Mstari wa msingi Mithali 16;20 “ …….Na kila amuaminiye ana
Heri”
Ni vigumu kujifunza katika somo
moja kama hili furaha zinzoambatana na wokovu, hata hivyo tutaangalia kwa ufupi
sana maeneo machache katika furaha hii maana furaha hii haina mwisho, inaanzia
hapa duniani na itaendelea mbinguni milele na milele,siku ile ulipokata shauri
ulifanyika kuwa mtoto wa Mungu Yohana
1;12-13, “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo kufanyika watoto wa Mungu ndio
wale waliaminio jina lake waliozaliwa si kwa mapenzi ya mwili wala si kwa
mapenzi ya mtu bali kwa Mungu” wewe sasa ni mtoto wa Mungu hapo mwanzo wewe
ulikuwa mtoto wa Ibilisi kwa sababu kila atendaye dhambi ni wa Ibilisi na tamaa
za ibilisi ndizo apendazo kuzitenda Yohana 8;44,1Yohana 3;7-8 sasa basi kwakuwa
wewe ni mtoto wa Mungu Mungu anajishughulisha sana mambo yako yote na hivyo
mkono wa Mungu uko juu yako katika maswala kadhaa wa kadhaa kama yafuatayo.
ULINZI
Wewe sasa unalindwa
na nguvu za Mungu kwa sababu umekuwa mtoto wake na umtii kwake alipokuita
ulikubali kutubu dhambi zako na kumfuata hivyo tangu sasa inakupasa kumtegemea
yeye kwa ulinzi wa kila aina haupaswi kuogopa Uchawi wala wachawi, nguvu za
giza hazina nguvu kwako tena unapoonewa sasa Mungu ndiye ngao yako yeye ndiye
anayekutetea moja kwa moja huna haja ya kuogopa tena
§
Zekaria 2;8 “…………..awagusaye ninyi aigusa mboni
ya jicho langu”
§
Zaburi 34;7 “Malaika wa Bwana hufanya kituo
akiwazunguka wamchao na kuwaokoa”
§
2Nyakati 16;9 “Kwa maana macho ya Bwana hukimbia
kimbia duniani mwote ili ajionyeshe mwenye nguvu kwaajili ya hao, waliokamilika
moyo kuelekea kwake”
§
Zaburi 91;4-7 “Kwa manyoya yake atakufunika ,
chini ya mbawa zake utapata kimbilio…”
§
Zaburi 125;2 “Kama milima inavyoizunguka
Yeruselem Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake tangu sasa na hata milele”
WATU
WANAOKUPIGA VITA AU KUKUONEA MUNGU ATASHUGHULIKA NAO.
Kuanzia ulipokata
shauri kuokoka wewe ni wa thamani mno machoni pa Mungu hivyo vita si vyako tena bali ni vya
Bwana wako Yesu Kristo 2Nyakati 20;15
Yeye Bwana ni mtu wa Vita Kutoka 15;3 na anauwezo wa kukupigania wewe nawe
utanyamaza kimya Kutoka 14;14 yafuatayo ni maandiko kwaajili yako
§
Yeremia 15;20-21 “nami nitakufanya kuwa kama
ukuta wa boma la shaba juu ya watu hawa
nao watapiganna nawe lakini hawatakushinda maana mimi nipo pamoja nawe ili nikuokoe na kukuponya asema Bwana , nami
nitakuokoa na mkono wa watu wabaya nami
nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha”
§
Isaya 54;17 “Kila silaha itakayofanyika juu yako
haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa
mkosa huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana na haki yao inayotoka kwangu mimi
asema Bwana”
§
Isaya 43;1-2 “Lakini sasa Bwana aliyekuhuluku
Eee Yakobo yeye aliyekuumba Ee Israel asema hivi Usiogope maana nimekukomboa ,
nimekuita kwa jina lako,wewe u wangu, upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja
nawe na katika mito haitakugharikisha, uendapo katika moto hutateketea wala
mwali wa moto hautakuunguza”
KWA
HABARI YA MAGONJWA AU MATESO
Mapenzi yake
Bwana aliyetuokoa ni wewe uwe na uzima
tena uwe nao tele Yohana 10;10 kazi za magonjwa ni kazi za Ibilisi
lakini Kristo alidhihirishwa ili azivunje kazi za Ibilisi 1Yohana 3;8 kwa
msingi huo litumie jina la Yesu kukemea mateso ya aina yoyote na magonjwa yanayokutesa
wakati wote amini maandiko yafuatayo kwa ajili ya uzima wako.
§
Zaburi 34;19 “Mateso ya mwenye haki ni mengi
lakini Bwana humponya nayo yote”
§
Kutoka 15;26 “Akawaambia kwamba utaisikiza kwa
bidii sauti ya Bwana Mungu wako na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake na kutega
masikio usikie maagizo yake na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako
maradhi yo yote niliyowatia wamisri Kwa kuwa mimi ni Bwana Mungu wako
nikuponyaye”
§
Yeremia 30;17 “Maana nitakurudishia afya asema
Bwana Kwa sababu wamekuita mwenye kutupwa wakisema Ni sayuni ambao hapana mtu
autakaye”
§
Torati 7;15 “ Na Bwana atakuondolea ugonjwa wote
wala hatatia juu yako maradhi yoyote mabaya uyajuayo ya Misri”
KWA
HABARI YA MAOMBI.
Maombi yako
kabla ya kuokoka Mbele za Mungu yalikuwa ni kama kelele tu Mungu alikuwa
hakusikilizi dhambi zilikuwa zimekutenga mbali naye Isaya 59;2 “Lakini maovu
yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone hata hataki kusikia” sasa
baada ya kuokolewa anashughulika na maombi yako hivyo lolote utakaloliomba
atashughulika nalo zaburi 55;22, Umtwike Bwana mzigo wako naye atakutegemeza
hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele 1Petro 5;7 Yohana 16;24 tumuombe Mungu
kwa jina lake Yesu naye atatusikia huu ndio ujasiri tulio nao kwake kuwa
tukiomba kitu sawa na mapenzi yake anatusikia
1Yohana 5;14-15, Hatupaswi kumuomba Mungu kupitia majina ya watakatifu
waliotutangulia na Badala yake tunamuomba Mungu kwa jina la Yesu tu si Petro,
au Paulo au Mariam kuomba kupitia wao sio mpango wa Mungu Yohana 14;13-14
kumbuka mitume na hata Mariam naye alimuomba Yesu soma Matendo 1;14 Kumuomba
Mungu kupitia mtu mwingine ni machukizo kwa Mungu na ni kulitia unajisi jina la Bwana Isaya 48;11 Jina la Yesu ni jina
lililo juu ya majina Yote Wafilipi 2;9-10.
Wewe tangu sasa
umekuwa kiumbe kipya 2Koritho 5;17 na kwamba unao ndugu wengi kwa kuwa sasa
umaeingia katika familia ya Mungu kila aliye katika kristo Yesu yeye ni ndugu
yako undugu huo hauna mipaka ya nchi
,wala rangi wala kabila sote ni mwili wa
Kristo sisi tu wana wa Mungu na Mungu alituchagua tangu asili soma Warumi 8;29 “Maana wale aliowajua tangu
asili aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake ili yeye awe
mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi” Karibu sana katika familia ya
Mungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni