******************************************************************
Somo; Jinsi ya kuliongoza kanisa
Tunaendelea
kujifunza Mfululizo huu wa Masomo maalumu yahusuyo uongozi na sasa tunajifunza
somo hili Jinsi ya kuliongoza kanisa la Mungu tutajifunza somo hili pia kwa
kuzingatia vipengele viwili
Hatari
ya kuwa na Viongozi vipofu katika kanisa
Jinsi
ya kuliongoza kanisa.
Hatari ya kuwa na
Viongozi vipofu katika kanisa
Ni hatari kubwa kama tutakuwa na Viongozi
vipofu katika kanisa. kipofu alimuongoza kipofu mwenzake watatumbukia shimoni
wote wawili Luka 6;39 kwa kukosa akili au Ufahamu wa jinsi ya kuliongoza kanisa
sisi nasi tunaweza Kuhesabiwa miongoni mwa vipofu Mathayo 15;14-16 ilitupate
Ufahamu wa kutosha kuhusu kuliongoza kanisa tutachukua muda mwingi katika somo
hili kujifunza mambo kadhaa wakadhaa yahusuyo jinsi ya kuliongoza kanisa.
Jinsi ya kuliongoza
Kanisa.
Yako mambo kadhaa ambayo ni muhimu
kuyaangalia na kuyazingatia kwa makini ili tupate mafanikio yanayokusudiwa
katika kuliongoza kanisa
- Kujiamini.
Mungu anapokuwa ametuchagua
kuliongoza kanisa tunaweza kujikuta kuwa tuna umri mdogo kuliko wale
tunaowaongoza, hii sio ajabu Musa alikuwa mdogo kuliko kaka yake Haruni Lakini
ni Mungu aliyemchagua Musa aliye mdogo kumuongoza kaka yake Kutoka 7;7 sio hilo
tu Mungu aliwachagua Viongozi waliokuwa na umri mdogo mno na Biblia inaonyesha kuwa wengi kati ya hao
waliongoza vizuri na kwa mafanikio makubwa
Mfano ni Yoashi aliyeongoza akiwa na miaka saba 2Nyakati 24;1-2 Yosia
alinza kuwa kiongozi akiwa na umri wa miaka nane 2 Nyakati 34;1-2 Uzia alikuwa
na umri wa miaka 16 2Nyakati 26;3-4 Yothamu na Hezekia woote walikuwa na umri
wa miaka 25, 2Nyakati 27;1-2,29;1-2. Timotheo naye alikuwa kijana mdogo tu kama
Yeremia alipoanza kuongoza 1Timotheo 4;11-12,Yeremia 1;4-7 tunaweza kuwa sio tu
na umri mdogo Lakini pia Elimu ndogo kuliko wale tunaowaongoza hii pia sio
ajabu Viongozi wakubwa wa kanisa, Petro na Yohana walikuwa ni watu ambao walikuwa hawana Elimu
wala maarifa Matendo 4;13 lakini
waliifanya kazi ya Mungu kwa ujasiri na kuliongoza kanisa. Hatupaswi kamwe
kujidharau wala kubabaika kutokana na
vigezo hivyo vya kibinadamu tunapaswa Kujiamini na Mungu atawatiisha chini yako
wazee na wasomi nao watakusikiliza
kumbuka kuwa si sisi tuliojichagua wenyewe na kuwa ni Mungu ndiye
aliyetuchagua hivyo yu aweza kutupa uwezo wa kuongoza na kulisimamia kanisa
lake Yohana 15;16,Zekaria 4;6;Wafilipi 4;13 kwa sababu hiyo yeye aliye dhaifu
na aseme mimi ni Hodari maana uhodari wetu uko katika Bwana aliye tuwezesha maana amesema atakuwa pamoja
nasikatika utumishi wetu woote Yoel 3;10, 1Nyakati 28;20, Mathayo 28;19-20.
- Kuwa na utii uliotimia kwa Viongozi wetu wa juu.
Uasi wa namna yoyote kwa kiongozi wetu wa juu unamfanya Roho Mtakatifu
atuache, wakati wowote ni muhimu kwa Viongozi wa kanisa kuhakikisha kuwa
wanawatii Viongozi wao wa juu na wajuu wanawatii wale wa juu, utii huu ni kama
ule utii wa jeshini ni utii usio na
ubishi wala majadiliano hata kama moyoni
unadhani kuwa agizo hilo lina dosari, mradi sio agizo la kufanya dhambi ni muhimu kulitii kwanza tukijiona kuwa tuna kitu chochote cha ziada
kuliko kiongozi wetu wa juu na kuacha
kumtii basi Roho Mtakatifu anatuacha Barnaba alipoacha kumtii kiongozi wake
Paulo na kushindana naye kuanzia hapo Roho wa Mungu aliacha kutupa historia
yake akiwa na Marko Bali Roho anatupa ripoti ya Paulo na wale aliofuatana nao
katika utumishi yaani Silla na Timotheo Matendo 15;36-41,16;1-3 kama Viongozi
wa kanisa tunataka kuona Roho wa Mungu akiwa pamoja nasi na kututumia katika
viwango vya kupita kawaida basi siri ni utii uliotimia 2Koritho 10;4-6.na
tatizo la Viongozi wengi katika makanisa ya kiroho shida yao kuu ni kukosa utii
na hasa utii uliotimia, Viongozi wengi watataka kufanya kazi kwa kusukumwa
sukumwa tu na kwa msingi huo utendaji wa Mungu na karama za Roho Mtakatifu
hufifia Bwana ampe neema kila mmoja wetu kuwa mtii na kuzidi katika Yesu
- Kuwaongoza watu kwa kutumia maombi
Kiongozi wa kanisa hana budi kuwa mtu muombaji siku zote akiwaombea wale
anaowaongoza kwa kuwataja majina na
kuwaombea juu ya udhaifu walio nao, tukiwa tunapenda kufoka tu bila maombi ya
kutosha pamoja na kufoka kwetu sana
tutaona mambo hayatendi kama inavyokusudiwa Yeremia 31;9 kuomba ni kumhudumia
bwana inatupasa kumhudumia bwana zaidi kabla ya kuwahudumia watu tunao waongoza
ili tuone mafanikio maombi ni kama mafuta yanayolainisha msuguano au ugumu wa
mioyo ya watu tunaowaongoza bila maombi ya kutosha kanisa letu haliwezi kukua
kiidadi na pia wale tunaowaongoza hawawezi kukua kiroho na watadumaa kadiri mtu anavyopewa majukumu makubwa ndivyo
anavyopaswa kuomba zaidi maombi husaidia kunyonya kiburi cha kibinadamu
tukipenda kuwahudumia watu bila maombi ya kutosha ni rahisi kujidhuru kiroho sisi wenyewe
- Kuacha kuongoza pale tunapokuwa vipofu.
Katika sheria za usalama
barabarani dereva anashauriwa kusimamia
ikiwa haoni vizuri mbele kutokana na ukungu au moshi n.k vilevile dereva
anashauriwa kuegesha gari pembeni na
kulala ikiwa anaona usingizi Dereva
akipuuzia ushauri huo ni rahisi kupoteza maisha
vivyo hivyo kama Viongozi wa kanisa hatupaswi kumshauri mtu kitu ambacho
hatuna uhakika nacho tukiwashauri watu makosa tutapata adhabu iliyo kubwa
zaidi Yakobo 3;1,Mathayo 18;6-7 lolote
lile tusilokuwa na uhakika nalo ni vema kuulizwa kwa uongozi wa juu zaidi kisha
kutoa majibu yapasayo hivyo ni muhimu
kuacha kufanya jambo lolote tusilolifahamu vema.
- Kuongoza kwa neno la Mungu
Tukiona lolote kwa wale tunaowaongoza lisilofaa inatupasa kutumia neno
la Mungu kulirekebisha kwa upendo na sio
Maneno matupu ya kibinadamu Neno la Mungu lina uwezo mkubwa wa kumbadilisha mtu
wala sio adhabu zetu au Maneno yetu ya kuumiza mwanadamu huwezwa na Mungu tu
Maneno ya kibinadamu husukumia tatizo kuzidi Mithali 6;21-23; 2timotheo
3;16-17,4;2.
- Kutokubali kuvunjika moyo.
Adui Ibilisi humwandama kiongozi wa kanisa na kutumia kila aina ya mbinu
ili kumvunja moyo, iwe ni kwa matatizo ya kikazi, kifamilia au kibiashara,
kusengenywa, kunenewa vibaya kwa kila aina ya Maneno, n.k na wakati mwingine atatuonyesha hali za
kutokufanikiwa kwa njia mbalimbali hata kukuonyesha jinsi kanisa lako
lisivyokua na atakushauri ni afadhali
uache yamekushinda kamwe hatupaswi kusikiliza ujinga huo na
kukubali kuvunjika moyo kwa lolote hata kama tuna watu waili au mmoja katika
kanisa Endelea kuwalisha kwa uaminifu na tudumu katika kazi ya bwana kwa
uaminifu kwani kuna majira ya kupenda na kuvuna Matendo 21;9-14 Zaburi 126;5-6
Muhubiri 3;1-2 marufuku kukata tamaa tusikubali kuvunjika moyo kwa namna
yoyote.
- Kuongoza kwa Hekima.
Ni vigumu kuongoza kanisa la Mungu
huku hatuna Hekima Hekima inatusaidia kujua kuwa tuseme nini, tujibu nini au
tufanye nini na kwa wakati gani Hekima
ya Mungu ndio ufumbuzi wa tatizo hilo na hufumbua kwa amani Hekima humfanya mtu
ajue neno la kuzungumzia wakati Fulani na sio kuropoka tu na kusababisha
matatizo zaidi Mithali 25;11-12 kwa Hekima tunaweza kuwapa watu Elimu ya Mungu
Mithali 16;21 hekima hutupa kujua jinsi ya kuwashughulikia wazee Tofauti na
vijana n.k 1Timotheo 5;1 kwa sababu hii Suleimani alipofanywa kuwa mfalme jambo la kwanza lilikuwa ni kuomba Hekima
sisi na si ni muhimu kumuomba mungu atupe Hekima kila siku katika shughuli zetu za maongozi
2Nyakati 1;7-10,Yakobo 1;5.
- Kufanya kazi ya Mungu kwa bidii.
Hatuwezi kuwa na mafanikio makubwa katika kazi yoyote ya Bwana kama sisi
wenyewe ni watu wavivu au walegevu inahitajika bidii kubwa ili kufanikiwa
Yeremia 48;10 Warumi 12;11 hata hivyo ni muhimu kukumbuka kuwa na vipindi vya
mapumziko na kukumbuka kula chakula vizuri ili tusimpe ibilisi nafasi Marko
6;31-33.
- Kumbuka kuwaita moyo wale tunaowaongoza.
Kiongozi wa kanisa hapaswi kuwa mtu wa kuchokonoa mabaya tu ya kondoo
wake na kutaja mapungufu yao tu inatubidi pia kutafuta yale yaliyo meme hata
madogo na kuyainua hayo na kuwaita moyo na kuwapongeza kwa kawaida pongezi
humtia mtu moyo wa kufanya vizuri zaidi na husaidia kuondoa makosa makubwa ya
mtu na kufanya bidii zaidi 2samuel 11;22-25,Kumbukumbu 3;28.
- Kutangulia mbele ya Kondoo
Mchungaji hutangulia mbele ya kondoo wake kuongoza , hii maana yake ni
kuongoza kwa mfano huku ndio kuongoza kunakoleta mafanikio makubwa kiongozi
anayechelewa kufika mahali pa ibada na kuonyesha udhaifu Fulani Fulani huyo sio kiongozi anayewatangulia kondoo
Yohana 10;4 Waamuzi 5;2 Marko 10;22-25 Kumbukumbu 3;28.
- Kuwa na utayari wa kuwapa wengine majukumu
Kiongozi aliye botra hafanyi kazi yeye mwenyewe bali huwa tayari kuwapa
wengine majukumuhususani wale anaowaongoza na wakati mwingine hata wale
wachanga Kutoka 18;13-17.
- Kuheshimu mipaka ya madaraka uliyo nayo.
Mithali 22;28 ni muhimu kutakuwa na kimbelembele kwa mambo yasiyohusiana
na madaraka uliyo nayo fanaya kazi ndani ya mipaka yako mfano kama wewe sio
msomaji wa kanisa usipendelee kuzungumzia lolote kuhusu kanisa acha wenye
mamlaka kuu zaidi wazungumzie.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni