajika
katika kuendesha ubongo kuzalisha nguvu ya kisaikolojia kukabiliana na hali
halisi pia huweza kusababisha Kuzaliwa kwa Hormones iitwayo adrenaline kuachiwa
katika mishipa ya damu na kumfanya
mwanadamu kujiandaa kukabiliana na hatari au kukimbia hivyo kadiri mtu
anavyokuwa na waoga au wasiwasi sana husababisha kuzalishwa kwa kemikali hiyo
kwa wingi katika damu yake na matokeo yake huweza kusababisha tabia ya hofu au
hasira na hatimaye muhusika huathiri afya yake ndio maana Biblia inasema
furahini katika Bwana tena nasema furahini
Msongo
wa mawazo Depression
Msongo wa mawazo
ni moja ya matatizo makubwa sana kwa kizazi hiki kwa ujumla huu ni ugonjwa wa
moja ya matatizo ya kiakili hujumuishwa na mchanganyiko wa matatizo mengine
kama kukata tamaa, kujiona hufai, upweke hali ya kutokujisikia vizuri kwa
ujumla ni hali ya kihisia inayohusisha kutokujisikia vizuri wakati mwingine
huambatana na kilio au maumivu ya ndani ni kama inafanana na hali ya wasiwasi
isipokuwa hii ni nzito
Hasira
Anger
Ni msukumo wa
ndani wa kukabiliana na hali iliyopo kutokana na kile tunachokiona kuwa ni haki
yetu kuathiriwa yaani mtu anapata hasira kwa sababu fulanihasa kwa kuharibiwa
lililo haki yake “Violate the rights of a Person” Hasira ziko za aina
mbalimbali kwa mujibu wa Biblia Efeso 4; 31-32, hasira inatajwa katika ngazi
tofauti tofauti “Ondoeni kabisa uchungu, ghadhabu, hasira, makelele na
masingizio pamoja na kila aina ya uovu. Iweni wafadhili na wenye kuhurumiana
ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo
alivyowasamehe ninyi.” wakati mwingine mtu mwenye wasiwasi huwa na hasira na
mtu mwenye hasira huwa na wasiwasi kuna aina mbalimbali za hasira kama Biblia
ilivyoainisha hapo juu
·
Uchungu
“Bitterness” - hali ya kutaka
kumfanyia mtu jambo baya au kutaka baya limtokee kama kisasi kwa mambo
aliyokufanyia
·
Kuwa
na kusudio ovu “Malice”au nia ya kutenda mabaya pia hutokana na kuchokozwa au
kuingiliwa kile ambacho akili yako inakiona kuwa ni haki yako na malipo ni
ubaya unaoukusudia
·
Mgomo
“clamour”- hii ni hali ya kudai
jambo kwa ghasia na kelele au kusababisha vurugu au kugoma ni hasira itokanayo na
kudhulumiwa,kukandamizwa au kile akili inachokiona kuwa ilikuwa haki yako
kufanyiwa
·
Uchungu
“Envy”- Ni uchungu unaotokana na
mafanikio ya mtu mwingine
·
Kujisikia
vibaya “Resentment”- kujisikia
vibaya kwa sababu ya hali ya mtu au mafanikio yake
·
Kushindwa
kuvumilia “Intolerance” – ni hali ya
kushindwa kuvumilia na kukubali kuwa
tayari kutenda jambo litakaloleta madhara
·
Kukosoa
“Criticism” - ni hali ya kusuta kwa
Maneno ya hukumu au kukosoa au kutafuta
kosa katika kila jambo hata zuri likitendwa na mtu aliye na uhasama nawe
·
Kisasi
“Revenge”- kujibu kwa kufanya jambo
baya kwa sababu ulifanyiwa jambo baya kwa Maneno au kwa vitendo
·
Ghadhabu
“Wrath”- Hasira kali au uchungu
mzito ulio tayari kufanya jambo baya sana
au kitendo kiovu kikubwa
·
Chuki
“Hatred”- hali ya kutokukipenda kitu
au mtu kutotaka hata kumuona au
kujisikia vibaya unapomuona na wakati mwingine kumkusudia mabaya
·
Uchochezi
“Sedition”- hutuba au mazungumzo
yenye kuamsha hasira ili watu waasi au wagome au wachukue hatua kali dhidi ya
kile kinachochochewa
·
Wivu
“Jealousy”- hali ya chuki
inayokusudia kumshinda mtu au kumtakia
mabaya au awe chini au akome wakati mwingine kwa sababu ana ubora unaozidi wako
·
Uvamizi
“attack” – hali ya kumshambulia mtu
kumuumiza au kumuangushia kipigo
·
Kusengenya
“Gossip” – ni hali ya kumsenenga mtu
kwa Maneno au kwa maandishi au kutumia nafasi uliyo nayo kukanadamiza
·
Kudhalilisha “sarcasm”- ni mazungumzo yenye uchungu yanayolenga kumdhalilisha ama
kumuumiza mtu au kudhalilisha hata ingawaje yaweza kuzungumzwa kama utani
·
Kutokusamehe
“unforgiveness”- hali ya kutokuweza
kuachilia kabisa kutunza lawama moyoni siku zote kwa sababu ya jambo fulani
ulilotendewa lenye kuumiza
Madhara
yatokanayo na hasira
a.
Humfanya
mtu aache kuwa mwenyewe na hivyo kuweza kutoa maamuzi ya kinyama au kufganya
bvitendo hangeweza kufanya kama angekuwa hajakasirika
b.
Huumiza
halui za kihisia na kuharibu amani na upendo
c.
Husababisha
Stress au hormonies kuenea mwilini na kubaki kwa muda mrefu na huweza
kujitokeza kutoka kazini kwenda nyumbani na kadhalika au hata makanisani na hii
inakufanya uwe mtumwa wa yule mtu unayemchukia
d.
Husababisha
matatizo ya kijamii hutatakiwa katika jamii yoyote wakati mwingine vita huweza
kutokea kwa sababu ya watu wenye hasira
e.
Kunakuwa
na madhara ya kiafya kwa mtu mwenye hasira asilimia 60% - 90% ya magonjwa ya
moyo na Emotion disorders husababishwa na hasira hii huathiri utendaji wa mfumo
wa fahamu na kuleta maafa kadhaa, kuathiri mzunguko wa damu na kudfhuru viungo
kama fogo, nyongo, utumbo n.k kunaweza kuweko kwa madonda ya tumbo na maumivu
ya kichwa au kukosa usingizi kwa sababu ya kusukumwa kwa damu nyingi kwenye
ubongo kuliko inavyotakiwa
f.
Kuathiri
uhusiano wako na Mungu kuathiri utendaji wa Roho Mtakatifu na kasi ya kutumiwa
na Mungu au kuzuiliwa maombi yako
Furaha.
Hii ni hisia au
Msisimko wa kihisia unaonyesha ya kuwa mambo ni mazuri na ya kufurahisha hii ni
kinyume kabisa na mgandamizo wa mawazo au hasira mtu anapokuwa na furaha maisha
huwa na maana na hujisikia vema anakuwa na matumaini na kunakuwa hakuna hofu
wala hasira wala wasowasi matumaini ya mbele huwa mazuri wakati mwingine hali
ya hisia za ndani huweza kujitokeza usoni lakini si kila wakati ikawa ni sahii
Furaha
Hisia zetu za
ndani zinaweza pia kuathiri ile tabia yetu yanje au muonekano wetu wa nje nyuso
hizi mbili moja inaonyesha furaha na ya pili inaonyesha huzuni muonekano ho ni
athari ya ndani ingawaje wanasaikolojia hawakubali kupima kwa muonekano tu
wanataka kuenda ndani zaidi ya hapo
Muonekano
wa kweli wa Hisia
Muonekano wa kweli
wa hisia za wanadamu hazionekani kupitia usoni pekee kwani wanasaikolojia wengi
huamini kuwa uso unaweza kukudanganya na usipate usahii wa mambo wao wanapima
hisia hizi kupitia njia zifuatazo
1.
Yakupendezayo
na yasiyokupendeza
2.
Yakuchukuayo
na yasiyo kuchukua
Wanasaikolojia
wanaaminikuwa kupitia aina hizo mbili za misukumo unaweza kupima muonekano wa
hisia za kweli kuliko kutegemea uso pekee ambao hauleti majibu ya kweli ya
kihisia, ni wazi kuwa mtu akifurahi uso hushuka na tabasamu huonekana na mtu
akikasirika uso hupanda na kuonyesha kutokufurahi hivyo kwa namna fulani mtu
aweza kusoma Saikolojia ya tu usoni lakini hii ni sawa na kusoma box na kujua
kilichomo ndani lakini wakati mwingine box hilo halina hicho kinachofikiriwa
kuwa kimesomwa hivyo kisaikolojia
tunapaswa kwenda ndani zaidi ya uso wa mwanadamu
SAIKOLOJIA YA
UFAHAMU AU TABIA ZINAZOJENGEKA KUPITIA MITAZAMO SENSES & PERCEPTIONS
Tunaufahamu
ulimwengu huu na kufurahia jinsi ulivyo na rangi nzuri vivuli, sura mbalimbali
za kupendeza milima kwa mabonde pia sauti nzuri na makelele baridi na joto
ukavu na takataka maumivu na hali nzuri utamu na uchungu hii yote ni kupitia
milango yetu mikuu mitano ya fahamu hivyo tunaujua ulimwengu huu kupitia
milango hii mitano ya fahamu hivyo milango hii mitano ya fahamu ni ya muhimu
sana katika maisha yetu kwani kwa hiyo ndiposa tunaweza kujua au kugundua mambo
fulani yanayopelekea kusisismka
Kuona, Kusikia, Kuonja, kunusa na kugusa hukamilisha milango mitano ya fahamu
Milango
mitano ya fahamu ni mfumo muhimu na maalumu sana wa viungo vya fahamu
vinavyowekwa katika kundio hili ni viungo vyenye uwezo wa kutafasiri hisia za
kawaida kuzipeleka katika hisia za kufahamu kwa mfumo wa fahamu uitwao Nerve
impulses ambayo tungweza kusema lugha ya kiufahamu au midundo ya kiufahamu katika mfumo wa ubongo kwa mfano kitu
kinapogusa ngozi yako kinatafasiriwa katika midundo hiyo ya kiufahamu ili
kwamba ubongo uweze kutambua na kurudisha tafasiri kwa kasi ya ajabu na ndipo
ufahamu kamili wa hicho kilicho kugusa hujitokeza ufahamu huu hupitia mishipa
ya fahamu mpaka kupitia katika uti wa
mgongo na kutumwa katika ubongo na ubongo kutafasiri na jibu la ulichokigusa
kupatikana na ndipo tunajua nini kinatuzunguka
katika ulimwengu huu tulio nao
Kusikia
Ni
moja ya kiungo cha ajabu sana na cha kipekee yaani sikio kinasafirisha au
kutafasiri mawimbi ya sauti kutoka katika mazingira kupeleka katika
midundo na inapofikishwa katika ubongo
ule wa kati hutafasiriwa na ndipo tunaweza kujua kile tunachokisikia kama ni
mlio wa ndege radio n.k mawimbi ya
muungurumo fualani yanapoigia sikioni hugonga ngoma za masikio ziitwazo eardrum
ni kama ngoma za kawaida lakini ni ndogo sana na laini sana na ziko makini
sana na hivyo ngoma hiyo hutikiswa na
ndipo inapogeuza midundo hiyo nakuipeleka katika sikio la kati ambalo lina vijifupa vitatu vidogo ambavyo
hubeba mitetemo ile katika sikio la ndani na
sikio hilo hutafasiri ile midundo katika mtetemo wa midundo ya ufahamu
ambayo hupeleka katika ubongo na kutafasiriwa ndipo sasa tunaposikia sauti ya
asili ndani ya ubongo na sio huku nje hewani mambo haya hufanyika kwa kasi sana
na kasi ya ajabu ni zaidi ya mara kumi kuliko sekunde kiasi cha kufikiri kuwa
tunaisikia sauti hiyo moja kwa moja hii ni kwa sababu kuu mblili
1.
Namna ya muundo wa Umakini wa sikio na sikio la kati na la ndani
2.
Ukaribu wa sikio la ndani na mfumo wa Fahamu nerve
Aidha
sikio la kati pia hufanya kazi za kumfanya mwanadamu asimame na kutembea wima
bila kuanguka yani hutupatia Balansi huweka uwiano wa mwanadamu
Njia kuu tano za
fahamu zilizo makini sana katika utendaji wa mwanadamu duara kubwa kabisa
linaonyesha uwezo mkubwa kabisa wa ufahamu kupitia kiungo hicho na duara ndogo
ni uwezo mdogo kwa kiungo hicho katika kutupatia fahamu kuujua ulimwengu
Kuona
Moja ya kiungo
muhimu sana katika ufahamu wa mwanadamu ni kuona kuona ni kiungo muimu zaidi ya
viungo vingine vyote vya fahamu, Jicho limejengwa kwa ufundi mkubwa wa viungo
mbalimbali na limeumbwa duara kama mpira limejazwa kwa ute mzito unaolifanya
liwe la mviringo limeumbwa kwa kusudi la kutafasiri mwanga na picha kwa kupitia
mishipa ya mfumo wa fahamu na linafanya hivyo kwa njia ya kipekee sana
Picha hipitia katika mlango mwembamba
sana wa duara uitwao kitaalamu pupil au mboni kwa Kiswahili,mwanga unaoruhusiwa
kupita hudhibitiwa na kijinyama vinavyozunguka mboni viitwavyo Iris kijinyama
hiki hufunguka sana kunapokuwa giza na hufunga kunakokuwa na mwanga mwingi
mwanga hupita kulingana na ruhusa ya Iris na huingia katika lenzi (Lens) ambayo
inafanana na ile lenzi ya kamera baada ya kufika hapo nguvu ya mwanga huo inatupwa nyuma ya jicho huko husisimua cells
za jicho ambazo ziko kwa wingi zaidi ya cells 130 milioni hizi ni seli maalumu
za mfumo wa fahamu zinazotafasiri picha
kupeleka katika vijishipa vya fahamu impulses vijishipa hivyo
vitumikavyo mchana huitwa Cones na vitumikavyo usiku huitwa rods mara zote
Cones hufanya kazi ya kutafasiri vitu vya rangi mbalimbali na Rods hufanya kazi
ya kutafasiri vitu vyeusi na vyeupe
vivuli na kijivu vijishipa hivi huipokea picha katika eneo liitwalo
Retina ambako picha huangukia ikiwa kichwa chini miguu juu na hishafirisha
kupitia mishipa maalumu ya kuonea vitu iitwayo optic nerves kuelekea katika
ubongo huko picha hutafasiriwa na ndipo tunapoiona ikiwa sawasawa kwa rangi
zake na aina yake kazi hii hufanyika kwa kasi sana na ndipo tunaposoma tunaona!
Muundo wa jicho la mwanadamu kama jinsi
linavyoonekana kwa ndani
Kunusa
na kuonja
Viungo vingine vya
mfumo wa fahamu hufanya kazi kama ilivyo kwa sikio na jicho vifanyavyo aina
fulani ya vichocheo huweza kuufanya nerves maalumu katika pua kwa kunusa na
katika ulimi kwa kuonja na husafirishwa kupitia vijishipa vya fahamu katika ubongo
na na kutafasiriwa kama utamu au harufu wanyama wana uwezo mkubwa zaidi ya
wamwanadamu wa kunusa ili kuwinda au kujinusuru na kuwindwa na wanyama wenazao
katika ulimi kuna aina fulani ya mishipa ya kiufahamu iitwayo test Buds ambayo
ina uwezo wa kuhisi na kugundua aina nne za utamu yaani uchungu, utamu,
uchumvichumvi na ungwadu.
Kugusa
Mishipa ya fahamu
inayoweza kutafasiri mazingira ya asili kupeleka katika midundo ya mishipa
iliyomo katika ngozi kila eneo huweza kusafirisha hisia hizo mpaka katika ubongo
mishipa hii kama ulivyo utendaji katika ulimi huweza kuhisi katika mifumo mikuu
minne
1.
Mitikisiko
kama kuna mtikisiko wa kitu chochote
2.
Maumivu
kama sindano ya daktari
3.
Baridi kama mtu alalapo katika sakafu
4.
Joto
kama wakati wakuota moto wakati wa baridi
Ingawaje mishipa
hii ina kazi tofauti sawa na kazi hizo hapo juu katika kuhisi yoote hufanya
kazi kwa pamoja kuuuambia ubongo nini kinatokea katika mwili na ndipo ubongo
hutafasiri na kwa pamoja mwili unahisi kuna nini ulimwenguni jato au baridi au
maumivi au mitikisiko na kadhalika
Mitazamo
Perceptions
Ingawaje katika
maisha tunasisimuliwa na vitu vingi sana aidha kupitia milango hii mitano ya
fahamu lakini ni kwa ujumla wake ndio vinaleta maana inavyokusudiwa kwetu sasa
jumla ya mkusanyiko huu wa kazi za milango yoote ya fahamu ndio unatupa kitu
hiki kinachoitwa matazamo Perception hivyo milango ya fahamu ni milango ya ubongo
katika kutupatia mtazamo ni ya muhimu katika kutupatia mtazamo wa ulimwengu
wetu
Sifa
za mitazamo
Matazamo ni
mchakato wa ukusanyaji wa tafasiri kupitia mishipa ya fahamu kutuleta katika
ujumla wa maana ya kitu fulani ni jumuisho la kazi za utendaji wa milango ya
fahamu katika kutufunza mazingira yanayotuzunguka na kupata picha kamili ya
kiufahamu, Mtazamo unaweza kujengeka kwa ghafla au taratibu kulingana na jinsi
tunavyoathiriwa na mazingira yetu hii ni kwa mfano mtu kutoka ulaya anaposafiri
kuja ngorongoro na kuona vumbi kubwa likitimka juu yeye anaweza kudhani kuwa ni
Gari kubwa linakatiza katika barabara za Afrika zisizo na lami wakati mkazi wa
ngorongoro aweza kudhani ni Tembo wanao pigana n.k kwa msingi huu tunaweza
kuufahamu ulimwengu na kuwa na mtazamo fulani kwa sababu ya mtazamo wa
mazingira tuliyokulia, kwa hivyo basi mtazamo hujumuisha ufahamu wa akili
katika kutambua mambo watu,vitu na hali halisi lakini uwezo wetu wa kuipokea
unatofautiana hata kama mishipa ya fahamu inafanya kazi vizuri na ubongo
unafanaya kazi vizuri lakini mitazami yaweza kutofautiana kupitia mazingira
Mitazamo
na mkazo au mvuto
Ni muhimu kufahamu
kuwa matazamo pia huweza kuathiriwa na mikazo au mvuto wa kitu hii inatufanya kila mmoja kuuona ulimwengu
akiwa nadani ya miwani yake au kulingana na mahitaji ya mtu au yala
yanayomvutia au anayoyakazia kwa hivyo hii ni hali ya kuangalia jambo wakati huo
huo bila kupuuzia upande wa pili wa jambo hilo kadiri unavyokazia katika eneo
moja bila kupuuzia yale mengine ndivyo unavyoweza kupata picha iliyo wazi wa
kuelewa jambo lingine au lileliel kwa upana zaidi kwa hivyo ni muhimu kufahamu
kuwa mvuto wa kitu huchangia katika kusaidia mtazamo ni wazi kuwa kuna vitu
huvutia watu zaidi kwa mfano
1.
Picha
– huvutia watu kwa kasi zaidi kuliko Maneno
2.
Mpangilio
– kwa mfano inasemekana kitu kikipangwa mbele ya macho huonekana vizuri zaidi
kuliko kilicho pangwa pembeni
3.
Upya
– mlio mpya harufu mpya inavutia kwa haraka kuliko iliyo zoeleka
4.
Mtazamo
– mlio au mwanga unagusa mwili na kuliko vichocheo vingine
5.
Mkazo
– Mkazo wa sauti kubwa ,mwanga mkali, huvutia watu kwa haraka zaidi kuliko
vingine
6.
Mwendo
– vitu vitembeavyo huvutia kuliko visivyotembea
Mtazamo wa mtu
unaweza kuathiriwa na mazingira mwana Saikolojia R. Chalks alijaribu kuchora
mchoro wa glasi katika ubao mweusi na katika matazamo ya watu iliweza
kutafasiriwa tofauti wakati mwingine tunaweza kuonyesha mkazo katika kuangalia
rangi nyeusi zaidi kuliko nyeupe au nyeupe zaidi kuliko nyeusi na tukapata
picha tofauti na iliyokusudiwa aidha michoro ya mishale inayopelekea nje na
mishale inayopelekea ndani tunaweza kupata picha ya umbo refu au fupi zaidi
kupitia matazamo hata kama vipimo vya umbile hilo viko sawa angalia picha
zifuatazo
Pichani
juu unweza kuona picha hii ni ya glasi au watu wawili wanaotazamana mtazamo
wako utaamua kuwa unaweza kuona nini lakini ilikusudiwa kuchorwa glasi na sio
watu wawili unaona!
A
B
Pichani juu ni michoro uliyochorwa kwa vipimo
vinavyo fanana kabisa lakini ni rahisi kufikiri mchoro “a” kuwa ni mfupi zaid
ya mchoro “b” kulingana na mtazamo wako ulivyozoezwa
Mara nyingi
tunaparaganya mambo kupitia matazamo yetu kwa kuwa matazamo yetu imezoea mambo
fulani au imetoka kipaumbele katika jambo fulani basi tunashindwa kupata maana
sahihi ya mambo kwa mfano kama unasoma kitabu na nia yako ni kupata kujifunza jambo
fulani ni viguymu kuona makosa ya kitabu hicho hivyo uwezo wetu wa kuona mabo
sio kwamba uko sahii wakati wote kwa msingi huo tunaweza kukosa maana ya jambo
katika tafasiri ya mambo kwa sababu ya matazamo
Kwa msingi huu
Biblia inaonya kuwa ili tusiweze kujichanganya katika mambo ya kufikiri isivyo
sahihi ni muhimukuwa na tabia ya kutafakari mambo yaliyo mema Wafilipi 4; 8
Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo na sifa
njema, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote ya kupendeza, yo
yote yenye staha, ukiwako uzuri wo wote, pakiwepo cho chote kinachostahili
kusifiwa, tafakarini mambo hayo. Tito 1; 15 Kwa wale walio safi, kila kitu ni
safi kwao. Lakini kwa wale waliopotoka na wasioamini, hakuna cho chote kilicho
safi. Kwa kweli nia zao na dhamiri zao zimepotoka. Kwa msingi huo basi mtazamo wa mtu unaweza
kuwa mbaya pia kama mtu huyo ni mbaya na mtazamo wa mtu unaweza kuwa safi kama
mtu huyo ni safi
Jinsi
mitazamo inavyoathiri tabia
Kwa kawaida
matazamo ina uwezo wa kuathiri tabia katika namna ya kutia nguvu hisia zetu
ambazo kwa kawaida tunakuwa tumejifunza tangu tukiwa watoto na Tunaendelea
kujifunza kwa kadiri tunavyoendelea katika maisha ya siku zote kwa njia
mbalimbali kwa mfano propaganda na matangazo inaweza kuchangia kujenga matazamo
yetu, kumbuka kuwa taarifa zinapotoka kwa mtu mwengine kuja kwa mwengine lazima
ile taarifa itakuwa imeathiriwa na mtazamo wa mtu yule
Mitazamo
ni hisia au
mwelekeo uliotayari kufikiri au kutenda kuhusu watu, jamii hali, vyuo , taasisi,n.k.
“mwanangu siku hizi hanionyeshi heshima “ vijana wa siku hizi hawana adabu kama
vijana wa siku zetu, kanisa langu siku hizi hawanijali,siwezi kuishi bila
kuabudu, hii ni baadhi ya matazamo ya watu ambayo mingine inachochea migogoro
na mingine inahusisha hisia za faraja na usalama, kulingana na matazamo mtu
anaweza kulichukia kabila fulani kwa sababu ya taarifa zisizo sahihi alizopokea
toka vyanzo potovu
Matangazo ni tendo la kukusudia kivitendo
kuwavutia watu katika jamii kujua jambo ili kuwaumbia ushawishi au mvuto ili
waweze kununua bidhaa au kuja katika kanisa lako au vinginevyo hivyo kwa
kutumia matangazo unaweza kubadilisha tabia ya mtu au mtazamo wake
Propaganda hii ni njia ya msukumo wenye
kushawishi mwili wa mtu kukuunga mkono au kupokea aina fulani ya wazo, mtazamo
au tendo ili kujijumuisha katika wazo lako au kusababisha kupinga la mwingine
si kila wakati propaganda inaweza kuwa ya kweli lakini zinaundwa tu kwa lengo
la kuishawishi jamii au chochote kukujengea tabia au mtazamo fulani na sio
vinginevyo
Slogans
ni misemo yenye
kuubeba ujumbe wenye ushawishi wa kukuhamasisha ili utende au upige kura au
kuhamasisha taifa,shule au kanisa au jamii kutenda jambo fulani au kuhamasika
kupambana na jambo fulani aina hizo za slogan ni kama Maralia haikubaliki! Au
Hari mpya nguvu mpya na kasi mpya.
SAIKOLOJIA YA TABIA NA UTU: JINSI UTU WA
MTU UNAVYOCHANGIA TABIA ALIYO NAYO
Neno
utu ni gumu kulielezea kwani watu huelewa utu katika matazamo mbalimbali
kulingana na jinsi wanavyowaona watu na kuwa kila mtu ni tofauti na watu
wengine wote, katika mitazamo tofauti tofauti kwa msingi huo tunaweza kusema
kuna utu wa aina nyingi kwa sababu ya kuwa na watu tofauti tofauti ulimwenguni
kwa msingi huo tunapochukua makundi ya watu na tabia walizonazo tunaweza kupata
maana ya neno utu na pia kujaribu kutafasiri watu kulingana na utu wao kisha
tunaweza kusema ni mpole au mtaratibu au mkali na kadhalika
Maana ya neno utu
Presonality
Utu
au personality ni jumla ya mtu na tabia zake, hii ina maana namna mtu huyo
anavyo fikiri.anavyohisi, na anavyotenda na tabia zake kwa msingi huo utu ni
mkusanyiko wa tabia zote za mwanadamu ni jumla ya sifa na ubora wa mtu katika
uhusiano wake na wengine kwa maana nyingine utu wa mtu hudhihirika pale
anapohusiana na wengine kwa hivyo hakuwezi kupatikana utu bila mtu kuhusiana na
wengine kwa maana hiyo pasipo wengine katika maisha yetu utu hauwezi kuweko
kabisa
Mahitaji ya afya ya
utu
Kila
mtu ana mahitaji ya kisaikolojia ambayo kwa ujumla wake yana athiri afya au
kutia nguvu utu mahitaji hayo yanapotimizwa maisha huonekana kuwa mazuri na
tunapata afya hata katika muonekano lakini yasipotoshelezwa au yasipotimizwa
matatizo ya afya ya akili hujijenga
Mahitaji makuu ya
afya ya utu
1.
Kudhibiti
mazingira yetu – hakuna mwanadamu anayependa
kuona anazidiwa na mambo au mabo yako juu ya uwezo wake inapo kuwa jambo
liko juu ya uwezo wetu hapa duniani
tutahitaji anagalau tuyafahamu ni mpaka tuone utaratibu na jinsi jambo hilo
linavyotabirika kudhibitiwa ndipo tunaweza kuzipumzisha akili zetu kuacha kushughulikia
nalo
2.
Usalama
– woote tunahitaji kuwa na uwezo wa kustahimili Migandamizo ya ya maisha hivyo swala la usalama kadir
tunavyoendelea linakuwa ni jambo la muhimu kila mtu anahitaji kujilinda kwa
usalama wake
3.
Upendo
na mahusiano – Hitaji la kupenda au kupendwa ni moja ya mambo ya muhimu katika
kuendeleza utu kama kuna jambo linavutia
nyumbani ni wazazi kuonyesha wanampenda mto lakini hata hivyo hitaji la
kuhusiana na watu wengine litaendelea kukua
na hii ndio maana watu hupenda kuwa na klabu au vyama vya kijamii
4.
Hitaji
la kujitambua na kutambuliwa – kila mwanadamu ana hitaji la kujitambua au
kujiona anastahili na zaidi ya hilo anahitaji kutambuliwa na kuthaminiwa utu
wake kujitambua kwa mtu hata hivyo
kunatokana na jamii inavyotoa uthamani
wa kiwango cha mtu huyo katika jamii
jinsi tunavyojifikiri sisi wenyewe ni moja ya kioo kikubwa cha wengine
watakavyofikiri kutuhusu
5.
Uthamani
maana na matumaini – kila mwanadamu analo hitaji la kutafuta uthamani wa maisha
na kujikabidhi, katika hali kama hii ndipo tunapokutana na migandamizo fulani
ya maisha na tunahitaji umaana na psipo maana maisha yanakuwa hayana matumaini
na kunakuwa hakuna sababu ya kuishi inasemekana baadhi ya mateka au wafungwa
wakati wa vita hufa kwa kukosa matumaini katika maisha na baadhi wanaoona
umuhimu wa maisha hao huishi
6.
Kujitosheleza
– hatuhitaji kuhakikisha ya kuwa tunaishi tu bali pia kujiendeleza wenyewe kujiendeleza hata kufikia uwezo wa juu wa
kiungu aliotupa kama watatwala wa viumbe vyote
hapo ndipo mwanadamu anapotafuta kujitosheleza hali hii iligunduliwa na Dr. Abrahamu Maslow
ambaye aliorodhesha mambo kadhaa chini kama sifa za mtu aliye jitosheleza
·
Anakubaliana
na hali halisi bila kutafuta kujiridhisha
·
Hufikia
ngazi ya juu kabisa ya kujikubali
·
Anaishi
kwa kujitosheleza badala ya kupambana na maisha
·
Anahitaji
kukaa peke yake ingawa hachukizwi kuwa na watu
·
Anakuwa
na viwango vya juu vya ufahamu na hubakia kuwa mkeli kwa nafsi yake
·
Anakuwa
na urafiki wa karibu na marafiki wa karibu au mpenzi wake
·
Anakuwa
na ucheshi
·
Anakuwa
amekomaa kimaadili na kitabia
·
Anakuwa
na uwezo wa kubuni na kugundua
Mtu aliyejitosheleza au kuridhika katika
Saikolojia ndiye mwenye afya nzuri kisaikolojia katika hali fulani za maisha ni
vigumu kuwa na uwezo wa kuridhika au kujitosheleza hususani wakati wa
migandamizo, matatizo, maumivu, kutishiwa, katika wakati kama huo tunajaribu
kujilinda lakini kuridhika kunabaki kuwa lengo lenye maana la maisha la kila
mmoja wetu.
SAIKOLOJIA
YA AKILI NA MASWALA YA KUJIWEKA SAWA KWA MAPAMBANO YA KIAKILI
Wataalamu
wa maswala ya Saikolojia wanaamini kuwa mwanadamu wakati wote yuko katika vita
au mapambano na Yeye mwenyewe au na mazingira yake kiakili lakini wengine
wanaamini kuwa mwanadamu aweza kuishi kwa amani na Yeye mwenyewe na wengine
lakini tofauti hii ni kubwa kwani ni lazima mwanadamu ajiweke sawa kwa namna
fulani katika mapambano ya kiakili ili aweze kumudu kuchukuliana na mengi
katika ulimwengu
Kujiweka
sawa kunahusu tabia,mawazo na maswala yote ambayo watu waweza kuchukuliana nayo
katika mazingira, inaaminika kuwa kila mwanadanmu huweza kujiweka sawa katika
aina fulani ya mazingira na migandamizo
tunayokutana nayo katika maisha lakini ni kitu gani kiaweza kumfanya mwanadamu
kujiweka sawa?Baadhi ya waandishi wanasema
ili kujua kuwa mwanadamu ana afya nzuri kiakili muulize swali jepesi JE UNA FURAHA? Kama tunalenga furaha kama
lengo la maisha ndipo tunaweza kujua kuwa mtu yuko sawa au la kama mtu huyo
anaweza kuwa na uhusiano mzuri na wengine na kuonyesha kua anajitambua na kuwa
na matumaini katika maisha mtu huyo aweza kujibu ndiyo katika swali hili muhimu
je una furaha
Kujitambua/kustahili kama moja ya
njia muhimu ya kujiweka sawa kisaikolojia
Wengi
wa wanasaikolojia wanaamini kuwa moja ya njia muhimu sana za kujiweka sawa
katika maisha ni kujitambua hii ndio inaonekana kuwa msingi mkubwa wa kuridhika
aku kujitosheleza Dr.Stanley Coopersmith aliandika kuwa kujitambua ni njia rahisi ya uhakika na
uaminifu wa nafsi ya mwanadamu lakini pia ni kama dhambi ya kiburi
Sambamba
na hilo hapo juu upendo usio na sababu ni moja ya mambo yanayokuwa dawa kwa
kujiweka sawa kisaikolojia huu ni upendo kama ule unaotolewa kwa wazazi kwa
mtoto wao kwa sababu ni sehemu ya familia
athari ya upendo huo unaotolewa bure bila mipaka au sababu unaumba
kukubalika kwa wazazi na familia na
ndipo unamsaidia mtoto kujikubali na
kuridhika hata hivyo si kila mtu anaweza kuridhika katika kujiweka sawa kwa
maisha mtu mmoja alitoa dalili za watu
wlio ridhika na wasioridhika au watu walio na uwezo wa kujiweka sawa kiakili na
watu wasioweza kujiweka sawa kiakili
Sifa
za watu wenye uwezo wa kujiweka sawa kiakili na wasio na uwezo wa kujiweka sawa
kiakili
Wanashughulika
katika maisha
|
Wanakata
tamaa katika maisha
|
Wanadhamiri
safi
|
Wanadhamiri
iliyojikunyata
|
Wanjihisi
wanaweza
|
Wanajihisi
kutokuweza
|
Wanamudu
hisia
|
Hawana
hisia zilizo imara
|
Ni
rafiki wazuri
|
Hawana
urafiki mzuri
|
Wanajilaumu
wenyewe kwa matatizo
|
Wanalaumu
wengine kwa matatizo
|
Wanafurahia
maisha
|
Hawafurahii
sana maisha
|
Migogoro ya
migandamizo na ujiwekaji sawa kisaikolojia
Uwezo
wa mtu kujiweka sawa kisaikolojia unaweza kuonekana mtu huyo anapopatwa na
matatizo na migogoro mtu huyo anapoweza kustahimili hali halisi na kutumia
vyanzo vilivyoko kujiweka sawa tunasema mtu huyo ana uwezo wa kujiweka sawa
kisaikolojia kama migogoro na matatizo yatampelekea mtu huyo kuwa na tabia
tofauti na hisia tofauti tunaweza kusema
kuwa mtu huyo hana uwezo wa kujiweka sawa kisaikolojia kwa hivyo swala linakuwa
katika kujiweka sawa na kutokujiweka sawa hili pia linaweza kuonekana kwa mtu anapotoka
katika tamaduni moja kuelekea katika tamaduni nyingine kama wamishionari,au
inaweza kuonekana kwa Mwanafunzi anapotoka nyumbani kwenda kuishi maisha ya
shuleni kwani katika hali ya kawaida kwa mazingira ya kawaida mtu hutimia mbinu
zake za kawaida kukutana na mahitaji yake lakini katika mazingira mapya mtu
anahitaji mbinu mpya kukabiliana na mahitaji na kushinda vikwazo vipya akiweza
hilo tunasema pia kuwa anao uwezo wa kukabiliana na migandamizo na kujiweka
sawa kisaikolojia
Hali za kukatisha
tamaa (Frustration)
Hii
ni hali ya mtu kutakuwa na uwezo wa kufikia malengo kwa sababu ya hisia fulani
kwa mfano mtu mwenye njaa anapokosa chakula
na kwa kuwa hana njia nyingine labda hana Fedha basi anaweza kukasirika na kukata tamaa kwa
msingi huo hali za kukatisha tamaa huweza kutokea pale mahitaji yetu na tamaa
zetu zinakosa kutimilizwa na hapo ndipo
mtu hukata tamaa ikiwa ataendelea kutafuta namna nyingine ya kutimiliza
mahitaji yake basi kisaikolojia tunasema mtu huyo anauwezo wa kujiweka sawa
kukabiliana na vikwazo au migogoro katika maisha lakini anapoonyesha kukata tamaa na kutamani
au kuona maisha hayana maana tunasema mtu huyo anauwezo mdogo wa kujiweka sawa
kukabiliana na mabo magumu au napoanza kuwa na tabia zisizo fanana na
alivyotakiwa kuwa kitaalamu watu hao huitwa “Poor adjustiment Person” na wale
wenye uwezo wa kujiweka sawa tunawaita “well au Good adjustiment Person”
Hali za mapambano
au migogoro (Conflict)
Hali
hii haitofautiani sana na hali ya hapo juu lakini mgogoro hapa ni matokeo ya vitu
zaidi ya viwili au zaidi ya malengo au mahitaji au mwelekeo wa maisha haya ni
mapambano ya kimaisha yanayoweza kumfanya mtu asukumwe katika mwelekeo mwingine
au hali inayo mfanya mtu ashindwe kuchagua mwelekeo mwingine kwa mfano mtu
amekusudia kuoa mwanamke mzuri basi hawezi tena kuwa na uwezo wa kuamua kuoa
mwanamke mwengine aliye mzuri na anayemvutia huu ni migogoro au kijana anataka
kwenda chouni lakini anaogopa kuiacha familia hii pia tunaweza kuiita
migogoro,kwa hivyo migogoro hutokea tunapokuwa na mawazo mchanganyiko kwa mfano
shauku na woga au hofu hizi ni hali za migogoro kisaikolojia
Kuchukuliana na
kujiweka sawa
Mwanadamu
anapokutana na hali za mapambano naq migogoro kwa kawaidea atajaribu kutafuta
njia za kutatua tatizo hilo mwenye njaa aweza kutafuta Fedha ili kununua chakula au kutafuta chakula kwa
njia nyingine lakini kuna wakati amabapo mbinu zetu haziwezi kukidhi hali
halisi katika wakati huo ndopo tunaunda uwezo wa kuchukuliana na tatizo
tulilonalo ili kufanya fidia fulani ya kiakili, fidia hizo kwa asili huzalishwa
kwa kusudi la kujilinda Defensive hizi
ni fidia za kujilinda kisaikolojia ambazo kitaalamu huitwa “Cognitive Defense
Mechanism” hizi ni mbinu za kibinadamu za kuchukuliana au kutafuta kuziba pengo
la tatizo lililoshindwa kutatulika kwa kawaida nyingine ni za kawaida na
nyingine si za kawaida lakini ni matatizo ya kiakili yanayo ziba hali ya tatizo
fulani ili kufidia au kujiweka sawa au kuchukuliana na matatizo halisi miongoni
mwao chache tutazijadili hapa chini kama ifuatavyo;-
1. Kukandamiza (repression) Hii ni hali ya kufidia kitu usichokipenda au wazo la
kitu usichokipenda ambacho kinaweza kukujia hata katika mawazo lakini hutaki
kukipa kipaumbele si kuwa hutaki kukiwaza tu lakini hutaki hata kukumbuka tukio
hilo kabisa na kutaka kusahau hata kuwa umekisahau yaani unaweza kukumbuka kuwa
kuna shida fulani lakini hutaki hata au huwezi hata kukumbuka namna ilivyotokea
mwizi anapokamatwa anaweza kuuawa na wezi wenzake walioko katika jamii kwa
kupigwa mawe ili kukandamiza miongoni mwa jamii wasionekane kuwa nao ni wezi
bali wanachukizwa na wizi huo kwa kisi kikubwa katika hali halisi wao ni waizi
lakini hawataki hali hiyo wasije nao wakaonekana kuwa ni wezi
2. Kukanusha (Denial) hii ni hali ya kufidia kwa kukataa hali halisi ya jambo
ambalo limetokea kwa dhati,kwa hiyo ni hali ya kujaribu kukataa kabisa hali
fulani ambayo kwa kawaida imetokea kweli kwa mfano ni rahisi baadhi ya watu
kukataa tukio la kweli la habari za kufa kwa mtu unayemfahamu sana kwa watu
wenye uwezo wa kuchukuliana vema jambo hili linaweza kutokea kwa muda kisha
akakubaliana na hali halisi lakini mwenye tatizo la kuchukuliana ataendelea
kukataa ili kuondokana na tukio hilo lenye maumivu
3. Ndoto za mchana (Fantasy) hii ni hali ya kufidia ambapo
mtu asiyeweza au aliyeshindwa kufikia mafanikio fulani hubaki na mawazo amabayo
tunayaita ndoto za mchana akiifurahisha akili yake kwa kamchezo ka
kujifurahisha kujiona bingwa au shujaa kwa kutengeneza picha tu akilini .aweza
kujiona kuwa amaekuwa Rais, au yuko kama Yesu au kiongozi yeyote mkubwa
ulimwenguni mtu wa jinsi hii huweza kuwaza kuwa amejenga ghorofa anamiliki gari
au yuko mahali fulani katika inchi iliyoendelea n.k kwa ujumla huyu haishi
katika ulimwengu halisi kwani katika ulimwengu halisi tatizo liko palepale
ingawaje hata wale wenye uwezo wa kuchukuliana wanaweza kuwa na ndoto hizi
kabla ya kuzifanya ziwe halisi kivitendo lakini wagonjwa hubaki na wakati mgumu
4. Kutafuta sababu (Rationalization) hii ni hali ya kufidia
tatizo kwa kutafuta sababu au kusingizia
kwa mfano Mwanafunzi wa chuo cha Biblia aweza kuacha kwenda Kanisani kwa
kisingizio kuwa amekuja kusoma na sio kufanya ibada hali ya kutafuta sababu pia
hutumika katika kuwepa migogoro kwa mfano
kijana anapotaka kuoa na ana wasichana wawili aliowapenda na mmoja kati
yao ana mchukia ili apate sababu ya kumuachia anasingizia kuwa hana tabia nzuri
ili kuhalalalisha kuwa huyo aliyemuoa ndio uchaguzi sahihi na sio vinginevyo
5. Kulaumu wengine (Projection) hili ni tendo la kufidia
ambapo mtu hulaumu watu wengine kama njia ya kujitetea katika hali fulani aidha
projection ni tatizo liwezalo kufanyika kivitendo kwa mtu kuamua kuudhi wengine
kwa sababu yeye ameudhiwa hii ina maana ya kuwa kama Bosi kazini alikuwa mkali
baba anaporudi nyumbani anakuwa mkali kwa mkewe na mke kwa watoto na watoto
waweza kumalizia hasira zao kwa paka ni
tendo la kuamini kuwa watu wengine ndio walio na hali ya kumkataa mwingine
kihisia na kimawazo hivyo muathirika huwalaumu wao kama njia ya kujilinda
6. Kujiondoa (Withdrwal) ni hali ya kufidia kisaikolojia ambapo mtu hujitoa
katika hali inayoonyesha kuwa kuna migogoro anawea kufanya hivyo kwa kuondoka
kabisa katika eneo husika au kwa kujifanya haoni wala hasikii ili asihusishwe
kwenye matatizo hayo au migogoro huo ni kama anawsema mimi simo kivitendo au
kisaikolojia.
7. Kujilinganisha (Identification) ni hali ya mtu lijaribu
bila kukusudia yaani sio kwa Makusudi,kujifanya kama mwingine au ni kuiga tabia
za mwingine, au kujifananisha na jamii ya watu wengine na kuficha ya kwake ili
asionekane duni kwa mfano mtu anaweza kuwa mmbugu akajifanya msambaa,au
kujifanya ni moja ya wanafamilia ya mtu mmoja mkubwa serekalini au rafiki wa
mtoto wa mtu mkubwa n.k hata hivyo tabia hii hujitokeza zaidi sana wakati wa
utoto au ujana
8. Kutafuta visingizio (Dispaced Agrgession) ni hali ya kufidia
kisaikolojia kwa mtu aliye sababisha tatizo kwenda kwa mtu au kitu kingine au
kujilaumu mwenyewe mtindo huu unapokuwa endelevu unatengeneza hali ya kujificha
katika kitu kingine Scape goating
wakati mwingine mtu anaweza eti hata kutishia kuwa atajiua
Hali ya kushindwa
kuchukuliana na kujiweka sawa (Maladjustment)
Ingawa
tunapenda isiwe hivyo lakini wako watu wengine ambao hawawezi kuchukuliana na
kujiweka sawa wanapopatwa na matatizo watu hao huteseka sanqa kihisia na maisha
kwa ujumla wake kwao hayana maana tungetamani kuwa kila mkristo asiwe na tatizo
la kushindwa kuchukuliana ingawaje tunajua kuwa baadhi hufanya hivyo
Woote
tunajua kuwa kinyume cha afya nzuri ya akili ni afya mbaya ya akili lakini
wanasaikolojia wengi na matabibu wa maswala ya kisaikolojia au matatizo ya akili humchukulia mtu yeyote anayeshindwa
kuchukuliana na kujiweka sawa kuwa ana matatizo ya kiakili ingawaje watu hao
wanaosumbuliwa hawapendi kuitwa watu wenye matatizo ya akili au vichaa
watawaita tu watu wasio weza kuchukuliana au wasiojitambua kuna matatizo mengi
sana ya kiakili kwa wanadamu lakini muda hautoshi kuweza kuyaangalia moja baada
ya jingine lakini tunaweza kujadili kwa mukhtasari machache kati ya hayo kwa
ujumla wake kuna matatizo ya kihisia makuu
matatu yaani kuchanganyikiwa kiasi
Affective disorders, kichaa,au kuchanganyikiwa kwa kiasi kikubwakidogo
Neuroses, na kuchanganyikiwa kukubwa zaidi kisaikolojia Psychoses.
Kuchanganyikiwa
kiasi affective disorders
Hii ni hali ya kuwa katika hali isiyo ya
kawaida kihisia katika hali fulani mtu anaweza kujikuta anaharakisha kufanya
mambo bila kufikiri au kwa nguvu kubwa tatizo hili huitwa mania watu wa jinsi
hii wanapenda juu kwa jazba na kitabia na inaweza kuchukua muda kuwa katika
hali ya kawaida wanakosa usingizi hawaoni uhalisia na hawako katika hali ya
kawaida mania ni hali ya migandamizo depression hali hii huwapata sana watu wa
magharibi kuliko Afrika ingawaje watu wa Afrika wanapenda kuiga tabia ya watu
wa magharibi hivyo migandfamizo iatakuwa sehemu ya maisha yao waigizaji watu wa
jinsi hii wanavunjika moyo,hawawi kawaida mood wanajitenga na jamii hawali
vizuri wala hawalali vizuri maisha ya baadaye kwao si ya matumaini na takwimu
zinaonyesha kuwa 75% ya watu wanao teseka mateso hayo hufikiri kuwa hawataweza
kupona wengi hufikia hatua ya kujiua kwa kukata tamaa
Kuchanganyikiwa kwa
kiasi kikubwa kidogo neuroses
Hii
ni hali mbaya zaidi ya hiyo ya kwanza ni usumbufu mkubwa wa akili na kihisia na
huwapata watu wasioweza kustahimili au kuchukuliana watu wa jinsi hii wanaweza
kuwa na hali ya kuhofia kila wakati anxiety bila sababu na wanaweza kuwa nje tu
wakati mwingi au anaweza kuwa na woga wa kupita kawaida Phobias watu wa jinsi
hii ni vigumu sana kuwatibu maumivu yao wanaweza kujikuta wananawa mikono mara
nyingi au kula saa wanaweza kususa kukaa endapo atakuta mtu amekalia kiti chake
wanasaikolojia hudai kuwa hali hii inaweza kutupata watu wote au watui wote
tunayo lakini kila mmoja ananjia yake isiyo ya kawaida ya kupambana na hali
hizi na kwa ajili ya kujitambua watu wenye kustahimili hurejea katika hali ya
kawaida lakini viwango havifanani hivyo wale wanaozidiwa wanaoitwa wagonjwa
kisaikolojia na hawa hudhani kuwa hawawezi kustahimili hali iliyowakuta hivyo
hujaribu kujilinda wenyewe na hali ya maumuvi ya ulimwengu huu kumbe wanajikuta
wamechanganyikiwa
Kuchanganyikiwa kwa
kiasi kikubwa Psychoses
Hii
ndio hali mbaya na ya juu zaidi kuliko hizo mbili hapo juu , kuna aina nyingi
za usumbufu wa aina hii lakini hii
inakuwa nje zaidi ya uhalisia ulimwengu kwao unakuwa ni sehemu ya maumivu na
kutosha na wakati mwingine hufuikia hatua ya kusikia makelele ambayo huwezi
kuyaona au kuyasikia wala sio halisi lakini yeye huyasikia hali hii huitwa
Hallucinations, wakati mwingine hali hii huweza kufikia kiwango cha mtu kushindwa
kujua nini kinaendelea katika mwili wake au kujijali anaweza kujisaidia kuvua
nguo kuchora chora n.k kwa ujumla watu wa naman hii hutakiwa kulazwa
hospitalini chini ya uangalizi wa madaktari Kikristo wengi wwenye hali hizi
huweza kudhaniwa kuwa wana mapepo lakini hata hivyo wanasaikolojiwa wa Kikristo
wanasema si kila wakati wanaochanganyikiwa kiwango hiki wana mapepo hivyo
wanapaswa kuwa na uwezo wa kupambanua kati ya mapepo na ukichaa wa kawaida
ingawa ukweli unabaki kuwa tiba ya kiroho ya watu wengi wenye matatizo ya
kisaikolojia ni ya muhimu sana kwani mtu anapoungama na kutubu dhambi zake
kisha kuombewa anaweza kuwa na maendeleo mazuri ya afya ya kiakili na kuwa na
matumaini kanisa lina nyenzo kubwa sana ya uponyaji wa mwanadamu kwa ukamilifu
wake kumtoa katika ulimwengu wa maumivu kuliko tiba nyingine
Viwango vya athari
na maumivu wayapatayo watu LCU.
Kwa
mujibu wa Dr.Thomas H Holmes na timu ya wenzake katika chuo kikuu cha
Washington school of medicine walijaribu kufanya utafiti wa maumivu
yanayowapata watu na kusababisha athari ya mgandamizo wa mawazo au msongo na
kuupa jina la kipimo cha mabadiliko ya maisha na miganadamizo yake yaani LCU
“Life Change Units” na kugundua ya kuwa kama kiwango hicho kitafikia asilimia
300 LCU kwa miaka miwili Mfululizo kwa mwanadamu mmoja kuna uwezekano wa mtu
huyo kupatwa na ugonjwa mkubwa sana wa kisaikolojia
Tukio
|
Kiwango LCU
|
Tukio
|
Kiwango LCU
|
Kufiwa
& mpenzi
|
100%
|
MtotoShuleni
|
29%
|
Takaka
|
73%
|
Shida
kisheria
|
29%
|
Watoto wapweke
|
65%
|
Mke
kuacha kazi
|
26%
|
Kufungwa
|
63%
|
Hali
ya hewa tofauti
|
25%
|
Kufiwa
na ndugu
|
63%
|
Kupitia
tabia
|
24%
|
Kujiumiza
|
53%
|
Boss
mkali
|
23%
|
Shughuli
za ndoa
|
50%
|
Kubadili
saa za kazi
|
20%
|
Kufokewa
kazini
|
47%
|
Mabadiliko
shule
|
20%
|
Ndoakupatanisha
|
45%
|
kuhama
|
20%
|
Kujiuzulu
|
45%
|
Mabadiliko
Kanisani
|
19%
|
Afya
mbaya
|
44%
|
…”…kulala
|
19%
|
Mimba
|
40%
|
…….kula
|
15%
|
Ugumu
ktk sex
|
39%
|
sikukuu
|
13%
|
Mtoto
mpya
|
39%
|
likizo
|
13%
|
Biashara
mbaya
|
39%
|
Ukiukaji
mdogo wa sheria
|
11%
|
kuchacha
|
38%
|
|
|
Kifo
cha rafiki
|
37%
|
|
|
Kuhamishwa
|
36%
|
|
|
_____________
Used
by Permission of Holmes,T.H & Rahe,R.H.The Social readjustment rating
Scale.Jounal of Psychosomatic Research II:213-218,1967.
SAIKOLOJIA
YA MIGANDAMIZO DEPRESSION PSYCHOLOGY
Ni
moja ya matatizo makubwa sana ya kiakili ambapo mtu huhemewa au huelemewa na
huzuni kubwa na ya ndani kiasi cha hata kufanya jambo lolote isipokuwa kukata
tamaa watu wa jinsi hii hujisikia upweke, kukataliwa, kutokustahili na kukata
tamaa na mwisho wa yote watu wa jinsi hii hutamani hata kujiua gonjwa hili la
akili pia liko katika migawanyiko ile mitatu ya nafuu, wastani na hatari kabisa
kwa wanansaikolojia hili ni tatizo kamili la kiakili linalohitaji tiba. Tatizo
hili halijali jinsia ya kike au ya kiume inamsumbua mtu yoyote
Athari za
saikolojia ya mgandamizo
A.
Mabadiliko katika kupata Usingizi
Mtu
mwenye migandamizo mara nyingi matatizo yake ya hamu ya kitu huweza kuongezeka
sana au kupungua ingawaje mara nyingi hupungua Kwa mfano tabia ya mabadiliko
katika kulala watu wenge Migandamizo wanaweza aidha kulala sana au zaidi sana
kukosa usingizi au kulala muda mfupi, Mtu mwenye migandamizo anaweza kuchelewa
sana kwenda kulala na anaweza kuamka mapema kama saa 11 alfajiri na usingizi
wake ni wa man’gamung’amu au aweza kuamka asubuhi akiwa amechoka sana na hivyo
kwa watu wengi wenye tatizo hili asubuhi huwa ni wakati wa huzuni kwao
B.
Mabadiliko katika Nguvu
Migandamizo
hii pia husababisha mabadiliko katika nguvu za muathirika baadhi yao hujisikia
kutokupumzika na hijitia katika Shughuli nyingi sana na hawapendi kula wengine
hujisikia uvivu na kutokutaka kufanya lolote hujisikia wamechoka sana na nguvu
zimepungua na au kujisikia kama watu waliobeba mzigo mzito sana wanapunguza
uwezo wa kufikiri na hawawezi kuwa makini kusikiliza jambo moja Poor
concentration na pia huwa na matatizo ya kukumbuka vizuri
C.
Uwezo duni wa kujitambua au
kujiona anastahili
Watu
wenye miganadamizo mara nyingi hujiona kuwa hawastahili kabisa,hukosa matumaini
na kujilaumu wanaweza kutafasiri jambo dogo tu au kushindwa kidogo tu kama njia
ya kutokuwezekana kabisa na wanaweza kutafasiri kukosolewa kidogo tu kama
wamehukumiwa wengine hujilaumu kuwa wamekufa kiroho au kimaadili na kioo kwao
wanapojiangalia huona uso mbaya au wenye hatia ya kudanganya wengine watu wenye
migandamizo mikali zaidi huamua kujiua kwani migandamizo husababisha maumivu ya
kihisia asilimia 15% ya watu wenye migandamizo huishia kujiua au wengu
wamejaribu kujiua
D.
Matatizo ya kuufahamu
Wakati
mwingine watu wenye matatizo haya wanaweza kuona picha za Matukio mbalimbali
zikiwajia ambazo kitaalamu tunaziita False beliefs & Hallucinatios ambapo
mtu huona matazamo isiyo sahii hali inapokuwa hivi tatizo hili la migandamizo
ujue limekuwa baya zaidi Psychotic symtoms tayari ni ugonjwa mbaya wa
kiakili,hwana raha,na hujisikia kujiuua hata baada ya kulazwa hospitalini kwa
muda mrefu
Sababu kubwa za
Matatizo ya Migandamizo
Baadhi
ya migandamizo inatokana na haliza uchovu tu hata kama mtu hana matatizo yoyote
na mabo yako vizuri tu, lakini wengi hupatwa na matatizo haya kwa sababu za
matatizo ya unyumba ndani ya ndoa kama hakuna amani,Maswala ya kifedha kuwa
mabaya,kushindwa vibaya kwa mfano anguko la kiroho,kushushwa cheo kushindwa
uchaguzi, ingawaje baadhi ya wanasaikolojia pia huamini kuwa matatizo haya pia
husababishwa na matokeo ya mtu aliyetoka katika maishauonevu na mateso kwa
hivyo muingiliano wa mambo fulani na mtu wa namna hiyo unaweza kusababisha
matatizo haya ya kisaikolojia, aidha utafiti mwingine unabainisha kuwa unaweza
kusababishwa na maswala ya kibaiolojia kwa mfano watu waliozaliwa mapacha baada
ya kufanyiwa utafiti wengi wananonekana kuwa na migandamizo, hivyo kuna
uwezekano wa kuurithi kibaiolojia migandamizo pia inasadikiwa kuwa wengi
waliopitia hali hii huweza kuwaganadamiza wengine,sababu nyingine ni kutakuwa
sawa kwa kemikali za ubongo zinazo shughulika na maswala ya hisia ya mwanadamu
ziitwazo kitaalamu Neurotransmitters na matatizo ya
homoni “An imbalance of hormones”
yanaweza kuchangia tatizo hilo,aidha matumizi ya baadhi ya madawa kama vitamin
B6, vitamin B12, and folic acid na mengineyo huweza
kusababisha migandamizo depression na matatizo yenye kuumiza au Matukio yenye
kuumiza kama kufiwa na mpenzi au mtu unayempenda inaweza kusababisha matatizo
kama hayo tatizo la kufiwa na mpenzi huweza kuchukua 100 LCU hivyo ni tatizo la
juu sana kama tulivyoona mwanzoni huko juu
Matibabu
ya matatizo ya migandamizo
Kwa watu wenye matatizo makubwa kabisa ya migandamizo ya
kisaikolojia mara nyingi ni vigumu kutibika kwa kupewa ushauri wa kawaida
tu lakini kuna njia kama nne hivi
zinazoweza kufaa katika kutibu matatizo makubwa kiasi hiki ,kuna vidonge
vinavyotenda kazi kinyume na miganadamizo ambazo kitaalamu huitwa Antidepressant Drugs , halafu uponyaji wa
kisaikolojia Psychotherapy, ambao wakati mwingine huambatana pamoja na vidonge
au njia nyingine ya kutumia umeme iitwayo kitaalamu
Electroconvulsive therapy ambayo muathirika huvurugwa akili ili zianze kwa
upya kwa kutumia kifaa maalumu hii hufanyika njia nyingine zinapokuwa
zimeshindikana aidha pia maombezi na ushauri wa kichungaji nao umekuwa na
matokeo mazuri na makubwa katika maswala ya kutibu matatizo ya migandamizo
SAIKOLOJIA YA MIGANDAMIZO YA MSONGO WA
MAWAZO MSONGO STRESS
Stress (psychology)
Msongo
wa mawazo au stress ni hali isiyopendeza ya kisaikolojia ambayo watu hujisikia
kulingana na hali wanazozipokea aidha zenye kuashiria hatari kuwatishia au
kuwafanya wasijisikie vizuri hata hivyo msongo unaweza kuwa na maana nyingine
kwa sababu tofauti wengine huuelezea msongo kama tukio la hali inayomsababishia
mtu kujisikia yuko juu juu, pressure inapanda na kushika au kuogopa hofu na
hali zisizoweza kuelezeka mara nyingi hili huchangia pia kuleta mabadiloko ya
Mapigo ya moyo na hivyo pia husababisha mpanuko wa misuli ya Mapigo ya moyo na
mababdiliko ya tabia za kihisia hata hivyo msongo unategemeana sana na hali
halisi za tafasiri za mtu binafsi na hali ananzokutana nazo hivyo si rahisi
kuelezea kwa wazi kuwa
Ni
muhimu kufahamu kuwa pia msongo ni hali ya kawaida tunayokutana nayo kila siku
inaweza kukupata unapokuwa na Shughuli nyingi, au tunapokuwa na jambo la muhimu
sana la kutimiza na ukawa na muda mfupi sana wa kutimiza hapo msongo unaweza
kutokea.msongo unaweza kutokea pia kwa sababu ya matatizo kazini au kautokana
na mahusiano mabaya katika jamii muingiliano na marafiki n.k aidha Matukio
yenye kuumiza katika maisha kama kifo cha mtu uliyempenda sana na kuogopa
maeneo ya kawaida yanayotisha n.k huweza kusababisha msongo. Msongo unaweza
kuleta athari nzuri au athari mbaya mtu anapotishiwa na jambo anaweza kuzalisha
nguvu mbili kujilinda au kuepuka msongo unaweza kusababisha utimize jambo
fulani na pia unaweza usababishe kushindwa lakini katika upande mbaya Msongo
unaweza kusababisha tatizo kubwa sana
Vyanzo vya msongo
Msongo
unaweza kusababiswa na sababu mbalimbali ziitwazo Stressors lakini sababu kuu
hizo hugawanywa katika maeneo makuu matatu Matukio ya ghafla Catastrophes hii huweza kusababishwa na
uvamizi,ajali,vitana kadhalika Matukio yenye kuhusisha mabadiliko makubwa ya
kimaisha Mojor life changes haya ni Matukio kama ya talaka,kufungwa kwa baba au
mama,kuuguliwa kufiwa na baba au mama,mipango ya kuoa nk chanzo cha tatu ni
Matukio ya kila siku katika maisha haya ni msongo unaotokana na mwingiliano wa
maisha ya kila siku kazini ndugu jamaa nk.
Athari za msongo
·
Kutokuwa na Kumbukumbu nzuri
·
Kutokuweza kumudu kazi zako kama inavyopaswa au katika hali ya
kawaida
·
Kupatwa na magonjwa ya moyo na athari za viungo vingine
SAIKOLOJIA YA
UTU NA MAUMBILE YANAVYOUNDA TABIA YA MWANADAMU
Mwana
Saikolojia wa zamani sana aitwaye Galen alijaribu kugawa mafungu makuu manne ya
aina za utu ambazo huumba tabia kutokana na maumbile yao aina hizo nne za utu
ni Sanguine, Phlegimatic, choleric na melancholic aliyagawa makundi haya makuu
manne kutokana na maumbile ya mkao wa maji Body Fluids unaomkalia kila mtu
mafungu hayo manne ya watu yanaungwa mkono na Biblia katika Mithali 30; 11-14
katika muonekano wao waloonekana hivi;-
Kutoka kushoto Sanguine, Phlegmatic, Chini choleric na melancholic
katika picha kama wanavyoonekana kwa mujibu wa mwanasaikolojia Galen haya ndio
makundi makuu manne ya watu
Jinsi ya
kuchukuliana na watu tofauti tofauti
Kuna
wakati inatulazimu katika maisha kuvunja urafiki na baadhi ya watu kutokana na
kushindwa kuchukuliana nao au kushindwa kuwaelewa wewnzetu kuwa ni watu wa
namna gani na ni wa kundi gani katika tabia sehemu hii itatusaidia kufahamiana
na pia kijifahamu ili iwe rahisi kwako kuchukuliana na watu woote rafiki
aliyekomaa hawezi kupoteza marafiki kwani anawajua rafiki zake nguvu zao na
udhaifu wao Biblia ina tuambia kuna aina nne za watu ona (Mithali 30;11-14).jamii hizi kisaikolojia huitwa Melancholic (mst
11), Phlegimatic (mst 12), Sanguine (mst 13) na Colerich (mst 14). Jamii hizi
zina sifa na madhaifu, mbalimbali ambazo ni taa ya kutuonyesha sifa zao Sifa
hizo ni kama ifuatavyo;-
Melancholy Kundi la
watu wenye Nafsi inayoumia.
Kwa
kawaida hili ni kundi la watu makini, wenye kuweza kunyambulisha mambo,ni wenye
kupendelea ukamilifu,wana mpangilio wa mambo wana mawazo mazuri na wenye
kujitoa jamii hii ya watu wengi wamekuwa wanasayansi wasanii wanafalsafa na
wagunduzi wa kubwa pia ni wachoraji,Hata hivyo ni kundi la watu
wasiojichanganya na jamii wapweke na wanaoumia mioyo,wanatazamia mambo ya
kuumiza ni wabinafsi,hana ushirikiano anatunza visasi wanahitaji tunda la roho
la furaha na amani.
Phlegmatic. Kundi
la watu wenye Nafsi iliyotuliana taratibu.
Hili
ni kundi la watu wanaojiamini,wanaojitegemea na kujitosheleza na ni wapenda
amani,kundi hili ni la watu wasioweza kubadilika kwa haraka na hupenda kusanifu
mambo,hata hivyo kundi hili hupenda kujilinda ni waoga,wachoyo hawahamasiki na
ni wavivu wanapenda usingizi na mambo yao ni polepole na ni wachokozi
chinichini hufanya chochote wanachoshauriwa
Sanguine. Kundi la
watu wenye Nafsi Changamfu.
Kundi
hili ni kundi la watu wachangamfu sana wanaweza kufanya marafiki kwa haraka
sana ni waigizaji wazuri na wasanii,ni wasemaji sana ,wacheshi,ni
marafikihawatulii na wasiojitegemea,hata hivyo sanguini ni wadhaifu,wanaonekana
kama hawana nidhamu waoga,wana haraka.
Choleric .Kundi la
watu wenye Nafsi Katili.
Kundi hili ni kundi la watu
jasiri,wanaojiamoni,ni viongozi hufanya mambo yatokee ni watendaji wanaona
mbali wanaweza kufanya maamuzi lakini ni wenye hasira ,hila,kujigamba,hana
hisia za huruma,ni katili anajitoa sadaka kwa kufanya kazi kupita kawaida.
Kuna
uwezekano wa kujijua kuwa uko kundi gani kwa kuangalia sifa za makundi hayo
nzuri na dhaifu kisha unachukua idadi ya sifa utakazozipata unazidisha kwa mia
na kugawa kwa idadi ya sifa zote hapo utajijua.
Mfano tunamjadili
Kamote kujua kuwa Yeye ni kundi gani hivi ndivyo tutakavyofanya
Melancholy
|
|
|
Phlegmatic
|
|
|
Sanguine
|
|
|
Choleric
|
|
|
Anauchungu
|
|
|
Anajiamini
|
|
|
Mcheshi
|
|
|
Ni katili
|
|
|
Ana jitoa
|
|
ü
|
Mtaratibu
|
|
|
Msemaji
|
|
|
Anahasira
|
|
|
Ana kipawa
|
|
|
Anajitosheleza
|
|
|
Muigizaji
|
|
|
Jasiri
|
|
|
Ni mkamilifu
|
|
|
Habadiliki
|
|
|
Anakelele
|
|
|
Mzalishaji
|
|
|
Mbunifu
|
|
|
Hahamasiki
|
|
|
Muoga
|
|
|
Mtendaji
|
|
|
Makini
|
|
|
Ana sanifu
|
|
|
Muongo
|
|
|
Kiongozi
|
|
|
Hashirikiani
|
|
|
Mvivu
|
|
|
Muhamsishaji
|
|
|
Anaamua
|
|
|
Hanaharaka
|
|
|
Ana choyo
|
|
|
Hana aibu
|
|
|
Anakisasi
|
|
|
Mgunduzi
|
|
|
Hana haraka
|
|
|
Si mtendaji
|
|
|
Hujisifu
|
|
|
Mchoraji
|
|
|
Hujilinda
|
|
|
Kigeugeu
|
|
|
Ana hila
|
|
|
hunyambulisha
|
|
|
Hupendaamani
|
|
|
Ana haraka
|
|
|
hajihurumii
|
|
|
Unaweza
kuona kuwa alama za x zinaonyesha sifa ambazo Kamote hana hivyo katika
Melancholy Kamote hana alama tatu na
alama nane zilizo tupu ni sifa alizo nazo sifa zitakazopatikana utazigawa kwa
12 sawa na jumla ya sifa zote za kila sifa hivyo katika melancholy Kamote ana
sifa nane na anakosa tatu hii ni kusema kuwa katika melancholy na sifa
nnyingine Kamote atakuwa na sifa zifuatazo kwa kila moja ile itakayokuwa na
asilimia kubwa zaidi ya wengine ndiyo sifa ya mtu huyo mfano mzuri ni huo hapo
chini
Melancholy
kwa Kamote ni = 8/12 X 100=66 %
Phlegmatic
kwa Kamote ni= 7/12 X 100=58%
Sanguine
kwa Kamote ni=7/12 X 100=58%
Choleric
kwa Kamote ni = 12/12 X 100=100%
Hivyo Kamote ni Choleric
kwa asilimia 100 lakini anazo sifa nyingine kutoka katika makundi mengine na
kwa kawaida zile zinazojitokeza kwa wingi zaidi zile mbili hutabiri wazazi wa
Kamote kuwa mmoja ni Melacholy na mwingine ni Choleric na kwa kawaida Melancholy akioana na choleric melancholic
huumizwa hivyo mmoja wa wazazi wa Kamote katika ndoa alikuwa ni nafsi
iliyoumizwa na kitaalamu Yule anayeumia hufa haraka na ni kweli mzazi mmoja wa
Kamote yaani mama yangu alikufa mwaka wa 1984 hivyo chati hizi husaidia hata
kujua sifa za wazazi na taabu zao katika ndoa na kama mmoja yuko hai au lapia unaweza kufanya utabiri usiorasmi
Jinsi ya kufanya
majaribio mengine ya kisaikolojia
Saikolojia
ni sayansi hivyo inahitaji majaribio wakati mwingine unaweza kupima uwezo wa
mtu wa kiakili na utendaji wake au kupima aina kuu za watu yaani yale mafungu
manne na utendaji wao wa ubongo lakini kabla hatujaonyesha namna majaribio
hayao yawezavyo kufanyika ni muhimu tukajifunza kwanza uwezo wa utendaji wa
ubongo Intelligence
Intelligence
inapimwa katika kipimo cha uwezo wa akili mara mia kugawanya kwa umri wa
muhusika ndipo unapata uwezo wa utendaji wa akili ambao kitaalamu unaitwa
intelligence Qutient (IQ) hivyo
IQ Intelligence Quotient = Uwezo wa kiakili X 100
Umri husika
Matokeo
ya kipimo hiki yatakuonyesha kuwa watu wenye uwezo mkubwa kiakili watakuwa
hivi;-
Watu
wenye IQ kutoka 50 - 75 wanaitwa Morons
Watu
wenye IQ kutoka 25 – 50 wanaitwa Imbeciles
Watu
wenye IQ kutoka 0 - 25 wanaitwa Idiots
Watu
wenye IQ kutoka 75 -100 wanaitwa Nomal
Watu
wenye IQ kutoka 100- na zaidi ni Geniases
Aidha
mazoezi ya kisaikolojia ya kupima ubongo wa mwanadamu unaweza kufanyika kwa zoezi
kama lifuatalo
Maelekezo
chagua Fedha kama za sarafu sio za note kama kumi kisha zitengeneze katika
mfano wa Piramidi au umbile la pembe tatu mfano huu
Baada
ya kuwa na kiasi hiki cha Fedha zilizo
katika mtindo wa umbo la pembe tatu wajaribu wahusika kama kumi hivi watano wa
kike na watano wa kiume waambie wanaruhusiwa kugusa sarafu tatu tu ili kubadili
umbile la pembe tatu ielekee chini wakati huu utakuwa unahifadhi Kumbukumbu za
utendaji wao na zoezi litafanyika kwa Dakika tatu tu kama atashindwa mzuie kuendelea na rudisha
piramidi katika hali ya kawaida na jaribu watu wengine unaweza kufganya hata
kwa watu 15-20 nusu wawe wanawake na nusu wanaume majibu utakayo pata yatakusaidia kujua uwezo
wa mtu kiakili na utaweka Kumbukumbu katika namna ifuatayo
Jina…………………………………………………….Jinsia……………………………………………...
Muda
aliotumia…………………….Dakika………………….Sekunde………………………………..
Je
alikuwa na shauku yoyote kuhusu somo au kazi uliyompa………………………………………..
………………………………………………………………………………………………………………
Baada
ya zoezi jumlisha muda woote uliotumika gawanya kwa idadi ya watu uliowafanyia
zoezi la somo, kisha tafuta wastani wa muda uluiotuiwa na wanaume na kisha
wastani wa muda ulio tumiwa na wanawake kisha jibu maswali haya ukikumbuka kuwa
lengo ni….Kujua utendaji wa akili za wanawake na wanaume, ukikumbuka idadi ya
watu uliowafanyia zoezi wanawake wangapi na wanaume wangapi ni nini wastani wa
Muda uluiotumika kwa pande zote kisha kwa wote, kisha ni kundi ganimliko juu
wanawake au wanaume? Kisha umejifunza nini katika kupima bongo za wanawake na
wanaume kisaikolojia au hata mtu moja moja.
UHUSIANO WA SAIKOLOJIA NA ANTHROPOLOJIA
(ANTHROPOLOGY
& PSYCHOLOGY)
Maana ya Jumla
Anthropology ni neno lenye asili
yake katika lugha ya Kiyunani/Kigiriki. Neno hili ni muungano wa maneno mawili:
anthropos na logia. Anthropos maana yake ni mwanadamu na Logia maana yake ni
elimu juu ya jambo fulani. Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa anthropology ni elimu
inayohusu mwanadamu na Nyanja mbalimbali za maisha maisha yake.
Kwa
ujumla anthropology inajaribu kuchunguza mambo yanayomhusu mwanadamu kama vile;
jinsi watu wanavyoishi, wanavyofikiri, wanazalisha nini na kwa jinsi gani watu
hao wanaishi katika mazingira waliyomo. Pia wanataalamu wa anthropology
(anthropologists) wanachunguza tofauti kati ya watu na watu na mambo ambayo
watu hao wanayo kwa pamoja (diversity and what they have in common).
Anthropologists wanafanya utafiti wao kwa kujiuliza maswali kama vile lini,
wapi na jinsi gani mwanadamu ameanza na kuendelea (evolve)? Kwa jinsi gani
jamii zimeanza na kuendelea tangu zama za kale hadi leo hii?
Anthropologia
ya Kikristo (Christian Anthropology)
Anthropologia
ya Kikristo ni elimu juu ya mwanadamu na uhusiano wake na Mungu. Inatofautiana
na anthropologia ya elimu jamii kwa kuwa yenyewe inajifunza habari za mwanadamu
kwa kutumia kipimo cha theologia ya Kikristo. Anthropologia hii inachunguza juu
ya asili ya mwanadamu au vitu vinavyofanya mwanadamu awe
mwanadamu.Inajishughulisha na uhusiano uliopo kati ya mawazo makuu kama vile mwili,
nafsi na roho vitu ambavyo muungano wake kwa pamoja ndivyo vinavyotengeneza
mwanadamu. Vinachunguza mambo mambo kwa kuweka msingi wake katika maandiko
matakatifu, yaani Biblia.
Mwili,
Nafsi na Roho
Tunapojifunza juu ya
anthropologia ni muhimu sana kuchunguza juu ya mambo hayo matatu.
i.
Mwili: Hii inatokana na neno la Kiyunani
lijulikanalo kama Soma .Hii ni sehemu ile ya mwili ambayo inaonekana na inaweza
kuguswa kwa mikono ya nyama. Hii ni sehemu ambayo huoza na kuharibika wakati
mwanadamu anapokufa. Lakini Kanisa kulingana na mapokeo ya Kanisa ni kuwa mwili
utafufuliwa katika mwisho wa duni.
ii.
Nafsi: Neno hili linaelezwa vizuri na
dhana mbili; moja ya Kiyahudi na nyingine ya Kiyunani. Kwa Kiebrania Nafsi ni
Nephes. Kwa kiyunani neno hili lina julikana kama Psyche. Neno hilo ndiko neno
Psychology linapotokea. Katika Kiebrania Nephes ina maana inayokaribia na pumzi
au kiumbe kinachopumua. Katika upana wake nephes ina maana ya uhai kamili wa
kiumbe. Hapo zamani neno hili halikuwa na maana kama tuliyonayo leo ya roho
isiyokufa hata kama mwili utakufa. Neno hili lilimaanisha mwadamu katika ujumla
wake. Agano Jipya ambalo liliandikwa Kigiriki limetumia neno Psyche. Wayunani
waliona kuwa Psyche ni nguvu isiyoonekana iliyomo ndani ya kiumbe hai ambayo
inakipa nguvu na mwendo. Kumekuwa na mabishano kuwa je mwanadamu ana nafsi au
yeye mwenyewe ndiye nafsi. Kulinga na mwanzo 2:7 mwandamu yeye mwenyewe ndiye
nafsi hai.
iii.
Roho: Katika Kiebrania neno hili
linajulikana kama Ruah na katika Kiyunani neno hilo linajulikana kama Pneuma.
Neno hilo lina mana ya pumzi. Ni sehemu ya mwanadamu ambayo haionekani kwa
macho ya nyama. Kuna baadhi ya wasomi wanaamini kuwa roho na nafsi ni kitu
kimoja na wengine wanaona kuwa roho na nafsi ni vitu viwili tofauti.
Mwanadamu
ni Nini
Historia inaonenyesha kuwa
watheologia wa Kikristo wanekuwa katika mabishano bila ya kukubaliana juu ya
suala la kuwa mwanadamu ni muunganiko wa mambo gani au mwanadamu amegawanyika
katika sehemu ngapi? Kwa ujumla yapo mawazo ya aina kuu tatu ya mgawanyo wa
mwanadamu. Mawazo hayo ni Dichotomism, Trichotomism na Monism.
i.
Dichotomism (sehemu mbili): Wanazuoni wa kundi hili wanasema
kuwa mwanadamu amegawanyika katika sehemu kuu mbili: Mwili na nafsi au
roho(roho na nafsi kwa watu hawa ni kitu kimoja). Mwili ni sehemu inayoonekana
na kushikika (material) na roho au nafsi ni sehemu isiyoonekana au kushikika (spiritual).
Haya ni mawazo yanayoungwa mkono na watu wengi. Kulingana na mawazo hayo, roho
au nafsi vinakaa ndani ya mwili. Roho na nafsi huondoka katika mwili mtu anapokufa.
Lakini vitarudi tena katika mwili wake siku ya ufufuko.
ii.
Trichotomism (sehemu tatu): Watheologia wachache wanaamini
kuwa mwanadamu amegawanyika katika sehemu tatu yaani mwili na roho na nafsi.
Watheologia hawa wanatumia vifungu vituatavyo vya Biblia kuelezea jambo hilo;
1Thes. 5:23 na Ebr 2:12.
iii.
Monism (sehemu moja): Wanatheologia wa kisasa (modern)
wanashikilia msimamo kuwa mwanadamu ni sehemu moja tu. Mwanadamu hawezi
kugawanyika (holism).Kwa hiyo hao wanataka mwanadamu achukuliwe kama mtu bila
ya kumgawanya.
Asili/Chanzo(origin)
cha Mwanadamu
Swali juu ya asili ya mwanadamu
limesumbua wasomi wengi duniani tangu kale hadi hivi leo. Mila, desturi,
ustaarabu na dini mbalimbali zina hadithi au hekaya tofouti juu ya wapi
mwanadamu ametoka au jinsi gani mwanadamu amepata kuwepo duniani. Elimu juu ya
asili ya mwanadamu na maendeleo yake ya kibailojia ni tawi la anthropologia
linalojulikana kitaalam kama paleoanthropology.
Tawi hili la anthropologia linachunguza juu ya mila na desturi za watu,
jamii, na yaliyomo katika bailogia ya mwanadamu. Paleoanthropology inachunguza
zaidi juu ya tabia za kibaologioa na tabia za nje za mwanadamu (physical traits
and behaviors). Kwakifupi tunaweza kusema kusema kuwa paleoanthropology
inachunguza juu ya evolution. Kwa kufanya hivyo uwanja huo wa elimu unaangalia
juu ya uhusiano wa kitabia uliopo kati ya mwanadamu na viumbe wengine duniani.
Yapo mawazo mbalimbali na mapokeo
mengi yanayozungumzia suala la asili ya mwanadamu, kati ya mawazo hayo nadharia
mbili ndizo zinazotumiwa na kuelezea asili ya mwanadamu. Nadharia hizo
evolution theory na creation theory.
i.
Evolution Theory
Wataalamu wanaofundisha asili ya
mwanadamu kutumia nadharia hii wanasema kuwa mwanadamu alibadilika kutoka
katika viumbe rahisi (simple) kwenda katika viumbe vigumu zaidi (complex). Wao
wanaamini kuwa mwanadamu alibadilika kutokana na mazingira na mahitaji hadi
kufikia katika hali aliyonayo sasa.
Watu hawa wanaamini kuwa
mwanadamu yupo katika kundi moja na wanyama wa jamii ya nyani (chimpanzee) wote
wanatoka katika genus iitwayo homo. Kwamba mwanadamu na nyani wanatoka katika
wazazi (ancestors) wa aina moja. Walitoka katika babu hao kiasi cha miaka
milioni tano hadi saba iliyopita.
Watalaamu hao wanasema kuliwahi kuwepo na species nyingi sana za homo
lakini zimetoweka zamani sana. Miongoni mwao ni Homo erectus ambayo ilipatikana
kule Asia, Homo Neanderthalensia ambaye alikuwa anapatika huko Ulaya na Homo
Sapeans ambao walipatikana hapa Afrika. Inasemekana kuwa Homo Sapeans
walikuwepo duniani kati ya miaka Laki nne na Hamsini elfu iliyopita.
Wataalamu wanasema kuwa mwanadamu
aliyepo duniani leo hii ni matokeo ya Homo Sapean. Wanasayansi wanaamini kuwa
bara la Afrika ndilo asili ya wanadamu ulimwengu. Hii ni kwa sababu Homo Sapean aliishi Afrika
alihamia katika bara la Asia na Ulaya na kuchukua nafasi ya Homo erectu na Homo
Neanderthelensia.
Hata hivyo nadharia hiyo inashindwa
kuonyesha asili ya uhai. Kumekuwa na mawazo kuwa uhai ulianzia majini kwa
wanyama wadogo sana hadi kufikia wanayama wakubwa. Lakini bado haijafamika kuwa
uhai huo uliokuwa majini unatoka wapi. Wazo la msingi hapa ni wanasayansi
wameshindwa kufahamu asili ya DNA. Kwa hiyo bado kunahitajika njia nyingine ya
kuelezea kuwepo wa uhai ulimwenguni. Haja hiyo ndiyo inayoleta suala la
nadharia ya uumbaji.
Hatari ya mawazo hayo ni kuwa
yanapunguza heshima ya mwanadamu. Pia yanaondoa uwepo wa muumbaji. Zaidi ya
yote yanataka kusema kuwa mwanadamu hawajibiki kwa mtu yoyote.
ii.
Creation Theory
Imani juu ya uumbaji inajulikana
kama creationism. Nadharia ya uumbaji inaonyesha kuwa dunia na viumbe vilivyomo
vimeumbwa na muumbaji na kuwekewa utaratibu wa jinsi ya kuenenda. Uumbaji huu
unajulikana kama exnihilo. Hii maana yake ni kuwa uumbaji huo ulifanyika
pasipokuwa na kitu cha kuumbia. Yaani uumbaji ulifanyika kutoka katika hakuna
kwenda katika kuwepo (from nothing to something). Mawazo haya yanapingana na
mawazo yanayosema kuwa mwanadamu hakuwaameumbwa kama alivyo leo bali alikuwa
mnyama kama nyani hapo zamani. Nadharia hii inaonyesha kuwa mwanadamu ameumbwa
na mamlaka kubwa kuliko yeye. Tena anaowajibu wa kufuata kile ambacho muumbaji
wake anataka kifuatwe na mwanadamu.
Kulingana na Biblia (Mwa 1:26,
27/2:7) mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Kulingana na maandiko kuna mambo
makuu matatu katika uumbaji wa mwanadamu: mavumbi ya ardhi, Pumzi na Nafsi
hai.Mwanadamu ameumbwa (kwa mfano na sura ya Mungu, Image and likeness of God).
Kwa kuwa wanadamu wote wameumbwa kwa mfano wa Mungu, wanadamu wote ni sawa na
wote wanahitaji heshima sana. Wanadamu wote wana haki sawa.
Umoja
wa tabia ya Binadamu
Ushahidi
unaonyesha kuwa wanadamu wote duniani wanafanana katika tabia zao.Tofauti zao
za rangi, taifa sio kitu. Ndani yao ni sawa katika mahitaji na tabia zao ja
jumla (Mdo. 17:26; Rum5:12,19; 1Kor.25:21,22). Kuna aina nne za ushahidi
unaothibitisha jambo hilo. Ushahidi wa kihistoria, ushahidi wa lugha, ushahidi wa
saikolojia na ushahidi wa asili au maumbile ya kimwili ya wanadamu.
Swali
kuhusu asili ya roho ya Mwanadamu
Wanatheologia wakubwa wamekuwa
katika mabishano makali juu ya nini asili ya roho ya mwanadamu. Yapo mawazo
makuu matatu yanayoshughulikia swali hilo.
i.
Kabla ya uumbaji: Watheologia wanaunga mkono wazo
hili ni pamoja Origen ambaye ametumia mawazo ya Plato. Wao wanasema kuwa roho
ya mwanadamu ilikuwepo kabla ya kuumbwa kwa mwanadamu. Wao waliamini kuwa roho
ya mwanadamu ilikuwepo duniani na unapofika wakati wake inazaliwa duniani.
ii.
Kurithi Kutoka kwa wazazi: Miongoni mwa watheologia
wanaoamini nadharia hii ni Tertuliano, Marthini Luther. Wao wanaona kuwa ni
kweli Mungu amemuumba mwanadamu. Lakini Mungu aliumba roho mara moja na kuiweka
ndani ya Adamu na Hawa. Baada ya hapo wanadamu wanarithi roho zao kutoka kwa
wazazi wao. Yaani wengine huzaliwa na roho zao.
iii.
Uumbaji katika wakati: John Calvin na Jerome ni miongoni
mwa watheologia wanaounga mkono wazo hili. Wao wanaamini katika wakati Fulani
wa maisha ya mtu roho yake inaumbwa na kuwepo duniani.
DHAMBI
Tawi la theologia
linaloshughulika na masuala ya dhambi linajulikana kitaalam kama hamartiology.
Elimu hiyo inashughulika na asili ya dhambi, madhara yake kwa mwanadamu matokeo
yake na jinsi ya kuepukana na dhambi.
Dhambi
ni neno la kawaida sana katika maisha ya kila siku. Lakini ni neno gumu sana
kuelezea mana yake. Pia ni vigumu sana kusema ni tendo gani au jambo gani
linapofanywa huwa dhambi au sio dhambi. Pia ni vigumu sana kufahamu kuwa jambo
gani au tendo gani hugeuka wakati gani kuwa dhambi.
Lakini
sisi kama Wakristo tunacho kipimo cha kupimia dhambi, yaani Neno la Mungu.
Lakini pia pamoja na kuwa na kipimo hicho cha kupimia dhambi, bado hatuwezi
kuwa njia moja tu ya kuelezea dhambi. Mahali pengine dhambi inategemea
mazingira na mapokeo ya watu husika. Kwa hiyo hata suala la dhambi linahitaji
kufanyiwa Contextualization.
Mtazamo
wa Biblia Kuhusu Dhambi
Mtazamo wa Biblia kuhusu dhambi
umegawanyika katika sehemu kuu mbili kama Biblia yenyewe ilivyogawanyika. Upo
mtazamo wa Agano la Kale ambao ni mtazamo wa Kiyahudi na mtazamo wa Agano Jipya
ambao ni mtazamo wa Kiyunani.
i.
Mtazamo wa Dhambi katika Agano la
Kale.
Kwa
mtazamo wa Kiyahudi, dhambi ni kitu chochote kile kinachokwenda kinyume amri
takatifu za Mungu. Wayahudi walifundisha kuwa dhambi ni tendo la wala siyo
hali. Katika lugha ya Kiebrania dhambi inajulikana kama avera. Kwa Wayahudi
dhambi ipo katika viwango vitatu. Kwanza mtu afanye dhambi kwa kukusudia (B’mezid).
Hii ni aina mbaya zaidi ya dhambi. Pili ni mtu anayefanya dhambi bila ya kukusudia
(B’shogeg). Mtu huyu atawajibika kutokana na dhambi yake, lakini dhambi hii
inachukuliwa kama dhambi ndogo.Na aina ya mwisho ni dhambi anayoifanya mtu kwa
kuwa amekulia katika mazingira ambayo siyo ya Kiyahudi na hivyo akajikuta
amevunja sheria. Mtu huyo alijulikana kama Tinok Shenishba. Mtu huyu hawajibiki
kwa dhambi yake aliyofanya.
ii.
Mtazamo wa Agano Jipya Kuhusu dhambi
Kwa
Wakristo dhambi ni uvunjaji wa sheria. Neno la Kiyunani linalotafsiriwa kama
dhambi linaitwa Hamartia. Hamartia maana yake ni kupita njia isiyo sahihi au
kukatiza njia. Maana nyingine ya dhambi ni kukosea shabaha. Kwa kifupi dhambi
ni uasi (1Yoh.3:4). Missing the mark kuacha alama ya mstari au kupuuzia alama
za barabarani katika hali kama hii kile kilichokatazwa katika agano jipya na
mtu akakikiuka anakuwa amefanya dhambi hata hivyo dhambi hutendwa kumuelekea
Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni