Ijumaa, 5 Februari 2016

Vijana na Ufahamu Kuhusu Uhalifu !



Somo la kumi

Vijana na ufahamu kuhusu uhalifu.

Uhalifu ni hali ya kwenda kinyume na maadili au nikinyume na sheria zilizowekwa katika jamii ni uvunjifu wa maadili, uko uhalifu wa namna mbalimbali ambao ni uovu kwa ujumla na na adhabu mbalimbali kijamii kisheria au kidini zinaweza kutolewa kulingana na uhalifu huo,wengi hata hivyo wanaojiingiza katika matendo ya uhalifu ni vijana,ni muhimu basi tukiwa na ufahamu japo wa ujumla tu kuhusu uhalifu au matendo ambayo yaweza kuhesabiwa kuwa ni uhalifu ili kwamba vijana wajihadhari kuyetenda katika jamii ili kupata vijana waliobora, kanisa lililo bora na taifa lililobora.Kwa ufupi  swala la uhalifu ni swala pana na lina adhabu mbalimbali za kisheria kulingana na tukio lenyewe lakini tunaweza kujumuisha matukio ya uhalifu kama ,Kujeruhi,kuua Mwanadamu mwenzio,kupoteza vitu vya watu,kuiba,Uhalifu wa kimapenzi,kubaka kulawiti.kufanya mapenzi na watoto wadogo au vikongwe,kusababisha hatari kwa serikali,kuikosesha amani serikali kwa migomo maandamano yasiyo na kibali,utekaji nyarakutishia kuua,kununua mali za wizi,kugushi vyeti,Kufanya ngono na ndugu yako wa damu,Ukahaba,kuwa na madanguro,Rushwa n.k haya kwa ujumla wake yanapokuwa hayakubaliki katika jamii Fulani kimaadili na kisheria katika jamii tunayaita uhalifu kwa hiyo mimi ninayazungumzia kwa sababu chimbuko kubwa la matendo ya uhalifu pia ni kutokana na kutokumcha Mungu hivyo vitendo vya uhalifu huligusa kanisa nasi tunawajibika kuwaonya waamini wetu kuwa makini hata kusababisha vitendo hivi vya uhalifu visijitokeze kwa kusudi au hata kwa bahati mbaya.Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia vipengele  vitano vifuatavyo;-

·         Ufahamu kuhusu sheria ya uhalifu.
·         Makusudi ya sheria za uhalifu,
·         Falsafa za maswala ya uhalifu
·         Aina za uhalifu
·         Je Magereza inaweza kupunguza uhalifu?

Ufahamu kuhusu sheria ya uhalifu.
   Sheria ya uhalifu ni tawi la sheria linalojihusiha na kuchambua uhalifu na kutoa adhabu husika kulingana na tukio,uchunguzi wa tukio kwa kuzingatia haki husika kwa jamii na mtendaji wa uhalifu,hivyo sheria hii inasimamia haki ili kutoa adhabu inayostahili kwa muhalifu husika,kufuata taratibu husika katika kutoa hukumu,Kuiridhisha jamii na kudhibiti kutokea kwa matendo hayo ya kihalifu.
         kama Mungu akipewa nafasi kubwa katika jamii na shetani akanyimwa nafasi Uhalifu utapungua


      Hivyo sheria hii inaangalia kwa mfano mtu ameua apokee adhabu gani,aliuaje kwa bahati mbaya au kwa kukusudia?ulinzi wake kwa jamii husika,utetezi wake kwa jamii husika,sheria inasemaje,jamii inalionaje The common law system,sheria za taifa husika zinasemaje Civil law system na hivyo mtoa hukumu atazingatia vigezo vya kanuni zilizowekwa kwa kawaida sheria ya uhalifu inaangalia zaidi matendo yenye kuelekea mahusiano yetu na jamii kwa ujumla.

Makusudi ya sheria za uhalifu
Sheria ya uhalifu ina makusudi ya kuilinda jamii isimdhuru au isiwadhuru wale ambao tayari wameshadhuru na kuwafundisho kwa wale wanaojaribiwa kutaka kudhuru wengine,Madhara ambayo sheria ya uhalifu inataka kuyadhibiti ni pamoja na kutokupotea kwa mali ya mtu,kuuana.kudhuru mwili,kudhibiti uhalifu wa kingono,usalama wa taifa n.k kusudi la sheria zote kwa ujumla ni kuitikia matendo yoyote ya kudhuru yawezayo mkufanywa na mtu ingawa kila sheria ina mkondo wake,kwa hivyo endapo mtu amesababisha madhara atashighulikiwa chini ya sheria ya uhalifu aidha kwa kulipa faini,kufungwa kunyongwa au vyovyote endapo atakutwa na hatia kulingana na kosa husika

Falsafa za maswala ya uhalifu
Kuna mawazo mbalimabali  yatolewayo na watu  kuhalalisha au kuchanganua malengo ya adhabu za kihalifu,mawazo haya ni kama yale ya Jino kwajino,Kutoa onyo,Kutishia,kutibu,Kupatanisha.

Falsafa ya jino kwa jino (Retribution).
  Wanaotetea falsafa hii wanadai au wanaamini kuwa muhalifu anapopewa adhabu kali lawama na hasira za jamii inaondoka hii haiondoi uhalifu lakini inathibitisha tu kuwa muhalifu amevuna kile alichokipanda.

Falsafa ya kutesa ili iwe Fundisho kwake na kwa wengine (deterrence).
Wanao amini katika falsafa hii wanaamini kuwa adhabu atakayopewa Muhalifu m,kulingana na uhalifu wake  itamtia adabu au nidhamu yeye na wengine na hivyo haitarudiwa tena hawa kwao adhabu ni mfano kwa jamii na tishio hivyo muhusika na wengine wanaokusudia kutenda wataogopa kurudia makosa kama yale.

Falsafa ya Kutishia kwa nguvu ili jambo hilo lisifanywe tena .(Restraint)
 Wanaoamini katika sheria hii wanaamini ju ya adhabu itakayolenga kukomesha kabisa uhalifu usitokee tena hii inahusu kumpa muhalifu adhabu kali sana kama wafanyavyo waislamu kukata mkono wa mwizi na mguu,au wale wanaopenda mtu akibakwa aasiwe au auawe nk wanaamini adhabu kali itakomesha kabisa tabia mbaya.Mfano katika biblia Mungu aliagiza mtu akilala na mnyama auawe (Kutoka 22;19) au mtu anayejihusisha na uchawi auawe (Kutoka 22;18) Lengo ni kukomesha kabisa tabia hizo.

Falsafa ya Kuponya na kuelimisha (Rehabilitation).
 Wanaoamini katika falsafa hii wanaamini kuwa adhabu anayopaswa kupewa muhalifu ni kumsaidia, kumuelimisha na kitibu tabia yake vyovyote iwezekanavyo ili aweze kuzalisha asiibe tena na kuwa raia mwema

Falsafa ya kurejesha katika hali ya kwanza (restoration).
  Hii ni falsafa ya kumfanya muhalifu apone na kurudia hali yake ya kwanza  inafaa kwa mfano kwa watu walioathirika na Madawa ya kulevya wanapo jisalimisha serikali inaanza taratibu za kuwatibu kanuni hii inakazia kumfanya mtu arudie tabia yake ya asili iliyo njema hata hivyo kuna bishano katika falsafa hii ambayo pia hukazia Msamaha mtu anapotubu,jamii inaridhika na asamehewe,Hii anaweza Yesu na watu wachache sana kwani hata makanisani wanatenga na kudhalilisha kabisa,hata hivyo kunaweza kuwepo kwa mabishano katika falsafa hizo kulingana na mitazamo mbalimbali ya watu katika jamii na dini na historia hiyo inakaribishwa.

Aina za uhalifu
Kuna aina nyingi sana za uhalifu na ambazo kesi zake zinahitaji uangalifu Mtu anaweza kufanya uhalifu kwa sababu Hana akili vizuri hii ni Mental fault,au akafanya uhalifu kwa sababu alikua anajilinda na uhalifu Defenses to crime ambayo ina upana sana kwani wakati mwingine inahitaji kupima ufahamu wa mtu katika kujua mema na mabaya n.k insanity, uhalifu mwingine ni ule unaofanywa na mtu mwenye Umri mdogo Age hii mara nyingi ni kuanzia miaka saba kushuka chini ambapo ujuzi wa mema na mabaya ni lazima uangaliwe,Uhalifu unaofanywa kwa sababu ya ulevi Intoxication hii inaangaliwa kama mtu alilewa alilewa nini Madawa? Pombe?pombe gani kwa kiasi gani na kwa vipi kwa kawaida gani n.k,uhalifu wa Bahati mbaya Mistake mfano mtu alichukua koti la mwenzake akifikiri kua ni la kwake n.k mazingira yatazingatiwa,makosa yatokanayo na kuchochewa Duress,Hii hutokea pale  mtu mwingine anapochochea mtu mwingine na kumsababishia mtu huyo kudhuru,hii pia utetezi wake huitaji uchunguzi wa kutosha,Kujihami Self Defense inaweza kutokea kwa jambo la kustukiza na katika kujihami mtu huweza kufanya uhalifu,Kutegewa ni swala linaloweza kumfanya mtu afanye jambo ambalo asingeweza kulifanya na kuingizwa hatiani Entrapment hizi ni kesi za kubambikiwa mara nyingi polisi hufanya michezi hii utapaswa kujua namna ya kujitetea. Pia uko uhalifu mwingine kuhusu mtu kama kuua Murder,Unyama Manslsughter,ubakaji Rape,utekaji nyara kidnapping,Uhalifu kuhusu vitu au maliUtapeli False Pretenses,ukabaji Robbery,Kutishia extortion,Kununua au kukutwa na vitu vya wizi receiving Stolen Property,Kugushi au kufoji Forgery na aina nyingine nyuingi za uhalifu.Kwa nini nimezungumzia haya kusudi langu ni kuwa na vijana waliobora hapa nchini  na hivyo tunapaswa kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu uhalifu ili sisi kama vijana tulio bora tujitahidi kujiepusha na maswala ya uhalifu na kwa kuwa sisi ni wanadamu inaweza ikakutokea bahati mbaya pia ujue ni nini cha kufanya aidha itakusaidia kuwaonya vijana wenzako wajiepushe na matendo ya uhalifu yako mengi ambayo ningeweza kuyazungumzia lakini Muda hauruhusu Mungu na atulinde Amen

Je Magereza inaweza kupunguza uhalifu?
   Je magereza zinaweza kusaidia kupunguza uhalifu? Lazima tujiulize swala hili la Muhimu wanasheria wengi hujiuliza swala hili na wako wanaounga mkono na wanaokataa,hali za magereza zetu tunazijua,Gharama za kuendesha magereza tunazijua na woote tunajua jinsi zinavyojaa nafaida inayopatikana na hasara zinazopatikana kutokana na magereza nab ado matendo ya uhalifu hayakomi nini tatizo tatizo ni tiba ya kiroho unapofanikiwa kutibu shida ya kiroho unaweza kufanikiwa kupunguza uhalifu kwa kiwango kikubwa ni vema nikichukua nafasi hii kukuasa kijana mwenzangu na kuiasa serikali kuturuhusu kuhubiri injili katika taifa letu tunao wajibu si wa kuliombea taifa tu bali kulibadilisha Yesu alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kubadilisha tabia ya mtu hivyo aliona hakuna sababu ya kuhukumu ingawa ni muhukumu wa ulimwengu yeye anayo majibu yaliyoshindikana kwa serikali kwa Yesu yawezekana Ni injili ya Yesu pekee inayoweza kupunguza uhalifu

Hakuna maoni: