Ni muhimu kufahamu kuwa kuna uhusiano
wa karibu kati ya kutafasiri Maandiko na utii. Jinsi gani tunalijua na
kulifahamu neno la Mungu inatokana na jinsi ambavyo tunalitii shida kubwa sana
ya wanadamu haiko katika kujua bali iko katika kutenda kwa mfano Wafilipi 2;14
inasema “Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano” mahali hapo
shida haiko katika kuelewa iko katika kutii yaani kulifanyia kazi hilo
Mtafasiri mzuri wa Maandiko lazima awe analitendea kazi Neno la Mungu
I. UTII ni njia ya kufungua mlango wa
Mungu kuzungumza nasi Mithali 8;17, Yohana 14;21.
A. Mungu hufunua kweli zake kwa watu
ambao wako tayari na wenye mioyo iliyopondeka
·
Kama tunaweza kutii katika kidogo
tulichonacho Mungu hutufunulia makubwa kuliko hayo
A. John
7:17: Kutii mapenzi ya Mungu kunafungua mlango mkuu zaidi wa Ujuzi wa neno la
Mungu
II. Kutokutii
kunafunga mlango wa Kuifahamu kweli ya kimungu kwa upana zaidi Matth. 13:10-15,
Rom 1:18-25, 5:11-14
III.
Ufahamu wa mtu asiyetii unaharibika Mtu anayeishi katika maisha yasiyo na utii
hafai kuwa mtafasiri bora wa Maandiko kwa kawaida dhambi na kukosa toba
kwaajili ya dhambi hiyo kunachangia mtu asiwe mtafasiri mzuri wa Maandiko Mungu
husikitishwa sana na mtu asiyefanya yale aliyoamuriwa kuyafanya 1Samuel
15;2210-23 Mtu anapolikataa neno la Bwana Mungu naye humkataa mtu huyo asiwe
mtafasiri halali wa Neno lake, aidha tabia ya kutokulitendea kazi Neno
inakufanya kudumaaa na hivyo inakuwa ngumu kufundishika kama watu wamedumaa
kiroho
Mwandishi wa kitabu cha Waebrania
alisema ni vigumu kufundisha watu ambao wamedumaa au wasiolitendea kazi neno la
Mungu au wasio na utii kwa neno la Mungu hawa watahitaji maziwa ili wakue kwani
wamedumaa soma Waebrania 5;11-14, pia kuna hukumu kwa ajili ya watu wanaoijua
kweli kisha wakaikandamiza kwa Matendo maovu Warumi 1;18-19, ufahamu wao hauwezi
kuwa sawasawa, Warumi 1;21-22 na Warumi 1;24-25 kumbuka kuwa watu wengi walio
katika imani potofu wanaufahamu wa kweli kuhusu kweli ya Mungu lakini
wanaipuuzia tu na matokeo yake watu
wanashindwa kupambanua iliyo kweli na yasiyo kweli kwa sababu ya maisha yao ya
uasi , Aidha watu waasi pia huishi maisha ya ukristo wa mwilini Paulo mtume
alizungumza na wakristo wa Koritho na sio watu wasioamini ambao walikuwa na
tatizo la kutokuelewa mambo ya kiroho kwa sababu ya tabia ya mwilini 1Koritho
3;1-3 hawa ni watu waliokuwa na wivu, Faraka na maswala ya kisiasa na kwa
sababu hiyo pia walihitaji maziwa
wanafungwa na vifungo vya kuijua kweli kwa sababu wako mwilini canal
Christians Mwandishi wa Zaburi akasema “mimi ninao ufahamu kuliko wazee kwa
sababu nayatii mausia yako” Zaburi 119;100. Kumbe basi utii unasaidia kuwa na
ufahamu wa neno la Mungu, Neno la Mungu linaweza kueleweka vema kwa
namnazifuatazo
·
Ufahamu wa kawaida wa kiakili “Oida”
·
Ufahamu wa kawaida wa kisomi au
kisayansi “Ginosko”
·
Ufahamu wa kawaida mwepesi
“lambano”
·
Ufahamu unaotokana na Ufunuo wa Roho wa
Mungu na shuku ya kiungu “Dechomai”
Ufahamu huu unaotokana na Maneno
aliyoyatumia Paulo mtume katika 1 Wakoritho
2 ; 10-16 kufunuliwa kwa Roho Mst 10,kuyajua na kuyakubali Dechomai hii
humtokea mtu wa Rohoni, kutokupokea na kuona ni upuuzi hii humtokea mtu wa
mwilini hivyo hawezi kufahamu. Hii ni athari ya kuto kumtii Mungu wala Roho
wake kwa hivyo mtu asiyetii Hastahili kuyatafasiri Maandiko Neno hilo Dechomai
humaanisha pia kupokea kwa moyo na sio kwa kichwa Ginosko, moyoni ni mahali
ambapo hisia ,nia ,mawazo na misukumo huanzia hapa ndipo ambapo Roho wa Mungu
huanzia kazi zake Hivyo mpokeaji kutoka kwa Mungu Dechomai pia hupokea kwa
shauku hata hivyo upokeaji wa neno kati ya muumini na muumini hutofautiana kwa
hivyo inahitajika Roho ya Hekima na ufahamu ili kuweza kujua vizuri kwa
kufunguliwa macho ya mioyo yetu ambayo kwa hiyo sasa tunapata kujua utajiri wa
utukufu na urithi wa watakatifu Efeso 1;17-18,Kolosai 1;9 kutofautiana katika
kuipokea kweli kati ya muamini na muamini kunaathiriwa na mitazamo Perception
watu wa Beroya walikuwa waungwana kwa sababu hii walilipokea neno kwa moyo na
pia walichunguza waone kuwa Maandiko hayo ndivyo yalivyo Matendo 17;11 Hivyo
hata akihubiri malaika lazima neno lake lipimwe kama ndivyo lilivyo hii ni kwa
sababu mtazamo unaweza kuchangia mtu atafasiri Maandiko isivyo halali mtazamo
ni moja ya vizuizi vya kutafasiri Maandiko kitaalamu unaitwa Bias Grid
unakufanya usilione neno sawasawa
Mtafasiri wa Maandiko Kizuizi cha kutafasiri a
Bias grid Neno la Mungu Biblia
Mtafasiri wa Maandiko asiye na Mtazamo sahii hawezi kulielezea vema Neno la Mungu kwa ulinganifu sahii mpaka kizuizi kiondoke.
Hivyo anachokifanya Roho wa Mungu sio
kuleta kweli mpya bali ni kusaidia kuondoa kizuizi kwa moyo wenye utii au
shauku ya kutaka kujua kweli ili kuipokea kweli kwa halali na kutafasiri
Maandiko kwa usahii Ufunuo huu huitwa Illumination yaani kuangaziwa kuijua
kweli ya neno la Mungu
Athari za mitazamo katika kutafasiri neno la Mungu
Wote tunajua kuwa historia zetu za
Nyuma zinaweza kuathiri utafasiri wa Maandiko na wakati mwingine kunaweza
kukufanya usitafasiri Maandiko ipaswavyo au sawa na maana iliyokusudiwa na
Mwandishi kwa mfano angalia picha hii Mwandishi alikusudia kuchora kikombe
lakini unaweza kuona picha ya watu wa wili wanaokaribiana uso kwa uso
Pichani inaonekana picha ambayo
Mwandishi alikusudia kuchora glasi lakini unaweza kufasiri zaidi ya glasi kwani
unaweza kuona sura za watu wawili wanaokaribiaana uso kwa uso matazamo inaweza
kuathiri ufasiri wa kimaandiko Picha na maelezo kwa hisani ya maktaba ya Mchungaji
Innocent Samuel Kamote
IV. Ufahamu wa Mtu mtii utaongezeka
Ni muhimu kufahamu kuwa wale wanaojua
kidogo mara baada ya kuipokea kweli fulani Mungu atawapa maarifa zaidi kumbuka
wakati Yesu alipozaliwa mamajusi toka mashariki walianza kuifuata nyota wakijua
kua inaashiria Kuzaliwa kwa masihi hata hivyo baadaye waliweza kubaini ukweli kuwa
masihi amezaliwa Bethelehemu kama yanenavyo Maandiko Mathayo 2;1-5 ni kupitia
utii wao kwa Maandiko waliweza kujua kweli na hatimaye kumuona masihi kumpenda
kwetu Mungu ni lazima kuambatane na utii makuhani wa kiyahudi walifahamu kuwa
masihi azaliwa wapi lakini hawakuwa na utii hivyo kumuona masihi aliyezaliwa
kwao halikuwa tukio la mvuto Mtu asiyetii aweza hata kuelekeza neno lakini
kwake lisifanye kazi.
SURA YA PILI KANUNI YA UVUVIO
(INSPIRARION)
Mwaka wa 303 BK mtawala wa kirumi
Diocletian aliamuru Biblia zitiwe moto katika ufalme wake hii iliwasumbua sana
wakristo lakini leo Biblia imetefasiriwa katika lugha zipatazo 2000 na
mamilioni ya nakala zinapatikana kote ulimwenguni, kuteseka kwa Biblia
kulitokana na watu wenye mashaka nayo kuwa ni neno la Mungu au imetungwa tu
watu hawa hawakuwa wanaamini kuwa Biblia ina pumzi ya Mungu yaani imevuviwa
Mtu yoyote anayetaka kuingia katika
kazi ya kuitafasiri Biblia lazima aamini kuwa imevuviwa ni lazima ieleweke kuwa
Biblia imeletwa kwetu kupitia uvuvio na ndio maana unaweza kuifikiria kuwa ni
wazo la mtu mmoja ijapokuwa ukweli unabaki kuwa iliandikwa na waandishi wapatao
40 hivi walioishi nyakati tofauti kwa Elimu na nyadhifa tofauti na majukumu na
matazamo tofauti lakini inabeba mamlaka kubwa moja na wazo la ukombozi moja na
ndio mamlaka ya mwisho ya kufaa kwa watu wa Mungu
Maana ya uvuvio
Neno uvuvio maana yake ni Pumzi ya
Mungu Hivyo tunaposema Biblia imevuviwa maana yake ina Pumzi ya uhai wa Mungu
1Timotheo 3;16 neno hilo Pumzi kwa
kiyunani ni Theopneutos “” ambalo halijatumika mahali
popote katika Biblia na wala halitumiki katika Maandiko yoyote ya kiyunani
zaidi ya hapa katika Timotheo nane hilo maana yake “Limetolewa
na Roho wa Mungu” kwa hiyo linamaanisha pia
ni zao la mwisho ambalo Mungu anazungumza na mwanadamu
Uvuvio ni mchakato ambapo Mungu
alipilizia Pumzi yake kupitia waandishi kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kuwawezesha
watu hao kuandika kile alichokikusudia
kuwafikia wanadamu Bila kukosea hivyo haikuwa wanaandika kwa mapenzi yao
bali Roho wa Mungu aliwasukuma kufanya hivyo 2Petro 1;20-21 “Awali ya
yote, yawapasa mjue kwamba hakuna unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama
apendavyo mtu mwenyewe.Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu,
bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”
ROHO MTAKATIFU
NDIYE ALIYEVUVIA MAANDIKO
Maandiko yaani Biblia ni kazi ya Mungu
na Roho Mtakatifu ndiye muhusika mkuu wa usimamizi wa kazi ya maandiko
Umuhimu wa
maandiko
Neno la Mungu lililoandikwa lilihitajika kwa ajili ya wokovu kwa sababu
tunahitaji ujuzi na kweli za wokovu wetu ambao msingi wake ni katika kufa na
kufufuka kwake Yesu Kristo kwani hatuwezi kujiokoa wenyewe kupitia matendo yetu
mema na mawazo yetu mazuri
Mungu ni Mungu aliyetamani
kujifunua kwa wanandamu yeye mwenyewe na ili kazi yake anayoifanya iweze
kujulikana kwa miaka na miaka mpaka wakati huu tulionao leo watu wanahitaji nakala ya yale Mungu
aliyokuwa na ambayo anatenda.Kwa hivyo neno la Mungu ndio njia pekee ambayo kwa
hiyo tunaweza kujua na kuelewa na kuamini kweli kuhusu Mungu na mpango wake kwa
wanadamu na hivyo neno lazima lienezwe Warumi 10;13-17.
Matendo ya Roho
Mtakatifu na Neno lililovuviwa
2Petro 1;20-21Manabii ambao
waliandika neno la Mungu waliongozwa na Roho Mtakatifu walitii na kukubali
kuubeba mpango wake kwa wanadamu wengi walijitambulisha kwa jumbe zao kuwa
zinatoka kwa Mungu Neno kama Neno la Bwana likanijia limetajwa mara 3,800
katika Biblia hii ikijumuisha neno asema Bwana wa majeshi Roho aliwaongoza
katika njia ya moja kwa moja akiwapa wao neno la Mungu
Matendo mengine yalifanywa na watu katika agano la kale kwa uongozi wa Roho
Mtakatifu mfano
·
Gideoni alipiga
tarumbeta baada ya kujiwa na Roho wa Mungu Waamuzi 6;34
·
Samsoni alimchana
mwana simba vipande baada ya kujiwa na Roho Mtakatifu Waamuzi 14;4
·
Sauli aligeuzwa
kuwa mtu mwingine na aliweza kutabiri baada ya kujiwa na Roho wa Mungu 1Samuel
10;6
·
Wanafunzi walinena
kwa lugha baada ya Roho Mtakatifu kuja juu yao Matendo 24; 10;46 19;6.
·
Roho alivuvia watu
kuandika Neno la Mungu- wengi walioandika neno la Mungu hawakufanya hivyo kwa
mapenzi yao walifanya hivyo kwa kuwa Mungu Roho Mtakatifu aliwataka kufanya
hivyo
·
Roho Mtakatifu
hufanya kazi ya kutuangazia au kutufunulia neno la Mungu kusudi tulielewe
vema,Roho Mtakatifu ambaye aliwaongoza waandishi kuandika neno la Mungu hufanya
kazi ya kumuangazia au kumpa ufunuo mtu anayelisoma neno la Mungu akiwa na Moyo
uliovunjika na kutaka kujua humpa ufahamu.tafasiri na namna ya kulitumia neno
hilo kwa usahii kusoma pekee hakuwezi kusaidia kupata ufahamu kuhusu kweli za
kimaandiko 1 Koritho 2;14 Mungu hakumtoa Roho Mtakatifu kwa kusudi tu la
kuongoza waandishi bali pia kwa kusudi la kuangazia neno la Mungu kwetu ili kutimiza kusudi ambalo
Mungu amelikusudia liweze kutimizwa hivyo kuangaziwa au ufunuo hutusaidia
katika kuyaelewa maandiko,kutafasiri na kuyatumia.
Asili ya uvuvio
Ni nini maana ya neno uvuvio? Kwa bahati mbaya si makanisa yote yanakubaliana na wazo la
uvuvio. Kwa miaka mingi sana kumekuweko na hoja mbalimbali na mawazo
mabalimbali yatolewayo kuhusu uvuvio wakati mwingine yana ukweli lakini
yanakuwa magumu kuelezeka.
A: Mawazo mbalimbali
yasiyo sahii sana kuhusu uvuvio
Uvuvio Asili au Ufahamu wa kupita kawaida
intuition theory
Wao huamini kuwa uvuvio ni tendo la kawaida la uwezo wa
kufahamu ulio juu ya viwango vya kawaida wao huamini ni uwezo wa kawaida wa
binadamu kuwa kwa uwezo wa asili anakuwa na viwango vya juu vya ufahamu ambapo
huweza kupata kweli za rohoni.
Udhaifu wa wazo
hili
Hufanya uvuvio wa kibiblia uwe hauna tofauti na maandiko yoyote ya kawaida
yaliyoandikwa kwa viwango vya juu kama yale ya akina Shake speare na nyimbo kuu
za kanisa, Hii inachanganya kati ya kazi za Roho mtakatifu aktika kuvuvia na
kuangazia au kufunulia,Kuangazia hakuhusiani na kuleta kweli mpya bali kuielewa
kweli ambayo tayari imekwisha funuliwa katika neno
Uvuvio wa baadhi ya maandiko tu Partial inspirations
theory
Wao huamini kuwa Mungu alitoa uwezo uliohitajika na wa
kuaminika katika kulileta neno la Kweli la Mungu kwa waandishi walioamriwa
kuandika kwa hivyo iliwafanya wasikosee katika baadhi ya mambo ya imani lakini
si katika mambo mengine mfano waliweza kukosea katika maswala ya kihistoria na
kisayansi
Uvuvio wa mawazo na sio maneno
Wao huamini kuwa Mungu alivuvia wazo la ufunuo fulani lakini aliwaachia
wanadamu hao kuamua kuwa watayaandika vipi. Dhana ya wazo hili si sahii ni
vigumu kufikiri wazo kisha ukaandika tofauti,wazo linaweza kutafasiriwa vizuri
kwa maneno hivyo tunaamini kuwa maneno yalivuviwa na sio swala la mawazo.
Uvuvio
Huria
Hawa huamini kuwa Biblia ina maneno ya Mungu hii ina
maana kwamba pia yako maneno ya kawaida ya watu ambayo yamechanganyika,
wanaamini kuwa ni kitabu hasa cha kidini lakini kuna
Historia,Habari,vizazi,mashairi ya kimapenzi,mipangilio na mambo
yasiyopangiliwa wala kujali mtiririko maalumu au kamili. Dhana hii inataka kuhatarisha kwani ina maana kuwa
waandishi walijiamulia tu wapi waandike wapi ni uvuvio wapi hawakuvuviwa wapi
Mungu anazungumza na wapi mwanadamu anaweka mkono wake
Uvuvio wa Imla
Hawa huamini kuwa
manabii walipopokea uvuvio wa kuandika waliandika moja kwa moja kile ambacho
Mungu alikuwa akikisema hii inamaanisha wao walikuwa kama kalamu tu,Roho
aliwavaa kiasi ambacho hawakuwa na uhuru wao wenyewe isipokuwa kuandika kile
Mungu anachokusudia kwa hivyo huamini
kuwa kila neno lilitoka moja kwa moja kwa Mungu na hivyo wao walifanya kazi
kama mashine tu Dhana hii siyo sahii kwani Mungu alitumia watu na sio mashine
au vifaa,Mungu hakuwafanya wasiwe na ubinadamu wao hivyo si kila kitu
waliandika si kama bomba la kupitishia moja kwa moja kile Mungu alichokisema
lakini waliandika kile ambacho Mungu alikuwa akikiweka katika mioyo yao
B; Mawazo
Mbalimabli sahii kuhusu uvuvio
·
Uvuvio shirikishi-Uvuvio lilikuwa tendo
la Roho Mtakatifu kwa waandishi akifanya kazi pamoja nao na kazi yao ilikuwa ni
kusikiliza na kutii na kuandika
·
Uvuvio ulikuwa ni
muongozo wa Roho mtakatifu kwa waandishi akiwaongoza katika kuchagua nini cha
kuandika na maneno ya kuandika
·
Roho mtakatifu
aliwalinda waandishi kutoka katika kukosea na kuruka uvuvio huu ulihusu kile
kilichoandikwa na haikuwa lazima yawe mawazo au fikra
·
Mungu aliwafanya
waandishi kuwa wafanya kazi pamoja naye
akitumia misamiati yao,mitindo yao ya uandishi na uzoefu wao katika
kuzipeleka kweli
·
Maandiko
yamevuviwa kwa sababu ni matokeo ya kazi ya Roho Mtakartifu kupitia waandishi
yeye aliwaongoza katika kazi nzima ya uandishi ili kwamba kweli ya Mungu iweze
kunukuliwa katika Biblia kama neno kamili la Mungu
C; Kweli halisi
·
Uvuvio ni msingi
wa kuaminika kwa Biblia na hapa tunaizungumzia Biblia yoote
·
Biblia nzima kwani
imevuviwa ni sahihi haina makosa na ni halisi haijatiwa mkono
·
Ni sahii katika
maswala yoote ya kihistoria au kisayansi na maadili na maswala ya mafundisho
kwa wanadamu
·
Ukweli huu ni kwa
maandiko yoote katika Biblia bila kuwekea mipaka baadhi ya mafundisho yake
D; Tafasiri sahii
·
Neno lina mawazo
mbalimbali kuhusu Mungu,Kristo,Msalaba,Ufufuo na ubatizo wa Roho Mtakatifu
·
Ina nukuu halisi
na tafasiri sahii kuhusu kweli nyingi
·
Ndiyo inayotupa
ukweli na muongozo sahii kwa ajili yetu
E; Roho Mtakatifu ni Roho wa kweli na
nguvu.
·
Mungu ni Mungu mkamilifu
na mnyoofu katika njia zake
·
Yesu ni Kweli
·
Roho Mtakatifu ni
Roho wa kweli
·
Kila
kinachozungumzwa katika maandiko kuhusu Mungu,Yesu na Roho Mtakatifu ni cha kweli Biblia inatuambia kweli zote
zinazomuhusu Kristo na Mungu na kile ambacho Yesu alisema kuhusu Roho Mtakatifu
ni halisi Roho anabeba ushahidi huo
Mamlaka Ya Roho
Mtakatifu
Uvuvio unaifanya Biblia kuwa
kitabu pekee ambacho ni muongozo wa kweli wa imani na maisha
Mamlaka ya Biblia
Imefungwa pamoja na mwanadamu
inajua mawazo yake ,dhamiri yake moyo wake na matakwa yake na inamuongoza
katika imani sahihi, aidha Biblia ina njia sahii na muongozo sahii Roho
aliivuvia na analitumia neno kuwa
muongozo wa maisha yetu,Jukumu letu ni kulisoma, kulitafakari na kulitendea
kazi Roho pekee anajua mapenzi kamili ya Mungu na kwa msingi huo anajua ni
namna gani atuongoze na amechagua maandiko yawe Muongozo wetu kwa kuyavuvia.
Andiko huua
Ukitumia akili zako tu kutaka
kuyafahamu maandiko utaharibikiwa wengi wanaofuata yaliyoandikwa tu bila msaada
waRoho Mtakatifu wameishia katika ufarisayo uliokithiri au uhuru usio na mipaka
Msingi wa
Kumtegemea Roho katika Kuyafahamu maandiko
Yesu aliyajua maandiko na alifahamu kuwa yanaongoza lakini alitaka watu
wayafahamu kwa usahii kwa hivyo alileta tafasiri sahihi kwa matumizi ya neno,Roho
Mtakatifu anayajua maandiko na hutusaidia kuichunguza Biblia kupata muongozo
unaohitajika,Hivyo basi tunahitaji msaada wa Roho Mtakatifu katika kuielewa
Biblia vema na kuitii,Tunahitaji kufikiri zaidi ya andiko moja kuelewa lipi
jema na lipi baya
Roho Mtakatifu
hutumia neno.
Baadhi ya watu hujaribu kumfuata Roho Mtakatifu bila kukubaliana na neno au
mamlaka ya Biblia. Kifaa kikuu Roho Mtakatifu anachokitumia katika kutuongoza
ni maandiko yaani Biblia, Neno la Mungu pia huitwa upanga wa Roho kwa hivyo
basi Neno ni silaha ya pekee ya Roho Mtakatifu ni kupitia neno na Roho Mtakatifu
sisi nasi tunaweza kuwa nyenzo yake Roho husimama na neno na hajipingi mwenyewe
Biblia ni nakala iliyovuviwa
Makanisa yote ya Kiinjili yanakubali kuwa Biblia
imevuviwa yote ingawaje inachohitaji ni matumizi mazuri au kuitumia kwa halali
2Timotheo 2;15, hii ni kwa sababu Biblia ina nakala sio tu maneno ya Mungu na mitume na malaika lakini pia kuna maneno
ya shetani wazushi,na hata mapepo,Aidha
Mungu aliona anukuu matukio yote yatakayomfaa mwanadamu mafanikio yake na
kushindwa kwake ufunuo kwa mwanadamu na uongo wa wanadamu waandishi wa biblia
walivuviwa kuweka nakala zote hizo ili kwamba Mungu atusaidie kuelewa nini
kilizungumzwa Kwa mfano Petro alisema Hata kama wote watakukana mimi
sitakukana kamwe Mathayo 26;33 usemi huu
umevuviwa jibu ni ndio na sio ndio ni kwa sababu Roho alimvuvia mathayo
kuliweka kwa ajili yetu ili kwamba
tujifunze kupitia makosa ya Petro kwa hivyo Mathayo 26;33 imevuviwa na ni kweli Petro alisema ingawaje Petro
mwenyewe hakuwa amevuviwa kusema hayo alichokisema ni uongo Yesu alitaka kumsaidia Petro kuhusu ujasiri
wake na kujiamini katika kile alichokisema
lakini Petro hakuweza kuona kiburi cha kujiamini kwake alichokuwa nacho
kwa hivyo kunukuliwa kwa usemi huu wa petro
kumevuviwa ingawaje usemi wenyewe ni uongo
Kuvuviwa kunaifanya Biblia yote iwe
·
Inafaa kwa
Mafundisho na kusahihisha na kumfanya
mtu wa Mungu awe kamili apate kukamilishwa kwa kutenda kila tendo jema
2Timotheo 3;16
·
Inafaa kwa huduma
Warumi 15;4 hii ikiwemo agano la kale
·
Inafaa kwa
mafundisho na kwa matumizi ya mtu binafsi
Pamoja na sababu hizo za msingi hapo juu na ujuzi kuwa
neno la Mungu klimeviviwa bado hatuwezi kutumika kila andiko vyovyo te
tutakavyo maandiko yana faa kwa mafundisho lakini pia si kila andiko linafaa
kwa mafundisho hivyo tunapaswa kuwa makini katika matumizi ya maandiko kwa
mfano Nyaraka nyingi ziliandikwa kwa kusudi la kufundisha lakini ukitoa salamu,maswala
binafsi ya waandishi,na tamaduni zisizoweza kuhamishika kwetu mengi ya
yanayobaki hutusaidia kwa ajili ya mafundisho na tunapata mafundisho mengi
katika nyaraka kwa kuwa hutafasiri injili kwetu
1Petro 5;14, Salimianeni kwa Busu takatifu kwanini hatuwezi
kujenga fudnisho katika andiko hili?
Injili na kitabu cha matendo viliandikwa kwa kusudi la
kutupa sisi historia kuliko mafundisho ingawaje yako mafundisho tunayoweza
kuyapata kutoka katika yale aliyoyafundisha Yesu na mitume ingawaje bado
inatupasa kuwa makini ili tusitunge mafundisho yaliyolalia kwenye historia
Kwa mfano huwezi kuweka Fundisho katika Marko 11;2,
kuhusu kumfungua mwana punda asiyepandwa bado pia Mathayo 10;9,Yohana 21;18
Matendo 4;32-33 karibu maandiko yote hayo hapo juu hayajajirudia na hivyo
huwezi kutengeneza fundisho
Angalia Mtu anayetumia andiko moja lenye utata kufanya
fundisho hawezi kuwa salama kama anayetumia maandiko yenye ushahidi huyo
anakuwa kama aliyekalia stuli yenye miguu minne ukitumia nadiko moja imekula
kwako! na nirahizi kuanguka lakini ukikalia ya miguu minne uko salama
KUNOA UPANGA
KANUNI YA KUFAHAMU HISTORIA YA ANDIKO
(CONTEXT)
A. Ni ni maana ya historia ya andiko?
Neno kufahamu historia ya andiko
limetokana na neno la kilatini Context ambalo ni muungano wa Maneno mawili
“Con” na “Textus” ambalo maana yake ni weave together yaani kukusanya pamoja
maana ya kila andiko au mstari aya kulingana na historia yake ya nyuma na
mazingira ya kawaida
Historia ya andiko yaani Historical
context inahusu mambo ya muhimu na msingi kuhusu mazingira ambayo kwayo andiko
linatokea kwa msingi huo ili mtu aweze kuwa mtafasiri mzuri wa andiko au
Maandiko anapaswa kuijua historia ya Maandiko hayo aelewe mambo muhimu ya
msingi yafuatayo
·
Mwandishi na wakati au tarehe ya
uandishi
·
Watu aliokuwa akiwaandikia ni akina
nani
·
Tamaduni zao zilikuwaje na desturi zao
zilikuwaje
·
Mwandishi alikuwa akishughulikia tatizo
gani
Huwezi kumchunguza kanga na kumuelewa
kupitia unyoya wake mmoja tu itakupasa kuwa na kanga mzima ili kuweza kumuelewa
vema kwa msingi huo huwezi kulielewa vizuri andiko bila kujua limetokea katika
historia gani
B. Namna ya kuchunguza Historia ya andiko
Kwa ujumla tunasema kuwa kutafasiri
Vitabu vya Nyaraka ndio swala gumu zaidi kuliko kutafasiri vitabu vya Injili na
kitabu cha Matendo ya mitume kwa msingi huo tutaangalia zaidi namna ya
kutafasiri nyaraka ingawaje pia huko mbele tutashughulikia swala la kutafasiri
Unabii kwani nalo pia ni swala gumu, Ni muhimu kufahamu kuwa kuna hatua kuu
tatu za kuchunguza historia ya andiko na swala hili sio jepesi ni swala gumu
mambo ya msingi unayopaswa kujiuliza ni pamoja na
1. Jiulize
kuhusu Mwandishi
·
Ni nani
·
Aliandika lini
2. Jiulize
kuhusu walengwa waandikiwa
·
Ni akina nani?
·
Walioishi katika mji gani na mji huo
ulikuaje?
·
Walikuwa watu wa jamii gani wayahudi au
mataifa na hali zao zilikuwa za namna gani matajiri au masikini
·
Wana uhusiano gani na Mwandishi
3. Chunguza
ni tatizo gani Mwandishi alikuwa anajaribu kulitatua kupitia kitabu chake
·
Tatizo siku zote litakusaidia kujua
kiini cha Mwandishi na kitaakisi waraka mzima au kitabu husika
Kwa mfano ni namna gani tunaweza kujua
historia ya Maandiko katika 1Wakoritho?
1.
Kuhusu Mwandishi
·
Alikuwa ni nani jibu ni Paulo mtume
·
Aliandika 1Koritho kati ya Mwaka wa 56
B.K hii ni baada ya Kuweko pale Efeso kwa miaka mitatu Matendo 20;31 Ikorotho
16;5-8
2.
Walengwa wa waraka huu ni
·
Wale waliomwamini Mungu huko Koritho
·
Koritho ulikuwa mji wa bandari katika
bahari ya mediteranian na ni mji uliokuwa unakaliwa na jamii ya wapagani na
ulikuwa maarufu kwa kuabudu miungu na tabia za uasherati na uchafu wa kingono.
·
Hali ya mji wa koritho ulikuwa ni
mchanganyiko wa wayahudi wachache na wayunani wengi 1Korittho 6;9-11,8;10,12;13
na watu wake walipenda Hekima na maarifa 1;18-2;5,4;10,8;1-13 na walikuwa watu
wa kujivuna sana
·
Mwandishi ndiye aliyewahubiri injili
Matendo 18;1-18
3.
Matatizo aliyokuwa akijaribu kuyatatua
Mwandishi kupitia kitabu chake ni
Ø
Kulikuwa na Faraka na migawanyiko
1Koritho 1;10-4;21
Ø
Kulikuwa na zinaa isiyokuwa ya kawaida
5;1-13
Ø
Kulikuwa na maswala ya wakristo
Kushitakiana mahakamani 6;1-11
Ø
Kulikuwa na matatizo ya uasherati watu walikua
wakifanya zinaa 6;1-11
Ø
Kulikuwa na tabia mbaya katika maswala
ya ndoa 7;1-24
Ø
Kulikuwa na tatizo kuhusu wanawali
7;25-40
Ø
Kulikuwa na tatizo la vitu
vilivyotolewa sadaka kwa sanamu 8;1-11;1
Ø
Kulikuwa na tatizo la wanawake
kutokuvaa Vilemba 11;2-16
Ø
Kulikuwa na matumizi mabaya ya meza ya
bwana 11;17-34
Ø
Kulikuwa na matumizi mabaya ya karama
za rohoni 12;1-14;40
Ø
Kulikuwa na mafundisho potofu kuhusu
Ufufuo 15;1-58
Ø
Swala la kuwasaidia masikini huko
Yerusalem 16;1-11
Wapenzi Biblia ni neno la Mungu
tunapaswa kulisoma na kulitii wako watu wanaosema kuwa unahitaji kuisoma na
kuitii tu na wala usiitafasiri hii ni sawa lakini ni uongo kwani kila mtu
hutafasiri kwa asili kile anachokisoma unaposoma andiko unajaribu kujua kuwa
Mwandishi alikuwa anamaanisha nini? Kule kujiuliza ili uweze kuelewa ndio
kutafasiri kwenyewe
Biblia ni neno la Mungu limetolewa kwa
wanadamu katika nyakati tofauti kwa historia tofauti kwa kuwa Mungu amechagua
kuzungumzia na wanadamu kwa Neno lake alizungumza na mwanadamu halisi lakini
kwa wakati halisi, kwa Matukio halisi, kwa historia halisi kwa hivyo lazima
litafasiriwe kwani neno limekuja kwa tamaduni tofauti na vizazi tofauti na ndio
maana ndani ya Biblia kuna Mashairi, Mithali, Nyakati, Mifano, Hadithi, Sheria,
Unabii, Nyaraka, injili na maswala ya Ufunuo.
Mungu alikusudia tuelewe katika lugha zetu na mazingira yetu
Na anazungumza nasi kwa namna
mbalimbali katika nyaraka utagundua kuwa nyaraka nyingi ni OCCASIONAL yaani zimetokana na Matukio fulani
kwa asili kwa hivyo ziliandikwa kwa sababu ya msukumo fulani aidha kutoka kwa
walengwa au Mwandishi kwa hivyo ni lazima ujue
·
Kwanza Historia ya wakati ule ilikuwaje There and then
·
Tatizo au mazingira na kujiuliza
Mwandishi alimaanisha nini alipokuwa akijibu hoja za wakati ule then and there
·
Kile alichokuwa akikijibu Mwandishi ni
neno la Mungu kwa watu wa wakati ule na kwa wahusika halisi wa wakati ule
·
Je wakati huu sasa Mungu ansema nini
nasi? Here and Now kwa hivyo leo tunatumiaje lile neno katika wakati wetu hapa
ndipo Hermeneutics inapotenda kazi
Kama hili halina umuhimu basi Hebu
jaribu kuwaza wale wafanya kazi katika Mathayo 20;1-16 waliolipwa Dinari kama
mshahara wa kutwa wa kazi je leo hii
tutalipwaje kwa Siku kwa hivyo ni muhimu
kujua Historia ya kila kitabu na sababu kwanini kiliandikwa
Tafasiri kwa kuzingatia pia mazingira
ya aya husika Literal context
Mazingira ya andiko au aya ni mazingira
ambayo yanalizunguka andiko unalotaka kulifasiri mara nyingi Maandiko hayo huwa
na Vifungu vya Maneno na sura kwa hivyo kumbuka kuwa vifungu ni sehemu ya sura
na sura ni sehemu ya kitabu na kitabu ni sehemu ya Biblia kwa msingi huo
unapolichukua andiko tu na lifasiri bila kuzingatia mazingira yake unaweza
kusababisha madhara ni kama kunyofoa uzi katika gauni unaweza kuharibu vyote
gauni na nyuzi pia kwa sababu vyote kwa pamoja ndio hufanya gauni.
Andiko linapochukuliwa pekee nje ya
mazingira husika ni silaha ya shetani na ameitumia kudanganyia wakristo wengi
angalia Mathayo 4;5-6 hapa shetani aliitumia Zaburi ya 91;11-12ambayo inasema
hivi “Kwa kuwa atawaagiza malaika zake kwa ajili yako, wakulinde katika njia
zako zote. Mikononi mwao atakuinua juu, ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.
Sasa kuna namna tano za kuchunguza mazingira
ya andiko
1. Jiulize kuwa
andiko unalolisoma limetokea kitabu gani na nini somo kuu la kitabu hicho
2. Jiulize andiko
unalolitumia linatoka kifungu gani?
·
Ni Maandiko mangapi kifungu hicho kinayaweka pamoja?
·
Chini ya kifungo hicho kuna somo gani?
·
Je kile unachotaka kukihubiri ndicho kinaelezwa na vifungu
hivyo?au na wazo zima la kitabu?
3. Jiulize pia
kuhusu vifungu vidogo katika mazingira ya andiko husika
·
Kuna hali gani au ahadi gani
·
Kuna tatizo au suluhisho lielezee
·
Kama kuna mfano nini maana kuu ya mfano huo
4. Fupisha kifungu
kizima kwa Maneno yako mwenyewe katika sentensi moja kwa kila kifungo
5. Jiulize mtu
anapoyatumia Maandiko hayo je kuna
·
Maneno halisi ya andiko husika eleza
·
Mwandishi alimaanisha nini katika migawanyo husika
·
Kitabu kilimaanisha nini
Mfano sasa Zaburi ya 91; 11-12
Zaburi nyingine zina waandishi na zina
Matukio fulani lakini Zaburi ya 91 hijulikani Mwandishi hivyo tutaendelea
1. Kiini kikuu cha
zaburi ni Kusifu na kumuabudu Mungu
2. Zaburi hii ina
mistari yake inatoka katika kifungo cha mstari wa 1-16
·
Zaburi 91;1-16
·
Somo ni kuhusu ulinzi wa Mungu
·
Wazo zima la kitabu ni kumsifu Mungu na zaburi hii
inasisitiza sababu maalaumu za kumsifu
Mungu
3. Mazingira ya
andiko husika yako hivi
·
Kuna ahadi lakini ina neno kama kwa hivyo kuna ahadi za
ulinzi wa Mungu lakini kama mtu ataendelea kukaa na Mungu
·
Tatizo lililoko ni hatari katika maisha kuna nyoka, mitego,
wapiga mishale lakini suluhisho lake ni ulinzi wa Mungu Zaburi 91;1-2,9
·
Kuna mfano wa kuku anavyofunika vifaranga vyake vifaranga
hupata pa kukimbilia lakini kama tukikaa kwake tunayo makimbilio
4. Kwa ufupi wale
wanao mwamini Mungu na kukaa ndani yake hawataogopa wakati wa mabaya Bwana
atakuwa ulinzi wao na kimbilio lao
5. Maneno halisi
ya andiko husika
·
Shetani aliruka neno kukulinda katika njia zako zote
·
Mwandishi alimaanisha katika mapito yetu yote hivyo
kujirusha kutoka katika kinara cha hekalu sio kulindwa katika mapito yetu yote
·
Kusudi kuu la kitabu ni kumsifu Mungu je unafikiri kujirusha
kutoka katika kinara ndio kusudi la kitabu?
·
Kwa hivyo shetani hakutumia Maandiko kwa halali na hivyo
alitaka kumtia Yesu katika mazingira ya kumjaribu Mungu.
KANUNI YA KUCHUNGUZA MAANA YA ANDIKO NA
MAMBO YALIYOMO NDANI YAKE (CONTENT)
A.
Umuhimu
wa kuchunguza kilichomo ndani ya andiko unalolitafasiri
Kanuni ya kuchunguza maana ya andiko na kile kilichomo ni kanuni ya msingi
sana wakati wa Yesu Kristo Duniani mwishoni mwa huduma yake aliwahi kukaririwa
vibaya na wanafunzi wake na uongo ukawa duniani kwa karibu zaidi ya miaka 40
hivi uongo huo ulivumishwa kutokana na Yohana 21;21-23 ambapo inasemekana kuwa
baadhi ya wanafunzi walifikiri kuwa Yesu alimwambia Yohana ya kuwa hatakufa
maandiko haya husema hivi;- ” Petro alipomwona huyo
mwanafunzi, akamwuliza Yesu, “Bwana na huyu je?’’ Yesu akamjibu, “Ikiwa nataka
aishi mpaka nitakaporudi, inakuhusu nini? Wewe inakupasa unifuate!’’ Kwa sababu
ya maneno haya ya Yesu, uvumi ukaenea miongoni mwa ndugu kwamba huyu mwanafunzi
hangekufa. Lakini Yesu hakusema kuwa hangekufa. Yeye alisema tu kwamba,“Ikiwa
nataka aishi mpaka nitakaporudi, imekupasaje wewe?’’
Hatuna shaka kuwa wanafunzi walikuwa watu waaminifu hata pamoja na
kusambaza uvumi kuwa Yohana hatakufa lakini uaminifu pekee hautoshi katika
kuzuia uongo usisambae kwa msingi huo Maandiko yasipotafasiriwa kwa kuzingatia
kanuni zake uaminifu pekee pia hautoshi kuzuia kuenea kwa uongo
Wasomi wanaamini kuwa injili ya Yohana ndiyo ya mwisho kuandikwa na
iliandikwa baada ya miaka 40 hivi na ndipo Yohana alipoweza kuitumia nafasi
hiyo kuelezea kweli kuwa Yesu hakumaanisha kuwa yeye hatokufa kwa hivyo unaweza
kuona athari ya uongo wa dhambi ya kutafasiri Maandiko vibaya inavyoweza
kuchukua miaka na kuleta athari mbalimbali kwa msingi huo basi ni lazima mtafasiri
wa Maandiko azingatie nini kimo ndani ya andiko analotaka kulitafasiri
B.
Chunguza
mamneno yaliyomo ndani ya andiko unalotaka kulihubiri
Kwa kawaida kuna sheria kuu tatu za
kuweka akilini kila unapotaka kutafasiri Maandiko hapa tunamaanisha ni lazima utafute
maana ya kila neno unalokutana nalo katika sentensi husika na uchunguzi lina
uhusiano gani na mangineyo hii itatusaidia tusiharibu mambo kama ilivyokuwa kwa
wanafunzi wa nyakati za kanisa la kwanza waliovumisha kuwa Yohana hatokufa kwa
sababu walitafasiri vibaya alichokisema Bwana Yesu.
1. Chunguza Neno
unalojua kuwa hulijui
Unaposoma Maandiko unaweza kukutana na
neno ambalo hulijui hii peke yake ni kama Tahadhari inayokuambia kuwa hakuna
daraja mbele na hivyo unapoendelea na safari basi utapata ajali Simama na
zingatia kwanza kutafuta maana ya neno usillolijua liangalie linasomeka vipi
katika matoleo mengine ya Biblia au fuatilia katika Kamusi unapojaribu kuliruka
neno ambalo hujalifahamu basi nakuhakikishia kuwa utatafasiri vibaya Maandiko
2. Chunguza Neno
unalofikiri kuwa unalijua
Wakati mwingine kuna neno ambalo unadhani
kuwa unalijua kabisa pia unapaswa kulichunguza
kwa sababu kuna uwezekano ukawa hulijui au limetumika tofauti na
unavyofikiri kwa mfano wote tunajua neno Imani vema si ndivyo sasa jiulize
limetumikaje katika Warumi 14; 23 na Wagalatia 1;23 Hapo utagundua kuwa neno
imani lile unalolijua hapo limetumika vinginevyo kati ya Warumi na Wagalatia
3. Jiulize swali
linalokusukuma kutafasiri Maandiko na kisha tumia kile ulichogundua
Je umewahi kusoma kifungo cha Maneno kisha
ukajikuta unakirudia tena kwa sababu ulikuwa hujafikiri? Kumbe inawezekana mtu
kusoma kisha asielewe? Msomi mzuri wakati wote hujiuliza swali kuwa jambo hili
lina maana gani? Kisha husoma tena ili kuona kama umeelewa vizuri
Kwa mfano sasa Tuchunguze Yohana
21;21-23
Yesu alisema nini? Kimsingi alikuwa
akimweleza Petro kile ambacho kingempata mwishoni mwa huduma yake na kumtabiria
mauti yake itakavyokuwa lakini kama ilivyo desturi ya wanadamu tunapenda sana
kujua na mambo ya wengine Hivyo Petro aliuliza Je kuhusu Yohana itakuwaje? Yesu
hakutaka kumpa Petro faida ya kujua maswala ya wengine hivyo alimjibu Hata kama
au hata ikiwa nataka huyu aishi hata nitakaporudi wewe inakuhusu nini? Kimsingi
Yesu alivunja moyo hali ya kupenda kujua mambo ya wengine au mipango ya Mungu
juu ya mtu mwingine wewe pokea kile Mungu alichokujalia na sio kutafuta mwisho
wa wengine utakuwaje? Unaona Kumbe Maandiko yasiposomwa vema yanaweza kupotosha
maana iliyokusudiwa
Chukua mazoezi fuatilia maana za meneno
haya
-
Mwanzo 30;14 Tunguja
-
Wagalatia 4;6 Abba
-
Mathayo 25;14-30 Talanta
-
Marko 5;41 Talitha koumi
-
Marko 7;34 Ephatha
-
Marko 15;34 Eloi, Eloi lama Sabachatani?
Ni muhimu sana Kufahamu kile unachotaka
kukihubiri kwani kuna tofauti ya kusoma
na kufahamu au kusikia na kufahamu Maroko 7;14 Yesu alisema “Nisikieni nyote na Kufahamu” kusikia na
kufahamu ni maswala mawili tofauti wote tunajua kuwa katika mazingira haya
ndipo Yesu alipotakasa vyakula Vyote na tunajua kuwa Petro alisikia lakini je
alielewa alifahamu? Matendo 10;9-16 Petro hakuweza kufahamu kile Yesu alikisema
katika Marko 7;14-19.
Mfano
mwingine;-
Watu wengi wamehubiri kuhusu njaa iliyoikumba Samaria 2Wafalme 6; 25
ambapo Biblia inasema hivi
“Njaa ikawa kuu huko Samaria; na tazama
wakauhusuru hata kichwa cha punda kikapata kuuzwa kwa vipande themanini vya
Fedha na kibaba cha mavi ya njiwa
kwa vipande vitano vya Fedha” watu wengi wamehubiri kuwa mavi ya njiwa yaliuzwa
je umawahi kujiuliza kuwa ni katika tamaduni gani watu hula mavi ya njiwa? Neno
mavi ya njiwa ni neno geni lazima ujiulize lina maana gani kabla ya kuhubiri!
Kibaba cha mavi ya njiwa Biblia ya RSV
Revised Standard Version inasema fourth
part of a Kab of doves dung
Biblia ya NIV New International Version
inasema a Cab of seeds ambapo kwa
lugha nyepesi kumbe Biblia inazungu mzia robo ya kibakuli cha mbegu RSV na NIV
ni Kibakuli cha mbegu kibakuli hicho cha mbegu ndio kiliitwa Kibaba cha mavi ya
njiwa kwa msingi huo unaweza kuona kuwa kutokuzingatia Maneno ndani ya kile
unachokisoma kunaweza kabisa kusababisha upotofu wa maana halisi iliyokusudiwa
Mathayo 24;28 “ Kwakuwa popote ulipo mzoga ndipo watakapokusanyika tai”
Yesu alisema mfano huu au usemi huu katika mazingira ya unabii unaohusu kuja
kwake mara ya pili duniani kwamba kimsingi ujio wa Yesu mara ya pili duniani
hautakuwa wa kificho kwani utaambatana na kuuawa kwa maadui wa masihi na taifa
la Israel jeshi hilo la mpinga Kristo watauawa kwa maelfu yao na kukosa wa
kuwazika kwa hivyo miili yao itakuwa chakula cha tai ni katika mazingira kama hayo
Yesu anatamka neno kwa kuwa popote ulipo mzoga ndipo watakapo kutanika
tai.unaona!
Mathayo 11;12 ‘Tangu siku za Yohana
mbatizaji hata sasa ufalme wa Mungu unapatikana kwa nguvu nao wenye nguvu
wauteka”Nyakati za Kristo na Yohana mbatizaji kulikuwako na makundi ya wana
mapinduzi waliojulikana kama Zealots au mazerote hawa walikuwa na nia ya kuleta
mapinduzi ili kuhakikisha kuwa Israel inajitawala na kuwa na ufalme wao wenyewe
kwa nia ya kijeshi walikuwa na Shauku kubwa wivu mkuu Yesu alimtumia shauku
waliyokuwa nayo wana mapinduzi hao na kuioanisha na mtu yeyote yule anayetaka
kupata ufalme wa Mungu kwamba hata kama ni kwa gharama ya kimapinduzi ufalme
upatikane watu wenye shauku hiyo wanaweza kupata ufalme wa Mungu.
Nyenzo
za kuzingatia
Kama tulivyoona kuwa kumbe basi ili mtu
aweze kuwa Mtafasiri mzuri wa Maandiko katika viwango vya juu anahitaji Nyenzo
za viwango vya juu vitakavyoweza kumsaidia na nyingi ya nyenzo hizo ziko nje ya
Biblia yenyewe hii ina maana gani ninakukumbusha ya kuwa unahitaji kuwa na
Matoleo mabalimbali ya Biblia,unahitaji Kamusi za Biblia,unahitaji mafafanuzi
Commentary nzuri za Biblia,na nyenzo nyingine zitakazoweza kukusaidia katika
usomaji wako wa Biblia na pia ni muhimu kuisoma Biblia yenyewe kitabu kwa
kitabu kila mara kwani nayo ni silaha nzuri lakini zaidi sana tafuta Biblia
inayosadikiwa kuwa na tafasiri nzuri ziko nyingi lakini inatakiwa ile
inayotafasiri maana iliyokusudiwa katika Lugha halisia kinyume cha hapo basi
lazima ukubali kujifunza Lugha ya kiyunani na kiibrania zitakusaidia katika
kujisomea moja kwa moja na kupata maana halisi zilizokusudiwa
Kumbuka! Msomi mzuri wakati wote hujiuliza swali kuwa
jambo hili lina maana gani?
KANUNI YA KUCHUKUA ANDIKO KAMA LILIVYO RAHISISHA.(SIMPLICITY)
Kanuni hii inahusu kutafasiri andiko kwa
kurahisisha kama lilivyo bila kujaribu kutafuta maana kwamba hili ni fumbo au
bila kujali lugha iliyotumika kuwa ni ya namna gani Kanuni hii inaruhusiwa kwa
sababu Mungu alikusudia Maandiko yaweze kueleweka kwa kila Mtu na Mungu anataka
ajifunue kwa watu hivyo alitupa Biblia kwa msingi huo kusudi la Biblia liko
wazi na ni kuweka wazi kweli zote na sio kuwachanganya watu wala Maandiko sio
mkusanyiko wa mafumbo na siri ni ujumbe wa Mungu kwa watu wake kwa hivyo
unapoitafasiri Biblia tafuta maana nyepesi ya asili na itumie lakini yako mambo
ya msingi unapaswa kuyazingatia
1. Kuhusu Lugha ya kawaida
Lugha ya kawaida iko wazi katika maisha
yetu ya kila siku wala hatuna mafumbo katika maisha yetu ya kila siku kila kitu
kikowazi na kimenyooka angalia kwa mfano katika Maandiko haya Matendo 20;7-12
“Siku ya kwanza
ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. Paulo akaongea na watu,
naye kwa kuwa alikuwa amekusudia kuondoka kesho yake, aliendelea kuongea mpaka
usiku wa manane. Kwenye chumba cha ghorofani walikokuwa wamekutania kilikuwa na
taa nyingi. Kijana mmoja jina lake Eutiko, aliyekuwa amekaa dirishani, wakati
Paulo alipokuwa akiendelea kuhubiri kwa muda mrefu, alipatwa na usingizi mzito,
akaanguka kutoka ghorofa ya tatu, wakamwinua akiwa amekufa. Paulo akashuka
chini, akajitupa juu ya yule kijana na kumkumbatia, akasema, “Msishtuke, uzima
wake bado umo ndani yake.” Kisha Paulo akapanda tena ghorofani, akamega mkate
na kula. Baada ya kuongea mpaka mapambazuko, akaondoka. Watu wakamrudisha yule
kijana nyumbani akiwa hai nao wakafarijika sana.”
Katika kifungo kama hiki lugha ni ya
kawaida na hakuna mafumbo yoyote kwa msingi huo ni dhambi kuanza kufikiri kuwa
kuna mafumbo usianze kufikiri kuwa kuna maana ya Neno usiku, ghorofa, na
dirisha na Eutiko mwenyewe ukafikiri kuwa kukaa karibu na dirisha ni mkristo
kukaa karibu na dhambi kusinzia ni kutokuwa makini na mafundisho na hatimaye
anguko likatokea na kifo cha kiroho hapohapo! Hii haitakuwa maana sahii ya
Maandiko haya kwani yako wazi hivyo ulitakiwa kuchukua maana Rahisi tu
Rahisisha!
Ni muhimu kufahamu kuwa katika maisha
ya kawaida mafumbo hayatumiki sana kwa mfano kama mtu ametoka Tanzania akaruka
na ndege kwenda Ulaya akaivuka bahari ya Hindi anapotoa taarifa hiyo mtu huyu
haimaanishi kuwa anazungumza fumbo wala haimaanishi kuwa amekwenda katika inchi
ya ahadi kwa msingi huo ni muhimu kufahamu kuwa si mara zote basi Biblia
inamaanisha mafumbo wakati mwingi na sehemu nyingi iko wazi kabisa
Tahadhari
Msingi wa kanuni hii ni kulinda kile
ambacho kimewahi kutokea miaka mingi kabla ya Kuzaliwa kwa Masihi walikuweko
watu waliopenda kutafasiri Maandiko kiroho “Spiritualizing of a text” na katika historia ya aknisa jamii hizi
zilikuweko watu hao ambao hupenda kutafasiri Maandiko Kiroho walitumia njia
iitwayo “allegory”njia hizi zilikuja
kusaidika baada ya wasomi kama Martin Luther na John Calvin ambao walisisitiza kuwa
maana ya Maandiko ni wazi kabisa kuwa ni ile iliyokusudiwa na andiko kwa hivyo
Mtindo wa kutafasirti Maandiko kiroho ni moja ya dhambi mbaya za watafasiri wa
Maandiko hii ni hatari sana kwa sababu unapokataa maana halisi iliyokusudiwa na
andiko unakataa neno la Mungu na unapohubiri maswala hayo unahubiri kisicho
neno la Mungu kwa hivyo unahubiri vitu vya kufikirika tu na hivyo Baraka za
Mungu nje ya neno lake haziwezi kumiminika kwetu
Angalia mfaono wa andiko hili siku Yesu
alipoingia Yerusalem kwa shangwe Mathayo 21;5 Biblia inasema “Mwambieni Binti
Sayuni, ‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako, ni mnyenyekevu, naye amepanda
punda, juu ya mwanapunda, mtoto wa punda.’
Watu wanao tafasiri kiroho wanaweza kudhani
kuwa Punda anawakilisha Gari basi au shangingi lakini Punda hawakilishi
chochote hapa ametajwa punda kwa sababu Yesu alimpanda hapa! Hakuna neno la
ndani lililojificha kuhusu Punda hapa! Msingi wa andiko hili ni kutimizwa kwa
agano la kale kuhusu unabii wa Yesu kumpanda Punda kwa hivyo andiko hilo
halihitaji ufafanuzi wowote linatakiwa lichukuliwe kwa maana rahisi na ya
kawaida
Hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa
tunachukua maana rahisi ya kawaida katika Maandiko ambayo yako kawaida ambayo
yakitafasiriwa kawaida yanaleta maana hii haimaanishi kuwa hakuna Maandiko
yasiyohitaji kujua maana yake yako na tunayashughulikia sehemu ifuatayo
Ufahamu
kuhusu Lugha za Mafumbo
Hapo juu tumesisistiza kuhusu
kuichukulia Biblia katika maana ya kawaida na rahisi lakini ni muhimu
kuzingatia pia kuwa iko mistari ambayo huwezi kuichukulia kirahisi kwani ni
lazima ufahamu kuwa iko katika lugha za kifumbo kama tulivyoona kuwa mtu
anaweza kutafasiri fumbo katika eneo ambalo linapaswa kuchukuliwa kirahisi na kikawaida
hali kadhalika mtu huweza kufanya makosa kwa kutokuzingatia lugha hizi za
mafumbo
Kwa mfano nikodemo hakuweza kumwelewa Yesu
pale alipochukulia Maneno ya Yesu kuhusu Kuzaliwa mara ya pili kama tafasiri
rahisi na ya kawaida na kumbe Yesu hapa alimtumia lugha ya fumbo Yohana 3;3-4
“Yesu akamjibu, “Amin, amin nakuambia, mtu
hawezi kuuona Ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.’’ Nikodemo akauliza,
“Awezeje mtu kuzaliwa wakati akiwa mzee? ‘‘Hakika hawezi kuingia mara ya pili
kwenye tumbo la mama yake ili azaliwe!”
Hapo Nikodemo alitaka kutumia namna rahisi na ya kawaida kutafasiri alilolisema
Yesu lakini Yesu alimtumia Fumbo
Mwanamke msamaria pia alifanya kama
Nikodemo alichukua Maneno ya Yesu kama kawaida na katika namna rahisi kumbe
Yesu alizungumza Lugha ya fumbo Yohana 4;10-11
“Yesu akajibu akamwambia, ‘‘Kama
ungelijua karama ya Mungu, naye ni nani anayekuambia, Nipe maji ninywe, wewe
ungelimwomba Yeye, naye angelikupa maji yaliyo hai.’’Yule mwanamke akamjibu,
“Bwana, Wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji
ya uzima utayapata wapi?”
Hapa pia Mwanamke msamaria alichukua Maneno
ya Bwana Yesu katika namna ya kawaida hakujua kuwa Yesu alizungumza lugha ya
Fumbo
Kumbe basi baadhi ya Maandiko ni wazi
kuwa yako wazi na unaweza kuyachukulia kwa urahisi na kwa njia ya kawaida
lakini mengine ni mafumbo na unapaswa kuyatafasiri
Inasemekana nyakati za Martin Luther
mzozo wa kitheolojia ulitokea kuhusu andiko la kula mwili wa Yesu na kunywa
damu yake Mathayo 26;26 kwa sababu Lutha
alikua akikazia swala la kuchukua andiko kama lilivyo walimletea kisu
Mezani ili ajikate naye waweze kuliwa
kumbe si kila andiko linapaswa kuchukuliwa kama lilivyo Hebu angalia Maandiko
yafuatayo na jiulize kama yangechukuliwa kama yalivuyo leo tunagekuwa na
wakristo wa namna gani?
1. Mathayo 5;29
jicho lako lakuume likikukosesha ling’oe………………..
2. Mathayo 5;30 Na
mkono wako wa kuume ukikukosesha………………
Aina
mbali mbali za Lugha za Mafumbo
Kuna aina mbalimbali za Lugha za mafumbo
zinzotumika katika Biblia inasemekana ziko lugha za mafumbo zilizotumika katika
Biblia zaidi ya 200 pamoja na mifano yake ipatayo 800 lugha hizo za mafumbo ni
kama vile kama vile
·
Mifano na fumbo la maneno
(Parable and allegories)
·
Ulinganisho unaotumia maneno
kama, na na ulinganishi usiotumia
neno kama na (Similes and Metaphors)
·
Maneno ya kuongoza chumvi (Hyperboles)
·
Maneno ya kuhuisha au kukipa kitu au mnyama uhai au
ubinadamu ( Personification)
·
Kumliganisha Mungu na mwanadamu (Antropomorphism)
·
Jina moja kwa niaba ya linguine (Metonymy)
·
Sehemu moja kwa jambo lote au Sehemu nzima kwa sehemu (synecdoche)
·
Kuzungumza kinyume cha uhalisia ( Irony)
·
Lugha za mficho inayotumika badala ya neno chafu Figurative
language au (Euphemism )
·
Misamiati au Maneno magumu au Mithali na misemo
A.
MIFANO NA FUMBO
LA MANENO (PARABLE AND ALLEGORIES)
Moja ya njia kubwa sana alizotumia Yesu
kufundishia ni stori na mifano hizi ni hadithi fupi ambazo kwa kawaida hubeba
maana moja ya kiroho au somo moja maalumu ndani ya hadithi hizo kunauchambuzi
unaotolewa kwa kusudi tu la kufikisha ukweli uluiokusudiwa, kwa mfano katika
mfano wa msamaria kuna ukweli mmoja tu katika mfano huo Yesu alikuwa akijibu
swalai Jirani yangu ni nani? Kuna mambo mengi ndani ya mfano huo ambayo
hayapaswi kuchambuliwa na katika fumbo
la Maneno Allegories au kisa kilichofichwa kuna weza kukawako na kweli nyingi
mafano ni Yohana 10, “Yesu anaposema
Mimi ndimi Mchungaji mwema” hapa unaweza kupata mambo mengi kuhusu
Mchungaji,kondoo, mwivi, mgeni, kukodisha, mbwa mwitu, Tunawezaje kujua kuwa
huu ni mafano na haya ni fumbo la Maneno mara nyingi utaweza kuona kuwa Yesu
mwenyewe alitafasiri maana aliyoikusudia na kama hukufanya hivyo basi tunapaswa
kuchukua kama mfano au lugha ya mafumbo hata hivyo tutashughulikia swala hili
katika kanuni maalumu ya kutafasiri mifano huko mbele
B.
ULINGANISHO
UNAOTUMIA MANENO KAMA, NA NA ULINGANISHI USIOTUMIA NENO KAMA NA
(SIMILES AND METAPHORS)
1. Similes ni
mifano ya ulinganisho inayotumia neno kama au na moja kwa moja neno simile
limetoka katika kilatini lnye maana ya
kufanana au kama kwa mfano “anatenda
kama nguruwe” huu ni mfano wa moja kwa moja wa ulinganisho wa Maneno similes
mingi ya mifano ya yesu pia iko katika lugha za ulinganifu Mfano ni
·
Luka 10;3 “…Nawatuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu”
·
Marko 4;31 “…..Ni kama punje ya haradali…..”
·
Mathayo 24;27 “……kama vile umeme utokavyo mashariki…”
·
Kutoka 16;14 “……Kidogo kama sikitu juu ya nchi”
Kwa msingi huo ulinganishio wa
Maneno unaotumia neno kama au na huitwa similes na kwa mchoro wa mfano huonekana namna hii
Na
|
umefanana na chachu
2. Metaphors ni
ulinganisho wa Maneno wa moja kwa moja usio na kiungo kama na au kama kwa mfano
Mungu ni Mwamba wangu, Bwana ni ngome yangu, au ngao yangu au wokovu wangu Zaburi ya 18;2. Au
Yesu anaposema Mimi ni mkate wa uzima Yohana 6;35
Yesu alimtumia
Maneno haya pia katika kufundisha kwa mfano Maneno kama ninyi ni chumvi ya
ulimwengu,au ninyi ni Nuru ya ulimwengu kwa msingi huo Metaphors hazina
kiunganishi katikati bali ni neno la moja kwa moja lakini la ulinaganifu
Ninyi ni Nuru Ya Ulimwengu
Ni muhimu kufahamu kuwa pia uko
ulinganifu ulio kuinyume au ulinganifu unaokanusha ambao pia hutumika katika
Maneno kadhaa ya kibiblia kwa mfano Hesabu 23;19 unaosema Mungu si mtu aseme
uongo wala si mwanadamu ajute
Ulinganifu ulio kinyume Mungu si Mtu hata aseme uongo Hes 23;19
C.
MANENO YA KUONGOZA
CHUMVI (HYPERBOLES)
Lugha ya kutia chumvi ni lugha ya
kukuza au kukazia au kuonyesha msisistizo wa jambo fulani muhimu kwa mafano
Yesu alipowaambia mafarisayao Rnyi wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia Mathayo
23;24 hii ilikuwa ni lugha ya kusisitiza hapa yesu alikuwa akiwakosoa tabia yao
ya kusisitiza mambo madogo ya sheria huku wakisahau mambo muhimu ya sheria
ambayo ni Haki, Rehema na uaminifu kwa kutumia lugha ya mficho na ya kutia
chumvi ukweli ulifika mahali pake kwani ni kweli mtu aweza kuchuja mbu wakati
wa kunywa maji lakini kimsingi hakuna mtu awezaye kumeza ngamia unaona!
Maandiko
mengine ambayo ni yenye Maneno ya kukazia au kuonyesha msisitizo au kutia
chumvi ni pamoja na
·
Mathayo 19;24…..Ni rahisi kwa Ngamia kupenya katika Tundu ya
sindano
·
Mathayo 16;26…..itamsaidia nini mtu akiupata ulimwengu wote
na kisha kuipotyeza nafsi yake
·
Zaburi 6;6………..Nalilowesha godoro langu kwa machozi yangu
·
Zaburi 79;3………Wala hapakuwa na mzishi au hapakuwa na wa
kumzika mwingine
·
Yohana 21;15……Ulimwengu usingelitosha kwa vitabu
·
Wagalatia 4;15…..ngelinipa macho yenu
D.
MANENO YA
KUHUISHA AU KUKIPA KITU AU MNYAMA UHAI AU UBINADAMU( PERSONIFICATION)
Uhuishaji ni tendo la kukipa kitu siku
au mnyama ubinadamu. Hali hii hutokea pale mnyama au mahali au kitu au kitendo,vitu
vinapoelezwa vikiwa na sifa kama ya binadamu halisi
Kwa mfano
·
Tamaa ikiisha chukua mimba huzaa dhambi Yakobo 1;15
·
Kwanini (Yuda) unataka kupigwa tena? Isaya 1;5
·
Ingawaje dhami zenu zinatushuhudia Yeremia 14;7
·
Milima na vilima vitaimba nyimbo Isaya 55;12
·
Acha Kesho ijisumbukie yenyewe Matahyo 6;34
E.
KUMLIGANISHA
MUNGU NA MWANADAMU (ANTROPOMORPHISM)
Kwa kawaida Lugha kubwa inayotumika
kumuelezea Mungu katika Biblia ni ile inayompa Mungu hali ya ubinadamu ingawaje
Mungu sio mwanadamu ni Roho na haonekani Mungu amepewa tabia hisia na vitenzi
vinavyofanana na mwanadamu penginepo ili wanadamu waweze kuelewa katika akili
za kawaida za kibinadamu Kolosai 1;15 Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana,
mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.na 1Timotheo 1;17. Kwa msingi huo utaweza
kuona kuwa
·
Mungu anapewa uso,kutoka 33;23
·
na anapewa macho 2Nyakati 7;16
·
anapewa masikio zaburi 31;2
·
kinywa 1falme 8;24
·
Mikono Isaya 52;10
F.
JINA MOJA KWA
NIABA YA LINGINE (METONYMY)
Hii ni njia iliyotumika kuelezea kwa
kuataja jina moja lenye kumaanishwa kwa niaba ya wengine kwa mfano Badala ya
kusema serikali ya Marekani waandishi wa habari wanaweza kusema ikulu ya
Marekani au badala ya Urusi imesema wanaweza kusema Moscow imesema au badala ya
Tanzania imesema unaweza kusema Dare es Salaam imesema; jambo hilo kitaalamu
huitwa Metonymy ambalo maana yake Meta kubadili na Onoma maana yake jina kwa msingi huo katika Biblia utaweza kuona
wakati mwingine nenoYakobo likitumika kwa Israel nzima au wayunani likitumika
kwa ajili ya mataifa mengine nje ya wayahudi
Hili linaweza
kuonekana katika vifungu vya mfano vifuatavyo
·
Wapenzi wangu msiiamini kila roho bali zijaribuni 1Yohana
4;1 hapa anamaanisha mafundisho yatokayo kwa Mungu au kwa roho nyingine
·
Isaka ataharibiwa Amosi 7;9
·
Wanao Musa na Manabii na wawasikilize wao Luka 16;29
·
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu Yohana 3;16
·
Tukilitizamia tumaini lenye Baraka Tito 2;13
·
Kwakuwa pale hazina yako iliko ndipo na moyo wako Matahayo
6;21
·
Upumbavu wa Mungu 1koritho 1;21,25
G.
SEHEMU MOJA KWA
JAMBO LOTE AU SEHEMU NZIMA KWA SEHEMU (SYNECDOCHE)
Ni muhimu kufahamu pia kuwa abiblia
hutimia lugha ya mficho ambapo sehemu moja huwakilisha sehemu nzima hii hutokea
pale kitu kinapozungumzwa kwa sehemu na kumbe kinyume chake kinazungumzwa kwa
ujumla wake hali ndio huitwa synecdoche mifano ya sehemu moja kuwakilisha
sehemu nzima ni kama hii ifuatayo;-
·
Baraka humkalia mwenye haki kichwani Mithali 10;6 – kichwa
hapa huwakilisha mtu kamili
·
Jinsi ilivyo mazuri miguu yake aletaye habari njema Isaya
52;7 miguu huwakilisha huyo atangazaye
·
Nafsi zaburi 103;1 nafsi huwakilisha mtu mzma au mtu kamili
·
Jicho 1Koritho 2;9 hapa jicho humwakilisha mwanadamu kamili
·
Heri mtu Zaburi 1;1 hapa inawakilisha wanadamu wote ingawaje
anatajwa mtu
·
Sheria Yakobo 2;10 ikimaanisha Agano la kale
·
Agano la kwanza Waebrania 9;1 ikimaanisha agano la kale
·
Sheria na Manabii ikimaanisha agano lote la kale Mathayo
7;12
Kwsa msingi huo utaweza kuona kuwa
wakati mwingine wana ikiwakilisha wanadamu wote au baba zetu ikimaanisha wazazi
wetu wa kale waliopita au Yoeli 2;28 inaposema nitawamwagiwa watu wangu au kila mwenye mwili si wakati wote
humaanisha hivyo wakati mwingine inaweza kumaanisha wayahudi na mataifa wale
watakao mwamini au 1Timotheo 2;4 ambaye anataka watu wote waokolewe hii
humaanisha ingawa Mungu anataka watu wote waokolewe bado ni wale tu wanaokubali
mpango wake katika maisha yao ndio wanaookolewa kwa hivyo Synedoche humaanisha
“sehemu kwa lote au lote kwa sehemu”
H.
KUZUNGUMZA
KINYUME CHA UHALISIA ( IRONY)
Hii ni hali ya kuzungumzia jambo
kinyume na uhalisia kwa mfano mtu wakati wa baridi kali anaweza kusema mzee
vipi joto la leo nawe ukajibu joto leo mzee kali sana hii inamaanisha kuwa
mnazungumza kwa kujmaanisha lakini kinyume na hali halisi ya tukio husika kwani
uhalisi unabaki kuwa kuna joto sana halii hii huitwa Irony kitaalamu mifano
halisi ya kibiblia ambayo inaonyesha maeneo ambayo misemo hii ilitumika baadhi
ni kama
·
Ayubu 12;2 hakika ninyi ndio watu na bila shaka Hekima
itakufa na ninyi
·
Mwanzo 3;22 Bwana Mungu akasema Basi huyumtu amekuwa kama
mmoja wetu kwa kujua mema na mabaya na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa
matunda ya mti wa uzima akala akaishi
milele hapa Mungu hakuwa anamaanisha kuwa sasa ni hakika kuwa mwanadamu amekuwa
kama Mungu kimsingi mwanadamu aliumbwa akiwa kama Mungu na kwa kula matunda
aliasi na alipoteza hali ya kuwa kama mungu
hivyo hapa Mungu anasikitishwa na kile kilichotokea na anatumia msemo
huu uitwao Iron
·
Ezekiel 20;39 Enendeni mkavitumikie vinyago vyenu kila mmoja
Mungu hapendezwi na kuabudu sanamu wala hajaruhusu ila ana akisi dhambi za
Israel hivyo anazungumza kwa kutumia Iron
·
2Wafalme 8;10 Enenda ukamwambie utapona nabii anatumia Iron kwani Mungu alimwambia
mfalme kuwa atakufa wala hatapona
·
1Wafalme 22; 15 Ahabu anaambiwa aende vitani na kushinda
lakini uhalisia ni kuwa atakufa
·
2samuel 6;20Mfalme wa Israel alikuwa mtukufu leo kumbe
alikuwa akimsanifu
·
Mathayo 23;32 Kijazeni basi kikombe cha baba zenu hapa
Kristo alikuwa akikazia dhambi ambayo ingefanya na kizazi kilichomsulubisha
ambayo kimsingi hata baba zao hawakuwahi kuifanya ingawa waliwakataa Manabii
wengi lakini kwa kitendo cha wao kumkataa masihi wanawazidi hata baba zao na
kuti miliza ile chuki yao dhidi ya Manabii Yesu hakuwa anasisistiza waifanye
dhambi hiyo bali alitaka kuonyesha ni jini gani wako mbali na Mungu zaidi ya
baba zao
I.
LUGHA ZA
MFICHO INAYOTUMIKA BADALA YA NENO CHAFU
FIGURATIVE LANGUAGE AU (EUPHEMISM )
Lugha za mficho ziko karibu katika kila
utamaduni ambapo watu huweza kutumia Lugha hizo kwa ajili ya kuficha mambo fulani
kama Ngono au kwenda choo kujisaidia n.k kwa mfano mtu anaweza kutumia neno
mzigo akimaanisha ngono Paulo mtume alimtumia Lugha ya mficho katika 1Wakoritho
7; 1 akikataza zinaa na uasherati alisema “….Ni heri mwanamume asimguse
Mwanamke” hivyo hapo haimaanishi kuwa Mwanamume asioe lakini wasizini au
kufanya uasherati
Miano mingine ya lugha za mficho ni
kama
·
Waamuzi 3;24 kujifunika miguu ni kunya lugha inayotumika
kufunika neno hilo Euphemism
·
Malaki 2;16 kufunika nguo kwa udhalimu ni kunyimia tedno la
ndoa
·
2Samuel 13;14 akamlazimisha akalala naye maana yake akambaka
·
Amosi 4;6 Nami nimewapa ninyi usafi wa meno neno hili
linamaanisha njaa na sio kupigwa mswaki
·
Mwanzo 31;35 nimeshikwa na mambo ya kike maana yake yuko
mwezini
·
Mwanzo 32;25 alimgusa panapo uvungu wa paja lake ukateguka,
alimvunja Mapumbu
J.
MISAMIATI AU MANENO MAGUMU AU MITHALI NA MISEMO
Watu wengi wanaposikia au kuzungumzia
kuhusu kutafasiri Maandiko haraka watafikiri swala la kushughulikia ni
misamiati hilo huwa katika akili za watu wengi na linaweza kuonekana kama swala
jepesi tu wanaweza kutafuta neno la kiingereza lenye maana sawa na ile ya
kiebrania na kiyunani lakini Ili mtu aweze kuwa na tafasiri nzuri lazima
atafute Neno sahii lililotumika na hii husaidia sana katika kupata maana sahii
ingawaje pia swala la kutafasiri linaweza kuwa Gumu zaidi kwa sababu ya kukosekana
Maneno ambatano na neno husika ingawaje kujua neno lililotumika au msamiati
uliotumika katika lugha ya asili itakusaidia kupata kweli za kibiblia katika
njia iliyo nyepesi zaidi
·
Zingatia matoleo mbalimbali ya Biblia
·
Zingatia mchezo wa Maneno hasa katika Vitabu vya mashairi
mara nyingu hauingiliani
·
Zingatia maswala ya Jinsia kunawakati mji au nchi inaweza
kupewa jina la kike au mwanaume akawakilisha watu wote au wa jinsia zote
KUUSHIKA UPANGA VIZURI
KANUNI YA MIZANI, ULINGANIFU, USHAHIDI
WA MAANDIKO MENGINE (HARMONY)
Moja ya maswala ya hatari sana katika
kujipatia tafasiri zisizo halalai za kimaandiko ni kutengeneza fundisho katika
andiko moja hii ni sawa na wale jamaa ambao mmoja aliamua kukalia kiti kimoja
na mwingine alikalia kiti cha miguu minne yula wa miguu minne alikaa salama
kuliko yule wa mguu moja unapotumia andiko moja kutengeneza fundisho hauwezi
kupata mlingano sahii wa kimaandiko na ni hatari kwani unaweza kupata
mafundisho yasiyo sahii
Kwa mfano angalia aya zifuatazo ikiwa
zitafanywa fundisho nini kinaweza kutokea
·
Msihubiri kwa mataifa bali kwa wayahudi
tu Mathayo 10;5 - 6
·
Msichukue Fedha safarini wala viatu
Mathayo 10; 9-10
·
Hubirini juu ya nyumba Mathayo 10 ;27
·
Hubiri na kufundisha ukiwa katika boti
au mtumbwi Marko 4;1
·
Kumfuata Yesu lazima kuambatane na
kuwachukia ndugu Luka 14 26
·
Yey achinjaye Ng’ombe ni sawa na yeye
auwaye mtu Isaya 66;3
·
Kumfanyia mtu maombezi mbali na watu
Marko 8;23
Kwa msingi huo tunaweza kuona kuwa
tayari tumepata picha kuwa kutumia andiko moja kutendeneza fundisho si halali
katika kanuni za kufasiri Maandiko na hivyo awaye yote atakayetegemea andiko
moja kwa fundisho amekalia kiti chenya mguu moja hawezi kuwa salama andiko
lazima liwe na masahidi wawili au watatu ili lithibitike, hii haina maana kuwa
mtu aliyekalia kiti cha miguu minne yuko salama pia hapana kunauwezekano pia
Maandiko yakawa mengi lakini ikawa sio yaliyolingana hata kama una Maandiko mengi yanayounga mkono
fundisho lako ni muhimu kufahamu kuwa tunahitaji Biblia nzima ikubalianae na
kile unachotaka kukihubiri kwani tumepewa Biblia nzima na sio manenno machache
tu kwa msingi huo mtafasiri wa Maandiko
hapaswi kudharau kile au andiko lililo kinyume na kile anachotaka kukifundisha
kwa hivyo Maandiko mengi bado hayakupi kuwa salama japo unaweza kupumua kuliko
yule wa andiko moja lakini hii sio taa ya kukuruhusu kuendelea mbele bado
unahitaji kuwa makini ili iwe hivyo zingatia mambo ya msingi yafuatayo
weka Mzigo nyuma ya Punda usiweke mzigo mbele ya Punda
1. Usiweke mzigo mbele ya Punda.
Tumeitwa
kuhubiri. Lakini tutahubiri nini ? Je tujiamulie tu kile tunachotaka
kukihubiri? Hapana Mungu amekataza Tumeitwa kuihubiri Biblia lakini ni eneo
gani la Biblia tunaweza kulihubiri? Je ni Maandiko yanayotuvutia tu? Au tuchague
ile mistari tunayoijua sana Mpaka hapo tutakuwa hatujaitendea haki Biblia
Hatuamui sisi kile tunachopaswa kukihubiri kisha tukaamua kutafuta katika
Biblia kuunga mkono kile tunachofikiri halii ndio dhambi ya kuweka Mzigo mbele
ya Punda ili ausukume
Ni
muhimu kwanza kwenda kwenye Biblia yenyewe na kuisoma tena na tena na
kuijuifunza inasema nini kisha hubiri kile Biblia inachosema katika hali hii
utakuwa na amani na Mungu mafundisho mengi leo sio kile Biblia inachokisema
bali ni kile watu wanasema na kwa msingi huu kuna mafundisho mengi ya uongo
duniani watu wengi hawalihubiri neno badala yake wanaangalia nini kimo mioyoni
mwao kisha wanakwenda katika Maandiko na kuyasingizia au kutafuta kuungwa mkono
kwa mawazo yao
Muhubiri
maarufu William Branham aliumba usiku na mchana na kupata Ufunuo kutoka kwa
Mungu na kupata wazo kuwa hakuna utatu isipokuwa ni Yesu pekee na alipata wazo
kuwa Yesu ndiye Baba na ndiye Roho na ndipo alipoanzisha imani iitwayo Jesus
Only pia alikwenda katika Maandiko na kutafuta kusapoti mawazo yake na akaktuta
andiko alilolidhani kuwa linaunga mkono mawazo yake Yohana 14;9 Branham
alipuuzia kuwa katika sura ileile kuna Maandiko ambayo yako kinyume na mawazo
yake au Ufunuo wake
·
Mna mwamini mungu niaminini na mimi
Yohana 14;1
·
Nitamuomba baba sio nitajiomba mwenyewe
Yohana 14;16
·
Yeye anipendaye mimi atapendwa na baba yangu Yohana 14;21
·
Nasi tutakuja kwake na kufanya makazi
ndani yake Yohana 14;23
·
Maneno niliyowaambia si yangu bali
Yohana 14;24
·
Lakini huyo Roho ambaye baba atampeleka
Yohana 14;25-26
·
Baba ni mkuu kuliko mimi je mtu
anawezaje kuwa mkuu kuliko yeye mwenyewe? Yohana 14;28
Unapopuuzia
kile kinachosemwa na Biblia nzima na kukaa katika andiko moja na kutengeneza
Fundisho au kutafuta Biblia iunge mkono mawazo yako ni sawa na kuweka mzigo
mbele ya Punda usiweke mzigo mbele ya Punda Picha na maelezo kwa hisani ya
maktaba ya Mchungaji Innocent Samuel Kamote Mwandishi wa somo
2. Kumbuka kusema kuwa Imeandikwa pia
Mathayo 4;5-7 “Ndipo ibilisi
akamchukua Yesu mpaka mji mtakatifu wa Yerusalemu na kumweka juu ya mnara mrefu
mwembamba wa hekalu, akamwambia, “Kama Wewe ndiye Mwana wa Mungu jitupe chini,
kwa kuwa imeandikwa,
“Atakuagizia malaika zake nao
watakuchukua mikononi mwao ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.’ Yesu
akamjibu, “Pia imeandikwa: ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’
Kumbuka kuwa si kila wakati mtu
akiinukuu Biblia ndio anahubiri kweli haisaidii kunukuu Maandiko pekee, Baadhi
ya watu wanaitafasiri vibaya Buiblia kwa bahati mbaya Lakini wengine ni Mbwa
mwitu wakali katika mavazi ya kondoo kumbuka Shetani pia alisema “Imeandikwa”
alinukuu mstari au aya hii kwa kusudi la kumkosesha Bwana Yesu Neno la Mungu
litakuwa ni taa ya miguu yetu pale tu linapotafasiriwa kwa halali na kwa
ulinganifu na Maandiko mengine
Yesu hakupambana na shetani kuhusu
andiko alilolitumia wala hakukanusha kuwa wako malaika ambao wanatulinda,
lakini Yesu alimshinda adui kwa kutumia kanuni ya ulinganifu alimwambia kuwa
“Pia imeandikwa usimjaribu Bwana Mungu wako”kwa kufanya hivyo aliweka ulinganifu
wa andiko kwa andiko jingine ,Hiii inafanyika pale andiko linapotumika kwa
kusudi la kudhuru badala ya kusaidia,Neno la Mungu ni upanga ukatao kuwili
unaweza kukata huku na huku kwa mfano hebu tuangalie Maandiko yanayohitaji
kufanyiwa ulinganifu ili kupata ukweli halisi wa kibiblia
A.
Swali: Kama
Yesu hakuja kuleta amani duniani kwanini malaika waliimba amani duniani?
Luka 2;14
“Atukuzwe Mungu juu mbinguni na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.”
Imeandikwa pia
Mathayo 10;34”
Msidhani kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani bali upanga.
Namna ya kuweka
ulinganifu;
Yesu alikuja kuleta amani Duniani kwa watu
wote wanaomkubali lakini pia kwa wale wanaomkataa hakuja kuleta amani kwao kwa
msingi huo kumpokea Mfalme wa amani kunaweza kuwafanya wasiomwamini kutuchukia
kabisa.
B.
Swali: Je Yesu alikuja kuleta hukumu?
Yohana 9;39
“Yesu akasema, “Nimekuja ulimwenguni humu kwa ajili ya kuhukumu, ili wale walio
vipofu wapate kuona, nao wale wanaoona, wawe vipofu.’’
Likini pia
imeandikwa
Yohana 12;47
Mimi simhukumu mtu ye yote anayesikia maneno Yangu na asiyatii, kwa maana
sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa.
Namna ya kuweka
ilinganifu
Yesu alikuja
kutafuta na kuokoa kile kilichopotea na sio kuuhukumu kwa dhambi zao ingawaje
wale walio mkataa watahukumiwa
C.
Swali: Kama
Roho anatufundisha je hatuhitaji waalimu?
1Yohana 2;27
Kwa habari yenu ninyi, Mafuta yale mliyoyapokea kutoka Kwake yanakaa ndani
yenu, wala ninyi hamna haja ya mtu ye yote kuwafundisha. Lakini kama vile
mafuta yale yanavyo wafundisha kuhusu mambo hayo yote nayo ni kweli wala si
uongo, basi kama yanavyowafundisha kaeni ndani Yake.
Lakini
imeandikwa pia
Efeso 4;11
“Naye alitoa wengine kuwa Mitume,wengine kuwa Manabii,na wengine kuwa
wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu”
Namna ya kuweka
ulinganifu
Mafuta ya Roho
Mtakatifu yanamfundisha mwamini kweli nyingi na hivyo haupaswai kupuuziwa
lakini kuheshimika kwani ni njia ya pekee ya kufundishwa na Mungu mwenyewe, kwa
hivyo hatuhitaji mwalimu anayeweza kudai kuwa ana Ufunuo au ameangaziwa siri
fulani kwa ajili yetu Lakini Mungu pia ameweka waalimu kama zawadi kwa kanisa
ili kulikamilisha na kuwakataa ni kumkataa Mungu
D.
Kama Mungu
anaweza kufanya miujiza mikubwa kwanini wakati mwingine anaacha watumishi wake
wanaugua?
Matendo 19;11 “Mungu
akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida…”
Lakini pia
imeandikwa
2Timotheo 4;20
“…..Trofimo nimemwacha huko Mileto Hawezi (Mgonjwa)
Namna ya kuweka
ulinganifu
Mungu anaponya
wagonjwa hii ni wazi kabisa katika neno lake hususani Agano jipya Lakini kuna
wakati ambapo hata maombi ya mitume wakubwa waliotumiwa sana na Mungu hayakuweza
kuponya wagonjwa katika wakati huu Tunaendelea kuamini kuwa Mungu ni mponyaji
lakini ni lazima tukubali kuwa si kila wakati Mungu anaponya kwa sababu zake
ambazo hatuwezi kuzieleza
E.
Kama Mungu
akiwa upande wetu hakuna wakuwa kinyume nasi kwanini wakristo huuawa?
Warumi 8;31
“…Mungu akiwapo upande wetu ni nani aliyejuu yetu”?
Lakini pia
imeandikwa
Warumi 8;36
“…Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa”
Namna ya kuweka
ulinganifu
Kunawakati
walinzi 16 walishindwa kumlinda Petro Gerezani Matedno 12 kuna wakati ambapo
Mungu aliacha Paulo mtume kupigwa mawe Matedno 14 mungu anaweza kuruhusu mpigwe
bakora,mburuzwe na kutiwa Gerezani lakini pia anaweza kuleta tetemeko kubwa na
milango ya gereza ikafunguka Matedno 16 ili Mungu abaki kuwa Mungu tumewekewa
si kumwamini tu bali na kuteswa kwa ajili yake Wafilipi 1;29.
Kwa msingi huu basi kumbe tunajifunza
kuwa andiko moja likiachwa bila ulinganifu wa Maandiko mengine linakuwa dhaifu
kama ilivyo kwa Nyuzi moja ya kamaba ya katani inakuwa dhaifu inapoachwa pekee
kuliko inaposokotwa pamoja na kundi la nyuzi nyingine ndipo linapokuwa imara
kwa hivyo kanuni ya kubalance au mizani ya Maandiko ni muhimu katika kujifunza
na kupata kweli ya kuifahamu Biblia si kila wakati mtu anapopatwa na mabaya au
kukosa Fedha au kulala na njaa ni kuwa hana imani kunawakati utaamini na
kuokolewa na kuna wakati utaamini na utakufa angalia mifano mingine ya
kumizanisha Maandiko kupata kweli
F.
Kwaimani watu
waliokolewa na kwaimani watu walikufa
Waebrania11;32-35a
“Basi niseme nini zaidi? Sina wakati wa kusema habari za Gideoni, Baraka,
Samsoni, Yeftha, Daudi, Samweli na manabii, ambao kwa imani walishinda milki za
wafalme, walitekeleza haki, walipokea ahadi za Mungu, walifunga vinywa vya
simba, walizima makali ya miali ya moto, waliepuka kuuawa kwa upanga, udhaifu
wao ukageuka kuwa nguvu, walikuwa hodari vitani wakayashinda majeshi ya wageni
na kuyafukuza. Wanawake walipokea watu wao waliokuwa wamekufa wakafufuliwa.
Lakini pia imeandikwa
Waebrania 11;
35b-39a “Lakini wengine waliteswa nao wakakataa kufunguliwa, ili wapate ufufuo
ulio bora zaidi. Wengine walidhihakiwa na kupigwa, hata walifungwa minyonyoro
na kutiwa gerezani. Walipigwa kwa mawe, walipasuliwa vipande viwili kwa
msumemo, waliuawa kwa upanga, walizunguka-zunguka wakiwa wamevaa ngozi za
kondoo na mbuzi, wakiwa maskini, waliteswa na kutendwa mabaya, watu ambao
ulimwengu haukustahili kuwa nao. Walizunguka majangwani na milimani, katika
mapango na katika mahandaki ardhini. Hawa wote walishuhudiwa vema kwa sababu ya
imani yao,
Namna ya kuweka
ulinaganifu
Wakati mwingine
Imani inatuwezehs kuhamisha milima na wakati mwingine inatuwezesha kuipanda
milima Ayubu akasema tupate mema kwa Mungu tusipatwe na mabaya Ayubu 2;10
G.
Je ni kweli
Yesu alisema tuwachukie ndugu zetu?
Luka 14;26
“Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake na mama yake na mke wake na
wanawe na ndugu zake naam na hata nafi
yake mwenyewe hawezi kuwa Mwanafunzi wangu.”
Lakini pia
imeandikwa
Mathayo 10;37
“Ampendaye baba yake au mama yake kuliko mimi hanistahiliwala ampendaye mwana
au binti kuliko mimi hanistahili’
Namna ya kuweka
ulinganifu
Maandiko yana
tabia pia ya kujitafasiri yenyewe kwa yenyewe hivyo wakati mwingine kwa kutumia
Maandiko sambamba yaani Cross reference inakusaidia kupata majibu kwa msingi
huo neno kuchukia katika injili ya luka lilipaswa kutumika kupenda ndugu zaidi
yangu.
H.
Kwa msingi huo
kila ahadi ya Mungu pia inapaswa kuchukuliwa kwa ulinganifu
·
Amehaidi kutuokoa lakini lazima tujitie nidhamu kuiutunza
wokovu
·
Amehaidi mbingu lakini pia ameahidi hukumu
·
Amehaidi kukubalika lakini pia ameahidi kukataliwa
·
Ameahidi ushindi lakini pia ameahidi mateso
·
Amehaidi kuzaa sana matunda lakini pia ameahidi kukata tawi
lisilozaa matunda
·
Ameahidi furaha lakini pia ameahidi dhiki
Kumbe ahadi za Mungu zinajumuisha wakati
mzuri na wakati mgumu
KANUNI YA UHUSIANO WA AGANO LA KALE NA
AGANO JIPYA (COVENANTS)
Mtafasiri wa Maandiko anapaswa kuuelewa
uhusiano ulioko kati ya ukristo na agano la kale au uhusiano ulioko kati ya
Agano jipya na la kale. Agano la kale lina sheria zipatazo 600, Je mkristo
anapaswa kuzishika hizo zote? Kama tunapaswa kuzishika zote, Je itawezekanaje
pasipokuweko hekalu?. Na madhabahu za wanyama za kuteketeza? Na kama hali
tuhusu kwanini ni sehemu ya Biblia? Na kama hatuko chini ya sheria kwanini Yesu
alisema ‘Msidhani ya kuwa nimekuja kuitangua torati na Manabii, Sikuja
kuitangua bali kuikamilisha” Mathayo 5;17
Biblia yetu imegawanyika katika makundi
makuu mawili agano la kale na agano jipya sisi wakristo tuko chini ya agano
jipya na waisrael walikuwa chini ya agano la kale kwa mukhtasari agano la kale
lina mambo muhimu yafuatayo
Ø
Kuumbwa kwa ulimwengu na vitu vyote
Ø
Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu baba yao wote waishio kwa imani
Ø
Kutoka kwa wana wa Israel huko Misri
Ø
Kupewa Sheria , Mungu aliagiza yale Israel walipaswa
kuyatimiza
Ø
Kuhangaika katika jangwa
Ø
Kuingia kanaani na kuimiliki nchi ya kanaani
Ø
Kipindi cha Waamuzi
Ø
Kipindi cha Wafalme
na manabii
Ø
Mashairi
Ø
Kupelekwa utumwani na kurudi kutoka utumwani
Mungu ametupa Agano la kale hata kama
hatuko chini ya agano la kale kwa msingi huo ni muhimu kwetu kujifunza Muongozo
wa kuelewa uhusiano wa Ukristo na agano la kale
1.
Agano la kale
(Sheria ) ni sehemu ya Agano
Agano ni mapatano ya pande mbili husika
huku zikimuhusisha Mungu katika agano kuna majukumu ambayo kila upande unapaswa
kuyatimiza, Leo hii tunaona watu wanapouziana Ardhi wakiandikishana hiki kinasaidia
kutujulisha kuwa muuzaji amesema nini na mnunuzi amesema nini yale
waliyokubaliana huonekana katika mkataba wote watapaswa kukubaliana na mkataba
wao au inaweza isiwe lazima, Agano la
kale ni mkataba wa Mungu na Waisrael ni agano na ndani yake Mungu amewapa amri
zaidi ya mia sita 600 kama wakizishika Mungu angewabariki na kuwalinda sheria
hizi ziko kati ya Kutoka 20 mpaka Kumbukumbu la torati 33.
2.
Agano la kale
sio agano letu
Agano la kele ni agano la Mungu na
Waisrael limekalia katika mamia ya sheria na linahusu uchinjaji wa wanyama na
utoaji wa sadaka za kuteketezwa za kila mwaka
wakristo hawako chini ya sheria hii ya kale tunaweza kuliona hilo
wazi katika Maandiko yafuatayo.
·
Warumi 6; 14 - Kwa maana dhambi haitakuwa na mamlaka juu
yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema.
·
Yohana 1; 16-17 - Kutokana na ukamilifu Wake, sisi sote
tumepokea neema juu ya neema. 17Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa
Musa, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo.
·
Wagalatia 5; 4 Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa
njia ya sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu.
Yesu hakuja kuitangua Torati lakini
alikuja kulitimiza na agano ambalo lilikuwa limekamilishwa au limamaliza kazi
yake ya Ufunuo, Yeye alikuja kutuhesabia haki inayozidi haki ile ya mafarisayo
haki itokanayo na neema na sio kwa sheria au Matendo ya sheria, haki itokanayo
na imani kupitia sadaka aliyoitoa yeye msalabani iliyochukua nafasi ya zile za
wanyama za agano la kale Warumi 10;4 “Kwa maana Kristo ni ukomo wa
sheria ili kuwe na haki kwa kila mtu aaminiye”.
3.
Maagizo mengi
katika agano la kale hayakurudiwa katika agano jipya
Agano la kale limegawanyika katika
maeneo makuu matatu ya sheria yaani sheria za Kimaadili Moral law, Sheria za
kidini Ceremonial law na sheria za kisiasa au za kiraia Civil laws, kundi
lililo kubwa zaidi ni la sheria za Kidini hizi hupatikana kwa wingi katika
walawi na sehemu kadhaa za kitabu cha kutoka, Hesabu, na Kumbukumbu la torati
hizi sheria za kidini kwa ujumla zinamuhusu Mungu hizi zinawajulisha wayahudi
Mungu anatarajia nini kutoka kwao pamoja
na kumuabudu namna gani watengeneze hema vipimo gani vitumike sanduku liweje
madini gani yatumika n.k. wajisafisha wakati gani na waabudu vipi sheria hizo
zinafanya kazi kwa Raia wa zamani wa Isarael pekee na hakuna hata moja
imerudiwa katika Agano jipya, leo hii vyakula vyote vimetakaswa 1Timotheo
4;1-5, Maswala ya Hekalu, Sadaka za kuteketezwa na ukuhani vimeondolewa milele
Yesu amekuwa kuhani wetu mkuu
Kwa nini tunasema sheria za kidini ziliwahusu
waisarael kwa Mungu?
Waebrania 10;1-10 “Kwa kuwa Torati ni
kivuli tu cha mambo mema yajayo, wala si uhalisi wa mambo yenyewe. Kwa sababu
hii, haiwezekani kamwe kwa njia ya dhabihu zitolewazo mwaka hadi mwaka,
kuwakamilisha wale wanaokaribia ili kuabudu.Kama dhabihu hizo zingeweza
kuwakamilisha, hazingeendelea kutolewa tena, kwa kuwa hao waabuduo wangekuwa
wametakaswa mara moja tu, wala wasingejiona tena kuwa na dhambi. Lakini zile
dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka, kwa sababu haiwezekani damu ya
mafahali na mbuzi kuondoa dhambi. Kwa hiyo, Kristo alipokuja duniani
alisema,“Dhabihu na sadaka hukuzitaka, bali mwili uliniandalia, sadaka za
kuteketezwa na za dhambi hukupendezwa nazo. Ndipo niliposema,‘Tazama niko hapa,
kama nilivyoandikiwa katika kitabu, Nimekuja kufanya mapenzi Yako, Ee Mungu.’ ”
Kwanza alisema,“Dhabihu na sadaka, sadaka za kuteketezwa na za dhambi
hukuzitaka, wala hukupendezwa nazo” (ingawa sheria iliagiza zitolewe).Kisha
akasema “Tazama niko hapa, nimekuja kuyafanya mapenzi Yako.” Aondoa lile agano
la kwanza ili kuimarisha la pili. Katika mapenzi hayo sisi tumetakaswa na
kufanywa watakatifu kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara
moja tu”.
Sheria za kidini za agano la kale
hazikurudiwa katika agano jipya ,agano la kale sio tu lina sheria za kidini
bali pia lina sheria za kiraia na kimaadili ambazo hizi zinahusu uhusiano
ulioko kati aya mwanadamu na mwanadamu mwenzake hizi zinajibu maswala ya
matatizo yajitokezayo siku kwa siku Israel wanapoishi kwa pamoja sheria hizi ni kama vile nini kifanyike
Ng”ombe anapoua mtu,Mtoto anapomshutumu baba yake,mwizi anapokamatwa,Mtu
anapofanya zinaa sheria za kiraia na kimaadili zilikuwa zikitoa majibu ya
matatizo kama haya kwa msingi huo chini
ya agano Jipya Je Mungu anatutaka tukaangalie sheria zile za kale zinasema nini
na kuzitenda? Jibu ni la hasha Leo hatumpigi mtu mawe anapofanya zinaa au
anapokuwa amemtukana mzazi wake hatuko chini ya sheria yoyote au hata moja ya
agano la kale.
Mtafasiri mzuri wa Maandiko atatofautisha
sheria za kidini na za kiraia na wakristo hawako chini ya hizo
4.
Sheria za
kimaadili za Agano la kale zimerudiwa au zimefanywa upya katika agano jipya
Tumekwisha kusema kuwa Yesu hakuja
kuitangua Torati bali kulitimiza lakini zingati mstari wa 19 katika Mathayo 5;
19 unaosema Kwa hiyo, ye yote atakayevunja mojawapo ya amri ndogo kuliko zote
ya amri hizi, naye akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa
katika Ufalme wa Mbinguni, lakini ye yote azitendaye na kuzifundisha hizi amri
ataitwa mkuu katika Ufalme ya Mbinguni.
Hapa Kristo anazungumza na wale walio
wa Ufalme wa mbinguni wafahamu kuwa nyingi ya sheria za agano la kale
zinakubaliana na mfumo wa agano jipya kwa maana hii Nyuma ya kila sheria kuna
kanuni ya msingi ya kuizingatia Hivyo wakristo wanapaswa kuishi kwa kanuni hizo
Yesu hapa alienda mbele zaidi ya sheria
ambapo Nyuma ya kosa la mtu kuua kuna chuki hii ni dhambi Mathayo
5;21-24,Nyuma ya sheria ya zinaa kuna tamaa isiyoweza kuzuiliwa hii ni dhambi
Matahayo 5;27-30 nyuma ya sheria ya kuapa kuna kanuni ya kuwa mkweli Mathayo
33-37
Sheria hizi zimetolewa kwa kusudi la
kukwepa maswala ya kulipizana klisasi kama jino kwa jino au jicho kwa jicho kwa
msingi huo Yesu alitupa kanuni za msingi za kutusaidia kimaadili kuweza kuishi
kwa kanuni zilizo juu ya sheria
·
Uhusiano wetu na Mungu katika agano jipya haujengwi na uwezo
wetu wa kuishika sheria Tito 2;11-12
·
Wakati wa agano la kale sheria ziliandikwa katika jiwe
katika agano jipya zinaandikwa katika moyo Waebrania 8;8-10.
·
Tunatimiza sheria yote kwa Roho ya upendo na sio kwa ulazima
wa sheria Matahayo 22;36-40,Warumi 13;8-10
·
Jinsi gani mkristo anaitimiza sheria ya agano la kale
Kumpenda Mungu na kumpenda jirani yake
5.
Agano la kale
sio amri ya Mungu kwetu lakini ni njia
ya kujifunza kwetu
Biblia imejaa amri nyingi na mifano
amabayo kwayo Mungu anataka tujifunze na kutii Binafsi kwa mfano Mungu
alimuamuru Nuhu kuijenga safina ya mti wa Mvinje Mwanzo 6;14 ingawaje alitaka
sisi tujifunze kuhusu amri zake
hatarajii kuwa na sisi tutaanza kujenga safina tunajifunza nini hapa?
Agano la kale ni neno la Mungu kwetu
lakini sio Amri ya Mungu kwetu
Ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu ni
endelevu na hujifunua kwetu hatua kwa hatua watu wa agano la kale walimfahamu
Mungu kwa kiasi kidoko kuliko ambacho sisis tunamfahamu walimfahamu kwa mbali
lakini sisi tumepewa Roho wake Waebrania 12;18
Agano jipya Bora zaidi katika kumfunua
Mungu kwetu kuliko katika agano la kale lakini tunalihitaji agano la kale ili
kulielewa agano jipya kwani agano jipya lina nukuu zaidi ya 1100 kutoka agano
la kale hatu wezi kuelewa misemo kama Mwana Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi
ya ulimwengu bila kuwa na ufahamu wa agano la kale kwa msingi huo agano la kale
nui neno la Mungu kwetu ingawaje hatuko chini ya agano hilo bali agano jipya
Ona mfano wa matumizi yake 1Koritho
9;9-10 “Kwa maana imeandikwa katika sheria ya Musa? “Usimfunge ng’ombe kinywa
apurapo nafaka.” Je, Mungu hapa anahusika na ng’ombe? .Je, Mungu hasemi
haya hasa kwa ajili yetu? Hakika yameandikwa kwa ajili yetu, kwa sababu mtu anapolima
na mwingine akapura nafaka, wote wanapaswa kufanya hivyo wakiwa na tumaini la
kushiriki mavuno.”
Kwa msingi huo kuna mengi ya kujifunza
kutoka katika agano la kale na moja ya somo muhimu tunalojifunza ni hitaji letu
la kuwa na agano jipya ambapo haki hupatikana kwa imani na sio kwa kuishika
sheria shera ni mwalimu mzuri wa kutuonyesha hitaji letu kwa neema ya Mungu
Wagalatia 3; 23-25 “Kabla imani haijaja tulikuwa tumewekwa chini ya sheria,
tumefungwa mpaka ile imani ifunuliwe. Hivyo, sheria ilikuwa kiongozi
kutufikisha kwa Kristo, ili tupate tuhesabiwa haki kwa imani. Lakini sasa kwa
kuwa ile imani imekuja, hatusimamiwi tena na sheria.
6.
Ahadi katika
agano jipya ni tofauti na Ni bora zaidi kuliko
ahadi katika agano la kale
Agano la kale ni patano la Mungu na
wana wa Israel aliwaahidi inchi ya maziwa na asali hii ilikuwa ni nchi yenye
mipaka maalumu kabisa na hata leo nchi hii inajulikana kama Israel kuingia
katika inchi hii kulimaanisha vita vya kisiasa kwa sababu kulikuwa na mataifa
mengine yaliyokuwa yanaitawala nchi hiyo na wakati mwingine Mungu aliwatia hofu
maadui ili Israeal wawashinde
Wakati wa agano la kale Israel ilikuwa
chini ya utawala wa Mungu kazi yao ilikuwa ni kutimiza sheria 600 na Mungu
angefanya sehemu yake kuwapa ushindi na kuwalinda na kuwabariki kuna ahadi
nyingi ambazo Mungu alizifanya kwa wana wa Isarael wakati wa agano la kale
kumbuka kuwa tumesema agano la kale sio agano letu wala kanisa halipaswi
kuzishika sheria 600 za agano la kale swali linakuja je kanisa linaweza kudfai
kuwa ahadi za agano la kale zina lihusu? Au zinawahusu Israel tu? Jibu Ni ndio
na hapana Hebu msomaji (uwe mvumilivu)
A.
Ndio ahadi hizo
zinalihusu kanisa leo
Hakuna taifa ambalo leo ni kanisa na
hakuna kanisa ambalo leo ni taifa Mungu anshughulika na mataifa mengi leo na kanisa lililoko chini ya agano jipya
hii ni tofauti kabisa na alivyokuwa akishughulika na Israel wakati wa agano la
kale kwa hivyo hawezi kwa mfano kututia
mikononi mwa wamidian au wafilisti au amaleki,kwa sababu eti hqatushiki sheria
600,wala Mungu hajaliahidi kanisa kuwa adui yako atakimbia mbele yako
Kumbukumbu 28;7 bali kinyuma na hayo Yesu amehaidi kuwa watatutesa watatusaliti
na kutuchukia kwa sababu ya imani yetu angalia yaliyompata Paulo 2Koritho
11;24-27 “Mara tano nimechapwa viboko arobaini kasoro kimoja na Wayahudi. Mara
tatu nalichapwa kwa fimbo, mara moja nalipigwa kwa mawe, mara tatu
nimevunjikiwa na meli, nimekaa kilindini usiku kucha na mchana kutwa. Katika
safari za mara kwa mara, hatari za kwenye mito, hatari za wanyang'anyi, hatari
kutoka kwa watu wangu wenyewe, hatari kutoka kwa watu Mataifa, hatari mijini,
hatari nyikani, hatari baharini, hatari kutoka kwa ndugu wa uongo. Nimekuwa
katika kazi ngumu na taabu, katika kukesha mara nyingi, ninajua kukaa njaa na
kuona kiu, nimekaa mara nyingi bila chakula, nimesikia baridi na kuwa uchi”.
Maadui wa Paulo hawakukimbia na badala yake
walimuandama mji kwa mji wala Paulo hakusema kuwa imeadnikwa adui zako watakuja
kwa njia moja na watatawanyika kwa njia saba, hakuwa mtakatifu wa agano la kale
alikuwa mtakatifu wa agano jipya kwa hiyo hakuweza kunukuu ahadi za agano
lililokuwa limepitwa na wakati Waebrania 8;13
Angalia kisa hiki
Kijana mmoja
alikuwa na wachumba wawili mmoja anaitwa Kanuni na mwingine anaitwa Neema kwa
msingi huo kijana alikuwa anasumbuka atamuoa nani? Kadi ya kina dada hawa
wawili,Kanuni alikuwa mzuri sana na wa kuvutia lakini alikuwa mwanamke wa
gharama sana na ingekugharimu kufanya kazi sana ili kumuoa na jamaa alijua kuwa
anaweza lakini kanuni ni mlalamishi sana anapokosewa na atanungu”nika sana
ukimkosea na baba yake alikuwa tayari kumsaidia kijana yule lakini akishindwa
kumfanya Kanuni kuwa na Furaha Kanuni pamoja na baba yake waliahidi kumlaumu
milele, tunapokuja kwa Neema naye ni msichana mzuri wa kuvutia wala si wa
gharama sana naye anafaa kuwa mke mzuri ni mchangamfu na hana maswala ya
kunung’unika na huitaji kufanya kazi sana ili kumpata haukumu mtu anapokosewa
wala baba yake hana mpango wa kukuhukumu unaposhindwa kutimiza ndoto zako kwake
na wataendelea kukupenda, wewe unajua kuwa ni dhambi kuoa wake wengi je uwewe
kama kijana yule ungemuoa nani?
Wakristo wameamua kumuoa Neema na sio
kanuni kwa sababu haturuhusiwi kuwaoa wote na kwa msingo huo hatuwezi kuweka
tumaini letu kwa ahadi za agano la kale yaani kanuni kwa sababu sio mke wetu
kwa sababu tumemuoa neema tunatarajia ahadi zote tulizoahiadiana na neema
,tutafurahia kile anachotupa na hatutatafuta mke mwingine na huo ndio utakuwa
uaminifu
B.
Hapana ahadi
zile za kale si kwa ajili yetu
Kwa namna nyingine agano jipya ni bora
zaidi kuliko agano la kale Waebrania 8;6 ,Mungu hakupendezwa na wale
walioshindwa kushika amri zake 600 kwa hivyo aliwatupilia mbali Waebrania 8;9
Mungu ameamua kutukubali sisi kwa imani kupitia Yesu Kristo aliwaahidi wao mchi
ya kanaani bali sisi ametuahidi mbingu, aliwaahidi wao kuwa atawashindia dhidi
ya adui zao bali ametuahidi sisi mkuwa kama kondoo wa Kuchinjwa katika maisha
sisi ni zaidi ya washindi Warumi 8;36-37 na Warumi 8;17-18.
Kumbuka
·
Agano la kale ni sehemu ya agano
·
Agano la kale sio agano letu
·
Maagizo mengi katika agano la kale hayakurudiwa katika agano
jipya
·
Sheria za kimaadili za Agano la kale zimerudiwa au
zimefanywa upya katika agano jipya
·
Agano la kale sio amri ya
Mungu kwetu lakini ni njia ya kujifunza kwetu
·
Ahadi katika agano jipya ni tofauti na Ni bora zaidi
kuliko ahadi katika agano la kale
KANUNI YA YALIYOTIMIZWA AU
YASIYOTIMIZWA KATIKA UFALME WA MUNGU (KINGDOM)
Mtafasiri wa Maandiko ni lazima
atofautishe yaliyotimizwa na yasiyotimizwa katika mtazamo wa maswala ya ufalme
wa Mungu, Unapozungumzia ufalme unazungumzia serikali au ulimwengu wenye Mfalme
Yesu alipokuwa akifundisha kuomba alisema tuombe Ufalme wako uje mapenzi yako
yatimizwe hapa duniani kama huko mbinguni
Swali sasa ufalme wa Mungu uko wapi? Je
umekwisha kuja ? kwanini Yesu aliwafundisha wanafunzi kuomba kuwa ufalme wako
uje?Mungu anatawala wapi?na yatafanyika wapi?Je mapenzi ya Mungu yanaweza
kutimizwa kwa ukamilifu Duniani kama mbinguni? Kama ufalme wa Mungu hauko hapa
kwa ukamilifu wake utakuja lini? Haya ndio maswala tutakayoshughulika nayo
katika sura hii
Biblia inazungumza mengi kuhusu ufalme
wa Mungu na kwa msingi huo tunapaswa kujibu maswali matatu kuhusu ufalme wa
Mungu
1. Ufalme wa Mungu
ulianza lini Duniani?
Tunaweza kusema kuwa Mungu aliitawala
dunia akiwa mbali nayo tangu wakati wa uumbaji, aliweka mipaka ya bahari na
aliahiza mahusiano ya jua na mwezi na nchi aliamuru wanadamu ndege na wanyama
na samaki kuzaliana na kuongezeka na kuanzia kitabu cha Mwanzo mpaka malaki
Mungu amekuwa akiwasiliana na ulimwengu kwa hivyo kuna mtazamo wenye
kuchanganya kuhusu utawala wa Mungu duniani ulianza lini kwa kuwa katika
Shughuli zake
Kwanini ni ngumu kujua kuwa ulianza
lini?
Mtahayo 8;11-12 Ninawaambia
kwamba wengi watatoka mashariki na magharibi nao wataketi karamuni pamoja na
Abrahamu, Isaka na Yakobo katika Ufalme wa Mbinguni. Lakini warithi wa ufalme
watatupwa katika giza la nje, ambako kutakuwa na kulia na kusaga meno.’’
2. Kuna uhusiano
gani kati ya ufalme wa Mungu na ufalme wa Mbinguni
Unaposoma kwa makini uhusiano wa ufalme
wa Mungu na ufalme wa Mbinguniutagundua kuwa hakuna tofauti na ni kitu
kimoja hii ni kwa sababu ilikuwa desturi
katika wakati wa Yesu watu kutumia neno Mbinguni kumwakilisha Mungu kwa hivyo
neno mbinguni na Mungu huingiliana katika Biblia
Mifano
·
Mathayo 8;11 – Ufalme wa Mbinguni
·
Luka 13;28-29 – Ufalme wa Mungu
·
Mathayo 11;11 - Ufalme wa Mbinguni
·
Luka 7;28 - Ufalme wa
Mungu
·
Mathayo 13;11 - Ufalme wa Mbinguni
·
Marko 4;11 - Ufalme
wa Mungu
·
Luka 8;10 - Ufalme wa
Mungu
·
Mathayo 13;31 - Ufalme wa Mbinguni
·
Marko 4;30-31 - Ufalme wa Mungu
·
Luka 13;18-19 - Ufalme wa Mungu
Mathayo alimtumia sana neno ufalme wa
Mbinguni kwa sababu aliwalenga wayahudi ambao walikuwa hawapendi kumtaja Mungu
moja kwa moja kwa kuwa kwao si vizuri kulityaja bure jina la bwana Mungu wako
3. Ni kwa njia ipi
ufalme wa Mungu tayari na yapi bado hayajatimia
Tumegusia awali kuwa ufalme wa Mbinguni
ni utawala ambao unatakiwa kuwa na mfalme na ufalme wa Mungu ulikuja na Kristo
Yesu hivyo tayari umekwisha anza ingawaje haujatimia kabisa hapa duniani kama
sasa umekwisha anza kujifunza Hermeneutics lakini bado hujamaliza kozi hii
tutayajuaje ni kwa kutumia chati hii ifuatayo
CHATI YA UFALME WA MUNGU
Swala husika
|
Tayari limetimia
|
Bado halijatimia
|
1.
Wokovu.
|
Wakristo wamesamehewa na wanaikulia
neema
|
Wakristo watakamilishwa kufikia
kiwango cha utimilifu wa Kristo Efeso 4;13
|
2.
Maarifa
|
Tunafahamu kwa sehemu 1Koritho
13;9-12 kwa jinsi ya fumbo
|
Kisha tutajua kama ninavyojuliwa sana
1Koritho 13;12
|
3.
Thawabu
|
Tunayo furaha,amani,upendo,kibali,uhakika,na
kujaliwa au kutunzwa
|
Tazama ninakuja haraka na ujira wangu
mkononi kumlipa kila mtu sawasawa na Matendo yake Ufunuo 22;12
|
4.
Afya
|
Kwa ujumla tuna afya njema,maombi ya
imani yanaponya wagonjwa Yakobo 5;14-15 Mungu ametupa pia madaktari,na madawa
ya aina mbalimbali
|
Hakutakuwa na kifo wala kilio wala
maombolezo kwakuwa mambo ya kale yamekwisha pita Ufunuo 22;5
|
5.
Utajiri
|
Mungu hukutana na mahitaji yetu
lakini sio na tamaa zetu tukitafuta kwanza ufalme wakeMathayo 6;33 wafilipi
4;19
|
Tutaona na kugusa hazina zote za baba
yetu katika ufalme ambao umetunzwa kwa ajili yetu mbinguni Luka 12;32-34
|
6.
Mateso
|
Mateso yetu ni ya kipimo na ya muda
mungu haruhusu tujaribiwe kupita tuwezavyo 1Koritho 10;13,2Timotheo 2;12,21Petro2;19-23,4;19
|
Atafua kila chozi, hakutajkuwako kifo
wala maombolezo wala kilio wala maumivu mambo yote ya kale yataopita Ufunuo 21;4
|
7.
Ulinzi
|
Wakatimwingine miujiza ya kulindwa
inatokea lakini Mungu si kila wakati hufanya hivyo,wakati mwingine huruhusu
waizi,ajali na mateso
|
Kila silaha itakayofanyika kinyume
nawe haitafanikiwa Isaya 54;17
|
8.
Hukumu
ya watakatifu
|
Watakatifu huadhibiwa kwa sehemu na kuhukumiwa Yohana
15;2!Koritho11;30,Waebrania 12;5-6
|
Kwani wote tutasimama mbele ya kiti
cha hukumu cha Yesu Kristo ili kila moja apokee kwa yote aliyoifanya
alipokuwa katika mwili kama ni mema au mabaya
|
9.
Hukumu
ya waovu
|
Wenye dhambi hupokea sehemu ya malipo
ya dhambi wametengwa kwa muda na Mungu na kuteseka kwa muda kama matokeo ya
dhambi zao Efeso 2;1,1Timotheo 5;24
|
Wafu watafufuliwa na wenye dhambi
watahukumiwa sawa na matedno yao na kila ambaye jina lake halikuonekana
limeandikwa katika kitabu cha uzima atatupwa katika ziwa liwakalo moto Ufunuo
20;12,21;8
|
10.
Hukumu
ya Ibilisi
|
Shetani ametupwa kutoka mbinguni
waamini hufurahi kwa ushindi huo kwa sehemu luka 10;18-19
|
Shetani atatupwa katika ziwa la moto
na kuteswa huko usiku na mchana Ufunuo 21;10
|
11.
Mapenzi
ya Mungu
|
Yanakubalika na watu wachache wengi
huyapinga Mathayo 6;18;141Timotheo 2;3-4
|
Kila goti litapigwa na kila ulimi
utakiri ya kuwa Yesu ni Bwana kwa utukufu wa Mungu baba Wafilipi 2;10-11
Ufunuo 21;1-4
|
Mtafasiri mzuri wa Biblia anapofundisha
maswala yoyote ya ufalme wa Mungu anapaswa kuzingatia yapi yamekwisha kutumia
katika ufalme wa Mungu na yapi bado ili asichanganye mambo na ndipo atakuwa
amelitendea haki neno la Mungu jambo hili ni muhimu kulizingatia katika eneo
hili la ufalme wa Mungu
KUUSHIKA
UPANGA KWA UANGALIFU
KANUNI
YA KUTAFASIRI MASWALA YA MIFANO (PARABLES)
Katika kanuni ya kutafasiri mifano
mtafasiri wa Maandiko anapaswa kuzingatia maswala ya kihistoria pamoja na
kukumbuka kuwa kuna somo moja tu katika kila mfano na pia kuweza kuondoa alama
ndogondogo zinazo tumika ndani ya mifano hiyo. Katika somo lililopita kuhusu
mambo yaliyo tayari na ambayo badi katika ufalme wa Mungu Wayahudi walitarajia
kuwa ufalme ungekuja mara moja na ghafla na kuonekana Yesu alijaribu sana
kurekebisha dhana hii na hivyo mafundisho mengi aliyoyatoa kuhusu ufalme wa
Mungu aliyatoa kwa njia ya mifano, kwa msingi huo maswala ya ufalme yaliyo
tayari na yasiyo tayari yatakuwa yakijitokeza ndani ya somo la mifano
A. Asili ya mifano
Katika eneo huili tutajifunza n amna ya
kutafasiri mifano ingawaje kwanza tutapaswa kujifunza nini maana ya mifano, kwa
nini Yesu aliitumia mifano na jinsi watu walivyoitumia vibaya mifano
Neno mifano linaweza kutumika katika
maana pana na maana ya kawaida katika
nmna pana mifano ni pamoja na Mithali,vitendawili,hadithi,stori nefu na
fupi,vijihadithi vya kusadikika na ulinganifu wa mambo lakini katika somo hili
tutaitafasiri mifano katika namna isiyo pana ambapo maana yake ni Hadithi rahisi fupi zenye maana fulani za
kiroho
B. Kwanini Yesu
alizungumza kwa mifano
Kama tulivyoona kuwa Yesu alimtumia
mifano sana katika mafundisho yake na ziko sababu kama nne hivi zilizopelekea
Yesu kufundisha kwa kutumia mifano
1. Alitumia mifano
kwa ajili ya usalama wake
Mafundisho yake yalikuwa ni tishio kwa
wengi katika nyakati zake alihukumu maisha na mafundisho yasiyo sahii ya
mafarisayo na masadukayo aliwatia changamoto na ilionekana kama wanapoteza
nafasi yao na heshima zao kwa watu kwa msingi huo waliamua kumfuatilia ili
wapate kumshitaki kwa Maneno au kuatfuta namna ya kukosoa na kupingana
naye aidha Viongozi wa kisiasa kama
Herode waliona kuwa Yesu alikuwa kiongozi tishio kwa usalama wao na kwa
serikali ya kirumi kwa hivyo walimuona ni hatari kwa hivyo alipotumia mifano na
hadithi fupi zenye maana fulani za kiroho maadui zake walikosa jambo la
kumshitaki kwa msingi huo matumizi ya mifano ilikuwa njia nzuri ya kujilinda na
kuwa salama wakatambua ya kuwa amewasema
wao kwa njia ya mifano marko 12;12 lakini huwezi kuthibitisha
2. Alifundisha kwa
mifgano ili kuwasilisha kweli
Mara nyingi ni rahisi kujifunza kwa
kulinganisha mambo kitu kipya kinapowasilishwa katika namna ambayo inalingana
na kitu kinachofahamika tunajifunza kwa
urahisi na kukumbuka vizuri na hii ndio maana pamoja na kuwa Yesu alimtumia
mifano bado leo mtu akiwasaidia wengine tunamuita Msamaria mwema hata kama
hatoki samaria kwa hivyo mifano hufanya
kweli ya Mungu kuweza kuzama ndani kwa urahisi na kukumbukwa mwalimu yeyote mzuri hutimia mifano kama
mjezi mzuri znavyotumia kichapio kujenga matofali karibu theluthi ya mafundisho
yote ya Bwana Yesu katika injili zote tatu zifananazo Synoptic gospel ni
mifano.
3. Alifundisha kwa
Mifano kwa sababu mifano inafanya kweli iweze kupenya katika mioyo ya watu
Kwa kawaida watu hujilinda wasiumizwe
na neno ambalo huwachoma na mtu akijua kuwa unamkosoa ni rahisi kufunga moyo
wake ili kupingana au kujilinda na kukosolewa hili ni jambo la kawaida katika
maisha ya kibinadamu lakini inasemekana
kuwa watu wengi sana wanapenda Stori kwa msingi huo unapotumia mifano kweli
hufika ndani ya mtu bila kuleta madara mfano anagaluia alichokifanya nathani
alipokwenda kuonya dhambi ya Daudi 2 Samuel 12;1-4 Daudi aliamua kumuhukumu mtu
huyo aliyetenda jambo lile na kumbe alikuwa akijihukumu mwenyewe kwa hivyo ili
mtu asijilinde afungue moyo stori zinafaa kupenyeza ukweli
4. Yesu alimtumia
mifano kama njia ya hukumu
Matahayo 13;10-15,
“Wanafunzi wake
wakamwendea wakamwuliza,“Kwa nini unasema na watu kwa mifano?’’ Akawajibu,
“Ninyi mmepewa kuzifahamu siri za Ufalme wa Mbinguni, lakini wao sivyo. Kwa
maana yule aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele, lakini yule
asiye na kitu, hata kile alichonacho atanyang'anywa. Hii ndiyo sababu nasema
nao kwa mifano: ‘‘Ingawa wanatazama, hawaoni, wanasikiliza, lakini hawasikii,
wala hawaelewi. Kwao unatimia ule unabii wa Isaya aliposema: ‘‘‘Hakika
mtasikiliza lakini hamtaelewa, na pia mtatazama lakini hamtaona. Kwa maana
mioyo ya watu hawa imekuwa mizito, hawasikii kwa masikio yao, na wamefumba macho
yao. Wasije wakaona kwa macho yao, wakasikia kwa masikio yao, wakaelewa kwa
mioyo yao, wakageuka, nami nikawaponya.’
Yesu
alimtumia mifano kama njia ya hukumu ilikuwa ni kama Password au kufuli maalumu
la kuifunga kweli na ni watu wenye shsuku ya dhati tu ambao wangeweza
kuzigundua kweli za ufalme wa Mungu na mtu aliye puuzia angetoka akiwa mtupu
matahayo 13;12-13, wayahudi walikuwa wameifanya mioyo yao kuwa migumu na walifunga masikio na mcho yao ili wasiwasikilize manabii Kwa msingi huo Yesu hakutaka kuwaongezea kitu
wale waliokuwa wameikataa kweli na hivyo aliificha kweli katika mifano kama sehemu ya hukumu kwa ajili ya kuasi kwao
C. Jinsi mifano ilivyotumika vibaya
Kwa Muda
mrefu mifano imetumika vibaya au imatafasiriwa visivyo halali kuliko Maandiko
mengine yoyote ukiondoa kitabu cha Ufunuo,wakati fulani katika historia ya
kanisa mifano ilikuwa ikitafasiriwa kirohoroho Allegorizing hii ni njia mbaya
na sio halali ki hermeneutics tunapo ruhusu kila kieneo cha mfano kutumika
kuwakilisha kitu kingine hapo ndipo
tunapokuwa hatuhubiri tena neno la Mungu wala hatufundishi tena neno la
Mungu kwani tunakuwa tuko mbali na maana
iliyokuwa imekusudiwa na Mwandishi na tunakuwa tumeongoza katika kile ambacho
Mungu hakukikusudia na huo sio uaminifu
kwa kusudi ambalo hata Bwana Yesu mwenyewe alikuwa amelikusudia kupitia mfano
huo katika karne ya kwanza Augustino alijaribu kutafasiri mfano wa msamaria
mwema kirohoroho na hivi ndivyo alivyofundisha
Mtu moja aliyekuwa anatoka
Yerusalemu kwenda Yeriko ni mwanadamu
Yerusalemu ndio mji wa mbinguni wa
amani ambapo Adamu alianguka
Yeriko inawakilisha kurudi nyuma
Wevi wanawakilisha Shetani na mapepo
Kumpiga inawakilisha kumshinda
katika dhambi
Kumuachia inawakilisha kufa kiroho
Kupita kwa mlawi kunawakilisha
huduma ya kikuhani ya agano la kale
Msamaria anamwakilisha Kristo
Kumfunga majeraha kunawakilisha
kusamehe dhambi zake
Kumpaka mafuta kunawakilisha
faraja ya Roho
Kumpeleka kwa watunzaji ni
kumuachia kwa kanisa
Ingawaje mfano umefafanuliwa kwa namna
ya kusisimua sana hiki sicho Yesu alichokuwa amekikusudia kukisema kwa kuwa
sasa tunajua kwanini Yesu alimtumia mifano na tunajua kwanini si vema
kuinyambulisha kwa mtindo huo ni muhimu basi kwa kila mtafasiri wa Biblia
kujifunza namna ya kuitafasiri mifano kwa halali
Jinsi ya kutafasiri mifano
Kuna hatua kubwa tatu za jinsi ya
kuitafasiri mifano kwa usahii
1. Tafuta historia
ya mazingira ya mfano
2. Tambua maana ya
mafumbo na malengo katika mfano
3. Tambua kuwa
kuna somo moja kubwa ambao mfano huo unalenga kufundisha
TAFUTA HISTORIA YA MAZINGIRA YA MFANO
Ni muhimu kukumbuka historia ya
mazingira ya mfano yaani mazingira ya asili ya eneo ambalo mfano umetolewa kwa
hivyo ni muhimu kila wakati kujiuliza mazingira ya kihistoria ya mfano, jiulize
Yesu alikuwa akamwambia nani mfano huo na kwanini Yesu alimtumia mfano huo kwa
mfano kwa habari ya mfano huu wa msamaria
1. Yesu alikuwa
akamwambia nani mfano huo?
Jibu alikuwa
akijibu swali la mwalimu wa sheria Luka 10; 25-30
2. Kwanini Yesu
alitoa mfano wa Msamaria?
Jibu kwa sababu
mwalimu wa sheria alimjaribu Yesu Luka 10; 25, mwalimu huyu pia alikuwa
akijaribu kujitafutia haki yeye mwenyewe kwa hivyo aliuliza Jirani yangu ni
nani? Luka 10; 29 Kwa msingi huo Yesu alimtumia mfano kujibu swali la mwana
sheria na kujaribu kuweka wazi tabia yake ya kujihesabia haki jinsi ilivyo
tofauti na mtazamo wa Mungu
TAMBUA MAANA YA MAFUMBO NA MALENGO
KATIKA MFANO
Katika ulimwengu huu tulio nao kuna milima na
vilima watu hawapendi kutoa kipaumbele kuangalia vilima kwa sababu ni vidogo na
ni vya kawaida watu huangalia mlima zaidi kwa sababu ni mikubwa na ni nadra
milima ina mvuto maalumu kwetu kwa msingi huo basi ni muhimu kufahamu kuwa
katika mifano kuna vilima na milima mifano ina fafanuzi nyingi ambayo ni sawa
na vilima fafanuzi hizo katika mifano kwa kawaida havina maana wala
haviwakilishi kweli fulani ya aina yoyote, Lakini kwa njia nyingine Mifano ina maana
kuu mbili au tatu kuu ambazo ni mambo ya msingi ya mlima wenyewe kwa mfano
katika mfano huu wa msamaria kuna pints kama tatu za msingi zinazosaidia
kuuelewa mfano wenyewe
·
Mtu aliyejeruhiwa anawakilisha mtu mwenye mahitaji
·
Msamaria anawakilisha jirani wa kweli anayejali
·
Kuhani na mlawi wanawakilisha majirani wasio jali
Ndani ya mfano huu pia kuna vilima
vingi kama Yerusalem, Yeriko njiani, punda, mtunzaji, malipo n.k , lakini hivi
sio vya maana viko kwa ajili ya kujenga mfano na hivyo ukijaribu kuanza
kuvitfasiri vinaweza kutupeleka mbali katika kuifasiri mifano kwa halali kwa
msingi huo tofautisha vilima na mlima kama sheria kuu ya kukuongoza kutafasiri
mifano ukikumbuka kuwa kunaweza kuwako points mbili au tatu za kukusaidia
kupata kweli ya mfano husika
TAMBUA KUWA KUNA SOMO MOJA KUBWA AMBAO
MFANO HUO UNALENGA KUFUNDISHA
Yesu alitoa mifano ili kuwakilisha
ukweli moja kuu kwa msingi huo unapaswa uweze kuelezea katika sentensi moja tu
maana ya mfano, kwa mafano kwa swala la mfano wa msamaria somo
“Jirani wa kweli” usijaribu
kutengeneza maana zaidi ya moja ya katika mfano wahubiri wote wazuri na waalimu
wazuri wa neno la Mungu hutimia mifano ili kukazia kweli katika mfano
wanaotumia mara nyingi mfano moja hutumika kukazia kweli moja na sio vinginevyo
kwa msingi huo unapoigundua kweli moja tu amabayo mafano huo unafundisha
usijaribu kuiharibu Elimu yako ua Hermeneutics kwa kutafuta maana nyingine
Taifa lina mji mkuu mmoja tu na mifano ina kweli moja tu inayowakilishwa
KUTAFASIRI NA KUITUMIA MIFANO
Kuna tofauti kubwa kati ya kutafasiri
na kutumia mifano ktafasiri ni kufanya kazi ya kutafuta maana na baada ya
kutafuta maana unatakiwa uitumie kwa hivyo baada ya kuwa umepata maana kwa
mfano wa mfano wa msamaria unapaswa kuitumia kwa watu kwa kuwahamasiha kwamba
washufghulike na watu wenye mahitaji kumbuka Yesu alipomaliza kutoa mfano
alisema “ Enenda ukatende vivyo hivyo” kwa msingi huo si vema kuwapita watu
wenye uhitaji kwa kufanya hivyo utakuwa umeitendea haki mifano Yesu aliyokuwa
akiifundisha
KANUNI YA KUTAFASIRI MASWALA YA UNABII
(PROPHECY)
Kutafasiri unabii kunahitaji uwe
mnyenyekevu huku ukizingatia Historia ya mazingira, lugha za mafumbo na sheria
ya kujirudia kwa unabii Multiple Fulfillment kutafasiri unabii na vifungu
vinavyohusu unabii ndio moja ya sehemu ngumu sana katika kuilewa Biblia
A.
Huduma za Manabii na wajibu wa nabii
Nabii alikuwa ni mnenaji kwa niaba ya
Mungu ilikuwa ni sauti ya Mungu, wao walisubiri mpaka neno la Mungu lilipokuja
kwao kisha walisimama na kusema kwa mamlaka Asema Bwana wa majeshi, Kusudi
kubwa la unabii wakati wote ilikuwa ni
kuwasaidia watu wa Mungu kumjua Mungu na kuyajua mapenzi yake waliifanya hivyo kwa kutabiri na kwa kufundisha , moja ya mifano ya
kutabiri au kuelezea mambo yajayo ni Isaya 9;6 “Maana kwa ajili yetu mtoto
amezaliwa tumepewa mtoto Mwanamume na uweza wa kifalme utakuwa begeni mwake
naye ataitwa mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, mfalme wa
amani “ Isaya alitoa unabii huu nyuma ya miaka karibu au zaidi ya 750 hivi
lakini anasema kwa ajili yetu kwa hivyo wakati mwingine waandishi wa Biblia
walizungumza wakati ujao kama wakati
ulioko ndani ya Agano la kale kuna nabii nyingi sana kama zile za
·
Kuelekea urtumwani kwa watu wa Mungu,
kuokolewa kwao ,kurudi na kutawanywa kwao duniani
·
Kuzaliwa , kuteseka , kufa na kufufuka
kwa Masihi,kuja kwake mara ya pili na ufalme wake milele
Kadhalika katika agano jipya kuna nabii
nyingi za nyakati zile na nayakati zijazo kwa mfano Njaa ya Yerusalem,
kukamatwa na kufungwa kwa Paulo, kubomolewa kwa Yerusalem na nayakati za mwisho
kwa msingi huo aidha nabii alitabiri katika agano la kale au jipya kusudi
linabaki lilelile kuwa ni kuwasaidia watu kumjua Mungu na kuyajua mapenzi yake
kwa hivyo huduma ya kinabii ilihusisha kufundisha na kutabiri yaani kulisema
neno la Mungu kwa jamii iliyokuweko na itakayokuja.
B.
Chunguza mazingira ya kihistoria ya
unabii
Hatuna Vitabu vya unabii kutoka kwa
Ibrahimu aliyeishi miaka 1800 K.K mpaka kwa Daudi aliyeishi miaka 1000 K.K
Vitabu karibu 16 vyote vya kinabii katika agano la kale viliandikwa kati ya
miaka 750 – 460 hivi miaka hii ilifunikwa na maswala ya kisiasa,vita,uchumi na
mamabadiliko katika jamii na kulikuwa na hali za kutokumcha Mungu na kulivunja
agano la Mungu alilowapa kupitia Musa mtumishi
wake watu walikuwa wakiongezeka
na mipaka ilikuwa ikibadilika kwa msingi huo Mungu aliwainua Manabii
kuwakumbusha Israel agano lake .
Sasa basi ilikuvielewa Vitabu vya
kinabii vyote 16 vya agano la kale inakupasa kujua historia ya mazingira ya
unabii ulikotolewa jiulize maswali muhimu yafuiatayo
1. Unabii
ulitolewa kwa nani Israel au Yuda?
2. Unabii
ulitolewa wakati gani? Kabla au baada ya kupelekwa utumwani?
3. Kwa
nini unabii ulitolewa ni kwa ajili ya kuwataka watubu au kuwatia moyo? Baada ya
kujiuliza maswali ya muhimu kama hayo ndipo sasa unaweza kujua vema mazingira
ya unabii yalikuwa ya jinsi gani?
C.
Chunguza Lugha za mafumbo ndni ya
unabii
Tulizungumza awali kuwa ikiwezekana
kila kifungo cha Maandiko kitafasiriwe kama kilivyo kwa njia rahisi na ya
kawaida Lakini kwa maswala ya unabii
wakati mwingine ni lazima upambanue mafumbo Vitabu vingi vya kinabii kama
Ezekiel,Daniel na Zekaria vina utajiri wa mafumbo na katika agano jipya kitabu
cha Ufunuo wa Yohana nacho kina lugha
nyingi za mafumbo tunapaswa kuyaelewa vema kwa mfano hebu angalia mafumbo
yaliyoko katika Ufunuo wa Yohana na maana zake kama yalivyoainishwa na moja ya
wasomi
·
Nyota saba 1; 16 zinawakilisha malaika
saba 1; 20
·
Taa yenye vinara saba 1; 13
inawakilisha makanisa Saba 1; 20
·
Mana iliyofichwa 2; 17 inawakilisha
utukufu wa Yesu Kristo Kutoka 16; 33-34.Waebrania 9; 4
·
Nyota ya asubuhi 2; 28 inawakilisha
kurudi kwa Yesu kabla ya kuja kutawala Ufunuo 22; 16,2Petro 1; 19
·
Ufunguo wa Daudi 3; 7 unawakilisha
nguvu ya kufunga na kufungua Isaya 22; 22
·
Taa Saba za moto roho Saba za Mungu 4;
5
·
Wenye uhai 4; 7 wanawakilisha tabia ya
Mungu na macho saba yanawakilisha Ufunuo kamili wa Roho wa Mungu 5;6
·
Chetezo cha dhahabu kinawakilisha
Maombi ya watakatifu 5; 8
·
Farasi na wapanda farasi 6;1
zinawakilisha mpangilio wa matukio ya takayoendelea wakati wa dhiki kuu
·
Nyota iliyoanguka 9; 1 inawakilisha
Shetani 9; 11
·
Nyota za mbinguni 12;4 inawakilisha
malaika walioanguka 12;9
·
Mwanamke na mtoto 12;1-2 inawakilisha
Israel na Kristo 12;5-6
·
Shetani anatajwa kama dragoni kama
nyoka wa zamani na shetani 12;9,20;2
·
Nyakati na nayakati na Nusu ya nyakati 12;14
ni sawa na siku 1260 12;6
·
Myama kutoka Baharini 13;1-10 mtawala
ajaye kutoka ulimwenguni na tawala zake
·
Mnyama kutoka katika inchi 13;11-17
Nabii wa uongo 19;20
·
Kahaba
17;1 unaelezwa kama mji mkubwa 17;18kama babeli mkubwa 17;5 kama
aketiywe juu ya vilima 17;9, inatafasiriwa kama wakristo waliorudi nyuma
·
Maji 17;1inawakilisha watu wa ulimwengu
huu17;15
·
Pembe 17;12 falme kumi zinazoambatana
na yule mnyama na mengineyo mengi .
Jambo la muhimu tunaloliona hapa ni
kuwa wakati mwingine Biblia inatabiya ya kutafasiri yenyewe lugha zile za
kimafumbo kwa mfano Yohana mwenyewe
anatuambia kuwa Zile nyota saba ni
malaika saba 1;16, na 1;20 kwa msingi huo pale inapotokea kuwa maana
imetolewa na mwandishi mwenyewe tunaweza kuhubiri kwa ujasiri na kwa furaha lakini wakati mwingine historia itatusaidia
namna ya kuweza kutafasiri mafumbo hayo kwa mfano wa ile ndoto ya
nebuchadneza ambapo tunajifunza falme
zilizofuata baada ya Babeli lakini pale unapokutana na mafumbo magumu
usiyoyafahamu basi haya ni mambo ya msingi ya kuzingatia
1.
Tafasiri katika hali ya kawaida na
rahisi mfano Mika 5;2 Masihi atazaliwa Bethelehemu hili liko wazi
2.
Tafasiri kwa kuzingatia kuwa kuna lugha
za mafumbo kwa mfano Malaki alitabiri kuja kwa matangulizi wa masihi na
alimtaja kuwa ni Eliya Malaki 4;5-6 Lakini nabii aliyetokea kumtangulia masihi
alikuwa Yohana Mbatizaji Yohana 1;21 na Kristo alikubaliana nalo Yohana
17;10-13 Yohana mwenyewe alisema mimi siye Eliya Lakini Yesu alisema ndiye
3.
Chunguza na kufahamu kuwa unabii una
tabia ya kutumia zaidi ya mara moja kwa mfano Kwa ajili yetu mtoto amezaliwa
Isaya 9;6 Ni kweli mtoto Yesu alizaliwa kwa ajili yetu lakini wakati huu uweza
wa kifalme haukuwa Begani mwake mpaka ajapo mara ya pili kwa hiyo sehemu ya
unabii umetimia na sehemu bado na mara nyingi Manabii walipotabiri kuhusu kuja
kwa Yesu hawakutofautisha ni ujio upi wa kwanza au wa pili hii ni kwa sababu
inasemekana wao waliona ujio wa Yesu kama mlima mmoja kumbe kulikuwa na milima
miwili
Mlima
wa Kalivari Mlima wa mizeituni
Mathayo 27; 33 Zekaria 14;4
Zaidi ya miaka 2000
Idadi ya milima
inategemea ni wapi wewe umesimama Manabii wengi walizungumza nabii za kuja kwa
masihi kama kitu kimoja sawa na mtu aliyekuwa anaona mlima mmoja kumbe iko
milima miwili Kielelezo kwaniaba ya Maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote Home
Bible library 2010 Mwalimu wa somo hili
D. Onyesha
roho ya unyenyekevu unaposoma na kutafasiri unabii
Kuna wakati kijana mmoja alijidai kuwa ana majibu yote kwa
habari ya maswala ya unabii na alipofundisha kila kitu alionekana akihitimisha
kwa kusema asema Bwana wa majeshi na hakutaka hata kidogo mijadala wala
kukosolewa na akamwambia mtu mmoja aliyekuwa akimkosoa kuwa nikisema hauko
sahihi maana yake hauko sahii kijana huyu alifikia hata kuweka tarehe ya April
2 kuwa ndiyo ilikuwa tarehe sahii kwa ujio wa masihi kwa mujibu wa kitabu cha
Daniel alichokuwa akikifundisha , siku moja usiku aliota ndoto akiwa yuko
mbinguni na aliona mambo mazuri ya ajabu na mziki mzuri pamoja na kumuona Bwana
Yesu akiwa ameketi katika kiti chake cha Enzi kwa unyenyekevu sana na mara
akasikia mtu akimshika katika bega na kumwambia ndugu umekuwa ukifundisha
maswala ya unabii ambao hata mimi Yesu mwenyewe sijawahi kuwatuma Manabii
wafanye hayo je unaweza kunielezea kwa ufupi kile unachokifundisha kabla
sijakuruhusu kurudi duniani kisha jamaa alistuka na kumbe ilikuwa ndoto Tangu
wakati huu ndugu huyu alijifunza kuwa mnyenyekevu na kuwa na tabia ya
kuwasikiliza na wengine
Kwa ujumla katika Eneo hili tumejifunza maswala ya muhimu Matano
1. Kutafuta
historia ya Unabii
2. Kutambua
lugha ya mficho iliyotumika katika unabii
3. Kuamua
kama unabii huu unapaswa kutafasiriwa kwa urahisi na kawaida au kama fumbo
4. Kukumbuka
kuwa unabii una tabia ya kutumia zaidi yamara moja
5. Kuwa
na tabia ya unyenyekevu unapotafasiri maswala ya unabii
MAMBO
YA MSINGI YA KUYAZINGATIA KATIKA KUTAKA KUIFAHAMU BIBLIA NA KUITAFASIRI KWA
HALALI.
Soma Biblia kwa kujiuliza maswali
Mtafasiri mzuri wa Biblia anapaswa kusoma Biblia kwanza kwa kujiuliza maswali
ili baadaye afanye kazi ya kuyajibu na kuyachanganua ili kutafasiri Biblia kwa
halali Kuna maswali mengi ya kujiuliza Mtu anapokuwa anaisoma Biblia miongoni
mwa mambo ambayo unaweza kujiuliza ni pamoja na
·
Kwa nini Daudi alikwenda kuwasaidia
wafilisti? 1Samuel 27;1-7
·
Tarshishi iko wapi na kwanini Yona
alitaka kwenda huko? Yona 1;3
·
Inakuwaje Yesu alikasirika na kuwatoa
nje wababdilisha Fedha kipi kilikuwa si sahii Mathayo 21;12-13
·
Kwa nini mwanamke msamaria Alisha ngaa
Yesu kuzungumzia naye Yohana 4
·
Je Viongozi wa kiyahudi walimtisha
Pilato alipotaka kumwacha Yesu huru? Yohana 19;12-13
·
Mwiba wa Paulo ulikuwa ni nini?
2Koritho 12,7-9
·
Kwanini Daudi alibaki Yerusalemu wakati
majeshi yake yalipokuwa yamekwenmda vitani ? 2samuel 11;1
·
Je ni kweli Ezekiel alitabiri kuwa
urusi itaivamia Israel? Ezekiel 38-39
·
Sanamu aliyoiona Nebukadreza katika
ndoto ilikuwa ina maana gani Daniel 2
·
Ni nini Ishara ya mti wa mtini katika
Matahyo 24;34
·
Kwanini Yesu anatumia siku za Nuhu
kuoanisha na kuja kwake mara ya pili?Matahyo 24;37-39
·
Je wale waliotiwa muhuri yaani 144000
ni akina nani huko mbinguni Ufunuo 7
·
Kwa maana gani Yakobo alizaliwa akiwa
amesmhika Esai kisigino?Mwanzo 25;26
·
Yesu alikuwa ana maana gani kusema
atalijenga kanisa lake juu ya Petro Mathayo 16;18
·
Mwandishi wa zaburi anasema Mungu yuko
kila mahali hatya kuzimu ana maana gani? Zaburi 139;8
·
Je Yesu aliweka kiwango cha kusamehe
tunapokuwa tumekosewa na wenzetu? Mathayo 18;22
·
Kwa Nini Mungu ambaye aliupenda
ulimwengu wote aseme nimempenda Yakobo lakini nimemchukia Esae?Malaki 1;2-3
·
Kwanini Ni rahisi kwa ngamia kuopenya
katika tundu ya sindano? Luka 18;23-25
·
Je Yesu aliposema ombeni lolote kwa
jina langu je tunaweza kuomba jambo Baya? Yohana 14;14
·
Inakuwaje watu wa kila taifa walikuwako
Yerusalemu siku ya Pentekoste? Matedno 2;5
·
Kwanini jina Nyota ya alfajiri
lilitumika kwa shetani na pia linatumika kwa Yesu? Isaya 14;12
·
Kwanini Yohana alimtumia namba 666 kama
alama ya mpinga Kristo? Ufunuo 13;18
·
Kwanini Adamu na Hawa hawakufa mara
baada ya kutokumtii Mungu Mwanzo 2;15-17
·
Je kaini aliwekwa alama ya namna Gani?
Mwanzo 4;3-4
·
Kaini alioa mke kutoka wapi? Mwanzo 4;17
·
Kwanini Mababa kabla ya Gharika
walioishi miaka mingi sana ? Mwanzo 5
·
Hao wanefili ni akina nani Mwanzo 6;1-4
·
Je Gharika ilikuwa ya ulimwengu mzima?
Kama ndio wanyama walifikaje kwenye visiwa?
·
Kwanini Kanaani alilaaniwa wakati
dhambi ilikuwa ya baba yake? Mwanzo 9;25-27
·
Kama Esau alimsamehe Yakobo na alikuwa
na amani naye kwanini alikuja kumpokea na watu wa vita 400 Mwanzo 32;6
·
Kwanini Mungu aliruhusu Yefta kuweka
nadhiri ngumu na kumtoa mwanae sadaka ya kuteketezwa? Waamuzi 11
·
Nini kilipelekea Isarel kuhitaji mfalme
Mwanadamu kama Mungu alikuwa Mfalme wao? 1Samuel 8
·
Kwanini Mungu alimchagua Sauli nkisha
akamkataa je si alifanya makosa kwa kumchagua kisha akabadili mawazo? 1Samuel
10-12
·
Je Elisha alikuwa mara mbili zaidi ya
Eliya 2Wafalme 2;9-14.
·
Kwanini Mungu aliruhusu Ayubu kuteseka
huku anajua kuwa alikuwa mwenye haki Ayubu 2;3,6
·
Je inawezekana mtu aliyeokoka akapoteza
wokovu Waebrania 6;4-12
·
Kama kunywa ni dhambi kwanini Yesu
mwenyewe alitengeneza Divai? Yohana
2;1-11,1Timotheop 5;23
·
Paulo anafundisha kuwa wanawake wawatii
waume zao jambo hili lina maana gani? Efeso 5;22-33
·
Kwa namna Gani Yakobo na Ayubu wanasema
walimuona Mungu na Yohana anasema hakuna mtu aliyewahi kumuona Mungu wakati
wowote hili lina maana Gani
·
Kama Paulo hakuruhusu wanawake kuwa na
mamlaka juu ya wanaumeKanisani kwanini wanasimikwa leo?
Maswala ya msingi ya kuyazingatia
wakati wa kutafasiri Maandiko
·
Kumbuka kutafasiri kama ilivyoandikwa
ni moja ya njia nzuri ya kutafasiri kwa usahii
·
Usitafasiri mafumbo katika hali ya
kawaida
·
Acha Maandiko yajitafasiri Yenyewe
·
Usijenge fundisho katika mstari wenye
utata au ulio mgumu
·
Achilia fundisho lililo sahii lisaidie
kujua kile kisichoeleweka
·
Tafasiri yoyote ya Maandiko itokane na
Maandiko
·
Usitumie andiko gumu kutafasiri andiko
gumu
·
Unapokutana na majina ya ukoo fulani
lazima ujiulize kusudi lake
·
Usitumie maswala ya kihistoria kujenga
fundisho
·
Usipindishe ukweli wa Maandiko kwa
ajili ya kukwepa hitimisho lisilo pendeza
·
Usitafasiri mafumbo kupitiliza au
kupita kiasi chake
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni