Somo la tatu
Vijana na Hatari ya madawa ya kulevya
Nyakati
hizi tulizonazo ni tofauti sana na nyakati zilizopita dunia inakabiliwa na
matatizo mengi yakiwemo mmomonyoko mkubwa wa maadili,rushwa,utoaji wa mimba,
kuongezeka kwa vitendo vya ushoga na usagaji,ubakaji, uhalifu, watoto wa
mitaani,ulevi wa kupindukia, na wimbi
kubwa la umasikini ,likiwemo wimbi hili la matumizi ya dawa za kulevya,kama
kanisa litakaa kimya,jamii hii ya watu wanaokumbwa na mikasa ya aina hii ndio
wataathiri hali ya taifa na kanisa la leo,na kama ilivyo kwa ukimwi,kushindwa
kuzungumzia msimamo wa kibiblia dhidi ya hali ya madawa ya kulevya ni sawa na
kuwa tayari na jamii au kanisa la watu dhaifu wasioweza kutumainiwa kwa namna
yoyote ile kuliendeleza kanisa na taifa, kwani madawa ya kulevya yana athari kubwa kwa msingi huo
nitazungumzia hali hii katika maeneo makuu matatu.
- Ufahamu kuhusu madawa ya kulevya.
- Madhara yatokanayo na madawa ya kulevya.
- Jinsi ya kuepuka madawa ya Kulevya.
Ufahamu kuhusu madawa ya
kulevya.
Madawa ya kulevya ni kemikali yoyote asilia
au ya kutengenezwa kiwandani, ambayo huleta badiliko la kihisia au ufahamu
pindi inapotumiwa. Dawa hizi huumba hali tegemezi (Drug dependens) ambayo ni
athari za kisaikolojia na madhara
yatokanayo na madawa haya hali hii tegemezi ni hali ya kutoweza kufanya
lolote bila kuyatumia au kushindwa kufanya jambo baada ya kuamua kuacha na kuwa
kadiri unavyotumia uajikuta unahitaji kutumia kwa kawaida madawa haya yana
shughuli maalumu kwani mengine hutengenezwa kwa kusudi latiba za kibinadamu
isipokuwa yanapotumika vibaya athari zake ni kama hizi,dawa nyingine zozote pia
zinapotumika nje ya maelekezo ya daktari au vipimo husia huweza kuleta athari
Fulani ikiwa ni pamoja na kuharibu ini,moyo,ubongo n.k. tabia hii huitwa
matumizi mabaya ya dawa (Drug abuse).katika somo hili sizungumzii zaidi
matumizi mabaya ya dawa bali nazungumzia madawa ya kulevya ambayo yamo katika makundi kama matano;
- Zinazopunguza maumivu makali na kasi ya ufanyaji kazi wa mfumo wa fahamu,hizi ni heroine,morphine,codein n.k.
- Zinazo punguza kasi ya utendajikazi wa ubongo (depressant) hizi ni kama vile valium, pombe, viyeyushia gundi, petrol, rangi n.k.
- Zinazoongeza kasi ya utendaji kazi wa mfumo wa fahamu (Stimulants) hizi ni kama Caffene,mandrax, nicotine,zikiwemo sigara,bangi,mirungi na pariki.
- Zinazoleta maono yasiyo na uhusiano halisi day dreeming hizi ni pamoja na bangi,aina Fulani za uyoga na mescaline n.k.
Dawa hizo nyingine ni za asili na nyingine
za viwandani, haya ndiyo madawa yanayotumiwa na watu wengi hususani vijana.
Madhara yatokanayo na madawa ya
kulevya.
Madawa ya kulevya yana madhara makubwa sana
kijamii, kiuchumi, kiafya na kiroho kwa msingi huu hatushauri kabisa vijana
kujiingiza katika swala zima la utumiaji wa madawa ya kulevya.
Pichani mtu yuleyule aliyetumia Dawa za kulevya kwa miaka mitatu tu
Athari
za kijamii.
Matatizo ya madawa ya kulevya yanaweza kusababisha matatizo makubwa katika jamii ,ikiwemo migogoro ya aina
mbalimbali,kwa mara ya kwanza kabisa katika biblia ,tunaonyeshwa jinsi familia
ya Nuhu ilivyokumbwa na matatizo yaliyotokana na ulevi ambapo ilibidi Nuhu kumlaani
mjukuu wake kupitia mwanae Hamu, Hii ni kwa sababu ya kutokujiheshimu kwa Nuhu
baada ya kuwa mlevi wa kupindukia na kupalekea mtumishi huyu wa bwana kuwa uchi
na mwanae na mjukuu wake wakaona uchi wa baba yao,(Mwanzo 9;20-23)Ulevi unapelekea kuvunjika kwa heshima hata kama mtu
huyo ni mwenye kuheshimika,ulevi unaweza kupelekea kuwepo kwa ngono hata zile
zisizotegemewa walevi wengi hujikuta wanafanya ngono bila tahadhari za kutosha
na hivyo kujikuta wakiwa na maambukizi, Biblia inaonyesha pia jinsi Lutu
alivyolala na binti zake na kuzaa nao watoto baada ya kufanikiwa kumlevya baba
yao na kufanikiwa kufanya naye ngono (Mwanzo
19;30-38) kwa ujumla muda usingeweza kutosha kusimulia visa na mikasa
itokanayo na ulevi katika jamii hata hivyo familia ambazo zimekulia katika ulevi huathirika sana na
baadhi ya maeneo ambayo watu huathirika ni pamoja na ,Ugomvi wa kupindukia
mateso na hata familia kukosa matunzo (Mithali
20;1),aidha tabia za kutumia vilevi
yakiwemo madawa hupelekea watu kuwa wezi,majambazi,vibaka na kuwepo kwa tabia
ya kuibiwa vitu vidogo kwa vikubwa,watu wa jinsi hii hawashindwi kabisa kufanya
ubakaji,kutokujali,umalaya uliokithiri, kukosa elimu, maendeleo duni, kufukuzwa
kazi kufanya uhalifu, kuharibu mamba au kuathiri afya ya mtoto kufungwa,ajali
za barabarani na uhalifu wa kutumia silaha, Aidha jamii inakosa mtu au watu wa
kuwatumainia kwa jambo lolote, na wakati mwingine kuwa na jamii ya watu
tegemezi.
Athari
za kiuchumi.
(Isaya
55;2).Watumiaji wa madawa ya kulevya pia huathiriwa na maswala ya kiuchumi
(Mithali 23;19-21).Kwa sababu madawa
haya ni ghali na hivyo mtumiaji anahitaji fedha ili kujikidhi na maawa
hayo,Watumiaji hao wakati mwingine kwa
sababu ya ulevi huvunja vyombo majumbani au kusababisha ajali za magari
barabarani,Kunakuwa na gharama za kimatibabu za kuwatibu punde wapatapo ajali
au wanapotibiwa kuwarejesha katika hali ya kawaida, watu hao huthamini ulevi
kuliko chakula.
Athari
za Kiafya.
Miili tuliyonayo ni mali ya
Mungu,tunapookolewa tunakuwa Hekalu la roho mtakatifu (1koritho 3;17,6;19-20), miili hii ni zawadi kutoka kwake na hivyo
tunapoitumia visivyo halali ni lazima
tutawajibika kuitolea hesabu,Bahati mbaya sana watimiaji wa madawa ya kulevya
wanakuwa addicted yaani wana kuwa na
tabia endelevu ya kutaka kuyatumia madawa hayo,na inakuwa vigumu kuyafurahia
maisha bila kutumia,Watumiaji wa madawa ya kulevya hukabiliwa na tatizo la
maambukizi ya vvu Virusi vya ukimwi kwa
sababu ya tabia zao za kuyatumia madawa hayo ambayo wakati mwingine huhitaji
kujichoma kwa kutumia sindano moja,Wengine hupoteza uwezo au hamu ya kujamiiana
au kushiriki tendo la ndoa,Wanawake wanaotumia madawa hayo huwa na uwezekano wa
kuzaa mtoto punguani yaani wenye akili taahira au ulemavu,kuna magonjwa kama
maradhi ya mapafu,Moyo,kansa, matatizo ya fahamu,usingizi kuuokosa au kulala
sana,kupoteza kumbukumbu,maamuzi ya hovyo homa ya ini na kupungua uzito kwani
watumiaji wengi hususani wa barani Afrika lishe zao ni duni hivyo wanakondeana
kupita kawaida.
Athari
za Kiroho.
Hebu jaribu kuwaza kuwa watu hawa
walioathiriwa na madawa ya kulevya
wanaokolewa na kuja kanisani na kuwa mshirika ama kiongozi au hata kuwa
na wito wa kumtumikia mungu je unadhani wanaweza kutumika ipasavyo(Efeso 5;18) “Tena msilewe kwa mvinyo
ambamo mna ufisadi bali afadhali mjazwe Roho” kimsingi Biblia inakataza ulevi na inaeleza kuwa walevi hawana nafasi katika ufalme wa
Mungu (1Koritho 5;11,Galatia
5;19-21,1Koritho 6;9) Mtu mlevi au muathirika wa madawa ya kulevya ni
vigumu kwake kuabudu katika roho na kweli kwa ni madawa haya huharibu nguvu
ambazo zingehitajika kwa utumishi (Mithali
20;29).Mungu hangependa kabisa kuwatumia vijana walioharibika akili kwa
dawa za kulevya kwani wakati mwingine wanakuwa wagumu kuelewa,busara
imeharibika,Hii haimaanishi kuwa walevi hawapokelewi na Mungu hapana
wanapokelewa isipokuwa watakua na athari za madawa yale na hivyo ni ngumu
kuwatumia kwa utumishi,Biblia inasema mpende Bwana Mungu wako wote na kwa roho
yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote,tunawezaje kuzitumia
nguvuzetu na akilizetu zilizo haribiwa na madawa ya kulevya katika kumpenda
Mungu? Muhubiri 12;1 Biblia inasema “Mkumbuke
muumba wako siku za ujana wako,kabla
hazijaja siku zilizo mbaya wala
haijakaribia miaka utakaposema Mimi sina furaha katika hiyo” Ningependa kuwaasa
vijana kuwa wautumie ujana wao vizuri kwa ajili ya Mungu na kwa ajili ya taifa
letu zuri alilotupa Mungu nchi ya baba zetu, tukiutumia ujana wetu kwa faida ya
mungu na jamii inayotutegemea na kama umejiingiza katika janga hili bado ziko
namna ya kutoka huko sehemu ifuatayo
inatuelekeza namna ya kujikwamua
na janga hili ubarikiwe unapoendelea kujifunza.
Jinsi
ya Kuepuka madawa ya kulevya.
Kwa
kawaida wengi wanao tumia mdawa ya kulevya huwa na visingizio mbalimbali vingi
sana, ambavyo huvitumia ili kuhalalisha matumizi yao ya madawa ya kulevya,
ulevi na uvutaji vifuatavyo ni baadhi ya sababu wazitoazo watumiaji wa madawa
ya kulevya wanasema wao hutumia ili kusahau matatizo, au baada ya kushawishiwa
na marafiki zao,kwa ajili ya upweke,kupunguza mawazo,umasikini,udadisi au
kuijifunza kutoka katika familia zao,kukataliwan.k.
Sababu hizi zote zinazotolewa na watumiaji
wa dawa za kulevya hazina msingi kama watakuwa wamezingatia zile staid za
kimaisha tulizojifunza katika somo hili.kama ni ushawishi kwa vyovyote
ukizingatia uchaguzi sahihi wa aina za marafiki huwezi kushawishika,Nimesema
sababu hizi si za msungi kwani Yesu Kristo alipitia aina yoote hiyo ya
matatizo,ambayo vijana wengi hupitia ,alifiwa na baba yake mlezi Yusufu alikuwa
mpweke duniani kuliko mtu awaye yote alikuwa na huzuni, na masikitiko,alikuwa
masikini roho yake ilikuwa na huzuni nyingi kiasi cha kufa alisalitiwa na watu
wake na hata rafiki yake wa karibu
aliyemgharamikia,aliteseka msalabani na kuaibishwa akiwa uchi kabisa mbele ya
watu waliomheshimu lakini pamoja na hayo yoote hakutafuta faraja kwa kilevi
kwani hata alipokuwa msalabani mtu alimletea kileo ambacho kingemfanya aiwena
fahamu,apunguze migandamizo na upweke lakini alikataa (Marko 15;23) lakini alipopelekewa kinyaji ambacho sio mvinyo
alikipokea (Yohana 19;18-30)Pamoja
na yote ambayo Yesu aliyapitia yakiwemo mashitaka ya
uongo,kukataliwa,kusalitiwa bado hakukatataamaa na kuamua kuwa mlevi.
Dawa ya kuvunjika moyo na kukatishwa tama
na upweke ni kujitoa kwa Mungu,katika sala na maombi,biblia inasema na tumtwike
yeye fadhaa zetu zote maana yeye hujishughulisha sana na mambo yetu,furaha ya
kweli haipatikani kwa kunywa gongo au madawa ya kulevya furaha ya kweli
hupatikana kwa Yesu kwa kumkubali na kumwamini moyono Yeye alisema njooni
kwangu ninyi nyote wenye kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha ,Mjaribu
Yesu,vunja urafiki na walevi,jifunze kujitia nidhamu jiwekee mipaka,muombe
Mungu na tembea na wenye hekima, Kuwa mtu waibada na utakuwa huru toka katika
madawa ya kulevya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni