Jumapili, 14 Februari 2016

Umuhimu wa Kutumia Neno la Mungu kwa Halali 3


LENGO LA KUTAFASIRI MAANDIKO:
Tumejifunza jinsi ilivyo muhimu kwa mtafasiri wa Maandiko kuwa mtu aliyeokoka au mtu wa Mungu,kuwa na akili timamu na sio mgerasi,kuamini kuwa Biblia imevuviwa na kama haitoshi kujifunza namna ya kuelewa Maneno na vifungu vya Maneno vya kila kifungo katika maandiko na kutafuta historia ya maandiko nakutafuta maana halisi ambayo mwandishi alikuwa ameikusudia lakini katika eneo hili tunaweka kipaumbele katika kuzingatia Madfhara ya kupuuzia kanuni za kuyatafasiri maandiko katika maana inavyokusudiwa mwana falsafa wa kihispania Jorge Augustin Nicolas alisema  baada ya kufabnya uchunguzi kuwa  Yeye asiyejifunza kutokana na historia amefungwa kuirudia” Vikler 1981 jambo hili ni sawa na lile Muhubiri analolilalamikia katika kitabu cha muhubiri 1;9 “Kile kilichokuwapo kitakuwapo tena, kile kilichofanyika kitafanyika tena,hakuna kilicho kipya chini ya jua.Moja ya mambo ambayo yamefanyiwa makosa mengi huko nyuma ni Biblia na hii ni kwa sababu ya Watafasiri wa Biblia kutokuitendea haki Biblia  na kupuuzia maana halisi zilizokuwa zimekusudiwa na waandishi katika agano la kale na jipya  na hii imetokana na kutafasiri kirohoroho au kwa ajili ya kupata mafunuo kwa kusudi na kwa sababu ya matazamo ya mtu tutaona mifano mingi yawatafasiri  kiyahudi na kikristo waliotumia njia hizo na kupotosha Maandiko.

·   Kuna usemi unaosema ukitaka kuogelea bahari saba basi lazima uwe na Dira
·   Kwa miaka mingi mabaharia wamekuwa wakisambaa katika ukanda wa ardhi kwa kuogopa kupotea ili ikiwa watapotea waweze kurudi nyumbani kwa usalama na wakifika hufurahi, jambo hili ni la muhimu kwa watafasiri wa Maandiko ni lazima tutafute maana ambayo Mwandishi aliikusudia katika kupata kweli za kibiblia  na tunapogundua kweli inaleta furaha
·   Pamoja na jambo hili kuwa muhimu kuna mifano mingi kwa wayahudi na wakristo ambao hawakuwa na mwelekeo katika kutafuta maana za Maandiko bali walijitafasiria Biblia katika mtazamo wowote waliojitakia na kupata maana zisizo halali
·   Wengine walitafuta maana za kiroho zaidi kuliko hata ile ambayo Mwandishi alikuwa amaikusudia
·   Wengine waliichanganya Biblia na Filosofia zao
·   Wengine walipuuzia kuwa Biblia ni neno la Mungu na maana zilizokusudiwa na waandishi ,wengine waliitafasiri kulingana na tamaduni zao na hivyo kupoteza kweli za kibiblia mabo haya husababishwa na nini

1.       Kutafuta maana za Kiroho zaidi
Baadhi ya wayahudi na wakristo walipoteza maana ya Maandiko kwa sababu ya wivu kwa ajili ya mambo ya Mungu na kutaka kujitafutia maana za kipekee sana za Maandiko wakatafasiri tofauti hata na iliyokuwa imekusudiwa na Mwandishi mfano Mathayo 23;23

2.       Kutafuta maana ya kiafisa inayokubalika
Hii ilifanywa na jamii ya kiyahudi pale kiongozi anayeheshimika aliposema neno lilihesabika kama sawa na neno la Mungu na hivyo walijaribu kutafuta katika Maandiko hicho alichokisema na kikajumuishwa katika Sheria ziitwazo Oral law  Baadaye hatimaye misemo hiyo ilijumuishwa pamoja na tamaduni zao na kuiweka katika kitabu kiitwavyo Midrash ambacho kimegawanyika katika maeneo makuu mawili moja  ilikuwa ni kama commentary ya kiyahudi ambayo iliitwa Halakah na sehemu ya pili ilikuwa ni maswala ya kuyatendea kazi kama jinsi ya kuhudumu na kutasfasiri Maandiko hii iliitwa Haggadah hii ilikubalika baadaye kuwa ni tafasiri halali za kimaandiko 1Timotheo 1;4 Paulo mtume aliziiita hizo hadithi na sio mamlaka kamili ya neno la Mungu katika Maandiko hayo kwa mfano Musa aliugonga mwamba katika kutoka 17 wayahudi waliamini kuwa mwamba huo ndio ule wa Hesabu 20 na kuwa huenda wayahudi waliubeba  kwa ajili ya kukidhi haja ya kunywa maji haya ndiyo yalikuwa mapokeo ya wanadamu  ambayo Yesu aliwakemea sana wayahudi kuwa waliacha neno la Mungu na kuyaangalia mapokeo ya wanadamu Marko 7.8-9
3.       Kutafuta maana zinazokubalika kwa akili za kibinadamu The reasonable meaning
Hizi ni njia zilizotumika kuifanya Biblia ikubaliane na mawazo ya kibinadamu kwa mfano kilichotokea ni
·         Kukifanya kila kitu kuwa ni cha kiroho
·        Kuona kuwa mafunuo yanayopatikana kwa watu kuomba sana na kufunga sana kuwa ndio ngazi ya juu kabisa ya ufahamu wa mabo ya kiroho
·         Kuifanya Biblia ikubalike katika Tamaduni za watu au kuitafasiri sawa na tamaduni zao watu hao akiwemo Origeni waliitafasiri Biblia kwa mtindo huu kwa mfano Kutoka 1;22-2;10 kwamba Farao ndiye shetani, au kuifanya Habari ya waisrael kutoka utumwani kwenda kanaani kama watu wanaotoka dhambini kwenda Mbinguni Tafasiri za namna hii ni za kuifanya Biblia iingie katika akili za kibinadamu lakini hiyo siyo maana Mwandishi aliikusudia
·         Kuileta katika maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia
Hawa huitafasiri Biblia kwa kuamini kuwa chochote ambacho akili haiwezi kukielewa na sayansi haiwezi kukithibitisha basi hicho sio cha kweli wao wanaamini kuwa waandishi hao wa Biblia waliandika katika namna na mtazamo ya ujinga pia
Lengo la Kutafasiri Maandiko
·         Kutafuta maana iliyokuwa imekusudiwa na Mwandishi
·         Kutumia kanuni maalumu zinazokubalika kila mahali Duniani kwa ajili ya kupata kweli za milele
·         Kutumia kanuni kwa mahitaji binafsi ya kila mtu kwa ajili ya Maandiko matakatifu
·         Kupata kweli zinazolingana na mahitaji yetu ya kila siku katika maisha

KWA NINI TUNASOMA HERMENEUTICS:

HERMENEUTICS   Inatufundisha kanuni na jinsi ya kuyatumia Maandiko kwa halali, Kwa nini tunahitaji kanuni za kuyatumia Maandiko Je Roho wa Mungu Hatoshi? Kanuni zinatusaidia katika maeneo mengi ya maisha na sio katika kutafasiri Maandiko tu
(a).  Mfano Dereva anahitaji kuzingatia kanuni za barabarani na kama atazipuuzia Ajali zinaweza kutokea
(b). Daktari anapaswa kuzingatia kanuni za utoaji wa madawa Dose na wanapaswa wasitoe chini ya kiwango   wala wasizidishe UNDERDOSE or OVERDOSE!
(c).  Muhubiri au mwalimu anapokuwa hatumii kanuni zinazohitajika wakati wa kutafasiri Maandiko na hususani Biblia, ajali zitatokea na watu wataumia na kutakuwa na fujo na mlolongo wa mafundisho potofu, uzushi na kutokuelewana na hatimaye ujumbe ambao Mungu ameukusudia kwa wanadamu hautawafikia
(d). Maandiko yanahitaji Mtafasiri angalia Matendo 8;30-31 Biblia inasema hivi “Ndipo Filipo akakimbilia na kumsikia yule mtu anasoma kitabu cha nabii Isaya. Filipo akamwuliza,“Je, yanakuelea hayo usemayo?” Yule towashi akasema,“Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia?” Hivyo akamkaribisha Filipo ili apande na kuketi pamoja naye”.

Kumbe yako Maandiko yanayohitaji ufafanuzi na ya kuwa bila ufafanuzi ni vigumu kuelewa mfano wa baadhi ya Maandiko hayo ni kama yafuatayo
1.                   1Yohana 2;27 Kama Roho atatufundisha yote haihitaji mtu kutufundisha kwanini kuna waalimu?
2.                   Mathayo 10;34 na Luka 2;14 Yesu alisema Sikuja kuleta amani duniani kwanini malaika waliimba  amani duniani kwa watu wote aliowaridhia?
3.                   Isaya 66;3 Yeye achinjaye ng’ombe ni kama yeye auaye mtu je ni dhambi kuchinja ng’ombe?
4.                   1Timotheo 5;23 Je ni halali kutumia mvinyo kidogo kwa sababu ya matumbo yetu?
5.                   Galatia 3;14 Je Baraka zote za Ibrahimu ni za kwetu?
6.                   Warumi 7;18-19 Kama yale mema tutakayo kuyatenda hatuyatendi je twaweza kutarajia jema?
7.                   Mathayo 10;9-10 Msichukue fedha wala dhahabu wala shaba… Je ni vibaya kusafiri na Fedha



Jamaa hawa wakiigombania Begi kwa kutumia kipande cha andiko katika 1Koritho 3;21 b lisemalo Kwa maana vyote ni vyenu Bila kuwa na kanuni za kutafasiri Maandiko dunia itakuwa na fujo kwa sababu ya kuyatumia vibaya picha na maelezo kwa Hisani ya maktaba ya Mchungaji Innocent Kamote

AMRI KUMI KWA MTAFASIRI WA MAANDIKO

1.       Biblia ni kitabu cha Bwana Mungu wako Usijifanyie tafasiri yoyote kinyume na iliyokusudiwa na Maandiko

2.       Usilitumie neno la Mungu kwa uzoefu wako wala kwa kanuni za kanisa lako wala tamaduni za wanadamu

3.       Usilisingizie neno la Mungu kwa kulibambikizia mafundisho yasiyofundishwa na biblia yenyewe

4.       Ikumbuke siku ya jumapili uiombee ,ujiandae kwa ujumbewako ziko siku sita za kujiandaa siku ya saba utoe ujumbe mzuri

5.       Zikumbuke kanuni za kutafasiri biblia uzishike na uziheshimu na kuzifuata ili upate kulitumia neno la Mungu kwa halali usije ukajipatia hukumu iliyokubwa zaidi

6.       Usiliharibu neno kwa kusisitiza kweli zake kupita kiasi bali ulitunze na kuhubiri sawa na kweli iliyokusudiwa

7.       Usilizinishe neno kwa kuchanganya na hekima ya kibinadamu wala ufunuo wako mwenyewe

8.       Usiiliibie neno la Mungu kwa kutunga lako mwenyewe na kulisingizia kuwa limesema

9.       Ushihubiri uongo wala kulibeba neno kwa kupuuzia kanuni zake za kulitafasiri

10.    Usitamani ujumbe wa mtu mwingine bali jifunze kutoka kwake ili nawe uweze kutengeneza jumbe sawa
na neno la Mungu.

Hakuna maoni: