Mstari wa Msingi;(Zaburi 103;12)’Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi”
Utangulizi;
Moja ya mbinu kubwa
anayoitumia shetani na kufanikiwa kuwarudisha watu nyuma Katika uchanga wao ni
kuwafanya wautilie mashaka wokovu, Atawatia mashaka kujihoji kama kweli
wamesamehewa dhambi zao, njia hii ataitumia pia kwako atakufanya ujiulize
maswali kuwa wewe nawe umneokoka? Au unajidanganya mwenyewe? Atakuuliza mbona
hakuna badiliko lolote? Mbona uko vile, au mbona umekasirika leo asubuhi na
waliookoka hawapaswi kuwa na hasira? Hii yote ni gea ya kukutia mashaka ili
uhisi kuwa hujaokoka na hatimaye kurudi nyuma.
Kurudi Nyumbani
Ni muhimu kufahamu kuwa tunapokea wokovu
kwa Imani na si kwa kuona au kwa hisia au kujisikia kuwa sasa nimeokoka, tunapookoka
miili yetu itakuwa vilevile na hakutakuwa na badiliko isipokuwa katika roho
kunatokea mabadiliko makubwa, Mambo ya kiroho yanatambulika kwa kungalia neno
la Mungu linasema nini tangu ulipoamua kukata shauri na kutubu dhambi zako kwa
kumaanisha kuziacha ukiamini kazi aliyoifanya Yesu pale msalabani haya ndiyo
yanayotokea katika ulimwengu wa kiroho;-
- Dhambi zako Zimesamehewa na Mungu hazikumbuki tena ;
Mtu anapoamua
kutubu dhambi zake kwa kumaanisha kuziacha Mungu humsamehe mtu huyo na
hakumbuki tena dhambi hizo (Zaburi
103;12).”Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi ndivyo alivyoweka dhambi
zetu mbali nasi” Isaya 1;18.
- Mungu huyafuta makosa Yetu kwa ajili yake Mwenyewe;
(Isaya 43; 25) Biblia inasema “Mimi naam
mimi ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe; wala sitazikumbuka
dhambi zako” Ni mpango wa Mungu mwenyewe kabisa kutusamehe na kutuketisha
katika pendo la mwana wake Tangu tulipookolewa tunao ukombozi yaani msamaha wa
dhambi (Kolosai 1;13-14,21-22)
- Dhambi zetu zilizokuwa nyekundu kama Bendera zinafutwa kuwa nyeupe kama Theluji.
Hii ni ahadi ya Mungu mwenyewe kuwa
anapotuita kwake na tukakubali hutupa thawabu ya msamaha na kutuhesabu kama
viumbe vipya huku akituhakikishia msamaha wa dhambi (Isaya 1;18).
- Sasa Unao uhakika wa uzima wa milele.
Kabla ya kutubu dhambi zetu kwa kumaanisha
kuziacha na kumwamini Yesu mwana wa Mungu aliyekufa kwa ajili ya dhambi zetu.Tulikuwa katika ghadhabu ya
Mungu na hivyo uzima wa milele ulikuwa Mbali nasi,Tulikua chini ya hukumu
Lakini sasa tu warithi wa pamoja na Kristo (Yohana 3;18,36,Warumi 8;14-17,1Yohana 5;11-13).
- Hutapotea kamwe ukiwa mikononi mwa Yesu
Kuanzia
ulipokata shauri kuokoka wewe sasa uko
mikononi mwa YesuKristo nay eye nia yake
na mapenzi yake kabisa ni kwamba
uendee mbinguni huko aliko na kufurahi
pamoja naye milele na milele ni mapenzi
ya Baba yake pia na kwa kua ana nguvu
kuliko Shetani atahakikisha ya kuwa
yeyote atakaye kukupokea kutoka katika mikono yake ili urudi katika ghadhabu ya milele
hatafanikiwa Yohana 10;27-29 hiyo ndiyo ahadi yake kwako Hata hivyo ni muhimu
kufahamu kuwa hata wewe una sehemu ya kufanya ili haya yaweze kutimia
kwako mambo yafuatayo ni muhimu sasa
kwako kuyafanyia kazi
a. Jifunze kuisikia sauti ya Bwana Yesu
Sauti ya Bwana
Yesu ni Neno la Mungu inakupasa kila uatakalojifunza katika Neno la Mungu yaani
Biblia ulisikie na kuliweka Moyoni, Ni lazima upende kusikia Neno la Mungu na
upende pia kulisoma na kulijifunza neno la Mungu
b. Jifunze kumfuata Yesu
Yesu alikuwa mtii kwa Baba yake sisi nasi kama kondoo wake
inatupasa kuwa watii pia, Neno la Mungu linapotutaka kubadilika ni muhimu tuwe
watii na kujifunza kumfuata bwana Yesu kila jambo analolitaka tulifanye basi
lifanyike mara moja huko ndiko kumfuata
bwana Yesu si vema kujiongoza wenyewe katika kila jambo lakini na tuyafuatae maongozi ya Bwana
Yesu Yeye ndiye mwokozi wetu na Bwana wetu Warumi 10;9 Jina Bwana
humaanisha mtawala hivyo kumkubali Yesu kuwa ni Bwana maana yake ni kukubali
atutawale, Hapo mwanzo tulifanya kila tuliloliona jema machoni petu lakini sasa
inatupasa kukubali maongozi ya Mungu wetu
sisi sio waasi tena Mungu alituokoa kutoka katika maasi 1Yohana 3;4 kwa msingi huo hatupaswi kumuasi tena
Mungu ukiyafanya haya hutapotea kamwe na
hakuna atakaye kutoa katika mikono ya Mungu na uzima wa milele ni wako na makao yako sasa ni mbinguni Yohana
10;27-29
Madhara ya kufanya dhambi baada ya kuokoka
Dhambi ni jambo la kuchukiza sana
machoni pa Mungu Mungu anawapenda sana watu lakini Mungu anachukia dhambi, kuna
uwezekano kwa mtu aliyeokoka kufanya dhambi lakini mara anapogundua kuwa
amefanya dhambi anapaswa kutubu dhambi
hiyo mara moja na Bwana atatusamehe 1Yohana 2;1 “Watoto wangu wadogo
nawaandikia ili kwamba msitende dhambi na kama mtu akitenda dhambi tunaye
mwombezi kwa baba Yesu Kristo mwenye
haki naye ndiye kipatanisho kwa dhambi zetu wala si kwa dhambi zetu tu bali na
kwa dhambi za ulimwengu wote” 1Yohana 1;9 “Tukiziungama dhambi zetu Yeye ni
mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi
zetu na kutusafisha na udhalimu
wote” Kwa msingi huo basi ni vema kuungama dhambi hiyo kwa toba na
kutokukusudia kuirudia tena hapo utakuwa salama
na wokovu wako utakuweko palepale.
Lakini ni muhimu kufahamu kuwa
mtu aliyeokoka hafanyi dhambi kwa kukusudia wala hapaswi kuishi maisha ya
dhambi 1Yohana 5;18 mtu aliyeokoka anachukia dhambi na anapokuwa ameifanya
anahuzunika sana na kutubu maana tumeitwa kuwa watakatifu, katika hatua
za mwanzoni mwa wokovu ni rahisi kukosea katika maeneo mbali mbali lakini inakupasa kutubu na kuacha Waefeso 1;4-5 Tumeitwa katika utakatifu
Kwa msingi huo sasa jitambue kama mtoto halali
wa Mungu na kuwa umeokoka uzima wa milele ni wako na kuamini ya kuwa yeye
aliyeanza kazi njema mioyoni mwetu ataikamilisha Wafilipi 1;6
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni