Ijumaa, 26 Februari 2016

Upendo wa Kwanza!



Nyakati hizi tulizonazo ni nyakati za mwisho , mwisho wa mambo yote umekaribia, Yesu kristo yu karibu kurudi, Yesu alitabiri kuwa katika nyakati hizi za mwisho upendo wa wengoi utapoa Mathayo 24:12, katika hizi nyakayti za mwisho, tunaambiwa kuwa upendo wa kweli kwa Mungu utatoweka, leo tutachukua muda kujifunza kutoika kwa kanisa la Efeso ambalo Kristo analionya kuwa wameuacha upendo wa kwanza hii ilikuwa na maana gani?

 Viwanja vya zamani vya Michezo ya Olympics huko Efeso Uturuki ya leo

Ufunuo 2:1-5 Katika mistari hii ingawa hatutaichambua yote , lakini tutakazia na kuangalia kwa nini Yesu analitaka kanisa lililoko Efeso kutubu na kurudia upendo wa kwanza Mstari 4-5 tuitajifunza somo hili kwa kuzingatia sehemu ku tatu zifuatazo

  • ·         Mazingira ya mji wa efeso
  • ·         Jinsi Kanisa la efeso lilivyopokea Injili
  • ·         Upendo wa Kwanza

Mazingira ya mji wa efeso
Mji wa efeso ulikuwa ni mji mkuu wa kibiashara na uliofunikwa na tamaduni za kiyunani katika asia ndogo, Mjii huu ulitumiwa kama bandari na njia ya watawala, Jina la mji wa Efeso maana yake ni wenye kutamaniwa , ulikuwa ni mji uliokaliwa na jamii kubwa ya Warumi, wayunani na wayahudi, ulikuwa ni mji wenye watu walioelimika sana na walikuwa wamejaa elimu za zamani za kiyunani na falsafa (SOPHIA) , kulikuwa na viwanja maarufu vya michezo ya Olympics ambao uko hata leo. Hata hivyo mjii huu ulikuwa mji uliojaa upagani uliokithiri na dini za uongo wa hali ya juu ulikuwa umeishika mji huu, Aidha kulikuwa na kaburi la Mungu mke wa kale aliyejulikana kama Anatolia, Pia kulikuwa na Ibada za sanamu ya miungu kama mungu mke aliyejulikana kama Artemis kwa kiyunani na Diana kwa Kirumi, 

 Sanamu ya mungu mke aliyejulikana kama Artemi au Diana huko Efeso akiwa na Maziwa mengi kifuani.

Mungu huyu alikuwa ni Mungu mwenye uso uliokuwa Mzuri sana ana alikuwa na chuchu za kunyonyeshea nyingi sana , alikuwa akitumikiwa na makuhani wa kike wapatao 1000 katika Hekalu lake  kama ilivyokuwa kwa mungu wa Koritho Aphodite, Artemi ni mungu aliyekuwa akihusika na uzao na ilikuwa inasadikiwa kuwa alitokea Mbinguni Matendo 19:28,35, aidha mji wa Efeso ulikuwa ni mji uliokuwa umejaa wapunga pepo na pia watu walijishughulisha sana  na mambo ya uchawi na Uganga na kwa ujumla ilikuwa ngumu sana watu kumuamini Mungu na kuokoka katika mji huu

Jinsi Kanisa la Efeso lilivyopokea Injili
Injili iliingia Efeso kupitia Paulo mtume na Apolo na aidha Prisilla na akila wakisaidiana na Paulo, Paulo baadaye alielekea mji mwingine na aliporejea alikuta wanaume wapatao 12 waliokuwa wameamini injili lakini walikuwa hawajampokea Roho Mtakatifu, hata hivyo Paulo mtume aliwawekea mikono na wakampokea Roho Mtakatifu, Paulo aliendelea kuhubiri injili katika mji huu, akiingia katika masinagogi ya Wayahudi, kwa miezi mitatu na baadaye alianzisha darasa kwa mtu aliyeitwa Tirano.

Mungu alifanya miujiza ya kupita kawaida kwa mikono ya Paulo Mtume Matendo 19:11-12
Waganga wa kienyeji na wachawi wengi sana waliokoka kwa kuiamini injili Matendo 19:17-20 kwa 

kuonyesha upendo wao mkuu kwa Mungu walichoma moto vitabu vyao vya uganga vyenye thamani ya shilingi ya kitanzania 50,000 sawa na shilingi 34,000 za mwaka 1952, Wengi wa watu na kanisa la Efeso walimpenda Bwana kanisa lilikua na likapata wachungaji wazuri akiwemo Timotheo aliyekuwa Askofu wa makanisa ya Efeso kwenye mwaka wa 62 na pia Mtume Yohana kwenye miaka ya 80

Upendo wa Kwanza
Miaka 30 baadaye yaani mwaka wa 90-95 AD Yesu alipomtokea Yohana na kumpa ujumbe wa kulionya kanisa kuwa wameuacha upendo wa kwanza na kwamba wanapaswa kutubu, Kila mmoja wetu na kila kanisa tunapaswa kujichunguza kwa makini, kuwa tulipoitwa na Kristo na kuondoka yaani kujitenga na uovu  katika dunia hii iliyojaa anasa za kuvutia za aina mbalimbali, wote tunakumbuka kuwa tulimpenda Munhgu kwa moyo kama ilivyokuwa kwa Kanisa la Efeso, tulichoma kazi zote mbovu za Ibilisi na kumfuata Yesu na kushinda vikwazo na majaribu ya aina mbalimbali ni muhimu kujipima kwamba je tunao ule upendo wa kwanza au tumeuacha?
Lakini nina neno juu yako ya kwamba umeuacha upendo wa kwanza basi sasa kumbuka ni wapi ulikoanguka ukatubu, na usipotubu ………………………………………………………

Hakuna maoni: