UFAHAMU KUHUSU MANABII WADOGO, STUDIES IN MINOR PROPHETS
UTANGULIZI;
-Moja ya majukumu makubwa
ambayo Taifa la Israel lilipewa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanalishika agano
la Mungu walilokabidhiwa katika mlima wa Sinai.
-Unapo
gusia tu kuhusu Historia ya Taifa la Israel ni lazima utakutana na vitu muhimu vitatu
vifuatavyo;-
Habari
kuhusu Mungu wa Israel
Historia
ya Israel na uhusiano wake na Mungu
Historia
ya kinabii na jinsi Mungu anavyo jishughulisha na wanadamu woote kupitia Taifa
la Israel.
-Historia
ya kinabii inatengeneza daraja muhimu kati ya Mungu na watu wake na kozi hii
Ufahamu kuhusu Manabii wadogo inagusa maeneo muhimu ya kinabii kuanzia kati ya
mwaka 853 k.k. Mpaka karibu na wakati wa uongozi wa Nehemiah mwaka 425 k.k,
Manabii waliifanya kazi kwa Nguvu na ujasiri katika wakati mgumu Mungu
alipowaita watu hao, Kazi kubwa ikiwa ni kuwaonya watu kumrudia Mungu na
kulitunza agano lake kwa usalama wao.
-Mungu
aliwatumia Manabii kushughulikia Maswala ya dini na siasa na maadili katika
siku zao ambazo hazikutofautiana na siku zetu, kulikuwa na hofu za
njaa,vita,Mmomonyoko wa maadili na imani potofu zikiwemo ibada mbaya za
mabaali,unafiki, kutokuamini na ukengeufu vilitawala
-Mungu
wakti huu aliwatuma Manabii kama sauti yake kwa watu wake ili kufundisha,
kuhubiri na kuwakumbusha watu agano la Mungu na jinsi wanavyopaswa kuwajibika
kwa ajili ya Mungu .Ni katika hali kama hii hii Mungu anataka kuwatumia watu
wenye huduma za kitume, kinabii, kiinjilisti, kichungaji na kiualimu kama
mashahidi na sauti ya kutoa mwito kwa watu wa Mungu kuishi kwa ajili ya Mungu
na kuepuka maangamizi
ASILI YA HUDUMA YA KINABII.
-Moja
ya sababu za kuwako kwa huduma ya kinabii ilikuwa ni kuhakikisha agano la mungu
alilolitoa katika mlima wa Sinai linashikwa agano hili liliitwa pia sheria ya
Musa Mosaic Covenant au Sinaitic Covenant
-Jukumu
hili linaonekana kuwa mwanzoni walipewa makuhani yaani kufanya kazi ya
kufundisha ,kuhubiri na kulisimamia agano lakini kadiri siku zilivyokwenda
inaonekana kuwa makuhani walishindwa kulitimiza Jukumu lao kwa uaminifu na
hivyo huduma ya kinabii ililzimika ichukue nafasi ili kusimamia agano na
viwango vya maadili mungu alivyovitaka kidini,kisiasa na kimaadili. Kumbukumbu
18; 9-22.
-Huduma
ya kinabii ilikuwa ni ya muhimu ili kuwalinda na uharibifu ukiwemo ule wa
mataifa yaliyowazunguka, mataifa yaliyoizunguka Israel yalikuwa na uovu na
hivyo huduma hii ilikuwa muhimu ili kuwalinada na wapiga ramli,ili kutofautisha
kazi za Mungu na za wachawi hivyo Manabii walionya wasiotii na kufundisha
,kuhubiri, na kutahadharisha kuhusu kuwepo kwa Manabii wa uongo
-Manabii
pia waliifanya kazi ya Mungu kwa kusimama mahali palipobomoka kati ya Mungu na
wanadamu ili kuwapatanisha
-Manabii
pia waliifanya kazi ya kuwandaa watu kwa ajili ya ujio wa masihi yaani Nabii
mkuu atakayetimiza vema na kwa ukamilifu
shughuli za kinabii huyu ni Yesu Kristo
Mlima wa Sinai eneo ambalo hutumika
kuteremka kutoka mlimani hapa ndipo mahali Mungu alisema na wana wa Israel na
kuwapa amri na sheria zake Kupitia Musa Mtumishi wake Picha na maelezo kwa
hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote
JINSI MANABII WALIVYOPATIKANA;-
-Kabla ya Nabii Samuel kulikuwa na makundi
makuu mawili ya Manabii
Manabii
wanenaji wa kale Old oral Prophets –Hawa ni wale waliohubiri kuonya na
kufundisha au kutia moyo bila jumbe zao kuandikwa hawa ni kama vile Abraham
Mwanzo 20;7, Henoko, Nuhu, Habili, Isaka, Yakobo na Yusufu, wengine ni
Miriam na Debora Manabii wa kike Waamuzi
4;4.
Manabii
waandishi wa kale – Hawa ni wale wa zamani lakini waliandika Vitabu na kati yao
ni Ayubu,Musa na Yoshua
Hao
woote hapo juu upatikanaji wao ulimuhusu Mungu moja kwa moja.
-Wakati wa Nabii Samuel
Uapatikanaji
wa Mnabii ulikuwa kitu cha wazi kabisa kwani Samuel alianzisha chuo cha wana wa
Mnabii au Manabii wanafunzi. Hawa hawakuwa watoto wa Manabii bali walikuwa
wanafunzi wa vyuo vya kinabii Mfano wa vyuo vya Biblia leo 1Samuel
10;5-13,2Falme 2;1-7 katika wakati huu pia kulikuwa na Manabii wanenaji wasio
wa kale sasa na Manabii waandishi wasio
wa kale.
Mnabii
wanenaji baada ya Samuel Latter oral Prophets ni pamoja na wale waliifanya kazi
wakati wa serikali ya umoja yaani Gadi, Nathan, Sadoki, na heman walioitwa pia
waonaji.aida Ahija alikuwa Nabii wakati wa serikali ya umoja katika wakati wa
Suleimani na sehemu wakati wa utawala wa Yeroboamu huko samaria wengi wa
Manabii wanenaji waliifanya kazi kabla ya Manabii waandishi mpaka wakati wa
Obadia na Yoel mwaka 2852-796 k.k.
Manabii
wanenaji uande wa Isarael ni pamoja na Iddo 2Nyakati 9;29,Shemaya,
Azaria,hanani,Yehu.Eliya na Elisha aida kunauwezekano kuwa wengine waliandika
lakini Vitabu vyao havikupita katika kanuni ya Waebrania
Manabii
wanenaji upande wa Yuda ni pamoja
na Mtu wa Mungu alitajwa hivyo tu katika
2nyakati 25;5-16,mikaya na Zekaria aliyeuawa.
Manabii
waandishi baada ya Samuel walifikia jumla yao 16 yaani kati ya hao wanne
Manabii wakubwa Isaya, Yeremia, Ezekiel na Daniel. 12 ni Manabii wadogo yaani
kuanzia na Hosea mpaka Malaki
SIFA ZA MANABII
§ Waliitwa na Mungu na walikuwa
chini ya upako wa Roho Mtakatifu 2Petro 1;21 Kutoka 4;16,Torati 18;18
§
Waliitwa
Manabii Neno Nabii maana yake ni “Navi” au “Nabi” kwa kiibrania ambalo maana
yake ni Msemaji kwa niaba ya Mungu au mwenye kusema kwa mamlaka ya Mungu
§
Waliitwa
watu wa Mungu “MTU WA MUNGU” hii ni kwa sababu walijitoa kwa Mungu kwa asilimia
mia moja “Total Committed” waliifanya
kazi wakati wa uharibifu na Mmomonyoko mkubwa wa kimaadili walikataliwa na
kuteswa lakini hawakukata tamaa.
§
Walitoa
ujumbe bila hofu au kujali uso wa Mtu
§
Walitabiri
mambo yajayo mengi yakimuhusu Masihi
§
Walikuwa
ni kama walinzi Ezekiel 3;17,33;7
§ Zamani waliitwa waonaji,
walikuwa ni wahubiri wa haki 2Petro 2;5 na pia waliitwa mdomo wa Yehova yaani
wasemaji kwa niaba ya Mungu Kutoka 4;16.
JINSI YA KUPIMA AU KUMTAMBUA
NABII WA KWELI
Ø
Nabii
wa kweli alipozungumza unabii uliotimia au alitakiwa kutumia ili kuthibitisha
kuwa ni Bwana amemtuma Torati 18;21-22
Japokuwa ni muhimu kufahamu kuwa unabii wakati mwingine huweza kuwa wa muda
mrefu au unaweza kubadilika kutokana na mazingira mfano ule wa Yona watu walipotubui Mungu
alihairisha hukumu au inaweza kukawia
kwa hukumu 1Falme 21;29
Ø
Unabiii
wa kweli nilazima ukubaliane na Maandiko Matakatifu yaani Biblia Wagalatia
1;6-9 Torati 13;1-5 Marko 7;8
Ø
Lazima
unabii wa kweli umuinue Kristo
Ø
Maisha
ya Nabii yawe na viwango vinavyokubalika kibiblia Mathayo 7;15-20 Ampende Mungu
na sio Fedha Mika 3;5,11
Ø
Atakuwa
ni mtii kwa Viongozi wa kanisa katika Bwana 1Koritho 14;26-33
Ø
Je
unabii wake unakusudia kulijenga kanisa
au kubomoa? 1Koritho 14;26-33
Ø
Atakuwa
ameitwa na Mungu kuifanya kazi hiyo au kuwa na wito maalumu Yeremia 23;21.
Ø
Atakuwa
anasukumwa na Roho Mtakatifu. 2Petro 1;20-21
Ø
Zamani
Manabii walithibitisha kile walichokisema kwa kuhitimisha na Maneno asema Bwana
wa Majeshi n.k. Amosi 3;8 unabii lazima upimwe au kupambanuliwa kwa sababu ya
utendaji wa Roho tatu ya Kimungu,kibinadamu na ya shetani. Hivyo lazima
ujaribiwe.
SURA YA KWANZA: WAKATI WA UTAWALA WA ASHURU YA
ZAMANI MANABII WASIOJULIKANA TAREHE
1UTANGULIZI KUHUSU MANABII WADOGO
Mungu
aliwatuma Manabii hao kwa paned zote mbili Yuda na Israel
Kwa
ujumla walihudumu kati ya Mwaka wa 760 – 625 k.k kwa upande waufalme wa
kaskazini na mwaka wa 760-43 kwa upande wa ufalme wa kusini yaani Yuda
Manabii
waliotumwa kaskazini yaani kwa Israel ni pamoja na Amosi,Hosea ambao walikuwa
ni raia wa ufalme wa kusini lakini walitumwa kufanya unabii huko kaskazini
Manabii
waliotumwa kwa mataifa mengine ni pamoja na Obadia kwa ajili ya Edomu, Yona
kwaajili ya Ninawi na Nahumu pia kwa ajili ya Ninawi
Manabiii
waliotumwa kwa ajili ya Yuda ni pamoja na Yoeli, Mika Zefania na Habakuki
Manabii
wengine waliotumwa baada ya utumwa wa babeli ni pamoja na Haggai,Zekaria na
malaki na hivyo kufanya jumla ya Manabii kuwa kumi na mbili
Ramani
ya Israel Kuonyesha shughuli za Manabii na maeneo ya huduma zao Nyakati za
Biblia na wakati wa Israel na Yuda Picha na maelezo kwa hisani ya maktaba ya
Mchungaji Innocent Kamote
UCHAMBUZI WA MANABII WADOGO;
OBADIA MTUMISHI WA MUNGU NABII WA HAKI
Mwandishi
wa kitabu cha Obadia.
A. MWANDISHI
NI NABII OBADIA MWENYEWE
-
Jina
lake maana yake ni mtumishi wa Mungu sawa na “Abdullah” la kiarabu
-
Ni
maarufu kama nabii wa haki
-
Kitabu
chake hakina nukuu yoyote kuhusu yeye kazi yake
na wito wake
-
Tunajua
kuwa alikuwa ni Nabii aliyetumwa huko Edomu kusini mashariki ya Yordani
-
Kitabu
chake ndio kifupi kuliko vyote katika agano la kale
-
Tareha
ya uandishi inakadiriwa kuwa mwaka wa 586 k.k.
-
Obadia
haelezi ni lini alipata maono na
ingawaje ni kutokana na yale anayoelezea unaweza kuhisi kuwa huenda ni baada ya anguko la
Yerusalem
B. UPEKEE
WA KITABU CHA OBADIA
-
Ni
kitabu cha pekee katika ujumbe wake na urefu wake
-
Ni
kifupi kuliko vyote katika Agano la kale na kinabeba Tangazo na hukumu nzito
kuhusu dhambi
-
Ujumbe
wa Obadia kimsingi uliihusu Edomu wana wa Esau
ingawa aligusia na kurejezwa tena kwa Wayahudi ambako kutatimia kwa
ukamilifu atakapokuwa anarudi Kristo baada ya dhiki ile kuu
C. HISTORIA
YA MATUKIO KATIKA KITABU CHA OBADIA
-
Mwanzo
25;21-34,27;32-33 Hesabu 20;14-21, 2samuel 8;11-14-14, 2Nyakati 20;1-24,21;8-16
-
Ili
kukifahamu kitabu cha Obadia Vizuri msomaji anapaswa kurudi nyuma na kuangalia
maisha ya Mapacha wa Isaka yaani Yakobo na Esau
-
Mashindano
yao yalianza tangu tumboni mwa mama yao na yaliendelea kwa karne nyingi katika
ya vizazi vyao Mwanzo 25;21-34 watoto wote walikuwa na wazazi wacha Mungu na
haki sawa ingawaje Esau alikuwa na shauku kwa mambo ya mwilini zaidi wakati
Yakobo alikuwa na shauku ya mambo ya kiroho licha ya kuwa mwenye dhambi alikuwa
na shauku katika Mungu na ahadi zake Waebrania 12;16 inasema Esau hakuwa mcha
Mungu
-
Mungu
aliona tabia zao hata kabla ya Kuzaliwa Mwanzo 25;23 Tabia tofauti na mitazamo
Tofauti iliwapelekea vijana hao katika muelekeo Tofauti kidini, kiuchumi, na
kimafanikio.
-
Upendeleo
ulionyeshwa na kila mzazi ulichangia katika kuelekea kwenye migogoro wao
-
Baraka
ambazo Isaka baba yao alikusudia kumpa Esau na zikaibiwa na Yakobo zilipelekea
Chuki kubwa ya Esau dhidi ya Nduguye, Esau aliapa kuwa atamuua Yakobo na hii
ilipelekea Yakobo kukimbia mpaka Padan- aram kwa mjomba wake Labani
-
Esau
alitunza kisasi hicho kwa miaka 20 hivi mpaka wakati Yakobo alipokuwa anarudi na Esau alituma kikosi cha
askari 400 kumuua Lakini kwa neema ya Mungu, Mungu aliingilia kati na wakapatana
-
Ingawa
Esau na kizazi chake chote hawakuweza kuushinda uchungu waliokuwa nao dhidi ya
Yakobo na kizazi chake
-
Miaka
300 baadaye kwa ajili ya uchungu na chuki Edomu haikuwaruhusu Israel kupita
katikati yao walipokuwa wakitoka Misri Hesabu 20;14-21.
-
Mwaka 1042
k.k yaani kama miaka 700 hivi baadaye Daudi alizipiga nchi jirani na kupanua
mipaka ya Israel na kuwafanya wana wa Esau yaani Edomu kulipa kodi yaani
kutimiza unabii kuwa Esau angemtumikia Yakobo.
-
Wakati
wa utawala wa Yehoramu Edomu waliasi 2Falme 8;20-22 na miaka 146 ilipita ndipo
Edomu wakiungana na Waamoni na Wamoabu waliivamia Yuda wakati wa utawala wa
Yehoshafati lakini Mungu alimpa Yuda ushindi.
-
Mwaka wa
586 k.k Edomu walifurahia ilipoanguka Yerusalem Zaburi 137;7 Ezekiel 35;15
-
Inaonekana
kuwa baada ya Waedomu kushirikiana na Wakaldayo waliruhusiwa kukaa kusini mwa
Israel baada ya wayahudi kuchukuliwa mateka huko Babeli
-
Walifanikiwa
sana, lakini Makabayo baadae aliwashinda na kuwalazimisha kushika sheria za
kiyahudi na baadaye wayunani na Warumi walipotawala waliliita eneo hilo Idumeya
-
Inasemekana
kwamba Mfalme Herode mkuu anatokea katika jamii hiyo na eneo hilo
-
Baada ya
mwaka wa 70 B.K Waedomu walimezwa na waarabu na wametoweka leo hawako kama
Taifa au kabila.
D. MISTARI
YA MUHIMU
-
Msatari
wa 3-4
-
15
-
17
-
21
E. MIGAWANYO
YA KITABU CHA OBADIA
-
Kuanguka
kwa Edomu Mstari wa 1-16
-
Kuhuishwa
kwa Israel Mstari wa 17-21
F. UCHAMBUZI
Hukumu
ya Mungu dhidi ya Edomu mstari wa 1-14.
-
Unabii
unahusu kuanguka kwa Edomu mstari wa
kwanza unaonyesha kuwa kile Mwandishi aliandika sio mawazo yake lakini Mungu
alikuwa amemfunulia “Tumesikia ujumbe kutoka kwa Bwana” hii inaweza kuhusu Obadia kusikia kutoka kwa Mungu kabla ya
kuandika na huenda Yeremia na Ezekiel pia walipokea ujumbe kama huo.
-
Mjumbe
aliyetumwa inaweza kuwa Malaika au Roho wa Bwana aliyetumwa kuyachochea
mataifa kuinuka dhidi ya Edom
G. HALI YA
EDOMU
-
Walikuwa
na kiburi Mstari wa 2-4 walijiinua kwa sababu walikuwa na eneo lisiloweza
kuvamiwa na mafanikio ya kijeshi na kisiasa waliyokuwa nayo iliwapelekea
Kujiamini na kuacha kumtumaini Mungu Zaburi 127;1 Bwana asipoulinda mji
aulindaye akesha bure.
Mabaki
ya mji wa wa Petra ambao ulikuwa chini ya serikali ya Edomu kama ngome zake
zinavyoonekana leo Picha na maelezo kwa hisani ya Maktaba ya Mchungaji Innocent
Kamote.
-
Ingawa
mji wao ulikuwa jangwani lakini mataifa mengi yaliionea wivu Edomu kwani
walikuwa matajiri wa visima vya maji na
mabonde mazuri
-
Walikuwa
na madini ya chuma na shaba na njia kuu za kibiashara hata kwa njia ya bahari hivyo utajiri wao pia ulichangia kiburi
walichokuwa nacho Mstari wa 5,-6.
-
Edomu
waliifanya biashara na Syria, Ashuru, India, Misri, Arabuni na Afrika
-
Mstari
wa 5-6 unaonekana katika maono ya Obadia
kwamba wangepoteza utajiri wao moja ya mji wao mzuri ungetekwa na huu ni mji wa Petra kiyunani au Sela
kiibrania ambalo jina hilo maana yake ni mwamba,
-
Ilikuwa
ni ngome kabambe isiyoweza kuanguka, tajiri na yenye kuzungukwa na mawe kila
upande Linganisha Edom na ushauri unaotolewa katika 1Timotheo 6;1-19 hasa 17.
-
Kumbuka
maagizo ya Mungu kwa Israel walipokuwa wakitoka Misri katika Kumbukumbu 2;4-5
na 23;7 na kitendo cha Waedom Hesabu 20;14-21 lakini pamoja na hayo chuki yao
iliendelea Zaburi 137;7 na kulingana na
Ezekiel 35;1-11 Kitendo cha Edomu kilitokana na chuki na wivu wa
kale Galatia 6;7wenye uchungu.
-
Kumbuka!
Mungu atayahukumu au huukumu mataifa kulingana na jinsi
yanavyoshughulika na watu wengine na hususani watu wake aliowachagua Edomu
walihukumiwa kutokana na tendo lao la kuwa kinyume na wanaoteseka katika
Mathayo 25;31-46 Yesu alifundisha kuwa tuwasaidie wale wanaoteseka au wenye
uhitaji kama wakimbizi, wathirika, masikini na wenye vita sasa ukilinganisha
Matendo ya Edomu na Mathayo 5;43-45 na 1Yohana 3;15-18 tunajifunza kanuni za
kuwapenda maadui zetu na chuki zinatufanya kuwa wauaji mbele ya macho ya Mungu
kama hatia iliyowapata Edomu.
H. SIKU YA
BWANA MSTARI WA 15-17.
Kwa
ujumla hii inazungumzia swala la siku ya hukumu ya Mungu dhidi ya Maadui zake,
Pia hutumiwa na Manabii kuelezea matukio ya mwisho wa dunia ambayo hujumuisha
·
Kunyakuliwa
kwa kanisa
·
Dhiki
kuu
·
Vita vya
Armageddon
·
Kurudi
kwa Yesu mara ya pili katika utukufu
·
Kuokolewa
kwa Israel
·
Hukumu
ya mataifa
·
Utawala
wa Yesu Kristo wa miaka 1000 duniani
Kwa ajili ya Edomu siku ya Bwana
ilimaanisha siku ya hukumu ya Edomu kwa ajili ya uchungu dhidi ya Ndugu zao
-
Kiburi
kingine cha Edomu ilikuwa ni rafiki zao Mstari wa 7 Waarabu walikuwa ndio
rafiki wa karibu wa Waedomu na walijiunga
nao katika kuishambulia Yuda Zaburi 83;5-6 pia rafiki zao Waamini, Wamoabu, na
wengine waliifanya biashara nao hawa waliwageuka
-
Kiburi
cha kisiasa Mstari wa 8-9 Waliwategemea wenye Hekima, Viongozi wao wa kisiasa
washauri na majeshi wataalamu wa Vita wa mlima Seiri walijulikana sana kwa Hekima na maarifa ya
ulimwengu inasemekana watu Rafiki wa karibu wa Ayubu mwenye Hekima Elifazi
Mtemani alitokea Temani ambazo ni sehemu
za Edomu Linganisha msatari wa 9 na
Ayubu 2;11. Hekima ya kibinadamu inaweza kutumiwa kwa ajili ya Mungu na
kwa utukufu wake kuufanya ulimwengu kuwa mahali pa salama Yakobo 1;5 Ingawaje
maarifa na Hekima pasipo Mungu haiwezi
kusaidia katika kuikwepa hukumu yake.
-
Kiburi
kilichotokana na nguvu za kijeshi mstari wa 9; na kuwa na makomandoo wa
kivita mashujaa watemani vilitilia hofu
mataifa mengine Yeremia 49;16 walijitumainia katika hali hiyo lakini
ilitabiriwa kuwa askari wake wangechinjwa na watu wangeachwa bila ya ulinzi
-
Sababu
kuu za Maangamizi ya Edomu ni Mstari wa 10-14.
Uasi
dhidi ya Ndugu zao
Kusimama
peke yao kujitenga kiburi cha Kujiamini
Kufurahia
maangamizi ya ndugu zao
Kuwadharau
ndugu zao na kuwasengenya siku ya taabu zao
Kufurahia
utajiri na mali za ndugu zao na Kuwashambuilia mateka waliosalia.
YOELI:
NABII WA PENTECOSTE
A. MWANDISHI
WA KITABU CHA YOELI
Ø Mwandishi ni Yoel baadhi ya wasomi wanaamini
alikuwa mwana wa Samuel (Samuel 8;1-2.) lakini Maandiko yanamtaja kama mwana wa
Pethuel yaani uaminifu wa Mungu ingawa hatuna taarifa alizaliwa wapi na
historia yake si kubwa sana ingawa inaonekana ya kuwa alikuwa kuhani Yoel
1;13-14,2;1 na 14-17.
Ø Jina lake maana yake ni Yehova ni Mungu wasomi wengi wanaamini kuwa alikuwa kuhani hii
labda huenda inatokana na kujishughulisha kwake zaidi na maswala ya hekalu na
kushughulikia na majukumu ya kikuhani
1;13-14, 2;1, 14-17.Na mkazo wake katika kitabu chake chote unawafanya
wasomi kuamini hivyo.
Ø Inaonekana pia kuwa alikuwa anaishi Yudea na ni
maarufu sana kama Nabii wa Pentekoste.Kwa sababu ya kuzungumzia swala la ujio
wa Roho Mtakatifu katika Yoel 2; 28.
B.
TAREHE YA UANDISHI.
Ø Tarehe ya uandishi wa kitabu cha Yoel
Haijulikani hasa ni lini Baadhi wanaamini kuwa huenda kiliandikwa wakati wa
baada ya Uhamisho wa Babel kwa sababu Yoel hajawataja waashuru wala wakaldayo
wala maswala ya kuabudu sanamu.
Ø Ingawaje baadhi ya wasomi wanaamini kuwa
uchanganuzi wa wadudu kama tunutu, Madumadu n.k ni Lugha ya mafumbo
inayohusiana na uvamizi wa majeshi ya kigeni hivyo kama hivyo ndivyo Basi
tarehe ya uandishi inaweza kuwa ni kabla ya utumwa na moja ya jambo
linalothibitisha kuwa hakikuandikwa wakati wa utumwa ni kwa sababu kinagusia
maswala ya ukuhani na hekalu hivyo kunauwezekano kikawa kimeandikwa 830 k.k.
kwani hekalu liliharibiwa mwaka wa 586 k.k.
C. HISTORIA YA MATUKIO KATIKA KITABU CHA YOEL
2Falme 11; 1-12;3.
Ø Ukweli kuwa Yoeli anashughulika na makuhani
zaidi na sio wafalme unashuhudia ya kuwa kitabu huenda kiliandikwa wakati wa
Yehoiada kuhani mkuu ambaye ni mtu mkubwa aliyechaguliwa kusimamia maongozi kwa
sababu mfalme alikuwa mtoto hivyo Yoel hajazungumzia maswala ya mfalme katika
kitabu chake.
Ø Malkia wa Yuda Athalia alikuwa amewaongoza watu
katika kuabudu mabaali. Lakini Yehoiada aliwaongoza kurudi kwa Mungu Na huduma
ya Nabii Yoel ilichangia kuwarudisha watu kwa Mungu
Ø Athalia alikuwa mtoto wa mchawi malikia
Yezebeli aliyeolewa na Ahabu na aliolewa na Yehoramu mwana wa Yehoshafati
mfalme wa Yuda. Athalia aliwaongoza Yehoramu na Yuda kuenda mbali na Mungu kuabudu
baali na kufanya dhambi nyingine Yehoramu aliwaua nduguze 6 ili kujihakikishia
anabaki kwenye kiti cha kifalme na alipokufa mwanae Ahazia akawa Mfalme Badala
yake, Athalia alimchochea Ahazia katika kuabudu miungu na baada ya mwaka mmoja
aliuawa na Athalia alitawala na kutoa amri kuuawa kwa watoto woote wa Ahazia
yaani wajukuu wake na warithi wa kiti cha ufalme.
Ø Dada wa Ahazia alikuwa ni mke wa kuhani mkuu
Yehoiada na kwa neema ya Mungu aliweza kumuokoa moja ya wana wadogo
aliyeitwa Yoashi na kwa kuwa alikuwa na
umri mdogo miaka 7 Yehoiada aliongoza
makuhani na wazee wa Yuda kisiasa kufanya mapinduzi na kumfanya Yoashi kuwa
mfalme na Athalia akauawa.
Ø Yehoiada aliendelea kusaidia kuongoza mpaka
Yoashi alipofikia Umri wa kuweza kutawala.
D. UPEKEE
WA KITABU CHA YOEL NA UJUMBE WAKE
a.
Yoeli alisisitiza
kuhusu Siku ya Bwana, majukumu ya makuhani ambao ni muhimili wa dini na
kumwagwa kwa Roho Mtakatifu, Pamoja na mapigo yanayohusiana na nzige ni vitu
maalumu sana katika kitabu hiki.
b.
Kitabu
chote kialenga katika siku ya Bwana, huku Yoeli akitumia mifano ya Nzige
kuwaonya dhidi ya hukumu ya Mungu itakavyokua isipokuwa kama watatubu. Jambo
hili ingawaje linaenda zaidi ya hali halisi ya siku hizo kwani pia inazungumzia
juu ya dhiki ile kuu siku za mwisho ambapo hasira ya Mungu itashuka ulimwenguni.
Nzige (Locust)
Moja ya wadudu waharibifu wakubwa wa mazao kwa mujibu wa Yoel ni miongoni mwa
Majeshi ambayo Mungu angeyatumia kuwashambulia watu wasipotubu uovu wao Picha
na Maelezo kwa Hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote.
E. MSTARI
WA MSINGI AU MISTARI YA MUHIMU
Yoeli
2;1 - Siku ya Bwana inakuja
Yoel
2;13. - Rarueni mioyo yenu
Yoel
2;28 - Nami nitawamwagia watu wangu Roho
yangu
Yoel
3;10 - Yeye aliye dhaifu na aseme mimi
ni Hodari
F. MGAWANYO
WA KITABU
Kitabu cha Yoeli kimegawanyika katika maeneo makuu mawili
a. Nabii
anazungumza 1;2-2;17
b. Mungu
anazungumza 2;18-3;21
G. MCHANGANUO WA KITABU CHA YOELI
·
Hukumu
na toba Yoel 1;1-2;27
Yoeli
anatoa kwanza sababu za ujumbe 1;1, Neno la Bwana lilimjia, mara nyingi kile
ambacho Bwana aliwapa Manabii walitakiwa kuwaambia watu na Mungu alizungumza
wazi kulingana na mazingira yao nini cha kukifanya ili waepuke hukumu zake na kufurahia Baraka
zake zaidi
·
Mapigo
ya Nzige 1;2-0
Mapigo
ya nzige kulikuwa kitu cha kawaida katika mazingira yale lakini nzige hawa anaozungumza
Yoel ni wa Tofauti na hawajawahi kuonekana mstari 2-3 ilikuwa ni kitu ambacho
wazazi wangewasimulia kizazi kijacho cha watoto wao, kule kuonyesha kuwa wazazi
hawatasahahu ni wazi kuwa watu wanapomuacha Mungu kwa hakika hukumu ya Mungu
huwa inakuja juu yao bila mzaha, 2-4, Mstari wanne unaashiria labda vipindi vinne
vya uvamizi wa nzige au hatua zao za kukua
·
Baadhi ya wanatheolojia wanaamini kuwa adhabu ya
aina hii ya nzige inawakilisha falme nne zilizoigandamiza Yuda na Israel kwa
miaka mingi
Ø Tunutu
– wanawakilisha Babeli
Ø Nzige
– wanawakilisha Waajemi na Waamedi
Ø Parare
- wanawakilisha Wayunani
Ø Madumadu
- wanawakilisha Warumi.
Hata
hivyo baadhi ya wanatheolojia wanasema hawa walikuwa ni wadudu halisi na
hawakuwakilisha falme yoyote I; 4 na 2;25-26
H. WITO WA KUTUBU 1;2-2;17
Ø Yoeli
aliwaita watu woote kutubu kuanzia na Viongozi 1;2,3,14, 2;15-16 na wote
walioishi juu ya nchi 1;2,3,14, Watoto wachanga na wanyonyao 2;16, Walevi 1;5 wakulima
na watunzaji wa mizabibu 1;11 makuhani 1;13,14,2;15,2;1,15,17.bwana harusi na
bibi harusi 2;16,8 walitakiwa kuomboleza kama mwanamke aliyefiwa na mume wa
ujana wake, walitakiwa kufunga na kuomba na kuitakasa siku ya bwana hili lilikuwa linadhihirisha nini watu
wanatakiwa kukifanya ili kuepuka hukumu ya Mungu
Ø Yoeli
aliwahakikishia watu kuwa Mungu ni mwingi wa Rehema na huruma na neema na si
mwepesi wa hasira na kuwa hughairi mabaya
Ø Uamsho
lazima uanze na Viongozi wa kidini hivyo
makuhani waliagizwa kuomboleza kati ya patakatifu na madhabahu
I. KUREJESHWA KWA BARAKA ZA MUNGU 2;18-27
Ø Yoeli
2;18-27 Inatoa majibu ya Mungu kwa maombi ya Nabii, makuhani na watu wote, toba
ya kweli inapofanyika Mungu Huiheshimu na kuikubali, hivyo Mungu alihaidi
kuwaondolea Mbali nzige na kuwa angerejesha mazao na mavuno yangepatikana, miti
ya matunda ingezaa na mashamba yangezalisha mavuno mengi
Ø Baadhi
ya wasomi wanatafasiri kuwa Yoel 2;20
jeshi la kaskazini kuwa kama ni Ashuru lakini mstari wa 25 unaweka wazi
kuwa Mungu anamaanisha ni nzige halisi
Ø Ingawaje
namna atakavyo wafukuza nzige hao kungewatia moyo watu wake kumuamini kwa wokovu dhidi ya
majeshi ya wageni
Ø Yoeli
2;21-27 inakazia maswala ya kiroho na Baraka ambazo zingewajilia watu wa Mungu,Baraka
hizo za kimwili na kiroho zingeipata Yuda kama wataamua kumgeukia Mungu na hii
pia iliwakilisha Baraka ambazo zingewapata kwa kumuamini Yesu wakati wa miaka
1000 ya Utawala wake duniani.
J. SIKU ZA MWISHO 2;28-3;21
Ø Kwa
Maneno Hata itakuwa baada ya hayo 2;28 Nabii alimaanisha kuhusu wakati ujao
mbali kutakuwa na utembeleo maalumu na hukumu
A.
Kumwagwa
kwa Roho Mtakatifu 2;28-29
Ø Watu
woote wa Mungu wangejazwa Roho Mtakatifu na kuna makundi sita yanatajwa kama
ambao wangetembelewa na Roho Mtakatifu Wana wenu, binti zenu, vijana, wazee
wanaume na wanawake.
Ø Hiki
alicho kitabiri Yoeli kilitimia kuanzia siku ya Pentecost Matendo 2;17-18 Petro
aliitumia tafasiri ya siku za mwisho na kuendelea kwa kawaida siku za mwisho
zilianza na Kuzaliwa kwa kanisa siku ya
Pentecost na kuendelea katika kipindi chote cha kanisa, Mungu aliwajaza watu wa
chache Roho wake kwa kusudi maalumu lakini sasa anasema kwa watu woote kila mtu
atakuwa na sehemu katika utumishi wa kazi yake Sehemu hii pia ya unabii wa
Yoeli unaeleza nini kitatokea kutokana na kumwagwa huko kwa Roho wa Mungu, watu
watatabiri, wataota ndoto, na kuona maono
Ø Ishara
hizi zoote zinafunua ushahidi wa Agano la kale
Mungu angaeendelea katika namna kama hiyo iliyokuwa wazi wakati wa Agano
la kale kujifunua mwenyewe lakini kwa
upana zaidi katika Agano jipya
B.
Dhiki
kuu 2;30-32.
Ø Ishara
na maajabu yanayotajwa katika mstari wa 30-32 yatatukia mwisho wa kipindi
cha kanisa, Danieli alisema kutakuwa na kipindi cha dhiki ambayo
haijawahi kuweko tangu kuumbwa kwa ulimwengu
lakini katika wakati huo watu wako kila atakayeonekana jina lake
limeandikwa katika kitabu cha uzima wataokolewa Daniel 12;1, Tunaona katika
Ufunuo 6;12-14 kile ambacho Yoel alitabiri lakini kwa undani zaidi
Ø Tetemeko
kuu jua kutiwa Giza na kuwa jeusi mwezi kuwa mwekundu kama damu lakini wale
watakaoliitia jina la Bwana wataokolewa.
C.
Hukumu
ya Mataifa 3;1-16 Isaya 2.
Ø Mwishoni
mwa dhiki ile kuu kutakuwa na hukumu kubwa kwa kuanziwa na vita vya Armageddon
watu wa Mungu watakapokuwa wamepatwa na maangamizo makubwa mwishoni wataliitia
jina la Bwana kwa wokovu 5;15
Ø Maombi
ya Israel wakati huu yatakuwa watelemshe
mashujaa wako ee Bwana Yoel 3;11 na Isaya 64;1
Ø Yesu
atakuja na watakatifu wake na jeshi la malaika
na atamshughulikia mpinga Kristo na Israel watakapomuona watatubu na
kumtambua kama Bwana na mwokozi wao, Kisha hukumu ya mataifa itachukua nafasi
yake na mataifa yoote yatahukumiwa katika msingi wa namna wanavyoshughulika na
Israel na kanisa.
D.
Utawala
wa Yesu Kristo wa Miaka 1000. 3;17-21 Isaya 35
Ø Ujumbe
wa Yoeli unamalizikia na Baraka kubwa iliyohaidiwa kwa watu wa Mungu
o
Bwana atakuwa kimbilio lao na Ngome yao kuu sana
3;16
o
Bwana atakaa katika Sayuni 17,21
o
Yerusalemu watakuwa watakatifu na haitovamiwa tena mstari
wa 17
o
Israel itapata chemuchemu za maji na nchi itakuwa
yenye kuzalisha sana mstari wa 18 na Yuda itadumu milele mstari wa 20. Mungu
atawasamehe Israel Mstari wa 21.
YONA:
MMISHIONARI MZALENDO
A.
UTANGULIZI
Ø Je
umewahi kusikia habari za Mwinjilisti ambaye amekasirika kwa sababu wenye
dhambi aliowahubiri wametubu na kuokolewa? Yona ni miongoni mwao
Ø Yeye
anaitwa Nabii asiyetii au Mmishionari
Mzalendo yeye alikuwa na uchungu dhidi ya watu ambao Mungu alikuwa amemtuma
akawahudumie, alikuwa mbishi muasi na mwenye ubinafsi wa hali ya juu alikosa
upendo na huruma na kama ungekuwa wewe na mimi Tusingelimtuma Yona kuwa Nabii
Ø Jina
lake Yona ni la kiibrania ambalo maana yake ni “Njiwa” Ni mwana wa Amittai ambaye maana yake ni kweli ya Mungu kutoka
Gath-Hepher ambayo ni kana ya wakati wa Agano jipya na ilikuwa karibu na Nazareth mahali
alipokulia Bwana Yesu
Ø Kitabu
kinahusu kufanya umisheni katika nchi ngeni na Mungu anamtumia Nabii asiyependa
kufanya umisheni wa kigeni kukiandika, Kitabu kinatufundisha jinsi Mungu
anavyojihusisha na mataifa mengine pia na kuwa hana upendeleo.
B. MWANDISHI
Ø Wanatheolojia
wengi wanaamini kuwa huenda kitabu kiliandikwa kati ya 780- 753 K.K mapema wakati wa utawala wa Yeroboamu wa pili
Ø Kuna
uwezekano kuwa alianza huduma yake wakati wa Nabii Elisha mwishoni kwani
kulingana na Tamaduni za Israel inasemekana kuwa ndiye mtoto wa mwanamke mjane
wa Sarepter ambaye Eliya alimfufua kutoka kwa wafu tarahe kamili inakisiwa ya
uandishi kuwa 780 K.K.
Ø Yesu
alinukuu Matukio ya Yona katika Mathayo 12; 39-41 Jambo linalothibitisha kuwa
kitabu chake kimevuviwa na sio hadithi tu kama watu wengine wanavyofikiri Yona
pia anatajwa katika 2Falme 14;23-25 kama mtu anayetambuliwa kuwa alikuwa Nabii
katika ufalme wa kaskazini wakati wa Yeroboamu wa pili mwaka 792-753 K.K.
C. HISTORIA YA WAASHURU WALENGWA.
Ø Watu
wa Ashuru walijulikana sana kwa ukatili wao baadhi ya watu waliochukuliwa
mateka na wafalme wa kiashuru waliwekwa katika visanduku vidogo vya chuma na
misumari na kupelekwa nje ya mji wa
Ninawi mji wao mkuu
Ø Visanduku
hivyo vilikuwa vidogo kiasi ambacho mtu hakuweza kukaa wala kusimamia waashuru
waliwaua wafungwa wengi kwa kuwakata miguu kila siku mguu moja na siku nyingine
mguu mmoja ili kuwafanya wasikie maumivu makali
Ø Wengine
walilazimishwa kuwachinja rafiki zao waliowafahamu zamani watu wengi waliona ni
afadhali kujiua kuliko kuwa kwenye mikono ya waninawi Nahumu 3;19
Ø Wanawake
waja wazito waliwapasua tumboni ili kuona ni jinsi gani kitoto kinakaa ndani ya
tumbo la mama zao.
Ø Inawezekana
hii ndio ilikuwa sababu iliyomfanya Yona kuchagua kufa kuliko kuwahubuiri watu
hawa katili aliokuwa amesikia habari zao na huenda pia Yona alifahamu kuwa
wangetumiwa na Mungu kuwaadhibu wa Israel. kwani mnamo mwaka wa 722 K.K. yaani
miaka 38 baada ya mahubiri ya Yona Waashuru waliivamia Israel na kuwachukua
mateka huko Ashuru
D. UPEKEE WA KITABU CHA YONA
Ø Kitabu
cha Yona ni Tofauti na Vitabu vingine vya kinabii kwa sababu ya maswala ya
msingi yafuatayo;-
1. Kimeandikwa
katika mtindo wa kihistoria kuliko Vitabu vingine vya kinabii ingawa kina kweli
nyingi ambazo zinaweza kuwa ni changamoto kubwa na kweli kuu ambazo zaweza
kufanya kazi katika maisha yetu leo.
2. Matendo
ya Mungu kwa asili katika kitabu hiki kina kweli kuu kuhusu Mungu kwa asili hii
inafundisha wazi kabisa kuwa Mungu yuko kila mahali na ni vigumu kukimbia au
kujificha mbali na uso wake Zaburi 139;7-12, kinafundisha pia kuwa Mungu ni
Bwana wa Historia, mataifa na Viumbe vyote na kuwa anahukumu kila jamii
inapokosea na anaweza kutumia asili kwa mfano alimtumia upepo, samaki mkubwa
mmea wa mtango, mnyoo Jua n.k. katika kukamilisha mpango wake kwa Yona kwenda
ninawi.
3. Kitabu
hiki kipekee sana kinasisistiza Umisheni
na kufunua Upendo wa Mungu na mpango wa Mungu wa wokovu sio kwa wayahudi
pekee bali kwa watu wote wa mataifa Yoote Matendo 10;34-35
4. Unabii
unaotegemea Conditional natural Prophecy Yona alitangaza kuwa Ninawi
utaharibiwa katika siku arobaini lakini haukuharibiwa mji kwa sababu watu
walitubu Yeremia 18;7-10
E. MGAWANYO
Ø Yona
kimegawanyika katika maeneo makuu mawili
1. Wito
wa kwanza na upinzani wa Nabii sura ya 1-2
2. Wito
wa mara ya pili na Manung’uniko ya Nabii 3-4
F. MSTARI MKUU AU MISTARI YA MSINGI
Ø 2;9
Wokovu unatoka kwa Bwana
Ø 3;9
Nani ajuaye ya kuwa Mungu ataghairi na kusamehe
Ø 4;2
Najua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma si mwepesi wa hasira u
mwingi wa rehema nawe wagahiri mabaya.
G. MCHANGANUO
WA KITABU CHA YONA
Kukimbia wito wa Mungu sura ya 1-2.
Ø Yona
hakuwa na mshaka kuhusu nini Mungu alikuwa anataka kukifanyaalipokea ujumbe kwa
Mungu kabla na hivyo alifahamu sauti ya Mungu lakni kile ambacho mungu alikuwa
amemtuma kilikuwa kimemshagaza kumbuka wakati Mungu alipomwambia Petro aende
kwa Kornelio Matendo 10;1-29
Ø Ninawi
ulikuwa mji wa kipagani na mji mkuu wa Ashuru Utawala ambao ulikuwa ni adui
mkubwa wa Israel kwa miaka Mungu alisema
uovu wao umepanda juu mbele zangu Mwanzo 18;25 Kwa hivyo yona aliitwa kwenda
kuhubiri dhidi ya Ninawi lakini yona hakutaka kulitimiza Jukumu hilo hivyo
alikimbia kwenda mbali ingawa alijua wazi kuwa Mungu yuko mahali kote
Ø Kumbuka
Ninawi ilikuwa karibu kuluiko alikokuwa anakimbilia yaani Trshishi ambayo
inaaminika kuwa ni sehemu za Hispania ya leo Mbali sana kutoka Yaffa
Ø Kilichofuata
ni adhabu kwa ajili ya kutokutii kwa Yona lakini kwa upande mwinginie ni Rehema
za Mungu ni upendo wake kumrejeza Yona katika hali ya utii Waebrania 2;10-11.Mungu
alituma upepo mkali na mabaharia walifikiri kuwa meli ingevunjika.
Ø Katika
hali hizo zote za dhuruba Yona alikuwa amelala usingizi na hakuwa anajua nini
kinaendelea 1;6 matoleo mengine ya Biblia kama Septuagint inasema alikuwa
anakoroma
Ø Yona
alipoamsahwa alitoa ushuhuda wa ajabu kuwa anamwabudu “Mungu wa mbingu aliyeumba
bahari na nchi kavu …. Na ya kuwa ninakimbia mbele zake” jambo la kushangaza ni
kuwa zaidi ya kuasi kwake Yona alikuwa anashuhudia kuhusu Mungu wa kweli na
kabla ya kutupwa watu hao waliomba sasa si kwa miungu yao bali kwa Mungu wa
Yona 1;14 walitoa sadaka na kuweka nadhiri kwa Mungu huyo huenda waliahidi
kumtumikia Ushuhuda wa Yona ulileta matokeo na watu walitubu ingawaje yeye
alikuwa akielezea kukimbia kwake
Ø Yona
aliyatoa maisha yake kwa hiyari yake mwenyewe ili wale walikuwa kwenye meli
waweze kuokolewa 1;12
Ø Huenda
Yona alijua wazi kuwa kama Ninawi watatubu Mungu atawasamehe na kuwaokoa lakini
la kushangaza Yona mwenyewe hakuwa tayari kutubu na badala yake alikuwa tayari
kufa kuliko kwenda Ninawi hii inaonyesha jinsi ambavyo kuna hatari katika kuasi
mapenzi ya Mungu na na jinsi chuki dhidi ya wengine inavyoweza kutenda kazi
ndani ya mtu.
H.
KUHIFADHIWA
NA KUOKOLEWA.
Ø Mungu
hakuwa amemsahau mtumishi wake na bado alikuwa na mpango naye na huduma yake
kwa ajili ya watu wa Ninawi aliandaa samaki mkubwa Nyangumi na kummeza Yona
baadhi ya matoleo ya Biblia yanasema Mungu akaandaa au akachagua samaki mkubwa
hii inaonyesha uweza wa Mungu dhidi ya mambo ya asili kuwa Mungu aweza
kuyatumia mazingira au Viumbe katika kutimiza mpango wake,wengine wana fikiri
kuwa labda swala la kumezwa na nyangumi ni hadithi lakini kumbuka kuwa ni
mpango wa Mungu, Mungu aliandaa samaki mkubwa hii imerudiwa mara nne katika
kitabu cha Yona
Ø MAOMBI
KWA AJILI YA WOKOVU.
Yona
alifanya maombi na kujiuhukumu mwenyewe ndani ya samaki, lakini Mungu kwa
huruma yake na Neema wakati mwingine anaruhusu sisi kupitia hukumu zake ili
kwamba tumlilie yeye na kumtegemea yeye na kwa wakati huu sasa Yona alikuwa tayari
kwenda Ninawi na kumtii Bwana
alithibitisha kujitoa kwake kwa Mungu na
Furaha ikaujaza moyo wake.
I.
KUTII
WITO WA MUNGU MARA YA PILI.
-
Hakuna ajuaye ya kuwa Samaki alimpeleka wapi Yona
huenda alimtapika huko Ninawi hata hivyo hili si la muhimu hapa la muhimu ni
kuwa Yona alikubali wito wakati, Mungu alipomtuma mara ya pili.
-
Watu wengine hukataa wito wa Mungu na hawapati
nafasi ya pili ya kumtumikia Mungu wengine hufikiri ya kuwa huenda Mungu hata
watumia tena,Yona alitii neno la Bwana lilipomjia mara ya pili na alikwenda
Ninawi
-
Inakisiwa watu wapatao 600,000. Waliishi Ninawi na
vitongoji vyake ilimgharimu siku tatu Yona kuihubiri Ninawi ingawa alipewa siku
39. Ujumbe wake ulikuwa katika siku tatu ninawi utaangamia, kwa mujibu wa Luka
11;30 tunajua kuwa huenda Yona alimtumia
uzoefu wake wa kumkimbia Mungu na kuokolewa na hii ilikuwa ishara kwa watu wa
ninawi kutubu mji mzima na kumrudia Mungu
J. KUMFAHAMU MUNGU NA MTAZAMO WAKE SURA YA NNE
-
Mwinjilisti anakasirika kwa sababu wenye dhambi
wametubu hiki nacho ni kioja ni wazi
kuwa alijua kuwa Mungu ni mwingi wa Rehema na ya kuwa atawasamehe waninawi na
ndio maana alikimbia wala hakutaka waninawi waokolewe
-
Wakati waninawi wanatubu kwa kufunga, Yona alikuwa
anajijengea kibanda cha mapumziko kwa ajili yake nje ya mji akisubiri kwa
tumaini kuwa Mungu atawaangamiza na siku arobaini zikapita patupu!
-
Yona alikasirika alikuwa na tatizo Kiburi,Ubinafsi
na kukosa upendo alijihusisha sana na heshima yake kama Nabii ametabiri na Mungu
ataitimiza unabii wake alikuwa tayari kufa kuliko kurudi Israel na kusimulia kuwa
mahubiri yake yamewafanya Waninawi watubu na kuokolewa
-
Mungu ana namna yake anavyoweza kuyaangalia mambo
na kutuonyesha makosa yetu na kutufundisha mtazamo wake aliandaa mtango kumpa
Yona kivuli na Nabii wake mwenye hasira
akapumzika kisha akaandaa mnyoo upepo na jua kali vikaharibu kile kivuli Yona
akakasirika zaidi
-
Kumbuka kuwa mungu alimuuliza yona unaona vema
kukasirika hatupaswi kulaumu kile mungu anachokifanya Yona alijibu kuwa
anafanya vema kukasirika hata kufa Hasira husumbua watu wengi na husababisha
kifo au kupooza Srtokes
-
Mungu alikuwa akimfundisha Yona na sisi kuwa Yeye
ni mwingi wa Rehema Yona alifurahia
faraja zake na starehe zake kuliko
maisha ya watu 120,000 watoto wachanga na wanyonyao Mungu aliwajali wao kwani
anaupenda ulimwengu mzima Yohana 3;16.
SURA YA PILI: WAKATI WA UTAWALA WA ASHURU NA
MANABII WA KARIBU NA ISAYA
AMOSI:
NABII WA UTAKATIFU
A.
UTANGULIZI
-
Amosi alikuwa miongoni mwa wanamapinduzi wakubwa
katika Isarael huduma yake ilifanyika kipindi ambacho Israel walikuwa
wameharibika vibaya na walikuwa katika
wakati wa mafanikio na starehe ambazo ziliwafanya Israel kuishi maisha ya dhambi
-
Jina lake maana yake ni “Mbeba mzigo” alikuwa na mzigo wa kutimiza agizo Mungu alilokuwa
amempa kulitangaza neno la bwana wakati wa ukengeufu mkubwa wa Israel alizaliwa
katika kijiji kiitwacho Tekoa miles 12 hivi kutoka Yerusalem
-
Alikuwa Mchungaji wa Kondoo na mtunzaji wa miti ya
mikuyu hakuwa Nabii aliyesomea 7;14
lakini alikuwa mnenaji Hodari “Great orator”Asili ndiyo ilikuwa shule yake na
anga ubao wake 5;8 Neno lake linaonyesha historia yeke 3;8
-
Amosi alikuwa mtu wa Yuda ingawa alitumwa kwa
Ufalme wa Israel
Pichani Juu wachungaji wakichunga kondoo katika
uwanda wa mashamba ya ngano huko Tekoa mahali alikotokea Nabii Amosi Tekoa iko
mail 12 hivi kutoka Yerusalemu katika tawala za Yuda Picha kwa hisani ya
maktaba ya Mchungaji Innocent Samuel Kamote
B. TAREHE YA UIANDISHI.
-
Kitabu kiliandikwa mwaka wa 755 K.K. wakati wa
utawala wa Yeroboamu II mfalme wa Isarael na Uzziah Mfalme wa Yuda
C.
WASIFU
WAKE.
-
Amosi alikuwa Mnyenyekevu na wala hakijaribu
kuficha maisha yake ya huko nyuma 7;14
-
Alikuwa na Hekima katika kupeleka kwake ujumbe alimtumia
misamiati amabayo ilikuwa wazi na ya kivitendo
-
Alikuwa mtu Imara thabiti alikataa kugeuzwa na
Amazia kuhani mwakilishi wa Yeroboamu huko Betheli 7; 10-17.
D.
HISTORIA
YA WALENGWA.
-
Wakati huu Israel walikuwa wanaishi maisha ya anasa
na mafanikio makubwa sana hata hivyo baadhi ya matajiri waliupata kutokana na
dhuluma
Masikini walikandamizwa Amosi 5;7,11
Mahakimu au Waamuzi walikuwa wakipokea Rushwa Amosi
5;12
Wafanya Biashara hawakutumia mizani za halali Amosi
8;5-6
Wenye haki waliuzwa utumwani amosi 2;7
Kulikuwa na uashaerati usio wa kawaida hata Baba na
Mtoto waliweza kutembea na mwanamke mmoja Amosi 2;7.
Waliwakataza Manabii kuhubiri Amosi 2;7.
Watu walioishi maisha ya Stareha na anasa Amosi 6;1
Uasi wa kidini ulitawala Amosi 4;4-5, 5;21-23
-
Utawala ambao ungeiangamiza Israel ingawa
haujaelezwa ni Ashuru.
E.
WAZO
KUU NA MISTARI YA MSINGI.
-
Wazo kuu katika kitabu hiki ni Samaria Inavuna
hukumu,amosi alikuwa ni Nabii wa kwanza
kutamka anguko la Samaria au Israel ambalo lilitimia miaka 40 baadaye ujumbe
wake ulikuwa hukumu ya Mungu kwa sababu ya Kukosekana kwa haki katika jamii
-
Mstari mkuu au wa msingi ni
-
Amosi 3;3 Je wawili waweza kutembea Pamoja
isipokuwa wamepatana?
-
Amosi 4;11-12 “Jiandae kukutana na bwana Mungu
wako”
-
Amosi 6;1 ole wao wanaostareha katika Sayuni
F.
MGAWANYIKO
WA KITABU CHA AMOSI.
-
Hukumu ya mataifa sura ya 1-2
-
Hukumu ya Israel sura ya 3-6
-
Uchanganuzi wa hukumu 7-9;10
-
Ahadi ya kurejeshwa upya 9; 11-15.
G. MCHANGANUO WA KITABU CHA AMOSI
-
Kabla ya
kutangaza hukumu dhidi ya Yuda na Israel
Nabii anachagua mataqifa kama sita hivi
ambayo pia aliyatangazia hukumu ya Mungu
-
Matatu kati ya hayo ni Dameski Syria,Gaza kwa
wafilisti na Tiro ambao hawa hawakuwa na uhusiano wa kindugu na Israel bna yuda
-
Mataifa mengine matatu ambao walikuwa na uhusiano
wa kidugu na Israel na Yuda ni Edomu, Ammoni na Moabu.
-
Kila tamko la hukumu kwa mataifa ya jirani na
Israel na Yuda ilianza na “Haya ndiyo asemayo Bwana kwa makosa matatu naam kwa
makosa manne sitazuia adhabu….”
-
Mtindo huu unamaanisha maovu yaliyopita kiasi na ya
kuwa maovu hayo yaliongezeka mwaka kwa mwaka
-
Amosi ndiye mwanzilishi wa mtindo wa kuliita taifa
kupitia jina la mji mkuu wake mfano anapoizungumzia Yuda anaitaja kama
Yerusalem na Israel kama samaria.
A.
HUKUMU
DHIDI YA DAMESKI SYRIA 1;3-5
-
Dameski
ulikuwa ni mji mkuu wa Syria na hapa Syria inatangqaziwa hukumu kwa sababu ya
kulitendea vibaya Gileadi Gileadi ulikuwa mji wa kale wa kabila ya nusu ya
Manase ambao walibaki ng’ambo ya Yordani watu walipokuja kuitamalaki inchi ya
mkanaani,
-
Dameski waliwachukuwa watumwa au mateka kwa vyombo
vya chuma na kuwaburu za kama mtu avunaye ngano mungu anahaidi kushusha moto na
kuwateketeza
B.
HUKUMU
DHIDI YA GAZA 1;6-8
-
Gaza ulikuwa mji mkuu wa wafilisti kusini magharibi ya Yerusalem,Dhambi yao
ilikuwa ni kusafirisha watumwa waliwachukuwa watu walioishi vijijini hususani waisreal na kuwauza huko edomu kama
watumwa
-
Mungu anaahidi kuwaletea hukumu ya kuwateketeza kwa
Moto na kuuchoma mji na majumba yake
C.
HUKUMU
DHIDI YA TIRO 1;9-10
-
Tiro iko kaskazini mwa pwani ya Israel na mji
uliokuwa kutuo kikuuu cha bahari au bandari Isaya ,Yeremia na Ezekiel
waliitangazia hukumu maalumu ulikuwa mji mkuu sana wa kibiashara na kajhba mkuu wa wakati ule
-
Inaonekana waliwachukuwa watu fualni kabila nzima
huenda Waisrael na kuwatia mikononi mwa Edomu hivyo dhambi yao ilikuwa ni
kufanya biashara ya utumwa na Edomu na walisahau agano la undugu huenda hili
lilikuwa ni agqano walilolifanya Daudi na Hiramu katika 2samuel 5;11
-
Hukumu yao ni moto na kuharibiwa majumba yake na ni
kweli Nebukadneza alijaribu kuuteka tiro lakini si kwa mafanikio sana na
mwishoni uliharibiwa vibaya na Alexander
mkuu.
D.
HUKUMU
DHIDI YA EDOMU 1;11-12
-
Hwa walikuwa ni uzao wa Esau pacha wa Yakobo na
walioishi kusini mwa bahari iliyokufa
sehemu iliyoitwa araba, wao wanahukumiwa kwa Matendo yasiyo ya
kindugu,alimtumia upanga na mateso hawakuwa na huruma na walikuwa na kisasi cha
hasira kwa siku nyingi na wanatangaziwa hukumu nya moto juu ya temmani na
Borsa miongoni mwa miji yao mikubwa na
kuiteketeza.
E.
HUKUMU
DHIDI YA WAAMONI 1;13-14
-
Waamoni na wamoabu ni Watoto,wajukuu wa Lutu
waliozaliwa kutokana na zinaa ya baba na watoto wake wa kike Mwazno 19;30-38
-
Wao wanahukumiwa kwa sabau ya ukatili wao kwa
Gileadi ,waliwapasua wanawake wenye mimba wa Gileadi wanatangaziwa hukumu dhidi
ya mji wao mkuu Raba au Raboth-ammoni
-
Inaaminika kuwa huko ndiko Daudi alikoagiza Yoabu
kuhakikisha Uria anauwa vitani 2Samuel 11.
F.
HUKUMU
DHIDI YA WAMOABU 2;1-3
-
Hawa walikuwa na kosa la kuichoma moto mifupa ya
mfalme wa Edomu hata ikawa chokaa
inaonekana hawakumpata akiwa hai hivyo kwa hasira walilipa kisasi kwa mifupa ya
mfalme Isaya 15;5,16;11 Yeremia 48;36
-
Wamoabu walihukumiwa kwa moto ,na kuuawa kwa
Viongozi ,Waamuzi na watu wakuu
-
Mungu anafuatilia sio tu mataifa wanavyolifanyia
taifa la watu wake bali hata kila taifa linavyolifanyia lingine.
G.
HUKUMU
DHIDI YA YUDA 2;4-5
-
Tofauti na mataifa haya mengine ya kidunia sita
Nabii anaigeukia Yuda ambao ni ufalme wa kusini lakini hawa wanahukumiwa kwa kutokishika
Sheria ya Mungu hivyo wao wanahukumiwa kwa maswala ya kidini yaani walikengeika
na kuiacha Shetia ya Bwana
-
Waliishi kama watu wa dunia nao watahukumiwa kwa moto na majumba yao
kuteketezwa
H.
HUKUMU
DHIDI YA ISRAEL 3;1-6
-
Pamoja na matangazo yoote hayo ya hukumu mungu
alikuwa akiilenga Israel wao ndio wanaoonekana kuwa na dhambi nyingi zaidi
kuliko mataifa mengine mlomlongo wa msururu wa dhambi kwa Israel ni mkuu
sana walionea masuikini,waliwauza watu
wenye haki ,waliabudu sanamu,waliifanya biashara ya utumwa, waliwafanya
wanadhiri kuvunja nadhiri zao na kulitii unajisi jina la bwana
-
Amosi aliorodhesha dhambi nyingi za Israel kuliko
za mataifa mengine huenda ili kuonyesha hatia kubwa waliyokuwa nayo na pia kwa
sababu alikuwa akiihubiri Israel na kuwaonyesha uhakika ya kuwa Mungu
angewahukumu wao.
-
Mungu anaihukumu Israel na kuwatangazia hukumu
hivyo akisisitiza katika matangazo makuu matatu yoote yakianzia na neno
lisikieni 3;1,4;1,5;1 na katika 3;3 anauliza je wawili waweza kutembea Pamoja
isipokuwa wamepatana? Mungu alikuwa anahoji anawezaje kutembea na Israel na
kukubaliana nao huku wanatembea dhambini
-
Amosdi alimtumia hata mifano kama simba na
mawindo,Mtego na tarumbeta ili
kuwaaamsha Israel kutoka katika usingizi wa maovu na starehe
-
Mungu hawezi kutuma hukumu kwanza kabla hajaifunua
siri hiyo kwa watumishi wake Manabii amosi 3;8
-
Israela walikuwa wameingia katika ile dhambi ya
kuabudu miungu 1Falme 12;25-33 na dhambi za starehe 3;15
-
Katika Sura ya 4 amosi aliendelea na ujumbe wake wa
hukumu aliwaita Israel Ng’ombe za bashani Bashani palijulikana sana kwa utajiri wa mifugo na mafuta na wanyama
waliolishwa vizuri sana Kumbukumbu
32;14-15, Wanawake matajiri waliokuwa wabinafsi waliitwa ng’ombe za bashani
walijali maswala yao ya starehe na anasa na waliwatia moyo waume zao
kujitajirisha na kuwaonea masikini 4;4 inaonekana kulikuwa na shughuli nyinfgi
za kiibada na za kidini lakini hakukuwa
na kujitoa kwa kweli kwa Mungu
-
Mungu alihaidi kuwatumia Mapigo makuu matano 4;6-11 yaani njaa ,ukavu dhuruba,nzige,magonjwa
-
4;6 Lugha ya kimafumbi inatumika “Euphenism
language” nimewapa usafi wa meno maana yake njaa. 4;12 wanaambiwa wajitayarishe
kukutana na Mungu.
-
Katika sura ya 5 nabii anaomboleza kwa ajili ya
dhambi ya Israel, wako watu ambao hudhani kuwa kuudhuria kwao ibada ni kwa
muhimu zaidi au kunaweza kuwapa kibali kwa mungu na kusahu wajibu wa kujitoa
kwake
H.
UFAFANUZI
WA HUKUMU AMOSI 7;-9;10
a. Eneo
hili lina ufafanuzi wa hukumu tano ambazo Mungu alimuonyesha Amosi katika maono
i. Nzige- Mungu wakati mwingine hutimia
majanga ya asili katika kuhukumu amosi
aliomba kwa niaba ya taifa likasamehewa pigo hilo 7;1-3
ii. Moto Mungu alikusudia uteketeze na
kuangamiza lakini pia amosi alimuomba
Mungu asamehe na ikawa hivyo
7;4-5
iii. Timazi kilikuwa kipimo cha kuonyesha kuwa
wamepotoka kiasi gani Bwana alimuonyesha amosi na wakati huu ikawa ndio mwisho
wa kusamehewa mungu ana kipimo chake kwa ajili ya maisha yetu
iv. Kikapu cha mavuno ya wakati wa hari 8;1-3
kuonyesha kuwa wanvuna kile walichokipanda
V.
Kuvunjwa kwa madhabahu 9;1-10 huku ni kuharibiwa kwa hekalu lililokuwako huko
Betheli kwa ufalme wa kaskazini
·
Amazia ambaye alikuwa ni kuhani mkuu kwa upane wa
Betheli 7;10-17 alishutumu Amosi na kumshutumu kuwa amafanya uongo fitina juu
ya Israel na hivyo hawawezi kustahimili Maneno yake na Amosi alisisitiza kuwa
wito wake ni kutoka kwa Mungu
I. AHADI YA KUREJEZWA TENA 9;11-15.
- Amosi
anamalizia kitabu chake kwa ahadi ya kurejezwa tena kwa Israel
- Kwamba
watatawanywa hukona huko kati ya mataifa lakini mabaki watarejezwa
- Nchi
itastawi na hawataweza kutawanywa tena 9;11-15
HOSEA:
NABII WA UPENDO
A.
Mwandishi wa kitabu cha Hosea.
-
Alikuwa Nabii kwa Israel katika Dakika za
mwishoni kabla kidogo sana Israel kuanguka katika mikono ya waashuru mwaka 722
K.K
-
Ni Nabii maarufu kama Nabii wa Upendo na
uaminifu jina lake Hosea ni la Kiebrania Hoshea ambalo maana yake ni wokovu au
msaada,jina kama Yoshua na Yesu yanatokea katika mzizi wa jina kama hilo.
-
Ni wazi kuwa Hosea alikuwa Mwiisrael
alizungumza kama ndugu na aliyataja mataifa kama Lebanon,Tabori, Bethel na
Samaria
-
Baadhi ya wasomi wanaamini kuwa alikuwa na
asili ya ukuhani kutokana na kutaja kwake maswala mengi yanayohusiana na
ukuhani
-
Alikuwa na Mambo mengi ya kukatisha tamaa
aliyokutana nayo katika familia yake, Huduma na hali halisi ya Taifa lake.
-
Hosea anazungumza na kuonyesha kwa nguvu
upendo wa Mungu kwa Israel licha ya kuwa na uovu mwingi, Dhuluma, mateso,
udanganyifu, Rushwa, kukosa uvumilivu, ulevi na maisha ya anasa, Mungu
aliwataka warejee kwake.
B.
Tarehe ya uandishi wa kitabu cha Hosea.
Inakisiwa
kuwa kati ya Mwaka wa 750-725 wakati wa utawala wa Uzzia, Jothamu, Ahazi na
Hezekia Mfalme wa Yuda na Yeroboamu ii mfalme wa Israel Inaonekana Nabii
ananukuu Wafalme wa upande wa Yuda kwa sababu kwanza alikuwa anaamini kuwa
walikuwa wafalme wa kweli na warithi halisi wa kiti cha enzi cha Daudi pili
wafalme wengi wa Israel waliomfuta Yeroboamu wa ii walioishi muda mfupi sana na
kuuawa hivyo huenda majina mengi yangeorodheshwa mfano ni orodha hii ifuatayo;-
Utawala wa wafalme wa Israel
2Falme 14-18
Yeroboamu
|
Miaka 41
|
2 Falme 14;23-29
|
Alikufa
|
Zekaria
|
Miezi 6
|
15;8-12
|
Aliuawa
|
Shalumu
|
Mwezi 1
|
15;13-15
|
Aliuawa
|
Manahemu
|
Miaka 10
|
15;16-22
|
Alikufa
|
Pekaiya
|
Miaka 2
|
15;23-26
|
Aliuawa
|
Peka
|
Miaka 20
|
15;27-31
|
Aliuawa
|
Hoshea
|
Miaka 9
|
17;1-41
|
Alifungwa.
|
Mwisho wa utawala wa Israel wakachukuliwa
utumwani Ashuru
-
Watu wa Israel walikuwa wamekataa kurudi kwa Mungu
Pamoja na mahubiri ya Nabii Amosi na matokeo hali ilizidi kuwa mbaya
-
Badala ya kumrudia Mungu watu waliendelea kuwa
waasi huku wakiwaua wafalme wakifanya mapinduzi kwa mapinduzi Mafalme Tiglath –
Pileser wa Ashuru aliishinda mashariki ya kati na kupanua mipaka yake mpaka
Misri na mataifa yoote yaliyotawaliwa
yalitakiwa kulipa kodi kwa waashuru
-
Syria na Israel waliamua kuishambulia Yuda kwa
sababu walikataa kuungana nao katika kuasi kulipa kodi kwa Ashuru
-
Hivyo Mfale Hoshea aligoma kulipa kodi na akaomba
msaada Misri kuungana nae katika kujitoa chini ya utawala wa Waashuru jambo
hili lilisababisha uvamizi wa majeshi ya waashuru huko Israel na kuwahamisha
ambapo Hoshea mfalme aliwekwa kizuizini.
C. DHAMBI
YA ISRAEL ZILIKUWA SURA YA 4-10
Kukosa maarifa ya kumjua Mungu Hosea 4;6,11
Kiburi 5;5
Kutokuridhika 6;4
Udunia na kuwa kama mataifa 7;8
Rushwa 9;9
Kurudi nyuma 11;7
Kuabudu sanamu 13; 2,4;11-12.
D. Upekee wa kitabu cha Hosea na ujumbe wake
-
Hosea ni mojawapo ya kitabu kirefu ukilinganisha na
vingine katika Manabii wadogo na kinakaribiana kidogo na cha Zekaria
-
Ujumbe wake unawezekana ulitolewa kwa muda mrefu
kiasi kwani kitabu kinaonyesha Upendo wa Mungu kwa Taifa lisilo na uaminifu la
Israel na kinatumia maisha ya Mwandishi yaani Nabii Hosea kama mfano hai wa
jinsi Mungu anavyojisikia kuhusu watu wake
-
Hosea anaonya
juu ya hukumu inayokuja ambayo inaweza kuepukika kwa kumrudia Mungu tu
E. Mstari mkuu na mistari ya Msingi.
-
Kiini kikuu cha kitabu hiki ni Pendo la Mungu kwa
Israel na hukumu dhidi ya dhambi
2;
19, 4;1, 4;6, 6;6, 7;8, 8;7.
F. Mgawanyo wa kitabu cha Hosea
-
Zinaa ya Israel ilikuwa ni kukosa uaminifu kwa
Mungu sura ya 1-3
-
Hoja za kinabii kutokumcha Mungu na hukumu ijayo
isiyoepukika 4-13
-
Kuamini kwa Israel na kusamehewa sura ya 14;
G. Mchanganuo wa kitabu cha Hosea
a. Familia
ya Hosea na Israel sura 1-3
i.
Mungu alimuagiza Hosea kuoa mwanamke kahaba hata
hivyo kuna mjadala wa kitheolojia kuhusu ukahaba wa mke wa Hosea kuwa ulikuwa
ni ukahaba wa aina ipi Zinaa au kuabudu miungu ambako nako kuliambatana na
ibada za zinaa? Katika Israel wazinzi walipigwa mawe je ni zinaa ya aina gani?
ii.
Mungu alitaka kuwafundisha Israel kitu kwani walikuwa wazinzi kiroho na Hosea
alikuwa ndio somo lenyewe
iii.
Mungu huihesabu tabia ya kuabudu miungu kama zinaa
ya kiroho na kwa kuwa Hosea alikuwa mwaminifu kwa mkewe Gomeri ambaye Yeye hakuwa
mwaminifu ndivyo na Mungu alivyokuwa mwaminifu kwa Israel.
iv.
Hosea aliwaita wanawe majina yaliyokuwa yakiashiria
unabii.
1. Yezreel
jina hili lilikuwa na maana ya kuwa Mungu “ametawanya au Muangu atapanda” hii
ilikuwa ni kwa ajili ya kuwakumbusha watu wa mji wa Yezreel juu ya mauaji
yaliyofanyika Yehu alipokuwa mfalme,Yehu aliagizwa na Mungu kuwashughulikia
watoto wa Ahabu lakini aliwashughulikia zaidi ya kiwango kwa sababu ya ubinafsi
aliwaua watoto70 wa Ahabu huko Yezreel, Mungu alimwambia Yehu kuwa wanawe
kizazi cha nne watamiliki kiti cha enzi, Yeroboamu wa pili alikuwa ni uzao wa
tatu na Zekaria mwane ndipo unabii ulikuja kutimia 2Falme 10;30,1-8,Zekaria
alitawala miezi sita tu kisha akauawa
2. Lakini
hata Hivyo Yezreel walikuwa na ujumbe mzuri pia
kuwa Mungu hupanda 1;45 yaani pamoja na kuwa wana wa Israel
walichukuliwa mateka utumwani Mungu angewarejeza tena katika inchi yao
3. Lo-Ruhama
1;6-7 mtoto mwingine wa Hosea jina hili maana yake Hakuna rehema
4. Lo-Ammi
maana yake sio watu wangu 1;8-9 majina haya mawili yanatufundisha na
kuwakumbusha wana wa Israel na Gomeri juu ya dhambi zao na jinsi walivyolivunja
agano lao na Mungu
v.
Kwa mujibu wa sheria ya Musa wazinzi walitakiwa
kuuawa kwa mawe lakini Hosea alimpenda mkewe na Mungu aliipenda Israel hivyo
Gomeri na Israel walikuwa wanapewa Muda ili kwamba waweze kubadilika lakini
haikuwezekana na hivyo talaka iliwakumba wote
vi.
Mwishowe Hosea aliamua kumrudia tena mkewe na Mungu
alikusudia kuwarejeza tena Israel matukio haya yana mambo ya kutufundisha sisi
wa kizazi hiki cha leo
vii.
Kwa ufupi sura ya 1-3 Inazungumzia maisha ya
kielelezo ya Nabii Hosea ambaye anamwakilisha Mungu Hosea alimuoa mwanamke kahaba anayefanya
zinaa kwa sababu hatosheki na mume mmoja hatosheki ashiki zake ni Malaya
anafanya zinaa pia kwa ajili ya kupata faida mapato, Huyo ni Gomeri mke wa
Hosea anayeiwakilisha Israel, Baada ya kuwa amezaa watoto watatu alimwachia
Hosea watoto hao na kwenda kuishi na mwanaume mwingine, wanaume wengine
wakamgombea na ikalazimu wamuuze mnadani ndipo Hosea akamnunua kwa upendo akamrudisha nyumbani.
b.
Ujumbe
wa Nabii Sura ya 4-14
i.
Kuanzia sura ya nne hadi ya 14 Nabii analeta mashtaka
ya Mungu kwa wana wa Israel
1. Anaonyesha
jinsi ambavyo hakuna rehema, Hakuna kweli, hakuna kumjua wala kumjali Mungu
katika Israel
2. Kwa
kusudi walijiingiza katika Ibada za sanamu na kuabudu miungu mingine
3. Nabii
anatoa wito wa kutubu lakini Israel wanakataa na kuendelea na dhambi zao
ii.
Kwa kukataa kwao kutubu Nabii analeta ujumbe wa
adhabu kwao anaitabiria Samaria kuanguka na Yuda pia wataadhibiwa
iii.
Mwisho Nabii anatabiri kurejezwa upya kwa Yuda na
Israel kuwa taifa moja na nchi moja na kuwa baadae watamtafuta Bwana Mungu wao
na Daudi mfalme wao bila shaka huu uatakuwa wakati wa utawala wa miaka 1000 ya
Kristo Duniani.
MIKA: NABII WA MASIHI
A.
Mwandishi
-
Mwandishi wa kitabu cha Mika ni Mika mwenyewe
-
Jina lake maana yake ni “Nani aliye kama Mungu” yeye alitokea Moresheth-Gath mji mdogo
kusini magharibi mwa Yerusalem kilomita zipatazo 40 kwa hiyo Tekoa alikoishi
Amosi ni Kilomita 27 hivi kutoka kijiji cha Mika
-
Kuna uwezekano ya kuwa Mika ameitembelea
Yerusalem mara nyingi na huko aliona jinsi dhambi ilivyosababisha vilio kwa
masikini
-
Katika mahubiri yake alikemea dhuluma ya
Yerusalem kwa jamii alikemea sana kama Amosi alivyokemea huko kaskazini
-
Alijulikana kama bingwa wa kuwatetea masikini
au Nabii wa uongozi wa haki yaani Nabii wa Masihi alihubiri kabla na baada ya
anguko la Samaria huduma yake inakisiwa kuchukua muda wa miaka kati ya 735-700 K.K. kabla kidogo ya Israel
kuchukuliwa utumwani na wakati huu Isaya na Hosea walikuwa Manabii sambamba
naye Mika alishughulika sana na watu, Isaya alishughulika na Wafalme.
B.
Historia
ya hali halisi ya Yuda.
-
Yuda ilikuwa na wakati wa amani na starehe
wakati wa utawala wa Yothamu na hivyo watu walijenga ngome na majumba ya
kifahari “Kasri” lakini uovu ulikuwa uimepamba moto
-
Wakati wa utawala wa Ahazia Yuda
walilazimishwa kulipa kodi kwa Waashuru na kwakweli ulikuwa mzigo mzito sana
kwao na hivyo matajiri walichukua mali za masikini
-
Na mpaka wakati wa Hezekia mfalme Yerusalemu
ilikuwa ni kitanda cha moto kisicholalika kwa ajili ya uovu, rushwa utapeli na
ufisadi- dhuluma
C.
Upekee
wa ujumbe na Kitabu cha Mika.
-
Mika alikuwa Nabii wa kwanza kitabiri kuhusu anguko
la Yerusalemu na kuchukuliwa utumwani BABELI watu watakuwa walishangazwa kwani
Babeli wakati huo ilikuwa bado hata haijajulikana wala kuwadola yenye nguvu Mika
4; 10.
-
Manabii wengi walitabiri pia kuja kwa Masihi
akiwemo Isaya lakini Mika alitabiri mpaka mahali atakapozaliwa kuwa ni
Bethelehemu Mika 5;5 Mathayo 2;6
-
Mwanzoni Mika alikazia kuhusu utakatifu wa Mungu
dhidi ya hali ya uovu wa watu wake, kwani utakatifu wa Mungu unataka utakatifu
kwa watu wake, Mika alisisitiza juu ya kumcha Mungu na mahusiano yaliyo mazuri
Mika anahitimisha kitabu chake kwa kuonyesha tabia ya Mungu katika Mika 6;8 na
kitabu chote kwa ujumla tunaona juu ya tumaini la ujio wa Masihi
-
Na ingawaje atazaliwa Bethelehemu alikuwako
tangu milele Mika 5;2 Mika anamwelezea Masihi na kuwa atatawala watu wake
Israel kama Mchungaji na kuwalisha na
hii itatimia atakapokuja mara ya pili duniani.
D.
Mstari
wa Msingi
-
Mika 5;2 “Lakini wewe Eeh Bethelehemu Efrata
uliye mdogo miongoni mwa Yuda….”
-
Mika 6;8 “Amekuonyesha yaliyo mema…”
E. Mgawanyo wa kitabu cha Mika
-
Hukumu na haki Sura 1-3
-
Mtawala na mabaki Sura ya 4-5
-
Matakwa na kurejezwa upya Sura 6-7
F. Uchanganuzi wa kitabu cha Mika.
a.
Hukumu
na haki Sura ya 1-3.
-
Soma kwa kulinganisha Mika 1;1, Amosi 1;1 na Obadia
1;1. Manabii hawa woote walipokea ujumbe wao kupitia maono waliyopewa na Mungu
-
Mika hakuwa na mafundisho yoyote kuhusu nini cha
kusema, maono ya maangamizi yalimjia na akajazwa Roho Mtakatifu na kupewa
Maneno ya kusema Mika 1;1,3;8.
-
Alisisitiza
Umuhimu wa ujumbe wake kwa kuuelekeza kwa watu wote 1;2 alimuona Bwana
anashuka kwa hukumu akitembelea mahali pa juu
na milima ikiyeyuka chini ya miguu yake na bonde likagawanyika
-
Kumbuka kuwa Biblia inazungumza kwa mafumbo na
wakati mwingine waziwazi mahali pa juu huweza kumaanisha Kiburi au milimani
ambako ibada za sanamu zilikuwa zikifanyika 1; 6, 3; 12.
-
Unaposoma Mika 1;3-4 na kulinganisha na 2Petro
3;10-15 na Ufunuo 21;1-5 utagundua kuwa hizi ni nabii mbili kwa Mfululizo yaani
i.
Kuanguka kwa Samaria na Yerusalemu na
ii.
Kufanywa upya kwa ulimwengu kwa moto
-
Woote Mika na Petro walisisitiza utakatifu katika
mtazamo wa kuja kwa Bwana, na kuyeyuka kwa milima kwa uhalisi kunaweza kuwa
wakati wa ujio wa pili.
-
Mika alifanya huduma miaka 13 kabla ya Ashuru
kuivamia Samaria na aliishi akaona sehemu ya unabii wake ikitimia. Mika
alionyeshwa namna samaria itakavyo haribiwa
na Ashuru 1;6-7
Bethelehemu mahali ambapo wachungaji waliwasikia
malaika akiwapa ujumbe wa Kuzaliwa kwa masihi na kisha kundi la malaika
wakaimba Ndivyo panavyoonekana leo ni katika mji huu Yesu Masihi alizaliwa Kama
alivyotabiri Mika 5;2 miaka 730 K.K, Picha na maelezo kwa Hisani ya maktaba ya
Rev.Innocent Kamote
-
Mika alimtumia baadhi ya Maneno kwa baadhi ya miji ambayo
ingetekwa na kufanyiwa uharibifu alimtumia mtindo wa Maneno kama au kinyume cha
jina halisi la mji kuonyesha kile ambacho kingewapata Mika 1;10-14.
-
Beth- le –afra
nyumba ya vumbi
-
Beth eseli - kuondolea tegemeo
-
Moroth -kuondoa Tegemeo
-
Lakishi - mikanda inayofungwa kwa farasi
-
Moresheth – gath zawadi ya kuagia
-
Akzibu- kijito kidanganyacho wafalme
-
Maresha -
kumilikiwa
-
Zaanani -hutotembea
G.
Hukumu
kwa Viongozi pamoja na watu 2-3.
-
Mungu aliamini kuwa Viongozi watasimamia ugawanyaji
wa ardhi kwa familia na kuwa urithi wao
wa kudumu lakini kwa sababu ya umasikini familia nyingi zililazimika kuuza mali
zao ardhi na ilitakiwa mwaka wa jubilee ambao uliazimishwa kila baada ya miaka
50 ardhi zirudishwe lakini watu wenye tamaa walipanga namna ya kuzidi kuwa matajiri
kwa kuendelea kumiliki mali za wengine 2;1-2.Mungu anaitikia mipango yao kwa
mpango wake 3-4,Pia tunaona sheria ya kuvuna na kupenda ikifanya kazi soma
2;1;3; 2;2,4;2;2,4-5, 2;8,10, 2;9-10.
-
Hata hivyo bado Mungu alikuwa na mpango na watu
wake yaani wokovu kwa wale watakaomfuata 2;12-13 Mungu angewasaidia mabaki ya
watu wake huko utumwani na angewarudisha katika nchi yao na ya kuwa Masihi
atahusika katika kuwaweka huru watu kutoka katika utumwa wa dhambi Mika 2;13
-
Manabii wa uongo walijaribu kumpinga Mika na ujumbe wake wakimuonya kuwa asihubiri mambo hayo 2;6, Linganisha
na Amosi 7;10-17 Jaribu kubwa walilokuwa nao Manabii hao katika siku zao
ilikuwa ni kuhubiri kile watu wanachokitaka watu ili walipwe na kulishwa 3,5,11
kama watajisahau katika hali hii wataanguka katika giza kubwa la kiroho alisema Mika 3;6-7
-
Katika sura ya tatu hukumu ya Viongozi inaonyesha pia tunatakiwa kuwa Viongozi wa
aina gani Viongozi katika Israel
walipenda uovu, walijitumikia wenyewe ubinafsi,
na hawakuwa na huruma juu ya watu wengine 3;3. Lakini Mika alikuwa amejazwa nguvu na
Roho Mtakatifu 3;8 Matendo 1;8
H. Unabii kuhusu Utukufu sura ya 4-7
Utawala wa Masihi 4-5
-
Tunamshukuru Mungu kwa kuwepo kwa ufalme wake
katika maisha ya mioyo ya watu wake lakini tunatazamia ya kuwa siku moja Kristo
atatawala katika ulimwengu huu pale Yerusalemu
-
Mataifa hayatapigana tena na wala hawatajifunza
vita tena 4;3
-
Mika 4-5 pia inatuambia baadhi ya matukio
yatakayokuwako ambayo yatatukia kabla ya utawala wenye utukufu wa masihi.
-
Katika 4;9-10 Mika anatabiri kuchukuliwa
mateka utumwani Babeli na kurejezwa tena
-
Mika 5;1 si ajabu ni unabii unaojirudia kwa ufalme wa Yuda na kwa ajili ya Masihi kwa
kupigwa Mathayo 26;67,27;30 wakati mstari wa 2 unaonyesha masihi atazaliwa wapi
na ya kuwa ni mtawala wa kimungu na mwenye kudumu milele.
I.
Furaha
baada ya mateso Mika 6-7.
-
Sura mbili za mwisho zinaonyesha Israel wakiwa
katika kipimo cha Mungu, Mungu aliwaita na kuwahoji kwanini wamemuacha wakati
amewaonyesha upendo na wema kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.
-
Israel walifikiri kuwa wanaweza kumpendeza Mungu
kwa sadaka zao 6;6-7
-
Mika 6;8 inaeleza kile ambacho Mungu anakitaka kwa
mwanadamu yaani Haki, Upendo, Rehema na kutembea kwa Unyenyekevu na Mungu kwa maana nyingine kulitii neno lake Yakobo
1;22
-
Mungu aliwashitaki Israel kwa ajili ya dhambi ya
uongo, uasi, ibada za sanamu, rushwa, uhaini, 6;10-12;16 17;2-6 na hukumu yake
ni anguko 6;16
-
Mika 7;18-20 inatoa suluhisho kwa Israel na ni
Pendo la Mungu katika kuwasamehe dhambi zao
SURA YA TATU: WAKATI WA UTAWALA WA BABELI
MANABII WA KARIBU NA YEREMIA
8
ZEPHANIAH: NABII WA HUKUMU YA ULIMWENGU
A.
Mwandishi
wa kitabu cha Zefania na Tarehe ya uandishi
§ Jina
zefania maana yake ni “Yehova amemficha”
§ Zefania
huenda alizaliwa wakati wa Mfalme Manase na inawezekana ni wakati ambapo mfale
huyo aliijaza Yerusalemu kwa Damu ya watu wasio na Hatia kwani aliwauwa watu
wengi wa Mungu 2Falme 21;16
§ Inawezekana
kuwa wazazi wake walimwamini Mungu juu ya ulinzi wa mtoto wao na hivyo kumpa
jina Zefania yaani Mungu amemficha
§ Alikuwa
ni moja ya vijukuu vya Hezekia kwa ule ukweli kwamba anatoka katika familia ya
kifalme na ndugu wa mfalme Yosia hii iliweza kusaidia kufanya ujumbe wake
kusikiwa vema siku zote Mungu pia huitumia historia ya mtu kwa utukufu wake ili
kuwafikia ndugu na jamaa
§ Inaaminika
kwamba Nyumbani kwao ni Yerusalem kwa sababu alifahamu hali halisi ya pale 1;4
Yeye ni maarufu sana kama Muhubiri wa utakatifu au Mwinjilisti anayewakwa
§ Tarehe
ya uandishi wa kitabu chake huenda ni
kati ya Mwaka wa 630-625 K.K
B.
Historia
ya Nyuma ya mambo 2Falme 21-23,2Nyakati 30-35.
§ Bwana
alimtumia Isaya Mika na Hezekia kujaribu kuigeuza Yuda kwa Mungu na hivyo
Israel walipokwenda utumwani Yuda ilihifadhiwa
§ Hezekia
alifanya kila jitihada kuangamiza ibada za sanamu lakini Mwanae Manase alirejeza
kila kitu ambacho baba yake alikiangamiza ,Alijenga tena madhabahu mahali pa
juu na madhabahu za miungu ya kipagani miungu kama Kemoshi, miliconi, Baali na
Ashera
§ Alimpa
hata mtoto wake jina Ammoni kwa ajili ya miungu ya Misri, Mungu alimtia nidhamu
kwa kumuachia achukuliwe utumwani na kufungwa huko Ashuru 2Nyakati 33;1-12 na baadaye Mungu
akamrudisha tena katika ufalme na alijaribu kufanya masahihisho kwa uovu
alioufanya ingawaje ibada za sanamu alizozianzisha ziliendelea na kukua wakati
wa utawala wa mwanae aliyemrithi ambaye alivitiamoyo kuendelea
§ Yosia
mwana wa Ammoni alikuwa mfale mwema na Zefania alihudumu wakati wa utawala
wake na huenda alimsaidia kufanya
mabadiliko huu ulikuwa ni wakati ambapo waashuru wanaanza kuanguka kama taifa
kubwa na Babeli ilikuwa inaanza kupata nguvu kumbuka kuwa Mika alikuwa Nabii wa
kwanza kitabiri kuhusu kuinuka kwa Babeli
C.
Upekee
wa kitabu na ujumbe.
§ Zefania
alianza kitabu chake kwa ujumbe wa kutosha kuhusu siku ya bwana na wakati wa
hukumu ya mataifa yote Sehemu ya ujumbe wake ilianza kutimia kuhusu Yuda kuaharibiwa lakini
hukumu ilihairishwa mpaka wakati wa Yosia alipofariki kwa kuwa alikuwa mwema na
alikuwa na watu waliomgeukia Mungu
§ Zaidi
ya hayo unabii utatimizwa wakati wa Dhiki kuu na mwisho ni hukumu ya dunia
kuhukumiwa kwa moto
§ Zefania
kutabiri kwake kuhusu hukumu ya ulimwengu ilikuwa ni dalili wazi za kuonyesha
Mungu ni Bwana wa mataifa yote na kuwa yeye ndiye atawalaye Dunia
D.
Mistari
ya Msingi ni
-
1;7 1;14, 2;3.
E.
Siku
ya hukumu na Maangamizi 1;1-3;8
1.
Hukumu ya ulimwengu woote 1;1-3,14-18
-
Kiini cha kitabu ni 1;2-3, Na neno siku ya
bwana ni wakati wa hukumu
-
Ulimwengu mzima na kila kiumbe kimeathiriwa
na dhambi 1;3
-
Kwa ajili ya Yuda Mungu atalitumia jeshi la Babeli 1;14-18 na siku ya Bwana kwao
ilikuwa karibu 1;14 Lakini Paulo anaizungumzia wakati ujao 1Thesalonie 5;2-3
-
Kumbuka matukio ya siku ya Bwana kama yanavyo
changauliwa katika kuwa itakuwa ni siku ya;-
a.
Uchungu na kilio 1;14
b.
Kulia kwa mashujaa 1;14
c.
Hasira 1;15
d.
Mgandamizo na kutisha 1;15
e.
Taabu na ukiwa 1;15
f.
Giza na utusitusi 1;15
g.
Mawingu na weusi 1;15
h.
Tarumbeta na kilio cha vita 1;16
i.
Damu kumwagika 1;17
j.
Moto na wivu wake 1;18
k.
Mwanadamu na mnyama kufutiliwa mbali 1;2-3
l.
Dunia nzima kuyeyuka 1;18
m.
Mwisho wa kustukiza kwa ulimwengu 1;18
Kumbuka
dalili tatu za mwisho katika k,l,m zitatimia katika mwisho ule uliozungumzwa na
Paulo
F.
Hukumu
dhidi ya Yuda 1;4-2;3
-
Mashitaka makuu ya Yuda katika kitabu cha
Zefania ni kuhusu kuabudu miungu ya uongo
-
Mwanadamu ameumbwa na Mungu kwa kusudi la
kuabudu lakini shetani hujaribu kumuharibu mwanadamu kutoka katika kusudi hilo
na kuwageuza kuabudu vitu vingine
-
Watu walidai kuwa wanamwabudu Mungu lakini
pia waliabudu miungu
-
2falme 23 watu wa Yuda waliabudu kila kitu
kinachohusiana na dini za uongo ambayo iliangamizwa na Yosia na wala
hawakuogopa 1;18 Mungu aliingiwa na Wivu na hasira yake ikawaka
-
2;1-3 Nabii aliwakumbusha kuwa kama kuna
tumaini lolote basi linapatikana katika unyenyekevu na haki na ndipo watu
waweza kufaidika katika katika siku ya
hasira ya Bwana.
G.
Hukumu
dhidi ya mataifa 2;14-15
-
Hukumu ya Mungu ilikuwa inakuja si kwa Yuda
tu bali na kwa mataifa mengine Nebukadreza angeivamia Yuda na mataifa mengine
na kustawisha utawala wake Amosi na Zefania walitabiri na ilikuwa inakaribia
kutumia
Hukumu
ya Mungu kwa mataifa zefania 2;4-15na Amosi 1;6-2;3
|
||||
Taifa
|
Hatia
|
Adhabu
|
Zefania
|
Amosi
|
Ufilisti
|
Kuchukua mateka na kuuza
|
Kuharibiwa na ardhi yao kupewa mabaki ya yuda
|
2;4-7
|
1;6-8
|
Moabu
Na
Amoni
|
Ukatili kwa watu wa Mungu,kiburi na
kuwacheka
|
Kuuawa katika vita,kuchukuliwa mateka,kama
sodoma na Gomora na ardhi itakuwa kwa mabaki wa Mungu
|
2;8-11
|
1;13-2;3
|
Kushi
|
Haikuelezwa
|
Kuuawa kwa upanga
|
2;12
|
|
Ashuru
|
Kiburi na majivuno
|
Ninawi uabaki ukiwa na kuchukiwa na watu
wote
|
2;13-15
|
|
H.
Hukumu
dhidi ya Yerusalemu 3;1-7
-
Katika eneo hili Nabii anawageukia watu wa
Yuda na Viongozi huko Yerusalem
-
Wao walikuwa wanawajibika kwa hali ya Taifa
na walihukumiwa kutokana na maswala makuu matatu Kugandamiza watu, Uasi na
unajisi 3;1 soma 3;1-7
-
Hukumu hizi zingewahusu Viongozi wengi walio
madarakani leo
I.
Siku
ya wokovu na Furaha 3;8-20
-
Baada ya ujumbe mzito wa hukumu Zefania anamalizia ujumbe wake kwa ushindi wa kurejezwa upya wakati wa
millennium
-
Ni kweli kuwa hasira zake zitamwagwa lakini
3;8 mabaki kutoka mataifa mbalimbali wataokolewa na kutakaswa 3;9-10
-
Bwana ambaye aliwahukumu atawarudisha nyuma
adui zao katika Msalaba na atakuwa pamoja nao 3;15 Bwana ataifanya Israel sifa
na furaha.
NAHUMU:
NABII WA KUANGUKA KWA NINAWI
A. Mwandishi wa kitabu cha Nahumu
-
Nahumu maana yake ni mwenye kufariji
-
Hakuna linalofahamika kuhusu wazazi wake au
historia yake wala mafunzo yake lakini ukweli unabaki kuwa kwa kuwa ujumbe wake
unahusu hukumu ni wazi kuwa ulitolewa
wakati mfupi kabla ya Uamsho mkubwa
uliokuja wakati wa Yosia 627-621
-
Nahumu anajulikana kama Nabii wa kisasi au Nabii wa
kuanguka kwa Ninawi kinakisiwa kuwa
kiliandikwa 621 K.K. katika mwaka wa 18
wa Yosia mfalme wa Yuda na kabla ya anguko la Ninawi la mwaka 612 K.K
-
Nahumu anajiita mwekloshi 1;1 na Ekloshi yenyewe Haijulikani
iko upane gani ila kuna wanaodhani kuwa
ni kijiji kidogo mashariki ya mto Tigrisi sio mbali kutoka Ninawi na
wengine wanafikiri kuwa ni kijiji kidogo huko Galilaya karibu na Kapernaumu
jina Kapernaumu maana yake ni kijiji cha Nahumu
B.
Kiini cha kitabu
-
Kiini cha ujumbe wa kitabu hiki ni anguko la Ninawi
katika Septuagint kitabu hiki kimewekwa mara tu baada ya kitabu cha Yona ikifikiriwa kuwa ni ukamilisho wa kitabu cha
Yona
C.
Historia ya nyuma ya mambo
-
Ninawi ulikuwa ni mji mkuu wa waashuru
-
Kwa karne nyingi waashuru waliwaonea sana watu wa
mashariki ya kati na kumuka ukatili waliokuwa nao katika kitabu cha Yona na
angalia Isaya 37
-
Lakini kwa huruma zake Mungu alimtumia Yona Ninawi
na watu walitubu na kuokolewa hata hivyo baada ya Muda watu walirudi katika
njia zao za uovu vilevile
D.
Mistari ya msingi
-
1;3 -
Bwana si mwepesi wa hasira lakini ana nguvu
-
2;13 – Niko kinyume nawe asema Bwana
-
1;7 – Bwana ni mwema kimbilio wakati wa Taabu
-
1;15 – Angalia huko milimani miguu yake yeye
aletaye habari njema
E.
Uchanganuzi
-
Hasira ya Bwana 1;1-8 Kuna Maneno sita ya nguvu
katika Nahumu yanayoelezea hisia za
Mungu na majibu yake kwa waninawi Wivu,
Kisasi, Hasira, Ukali, Ghadhabu, Kumwagwa
Nahumu 1;6. Ingawa nahumu amesema wazi kuwa mungu ni mwingi wa huruma
1;7 na hivyo rehema zake na upendo wake humfanya asihukumu kwa haraka dhidi yao
wamtendao mabaya lakini wakati unakuja
ambapo hulazimika kuadhibu maovu
-
Hasira ya Mungu ni Tofauti na ya wanadamu ya
wanadamu huchanganyika chuki kwa waliomuuzi na mwanadamu hawezi kujizuia katika
hasira yake yenye ubinafsi, Hasira ya
mungu haina haraka wala ubinafsi, au
isiyozuilika kama ya wanadamu 1;3, haki yake na kisasi chake kiko katika kanini
ya kupenda na kuvuna wanadamu na mataifa yote yatavuna kile walichokipanda.
-
Wivu wa mungu ni wa haki unasukumwa na upendo wake
kwa watu na unakusudia kuwalinda kutoka
kwao wanapojaribu kuwapeleka watu wake mbali na yeye na furaha aliyoikusudia
kwao kumbuka alivyomwambia “Sauli Mbaona waniudhi”
-
Kabla ya hasira za mungu milima ilitetemeka na vilima viliyeyuka na nchi ilitetemeka 1;6
F.
Upekee wa kitabu cha Nahumu na ujumbe wake
-
Nahumu ndiye Nabii pekee anayeuita ujumbe wake
kitabu 1;1
-
Nahumu kama Yona na Obadia wanashughulika na mataifa adui
waliozionea Israel na Yuda
-
Yona aliwahubiri waninawi huko ninawi lakini Nahumu
aliizungumzia Ninawi kwa Yuda hivyo ujumbe wake ulikuwa ni faraja kwa Yuda juu
ya ukombozi toka kwa adui zao na watesi wao na hakuna mashitaka kuhusu yuda
wala wito wa toba
-
Nahumu kinasisitiza Anguko la Ninawi na kinakazia
juu ya Hasira takatifu ya Mungu dhidi ya dhambi
-
Kumbuka kuwa ujumbe wa Ninawi kwa Yuda haukutokana
na chuki binafsi za Nahumu kwa adui zao Lakini mungu alimpa ili kuthibitisha
agano lake dhidi ya Yuda na kuwakumbusha kuwa Mungu atawapigania dhidi ya adui zao
Kumbukumbu 28;1,7.
G.
Mgawanyo
-
1 Anguko la
Ninawi linatangazwa sura ya 11;1-15
-
2 Anguko la Ninawi lina changanuliwa sura ya 2;1-13
-
3 Anguko la ninawi
linathibitishwa Sura ya 3;1-19
HABAKUKI:
NABII ALIYECHANGANYIKIWA AU MWENYE MASWALI
A.
Mwandishi
wa Kitabu cha Habakuki
-
Aliyeandika kitabu hiki
anajitambulisha kama Nabii Habakuk i(1:1
; 3: 1). Hakuna maelezo mengine ya ziada kuhusu maisha ya binafsi au ya
familia ya huyu mwandishi yaliyopo po pote katika Maandiko. Alikuwa nabii wa
Yuda na inajulikana kutokana na zaburi yake (sura ya tatu) na kwenye maelekezo kwa mkuu wa waimbaji (3:19) kwamba alikuwa wa kabila la
Lawi, mmoja wa waimbaji wa hekaluni. Habakuki maana yake “Kumbatia”
-
.Kitabu cha Habakuki kimeandikwa
kwa mtindo wa mazungumzo kati ya Mungu na Nabii.
-
Habakuki aliona
kwamba viongozi wa Yuda walikuwa wanawaonea maskini, kwa hiyo aliuliza swali
kwamba ni kwa nini Mungu anawaruhusu watu hawa waovu kustawi.
-
Mungu
alipomwambia kwamba Wakaldayo wangekuja kuwaadhibu Yuda, Habakuki aliumia
zaidi. Hakuelewa ni kwa jinsi gani Mungu angeweza kuwatumia Wakaldayo ambao
walikuwa waovu kuliko Wayahudi waovu, ili kutekeleza hukumu dhidi ya watu
walikuwa watu waliochaguliwa na Mungu. Jibu la Mungu lilikuwa kwamba wenye haki wangeishi kwa imani kwa
Mungu na kwamba walikuwa na uhakika kwamba Mungu alikuwa anafanya lililo
sahihi. Mungu alimwambia Habakuki kwamba punde si punde Wakaldayo wangehukumiwa
na kwamba hatimaye haki ingeshinda kwa ajili ya watu wa Mungu. Habakuki
anamalizia kitabu kwa zaburi ya sifa.
B.
Kiini Cha kitabu cha Habakuki.
-
Mungu anavyotumia
waovu kuadhibu watu wake wanapotenda uovu kwa nia ya kuwarudisha ili wamrudie,
lakini hao waovu wakiisha kutimiza kusudi la Mungu, wao huadhibiwa zaidi.
-
Yuda walitenda
dhambi ikiwa ni pamoja na kuabudu sanamu, lakini Mungu anatumia Wakaldayo walio
waovu zaidi kuwaadhibu na hatimaye Mungu anawaadhibu Wakaldayo.
-
Ilimshangaza Habakuki kuona waovu wakistawi
huku wakiendelea kutenda dhambi nyingi wala Mungu hawaadhibu upesi! Habakuki
anaelezea imani yake katika mamlaka ya Mungu na katika uhakika kwamba Mungu ana
haki katika njia Zake zote.
-
Ufunuo wa Mungu kwa wenye haki na nia Yake ya
kuiangamiza Babeli iliyokuwa ovu iliamsha wimbo wa sifa wa kinabii na ahadi
kuhusuwokovu katika Sayuni (3:1-19)
C.
Kusudi
-
Kuonyesha kwamba
bado Mungu anaitawala dunia hata kama tunaona kwamba uovu unashamiri na ya
kwamba iko siku Mungu atauhukumu na kuadhibu huo uovu hatimye kuuangamiza
kabisa usiwepo tena.
D.
Wahusika Wakuu
-
Habakuki,
Wababeli.
E.
Tarehe
-
Kitabu hiki
hakikuwekewa tarehe, lakini bila shaka kilikuwa kipindi cha Wakaldayo.
-
1.Hekalu bado limesimama (2 :20) na huduma ya
uimbaji inafanyika (3 :19),
-
2. Kuinuka kwa
Wakaldayo kuwa dola inayotisha miongoni mwa mataifa kunatokea wakati wa kizazi
hicho (1 :5,6) na kuchinjwa kwa
mataifa na Wakaldayo tayari kulishaanza
-
(1 :6,7).Wakaldayo walijulikana
na Wayahudi muda mrefu kwa kuyashinda mataifa mengine hadi kuongoza katika dola
za ulimwengu wakati wa kuanguka kwa Ninawi 612 K.K. au 606 K.K. na kwa ushindi
wao juu ya Wamisri huko Kerkemishi mwaka 605 K.K.
F.
Mgawanyo
-
Swali la Habakuki
na jibu la Mungu. (1 :1-11)
-
Swali la pili la
Habakuki na jibu la Mungu. (1 :12-2 :20)
-
Maombi ya
Habakuki. (3 :1-19)
SURA YA NNE: MANABII WA BAADA YA UTUMWA NA WA KARIBU NA EZRA
/NEHEMIA
HAGGAI:
MTIA MOYO WA UJENZI WA HEKALU
A.
Mwandishi
-
Hagai ni moja ya vitabu vitatu
vya kinabii vya Agano la Kale vilivyoandikwa baada ya uhamisho ambavyo ni
Hagai, Zekaria na Malaki.
-
Hagai anatajwa kwa jina mara
mbili katika kitabu cha Ezra (Ezr
5:1,6:14) kama “mjumbe wa Bwana” (1:
13). Inawezekana alikuwa mmoja wa wale waliorudi kutoka uhamishoni
waliorudi Yerusalemu, walioweza kulikumbuka hekalu la Solomoni lilivyokuwa
kabla halijaharibiwa na majeshi ya Nebukadneza mwaka 586 K.K. (2:3). Hagai na Zekaria ndio
waliowatia moyo wale watu waliorudi kutoka uhamishoni kujenga upya hekalu.
-
Ilikuwa ni mnamo
mwaka 538 K.K., miaka kumi na minane ilikuwa imepita tangu Dario alipopitisha
amri kuwaruhusu Wayahudi kurudi Yerusalemu kutoka uhamishoni. Watu walikuwa
bado wanashughulika kujenga nyumba zao, hivyo ujenzi wa hekalu la Mungu ulikuwa
bado haujakamilika.
-
Kundi la kwanza la Wayahudi
lililorudi Yerusalemu liliweka msingi wa hekalu jipya.mnamo mwaka 536
K.K.wakiwa na furaha na matumaini makubwa (Ezr 3:8-10).
-
Hata hivyo Wasamaria na
majirani wengine walipinga ujenzi huo kwa nguvu nyingi na kuwakatisha tamaa
wafanya kazi hata ikafanya ujenzi huo usimame mwaka 534 K.K..
-
Watu waliacha ujenzi wa
hekalu, wakageukia ujenzi wa nyumba zao wenyewe. Ujumbe wa Hagai ulikuwa kwamba
ni wakati wa kujenga nyumba ya Mungu. Hagai akiwa amefuatana na Zekaria
(taz.utangulizi wa kitabu cha Zekaria), yeye alianza kumhimiza Zerubabeli na
watu wote kuanza tena kujenga nyumba ya BWANA. Chini ya uongozi wa Zerubabeli
mtawala na Yoshua kuhani mkuu na kule kuhimiza kwa Nabii Hagai hekalu
lilijengwa mnamo 520 K.K. Miaka minane baadaye hekalu lilimalizika kujengwa na
kuwekwa wakfu (ling.Ezr 4-6).
B.
Kiini cha ujumbe wa Haggai
- Hagai aliwaambia watu kwamba utukufu wa hekalu walilokuwa wanajenga ungekuwa mkubwa kuliko ule wa hekalu lililotangulia, ingawaje halingekuwa imara kama la kwanza. Hili hekalu lingekuwa bora zaidi kwa sababu Mungu angelijaza utukufu Wake ndani yake.
-
Kuwahimiza watu
kujenga upya hekalu la BWANA na kuwahamasiaha kuyatengeneza maisha yao upya na
Mungu ili waweze kupata baraka Zake.
C.
Historia ya nyuma ya mambo
-
Hekalu la
Yerusalemu lilibomolewa mnamo mwaka 586 K.K. Mwaka wa 538 K.K,
-
Mfalme Koreshi wa
Uajemi alitoa amri Wayahudi warudi ili kujenga upya mji wa Yerusalemu na
hekalu.Mwaka 536 K.K.walianza kujenga hekalu lakini ilikuwa vigumu kumalizia
kutokana na upinzani waliokutana nao kutoka kwa Wasamaria na mataifa ya jirani.
-
Kupitia huduma ya
Hagai Zekaria na Yoshua, mwaka 520 K.K., walianza kujenga tena hekalu.Miaka
minane baadaye kazi hiyo ya ujenzi wa hekalu ilimalizika.
Mabaki
ya ikulu ya Mfalme Dario Mmedi /Mmuajemi ni katika utawala wake ndipo Nabii
Haggai aliandika kitabu chake cha kuhamasisha ujenzi wa Nyumba ya bwana makazi
haya ya iliyokuwa ikulu yako mahali paitwapo Persepolis Nyakati za Leo Picha na
maelezo kwa hisani ya Maktaba ya mwalimu Innocent KamoteMchungaji.
D.
Tarehe ya uandishi
-
Tarehe ya
kuandikwa kwa kitabu kwa hiki ni ya uhakika, yaani, mwaka wa pili wa Mfalme
Dario wa Uajemi (mwaka 520 K.K. (1:1).
-
Mpangilio wa
kihistoria ni wa muhimu sana ili kuuelewa ujumbe wa kitabu hiki. Mnamo mwaka
538 K.K., Mfalme Koreshi wa Uajemi alitoa amri ikiwaruhusu Wayahudi waaliokuwa
uhamishoni kurudi nchini mwao ili kuujenga upya Yerusalemu na hekalu katika
kutimiza unabii wa Isaya na wa Yeremia (Isa45:1,3; Yer 25:11-12; 29:10-14) na
maombezi ya Danieli (Dan 9).
E.
Wahusika Wakuu
-
Hagai, Zerubabel,
Yoshua.
F.
Mgawanyo
-
Wito wa kujenga
hekalu. (1:1-15)
-
Matumaini ya
hekalu jipya. (2:1-9)
-
Baraka
zilizoahidiwa. (2:10-19)
-
Ushindi wa mwisho
wa Mungu. (2:20-23)
ZECHARIA:
NABII WA MAONO KUHUSU MASIHI;
A. Mwandishi
-
Zekaria alianza huduma yake
mnamo mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa Dario (520 K.K.), miezi miwili baada ya
ujumbe wa kwanza wa Hagai. Maana ya jina Zekaria ni “BWANA amekumbuka.”
-
Haijulikani kwa uhakika
Zekaria aliendelea kufanya huduma hiyo kwa muda gani.Kwa kadiri ionekanavyo
alikuwa kijana (2:4) wakati
alipoanza huduma yake.
-
Ido, ambaye ni babu yake (Zek 1:1) alikuwa miongoni mwa wale
waliorudi kutoka uhamishoni mwaka 538 K.K.
-
Katika ujumbe
wake wa kwanza (1:1-6) Zekaria
anawaonya watu ambao ndio kwanza tu walikuwa wameanza kujenga upya hekalu
kwamba inawapasa kusikiliza ujumbe wa Mungu kupitia manabii na kudumisha
uhusiano wa muhimu na Mungu, wasije wakaharakisha hukumu ya Mungu.
-
Mfululizo wa
maono ya usiku (1:7-6:8) yanatia
moyo wajenzi ule wakati mgumu katika hatua ya kukata tamaa.
-
Ule utaratibu wa
ujenzi ulikuwa umesababisha maafisa wa Kiajemi kufanya uchunguzi na kuandika
taarifa ya malalamiko kwa Dario (Ezr
5-6). Huenda Wayahudi walikuwa wakingojea hukumu ya Dario wakati Zekaria
akitoa ujumbe wake uliowekewa msingi katika haya maono ya usiku. Mtazamo wa
jumla wa mfululizo wa maono haya manane yanawahakikishia wajenzi kwamba Mungu
anao mpango wa muda mrefu kwa ajili ya Israeli. Miaka miwili baadaye, (518 K.K.)
suala la kutia katika matendo kutii kufunga liliibuka (7:1-8:23). Zekaria kwa mara nyingine anaangaliza watu kwamba
njia ya kudumisha uhusiano sahihi na Mungu ni utii. Kule kufunga ili tu kwamba
mtu amefunga ni ubatili.Utaratibu wa kushika sheria kamwe hauwezi kutumika kama
njia mbadala ya kuonyesha upendo wa Mungu katika maisha ya kila siku. Sehemu ya
mwisho ya ujumbe wa Zekaria (9-14) haukuonyeshwa
tarehe. Uwezekano mkubwa ni kwamba ulitolewa baadaye, huenda mnamo mwaka 480
K.K. Hapa mkazo uko katika mpango wa maendeleo wa muda mrefu ukionyesha
kusimamishwa kwa ufalme wa mwisho. Mfalme anatambulishwa kama anayekuja kwa
tabia ya unyenyekevu akileta wokovu lakini akikataliwa na watu wake mwenyewe,
yaani, Waisraeli, ambao baadaye wanaachwa kwenye hukumu ya mataifa. Mataifa
yatakapokusanyika kwa ajili ya vita dhidi ya Yerusalemu, Waisreli watamtambua
Yeye “Yule waliomchoma mkuki” (Zek.12:10)
na wataibuka na ushindi. Ndipo mataifa yote yatakuja Yerusalemu
kumwabudu Mfalme, Bwana wa Majeshi.
B.
Kiini cha kitabu cha Zekaria
-
Zekaria
anaonyesha kwamba Mungu ana mpango wa muda mrefu na Israeli, hivyo anaita mwito
wa utii.
-
Anaonyesha jinsi
ambavyo watu wanaweza kufanya mambo “ Si kwa nguvu wala kwa uwezo bali kwa Roho
Yangu ”asema.( 4:6)..
-
Kuwapa watu wa Mungu matumaini kwa kuwajulisha watu mpango wa Mungu wa
baadaye wa ukombozi kupitia kwa Masihi.
C.
Historia ya Nyuma ya mambo
-
Huu ujumbe wa
mwanzoni unafuatiliwa na maono ambayo yaliwatia moyo wajenzi ambao Zekaria
aliwatia moyo kwa kuwaambia kwamba Mungu alikuwa na mpango mrefu kwa ajili ya
Israeli.
-
Katika sura ya 7 na 8 Zekaria
aliwataka watu wamtii Mungu, hii ikiwa ni njia ya kila mtu kumjali na
kumhurumia mwenzake. Mungu alitaka utii kwao katika kuhusiana naye.
-
Sura ya 9 mpaka
14 inazungumzia habari za miezi inayokuja, hukumu ya mwisho na kukua kwa muda
mrefu kwa ufalme wa mwisho.
D.
Mahali
-
Yerusalemu
E.
Tarehe
-
520-470 K.K.
F.
Wahusika
-
Hagai,
Zerubabeli, Yoshua na waliorudi kutoka uhamishoni.
G.
Mgawanyo
-
Wito
wa kuwa watiifu. (1:1-6)
-
Maono.
(1:7-6:15)
-
Hukumu
dhidi ya maadui wa Israeli. (9:1-8)
MALACHI:
NABII WA SIKU ZA UAMSHO
A. Mwandishi
-
Malaki aliishi katika nusu ya
pili ya karne ya tano Kabla ya Kristo, baada ya ujenzi wa hekalu kumalizika.
Malaki ambalo ni neno la Kiebrania ‘‘Malaki’’ kama lilivyo kwenye
Kiswahili, maana yake ‘‘Mjumbe
wangu.’’. Jina hili ni kifupi cha ‘‘Malakia’’
ambalo maana yake ni ‘‘Mjumbe
wa Bwana‘’ (1:1).
-
Jina hili la kitabu limetumika
vivyo hivyo kwenye maandiko ya Kiebrania na Kiyunani likionyesha kwamba hili likuwa
jina la nabii ambaye ujumbe wake umenukuliwa humu. Hakuna habari nyingine zo
zote za kibinafsi zinazofahamika za huyu nabii. Maisha ya kidini ya Wayahudi
yalikuwa mabaya :
-
Walikuwa wamekengeuka, wakawa wameoa wanawake
wa mataifa mengine, wakaacha kutoa zaka (fungu la kumi) na dhabihu ambayo na
sehemu ya Mungu, hata wakawa wamemwacha Mungu, hali ambayo ilifanana sana na
ile iliyokuwepo wakati wa Nehemia (444-432 K.K.).
B. Kiini cha ujumbe wa kitabu cha
Malaki
-
Masikitiko makubwa ya Malaki ni uhusiano kati ya Waisraeli na Mungu
haukuwa kama ulivyopaswa uwe. Walimwacha Mungu na kumdharau, wala
hawakumheshimu inavyostahili, wakashindwa kufuata yale Mungu aliyowaagiza.
Matokeo yake hukumu ikawa inawangoja, lakini watu wanaomcha Mungu
wamehakikishiwa kuwa wameandikwa kwenye kitabu cha Mungu, nao watafuhia wokovu
wa Mungu milele.
C.
Kusudi
-
Kuwahimiza watu wafanye
mabadiliko thabiti ya kimsingi katika maisha yao, kwa kuwakumbusha upendo wa
Mungu (1:1-5) na pia kwamba
adhabu yake iko karibu (2:17; 3:13)
D. Mchanganuo wa kitabu cha
malaki
-
Kitabu hiki kinaonyesha
kuwa:(1)Hekalu lilijengwa tena (516/515 K.K.), dhabihu na sikukuu zilirudishwa.
(2)Ufahamu wa jumla wa sheria ulirudishwa tena na Ezra (kama 457-455 K.K. ; tazama Ezra 7 :10, 14, 25-26) na
(3).Kurudi nyuma kimaadili kulikofuatia kulitokea miongoni mwa makuhani na mwa
watu pia (kama mwaka 433K.K.). Kutokana na hali hii hali ya kiroho na upuzi
Malaki anaouzungumzia kwa karibu vilifanana sana n aile hali aliyoikuta Nehemia
aliporudi kutoka uhamishoni Uajemi (kama 433-425 K.K.) ili kuwa mtawala wa
Yerusalemu (ling. 13 :4-30).
E.
Mahali
-
Yerusalemu. Malaki, Hagai na
Zekaria walikuwa manabii katika Yuda (Ufalme wa kusini) baada ya watu kurudi
kutoka uhamishoni.. Hagai na Zakaria waliwakemea watu kwa kutokumalizia ujenzi
wa hekalu. Malaki alipambana nao kwa sababu walipuuzia hekalu na kutokumjali
Mungu.
F.
Tarehe
-
Yale yaliyomo kwenye kitabu
hiki yanaonyesha kwamba huduma ya Malaki ilikuwa kwenye utendaji mnamo sehemu
ya pili ya karne ya tano Kabla ya Kristo. Hekalu lilikuwa tayari limeshajengwa
tena upya. Kutokana na wakati alioishi Malaki na yale yaliyomo kwenye kitabu
hiki, inawezekana kiliandikwa 557- 525 K.K.
G.
Wahusika
wakuu
-
Malaki na makuhani
H.
Mgawanyo
-
Upendo wa Mungu kwa Israeli.
(1:1-5)
-
Israeli yamtukana Mungu.
(1:6-2:16)
-
Hukumu ya Mungu na ahadi yake.
(2:17-4:6)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni