Jumatano, 3 Februari 2016

MFULULIZO WA MIJADALA KWANINI WANATOKA NJE YA NDOA 1



KWANINI WANAWAKE HUTOKA NJE YA NDOA? 
 
Nyakati za Karne za mwanzoni ilikuwa ni vigumu sana kusikia Mwanamke akitoka nje ya ndoa na kama jambo hili lilifanyika basi ilikuwa ni kwa usiri mkubwa sana kiasi ambacho jamii ya wakati huo isingeliweza kubaini, Kwa wanaume linaweza kuwa lilikuwa jambo la kawaida
Wanawake walikuwa wanafunzwa kuwafurahisha waume zao, kujitunza na kuonyesha wazi kuwa wao ni wanawake wenye adabu waluofunzwa kufundwa  na kufunzika tena wenye kujiheshimu na wenye heshima zao.

Lakini katika karne za hivi karibuni, ambapo wanawake wamekuwa wakijifunza maswala yaitwayo haki za binadamu, wakifundishwa usawa, wakifundishwa kujiamini, kuwa na mawazo yao na maamuzi na kutokuburuzwa, kuthubutu, kufanya kama wafanyavyo wanaume kusema hapana , kuzingumza kile wanachojisikia, kuhakikisha kuwa nao wanafurahia tendo la ndoa na wanafikia kilele na kuwa na ujuzi wa aina nyingi kulikochangiwa na uwazi wa taarifa, mipashano ya habari na mingi ikiwa imechangiwa na maendeleo makubwa ya sayansi na technolojia Mambo yamebadilika sasa wanawake wanaweza kuzungumza wanachokitaka na kutembea wanavyojisikia, Bila shaka hili limekuwa na mchango mkubwa katika kufikiria namna inavyotupasa kuenenda  na kuhusiana katika karne yetu ya sasa.

Kwa mujibu wa takwimu za miaka ya hivi karibuni kwa mwaka 2012 Gazeti moja liitwalo The Journal of Marital and Family Therapy limebainisha kuwa wanawake wanaotoka nje ya ndoa sasa idadi yao inafikia  asilimia 14% wakati idadi ya wanaume wanaotoka nje ya ndoa ikiwa ni asilimia 22%, Ingawa idadi ya wanawake haizidi ile ya wanaume lakini wanawake wamebainika kuongoza katika kutoka kihisia zaidi nikiwa na maana ya wanaweza wasishiriki ngono kamili lakini wanakubali, kushikwa shikwa, kuchezewa na kutafuta hisia za kimapenzi zaidi kuliko wanaume na wanafanya hayo nje ya waume zao, gazeti hilo hata hivyo limebainisha wazi kuwa hata inapotokea mwanamke anatoka nje ya ndoa inakuwa na ni kwa sababu ya kutafuta hisia za kimapenzi zaidi kuliko tendo lenyewe na kwa bahati mbaya wanashughulikiwa!. Wakati wanaume wao hutoka nje kutafuta starehe ya kivitendo zaidi.

Wanawake ni viumbe vya hisia zaidi linapokuja swala la mahusiano, wanahisia za kutaka kupendwa kujaliwa na kutamaniwa wanajisikia vizuri hata wakitongozwa tu na kujiona kuwa wamo ulimwenguni, ni sawa na vile Biblia na vitabu vitakatifu vinavyoelezea kuwa wanatoka katika Ubavu! Na kuingia katika ulimwengu ambao wanaume wameumbiwa kazi na kishughuliko na utafutaji wa ridhiki maisha na mengineyo, waoa hata wakifanya hayo wanatoka katika ubavu na hivyo wanahitaji Upendo na Hisia za kimapenzi. Sasa basi kwa msingi huo tunaweza kujibu swali hili kwanini wanawake wanatoka nje ya ndoa?

1.      Wanapokosa Kujaliwa na kutimiziwa Hisia zao
Unawezaje kuishi na maisha yakaenda bila mtu kukuonyesha anakujali na anakupenda? Baadhi wanaishi hivyo, siku zinaenda, majuma yanajipanga hatimaye mwezi na hata miaka, kwa wanawake ni adhabu kubwa sana na hata kwa wanaume pia, wanawake wanahisia wanataka kuguswa, kushikwashikwa, kupendwa ni lazima waonyeshwe kuwa unayajua hayo kiakili na kihisia na uwatimizie

Kama hawapokei hilo kutoka kwa Mumeo au Mchumba, haitochukua Muda wanaanza kutafuta nani anawajali, nanai anawavutia nani anawashibisha au atawashibisha mahitaji yao ya kihisia, hii itawazukia kokote waliko wakiwa kazini, wakienda sokoni, wakiingia Hospitali, wakipata ushauri kwa Wachungaji, au Mashehe na maaustaadhi, au hata kwa wasimamizi wa mazoezi wakienda Gym au kwa wapaka rangi za kucha wakiwasugua miguu yao na kucha zao na kuwaosha miguu au wanako fanyiwa Massage au saluni wakishukwa za kusokotwa na wanaume au wajinsia tofauti na yake na ikishindikana hata wa jinsia yake anayeonyesha kujali.

Wanawake wanatamani sana kuonyesha kujaliwa, kuhurumiwana kuhudumiwa kama malkia siku zote wako na hisia kali sana nah ii haimaanishi kuwa haitawaongoza katika kuliwa mzigo! Lakini wanapokuwa na mahitaji hayo ya muhimu na hawayapati ndani ya ndoa zao matokeo yake wanaanguka katika mikono ya wanaowajali na hapo ndipo huliwa mzigo nje.

2.      kulipa kisasi
Hakuna jambo gumu kusamehe kama mtu akikutokea nje ya ndoa, kwa wale ambao yamewahi kuwakuta mnajua ni namna gani mwenzi wako akitoka nje ya ndoa inavyouma, unajisikia umedanganywa, Hasira,kuumizwa, huzuni, na kuasi, inaathiri pia hisia zako, unapogundua kuwa mwenzio katoka nje ya ndoa mwili unatetemeka sana, jasho linakutoka, tumbo linakukatakata na kwa ujumla ni tukio baya

Kwa ujumla ni swala linaharibu kabisa uhusiano wenu, namna unavyohisi,hali yako, tabia na uwezo wako wa kumuamini tena aliyekudanganya, ni katika hali hii ya kufanyiwa hili wengi hujisikia hali ya kulipiza kisasi ili kwamba aliyekutenda ahisi uchungu wa kukufanyia vibaya  na hili ndilo linalopelekea wengi kutoka nje ya ndoa tena, Ukweli unabakia wazi kuwa kutoka nje ya ndoa hakuwezi kuwa suluhu ya kuondoa tatizo lililoko katika uhusiano wenu, suluhu iliyo bora zaidi ni kuongeza kujali, kuonyesha upendo, kudumisha mawasiliano na kuimarisha mapungufu yaliyokuwepo.

3.      Tendo la Ndoa lililo chini ya kiwango.
Ni muhimu kufahamu kuwa wanawake wanahitaji kulihisi na lifurahia tendo la ndoa kwa kiwango HALISI yaani kufikishwa kileleni,wanawake wanapopata tendo la ndoa lililochini ya kiwango, wasiporidhishwa, wasipofikishwa kileleni,wasipotoshelezwa, wasipoandaliwa au kupapuzwa, kupatashwa shaashaa katika swala la tendo la ndoa wanapoteza hamu na hisia za tendo hilo na hatimaye hata uhusiano na ndipo wataanza kuangalia ni namna gani wanaweza kutimiziwa haja zao na kupata tendo hilo katika kiwango kinachokusudiwa, hapo linatengenezwa jaribu la kutafuta kutimiziwa kutimiziwa haja ya kimapenzi na kihisia, kwa ushauri ni kwamba ni vema yanapotokea haya kutafuta namna nzuri na lugha nzuri ya kuwasilisha hisia zenu kwa kila mmoja na kutafuta namna nzuri ya kutimiziana kwa makusudi ya kutoka katika tatizo ninyi wenyewe au kwa washauri walio waaminifu kuhusu Maswala ya ndoa ukichukua tahadhari kuwa ulimwengu tulio nao ni wa uovu.

4.      Swala la Maumbile
Wanaume wako makini na huvutiwa sana na swala la Maumbile kuliko kiungo chenyewe cha Tendo la ndoa, wanaweza kuvutiwa sana na Makalio makubwa, Maziwa yaliyosimama, maumbile ya mabega, uso, wembamba, na kadhalika, Lolote linalokufanya ujisikie uwanawake hilo ni la Muhimu kwa mwanaume na ni jaribu kwao, kwa hivyo lazima utavutia kwa namna moja ama nyingine, yaani kama umezaliwa mwanamke kutongozwa utatongozwa tu inasemekana mwanamke anaweza kutongozwa na wanaume wapatao watatu kwa wiki hii maana yake kwa mwezi unaweza kutongozwa mara 12 na kwa mwaka mara 144, Kama uko katika nafasi ya muingiliano na wanaume mara kwa mara kwa hiyo ni vigumu wakati mwingine kushinda halia ya kujaribiwa mara 144, vyovyote vile kwamba u Mkristo mzuri mwaminifu au kwamaba u mwislamu mzuri na mwaminifu au mbudha, muhindu, na kadhalika, nimuhimu kujitambua na kuelewa kuwa mara unapotambua eneo lako dhaifu ambalo ni jaribu kwa wanaume, na maeneo ambayo ynaweza kuchokozeka nakupandisha hisia zako za kingono, unapaswa kujilinda kwa hekima na maeneo hayo, na unapaswa kuwa makini na kutumia hekima na kujiweka katika mazingira ya usalama wako, Mfano sasa unajua kuwa una makalio makubwa na hips nzuri kisha unavaa nguo fupi zaidi na hatarishi zaidi usitarajie ushindi hapo mfano hapa Pichani
Dada huyo anaweza kuwa na maumbile Mazuri lakini anakaribisha hali hatarishi kwa mkao wake na mavazi yake na kujihatarishia usalama wake, Maumbile ni kivutio kikubwa kwa wanaume, Chunga


5.      Utegemezi/Uhuru wa kifedha
Mwanamke anapojisikia kuwa hamtegemei Mumewe au mchumba wake kifedha ni rahisi sana kwa baadhi yao kujiamini kupita kawaida, inakuwa rahisi sana kufikia hatua ya mabishano na hata kuachana na uhusiano, Hofu ya kuwa peke yake na kutokuwa na fedha humfanya mwanamke kujisikia duni na kuwa katika nafasi ya chini, lakini linapokuja swala la kuwa ana fedha zake na anajua kutafuta fedha, anajua kufanya shughuli zake na kujipatia fedha na akawa ni mzuri katika swala zima la utafutaji, na anafurahia kufanya kazi na ni mzuri katika hilo, uwezekana wa kuendelea kuwepo katika uhusiano usio na amani ni jambo gumu kwao, wanajihisi wana nguvu na wako huru, wana uwezo wa kijitegemea na ni kama wanapita katika dhuria jekundu kutoka kwa mume kuelekea kwenye samaki wengine baharini

6.      Kushindwa kujitambua na kujiona duni
Unaposhindwa kujitambua na kujiona kuwa duni, na kuona kuwa uanataka kupandisha uthamani wako wewe mwenyewe, hili linaweza kutimizwa kwa kutamani, tendo la ndoa, kutimiziwa hisia zako, na kuwa na masikio ya kitafiti kutaka kujua wenzako wanaufurahia vipi ulimwengu, unaposhindwa kujitambua na kujithamini, unaweza kupeleka visingizio kwa mtu uliyenaye kwa kisingizio kuwa hakuthamini, hata kama Mumeo au mchumba wako anakuthamini na kukupenda kiasi gani, lazima utataoka nje ya ndoa, kwa sababu ni vigumu kwako kupokea upendo wa kweli na ni rahisi kwako kutafuta kutimiza upendo wa hisia zako, Dawa kubwa hapa ni kutafuta namna unavyoweza kujiamini na kujipa uthamani.

7.      kujihisi kuwa hupendwi au kutokuridhika
Ni muhimu kufahamu kuwa unapokuwa katika mahusiano, hakikisha kuwa unapenda kumpendeza mpenzi wako yaani mumeo, ni lazima umpikie kwa huba, na kufanya yote ambayo yanaweza kukupa uhakika kuwa atayafurahia na kuwa utaupata moyo wake, pia uwe mtu wa shukurani na mwenye kuridhika, jiulize je kama hatashukuru unajisikiaje kama haonyeshi kusisimkwa nawe na sikukuu zako za kuzaliwa zinapita na hafanyi lolote kukuhusu, na inawezekana hata kukumbuka hakumbuki? Ni muhimu kumjulisha kuwa unataka kufanyiwa nini kwa vile kila binadamu anapenda kushukuriwa, kuonyeshwa kupendwa na kutiwa moyo, mwanamke anaweza kukata tamaa na kujiona duni kama atajihisi apendwi na haridhiki na mahusiano yaliyoko.

8.      Upweke
Mwanamume ahaonekani hata, hapatikani yuko katika shughuli za utafutaji mali yuko busy, anaporudi kazini hufikia kuoga na kula chakula na kusikiliza taarifa za habari kisha hulala akiwa hoi, weekend pia anakuwa amechoka, na huo ndio mfumo wa maisha yake siku zote, huwezi kubaki katika ukurasa uleule, huwezi kuvumilia kuwa katika mfumo wa jambo hilohilo kila siku unaanza kuhisi kuwa mko mbalimbali, Na hapo moyo bila kukusudia unaanza kutafuta namna ya kujifurahisha na kujaza nafasi hiyo na mtu mwingine, swala hili halijalishi ngazi nyoyote ya cheo cha kiserikali au kidini, Unaaza kufikiri vinginevyo na kufurahia hali nyingineyo na hapo ndipo wenngi hutoka nje ya ndoa zao,

Tatizo hili pia linaweza kutengenezeka na mazungumzo baina yenu na kutafuta wazo jipya namna ya kuboresha penzi inaweza kuwa sababu ya kuyatengeneza.

Ni imani yangu kuwa utakuwa umejengeka kwa kuwa kusudi kubwa ni kujijenga jamii ili dunia iwe mahali panapomfaa kila mmoja wetu

Ndimi mkuu wa wajenzi mwenye Hekima
Rev. Innocent Kamote.
Kwa maswali maoni au ushauri/ nipigie/what’s up me
0718990796

Hakuna maoni: