Wokovu
ni nini?
Neno wokovu kwa asili lina maana
ya kuwekwa huru, neno linalotumika kuelezea kuhusu wokovu lina asili ya
kiyunani “Soteria”Kwa kiingereza “Deliverance” ambalo maana yake ni
kuwekwa huru, kuokolewa hatarini, kulindwa na hatari, kusamehewa dhambi na
kuponywa magonjwa yako yote na kufutiwa hatia yote, ni kuondolewa katika hali
ya hofu, kulindwa na maadui zako, kusitiriwa, na kushindiwa vita, Kuondolewa hali
ya aibu,n.k. Kazi hizi zote hufanywa na Mungu kwa kiebrania neno wokovu
linachanganuliwa kwa maneno Yeshu’ah” “Yesa” na tesu’ah sawa na jina Yesu. Ambayo kwa ujumla yana
maana ileile kama ya kiyunani pia liko neno la kiyunani Sozo ambalo pia lina maana ya kuokoa, kutoa katika migandamizo au
utumwa au kuokoa na hatari.
Katika mtazamo wa agano jipya wokovu maana
yake ni Kazi nzima aliyoifanya Bwana Yesu katika kumkomboa mwanadamu aliyepotea
na kumrejesha kwa Mungu, ni kazi ya Mungu mwana kumkomboa mwanadamu kutoka
dhambini na kurejesha uhusiano uliovunjika kati ya mwanadamu na Mungu hii ndio
kazi iliyomleta Kristo kufanya Luka 19; 10 Biblia inasema;-
“Kwa kuwa
mwana wa Adamu alikuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea”
Mkazo mkubwa katika agano jipya
kuhusu wokovu ni katika kusamehewa dhambi na uhusiano wetu na Mungu kurejeshwa
kama ilivyokuwa kwa Zakayo kwa hiyo Kusamehewa na Mungu hakuhitaji juhudi zetu
kwani kazi nzima ya wokovu ni mpango wa Mungu mwenyewe na hufanya kwa wale
anaotaka mwenyewe kwa neema wala sio kwa juhudi ya mtu au matendo Fulani ya
kumshawishi na kumpendeza yeye akionyesha wazi jinsi kazi ya wokovu ni ya
upendo na neema ya Mungu Paulo anawafundisha Waefeso hivi;-
“Waefeso 2;8-9 “ Kwa maana
mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu
ni kipawa (Yaani zawadi) cha Mungu wala sio kwa matendo mtu awaye yote asije
akajisifu.”
Kwa msingi huo kumbe wokovu
hautokani na juhudi za kibinadamu kuupata ni neema ya Mungu neema hii katika
Kiebrania hutumika neno Hen na kwa
kiyunani ni Charis ambayo maana yake ni upendeleo pasipo kustahili, kukubalika,
ni kutakiwa mapenzi mema ni wema
unaoleta upendeleo kwa mwenye dhambi asiyestahili. kwa hiyo neno hili lina
maana ya kuwa Wokovu ni Bure, unatokana na upendo wa Mungu unakufanya uwe mbali
na hasira ya Mungu, unakufanya usijihukumu, unakufanya usilipizwe kisasi wala
kuufanyia kazi ni upendeleo wa Mungu tu pasipo kazi yoyote. Ndio maana wengi
wetu siku ile tulipookoka hatukuhitaji kufunga na kuomba sana, hatukuhitaji
kusali sana au kuungama sana hatukufanya bidii ya aina yoyote huenda tulisikia
tu injili na tulipoikubali kutoka moyoni tayari Mungu akatukubali
tukabadilishwa maisha yetu,tukaondolewa hatia zote, tukajawa na furaha,
tukaumbiwa kiu ya kutaka kumpendeza yeye, kumuomba yeye, kumuabudu yeye,
kumtumikia yeye kwa sababu ni yeye aliyekuwa akitutafuta wala sio sisi ilikuwa
ni zawadi ya bure wala hatukuhitaji kuilipia
ni wema wa Mungu tu usiotokana na historia yetu kuwa huko nyuma
tulifanya nini wema huu wa Mungu ndio neema na neema hii ni kubwa sana kwa
wanadamu wote lakini kwa waliokolewa ni neema maalumu isiyo ya kawaida.
Aina
za Neema.
Kuna aina kuu mbili za neema
·
Neema
ya kawaida Common grace huu ni wema
wa Mungu ulio juu ya wanadamu wote bila kujali wanafanya nini au wanamuabudu
nani wana dhambi au la neema hii inaweza
kuwafanya wanadamu kuwa wema, kuishi kwa haki kwa utaratibu katika jamii, jamii
kupewa mvua, majira na nyakati, chakula na furaha, mavazi na mafanikio
mengineyo pamoja na elimu hii ni neema ya kawaida na haina uhusiano wowote na
wokovu kwa hiyo neema hii haitoshi kumfanya mtu aokoke ni neema njema inayoweza
kusaidia mwanadamu kuitikia neema ya Mungu ya wokovu Neema hii imesababisha
watu kuwa na maarifa ya kutengeneza silaha, kufuga wanyama, kuwa na maarifa ya
kitabibu na wagonjwa kupona mahospitalini wanapotibiwa, au kukimbizwa
hospitali, kuvumbua madawa na tiba za maswala mbalimbali, kuokolewa na ajali
mbalimbali na matukio mengine mengi yanayodhihirisha wema wa Mungu kwa viumbe
wake wote bila ya upendeleo hii ni neema ya kawaida Common grace.
·
Neema
maalumu Special Grace hii ni neema maalumu inayowezesha kumleta mtu
kwa Yesu Yohana 6;44 neema hii inakuja juu ya mtu na kumfanya mtu huyo kugeuzwa
nia yake, kuwekwa huru mbali na dhambi, hii ni neema maalumu ya Mungu ni neema
inayokuja kupitia Kristo Yesu Yohana 1;17, hii haimaanishi kuwa kabla ya Kristo
watu hawakuokolewa hapana watakatifu waliotutangulia waliokolewa lakini Kristo
ndio ufunuo kamili wa neema hii ya wokovu neno neema limetajwa mara 38 katika Agano
la kale na mara 128 katika Agano jipya na limefafanuliwa kama upendeleo au
kibali mara 64 katika Agano la kale na mara 6 katika agano jipya kwa kawaida neno hili huunganishwa pamoja na
Mungu katika shughuli nzima ya kusamehe
na kughairi hukumu au mabaya mfano soma Yona 4;2 na Nehemia 9;17
Yona
4;2 Biblia inasema “ Akamwomba Bwana akasema Nakuomba ee Bwana sivyo hivyo nilivyosema hapo nilipokuwa katika inchi yangu? Hii ndio
sababu nilifanya haraka kukimbilia Tarshishi kwa maana nalijua ya kuwa wewe u
Mungu mwenye neema, umejawa huruma,
si mwepesi wa hasira u mwingi wa rehema nawe
waghairi mabaya”
Nehemia
9;17 Biblia inasema “….. Lakini wewe u Mungu mwenye huruma nyingi mwenye neema, mwenye huruma, si mwepesi wa hasira,
u mwingi wa rehema basi hukuwacha”
Kumbe
basi katika neema ya Mungu kuna Rehema, Kuepushwa na hasira, kuhurumiwa, na kusamehewa
kutoka katika kupatwa na mabaya kwa sababu ya hukumu ya Mungu.Mungu anatamani
kumuokoa kila mtu 2Petro 3;9 , lakini ni
wale wenye kuitikia neema hii kwa kuiamini injili na kukiri kuwa Yesu ni Bwana
neema hii humshukia na kufanya kitu cha tofauti kabisa katika maisha ya huyo
aliyempokea Bwana Yesu ikiwa ni pamoja na kumfundisha kukataa ubaya na tamaa za
kidunia na kutufanya kuishi kwa kiasi na haki
na utauwa katika ulimwengu huu wa sasa.
Tito
2;11-12 Biblia inasema hivi kuhusu kazi ya neema hii maalumu “Maana neema ya
Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa nayo yatufundisha kuukataa ubaya na
tamaa za kidunia tupate kuishi kwa kiasi
na haki na utauwa katika ulimwengu huu
wa sasa.
Kumbuka
kuwa moja ya kazi ya neema hii maalumu ni kuwaelekeza walioamini kuwa na uamuzi sahii wa kuzikataa hisia
zisizo za kimungu na anasa za kidunia na
kuyaona mambo ya ulimwengu wa sasa kuwa chukizo na inatupa nguvu za kuishi
maisha sahii yenye kumcha Mungu, kwa msingi huo mpaka hapo unaweza kukubaliana nami
kuwa kuna maswala kadhaa ambayo mtu anapookoka tu anaweza kujua kuwa si mema au
mema Moja kwamoja tu kabla ya kujifunza maswala mengine mpaka wakati huu neema
ya Mungu inapofanya kazi wokovu unakuwa haujaharibiwa na uko salama yaani hadi
hapo mtu huyo anakuwa huru kutoka katika kongwa la dhambi na amani ya Mungu
Shalom humfunika.
Wajibu
wa mwanadamu katika kuitikia neema maalumu ya Mungu ya wokovu.
Ni muhimu kufahamu ndugu msomaji kuwa pamoja na
neema hii maalumu ya Mungu kutolewa bure mwanadamu anawajibika kuwa tayari
kupokea zawadi hii ya neema bure Kuna usemi wa zamani wa Kiswahili na hata
lugha nyingine kuwa “unaweza kumpeleka Punda kisimani kwa kusudi la kumnywesha
maji lakini asinywe” maana yake ni kuwa ni mapenzi ya Mungu watu waokolewe watu
wote kama biblia isemavyo katika 1Timotheo 2;1-5
“Basi kabla ya mambo yote nataka
dua na sala na maombezi na shukurani zifanyike kwaajili ya wafalme na wote
wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani katika utauwa wote na
usatahivu, Hili ni zuri nalo lakubalika mbele za Mungu mwokozi wetu ambaye hutaka watu wote waokolewe na
kupata kujua yaliyo kweli.”
Lakini sio kila mmoja anaweza
kuokoka kwa sababu Mungu hamlazimishi mtu hivyo watu wengi hukataa wenyewe
neema ya Mungu na hivyo kuukosa wokovu na hivyo Mungu anahuzunishwa, Sasa ili
mwanadamu aweze kupokea upendeleo huo wenye zawadi za wokovu anapaswa kukubali
lakini anakubali namna gani anakubali kupitia hatua muhimu zifuatazo na ambazo
hatimaye Mungu huzijibu kwa kufanya mambo kadhaa ambayo hukamilisha wokovu wa
mtu huyo anayekubali
1. Toba
ni Muhimu kwa ajili ya kupokea Neema ya wokovu.
Neno
Toba “repentance” ni kuhuzunika moyo kwa mujibu wa Biblia ya Kiebrania neno Sigh hutumika ambalo maana yake ni
kuhuzunika moyo, kujuta, kughairi, kuomboleza au kuwa na mpango mpya Tunaweza
kuona asili ya neno hili katika Mwanzo 6;6-7 Biblia inasema hivi “Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu
duniani akahuzunika moyo Bwana
akasema nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemuumba usoni pa nchi mwanadamu na mnyama na
kitambaacho na ndege wa angani kwa maana naghairi
ya kwamba nimewafanya” kwa msingi huo basi neno kutubu kwa kiibrania ni
kuhuzunika na kughairi mpango Fulani uliokuwa nao kwa hiyo kimsingi toba ni
lazima iwe na mfuatano wa kuhuzunika moyo na kuchukua hatua madhubuti.
Kuhuzunika bila kuchukua hatua sio toba kamili. Kama ulikuwa unafanya jambo
Fulani lazima ughairi Kutoka 32; 14, 1Samuel 15; 11
Neno
toba Katika Biblia ya kiyunani linatumika neno Metanoeo au metanoia au metamelomai ambalo maana yake ni kuwa
na hisia nyingine, au kuhuzunika na kuchukua hatua ni kubadilika hivyo toba ni
kuhuzunika na kubadilika au kuhuzunika na kuchukua hatua mfano Mathayo 21:
28-31 Biblia inasema hivi
“Lakini
mwaonaje mtu mmoja alikuwa na wana wawili, akamwendea yule wa kwanza akasema mwanangu nenda kafanye kazi katika
shamba la mizabibu, Akajibu akasema naenda Bwana asiende, Akamwendea Yule wa pili akasema
vilevile, Naye akajibu akasema Sitaki baadaye akatubu akaenda , Je katika hao
wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya babaye? Wakamwambia ni Yule wa pili…”
Bila
shaka ni wazi kabisa kuwa katika mfano huu wa Bwana Yesu alikuwa akionyesha ni
nani ametubu toba ya kweli kuhuzunika bila kuchukua hatua sio toba kamili ni
sawa na mwana aliyekubali kua atakwenda shambani lakini hakuenda,Yuda alihuzunika
alipokuwa amemsaliti Bwana Yesu alifanya vema kuhuzunika lakini hakufanya mapinduzi dhidi ya huzuni
yake Bali aliamua kwenda kujiua hii haikuwa toba kamili, Toba ya kweli
hujumuisha kuhuzunika na kubadilika kimtazamo na toba hii ya kweli itapelekea
maisha yako kuwa yenye furaha hutakuwa mtumwa wa huzuni tena utawekwa huru
kutoka kongwa la huzuni.
Toba
ni kama pembe tatu inahusisha pande kuu tatu ili iweze kukamilika na pande hizo
kuu tatu zinapokuwa zimekamilika ndipo tunapoweza kusema kuwa hiyo ni Toba kwa
hiyo toba inahusisha .Ufahamu (Akili), hisia na utashi au uamuzi.
Ufahamu
Toba
|
Hisia Uamuzi /ukiri
Ufahamu. (Intellectual aspect)
Ili mtu aweze kufikia toba
anapaswa kwanza kuwa na Ufahamu kuwa Amemkosea Mungu, ama hata kwa kuzaliwa
kwetu sisi ni wenye dhambi mbele za Mungu, hii ikiwa na maana kuwa sisi ni
wenye dhambi kwa kuzaliwa, kutenda, kuwaza kwa namna iwayoyote tumekuwa kinyume
na Mungu Hivyo kabla mtu hajafikia toba ni lazima awe na ujuzi kamili kuwa
amemkosea Mungu yeye mwenyewe, anapaswa kufahamu kuwa dhambi ni makosa mbele za
Mungu zaidi ya kufahamu tu kuwa dhambi ina matokeo mabaya yanayoambatana nayo
anatakiwa kujua tu kwamba dhambi inamuhuzunisha Mungu aliyemtakatifu, Daudi
alifahamu kuwa alipofanya dhambi na mke wa Uria na alipomuua Uria alikuwa amefanya
uhalifu kinyume na jamii, lakini alipotubu alikuwa naufahamu kamili kuwa
alikuwa amefanya dhambi kinyume na Mungu Zaburi 51;4 “Nimekutenda dhambi wewe
peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako,Wewe ujulikane kuwa na haki
unenapo. Utambuzi ya kuwa umemkosea Mungu ndio unaoleta huzuni inayotupelekea
kwenye toba. Angalia mfano wa mwana mpotevu na toba yake katika Luka 15;21
Biblia inasema hivi Yule mwana akamwambia Baba nimekosa juu ya mbingu (Mungu)
na mbele yako sistahili kuitwa mwana wako tena. Toba inapokuwa kama utambuzi
kamili kuwa umemkosea Mungu inaweza kuleta matokeo, wako watu wanaojiona kuwa
ni watakatifu sana na wenye kujihesabia haki Mungu anachukizwa sana na roho hii
ya kiburi, Mbele za Mungu mtu anayetubu lazima akubali kuwa ametenda dhambi
bila kujali kuwa anaishi katika haki kiasi gani Paulo mtume alikuwa ni Farisayo
aliyeishi sawa kabisa na sheria ya Musa na wala hakuvunja hata kidogo kila
alilolifanya kwa sheria lilikuwa ni haki kabisa hakuwa na hatia hata pale alipokuwa akiwaua wakristo kwa sheria
ilikuwa ni sahii soma Wafilipi 3;6
anasema “Kwa habari ya juhudi mwenye kuliudhi kanisa, kwa habari ya haki
ipatikanayo na sheria sikuwa na hatia “ unaweza kuona Kwamba kwa Ufahamu wake
Paulo alikuwa akimpendeza Mungu lakini siku moja Mungu alimwambia Sauli Sauli
mbona waniudhi? Matendo 9;4 alikuwa akifikiri kuwa anampendeza Mungu kumbe
anamchukiza na alitakiwa kujihoji na kuchukua hatua ya kuacha dhambi zake mara
moja na maisha yake yalibadilika mara baada ya toba ya kweli Mungu amekwisha
kusema kwenye neno lake kuwa wote tumefanya dhambi na tumepungukiwa na utukufu
wake Warumi 3;23 awaye yote anayekuja mbele za Mungu kwaajili ya kutubu lazima
akubali kuwa yeye ni mwenye dhambi mbele zake na neema ya Mungu itabadilisha
kabisa mfumo wako wa maisha na kuyafanya kuwa safi kabisa.
Hisia.
(Emotional aspect)
Mtu akiisha kuwa ametambua kuwa
amemkosea Mungu kwa Ufahamu wake wakati huohuo anakuwa na huzuni kwaajili ya
dhambi zake kinyume na Mungu, anasikitishwa na dhambi zake Zaburi ya 38;18
inasema “kwa maana nitaungama uovu wangu Na kusikitika kwa dhambi zangu” Kama
mtu anajigundua kuwa amemtenda Mungu dhambi pia atasikitishwa atajutia
ataombolezea dhambi zake atajuta Paulo mtume alipokuwa akiokolewa siku tatu
aliomboleza akiwa ameacha kula na kunywa Matendo 9;9, hali kadhalika mwana
mpotevu alizingatia moyoni mwake na kufanya mageuzi makubwa hali hizi ndizo
zinampelekea mtu kuwa na toba kamili Paulo baada ya hapo alikuwa mwenye wivu
mkubwa sana wa kumtumikia Kristo na alianza kumuhubiri Matendo 9;17-20
Uamuzi./ukiri
(Volitional aspect)
Hatimaye baada ya kuhuzunika
kunakuwa na utashi ambao Mungu ametuumba nao hapa ndipo mwanadamu huamua
kuchukua uamuzi tunapochukua uamuzi ndipo toba inapokuwa imekamilika kufahamu
kuwa umetenda dhambi kwa Mungu na kuhuzunika bila kuchukua uamuzi wa kuacha
njia zako mbaya basi au njia zetu mbaya Toba inakuwa haijakamilika lazima uchukue uamuzi wa kuacha Mithali 28;13 Biblia inasema “Afichaye dhambi
zake hatafanikiwa bali yeye aziungamaye na kuziacha
atapata rehema” Mtu anapofanya uamuzi wa kuacha njia zake ndipo sasa Msamaha wa
Mungu unapopatikana Isaya 55: 7 “Mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye
haki aache mawazo yake Na amrudie bwana
Naye atamrehemu na arejee kwa Mungu wetu naye atamsamehe kabisa” .Uamuzi wa mtu
una nguvu unapoungwa na Ufahamu kuwa amemkosea Mungu, huzuni ya moyo na uamuzi
wa kuacha dhambi unaifanya toba iwe imekamilika na hapo tunakuwa tumesamehewa dhambi
na kuupokea wokovu Luka 1;77 “Uwajulishe watu wake wokovu katika kusamehewa
dhambi zao”
Toba
na malipizi.
Baada ya toba wakati mwingine
toba inapokuwa imekamilika unaweza kuchukua hatua za kurudisha mali au vitu vilivyochukuliwa
kwa namna ambayo sio halali, hali hiyo ndio huitwa malipizi ni ushahidi wanje kimaisha na kivitendo kuwa
mtu huyo ameamua kubadilika au ametubu kweli
ni moja ya sehemu ya matunda yapasayo toba Luka 3;8 Zakayo aliwarudishia mara nne wale
aliokuwa amewadhulumu Luka 19; 8 Malipizi
yanaonyesha uzito wa toba lakini sio kwa Mungu bali kwa wanadamu, kwa msingi
huo malipizi hayaokoi, kwani tunaokolewa kwa neema lakini malipizi yanatangaza kwa wanadamu kuwa
sisi sasa tumeokoka tumeacha njia mbovu za zamani na sasa tunafuata njia mpya ni pokeo la kivitendo la toba malipizi sio
njia ya wokovu lakini ni njia ya kuonyesha kuwa tumeokolewa. Si kila malipizi
yanaweza kufanyika, Kristo hakumuagiza Zakayo kufanya, lakini alifurahia Zakayo
alivyofanya kufanya malipizi kwa zakayo kulitokana na uamuzi uliosababishwa na
Roho wa Mungu mwenyewe endapo wahubiri watakazia malipizi kama jambo la lazima
kufanyika wokovu utakuwa ni kitu kizito na cha kuiogopesha sana kwa msingi huo
inahitajika hekima sana na kumuacha mtu na moyo wake kuamua nini cha kukifanya
na sio kuwashinikiza watu kufanya malipizi endapo utashinikiza Wokovu unaugeuza
kuwa Kongwa zito na lisilo bebeka, Amani ya Kristo iamue ndani ya mtu mwenyewe
kufanya malipizo.Hili pia lilikuwa fundisho la Agano la kale Kutoka 22;1 na
Walawi 6;5,Hesabu 5;6-7 na tendo la Kristo kukaa kimya na kufurahia
kilichofanywa na Zakayo sawa na sheria
ni wazi kuwa Yesu amekubali fundisho kuhusu malipizi katika maana ya
kuwa ni ushahidi ulio wazi wa kuwa mtu huyo ametubu.
Mafundisho
ya Agano jipya kuhusu Toba.
Agano jipya limejaa mafundisho
yenye kuwaita watu katika toba mahubiri kuhusu toba yalikuwa ndio kiini kikuu
cha mahubiri ya Kristo na Yohana mbatizaji Mathayo 3; 2, 4; 17. Kristo katika
huduma yake alihubiri kuhusu toba aidha aliwaamuru mitume kuhubiri kuhusu toba
katika jina lake Luka 24;47, Petro alihubiri kuhusu toba siku ya pentekoste
Matendo 2;38, Paulo alihubiri kuwa Mungu ameamuru watu wote watubu Matendo
17;30,20;21 Patro alikazia kuwa Mungu anataka kila mtu atubu kwa ujumla neno
toba au kutubu limetajwa mara 36 katika agano jipya, Toba ni ya muhimu sana katika kutuletea neema
ya wokovu Luka 13;3,5.
Kila mtu anaitwa katika wito wa
kutubu hii inajumuisha wote wale wasio wakristo, kwa kuwa dhambi ni tatizo la
ulimwengu mzima kila mmoja anaitwa katika toba, Wakristo pia wanapaswa kutubu
makanisa katika kitabu cha ufunuo yanaitwa kutubu Ufunuo 2;5, 3;19 toba ndio njia
pekee ya kumrudia Mungu mara tunapokuwa tumemtenda Mungu dhambi, Mungu anathamini sana toba ya kweli hivyo hata wale waliookolewa wanaitwa kutubu
pale wanapokuwa wamekosea 1Yohana 1;9 Biblia inasema “Tukiziungama dhambi
zetu,Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu na kutusafisha na
udhalimu wote”
Kwa nini watu wanaitwa kutubu
jibu ni kwa sababu tumefanya dhambi swala hili linamjumuisha kila mmoja wote
tuna hatia kwa sababu ya dhambi, inawezekana tukawa tumefanya dhambi kwa
makusudi au kwa kutokujua zote hizo ni dhambi, dhambi ya kutokukusudia au
kutokujua huitwa sin of Omission na
dhambi za makusudi huitwa sin of
Commission Yakobo 4;17 Yeye ajuaye kutenda mema kisha asitende kwake huyo
ni dhambi, 1Yohana 3;4 Dhambi ni uasi, vyovyote iwavyo mwanadamu anawajibika
kuwa mwenye dhambi na kwa sababu hiyo kila mmoja anapaswa kutubu kwani iko dhambi
lakini tunapotubu Mungu huleta msamaha na rehema.
Toba
ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Ni muhimu kufahamu kuwa pamoja na
mafundishio hayo muhimu kuhusu hatua za toba zinazotupelekea kupokea wokovu ni
vema kukumbuka kuwa wokovu hauwezi kuwa neema kama kuna hatua tu za kufuata ni
muhimu kufahamu kuwa hatua hii ya kutubu yenyewe ni zawadi kutoka kwa
Mungu Biblia inaonyesha kuwa toba ni
zawadi kamili kutoka kwa Mungu angalia 2Timotheo 2;25 Biblia inasema “
akiwaonywa kwa upole wao washindanao naye ili kama ikiwezekana Mungu awape kutubu na kuijua kweli”
kumbe toba tunapewa na Mungu mpaka mwanadamu anatubu bado ni muhimu kufahamu
kuwa ni wema wa Mungu unaotuvuta kufikia toba Warumi 2;4 Biblia inasema “Au
waudharau wingi wa wema wake na usathimili wake na uvumilivu wake usijue kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?
Neno la Mungu pia linapohubiriwa pia linauwezo wa kusababisha watu kutubu watu
wa ninawi walitubu baada ya mahubiri ya Yona ambao ulikuwa ni ujumbe aliopewa
na Mungu Yona 3;8, wapinzani wanaweza kutubu kutokana na mafundisho ya neno la
Mungu 2Timotheo 2;25, kazi iliyofanyika
msalabani ya Kristio Yesu inapohubiriwa na upendo wake kufunuliwa pia
husababisha toba Kristo alikuja kuwaita wenye dhambi kusudi watubu Mathayo
9;132, Marko 2;17 na Luka 5;32 aidha maono kuhusu Mungu pia huweza kusababisha
toba Ayubu 42;5,6.
Matokeo
ya kutubu.
Toba kwa kawaida inaambatana na
Furaha kubwa miongoni mwa malaika huko mbinguni Luka 15;7,10 “kuna furaha mbinguni kwaajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye”mtu
anapokuwa amekubali kutubu na kumgeukia Kristo ni kama anavuta kengele za
furaha za mbinguni na kusababisha shangwe.
Toba na imani ni kama mapacha kwa
kawaida huenda pamoja wakati mwingine ni vigumu hata kuchanganua kuwa ni kipi
kinatangulia kati ya imani na toba lakini
ni kama vinakwenda pamoja
Toba inaongoza katika kupokea
msamaha,tunapoziungama dhambi zetu na
kumgeukia Mungu kupitia mwanae Yesu Kristo Mungu hutusamehe kabisa 1Yohana 1;9
“Tukiziungama dhambi zetu Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee
dhambi zetu na kutusafisha na udhalimu wote” kwa msingi huo toba,
imani na kusamehewa vyote viko katika mnyororo mmoja wa mtu kuokoka, kila moja
inajitegemea lakini kila moja ina makusudi ya kusaidiana na nyingine na hakuna hata moja inaweza kurukwa kwani
kila moja ina thamani yake katika swala zima la mtu kuokolewa.
2. Imani
ni Muhimu kwaajili ya kupokea Neema ya wokovu.
Kama tulivyoona kuwa neema ile ya
wokovu inapatikana kwa toba ambayo nayo ni zawadi ya Mungu, lakini pia kama
ilivyo Nyanja hizi zinategemeana sana toba haiwezi kuwa kamili kama hakuna
imani ndani yake Biblia inaweka wazi kabisa kuwa pasipo imani haiwezekani
kumpendeza Mungu, kwa msingi huo ni wazi kuwa mwanadamu anaokolewa kwa imani
Matendo 16;31 na Yohana 3;16 kwa msingi
huo hatuwezi kabisa kuzungumzia wokovu bila kuzungumzia maswala ya kuamini
kwani ndivyo Biblia inavyofundisha ona
Matendo 16;31“Wakamwambia mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja
na nyumba yako”
Yohana 3;16-18 “Kwa maana jinsi
hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanae wa pekee ili kila amwaminiye
asipotee bali awe na uzima wa milele” Maana Mungu hakumtuma mwana ulimwenguni
ili ahukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye Amwaminiye yeye
haukumiwi asiyeamini amekwisha kuhukumiwa kwa sababu hakuliamini jina la mwana
pekee wa Mungu.
Kwa msingi huo imani ya mtu itamuamulia
hatima yake katika kuupokea wokovu na kupata uzima wa milele au kutokuamini na
kujikuta katika hukumu, Kumjua Mungu kwenyewe ni swala la imani Mtu amwendeaye
Mungu ni lazima aamini kuwa yeye yuko na kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao Waebrania
11;6 ni wazi kuwa imani ni ya muhimu
kwaajili ya kumpendeza Mungu angalia mfano mtu anazungumza habari zako kwa mtu
mwingine kisha mtu huyo hataki kuziamini je utapendezwa naye? Mungu amekuwa
akijifunua kwa wanadamu kuhusu yeye na njia za kumfikia yeye kama mtu haamini
katika njia hizo je anawezaje kumpendeza Mungu?
Imani ni kuamini na kutegemea,
kama ilivyokuwa kwa toba imani nayo ina pembe tatu yaani kujua, kuamini na kutegemea.
Imani
|
Kuamini Kutegemea
Imani
ni nini?
Imani ni tendo la kujitoa kwa
hiyari kimaneno na kivitendo ambapo mtu anaweka uzito mkubwa wa mahitaji yake
na uongozi wa matendo yake kwa kile anachokiamini. Kwa mujibu wa Biblia imani
ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana.kwa
msingi huo Hatumuoni Mungu, na habari za Kristo tunazisikia tu, na tunaamua
kuamini kana kwamba sisi tu mashahidi kuwa Mungu yupo na kuwa ametupa thawabu
hii ya zawadi njema ya Kristo Kuja kusulubiwa kufa na kufufuka kwaajili yetu,
Kwa hiyo imani hii hujengeka kwa kusikia Neno la Mungu imani hiyo nayo ina sifa
zake
Imani sio kuamini kuhusu Kristo
bali ni kumuamini Kristo,wala imani sio kuamini sehemu Fulani ya mafundisho ya
injili bali kweli yote ya injili, Haianzishwi na matakwa ya mtu bali neno la
Mungu,Sio matumaini bali inafanana na matumaini, Bila tumaini maisha ya ukristo
ni bure lakini bila imani maisha ya ukristo hayako, Tumaini ni kutazamia uzuri
ujao kwa uaminifu, lakini imani inaleta uzuri huo pale tulipo, tumaini
linatufanya tuwe na mwanga kuhusu ahadi za Mungu kuwa zitakuja kutimia, lakini
imani inazifanya ahadi za Mungu kuwa halisi imani sio hisia au mawazo
yanayotembea ni uamuzi. Hata hivyo ni
muhimu kufahamu kuwa imani hii katika Kristo haiishii katika kuamini kwaajili
ya wokovu bali inatakiwa kukua na kuendelezwa ndani ya maisha ya Ukristo, mtu
anaweza kuwa na ujuzi kuhusu ndoa, anaweza kuwa amejifunza mengi kuhusu ndoa na
hatimaye akatamani na kuamua kuoa lakini kama hajaishi katika ndoa Bado
haijatosha kusema kuwa anaujuzi wa
kutosha kuhusu ndoa. Ndivyo ilivyo na imani baada ya kuokolewa ni lazima tuhakikishe
kuwa tunaikulia imani na tunaishi kwa imani.
Kuongoka
Tukio la kuamini linatupelekea
kuongoka “Conversion” Kwa asili neno
kuongoka kwa kiyunani ni Proselytos kwa kiingereza tunapata neno proselyte ambalo lilitumika kumaanisha
mtu wa mataifa aliyejiunga na dini ya kiyahudi, baadaye pia lilitumiwa na
wakristo kumaanisha mtu aliyejiunga na Kristo au mtu anayemfuata Kristo, au mtu
aliyebadilika kuwa mtu mwingine kitabia, mfano 1Samuel 10;6, Pia Bwana Yesu
alilitumia katika kufundisha maamuzi thabiti ya badiliko,mfano kunyenyekea na
kuamini kama mtoto mdogo n.k, lilitumika pia kumaanisha mtu anayerejea au
aliyeimarika kiimani, haliko mbali na neno ambalo tumelizoea siku hizi kuokoka,
napenda sana kutumia neno kuokoka kuliko kuongoka, Tendo hili la kuongoka
hutokea pale sasa mtu anapokuwa amemgeukia Yesu Kristo kutoka katika maisha ya
dhambi na kupokea msamaha wa dhambi na hasira ya Mungu na adhabu juu ya dhambi
kufutwa kabisa mtu huyu sasa anarejea kutoka katika njia ya dhambi kuelekea
katika njia ya haki hivyo kwa ufupi kuongoka ni kurejea Matendo 3;19 Biblia
inasema “Tubuni basi, mrejee ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za
kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana Yesu. Neno kuongoka limetumiwa na Kristo
pia katika Mathayo 18;3 ambapo Biblia inasema Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia
kamwe katika ufalme wa Mungu, Luka 22;32 Lakini nimekuombea wewe ili imani yako
isitindike nawe utakapoongoka waimarishe ndugu zako” Kwa ujumla kuongoka ni
kama kukamilika kwa tendo kamili la kutubu, kuamini na kurudi kwa ujumla wake
wote kumuelekea Kristo hii maana yeke ni kuwa kama mtu atatubu ataamini kisha
haendelei katika njia ya Bwana maana yake tendo la kuongoka halijakamilika
ndani yeke mtu aliyeongoka sasa anaishi ndani ya upande wa pili wa imani
aliyoipokea kuikiri na badiliko lililotokana na toba yake. Mtu ambaye
hajaongoka sasa anafananishwa na mbwa aliyeoshwa kisha kurudi kugaagaa matopeni
2Petro 2;22, Baada ya tukio hili la kuongoka yaani kuendelea katika imani ya
bwana Yesu Kristo sasa ndipo kunafuata marupurupu yanayoambatana na wokovu wa
mtu huyo.
3.
Mungu
anamfanya mtu aliyeokoka kuwa kiumbe kipya. (Kuzaliwa mara ya Pili) Regeneration.
Bila shaka kama ni mwanafunzi wa
maandiko utakuwa na Ufahamu wa karibu kuhusu neno Kuzaliwa mara ya pili
lililotumiwa na Kristo kwa mwalimu mkubwa sana wa kiyahudi aliyeitwa Nikodemo Yohana
3;1-8 Yesu alimwambia ni lazima uzaliwe mara ya pili hapa ndipo linapokuja
fundisho la kuzaliwa upya au kuzaliwa mara ya pili au kufanywa kiumbe kipya
Regeneretion kuzaliwa mara ya pili ni nini?
Kuzaliwa mara ya pili ni tendo la Mungu
kumbadilisha mtu aliyeokoka palepale kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, hii ni hali
ya kukarabatiwa kwa nia au nafsi ya mwanadamu ambayo kabla ya wokovu wakati
wote nia yake ilisukumwa kutenda dhambi kwa mawazo, maneno na matendo kila
alilolikusudia mwanadamu kabla ya wokovu ilikuwa ni uasi mbele za Mungu sasa
basi mtu anapoamini na kutubu na kuongoka nafsi yake inazaliwa upya inakuwa iko
tayari sasa kutenda mapenzi ya Mungu, Mwalimu wa Kiyahudi kama Nikodemo
alipaswa kuwa na Ufahamu kuhusu swala hili kwani wayahudi walikuwa wakipokea
watu kutoka katika mataifa waliokuwa wakiongoka kujiunga na dini ya kiyahudi na
watu hao walihesabiwa kama watoto wa changa
waliaozaliwa sasa penginepo Nikodemo alisha ngaa kwa sababu Yesu
alilitumia neno kuzaliwa mara ya pili kwake huku yeye ni Myahudi penginepo
Nikodemo alifikiri kuwa swala hili linahusu kuzaliwa upya katika tumbo la
mwanamke kwa kuingia tena tumboni kwani alifikiri kule kuwa myahudi hakumfanyi
yeye kuhitaji kuzaliwa Mara ya pili, Jambo hili linatukumbusha kuwa hata kama u
kiongozi wa kidini kama hujachukua hatua madhubuti za kutubu na kuamini na
kuongoka si rahisi kuzaliwa mata ya pili, kuzaliwa mara ya pili kunawakilishwa
katika lugha kadhaa za kimaandiko kama
Ø
Kuzaliwa
na Mungu Yohana 1;13
Ø
Kuzaliwa
mara ya pili Yohana 3;3
Ø
Kuzaliwa
kwa maji na Roho Yohana 3;5
Ø
Kuzaliwa
Mara ya pili Yohana 3;7
Ø
Kuzaliwa
kwa Roho Yohana 3;8
Ø
Kuzaliwa
kwa upya 1Petro 1;3
Ø
Kuzaliwa
tena Petro 3;23
Ø
Kuzaliwa
na Yeye 1Yohana 2;29
Ø
Kuzaliwa
na Mungu 1Yohana 3;9
Ø
Kuzaliwa
na Mungu 1Yohana 4;7
Ø
Kuzaliwa
na Mungu 1Yohana 5;1
Ø
Kuzaliwa
na Mungu 1Yohana 5;18.
Kuzaliwa mara ya pili ni swala la
kimuujiza linalofanyika mara mtu anapokubali kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na
mwokozi wa maisha yake, ni swala la kimapinduzi na sio uumbaji mpya mtu wa aina hii anapita kutoka mautini na
kuingia katika uzima wa milele Yohana 5;24, na hivyo mytu katika Kristo ni
kiumbe kipya 2Wakoritho 5;17 Wagalatia 6;15, hii sio kiumbe kipya kwa maana ya
kuwa nje mtu huyu ataendelea kuonekana kama vilevile alivyokuwa isipokuwa ndani
nia yake inaumbiwa shauku mpya ya kutaka kuishi maisha yanayompendeza Mungu kwa
msaada wake wala si kwa nguvu zake, hivyo haya sio mapinduzi ya kibinadamu bali
ni bali uweza wa kimungu ndani ya
mwanadamu.
Neno hili kuzaliwa mara ya pili
Regeneration kwa kiyunani ni Paliggenesia
ambalo maana yake ni kuzaliwa upya, au kufanywa upya au kurejeza au
kukarabati “re-creation” Tito 3;4-5 Biblia inasema “Lakini wema wake mwokozi
wetu Mungu na upendo wake kwa wanadamu ulipofunuliwa alituokoa si kwa sababau ya matendo yetu ya haki tuliyoyatenda
sisi bali kwa rehema yake, kwa kuoshwa kwa kuzaliwa
kwa pili na kufanywa upya na
Roho Mtakatifu”
Ni
nini umuhimu wa kuzaliwa mara ya pili?
Umuhimu wa kuzaliwa mara ya pili
ni tukio muhimu kufanyika kwa mwanadamu, ingawa wanadamu wanaweza kuzaliwa
wakiwa na maadili tofauti tofauti wengine wanazaliwa wakiwa na maadili mabovu kabisa wengine katikati na
wengine wema kabisa , wengine wasomo na wengine wana uwezo mkubwa na wengine
mdogo lakini pamoja na hayo mwanadamu
ameharibika katika ujumla wake kiroho,
kimwili na kiakili yaani Mwili nafsi na roho kwa sababu ya dhambi Warumi 5;12
na kwa sababu hiyo hakuna mwenye hakli hata mmoja Warumi 3;10 kwa sababu wote
wamefanya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu Warumi 3;23, hii maana yake
ni kuwa sumu ikidondokea kwenye glasi ya maji maji yote yana sumu, au kirusi
kikiingia katika damu ya mtu safi mtu huyo ataathirika kila eneo hivyo na
mwanadamu alipoanguka dhambini kila eneo la utu wake liliharibiwa roho yake
inakufa akili zinaathiriwa na mwili pia kiroho kuna kuwa hakuna mawasiliano na
Mungu unapookolewa sasa Mungu ainaifanya roho yako kuwa na mawasiliano
naye unakuwa umefufuka Luka 15;36 ndani yetu
kunakuwa hakuna jambo jema Warumi 7;14 tunakuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi
Warumi 7;18 na Efeso 2;1-3, unapookoka unafufuliwa , pia unajaliwa kuelewa
mambo ya kiroho kwani akili zako zilikuwa hazielewi mambo ya Rohoni 1Koritho
2;14 na miili yetu inakuwa na uponyaji , kwa msingi huo hata kama mtu ana akili
kiasi gani kama hajaokoka akili zake haziwezi kupambanua mabo ya kiroho
1Koritho 2;14 na ndio maana Nikodemo alikuwa mwalimu mkubwa sana katika Isarael
lakini alishindwa kuelewa jambo dogo kuhusu kuzaliwa mara ya pili kwa kuzaliwa
mara ya pili sasa tunapewa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu.kuzaliwa mara ya
pili ni wazi kuwa hakuji kwa matendo mema, wala hakusababishwi na ubatizo, wala
sherehe za kidini bali kwa kumuamini
Mungu kupitia neno lake , Tangu wakatu
huu ndipo mtu anakuwa na uwezo wa kuushinda ulimwengu 1Yohana 5;4 “Yeye
aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu” pia kunakuwezesha kuishi kwa kutenda
haki 1Yohana 2;29b “Kila asiyetenda haki hakuzaliwa na yeye” kwa hiyo tabia za
kale zinatawaliwa na tabia mpya utampenda Mungu na ndugu zako katika Mungu
!Yohana 5;2,4;20,3;14 hii haimaanishi kuwa mtu huyo hatatenda dhambi kabisa
lakini haishi maisha ya dhambi kwa sababu anaye mwombezi atatubia na dhambi
itamsumbua nitalizungumzia huko mbele zaidi swala hili 1Yohana 2;1,-2,1;9.
Kilele cha kuzaliwa mara ya pili tuwapo
duniani ni kumuelekea Kristo na kuwa kama yeye lakini atakapokuja tutafanana
naye na kuwa kama yeye 1Yohana 3;2 kwa hiyo hata kuzaliwa kwetu mara ya pili
kutakuwa kamili atakapofunuliwa kwetu Bwana
na wakati huo tutakuwa na utukufu mkubwa Warumi 8;29-30 hivyo kazi ya
kuzaliwa mara ya pili ni ya Mungu inaanzishwa nayeye na itakamilishwa na yeye
sisi tunatakiwa kuendelea kuitikia neema hii ya Mungu kwa kuyatii yele atakayo
4. Kuhesabiwa
haki.Justification.
Ni moja ya Nyanja muhimu sana za
wokovu kuhesabiwa haki kwa kawaida katika kiingereza hutumika neno Justification ni neno linalofanana na
lile linaloweza kutamkwa mahakamani na hakimu au jaji mwenye haki kwa mtu muhalifu kumtangaza kuwa hana hatia
ni tendo la kukubalika kuwa huna hatia “you
are Innocent” Mwenye hatia anasimama mbele za Mungu mwenye haki ili
ahukumiwe na badala ya kuhukumiwa anatamkiwa haki kukubalika na Mungu jambo hili pia hufanyika kwa imani
na hutolewa kama zawadi ya Bure na Mungu
kupitia kumuamini Bwana Yesu, kwa hiyo tunaweza kusema kwa uwazi
kuwa kuhesabiwa haki ni tendo la neema
ya Mungu ambapo Mungu humtangaza mtu
huyu mwenye hatia kuwa hana hatia kwa sababu tu mtu huyo ameweka imani yake kwa
bwana Yesu hii ni tofauti na kusamehewa dhambi na ni zaidi ya kumtangaza mtu
kuwa hana hatia kwa sababu ukweli
unabaki kuwa tuna hatia lakini ni ile
hali ya Mungu kutuchukulia kuwa ni kama hatujawahi kufanya dhambi kwa sababu ya
haki ya mwanae Yesu Kristo kuwa haki yake inawekwa juu yetu na anafanyika kuwa
haki yetu 1Wakoritho 1;30, tofauti na kuzaliwa mara ya pili ambalo ni tendo
linalofanyika ndani yetu baada ya kuamini kuhesabiwa haki ni tendo la muonekano
wa nje wakati Mungu anapokuwa ametusamehe. Kuhesabiwa haki kunabadilisha
mtazamo wetu na mahusiano yetu na Mungu badala ya Mungu kututazama kama chombo
cha hasira zake kwa sababu ya dhambi, sasa tunatazamwa kama chombo kipya chenye
kufaa mbele za Mungu kama ilivyo kwa
kuzaliwa upya tendo hili pia hutokea wakati mmoja tunapokuwa tumekubali
kumpokea Bwana Yesu na kwa sababu hiyo Yule mshitaki wetu Shetani anakuwa hana
uwezo wa kutushitaki kuwa tuna hatia mbele za Mungu Warumi 8;33-34 Biblia
inasema “Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu?
Mungu ndiye awahesabiaye haki, ni nani atakaye wahukumia adhabu? Kristo ndiye
aliyekufa, naam na zaidi ya hayo ndiye anayetuombea” kwa hiyo swala la
kuhesabiwa haki ndugu yangu kimsingi ni zaidi ya kusamehewa dhambi na hukumu ya
hasira au ghadhabu ya Mungu, Mungu anapotuhesabia haki anatuweka katika nafasi
ya mtu anayestahili kwa hivyo kama Mungu angekuwa anawahesabia haki watu walio
wema na wazuri kwa matendo injili isingelikuwa habari njema kwa watu wenye
dhambi hivyo tunasema kuwa mtu aliyeokoka ni “mwenye dhambi aliyeuchinja”
Hata hivyo tofauti na swala la
kutangazwa kuwa huna hatia kimahakama ambayo kwa kawaida hufanya kazi zake kwa
mujibu wa sheria kuhesabiwa haki katika
Mungu ni tofauti na uhesabiwaji haki wa kimahakama kwanini kwa sababu sheria
haiwezi kumuhesabia haki mtu mwenye hatia hata kidogo Sheria haiwezi kumuacha
muhalifu hata kidogo ni lazima itamuhukumu kwa hiyo sasa basi kuhesabiwa haki
kunakozungumzwa kibiblia ni tendo la neema ya Mungu lililokamilishwa kupitia
kazi aliyoifanya Bwana Yesu pale msalabani hivyo haki yetu si haki yetu wenyewe
ni haki kupitia kuamini kazi alizofanya Kristo pale Msalabani kwa hiyo basi mtu
anapookolewa anakuwa huru anatangazwa kuwa na haki ya kuwa hana hatia na
hastahili kuhukumiwa adhabu ni tofauti na msamaha unaoweza kutolewa na gavana
anapomsamehe muhalifu muhalifu huyo yu awezxa kuwa huru toka gerezani lakini
hawezi kuwa huru kutoka kwenye hatia na ile hatia ndani yake inapiga kelele na
kumnyima uhuru kwa sababu ukweli unabaki wazi kuwa mtyu huyu ni mwenye hatia
ambaye alifungwa na inagwa amefunguliwa alistahili adhabu na kwa sababu ana
kumbukumbu ya swala hilo hivyo anabaki na hatia
Kuhesabiwa haki pia ni zaidi ya
kutangazwa kuwa huna hatia “You are Innocent” kwani tangazo kama hilo kwa mtu
mwenye hatia kwakweli litabakia kuwa uongo, Mungu anatuhesabu kuwa hatuna hatia
kabisa kupitia haki ya mwanae Yesu aliyekubali kuteseka kwa ajili yetu na hivyo
Mungu anaridhishwa na Neema yake inatukuzwa na mwenye dhambi anafaidika
Tofauti
ya kuhesabiwa haki na sheria.
Sheria kamwe haiwezi kumfanya
mwanadamu akahesabiwa haki na kuna sababu kama tatu hivi kwanini haiwezi
kufanya hayo kwanza sheria ni dhaifu kwa sababu ya mwili Warumi 8;3 Biblia
inasema hivi “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria kwa vile ilivyokuwa dhaifu
kwa sababu ya mwili, Mungu kwa kumtuma mwanae mwenyewe katika mfano wa mwili
ulio wa dhambi na kwa sababu ya dhambi aliihukumu dhambi katika mwili” sheria
ina nguvu moja tu ya kutuonyesha ugonjwa wetu yaani dhambi lakini haina uwezo wa
kuponya au kuiondoa dhambi ni kama kioo ina uwezo wa kutuonyesha kuwa sisi tua
uchafu lakini kioo hakiwezi kuondoa uchafu hata kama utakuwa na vioo vingi
kiasi gani vioo hivyo haviwezi kuosha au kuondaoa uchafu ulio nao sheria ni kama kuhani au mlawi aliyempita mtu
aliyepigwa na majambazi wakamuacha bila msaada kumbe anahitajika msamaria mwema
anayeweza kututibu na kushughulika na tatizo letu.
Sababu ya pili kwa nini sheria haiwezi
kutuhesabia haki ni kuwa sheria haina rehema ni kama msumeno ili mtu aweze
kuhesabiwa haki kwa sheria analazimika kuyitimiza yote kwa ukamilifu na mtu
anayefikiri kuwa anaweza kuishika yote huyu yuko sawa na mlevi anayejaribu
kutembea juu ya kamba iliyofungwa toka ghorofa moja hadi jingine chini kukiwa
na maji, kwa asili yetu ya kibinadamu yenye anguko hakuna anayeweza kufanya
hayo na unaposoma historia yote ya mwanadamu katika Biblia haionyeshi kuwa kuna
mtu aliweza na kwa kuwa sheria ilikuwa ikitangaza Baraka kwa watakaoitii na
laana kwa watakaovunja hata moja kwa hiyo wote walioandikiwa kuyatii yote
katika kitabu cha torati wasiyafanye wamelaaniwa ndio soma Wagalatia 3;10b
Biblia inasema hivi “…Amelaaniwa kila
mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa
katika kitabu cha torati asiyafanye”
Sababu ya tatu ni kuwa sheria
haiwezi kufuta historia yetu kuwa sisi ni wenye dhambi na haiwezi kuosha asili
yetu ya dhambi ambayo kila mtoto wa Adamu anayo kwa msingi huo basi hata kama
mtu angeweza kuishika sheria yote kwa ukamilifu bado ndani yake angejikuta ni
mwenye dhambi kwa kulke kuzaliwa na mwanadamu mwenye asili ya dhambi Zaburi
51;10 ni damu ya bwana Yesu tu inayoweza kutusafisha na udhalimu wetu. Kwa
ujumla sheria haikutolewa ili kumkamilisha awaye yote bali kuihukumu dhambi ili
dhambi ionekane kuwa ni dhambi na izidi kuwa mbaya mno soma Warumi 7;13.Sheria
yenyewe haina shida ni takatifu na ni
njema lakini ilikuja ili kuonyesha
mwanadamu alivyo na hatia Warumi 7;12 ,Warumi 7;17-20 sasa mwanadamu ategemee
nini? Sheria ilikuja kwa mkono wa Musa bali neema na kweli zilikuja kwa mkono
wa Yesu Kristo. Kwa hiyo basi sheria ni maarifa yanayotufundisha kuwa sisi tu
wenye dhambi warumi 3;20, na kamwe haiwezi kutupa au kutuletea wokovu lakini
inatuongoza kuona kuwa tunamuhitaji mwokozi Wagalatia 3;24 Biblia inasema wazi
hivi “Hivyo torati imekuwa kiongozi kutuleta kwa Kristo ili tuhesabiwe haki kwa
imani” moja ya faida kubwa ya kuhesabiwa haki ni kuwa tumeokolewa
mbali na hasira ya mungu Warumi 5;9 hakuna hukumu ya adhabu juu yetu kwa
sababu Mungu ndiye anayetuhesabia haki Warumi 8;33, tunaingia katika kundi la
waliobarikiwa hatuko chini yalaana Zaburi ya 32;1 yasema hivi “Heri
aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake” mtu awaye yote aliyemwamini
bwana yesu amebarikiwa hayuko chini ya laana, faida nyingine ni kuwa tuna amani
na Mungu warumi 5;1 badala ya kujificha kamna Adamu tunamkaribia na mwisho tunakuwa warithi na sio watumwa
tena bali wana wa Mungu warumi 8;17,Tito 3;7.
5. Kufanywa
kuwa wana wa Mungu Adaption
Yohana 1;12 “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu
ndio wale waliaminio jina lake” Adaption au kufanywa wana wa Mungu ni
tendo la neema ya Mungu ambalo linatokea
kwa wale wanaomuamini Yesu Kristo kufanywa kuwa watoto wa Mungu wenye haki sawa
na marupurupu sawa na watoyo wa Mungu, mtu mmoja alisema hivi
Ø
Kuzaliwa
mara ya pili ni kubadilishwa kwa asili yetu ya dhambi
Ø
Kuhesabiwa
haki ni kubadilika kwa mtazamo wa Mungu kutuhusu baada ya kuamini
Ø
Kufanywa
wana ni kupoandishwa cheo kutoka kuwa watumwa kuwa watoto na warithi
Kwa msingi huo tunapokuwa
tumefanyika watoto wa Mungu Mungu hatuchukulii sisi kama watumwa au watoto
walio chini ya mwanagalizi bali kama warithi na wana kamili wa Mungu wagalatia
4;1-5, wajibu wetu ni kuamini tu na kwa
njia hiyo tunazaliwa si kwa mapenzi ya mwili bali kwa MunguYohana 1;12-13,
Anapokuwa amemtuma Roho wake wa uana
tunamlilia baba Warumi 8;15Wagalatia 4;6 kilio cha kuita baba kamwe hakiwezi
kutamkwa na mtumwa sasa kila
aliyeokolewa ni mwana wa familia ya kifalme ya Mbinguni, umeondolewa kutoka
utumwani wewe sio mtumwa wa sheria kwa sababu sasa tunapendezwa kufanya mapenzi
ya Baba, hatuko tena chini ya utumwa wa hofu ya dhambi Mungu anazifutilia mbali
kupitia damu ya Yesu 1Yohana 4;18 Biblia inasema hivi “Katika Pendo hamna hofu lakini pendo lililo
kamili huitupa nje hofu kwa maana hofu ina adhabu na mwenye hofu hukamilishwa
katika pendo, kufanywa wana kunatuweka katika ushirika usio wa kawaida na Mungu
kwani watu wote n I viumbe wa Mungu lakini si kila mtu ni Mwana wa Mungu ni
wale waliompokea Kristo tu wanaweza kuwa na uhusiano wa pekee na wa kweli na Mungu na mwanae wa Pekee
Kristo 1Yohana 1;3
6. Kutakaswa
“Santification”
Neno Utakaso limetokana na neno
la asili la kiebrania ambalo kwa kiyunani linatumika neno “Hagiazo”ambalo lina uhusiano mkubwa na maswala ya utakaso ya agano
la kale hususani katika sherehe za
kidini za kumfanya mtu awe na uwezo wa
kuukaribia uwepo wa Mungu au awe na hali zinazo mlazimu kuweze kumfikia au
kumkaribia Mungu kwa hiyo utakaso kwa kiebrania maana yake ni kufanywa kuwa
mtakatifu au kuhesabiwa haki mbele za macho ya Mungu na kwa hiyo kuweza
kukubalika na kumuabudu kwa hiyo kwa kiibrania kutakaswa ni sawa na kuhesabiwa
haki unaweza kuhisi mitazamo hii kwa kuangalia mistari ifuatayo Waebrania 9;13-14
Biblia inasema hivi “Kwa maana ikiwa damu ya mbuzi na
mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe walionyunyiziwa wenye uchafu hutakasa
hata kuusafisha mwili basi si zaidi sana Damu yake Kristo ambaye kwamba kwa
Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa
itawasafisha dhamiri zenu na matendo
mafu mpate kumuabudu Mungu aliye hai?”
ndugu yangu msomaji utakaso huu pia ni neema ya Mungu
Utakaso ni kazi ya neema ya Mungu ambapo
muumini anatengwa yeye mwenyewe na hali ya dhambi iliyoko ndani
yake na kwa kujazwa Roho Mtakatifu anatengwa kuwa mtakatifu kwaajili ya
utumishi, utakaso maana yake kwa ufupi ni kufanywa kuwa mtakatifu katika
kulihakikisha hilo linafanyika Roho Mtakatifu ni nyenzo muhimu na kupitia kazi
ya Kristo aliyoifanya ndani yetu 1Koritho 1;30.
Utakaso ni hali ya kukua na kukomaa
kuelekea kuwa na tabia za Kristo, ni mabadiliko ya kitabia na maisha na kufanywa upya kwa Roho Mtakatifu kuelekea
kuwa na tabia za kiungu Tito 3;5 maana yake ni kuwa mtu anapokuwa ameokoka
hawezi kuendelea kuishi maisha ya ndhambi 1Yohana 3;9 kwa sababu nguvu ya
maisha mapya ya kiroho inakuweka mbali katika kuishi maisha ya ufanyaji dhambi
hali hiyo ya kubadilishwa katika hatua ya mwanzoni huitw2a kutakaswa kwa hiyo mtu anapokuwa
ameokoka anakuwa ameoshwa ametakaswa 1Koritho 6;11 na Pia Matendo 20;32 Paulo
anajumuisha wakristo wote kuwa watu waliotakaswa
Kazi ya utakaso ni kufunja nguvu ya dhambi
kututawala Warumi 6 ; 14 Biblia inasema hivi “Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi
kwa sababu hamuwi chini ya sheria bali chini ya neema” tunapokuwa tumetakaswa
tunakuwa huru kutoka dhambini na kuwa watumwa wa haki
Kwa muhktasari tunaweza kusema
kuwa utakaso ni -;-
a. Kutengwa
Kuwa
mtakatifu kwa asili ni neno la kiungu ambalo kwa asili ni kutengwa kwa hiyo
kimsingi utakaso unawakilisha ile hali ya Mungu kuwa na kila hali ya kidunia na
kibinadamu na hivyo kuwa na hivyo kuwa mkamilifu kimaadili na kwa utukufu wake
Mungu na anapotaka kukitumia kitu au mtu huyu aliye mtakatifu hukitenga au
humtenga mtu huyo kutoka katika matumizi ya kawaida na kutumika kwa makusudi
yake tendo hilo pekee hukifanya kitu au mtu kuwa mtakatifu.
b. Kuwekwa
wakfu
Utakaso
hujumuisha pia swala la kutengwa lakini pia swala la kuwekwa wakfu, au kujiweka
wakfu hii ni hali ya kukubali neema ya Mungu kwa muitikio wa kukubali kujitenga
na dhambi na maswala ya anasa za kidunia
na kukubali kushiriki tabia za uungu na asili ya uungu na kujitoa au
kujiingiza katika ushirika na Mungu
kupitia neema katika Kristo, kuwa mtakatifu ni neno linalotumika pia katika
mswala ya ibada na alinapotumika kwa mtu
humaanisha pia kutumika kwaajili ya huduma za kiungu, kwa mfano Israel
liliitwa Taifa Takatifu kwa sababu waliwekwa wakfu kwa kusudi la kimungu pia
makuhani Walawi waliitwa watakatifu kwa sababu ya kuwekwa wakfu ili wamtumikie
Mungu na hata si ku au sikukuu zilizowekwa kwa ajili ya Mungu ziliitwa siku
takatifu
c. Kusafishwa
Utakaso
pamoja na kujumuisha kutenga au kuweka wakfu pia Mungu Yehova anapokuwa
amemtenga mtu au kitu kwaajili ya makusudi yake hukisafisha vyombo
vilivyotumika kwa kazi vilitakaswa kwa kunyunyiziwa mafuta Kutoka 40;9-11,
Israel walisafishwa kwa damu ya agano Kutoka 24;8 Waebrania 10;29 Makuhani
walitakaswa kuwa mawakili wa Yehova kwa kuoshwa kwa maji na kupakwa mafuta na
kunyunyiziwa damu na hivyo kuwa wakfu
Walawi sura ya 8 watu waliookolewa leo tunatakaswa kwa damu ya Yesu Waebrania
13;12
d. Kuishi
maisha ya utakatifu na haki
Kusihi
kwa haki maana yake ni kubadilishwa kwa neema ya Mungu na kuishi sawa na maagizo ya kiungu na kuishi kwa utakatifu
ni kubadilishwa kwa neema kutoka katika asili yetu na kupokea asili ya uungu Mungu alipokuwa
amewateua Israel kuwa taifa lake alielekeza pia ni namna gani wataishi na hivyo
Israel walijitoa kuishi maisha sawa na maagizo ya Mungu na hivyo kila
anayeokolewa sasa anapaswa kujitoa mwenyewe kuishi sawa na maagizo ya Mungu
e. Huduma
Agano
ni hali ya uhusiano ulioko kati ya Mungu na mwanadamu, mtu napoingia katika
huduma maana yake ni kuwa ameingia katika uhusiano wa Mungu na watu wake mtu
anayeingia katika huduma anaingia katika agano na kumtumikia Mungu kunamaanisha
kuwa umeingia katika huduma ya kikuhani na uchafu wowote ule unaweza kuharibu
uhusiano huo na hivyo ni lazima maji au damu itumike kusafisha na kurejesha
uhusiano kwa msingi huo kila mtu aliyeokoka ni Mtakatifu, kupitia damu na maji
aliyoyatoa Kristo Yesu pale msalabani kwa msingi huo tunafanyika kuwa taifa
takatifu kama ilivyokuwa kwa taifa takatifu la Israel Kutoka 19;6,1Petro 2;9,5
kwa msingi huo kumtumikia Mungu kuna uhusiano wa Karibu sana na utakaso na
utakatifu na hivyo Mungu anatumiliki na sisi tunakuwa wake Matendo 27;23.
Utakaso
unatokea wakati gani?
Ni muhimu kufahamu kuwa utakaso
umegawanyika katika maeneo makuu mawili
1.
Mtazamo
wa Mungu kwetu na unatokea mara moja tunapokuwa tumeokolewa kwa kuamini
2.
Kwa
kuishi na kuendelea kukubaliana na neema na mpango wa Mungu katika maisha yetu
mpaka kufa
Utakaso kama mtazamo wa Mungu na unaotokea
mara moja tunapokuwa tumeokolewa kwa kuamini,(Position & Instantaneous) ni kusafishwa kwa asili ya dhambi kwa
damu ya Yesu kupitia imani katika Yeye ni kazi ya neema ya Mungu kutuhesabia
kuwa tumekwisha kuwa safi mara baada ya kuamini kazi aliyoifanya Kristo
Msalabani kwaajili yetu hivyo katika macho ya Mungu tayari unakuwa mtakatifu na
saa ileile unapoamini tayari unakuwa mtakatifu kwa hiyo waamini wote ni
watakatifu 1Wakoritho 1;2,6;11 “Kwa kanisa la Mungu
lilioko Koritho wale waliotakaswa katika Kristo Yesu walioitwa wawe watakatifu
pamoja na wote wanaoliitia jina la bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana
wao na wetu.” “Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii lakini mlioshwa,
lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la bwana Yesu Kristo na
katika Roho wa Mungu wetu.” Pamoja na kuwa Paulo Mtume hapa anawaita wakoritho
watakatifu jambo la kushangaza katika waraka huo huo aliwaandikia kurekebisha
matatizo kadhaa ya wakristo ya kimwili na dhambi zilizo wazi angalia 1Koritho
3;1, 5;1,2,7,8 walikuwa watakatifu waliooshwa kwa damu ya Yesu lakini baadhi yao walikuwa mbali na maisha ya
kila siku waliyotakiwa kuyaishi kwaajili ya Mungu angalia msomaji wangu
walikuwa wameitwa kuwa watakatifu lakini baadhi yao walikuwa hawaenendi sawa na
huo utakatifu walioitiwa kwa ujumla utakaso una tofauti ndogo sana na
kuhesabiwa haki katika mtazamo mzima wa agano jipya
Utakaso katika mtazamo wa kuishi na
kuendelea kukubaliana na neema na mpango wa Mungu katika maisha yetu mpaka kufa
(Practical &Progressive) Utakaso
sio tu swala la mtazamo wa Mungu kwetu kutuhusu mara baada ya kuokolewa lakini ni pamoja na kuendelea kuishi maisha
ya utakatifu au kuendelea kutakaswa mpaka kufa
baada ya kuwa umemfuata Kristo kwa kumuamini ni lazima uendelee kumfuata
kila siku na kuendelea kumuamini na kukubali kutengwa kwaajili ya kusudi lake
na kuendelea kumfanania yeye Yesu Kristo katika maisha yetu ya kila siku, kwa
hiyo utakaso ni kazi ya Mungu inayotolea kwa neema bure ambapo tunabadilishwa
maisha yetu kuwa na mwelekeo wa kuwa kama Mungu na tunaendelea kuwezeshwa tena
na tena mpaka kufa kwa hiyo hii haimaanishi tunaukulia utakaso
la tuna endelea katika utakaso kwa hiyo tunakuwa nao kabisa na huku tunaendelea
kutakaswa Waebrania 10;14 kuendelea kwetu kunategemeana na kukubali kwetu
kuendelea kukua katika Kristo Waebrania 12;14 na ni lazima tujishughulishe kwa
kujitakasa sisi wenyewe kwa kuweka mbali uchafu wote wa mwili na Roho
2Wakoritho 7;1.
Kwa ujumla sasa
tumeona upana na urefu wa wokovu msomaji wangu mpenzi bila shaka mpaka hapa
utakuwa umeona wazi kuwa wokovu sio kazi ya mwanadamu ni kazi ya mungu na kuwa
katika kila marupurupu yanayohusiana na wokovu mwanadamu anasehemu ndogo sana
yaani kukubali neema ya Mungu kufanya kazi ndani yake lakini mimi nasema hata
huko kukubali kwenyewe ni zawadi ya Mungu wala si kwa kadiri ya kutaka kwetu.Hata
hivyo kabla sijamalizia katika eneo hili ni muhimu sasa nikukuelezea njia kuu
za utakaso ili mwanadamu aweze kutakaswa kuna njia kuu tatu ambazo zinahusika
na utakaso
1. Kazi
ya Yesu Kristo Msalabani.
Kazi aliyoifanya Bwana Yesu pale
msalabani ni kazi kubwa sana ya ukombozi ambayo waaminio wanatakaswa kupitia
kazi yake kuu ya umwagaji Damu kwa hiyo Damu ya Yesu inatakasa na kuondoa
dhambi na uchafu wote kumbuka kuwa wakati wa agano la kale ili mtu aweze kusamehewa
dhambi alitoa dhabihu ya wanyama kama Mbuzi na ndama wa ng’ombe walionona na
wanyama hao walimwaga damu kwa niaba ya watu waliotoa dhabihu hizo, lakini
ilipaswa kuwa jambo lenye kujirudiarudia,Kristo alijitoa mara moja tu kwa
kusudi la sisi kusamehewa dhambi mwandishi wa kitabu cha waebrania anaweka wazi swala hili
Waebrania 9;11-14 Biblia inasema hivi;-
“Lakini Kristo akiisha kuja aliye kuhani mkuu
wa mambo mema yatakayokuwapo, kwa hema
iliyo kubwa na kamilifu zaidi
isiyofanyika kwa mikono , maana yake isiyo ya ulimwengu huu, wala si kwa damu
ya mbuzi na ndama bali kwa damu yake
mwenyewe aliingia mara moja tu katika
patakatifu akiisha kupata ukombozi wa milele, kwa maana ikiwa damu ya Mbuzi na
mafahali na majivu ya ndama ya ng’ombe
walionyunyiziwa wenye uchafu hutakasa
hata kuusafisha mwili basi si zaidi swana damu yake Kristo ambaye kwamba kwa Roho wa milele
alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na mawaa itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu mpate kumuabudu Mungu aliye hai.”
Unaona ndugu yangu kuwa katika
damu ya Bwana Yesu kuna ukombozi wa milele, Kazi kubwa aliyoifanya Kristo
msalabani inatuhakikishia ukombozi milele hii haina maana kuwa mtu aliyeokolewa
hawezi kufanya dhambi anaweza kwani kwaasili sio mkamilifu lakini anaporudi kwa
Kristo ambaye ndie kuhani mkuu yaani mpatanishi na mwombezi na kuamini katika
kazi iliyofanyika msalabani mtu huyo husamehewa Neno la Mungu lasema hivi katika
!Yohana 2;2 andiko ambalo halipendwi
sana na wahubiri wenye misimamo mikali
ya kichanga andiko hili lasema “Watoto
wangu wadogo nawaandikia haya ili kwamba msitende dhambi. Na kama mtu akitenda
dhambi tunaye mwombezi kwa Baba Yesu Kristo mwenye haki naye ndiye kipatanisho
kwa dhambi zetu, wala si kwa dhambi zetu tu bali na kwa dhambi za ulimwengu
wote” ni muhimu kufahamu kuwa ukombozi huu wa milele kupitia Damu ya bwana Yesu
ni kuwa kila wakati mtu anaweza kukaribia kiti cha rehema cha Mungu kwa ujasiri
na kupokea msamaha wa dhambi, Kristo ni Yeye Yule jana Leo na hata milele Kwa
msingi huo Msamaha wake unapatikana kila sekunde na kila dakika na kila saaa na
kila siku hii ni neema ya milele Maandiko mengine ambayo unaweza kujisomea
kuhusu kazi ya damu ya Yesu ni pamoja na Waebrania 13;12,10;10, 10;14 na
1Yohana 1;7
2. Roho
Mtakatifu.
Roho Mtakatifu ndiye mwanzilishi
wa kazi ya Mungu katika mioyo ya wanadamu
ndiye anayewaongoza katika
maarifa kamili yanayopelekea kupokea wokovu na kuhesabiwa haki kwa msingi huo ni
moja ya njia zinazotumika kutuletea utakaso 1Wakoritho 6;11,2Wathesalonike 2;13
1Petro 1;1-2 na warumi 15;16
3. Neno
la Mungu.
Neno la Mungu linahusika katika
kazi nzima ya utakaso wa mwanadamu kama Kristo alivyosema yeye mwenyewe Yohana
17;17 Uwatakase kwa ile kweli Neno lako ndio kweli , tunaona pia katika Waefeso
5;26, Yohana 15;3,Zaburi 119;9 Yakobo 1;23-25 Kwa ujumla wakristo wanaitwa watu
waliozaliwa kwa neno la Mungu 1Petro 1;23,Neno la Mungu hufanya kazi ya
kutuamsha na kutukumbusha na kutuonyesha makosa yetu na tunapotambua uzoefu
wetu na kuliitikia katika kile kinachosemwa
na kutubu tunaoshwa kwa neno hilo
na kuanzia tulipoliamini na kuokolewa na tunapoendelea kulitiii linaendelea
kufanya kazi ya kutusafisha na kututakasa Yakobo 1;22-25
Mawazo
yasiyo sahii kuhusu utakaso na Wokovu.
Watu wengi waliookolewa watakuwa
wanafahamu kuwa kizuizi kukubwa cha watu kuishi maisha ya utakatifu ni mwili na
ndio unaokuwa kizuizi kukibwa katika maendeleo yao ya kuelekea kwenye ukamilifu
je mtu anawezaje kuushinda mwili? Hapa ziko dhana kama tatu hivi ambazo sio
sahii kuhusu namna tunavyoweza kutakaswa
1.
Imani
iitwayo Eradification au “inbred” hiii ni imani ya kuwa dhambi
inarithiwa kutoka kwa wazazi, imani hii iliandikwa na Lewis Sperry Chaefer
ambaye anafikiri kuwa kama asili ya dhambi ingekomeshwa kamwe kusingekuweko
kifo kwa sababu kifo ni matokea asili ya
dhambi wanatumia Warumi 5;12-21. Kwa hiyo wanaamini kuwa kwa kuwa wazazi wetu
waliishi katika dhambi ni lazima tutaendelea kuzaliwa wenye dhambi, Je hali ya
mwili kutupinga ikikomeshwa je kutakuwa na ukombozi kwa aina binadamu kuwawezesha
kuishi maisha matakatifu? Jibu ni sio kweli kwani Bado mwanadamu angepambana na
dunia na hali kadhalika ukiiacha asili
ya dhambi yuko shetani ambaye angeendelea kufanya kazi zake kutupinga
2.
imani
iitwayo legalism hii ni jamii ya
watu wanao amini katika kushika sheria Fulani na kuishi kwa sheria kali
kunaweza kumsaoidia mtu kuwa mkamilifu Paulo anaeleza wazi kuwa sheria haiwezi
kamwe kumtakasa mtu warumi 6 ukweli unawekwa wazi katika sura ya 3 ya Wagalatia
kwa ujumla mtu anayetaka kutakasika kwa kujikana na kujiminya katika sheria
kamwe hawezi kuwa mtakatifu hali ya wokovu wa mwanadamu inategemea nguvu kutoka
nje yake na sio ndani yake mwenyewe wewe huwezi kujitakasa ni sawa na mfano wa
kipima joto cha daktari ambacho kinaaaua kuwa leo nitapanda hadi kufikia nyuzi
joto 80 Bila hali joto ya nje kipima joto kitabaki vilele ndivyo ilivyo kwa
mtyu anayetaka kujiokoa mwenyewe utakaso na wokovu ni msaada kutoka kwa Mungu
mwenyewe na sio kwa mwanadamu kwa kukazana kujipendelkeza kwa Mungu kwa Kushika
Sheria
3.
imani
iitwayo Asceticism hii ni jamii ya watu walioamini au wanaoamini
kuwa mwili ni muovu hivyo unapaswa kuutumikisha na kuutesa ili uweze kuwa mtakatifu njia hizi hushikwa
sana na Wakatoliki na wahindu na watawa wa kibudha, Imani hii ilijengeka tangu
zamani sana kutokana na watu waliaamini
kuwa kila kitu ni kiovu ukiwamo mwili na mwili unaipinga sana roho hivyo ili
roho iweze kuwa na nguvu unautesa sana mwili ili roho iweze kuwa takatifu, hii
ni kinyume na maandiko Mungu alifanya kila kitu kuwa chema ni Nafsi ya mwanadamu ndio yenye shida na sio
kila kitu kuwa ni kiovu kwa hiyo wanaojaribu kujitesa ili kumpandeza Mungu
maaana yake wanajaribu kuzitesa nafsi zao wanajaribu kujiokoa kupitia nafsi zao
na nafsi haiwezi kuokoa nafsi wokovu na utakaso ni kazi ya Roho wa Mungu.
Rev. Innocent Kamote
Mkuu wa wajenzi Mwenye Hekima
0718990796
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni