Ijumaa, 5 Februari 2016

Vijana na Maswala ya Uchaguzi wa Mchumba !



Somo la kumi na moja
Vijana na maswala ya uchaguzi wa Mchumba
Uchumba ni kipindi cha mpito kwa vijana kuelekea Ndoa ,katika somo hili tunazungumzia kipindi hicho ambacho mara nyingi huanza kama Urafgiki,ingawa tulikwisha gusia swala la kuwa na marafiki katika somo la mahusiano lakini hata hivyo kama kuna mahali pana hitaji hekima ya kimungu ni wakati wa kuchagua na wakati wa uchumba,swala hili si jepesi kama ilivyo kwa hakimu anayepaswa kutoa hukumu ya kunyonga mtu,,hakimu aliye na kesi inayohitaji mtu kunyongwa ni lazima atakuwa makini sana kupitia madai yoote na ushahidi ili kupata uhakiki na uthibitisho ili aije akasababisha hatia katika dhamiri yake atakapo hukumu mtu kunyongwa,hivi ndivyo ilivyo kwa mtu anayedhamiria luwa na mchumba wa kutaka kuoana naye, Tutajifunza somo hili kwa kuzingatia maeneo manne yafuatayo;-

·         Umuhimu wa kuoa mtu wa imani sawa na yako.
·         Dhambi ya kumchagulia mtu Mchumba.
·         Umuhimu wa kuwa makini wakati wa kufanya uamuzi
·         Mambo ya msingi ya kuzingatia unapochagua mchumba.

Umuhimu wa kuoa mtu wa imani sawa na yako.
  Huu ni moja ya msingi muhimu sana mtu anapotaka kuoa/kuolewa,jambo la kwanza ambalo ni muhimu likapewa kipaumbele ni hali ya kiroho,Ndoa ni muungano wa watu wawili katika hali zao za kiroho,mwanamke na mwanaume wanapooana sio miiliyao tu inayokuwa mwili mmoja ni roho zao,Waebrania walipozungumzia mwili mmoja kwenye akili zao ilikuwa na maana ya Mwili,nafsi na roho.Hawakumgawanya mwanadamu (Mwanzo 2;21-24,Mathayo 19;6) kwa hiyo alichokiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe, Miili yetu ni hekalu la Roho mtakatifu (1Koritho 6;12-20) hii ina maana ya kwamba mkristo ni roho moja na Mungu,Hivyo unapoungwa na kahaba kwa hiyo mkristo kuungwa na kahaba ni kuvitwaa viungo vya Kristo na kuvifanya vya kahaba (Mst 15-16 1Koritho 6).

     Kwanini ni Muhimu kuoa mtu wa imani sawana yako Mungu katika hekima yake aliagiza jambo hilo na alitoa tahadhari kuwa watu hao wangekua mwiba na kuwa wangeigeiza mioyo ya waisrael isimuelekee Mungu  Kumbe basi kuoa/kuolewa na mtu wa imani nyingine kunaweza kukuletea madhara ya kiroho na kimwili na kinafsi unaona! soma (Yoshua 23;6-15),unapojifanya una hekima kuliko Mungu na kulidharau neno lake madhara yanaweza kukupata hii ilimtokea mfalme Sulemani Soma (1Wafalime 11;1-8), Biblia inasema hivi katika (2Wakoritho 6;14-18) nitanukuu kutoka katika toleo union version la kawaida ambalo kiswahili chake Hupendwa sana “ Msifungiwe nira pamoja na wasioamini ,kwa jinsi isivyo sawasawa kwa maana pana urafiki gani kati ya  haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza  tena pana ulinagifu gani   kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye anasehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai kama Mungu alivyosema ya kwamba Nitakaa ndani yao ,na kati yao nitatembea mimi nitakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wangu kwa hiyo Tokeni kati yao mkatengwe nao ,asema Bwana Msiguse kitu kilicho kichafu Nami  nitawakaribisha  Nitakuwa Baba kwenu nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike  asema Bwana mwenyezi”
 Unaweza kuona maandiko hayo yanenavyo, Tunapozungumzia Ng’ombe waliofundishwa kulima sote tunajua taabu iliyopo unapovalisha jembe kwenye mabega ya ngombe hao ili walime mmoja amefundishwa na wa pili hajafundishwa nini kinatokea huyu aliyefundishwa anajua kuwa sasa ni saa ya kuyalima majani asiyefundishwa anajua majani ni chakula hivyo mwenendo huwa mgumu ndivyo itakavyokuwa ndoa ya watu walio tofauti kiimani hivyo Imani na kiroho ni msingi wa kwanza katika uchaguzi wa mke au mume.

Dhambi ya kumchagulia mtu Mchumba.
 Tabia ya kuwaunganishia watu ni tabia ya wachungaji wengi sana huu umekuwa ni mtindo mbaya sana ambao unakomaa siku hadi siku, Sikatai kuwa Mungu ana njia nyingi katika kuwapa watu wenzi wao ikiwa ni pamoja na kuwatumia wanadamu lakini ninachotaka kutahadharisha hapa kuwa kiwango hiki kimezidi! Na kwa mtazamo wangu chimbuko la ndoa ni la Mungu mwenyewe Kumbuka yeye ndiye aliyeona si vema mtu awe peke yake kisha  Biblia inasema hivi “Na ule ubavu alioatwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke akamleta kwa Adamu” Biblia ya kiingereza inasema hivi “…God brought her to man.” Kwa msingi huu Mungu ndiye anayejua nani anamfaa nani? Kumtafutia mtu mke kwa kuchombezachombeza ni tabia mbaya naya kiburi ya kuchukua nafasi ya Mungu, Ni vizuri mtu akaamua yeye mwenyewe ili asije akakujutia wewe atakapokutana na magumu,kibiblia Mungu ndiye anayejua nani anakufaa wewe kijana na sio mwanadamu,Hata hivyo Mungu hutumia mazingira katika hali Fulani Mungu huweza kuwatumia hata wazazi,hata ambao hawajaokoka hana mipaka wala upendeleo,lakini natahadharisha wachungaji kwani ndoa nyingi ambazo zimeungwaungwa na wachungaji zina matatizo na nyingine zimevunjika na ushahidi wa utafiti wa kutosha ninao ndio maana nataka kutahadharisha watumishi katika eneo hili ni vema kushauri, ni vema kupata maongozi ya kiroho lakini linapowadia eneo la uamuzi waache watu wafanye wenyewe usiwaamulie wala uisiamuliwe.wengi leo wanalia kuwa isingelikuwa Fulani! Kwa nini wewe mtumishi watu wakulilie kwa kukulaumu jihadhari na tabia mbaya ya kuchombezea vijana kuwa huyu anakufaa huku unajua wazi kuwa hafai hii imeliza vijana wengi wache wafanye maamuzi yao wenyewe wakikutana na magumu watajifunza kuvumilia na sio kukujutia wewe 

Umuhimu wa kuwa makini wakati wa kufanya uamuzi.
Hakuna jambo la kuzingatia katika maisha kama kufanya uamuzi au uchaguzi katika maishayetu rejea staid za maisha kipengele cha kufaya maamuzi,Uamuzi tunaoamua leo ndio utakaotufanya trufurahie au tujute katika swala zima la uamuzi wetu uamuzi ambao huambatana na kutafuta mapenzi ya Mungu hauna majuto hata kama una magumu ambayo ni kawaida ya wanadamu (Ruthu 1;8-18),uamuzi unaozingatia tamaa ya kibinadamu huongoza katika majuto na matokeo yasiyo mazuri (Mwanzo 13;8-13,29;16-18,31;19,30-32,35;16-19). Kila mtu aliyeokolewa anapaswa kuzingatia sana maamuzi anayoyafanya ili yaendane na mapenzi ya Mungu,Mume au mke mwema hutoka kwa mungu na ili kufanikiwa kumpata fuata kanuni zilizo sahihi fuata mapenzi ya mungu (Mithali 19;14). Kufanya mapenzi na maamuzi yasiyo ya kimungu kunaweza kukuletea hasara kama yule binti aliyechagua kichwa cha Yohana mbatizaji(Mithali 14;1-12) kuuliza kutoka kwa bwana ni jambo la muhimu haijalishi uko kiroho kiasi gani Yoshua alifanya kosa la kuwaapia wagibeoni amani bila kuuliza kutoka kwa bwana na mungu alikuwa anaona lakini aliacha waingie mkenge amani ya kristo iamue mioyoni mwenu (Yoshua9;3-20 ) zingatia mstari wa 14 “…wasitake shauri kinywani mwa Bwana”Kuna wakati tunaweza kujifanyia mambo wenyewe tu bila kuuliza ushauri kutoka kwa Bwana,Mungu hataingilia kati ujinga wetu Tumuombe Mungu basi atupe kuwa makini wakati woote tunapokuwa au tunapokaribia kufanya maamuzi ili kwamba atusaidie katika jina la Yesu.

 wanandoa ambao wanaonekana kufanikiwa sana katika Ndoa Uchaguzi makini Maisha makini na Mafanikio!

Mambo ya msingi ya kuzingatia unapochagua mchumba.
Yako mambo ya msingi makuu muhimu mawili ya kuzingatia wakati tunapohitaji kuchagua mchumba
1. Zingatia kwanza maisha yako Binafsi.
2. Zingatia ufahamu wakokatika mambo muhimu matatu
·         Mungu na mapenzi yake
·         Ufahamu kuhusu ndoa
·         Ukomavu katika Pendo la Mungu.

Zingatia kwanza maisha yako Binafsi (Mathayo 7;12).
Biblia inasema basi yoyote mtakayo mtendewe na watu watendeeni ninyi vivyohivyo kwanza,Ni muhimu kuzingatia kanuni hii Mara nyingi tunapenda vitu vizuri au watu wazuri huku sisi wenyewe hatufanyi bidii ya kuwa wazuri! Kama uanatafuta mtu aliye sawa anza wewe kuwa sawasawa,kupata mume au mke mzuri hakutegemei neno “NATAKA AWE HIVI” bali kunategemeana na “ WEWE KUWA SAWA” Huwezi kudai unataka mtu mcha Mungu haku wewe mwenyewe humchi Mungu,au unataka mwanamke bikira huku wewe hujitunzi nani unataka akuchague wewe? Hivyo kabla ya kutaka kilicho chema mungu anakutarajia wewe kufanya mema Kaini aliona wivu nduguye Habili alipobarikiwa kwa kutoa sadaka njema na alikasirika alipoona kuwa Mungu hakumtakabali yeye Mungu alimshauri kuwa haitaji kukasirika na kuwa kibali chake kipo endapo tu nayeye angekubali kutenda vema “Kama ukitenda vyema hutapata kibali? Usipotenda vyema… (Mwanzo4;3-7)” Mungu yuko tayari kumbariki kila mtu wala hajaishiwa na baraka lakini wewe unafanya nini?Mungu alimletea Adamu wa kufanana naye je unafanana na yule unayemtaka? (Mwanzo 2;18).Hivyo ni muhimu kwa kila kijana kuamua kuwa karibu na Mungu  hali hii itaichonga tabia yako kuwa njema na kutakufanya uwe makini pale Mungu anapotoa muongozo;-

                                                Mungu
 

                                                                     
     Mwanaume                      ukaribu                             Mwanamke
                                               Ukaribu                                   
                                               Ukaribu   
                
Kadiri kila mmoja mwanamke au mwanaume anavyojitahidi kuwa na uhusiano mzuri na Mungu ndivyo wanavyoweza kuwa karibu, Kiroho, kinafsi na  kimwili na kwa ubara

Ufahamu wako kuhusu Mungu na mapenzi yake
Mtu anapotaka Mungu ampatie mume au mke maana yake anatafuta mapenzi ya Mungu,Wakristo ni lazima watafute mapenzi ya Mungu katika maeneo yote ya maisha Likiwamo hili la kutafuta mwenza,lazima tuyatende mapenzi ya mungu yote (Matendo 20;27)Mtu anayetafuta mapenzi ya mungu ni lazima atambue kuwa,Wakati mwingine mtazamo wako hautakuwa sawa na mtazamo wa mungu,Lakini katika yoote mtazamo wa Mungu ndio halali na unatufaa.Kuyafanya mapenzi ya Mungu  ni lazima kuambatane na kufanya mambo kadhaa katika maisha yetu yatakayosaidia kuyajua mapenzi ya mungu wakati Mungu anapotaka kujifunua kwetu
I.                     Maombi ni moja ya msaada mkubwa sana katika kuyajua mapenzi ya mungu (zaburi 40;8;Mithali 3;5-7b),Daudi alikuwa mtu mwenye kutafuta  mapenzi ya mungu,Kristo Bwana wetu alipenda kile ambacho baba yake anataka kitendeke hivyo aliomba (Marko 1;35)
II.                    Kusoma neno la Mungu (Zaburi 119;9-11,105).Kupitia Neno la Mungu tunaweza kujua nini mapenzi ya Mungu,mungu amatupa maelekezo ya nani wa kuoa na nani wa kutokuoa (Yoshua 23;12-13,2Koritho 6;14-18).Uchumba au ndoa  na mtu asiyeamini umewekwa wazi katika maandiko Hivyo hayo nayo ni mapenzi ya Mungu,Hata hivyo kama mtu atakazania tu aolewe na mume au mke asiyeamini Mungu hataweza kumzuia lakini yatakuwa si mapenzi kamili ya mungu bali mapenzi ruksa (1Samuel 8;1-9 Rumi 1;28-32) Wakati mwingine tunaweza kuwashauri watu na wakakataa neno la Mungu, tuwaache lakini mungu atawalipa sawa na Neno lake,watoto wanaweza kukataa hata ushauri wa wazazi bado tuheshimu maamuzi yao lakini tuwaonyeshe ni madhara gani yataambatana na maamuzi yao lakini Mungu katika mapenzi yake wakati mwingine anaweza kuwa na sababu fulani Mungu alimruhusu samsoni kumpenda mfilisti sio ili apate mke bali kutafuta kisasi (Waamuzi 14;1-4)
III.                  Kuongozwa na Roho (Wagalatia 5;16-17,Warumi 8;14) Mtu anayeongoza na Roho wa Mungu anaweza kuyafanya mapenzi ya Mungu kwa usahihi sana Ni rahisi kuyajua mambo ya rohoni, kujua wakati na kadiri mtu anavyojifunza kutembea na Roho wa Mungu ndivyo unavyojiweka katika nafasi ya  kusema naye na kukuongoza kupitia, Maandiko, mazingira, ushauri, Amani ya moyo, ndoto na maono, sauti ya ndani na msukumo, tamaa msisimko na hisia vina sehemu ndogo sana katika kutusaidia kupata mtu sahii Upendo ni zaidi ya hisia.

Ufahamu kuhusu ndoa.(Mwanzo 18-25).
  Ndoa ni wazo la Mungu “si vema....” ilianzishwa na mungu hivyo tunaoa ili kutimiza mpango wa mungu ndoa haipaswi kuwa sehemu ya kutimiza tamaa,Mtu anayeoa au kuolewa ili kutimiza tamaa tu ataendelea kuwa na tamaa hiyo hata baada ya kuwa na ndoa.
   Ndoa ni muungano wa watu wawili (Agano) ambao wanaunganishwa na Mungu hivyo ni Mungu ndiye anayewaunganisha na ndiye anayejua yupi anakufaa v.18
Muda wa mtu kuoa au kuolewa unaamuliwa na mungu yeye ndiye anajua muda muafaka “kisha akamleta kwa adamu” v.19-20. Mtu haoi au kuolewa kwa sababu anajisikia tu elewa kuwa wakati msukumo huo unaanza unaweza ukawa wakati sahihi au ukawa si wakati sahii
  Kukubalika ni mojawapo ya funguo ya mungu kwa maswala ya ndoa v.23
“Huyu ni nyama katika nyama yangu...”
Mungu amekwisha panga tayari jinsi hao wawili watakavyoishi, Kuacha, kuambatana na kuwa mwili mmoja v.24 lazima uwe tayari kuacha wazazi, jamaa na marafiki, uwe tayari kuambatana, kupenda na kutii, na uwe tayari kushiriki Tendo la ndoa.

Ukomavu katika Pendo la Mungu
   Kila mtu anaweaza kuwa na maelezo yake kuhusu kukomaa na kila mtazamo ukawaunathamani ya aina yake kwa sababu kukomaa kunaweza kugusa mtazamo wa kisaikolojia, kijamii, kisayansi kitheolojia, kihistoria n.k lakini tunaweza kusema kukomaa ni nguvu endelevu ya ufahamu wa maana kuhusu maisha  unaoendana na kiasi kati ya maswala yoote ya kimwili,kisaikolojia,kijamii,kiroho na mitazamo mingine katika maisha ambayo inamwezesha mtu kujitosheleza katika maisha akiwa na amani na mungu ,wanadamu na yeye mwenyewe na kusababisha maana katika ufalme wa mungu na maisha haya  hivyo tunaona kuwa ukomavu ni nguvu endelevu,ni kutoa maana katika maisha,kuwa na kiasi.kuridhika,amani katika mahusiano na maana katika ufalme wa Mungu (Mathayo5;43-44) Upendo kama ule upendo wa mungu unaweza kudhihirisha ukomavu wetu pale tunapowapenda hata adui zetu Mtu anayeingia katika ndoa akiwa na ukomavu huu hataona shida ya aina yoyote ile katika ndoa
 Ni lazima tuwe na upendo wa kweli  huu ni tofauti na upendo wa hisia  au upendo wa tamaa ambao nauita upendo wenye shauku ya kipumbavu huu ni upendo uliojaa ubinafsi  upendo huu huwa na shuhuda kama hizi Nikimuona ule weupe wake tu ninachanganyikiwa,ana hadhi ya kipekee anastahili kunioa,najihisi wa maana ninapokua naye,anaimba vizuri,anahubiri,ni maarufu sana anauwezo,ni mtoaji,ananipa zawadi, nk.utu wa mtu hauko katika vitu wala sura au umaarufu (Mithali 31;30) Mwanaume na mwanamke asiyemcha mungu hta kama ana uzuri kiasi gani  anaitwa hana akili na uzuri wake unafananishwa na  lulu katika pua ya nguruwe (mithali 11;22) “ Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili”au asiye mcha Mungu Hivyo ni muhimu kuwa na mwenzi atakayekupenda vile ulivyo Kumbuka ule mkanda maarufu wa Filamu Coming to America ,mtoto wa kifalme alivyojifanya masikini ili apate mtu atakayempenda vile alivyo na si kwa sababu yeye ni mtoto wa mfalme.

Uchumba wenyewe
 Baada ya kuwa tumeangalia mambo mengi ya msingi hebu sasa tuuangalie uchumba wenyewe sasa,Uchumba unaweza kufananishwa na Mimba na kuzaliwa kwa mtoto kunafananishwa na mwanzo wa maisha ya ndoa,Mimba hupatikana kwa yai la mwanamke kurutubishwa na mbegu ya mwanaume ndipo kiini huanza kukua na baadae watu huanza kuona tumbo likiongezeka  na baada ya muda mtoto huzaliwa hatua hizi zinafanana na hatua za uchumba kuelekea ndoa kwa msingi huo basi
1. Mwanzilishi wa uchumba kwa mila na desturi zetu wa Afrika ni mwanaume na hivyo mwanaume hapaswi kulazimisha kukubaliwa,bali ni lazima aanzishe kwa upendo na  wema na mwanamke anapaswa kujibu kwa upendo na wema hta kama hataki sio lo! Kwani umenionaje mwanaume hata kikombe hujai mi si saizi yako uchumba huanzishwa na mwanaume Mbugu huziendea yai, hata hivyo hii haina maana kuwa mwanamke hawezi kumjua mumewe Mungu aweza kusema na mwanamke pia kama atakuwa makini kwa Roho mtakatifu.
2.  Uanzilishi unapokubaliwa ni kama mamba imetunga, hata hivyo ni muhimu kufahamu kuwa siku mamba inaposhika hakuna mtu ajuae na huwezi kupiga kelele luwa nina mtoto (hii ni muhimu kwani kabla uchumba haujajulikana wakati mwingine hata kabla ya mchungaji kujua nendeni mkaangalie afya zenu kabla watu hawajajua ili endapo mtajibaini kuwa mmoja ameathirika watu wasijue ibaki kuwa siri yako)
   Lakini kama mambo ni mazuri wote tunajua kuwa mamba inapotunga yai hujifunga na haliruhusu mbegu za watu wengine kupita hivyo unapokuwa umechumbia huna haja ya kuanza kukubalia wengine ili ufanye ulinganishi hili sio sahii
3.  Uchumba unakua kama mimba inavyokua ndipo baadae watu hugundua kuwa kuna mimba ni vizuri kukawepo kipindi cha siri cha kufahamiana baadae ndipo muweke mambo hadharani wako watu wengine akichumbiwa leo tu kesho asubuhi kila mtaa umeshajua
4. Mtoto anazaliwa hii ni kilele cha kufikia Harusi na kukabidhiwa mwali na kuapiana kwa habari ya agano la ndoa,Jambo la msingi wakati woote wa uchumba ili ueweze kudumu ni  kuendelea kufanya mawasiliano,

Jinsi ya kuutunza uchumba
Endelea kutunza uhusiano wako na mungu na mahusiano yenu,jitunze katika usafi (Mwanzo 39;10-12 ,2Timotheo 2;22,!thesa 4;3-5),jilindeni mioyo yenu na tama ya kufanya dhambi (Mithali 4;23)usiangalie picha za ngono na mchumba wako,tunzeni ushuhuda ili watu wasipate nafasi ya kulaumu(Yohana 4;21)Yesu alikaa maeneo ambayo si ya maficho,jihadharini kukaa maeneo yenye maficho yasije yakachochea mawazo yasiyofaa na msipendelee kukutana usiku ,Lindeni uchumba usivunjike,endeleeni kuomba zaidi,anzeni kujifunza na kuuliza masali kuhusu ndoa na kusoma vitabu mbalimbali na maandiko.

Maoni 7 :

Unknown alisema ...

na kama nimechagua mchumba kimakosa na sijafanya hayo japo tumejitunza kwa usafi na sina amani moyoni na yeye anadai anaamani nifanyejeJe maana sitaki kuzikosa baraka za BWANA juu yangu

Mkuu wa wajenzi mwenye Hekima alisema ...

Daniel Aron hakuna bahati mbaya katika mpango wa Mungu endelea kumuomba na amani ya mungu ikutawale kama kiko kitu kinachofikiriwa kuwa ni makosa Mungu anaweza kurekebisha pamoja nawe kabla hamjaingia katika ndoa kumbuka kuvunja uchumba nako sio jambo jema linaweza kuleta uadui, Mungu atakupa hekima namna ya kumaliza au kurekebisha maswala yako kwa amani na haya ndio maombi yangu kwako

Unknown alisema ...

Ubarikiwe mtumishi maana ninawakati Mgumu mpaka nimefikiria mengi sana, naomba Mungu anipejinsi ya kufanya maana wakati mwingine najikuta namjibu vibaya pasipo sababu maana sisikii Amani moyoni japo wakati mwingine tunaongea vyema na kuelewana, but najua wakati mwingine ni mapambano ya kawaida, Endelea kutuombea tufikie ukamilifu wa MUNGU kuliko kutangatanga na Dunia leo huyu kesho huyu mwishowe tufikie pabaya na kumwacha MUNGU, Nashukuru kwa kuupata ujumbe huu na naua ni kwa wakat sahihi umenifikia

Unknown alisema ...

MUNGU akutie Nguvu, umeokoa taifa kubwa

Unknown alisema ...
Maoni haya yameondolewa na mwandishi.
Zachason alisema ...

Bwana Yesu Kristo apewe sifa?
Naomba ushauri wako ndugu,
"ikitokea ukawa na mchumba mlie ahidiana kuoana na mkatambulishana hata kwa wazee, lakini wakati huo wa uchumba mtu mke akatokea aka zini nje bila ww kujua tena zaidi ya mtu mmoja ie wa3, lakini ulimpata hajawahi jua mme, ikafika wakati ukamwoa ndo unakuta alikusaliti wakati wa uchumba, unamuuliza anakiri kufanya, inauma kweli, je mtu huyu afanye nn ili asidhoofu kwenye maisha yake? Ana hali mbaya ju ya hili mtumishi nisaidie ahsante

Tony jonas alisema ...

Habar, Mimi kazi yangu naendesha magar zaidi nimejiari na boda kubwa zaidi lililo nileta hapa nimemuomba Mungu sana na mala kadhaa naona Binti atakae nifaa nikiwashilikisha wananiuliza kuhusu kazi yangu badae wanakuja wakisema moyo wao haujalidhia niangalie sehemu nyingine. Ndugu mwandishi naomba ushauli wako