Mstari wa msingi Ufunuo 21;7 “Yeye
ashindaye atayarithi haya nami nitakuwa Mungu wake naye atakuwa mwanangu”
Yeye ashindaye
Safari ya mbinguni ni safari ya
mashindano;
Mara baada ya kuokoka unapaswa
kuwa na Ufahamu kuwa umeingia katika mashindano
ni yeye atakayeshinda ndiye atatakayeipokea taji ya milele na milele kila siku katika wokovu itakuwa ni siku ya
mashindano na vita lakini ni lazima
tushinde na kuumaliza mwendo kwa
kuilinda imani 2Timotheo 4;7-8
“Nimevipiga vita vilivyo vizuri
mwendo nimeumaliza imani nimeilinda baada ya hayo nimewekewa taji ya haki
ambayo Bwana muhukumu mwenye haki atanipa siku ile wala si mimi tu bali na watu
wote waliopenda kufunuliwa kwake”
Kwa msingi huo ni lazima kuvipiga
vita vya imani maana pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu Waebrania 11; 6
maisha ya wokovu ni maisha ya imani na kumtegemea Mungu katika kila jambo katika
maombi na neno la Mungu kinachotakiwa katika mashindano haya ni kujizuia katika
kila jambo linalokuja kinyume na mapenzi ya Mungu 1Koritho 9;25 “Na kila
ashindanaye katika michezo hujizuia
katika yote basi hao hufanya hivyo
kusudi wapokee taji iharibikayo bali sisi tupokee taji isiyoharibika”
Unaweza kushangaa kwamba wakati
unajiandaa kwenda ibadani ndipo wageni wanakujia tena wa muhimu ili usihudhurie
mafundisho kumbuka haya ni mashindano ni vita na inakupasa kupambana wageni waambie
twendeni kanisani pamoja kwa nini waje wakati unakwenda kanisani? Wakati
mwingine siku za ibada ndo kunatokea kila aina ya vikwazo na vizuizi jua hiyo
ni vita na kuwa adui yetu shetani yuko kazini kutuzuia tusiende kubarikiwa
kupitia maneno ya Mungu, uwe radhi kwenda ibadani hata kama ni mbali au kama
hauna nauli na utashangaa Baraka za Mungu zinamiminika kwako.
Siku zote kuanzia sasa lenga
kukua zaidi kiroho na katika wokovu usikose vipindi vya mafundisho kanisani kila unapopata nafasi soma Biblia na kufanya
maombi japo mafupi mafupi kwamba bwana
Yesu akusaidie kudumu katika wokovu na kushindana 1Timotheo 6;12 “Piga vita vile vizuri vya
imani shika uzima ule wa milele
ulioitiwa ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi” Tumia bidii uliyo
nayo usiwe mlegevu katika kujifunza uwe
na bidii yote Nunua daftari la kuandikia mafundisho yote na kuyatendea kazi na
uwe na tabia ya kuyapitia , uliza lolote kwa viongozi ambalo hujalielewa
vema Warumi 12;11 “ Kwa bidii si
walegevu mkiwa na juhudi katika roho zenu mkimtumikia Bwana” lolote
utakalojifunza lisiiishie katika dafatari bali ulifanyie kazi kwa vitendo ,
usiwe msikiaji wa neno tu bali mtendaji Yakobo 1;22-24 ni muhimu kustahimili siku hadi siku kwani tukistahimili tutamiliki pamoja naye
2Timotheo 2;12 Kama tukimkana yeye naye atatukana sisi.
Hatimaye tusikubali kabisa kurudi
nyuma katika wokovu tulioupokea usimkane Yesu halafu naye aje atukane sisi,
shindana hadi mwisho, Yako mengi mmno ambayo utazidi kujifunza kila siku
kanisani yashike na kuyatendea kazi , siku chache zijazo nawe utakuwa mwalimu
ukiwafundisha watu wengine waliookoka
nyuma yako ili nao wasimame katika
wokovu, simama kiume ni lazima ushinde katika jina la Yesu, zidi
kwenda kanisani kwa mafundisho mengine zaidi kumbuka Ufunuo 2;7 Yeye ashindaye nitampa kula matunda ya mti wa uzima ulio
katioka Bustani ya Mungu. Ubarikiwe sana Amen.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni