*********************************************************************
Somo ;
Wito wa kumtumikia Mungu
Somo tunalojifunza sasa katika Mfululizo
wa Masomo maalumu ya shule ya uongozi ni Wito wa kumtumikia Mungu hili ni moja
ya Masomo muhimu sana na tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele vitano
vifuatavyo;-
Mafundisho
ya msingi kuhusu wito wa kumtumikia Mungu
Aina
tatu za wito wa kumtumikia Mungu
Njia
Tofauti za kuteuliwa katika kushika nafasi za uongozi wa kanisa
Aina
ya watu wanaoitwa na Mungu
Neema
ya kuwekewa mikono katika Mpango wa Mungu
Mafundisho ya msingi
kuhusui wito wa kumtumikia Mungu
Wako
watu wengine katika kanisa la Mungu ambao kwa kukosa Ufahamu husema hawawezi
kukubali kumtumikia Mungu au kukubali nafasi yoyote ya uongozi katika kanisa
kwa madai kuwa eti mpaka wasikie Sauti halisi ya Mungu ikiwaita katika utumishi
huo, huku ni kukosa Hekima na sio sahihi Wito wa kumtumikia Mungu sio lazima
uambatane na kuisikia sauti halisi ya Mungu Elisha hakusikia sauti ya Mungu
alipoitwa ni Eliya alipita karibu naye na kumtupia vazi 1Falme 19;19-21 pamoja
na hayo Mungu alikuwa pamoja naye na alimtumia kwa upako maradufu kuliko Eliya,
Yoshua hakusikia pia sauti ya Mungu bali
alitwaliwa na Musa na kuwekewa mikono Hesabu 27;22-23 pamoja na hayo Yoshua
alikuwa mtumishi wa Mungu wa kipekee, upande mwingine pia wako watu ambao
hujipachika majina makubwa kama Mwinjilisti, Mwalimu, Mchungaji n.k bila ya
kuwa na wito maalumu wa kuwafanya wawe na nafasi hizo watu wa jinsi hii hufanya
makosa na wanapojaribu kufanya kazi hizo kamwe hawawezi kupata matokeo mazuri
mfano wa kibiblia ni kwa AHIMAASI mwana wa Sadoki na mkushi mmoja Ahimaasi alikuwa na moto wa kijipachika cheo
cha kuwa mchukuwa habari na kufikiria kuwa ni swala la kuwa na ubingwa wa kupiga
mbio na ni kweli alikuwa wa kwanza kufika kwa mfalme Lakini alipofika na kuulizwa habari
alibabaika tu na hakuwa na ujumbe maalumu kama ilivyokuwa kwa mkushi aliyekuwa
na wito maalumu wa mchukua habari 2Samuel 18;19-33. Awaye yote anayetaka
kumtumikia Mungu ni muhimu kuwa na wito.
Aina tatu za wito wa
kumtumikia Mungu
Ziko
aina kuu tatu za wito kuelekea katika kumtumikia Mungu
1.
Wito wa jumla katika wokovu- huu ni wito ambao mtu huitwa kutoka dhambini na
kusamehewa dhambi ili apate kumuabudu Mungu
na ili kuurithi uzima wa milele hata hivyo wito huu huambatana na wito
wa jumla wa kumtumikia Mungu yaani Mungu anapokuwa amekuokoa anataka pia
umtumikie
2.
Wito wa jumla wa kumtumikia Mungu- Mtu hawezi kuingia katika wito wa jumla wa
kumtumikia Mungu kabla hajaokoka, Lakini punde mtu huyo anapokuwa ameokolewa
anakuwa ameitwa katika wito wa jumla wa kumtumikia Mungu na wito wa kuyaishi
maisha matakatifu Waefeso 4; 1,1Petro 1; 15-16 kila mtu aliyeokoka amepewa wito
wa kuenenda ulimwenguni mwote na kuihubiri injili kwa kila kiumbe Mathayo
28;19-20 Marko 16;15 wito huu ni kwa jinsia zote, Nyakati za kanisa la kwanza
watu woote waliitikia wito huu pale walipotawa nyika na kwenda huko na huko
wakiwaacha mitume pale Yerusalem Matendo 8;1,4. Hivyo kila mtu aliyeokoka bila
hata ya kungojea sauti ameitwa katika wito huu wa kumtumuikia Mungu
3.Wito
maalumu wa kumtumikia Mungu- wito huu hutolewa na Mungu kwa Mtu maalumu ili kufanya utumishi Fulani wa kimaongozi
katika kanisa wakati mwingine wito huu
utaambatana na karama maalumu zitakazomwezesha mtu huyo kulitimiza Jukumu
alilopewa kwa ufanisi .Yusufu alipewa wito maalumu wa kuhifadhi roho za watu na
maisha yao wasife kwa njaa na alipewa karama maalumu za kutafasiri ndoto Mwanzo
45;5-8 wito huu ulioambatana na karama hizo maalumu ulimuwezesha kuwa waziri mkuu katika inchi ya
Misri, Esta 4;15-16 alikuwa na wito maalumu wa kuliokoa taifa la kiyahudi
lisiangamizwe na aliwezeshwa kuwa tayari kuangamia au kukutana na magumu ya aina yoyote ile
hivyo ili mtu awe Mtume, Nabii, Mwinjilisti, Mchungaji au Mwalimu lazima wito
wake uambatane na neema maalumu itakayomwezesha kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi wa
kipekee, aidha wito maalumu pia huambatana na mtu kuwa mwaminifu katika
kutekeleza wito wa jumla wa utumishi kabla ya kuingia katika wito maalumu wa
kumtumikia Mungu Matendo 13;1-3 Barnaba na Sauli walikuwa waaminifu sana katika
wito wa jumla wa kumtumikia Mungu kabla hawajaitwa katika wito maalumu wa
kumtumikia Mungu baada ya kupewa wito maalumu huduma zao zilibadilika kabisa.
Njia Tofauti za
kuteuliwa katika kushika nafasi za uongozi wa kanisa
- Kujipachika mwenyewe uongozi
Hii ni sawa na ule mfano wa Ahimaasi
mwana wa Sadoki 2Samuel 18;19-33 na tuliona kuwa matokeo yake haya kuwa mazuri,
Uzia alijipachika kufanya ukuhani na matokeo yake alipatwa na ukoma na kufa
2Nyakati 26;16-23 kora na wenzake hawakuwa tayari kuwa chini yza Musa yeye na
wenzake wakataka na ukuhani matokeo yake walipoteza hata nafasi ile waliyokuwa
nayo wakafa kifomcha aibu Hesabu 16;1-35 ni hatari kubwa mtu kijipachika
uongozi katika kanisa.
- Kuchaguliwa na wanadamu bila kufuata uongozi wa Roho mtakatifu.
Kiongozi wa kiroho kamwe hachaguliwi
kwa kupigiwa kura au baada ya kufanya kampeni nyingi kama za kisiasa,tunaweza
tukampigia kura mwanadamu Fulani na ikawa Bwana hakumchagua huyo Baada ya
Mathiya kupigiwa kura na kushindwa kwa kura katika Matendo 1;23-26 hatuoni jina lake likitajwa tena katika Biblia najua
kuwa Vitabu vya kihistoria vinaeleza kazi alizozifanya Lakini hatuoni tendo la upigaji kura
likirudiwa tena katika agano jipya Mungu ndiye anayechagua Viongozi katika 1Samuel
16;6-7 Samuel alimchagua Eliabu Lakini Bwana hakuwa amemchagua huyo, Ni
marufuku kuchagua kiongozi wa kanisa kwa kumpigia kura swala hili limeleta
migogoro mingi katika makanisa Kiongozi wa juu wa kiroho ndiye anayechagua Viongozi walio chini yake kwa kuongozwa na Roho wa Mungu Luka 6;12-16
Matendo 15;40-41;14;23;Toto 1;4-5 au Mungu kusema Kupitia Roho Mtakatifu
Matendo 13;1-3.
- Kuchaguliwa na Mungu Mwenyewe.
Mungu anaweza kuchagua mwenyewe
Viongozi mbalimbali wa kanisa Yeremia 1;15 Hata hivyo Mungu anapochagua
mwenyewe huduma ya mtu huyo itakuwa dhahiri katika kanisa na kutakuwa na
udhihirisho wa wazi wazi unaothibitisha
kuwa huduma ya mtu huyo imetoka kwa Mungu
- Kuchaguliwa na Mungu Kupitia watumishi wake.
Yoshua alichaguliwa na Mungu Kupitia
mtumishi wake Musa Hesabu 27;16-18.elisha alichaguliwa na Mungu Kupitia Eliya
1Falme 19;15-16 Paulo mtume alimchagua Silla
kwa uongozi wa Mungu Matendo 15;40 halikadhalika Viongozi wengi wa
Nyakati za kanisa la kwanza walichaguliwa na watumishi wa Mungu kwa uongozi wa
Mungu Matendo 14;23,Tito 1;4-5 kwa msingi huu basi Mchungaji akimchagua mtu
kuwa kiongozi wa kanisa la nyumbani sehemu au zone au kuongoza idara nyingine
yoyote hufanya hivyo kwa uongozi wa Mungu na hivyo mtu huyo aliyechaguliwa
hakujitwalia mwenyewe heshima hiyo Waebrania 5;4 na anakuwa ameitwa na Mungu.
Aina ya watu wanaoitwa
na Mungu
Mungu katika Hekima yake huwaita watu
wengi wasio na Hekima ya mwilini au wasio na nguvu wasio na cheo au
wanaoonekana kuwa wapumbavu na dhaifu wanyonge na wanaodharauliwa ili adhama na
sifa kuu ya uwezo wa iwe ya Mungu mwenyewe na sio ya mtu yule dhaifu 1Koritho
1;26-29, 2Koritho 4;7 hivyo hatupaswi kujiona kuwa hatufai Kuchaguliwa . Musa
alikuwa na kigugumizi, Yeremia alikuwa mtoto n.k sisi nasi tunaweza kujiona
kuwa tuna mapungufu Fulani wakati Mungu anapotuita kwenye utumishi hayo
yasikukatishe tamaa kwani yeye ndiye atakaye tuwezesha si kwa nguvu wala kwa
uwezo bali kwa Roho wangu asema Bwana wa majeshi Zekaria 4;6 Warumi 9;16.
Neema ya kuwekewa
mikono katika Mpango wa Mungu.
Tunapochaguliwa kuwa Viongozi wa kanisa na
kuwekewa mikono na yule aliyetuchagua kuwa Viongozi kwa uongozi wa Mungu Sehemu
ya heshima yake na uwezo wake aliopewa hutushukia Hesabu 27;18-23. Yoshua baada
ya kuwekewa mikono na Musa alibadilishwa
kabisa na watu wakamuheshimu Kumbukumbu 34;9.Kuwekewa mikono namna hiyo
huchochea karama zilizofichika ndani yetu na kizifanya zijitokeze 2timotheo 1;6
Kwa msingi huo Mchungaji anapotuwekea mikono ili tuwe Viongozi wa Makanisa na
idara na sehemu nyinginezo sehemu ya uwezo aliopewa huja kwetu na kutusaidia
kikamilifu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni