Jumatatu, 15 Februari 2016

UFAHAMU KUHUSU HISTORIA NA MAISHA YA NABII MUHAMAD.




 Historia ya Muhamad;-
      Historia inaonyesha kuwa kabla ya kuzaliwa kwa Muhamad hakukuweko na uislamu kama inavyodaiwa na wanaharakati wa kiislamu  quran inathibitisha kuwa mwislamu wa kwanza katika wanaume ni Muhamad mwenyewe soma  (surat al anaam – wanyama 6;14)….. “Sema hakika mimi nimeamrishwa niwe wa kwanza katika wenye kusilimu….”  Aidha kitabu cha Historia ya maisha ya nabii Muhamad cha Shehk abdallah Saleh Farsy uk 18 kifungu cha pili kinathibitisha kuwa mwislamu wa kwanza katika wanawake ni mke wa kwanza wa Muhamad bi Khadija 

“ Basi Mwislamu wa mwanzo kabisa ni…..Bi Khadija” kwa msingi huu jamii ya waarabu wa kikureshi nduguze Muhamad walikuwa wanaaabudu miungu mingi ya kipagani na uchawi miungu hiyo ni pamoja na baal ambae historia inaonyesha ana asili ya Moab mashariki ya palestina,mungu huyu aliitwa ha-baal na waarabu walimuita hu-baal ndiye Hubal.

     Vyanzo vya kuaminika toka kwa waislamu wenyewe vinatuambia kuwa babu ya Muhamad Abdul Mutalib hakuwa na watoto,Hivyo alikwenda al-kaaba na kuomba “Eee allah nipe  watoto” na aliweka mikono kwenye sanamu ya hubal /allah na kuomba,allah alimpa watoto kumi na aliporudi baadae kwenye ile sanamu ya hubal ambapo aliahidi kuwa akipewa watoto kumi atamtoa mmoja kuwa sadaka kwa hubal/allah alipata watoto hao na walipopigiwa kura watoto hao kura ilimwangukia abdallah,abdallah maana yak e ni mtumishi wa allah huyu ndiye baba wa muhamad ambeye kwa uongozi wa wachawi Hubal aliombwa apokee ngamia 100 kubadilishana na abdallah ambae aliishi mpaka miezi miwili kabla ya kuzaliwa muhamad akafa



Maiti za mamia ya watu waliokufa huko Mecca walipokuwa wakimpiga Mawe shetani wakizolewa na tingatinga na kuwekwa kwenye Roli tukio lililotokea mwaka 2015 wakati wa ibada ya hijja watu wengi walipoteza Maisha na wengine hawajulikani walik hata leo

Muhamad alizaliwa huko makka mwaka wa 570 hivi baada ya Kristo, mji wa makka uko pwani ya mashariki ya Saud arabia ni mji wa kibiashara na maarufu kwa ajili ya msikiti wenye jiwe jeusi al-kaaba,ambalo lilikuwa jengo maarufu kwa miungu ipatayo 360 na zaidi,Makka ulikuwa mji maarufu wa mungu aliyeitwa hubal mwenye nguvu au il-lah,aliyekuwa na wakeze/bintize lat,mannat na uzza walioabudiwa hapo, babae muhamad alikufa miezi miwili kabla ya kuzaliwa kwa Muhamad alipofikisha umri wa miaka sita hivi mamae nae alifariki, alichukuliwa na babu yake ambae nae alifariki mwaka mmoja baadae,ndipo alipochukuliwa na mjomba wake,inasemekana alilelewa na walezi wapatao watano mapaka alipofikisha umri wamiaka 25 hivi,Muhamad alitoka katika familia masikini sana jamii ya Hashemite moja ya ukoo wa waarabu walioitwa makuresh ilikua jamii ya waabudu miungu na mambo ya kichawi neno qirsh maana yake ni papa  yaani samaki aina ya papa.
     Muhamad alizaliwa Jumatatu mwezi wa 12 mfungo 6 sawa na tarehe 20/4au3/570,alipozaliwa tu babu yake alimfunika nguo na kwenda nae al-kaaba na kumuombea dua kwa Hubal/alla (kumbuka al-kaaba wakati huo lazimauende uchi na ilikuwa ibada za kipagani) soma maisha ya Muhamad uk 5 kifungu cha mwisho. 

     Muhamad alipokuwa kijana wa makamo hivi aliajiriwa na mwanamke mmoja tajiri sana aliyetuma watumwa kumfanyia biashara huko Shamu na Yemen mama huyu aliiitwa Khadija alikuwa ni mjane aliyepata kuolewa mara mbili,Watumwa waliokwenda na Muhamad walimsifia kwa bibi yao kuwa alikuwa muaminifu na hivyo baadae bi khadija aliona vema aoane naye,Muhamad alioana na boss wake huku akiwa na miaka 25 tu na Bi Khadija akiwa na miaka 40 bi huyu aliyewahi kuolewa mara mbili alikuwa na watoto watano aliozaa na wanaume hao kwa ufafanuzi soma kitabu maisha ya Muhamad uk 11 kifungu cha kwanza,aidha watoto wote aliozaa muhamad alizaa na bibi huyu tu watoto wa Muhamad walikuwa wakike tu. Baada ya kifo cha bi Khadija Muhamad alioa wake zaidi ya 11 na kuwa na masuria wengi, Kwa mujibu wa vyanzo vya kiislamu Muhamad alijifunza dini za kiyahudi na kikristo katika safari zake za kibiashara kwenda shamu (Syria) kutoka kwa marabi wa kiyahudi na mapadre jambo lililopelekea kuamini mungu mmoja tu, soma maisha ya nabii Muhamad uk 9 kifungu cha pili kutoka chini.

     Inasemekana kufiwa na walezi wake katika utoto na ujana kulimfanya awe mtu mpweke sana,hali ya kuabudu miungu na uchawi wa kutisha na ibada za mizimu ziliyafanya maisha ya Muhamad kuwa yenye kuleta utata.

 Jinsi Muhamad alivyopewa utume .
     Kutokana na athari za maisha ya upweke na mafundisho aliyoyapata kwa wayahudi kuwa mungu ni mmoja tu na sababu nyinginezo nyingi ikiwa pamoja na kutafakari kweli kuhusu maisha vilipelekea Muhamad kutokupenda tena kushiriki ibada za sanamu na ushirikina zilizofanywa na kabila yake na jamii yake, hivyo alianza tabia ya kufunga ramadhani ambao ulikua mwezi mtakatifu wa wale wapagani,alikwenda huko mbali na nyumbani kutafakari, kufunga na kujiuliza maswali mbalimbali kuhusu maisha, katika kutembea kwake huko jangwani hatimaye aligundua pango ambalo alikuwa akilitumia kwa mapumziko pango ambalo bi Khadija alilifahamu hivyo wakati mwingine kumpelekea chakula, Siku moja huko pangoni mwezi wa ramadhan 17 jumatatu akiwa na umri wa miaka  kati ya 35-40, aliona jitu limesimama mbele yake ghfla bila kujua limetokea wapi likamwambia “Soma” yeye akajibu mimi sijui kusoma  wala kuandika, akamwambia tena soma na Muhamad akajibu vilevile kama mara tatu ndipo lile jitu likamkaba kwa nguvu na kumlazimisha kusema kwa kiarabu maneno haya “Iqra bism Rabbikallaziikhalaq” yaani soma na ukariri kwa jina la mola wako. Sura hii ndiyo sura ya 96 katika quran iitwayo al-alaq yaani pande la damu au kuumba.kisha mtu huyu akatoweka

       Muhamad alishikwa na hofu kubwa sana na kuugua sana homa pamoja na kuweweseka,alirudi nyumbani na mkewe bi khadija alimfunika maguo gubigubi na ndipo muhamad alipomweleza yaliyomsibu bi khadija aliondoka mpaka kwa Mganga mmoja wa kienyeji jamaa yake na kumuelezea huyu aliitwa Waraqa bin Naufal  jamaa huyu aliamuru muhamad apelekwe na alipomueleza yoote mganga alimwambia mtu huyu aliyekutokea ni Jibril aliyemshukia Musa na Isa hivyo jibashirie kuwa wewe ni mtume wa umma huu soma kitabu Hisroria ya maisha ya Muhamad uk 17 kifungu cha kwanza.

Vyanzo vingine  vya historia ya maisha ya nabii Muhamad. 
                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                              
Chanzo kimoja cha historia ya maisha ya nabii Muhamad kilichoandikwa na mwanazuoni wa kiislamu aitwae Hussein Mubarak abdulsalama Sakur anaeleza msomi huyu mwenye digrii tatu za uislamu alizozipata Libya na Iraq kuwa Muhamad alipofikisha umri wa miaka 12 babu yake abdul Muttalib alimpa kazi ya kuchunga mbuzi,na akiwa machungani alipendelea kupumzika katika pango hilo mapango hayo yaliitwa Jibarul hira na majini yalikuwa yanaishi kwenye mapango haya na majini yalipo muona yalifurahi sana kumuona mwanadamu yuko katikati yao hivyo yalimuingia kwa uhakika zaidi soma Majumuatun saat al khabaru –kifungu 16 “Tumefurahi kumuona mwanadamu amekuja kwetu kwa hivyo sasa tutamwingia” inasemekana idadi ya majini yaliyomuingia ilikuwa 40,000 yaani walikuwa wengi mpaka wanasukumana ndani yake hali hii ilisababisha kuanguka kifafa mara kwa mara,alipofikisha miaka 30 majini yaliamua kujitambulisha kwa babu yake na kusema “usione shaka akianguka ni sisi majini rafiki zake” wakataka kumchukua kwao babu yake alikataa na wakamwambia watamuua endapo atakataa ndipo babu yake alipomruhusu alichukuliwa na kukaa siku 40 akila ubani na udi tu huko alifundishwa quran na walimpa upako wao akarudi na ndio maana wapinzani wake wa kwanza walikuwa ndugu zake kwa kuwa walijua chanzo,alianza kuhubiri uislamu na katika safari zake alikutana na majini akayahubiri na yakasilimu nahivyo majini ni marafiki wa waislamu na husali pamoja nayo (Surt  al Jinn 72;1,14),Hivyo uislamu na majini ni kitu kimoja, wakristo tumekatazwa kushirikiana na mashetani kwa kuwa miili yetu ni hekalu la Roho mtakatifu,(1 Koritho6;19).Hivyo Ukweli kuhusu uislamu una walakini kwa sababu vyanzo vyake vingine vinafichwafichwa katika hadithi zao mkristo jihadhari na kusilimu utakuwa nyumba ya mapepo.

Ufahamu Kuhusu Muhamad na wake zake.
      Muhamad anaonekana kuwa nabii aliyekuwa na uchu mkubwa sana wa wanawake jambo ambalo lilipelekea Manabii waliotangulia kabla yake kutokuwa mfano wa kuigwa kwenye eneo hili katika jamii zinazomcha Mungu mfano ni mfalme Suleman (1Falme 11;1-4).Tangu mwanzo Mungu alionya kuwa watawala wasijitwalie wake wengi kwani watawageuza mioyo(kumbukumbu la torati 17;17).Biblia inaonyesha wazi kuwa kila ndoa iliyokuwa na mke zaidi ya mmoja ilijaa wivu,ugomvi,huzuni na uchungu hata kama walioolewa walikuwa mtu na dada yake kama Rahel na Lea wake za Yakobo soma (Mwanzo 29) pia ona mfano wa Hana na Penina katika (1Samuel 1;1-15),pia soma habari za Sara na mjakazi wake Hajir baada ya mjakazi huyo kuzaa na Ibrahim (Mwanzo 16),Katika agano jipya Biblia inapokazia sifa za kiongozi inakazia kiongozi safi ni lazima awe mume wa mke mmoja(1Timotheo 3:2,12).Tofauti na mafundisho ya Biblia takatifu ya Mungu Yehova tunaoona mungu wa muhamad allah akionyesha upendeleo kwa waislamu na zaidi kwa Muhamad mwenyewe eti akimruhusu kuoa wake wengi zaidi kwa kadiri alivyotamani bila ya mahari.

      Muhamad aliruhusiwa kuoa na kutembea na wanawake wowote aliojitakia(Surat al ahazab 33;50-51),hivyo alioa wake wengi hasa baada ya kufa kwa bi Khadija mkewe wa kwanza ambae alikuwa na miaka 40 alipooano na Muhamad aliyekuwa na miaka 25 na aliishi nae kwa miaka 25,na alipokufa Muhamad  alioa  wake wengi na masuria,

     Muhamad alikuwa mwenye tama kiasi cha  kufikia hatua ya kuoa mke wa mtoto wake wa kuifika kwa madai ya kuamriwa na allh kuwa kijana wake huyo amuache ili amuoe yeye soma (surat al ahazab 33:37-38) katika mambo hayo yoote ilikuwa ni marufuku kumlaumu mtume,Swala hili ni  kinyume kabisa  na mafundisho yabiblia kwani itakumbukwa kuwa nabii Yohana(yahaya) alimkemea vikali Herode alipomchukua mke wa nduguye na ndio sababu Yohana aliwekwa gerezani na kuuawa ona (Mathayo 14;3-4) pia kwa jambo kama hili Mungu alimkemea Farao kwa kutaka kumchukua Sara mke wa Ibrahimu na Abimeleki kwa kutaka kumchukua Rebeka mke wa Isaka Tunashangazwa sana na mungu wa Muhamad aitwae allah! Aidha nabii huyu mkware alipiga marufuku mtu kuoa mkewe yeyote baada ya kufariki kwake soma(Surat al ahzab 33;52),wakati kibiblia mume anapofariki mke yu huru kuolewa!(Rumi 7;2-3).

     Muhamad aliendeleza ubabe wake huo ambapo licha ya kuwa na mke wa kupora toka kwa mwanae wa kufikia, mke huyo aliyeitwa Sawda bint Zama,Muhamad alioa mke mwingine ambae kama ingelikuwa nyakati za leo angeshitakiwa kwa kosa la ubakaji na kufungwa miaka 30 hivi,Binti huyo aliyeitwa aisha bint abubakar aliyekuwa na miaka saba tu na inadaiwa alimuingilia kimwili alipokuwa na miaka tisa wakati huu Muhamad alikuwa na zaidi ya miaka hamsini “50” jambo hili lilifanyika kutekeleza kile kinachoitwa “Sunnat al jamaa” kutokana na urafiki uliokuweko kati ya Muhamad na baba wa bint huyu aliyeitwa abubakar kwa kiarabu abubakar maana yake ni Baba wa Bikira.Je huu sio ubakaji? lakini ndivyo allah alivyoagiza.

        Wake wengine wa Muhamad ni pamoja  na Hafsa bint Umar(18), Zainab bint Khusama(30),Ummy Salama(29),Zainab bint Jash(38) ,Juweiriyah(20), Rayna(myahudi), Maryam(mkristo), Safia(35)Ummy Habiba(17) na Maimuna(27). Hawa woote aliwaoa baada ya kufa Bi khadija tena akiwa na miaka zaidi ya 50, katika mabano ni umri wa miaka ya wanawake hao.Muhamad licha ya kuwa na tabia hii ya kupenda wamama pia alikuwa na wivu wa kupita kawaida kiasi cha kuwakataza wake zake wasilegeze sauti zao waliposalimiana na wanaume wengine kama unabisha soma (surat al ahazab 33;30-33) hii ni kwa sababu  hakuhubiri wokovu na ndio maana aliwahami sana wakezake.

    Muhamad kwa visingizio kuwa amepewa aya alipiga marufuku kwa wanaume kufika nyumbani kwake na kushinda hapo hapo hovyo au kusubiri chakula kiive,Nabii huyu wa ajabu aliwaamuru wanaume hao wanapofika nyumbani kwake na kusalimiana na wake zake wawasalimie nyuma ya pazia soma kama unabisha katika quran (surat al ahazab 33;53),Bwana Muhamad pia kwa sababu hizohizo za wivu uliokithiri aliwaamuru wake zake na wake wa waislamu kujifunika gubigubi kila kiungo cha miili yao ili kuficha uzuri wao wasije wakatongozwa na wanaume wenye tamaa (ugonjwa) soma (Surat al ahazab 33;59),wakati mwingine aliwatishia wake zake kwa aya za maonyo au thawabu au hata kuwatishia kuwapa talaka na kuoa wake wengine soma (Surat at tahirym 66;1-5). Tahirym maana yake ni kuharimisha

      Kwa mujibu wa quran wakeze Muhamad wanaonekana hawakuishi kwa amani (Insaf) kwani waligombana na kuoneana wivu soma (Surat at-tahirym 66;4)Nabii huyu ambae ni mpenda ngono alipokuwa anaumwa karibu kufa tunaambiwa na vyanzo vya kiislamu kuwa hakuacha mambo mawili sala na Ngono kwani alikua akijikongoja kusali na kuwatimizia wakeze tisa ngono kila siku soma kitabu maisha ya nabii muhamad uk 79 kifungu cha pili kwenye sura ya 15.Nabii huyu ambae kihistoria alifia kwenye mapaja ya mkewe mdogo bi aisha soma maisha ya nabii muhamad uk 80 kifungu cha tatu “Bi aysha akampakata juu ya mapaja yake….”  Na alikua anaogopa sana kufa,

       Muhamad katika quran hakuwathamini sana wanawake yeye aliwaona kama bidhaa kama shamba ,wanaweza kuolewa na kuachwa wakati wowote kama kuna ndoa zenye tabu  ambazo hazina uhakika ni ndoa za wanawake wa kiislamu, hawana amani hawana haki wanapunjwa mirathi waume zao wanapofariki, hawana uhakika wa kuwa peke yao katika ndoa zao itakapokuja mahakama ya kadhi ndo watakandamizwa zaidi na sharia watakuwa wakipigwa mawe kama watapata ujauzito hasa ikiwa mwanaume hajulikani ukweli wanahitaji Upendo na wakristo tunaweza kuitumia fursa hii kuwapelekea habari njema,

        Shetani ameharibu fikra zao kiasi cha kufikiri ni ufahari kuolewa na kuachwa linapotokea hili wao hujiona ndio chuo kumbe wanajidhalilisha, Muhamad alifundisha kuwa waislamu wanaweza kuoa mpaka idadi ya wake wane na masuria yaani wale waliochini ya mkono wake wa kuume hivyo hata kama ni mke wa mtumwa au mtumwa mwenyewe maadamu uko chini ya mwislamu anaruhusiwa kukuingilia soma (Surat an Nisaa 4;3), pia alifundisha waislamu kuwaingilia wake za watumwa wao yaani kama kuna mwanaume ni mtumwa wa mwislamu na ana mkewe muislamu anaweza kumuingilia soma (Surat an Nisaa 4;24),endapo mwanamke wa kiislamu ataleta jeuri ni ruksa kuwapiga na kuwanyima unyumba soma (Surat an Nisaa 4;34) pia katika namna ya kushangaza sana Muhamad aliwafundisha waislamu kuwa wanawake ni konde (shamba) basi ziingilieni konde zenu vyovyote mpendavyo yaani akimaanisha wanaume waweza kuwaingilia wake zao katika tundu yoyote miongoni mwa tundu saba walizonazo wanawake Soma (Surat al baqara 2;223). Kwa ujumla mafundisho ya Muhamad na allah yanapingana sana na maadili ya biblia takatifu mwenye masikio ya kusikia na asikie!

 

Hakuna maoni: